Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Jumamosi, 8 Machi 2025

Ukimaliza Funika 42


 UKIMALIZA FUNIKA

SEHEMU YA ALOBAINI NA MBILI
MTUNZI @MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI NA MOJA: Nikweli, dakika chache baadae ukaingia ujumbe toka kwa Anna, ujumbe ambao ulionyesha wazi kukata taaa kwa Anna, na kwamba amekubari kuwa sasa Masoud soyo matawi yake, “nikweli Masoud, wewe ni mwanaume mzuri, mwenye kila kitu, lakini kubuka kuwa fedha nguo na uzuri wangu nimeutoa sadaka katika Elimu yako, nakutakia maisha mema, ila nakuombea kwa mungu nisikumbuke kila nilicho kufanyia mimi na familia yangu” ulikuwa ni ujumbe mrefu, sijuwi kama unachekesha kwako msomaji, kama ulivyo mchekesha Masoud…….endelea….

 ambae alicheka kwa furaha kubwa sana, “mjinga wewe nani anajari maneno yako” alisema Masoud huku anarusha simu pembeni yake pale juu ya kochi la kisasa.*******

Naaam! mpaka mida hii, ya saa kumi, pale kijijini Malangari, tayari habari za mzee Kizinge, kuahidiwa laki tano na kijana wake asoud, zilikuwa zimesha tapakaa karibu kijiji kizma, huku zikiambatana na habari za kwamba, kijana huyo kwamba muda flani alisahau simu kwenye gari lake, “unajuwa jembe langu siku hisi lipo busy sana, ebu fikilia leo asubuhi amepark gari lake nje ya ofisi, akaingia ofisini na kusahau simu ndani ya gari, anakuja kuikumbuka saa tisa, sasa unaani angekuwa kapuku asie na gari, kama watu wengine si angesahau simu kwenye dara dara” alisema mzee Kizinge akiwa na wezake kwenye ulanzi.

Habari ile ili leta wivu kwa vijana wengine wenye kutamani maisha kama yale, ila iliwaumiza watu wengine wenye kufahamu, juu uitaji wa fedha wa familia ya mzee Sinyangwe, kwaajili ya maibabu ya baba yao, kitu ambacho mzee huyu mwenye majisifu, amekataa kabisa kusaidia ata shilingi moja yake.*******

Yap! bus dogo aina ya Toyota Coster, lilisimama kwenye kituo cha daradara cha mizani, kituo ambacho kilikuwa kimechangamshwa na polisi kadhaa wa usalama barabarani na wale wa ukaguzi wa magari, ambayo yalikuwa yaesimama katika foleni moja ya kukaguliwa na kuingia katika mzani, pia kulikuwa na wafanya biashara wadogo wadogo, waliokuwa wanauza vinywaji na matunda, bila kusahau mikate korosho na karanga, pia kulikuwa na abiria wengi waliokuwa wanasubiri usafiri wa kuelekea mlandizi chalinze morogoro, na msata au mkata.

Ana alishuka toka kwenye lile gari la abiria, na kusimama pembeni ya barabara, akisubiri usafiri wa kwenda mafinga, huku kichwani mwake akiendelea kuwaza na kukumbuka kilicho mtokea, pia alifikili juu ya matibabu ya baba yake, alieko hospital, kule mafinga mjini.

Ukweli muda ulikuwa umeenda sana, alitakiwa kupanda gari haraka ili aweze kusafiri, ikiwa bado mapema kidogo, sasa basi kila gari la mizigo liliposimama pale mizani, alilisogelea na kuulizia linaenda wapi, na bahati ilikuwa upande wake, katika magari kumi ya mwanzo mawili yalikuwa yana pita pale Mafinga.

Lakini tatizo fedha aliyokuwa nayo, ndiyo iliyomponza na kuwafanya madereva wa mtazamemavazi yake na kumtilia mashaka, juu ya akili yake, hivyo kuachana nae, na wao kuingia mzani na kuendelea na safari yake, 

Ikawa kwa gari la tatu na la nne, mala gari la tano, hapo ndipo Anna alipojina kuwa mwenye mkosi, na sasa maisha yake yanaenda kuwa magumu zaidi, atarudi vipi Mafinga, angalau kunge kuwa na mashamba basi ange enda kulima vibarua kadhaa ambapo ange jipatia nauri ya kurudi Mafinga, achana na sehemu ya kulala, maana dar akuna joto angelala popote, sasa itakuwa kuhusu chakula maana mpaka sasa njaa, ilikuwa imesha mkaba vya kutosha, ni wazi alianza kuchanganyikiwa, alitamani aangue kilio kwa sauti ya juu sana, ilikupungiuza maachungu aliyokuwa nayo, baada ya hapo ndiyo aanze kufikiria namna ya kurudi Mafinga.

Lakini wakati akiwa amesha kata tamaa mala akaliona gari, linalofanana na lile aliloliona kule karibu na kiwanda cha feniture, ambacho boss wake ni Masoud, gari lililokuwa na wale vijana wawili, likiingia pale mzani lakini kwenye kituo cha daladala, kisha akashuka yule kijana mmoja ambae mala zote alimwona akiwa ndani ya gari, ambae ndie alionekana mwenye gari, ata mwonekano wake ulikuwa mzuri, na dalili zote za kuwa mwenye fedhana mwenye kujiheshimu, ambae mwenzie alimwelekeza kuwa aje hapa kupaa usafiri wa kwenda Mafinga alikomwacha baba yake.

Ukweli Anna aliamani amfwate kijana yule, na kumweleza shida yake ya kusafiri kwena Mafinga, lakini moyo wake ukasita, maana alifikilia kuwa, kama Masoud, mtu ambae alikuwa ndie tumaini lake kubwa, amemkataa a kumwita kichaa, itakuwaje kwa kijana huyu, ambae ata awafahamiani, zaidi ya kuonana leo asubuhi, hivyo akaamua atulie pale alipokuwa, huku anamtazama yule kijana, ambae kimwonekano, japo Masoud, ameonekana kupendeza na kuvutia, tofauti na zamani, lakini kwa huyu kijana ungeweza kusema ni mfanyakazi wa nyumbani kwao.

Anna alimwona kijana yule alie simama pembeni ya gari lake, akitazama kule waliko watu wengi, kama vile kunamtu anamtafuta, lakini niwazi akufanikiwa kumwona, akatazama usawa wa magari makubwa, ambako Anna alikuwepo, na alikuwa anamtazama, na bahati macho yao yakakutana, yule kijana akatabasamu, kama vile amekiona alichokuwa anakitafuta, ata Anna alishawishika kutazama kile ambacho kijana yule mtanashati alikuwa anakitafuta.

Ana alitazama kushoto na kulia, lakini akuona chochote, au mtu yoyote wanae tazamana na kijana yule, akamtazama tena kijana yule ambae sasa alikuwa amenyomkono, akifanya ishala ya kumwita mtu flani, ambae pia Anna aligeuka kumtazama, lakini akuweza kumwona, mtu yoyote mwenye alili ya kuwa anatazamana na kijana huyo, “we dada unaitwa na yule jamaa kwani uoni” alisema sema mtu mmoja alie kuwa amesimama jilani yake, hapo Anna akamtazama tena yule kijana, ambae mimi na wewe tuna mtambua kwajina la Sebastian, ambae alikuwa bado anaonyesha ishala ya kuita huku macho ameyaelekeza kwake yeye Ana, aliekuwa amesimama mita kama ishilini toka pale alipokuwa Sebastian. …….endelea…. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu