Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Jumamosi, 8 Machi 2025

Ukimaliza Funika 43_44

 



SEHEMU YA ALOBAINI NA TATU


ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI NA MBILI: akifanya ishala ya kumwita mtu flani, ambae pia Anna aligeuka kumtazama, lakini akuweza kumwona, mtu yoyote mwenye alili ya kuwa anatazamana na kijana huyo, “we dada unaitwa na yule jamaa kwani uoni” alisema sema mtu mmoja alie kuwa amesimama jilani yake, hapo Anna akamtazama tena yule kijana, ambae mimi na wewe tuna mtambua kwajina la Sebastian, ambae alikuwa bado anaonyesha ishala ya kuita huku macho ameyaelekeza kwake yeye Ana, aliekuwa amesimama mita kama ishilini toka pale alipokuwa Sebastian. …….endelea….


Ariana akajigusa kifuani kama anauliza mimi, na yule jamaa , yani Sebastian akaonyesha ishala ya dore gumba, kwa maana ndiyo, hapo pasipo kujuwa anaitiwa nini na yule kijana, akatoka mbio kumfwata kijana yule, ambae ukiachilia Masoud, huku kichwani mwake akiwaza kuwa, aijarishi lolote ambalo yule kijana angemweleza, ila yeye alipanga kumwomba msaada wa nauri ili aweze kufika Mafinga, “kumbe unakumbu kumbu, nilizani uto nifahamu” alisema Anna, huku mala baada ya kumfikia Sebastian huku uso wake ukiwa umejawa na tabasamu la matumaini, “nitaweza kukusahau, wakati tumekutana leo hii asubuhi” alisema Sebastian ambae sasa uso wake ulikuwa katika hali ya uchangamfu wa kulazimisha, “kwahiyo kaka unaishi huku?” aliuliza Anna ambae aliuwa anasibiri kusikia alicho itiwa na kijana huyu, ambae alikuwa ananukia manukato mazuri, “hapana sikai huku, nimekuja kukufwata wewe” alisema Sebastian, huku anaingia kwenye gari.


Kusikia hivyo Anna akaachia tabasamu la nguvu, “Masoud amekutuma unifwate?” aliuliza Anna kwa sauti iliyojawa na mshangao wenye furaha, “usinitajie jina la huyo mpuuzi, nimeona alicho kufanyia, mimi nime kuja kukufwata ili ukapumzike usafiri kesho, jioni hii utasafiri kwa shida na pengine kuingia kwenye matatizo” alisema Sebastian, ambae sasa alikuwa tayari ndani gari, lakini baba yangu yupo hospital na wananisubiri mimi nipeleke ela ya matibabu, ndio maana ni muhimu kusafiri jioni hii” alisema Ana, kwa sauti iliyoonyesha msisitizo, “kwa hiyo umeshapata fedha ya matibabu?” aliuliza Sebatian, wakati huo gari lilikuwa linaendelea kuunguruma.


Swali lile la Sebastin, lilimfanya Arianna ainamishe chini uso wake uliojaa udhuni, maana siyo tu laki nane ya matibabu, pia ata ile fedha ya nauri akuwa nayo, nikama Sebastian alisha elewa, “ok! usijari dada yangu, mimi na familia yangu, tumeamua kukusaidia, kadiri tutakavyoweza, sasa ingia kwenye gari, tutaongea zaidi” alisema Sebastian, huku anamwonyesha Anna mlango wa mbele wa abiria.


Anna alikubariana na Sebastian, ambae siyo tu kumwonyesha mlango, pia alimsaidia mwanamke huyu, kumfungulia kwenye mlango, maana Anna akujuwa ata kufungua mlango, na vaada ya hapo Sebastian akageuza gari na kurudi mjini, umesema baba yako anaumwa, je unaweza kunieleza japo kwa kifupi, kuhusu baba” aliuliza Sebastian, na hapo Anna akaanza kumweleza huku akizingatia kuto ingiza hisoria yake na Masoud, maana alimsikia Sebastian akisema ataki ata kumsikia Masoud.


Anna alieza jinsi walivyoangaika na baba yake usiku, mpaka kumfikisha mafunga, na siku ya pili kupata vipimo, na nakutajiwa gharama ya operation, ok! usiwe na wasi wasi, fedha itawafikia muda siyo mrefu, na baba atatibiwa, mengine tutaongea tukifika nyumbani” alisema huku Sebastian anachukuwa simu yake toka kwenye kibano cha kuwekea simu juu ya dash board, na kubofya namba flani, kisha aikiweka sikioni, huku safari inaendelea.********


Yap! mida ya saa mbili na nusu za usiku, Salma ambae alikuwa ametimiza week nzima pasipo kuwasiliana na mchumba wake Sebastian, sasa alikuwa ndani ya gari lake aina ya Toyota IST, mpenzi wake Masoud akiwa pembeni, wamependeza kweli kweli, kwa mavazi yao ya mtoko wa usiku, nyumbani akiwa amemwacha shangazi yake anajipoza kwa cha kubwa ya pombe kali, aina ya #mbogo_land Gin.


Wapenda nao awa wawili, walopendeza kweli kweli, walisimamisha gari kwenye kituo cha mafuta, pale maeneo ya urafiki, karibu kabisa na njia panda ya shekilango, wakajaza mafuta tenk nzima, ambapo ilimlazimu Salma atoe kiasi cha shilingi za kitanzania elfu sitini na tano, na kubakiwa na elfu ishilini na mbili tu, kwenye pochi yake, lakini aikuwa tatizo maana Salma alikuwa na card ya benk, ya kampuni ambayo anaisimamia, ambayo ilikuwa na fedha nyingi sana, account ambayo ilitumika kumpangia Masoud nusu nyumba na kumnunulia vifaa vya ndani, huku vingine vikichukuliwa kiwandani.


Baada ya kumaliza kufanya malipo wakaondoka zao kuelekea upande wa magomeni, “mzee atakuwa anasubiri kwa hamu kubwa sana ela yake” alisema Masoud, nikama alikuwa anakumbushia kiujanja, ahadi ya Salma ya kumtumia baba yake fedha, kiasi cha laki tano, “wala asiwe na hofu, tena tutamtumia laki sita, hiyo nyingine itamsaidia kwa mambo mengine, alafu mwezi wa sita huu, tunatakiwa kulipia kkodi ya nyumba yako” alisema Salma ambae usiku huu alikuwa amevalia njigauni kifupi cha rangi ya blue, kilicho ishia usawa wakati kati ya mapaja, “nakuaminia mamaaa, ujawai kuniangusha” alisema Masoud akimsifia Salma.


Naam walipofika magomeni Kagera, Salma akaegesha gari kwenye Jengo kubwa la KAMANGA PLAZA, ambalo lilikuwa na ATM mashine za benk kadhaa, yeye akatoka shuka kwenye gari na kuelekea kwenye ATM ya benk ya biashara, na kutoa card kisha akaichomeka kwenye mashine, na tofauti na kawaida, card ukaenda moja moja na kupotea kabisa, Salma alishangaa, kuona hivyo, akaribu kubonya kitufe cha kukataa, lakini akukuwa na dalili ya Card kutoka, akasubiri kwa dakika kadhaa, lakini akukuwa na dalili ya card kurudi, uziri wa kuwa na card mbili mbili, kama vile Sebastian alijuwa kuwa kunasiku card itazama” alijisemea Salma, huku anahamia kwenye mashine nyingine, huku anapapasa kwenye mkoba wake, na kutoa tena card nyingine, ambayo ilikuwa ni card ya benk ya watu wa Dar es salaam. …….endelea…. 



SEHEMU YA ALOBAINI NA NNE


ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI NA TATU: akaribu kubonya kitufe cha kukataa, lakini akukuwa na dalili ya Card kutoka, akasubiri kwa dakika kadhaa, lakini akukuwa na dalili ya card kurudi, uziri wa kuwa na card mbili mbili, kama vile Sebastian alijuwa kuwa kunasiku card itazama” alijisemea Salma, huku anaamia kwenye mashine nyingine, huku anapapasa kwenye mkoba wake, na kutoa tena card nyingine, ambayo ilikuwa ni card ya benk ya watu wa Dar es salaam. …….endelea….


Salma alisimama mbele ya mashine ya PDB yani benk ya watu wa Dar es salaam, na kuchmeka card, na hapo ndipo alipojuwa kuwa ile ya kwanza aikuwa bahati mbaya, japo hii aikuzama kama ile ya kwanza, ila licha yenyewe aikuenda yote, yani ilikwama kama vile amekosea kwakuigeuza, akaichomoa na kuigeuza kisha akaichomeka tena, lakini licha ya kuigeuza, na kuichomeka tena hali ilikuwa ile ile, Salma akaitoa car na kuitazama vizuri, kuona kama card ilikuwa inatatizo, ya uaribufu.


Lakini Card aikuwa na dalili yoyote ya kuchubuka au kuaribika, “mh! imekuwaje tena?” aliwaza Salma, huku anarudi kwenye gari, akiwa mwenye sura ya unyonge, “vipi Salma, mbona kinyonge sana?” aliuliza Masoud, akimtazama Salma kwa mshangao, “atuna ujanja inabidi turudi tu nyumbani, card zote zime goma sijuwi mtandao, moja imegoma, nyinine imemezwa kabisaaa” alisema Salma huku anaingia nani ya gari, “au yule mwanamke ameenda kutuloga, maana ni mchawi kama nini” alisema Masoud, akimtaja Anna, mwanamke ambae kwa fedha yake imemsaidia kufika Dar es salaam  kwa mala ya kwanza, “aina shida nita wasiliana na Seba, afwatilie huko benk ktujuwe kuna tatizo gani” alisema Salma huku anageuza gari kurudi upande wa Sheklango.********


Yap! huko mafinga mida hii ya saa mbili, watu watano walikuwa wamekaa kwenye kibaraza cha jengo la mapokezi, yani mama yake Anna, mzee Mdemu, mzee Mwaisaka, mzee Sanga na kijana Emanuel aliekuwa anavua muda wa kwenda langoni, kuendelea na kazi yake ya Lindo, “basi kijana ata akuwa na tabisa tofauti na wazazi wake” alisema mzee Mwaisaka, akimaanisha kushangazwa na jambo ambalo limetokea, masaa manne yaliyopita, “mh! inashangaza yani million moja na laki tano chap chap” alisema mzee Sanga, kwa namna ya kustaajabu, “lakini mwenzenu ata sina amani sijuwi kwanini bado nahisi mwanangu yupo katika mazingira magumu” alisema mama Anna, ambae alionyesha kuto kuamini kuwa Masud ametoa fedha  ya matibabu, kwa ya mzee Sinyangwe, “unajuwa mama Anna mapenzi siyo kiu cha kubashiri” alisema mzee Mdemu, ambae pia, alikuwa anaamini kuwa, Anna amesaidiwa fedha na Masoud.


Ukweli ilikuwa faraja kwao, maana ukiachilia kuwa tayari mgonjwa alikuwa alikuwa amesha fanyiwa upasuaji, ambao ulienda vizuri, na alilazwa kati chumba cha daraja la kwanza, chumba ambacho alikuwa peke yake, na angepatiwa huduma zote muhimu, hii yote ilianzia mida ya saa kumi, wakati tayari kila mmoja wao, alikuwa amesha kata tamaha, ya kupona kwa mzee Sinyangwe, maana walijuwa asingepata matibabu yoyote, kutokana na kukosekana kwa fedha.


Ndipo ghafla walipomwona mwanaume mmoja mtu mzima akiingia pale mkononi amebeba bahasha kubwa ya kaki, akiwa ameongozana na mganga mkuu, walionekana kamawatu wanao fahamiana, “awa hapa ndio ndugu wa mgonjwa” alisema mganga mkuu, huku mala baada ya kuwafikia, “habari zenu jamani” alisamiliia yule mtu mzima, “nzuri habari yako” aliitikia mzee Mwaisaka, “nzuri tu, poleni na kuuguza” alisema yule jamaa, “asante lakini ndiyo hivyo mpaka sasa akuna matumaini ya kupata matibabu” alijibu mama Ana, kwa sauti ya kinyonge kweli kweli.


Wakati huo Doctor nae akadakia, “kwanini amkujitambulisha kama ni ndugu wa mtu mkubwa namna hii, unajuwa tunge mtibu mala moja, maana tungekuwa na uhakika wa kulipa fedha za watu kule kwa mdhabuni” alisema Doctor mkuu wa hospta ya Mafinga, akionyesha kujilahumu sana kwakuto kuwa fahamu mapema watu wale,


Maneno ya mganga mkuu yaliwashangaza wakina mzee Mwaisa, ambao walitazamana kwa kumshangao, “lakini akuna shida nazani matibabu yatafanikiwa” alisema yule jamaa, alie shikilia bahasha,  “ilo alinashida bwana Lubava, sasa wewe ongea nao, mimi naenda kuandaa operation” alisema mganga kuu, kisha akaondoka, akiwaacha wakina mama Ana wanashangaana, “bila shaka wewe ndie mama Ana” alisema yule jamaa alie tajwa kwa jina la Lubava, huku anamtazama mama Anna, “ndiyo ni mimi” alijibu mama Anna, “ok! nime agizwa kuwa letea hii fedha toka kwa Anna, huko Dar es salaam, nazani atawapigia baadae” alisema yule jamaa.


Wakati wanaendelea kushangaana, yule jamaa akaendelea “nime ambiwa niwakabidhi million moja na laki tano, na kama kuna tatizo lolote basi nitawaachia namba yangu ya simu, na pia muda mwingi napatikana hapo kiwandani Lubava Timba, hapo nyuma ya stendi” alisema yule mwanaume, na kuwashangazanga zaidi wakina mzee Sanga, ambao waliachia tabasamu la nguvu, kwakuona kuwa mpendwa wao anaena kupata matibabu, ambayo ni matunda ya safari ya Ariana, huko dar es salaam.


Bwana Lubava aliwapatia ile bahasha, ambayo ndani yake kulikuwa ma bunda mawili ya fedha, yaliyofungwa na mpira mdogo maalumu ya kufungia fedha, raba bend, “nitakuja kuwa tembea mala kwa mala, ila kama kuna dharula, basi namba yangu hii hapa mtanipigia” alisema bwana Lubava, huku anampatia mama Ana, karatasi ndogo ngumu yenye namba za simu. …….endelea…

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu