Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Jumapili, 18 Mei 2025

Hadithi: A CROWN OF BADNESS EP 21-25


Mpya
TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 21.

Jacob akiwa anakimbia aliona gari mbele yake inakuja hapo alisimamisha ili aombe msaada na hakujali atakuwa nani, kweli gari lilisimama na Jacob alisogea ili aombe walau msaada, lakini cha kushangaza aliyekuwa anaendesha gari hilo ni mrembo shaifa na alikuwa anatabasamu vya kutosha, Jacob hakuamini alibaki katumbua macho kama kabanwa korodani na mkasi.

Jacob aliona kama anaota ila ndo ulikuwa ni uhalisia na alikuwa hataki tena kumuona shaifa, Jacob baada ya kukuta kwenye gari yumo shaifa hapo ndo alizidi kuchanganyikiwa, alikimbia mpaka alihisi miguu inagonga kwenye kichogo, na alikuwa haelewi anakimbilia wapi alifika kwenye jumba lingine la kifahari aligonga mlango ili angalau aombe msaada wa hifadhi kwa muda huo.
Mlango ulipo funguliwa Jacob hakuamini macho yako uso kwa macho na Vicky, Jacob alibaki katumbua macho pale mlangoni akiwa haelewi aongee nini, alitamani amwambie Vicky kwamba mimi ni Jacob sikufa, ila alihisi ndo ataharibu kabisa.
Vicky naye baada ya kufungua mlango na kukuta mtu aliye gonga mlango ni Jacob alichanganyikiwa alijua mzimu wa Jacob umeamua kumfuata mpaka kwake, yaani alikimbilia ndani speed ya kufa mtu na alifikia kupiga simu kwa mr Derick, bahati nzuri Derick naye alikuwa macho muda huo, kwa sababu ndo alikuwa katoka naye kukurupushwa kule na makelele ya bwana nguna.
Vicky akiwa anahema alimusimulia mr Derick kuhusu Jacob, hapo Mr Derick naye kuna kawasi wasi kalianza kumujia na alianza kuamini mambo ya mizimu wakati huwa haamini, maana ni muda mchache huyo huyo mtu anayeambiwa kapita kwa Vicky pia kapita na kwake.

"Hiiiiiiii!!! Mke wangu mwaka huu tunalo !!" Mr Derick baada ya kusimuliwa na Vicky ilibidi naye ampashe mkewe maana wote walikuwa wapo macho

"Eheee!! Kasemaje??" Mama Jacob aliuliza
"Vicky anasema muda huu kuna mtu kaenda kwake kagonga mlango, alipo fungua amekuta mtu anaye gonga ni Jacob" mr Derick alisimulia
"Unaona Derick ubishi wako mi siku ile si nilikwambia ukasema naongopa, nguna kakwambia umesema anaota, haya huyo Vicky naye kajionea sijui bado huamini au mpaka ushuhudie mwenyewe??" Mama Jacob hapo ndo alianza kuaminika na Mr Derick
"Sasa mke wangu si ushauri tufanyeje sasa? Maana naona unaanza kuleta lawama tena?"
"Derick mi naona twende kwa mganga tu, maana mizimu siyo mizuri kabisa na ukiangalia sisi ndo sababu ya kifo"
"Aaaaaa!! We mwanamke unapenda mambo ya waganga kweli yaani!! Kwa hiyo hujaona ushauri mwingine zaidi ya kwenda kwa waganga??"
"Derick kama hutaki ushauri wangu, si na wewe uwaze wakwako mzuri bana"
"Aaaa basi tusubiri kukuche tutajua cha kufanya bana"

Hayo yalikuwa mazungumzo ya Mr Derick na mkewe baada ya zile kashi kashi za Jacob usiku ule.

Jacob naye huku, baada ya kutoka kwa Vicky aliamua kwenda kutulia kwenye varanda fulani ya nyumba ya mtu asiye mjua, aliamua kutulia hapo ili pakuche mpaka asubuhi alafu ndo ajue anaenda wapi.
Basi Jacob alipitiwa na usingizi hapo na alikuja kushituka kushakucha na pembeni yake kulikuwa na sura ya mtoto wa kike nzuri kuliko kawaida, Jacob alipoamka tu alimwangalia yule mdada aliye kaa pembeni.
Jacob alipo mwangalia vizuri mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio upya maana aligundua huyo binti ndo yule aliye muona kwenye jumba la shaifa kule jikoni na shaifa alidai yule ni mfanya kazi wake.
"We nani kwani??" Jacob akiwa anatetemeka alijikaza na kumuuliza yule binti

"Mi naitwa Sharifa mdogo wake na shaifa" yule binti aliongea kistaarabu na alikuwa anatabasamu na Dimpoz zake zikionekana kwa mbali.

Jacob baada ya kusikia hivyo alinywea hakujua hata aongee nini.
"Dada kanituma nikufuate" Sharifa aliongea na tayari alikuwa kashanyenyuka
Jacob alibaki amekaa tu yaani nguvu zilimwishia
"Hey tuondoke basi au nikamwambie kwamba umekataa??" Yule binti alizidi kusisitiza.
Jacob alinyanyuka na kuanza kumfuata yule binti maana aliogopa kwamba akikataa linaweza kumpata la kumpta.
Basi walifika mpaka sehemu ambayo yule binti kapaki gari lake walipanda kwenye gari na kuanza kuondoka.
"Kwani Sharifa we umejuaje kama mimi nipo hapa??" Jacob aliamua kujikaza kiwanaume na aliamua kuanza kumpeleleza Sharifa ili ajue wao ni kina nani haswa
"Jacob mi nimeelekezwa na Dada tu kwamba ntakukuta hapa, ila kusema yeye kajuaje upo hapa hilo hata mimi sijuwi labda ukamuulize yeye??" Sharifa naye alijibu tofauti na Jacob anavyotaka , sijui ndo alikuwa hajui kweli au alidanganya hilo mimi na wewe mpenzi msomaji hatujui na halituhusu.
Basi Jacob alitulia mpaka walifika kwenye lile lile jumba la kifahari tena na walizama mpaka ndani huku Jacob mapigo ya moyo yakiwa yanaenda speed na alikuwa anajua muda wowote anaeda kuonana na mzee wake huko kuzimu.
Basi Sharifa na Jacob walitulia pale sebuleni wakiwa wanamsubiri shaifa aje, wakiwa wametulia pale sebuleni kuna makelele Jacob alikuwa anayasikia kwa mbali, yaani yalisikika kama watu wanasali tena kwa sauti.
"Sharifa mbona kama nasikia makelele kwenye floor ya juu" Jacob aliamua kumuuliza swali Sharifa
"Jacob usijali dada atakuwa yupo kwenye ibaada tu" Sharifa alijibu kwa kifupi na kutokana na maswali ya Jacob ya kuchosha Sharifa aliamua kwenda chumbani kwake kupumzika na alimuacha Jacob pale sebuleni.

Jacob akiwa pale sebuleni bado aliendelea kuyasikia yale makelele, na Jacob akili ilikuwa inamtuma kwamba akachungulie aone makelele ni ya nini?
Basi Jacob alianza kufuata kule yanako tokea yale makelele na kwakuwa ilikuwa ni floor ya juu, alianza kupandisha ngazi taratibu taratibu.
Jacob alipo fika floor ya juu aligundua chumba ambacho ndo hayo makelele yalikuwa yanatokea kwa sababu alipo fika kwenye floor hiyo makelele yaliongezeka mara dufu na makelele yote yalikuwa sauti za kike tupu.

Basi Jacob alisogea na kuchungulia kwenye chumba hicho kwamba makelele hayo ni ya nini? Alipo chungulia tu Jacob hakuamini macho yake kile anaona alibaki kaganda mlangoni kama chuma kimenasa kwenye sumaku.


Itaendelea......

Usikose sehemu ya 22.





TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 22

Basi Jacob alisogea na kuchungulia kwenye chumba hicho kwamba makelele hayo ni ya nini? Alipo chungulia tu Jacob hakuamini macho yake kile anaona alibaki kaganda mlangoni kama chuma kimenasa kwenye sumaku.

Jacob aliona wanawake zaidi ya 50 wanasali na walikuwa wanasali kwa lugha zisizo eleweka, kilichomshitua Jacob siyo kusali bali ni kuona wanasali wakiwa uchi yaani wote mule ndani walikuwa uchi walivaa vichupi tu na kila mtu alikuwa anasali huku kashika kitana cha kuchania nywele na kakinyenyua juu, na wote humo ndani walikuwa ni wanawake na walikuwa ni wa rangi tofauti tofauti.
Jacob alikuwa bado haamini kile anaona, hakuelewa ile ni ibada gani inaendeshwa kivile yaani mnasali mkiwa uchi, Jacob aliona bado haimwingii akilini.
Jacob aliamua kutoka nduki pale mlangoni na wakati anakimbia alianguka kwenye ngazi za kushuka floor ya Chini na kile kishindo chake Sharifa alikisikia akiwa chumbani kajilaza.
Jacob alinyanyuka Fasta huku akiwa anaugulia maumivu na alikimbia Fasta Fasta kurudi pale sebuleni ili asije akashitukiwa, lakini wakati anafika pale sebuleni tayari Sharifa alikuwa ashafika.

"Eheeee umetokea wapi huko?? Au umeyachoka maisha yako??" Sharifa aliuliza kwa hasira
"Aaaaaa!! Aaaaaa! Nilikuwa naangalia tu mazingira ya hii nyumba yalivyo mazuri kwa hiyo nilikuwa nazurura huku na huku ili nione vizuri" Jacob akiwa kakodoa macho aliamua kudanganya, yaani kwa jinsi alivyokuwa anaongea hata kama ni zezeta kiasi gani angejua Jacob anadanganya maana alikuwa hajiamini kabisa.

"Jacob nisikilize vizuri, ukiwa humu ndani inatakiwa kila kitu uelekezwe la sivyo utajikuta unaingia kwenye matatizo ambayo hukutegemea hata huyo dada shaifa mpenzi wako atashindwa namna ya kukusaidia" Sharifa aliongea kwa kumuonya na baada ya hapo alizama chumbani kwake.
Jacob alibaki katulia na anatetemeka pale sebuleni kama mtu anaye subiri majibu ya vipimo vya HIV.

Lilipita kama lisaa limoja Jacob akiwa anasubiri kitakacho fuatia baada ya hapo maana aliambiwa anaitwa na mpenzi wake shaifa
"Duuuuuu!! Hapa kweli nimeingia cha kike yaani siku mbili tu nimeanza kukonda hivi?" Jacob akiwa katulia zake alikuwa anajiwazia pekee ake na kujilaumu.
Basi baada ya Jacob kusubiri sana mara shaifa mpenzi wake aliwasili akiwa kapendeza mno na alipiga gauni jekundu likiwa linawaka waka na alikuwa kanuna ni hatari.

"Jacob wyh unanifanyia hivyo?? We si ulinipenda mwenyewe na ulisema utanipeda kwa hali yoyote ile why unafanya hivyo sasa?? Na ujue umenisababishia matatizo kwa kuja kule juu kwenye ukumbi wa ibada? Nimepewa adhabu na wenzangu kisa wewe kuja kutuvurugia ibada, na hii adhabu ilikuwa inakuja kwako, sijui why unanifanyia hivyo Jacob??" Baada ya shaifa kufika tu pale sebuleni alianza kumulaumu Jacob kwa kile alicho kifanya na alikuwa anatoa machozi na kutia huruma mpaka Jacob mwenyewe alikuwa haelewi kinachoendelea.

"Jacob Mbona unakaa kimya sasa? ivi we unajua ni matatizo gani mi nimeyapitia mpaka mimi kuwa na wewe na unajua napitia wakati gani??" Shaifa alikuwa bado analalamika na alikuwa anaongea maneno ambayo hata Jacob mwenyewe alikuwa haelewi.

"Shaifa ujue mi sielewi kitu na sikuelewi pia na sijui wewe ni nani haswa?" Jacob alijikaza na kufunguka maana aliona mtoto wa kike anajiliza ovyo ovyo na hapo ndo angalau kaujasiri kalimujia kuona yule aliye kuwa anamhofia naye analia.
"Jacob unauliza hunielewi tena? Mi nishakwambia naitwa shaifa we unataka kujua nini haswa?, ila kuhusu wew kunielewa vizuri utanielewa wiki lijalo" shaifa aliongea na kufuta machozi, alinyanyuka na kuingia chumbani.

Baada ya kama dakika tatu Sharifa alikuja pale sebuleni
"Jacob dada amesema hatarudi mpaka kesho na amesema ikifika usiku nitakuoneshe chumba cha kulala" Sharifa aliongea kwa mapozi na Dimpoz zake zikionekana hadharani.

"Heeee! Hatarudi si nimemuona kaingia huko chumbani ama??" Jacob alishangaa kuambiwa eti shaifa hatarudi wakati yeye kumuona anaingia chumbani.

"Jacob acha utoto, kwa hiyo mpaka Saiz hujamujua mpenzi wako ni mtu wa namna gani??" Sharifa alilishangaa swali la Jacob

Basi ilibidi Jacob akae kimya ili kuona ni wapi wakati utampeleka maana alikuwa hana namna.
Kama kawaida usiku ulifika na ulikuwa muda wa kulala Jacob alioneshwa chumba chake cha kulala na kilikuwa chumba cha hadhi ya nyota tano kabisa mpaka nywele za Jacob zilishangilia kukiona chumba hicho.
Jacob alijilaza kwenye chumba hicho na alikuwa anaangalia TV ya hapo chumbani na gafra alipitiwa na usingizi.
Jacob akiwa usingizini alianza kuota ndoto za ajabu, yaani alikuwa anamuota mpenzi wake shaifa kawekwa katikati na kundi la wanawake na alikuwa anapigwa mijeredi ya kufa mtu na pia alikuwa anachomwa mwili wake na kwa mjibu wa ndoto ile shaifa alionekana kuna kitu analazimishwa kukubali ila yeye alikuwa anakataa na alizidi kutembezewa kichapo.
Jacob alishituka toka kwenye ile ndoto na alipo angali pale kitandani aligundua kama kalowana vile, ila alipo angali vizuri Jacob aligundua kwamba kwenye godoro alilo lalia kumejaa damu, alishituka na kuamuka ila akiwa pale kitandani wakati anashusha mguu ili akanyage sakafu aligundua mguu wake unazama kama kwenye kimiminika cha baridi, alipo angali vizuri Jacob alikuja kugundua kwamba godoro lake linaelea juu ya damu na chumba kizima kilikuwa kimetapakaa damu.
Jacob alihisi labda bado anaota alijaribu kujitikisa na kutikisa kichwa chake lakini aligundua ndo uhalisia wenyewe, hapo uoga ulizidi kuongezeka kwa Jacob.

Mwanaume uvumilivu ulimshinda alijikuta anaanza kupiga makelele ili kuomba msaada kwa mtu yeyote anayesikia, ila sauti yake haikufika popote.



Itaendelea......

Usikose sehemu ya 23.




TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 23.

Mwanaume uvumilivu ulimshinda alijikuta anaanza kupiga makelele ili kuomba msaada kwa mtu yeyote anayesikia, ila sauti yake haikufika popote.

Jacob alijikuta kila akipiga kelele ile damu ndo inazidi kulizamisha godoro chini yaani kiufupi mule chumbani ilikuwa kama bahari ya damu,Na zile damu zilikuwa zinamuwasha Jacob ni hatari, hapo Jacob alianza kupiga maombi ili Mungu ampeleke mahali pema peponi akifa maana aliona hakuna njia nyingine ya yeye kupona.
Kutokana na hofu kubwa ya Jacob na mapigo ya moyo kuwa juu Jacob alidondoka pale pale kwenye godoro na kuzimia.

Huku kwa upande wa akina Derick mambo yalikuwa yametindinganya ni hatari maana kwa akili zao walijua kabisa mzimu wa Jacob umekuja kulipa kisasi.
"Vicky ebu mwambie huyu bwana labda wewe atakusikiliza, yaani yeye kwenda kwa mganga hataki kabisa wakati anajua hakuna njia nyingine ya kuimaliza mizimu Zaid ya kwenda kwa sangoma" Mama Jacob alikuwa anamshawishi mke mwenza ambaye ni Vicky ili amwambie Mr Derick swala la kwenda kwa sangoma maana ilionesha Mr Derick anamuamini sana Vicky.

Basi Vicky alikubali kumshawishi Mr Derick ili waende kwa sangoma kumaliza mambo.
Vicky kweli alifanya kazi yake vizuri hatimaye Mr Derick alikubali kwenda kwa sangoma ili kwenda kujua ule mzimu wa Jacob unatokana na nini?

Huku upande wa Jacob baada ya kuzimia usiku ule alikuja kushituka asubuhi kushakucha na alipo angali mule chumbani hakuona tena damu, ila aligundua mwili wake umevimba kila sehemu, hapo Jacob hakutaka kukaa tena alikurupuka kutoka kule chumbani mpaka sebuleni moja kwa moja, alikuta Sharifa ametulia kwenye sofa anacheki taarifa ya habari ya asubuhi.
"We Jacob Mbona unatoka mbio kama unafukuzwa kulikoni??" Sharifa aliuliza baada ya kuona Jacob amekuja kwa speed pale sebuleni tena akiwa anahema

Jacob hakuongea neno lolote maana aliamini Sharifa anajua kila kitu ila ndo ana msanifu tu, basi Jacob alicho kifanya ni kumuomba Sharifa amuoneshe mlango atoke nje akaotee kijua cha asubuhi.

Sharifa kwa kuwa alikuwa hajui malengo ya Jacob kweli alimsindikiza mpaka nje na yeye alirudi ndani kuendelea na mambo yake, Jacob baada ya kupata fursa hiyo hakutaka kuzembea maana aliona chakufia nini pale ndani wakati uwezo wa kukimbia anao.
Jacob aliluka fensi na kutoka mpaka nje kabisa, Jacob hapo alianza kukimbia huku akiwa anakataa mitaa na watu wote wa mitaa hiyo walikuwa wanamshamgaa Jacob, ila wengine walijua labda ni jogging ya asubuhi kumbe jamaa alikuwa ndo anaelekea kuweuka maana akili ilikuwa haisomi kabisa muda huo.

Basi Jacob alifika kwenye kibanda kimoja ambacho kuna babu alikuwa anauza kahawa asubuhi hiyo.

"Babu shikamo?" Jacob aliamua kwenda kwenye kibanda hicho na alisalimia huku akiwa anahema

"Marhaba mjuu wangu vipi mbona unahema hivyo kaa tu hapo au siyo mteja??" Babu aliitikia vizuri kabisa

"Samahani babu mi siyo mteja, ila nilikuwa naomba tu msaada, kuna kitu nilitaka kuuliza?" Jacob akiwa anaangaza huku na huku alikuwa anamwambia yule babu

"Kijana tulia kwanza naona una mapepe sana, alafu unaonekana una wasi wasi sana, ebu kaaa hapo unielekeze kwa utaratibu" babu aligundua kama Jacob ni mtu mwenye wasi wasi

Basi Jacob alikaa ila bado alionekana kuogopa kweli na alikuwa ni mtu mwenye wasi wasi kweli maana alikuwa anaangalia nje ya kile kibanda mara mbili mbili.

"Kijana Kwani vipi? Au umeiba sehemu ndo unakuja hapa mbona sikuelewi?" Babu alianza kumtilia mashaka.
"Hapana babu siyo hivyo" Jacob ilibidi ajikaze na kujichekesha ili asije ambiwa yeye ni mwizi
"Eheee nambie nini shida??" Babu aliuliza kwa utaratibu

"Samahani babu mi nataka kujua tu naweza kumpata wapi mganga wa kienyeji maeneo haya maana kuna matatizo kidogo ya kifamilia" Jacob alielezea shida yake.
"Aaaaaa!! Sasa kijana hicho ndo kina kufanya uwe na wasi wasi na kuhema hivyo??" Yule babu alimshanga Jacob kwa kuhemeana kote kule kumbe shida yenyewe ndo hiyo.
Basi yule babu alimwelekeza Jacob wapi anapatikana sangoma maeneo hayo. Jacob safari ilianza kwenda kwa sangoma huyo na alikuwa hana hata senti moja na lengo lake ilikuwa ni kwenda kutibia matatizo yake yaani alikuwa hataki tena kukutana na shaifa maishani mwake maana aligundua akiwa na shaifa maisha yake muda wote yatafika mwisho.

Huku nako kwa kina Mr Derick wakiwa mtu tatu ndani ya gari ndo walikuwa wanaelekea kwa sangoma ili kwenda kutibia matatizo waliyoamini yanatokana na mzimu wa Jacob.

Basi walifika sehemu ambayo gari haliwezi kupita waliamua kushuka kwenye gari na kuanza kukanyaga kwa Muguu maana mganga huyo alikuwa kajitenga nje ya mji na kalikuwa ni kamsitu ka kiani.

Jacob naye ndo alikuwa anakaribia kufika maeneo hayo kutokana naharaka aliyo kuwa Nayo Jacob alikuwa anakimbia njia nzima, Jacob akiwa anaelekea huko alikuta kuna gari limepaki njia ila kutokana na haraka zake hakutaka kuchunguza ni gari la nani maana huwenda angeangalia vizuri angeligundua kwamba ni gari la nani.

Basi akina Mr Derick nao wakiwa wameongozana na wamenyoosha kinjia ambacho kilikuwa chembamba na kilisongwa na majani walisikia kama kuna mtu nyuma anakuja kwa kasi alafu anahema.

Wote kwa pamoja waligeuka ili kuona nani anakuja, walipogeuka waliona Jacob anakuja kwa kasi mno, na macho yao yaligongana uso kwa uso na macho ya Jacob.
 

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 24.




TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 24.

Wote kwa pamoja waligeuka ili kuona nani anakuja, walipogeuka waliona Jacob anakuja kwa kasi mno, na macho yao yaligongana uso kwa uso na macho ya Jacob.

Hapo Mr Derick na wake zake hawakukumbuka hata swala la mganga tena kila mtu alipita njia yake yaani ilikuwa ni kila mtu na nafsi yake, Jacob naye akiwa kaganda kama kapigwa na shoti aliona anashuhudia tu vumbi watu wanavyotimuka, ukichanganya na hofu aliyo toka nayo Jacob naye alianza kukimbia ovyo ovyo bila hata kuelewa maana alihisi hata huko aliko enda ni hatari.

Jacob akiwa anakimbilia asiko kujua uso kwa uso alikutana na Mr Derick naye anakimbia kivyake, hapo Mr Derick mawazo yake yote alijua Jacob anamfukuza yeye.

Ukisikia speed ya kulazimisha, ndo kitu kilicho tokea kwa Mr Derick yaani alikimbia speed ambayo hajawahi kimbia yaani hakukumbuka kwamba alikuja na gari au laaa.
Jacob naye baada ya kuona kule anakoelekea kamuona Mr Derick aliamua kurudi kule alikotoka maana aliamini Mr Derick anaweza kumugundua, Jacob aliongeza speed mara dufu kuelekea kwenye barabara kubwa ya kupita magari, alipo karibia kwenye barabara Jacob alimuona Vicky na Mama yake mlezi ndo wanafika kwenye gari lililokuwa limepaki pale njiani ambalo yeye alilipita muda ule.
Akina Vicky nao baada ya kumuona Jacob waliamini anawafuata ni wao hapo waliingia kwenye gari Fasta na kutoka speed na gari, waliendesha gari kama wamechanganyikiwa walipo fika kwa mbele kidogo walimuona Mr Derick na kitambi chake anakimbia kama mwana riadha yupo kwenye olimpiki.

Akina Vicky walisimamisha gari na kumpakia Mr Derick, baada ya hapo walianza kukanyaga gia na dereva alikuwa Mama Jacob mwenyewe ila hawakufukika mbali kutokana na presha ya Mama Jacob alijikuta anagonga mti ambao ulikuwa pembezoni mwa barabara na hapo ilibidi washuke kuangalia kama gari lipo salama japo walikuwa wanashuka kwa mawenge.
Huku nyuma Jacob naye katika kimbia kimbia yake alipata lifti ya gari kwa mzee fulani hivi wa makamo kidogo na Jacob alikuwa hajawahi kumuona kabla, mzee huyo alimbeba Jacob mpaka Town kabisa na alienda kumuacha maeneo karibu na pub ya watu maarufu, kutokana na Jacob kuchoka sana aliamua kwenda kukaa nje ya pub hiyo kwenye korido na kutulia ili walau avute pumzi maana aliyo kutana nayo ni makubwa na kutona na joto ambalo lilikuwa mwilini mwake aliamua kuvua na shati ili kupunguza joto na alikuwa wala hata hajari watu ambao walikuwa wanaingia kwenye pub hiyo.

Huku kwa kina Mr Derick baada ya kugonga mti, walishuka ila waligundua gari ipo salama kabisa kumbe ilikuwa ni ajari ndogo ya kawaida, akina Mr Derick walipanda gari tena kuanza safari kurudi Town na myoyo yao ilikuwa inadunda kwa kasi mno na mawazo yao yote yalikuwa kwa mzimu wa Jacob.
Bahati mbaya baada ya kufika mjini nao waliamua kwenda moja kwa moja kwenye ile ile pub ya watu maarufu ili walau wakapumuzike na kupata kinywaji baridi maana so kwa kashi kashi walizo Kutana nazo.
Lakini baada ya kufika pale pub,kile kitendo tu cha kushuka kwenye gari walimuona Jacob akiwa katulia kwenye korido na alikuwa amekaa tena amevua na shati wala hana wasi wasi, baada ya kuona hivyo!! Heeeeeee ukisikia watu kuvurugwa ndo kule yaani akina mr Derick walichanganyikiwa ni hatari, maana mtu wamemuacha porini wanafika mjini wanamkuta kakaa anawasubiri, yaani hapo ndo waliamini kabisa ule ni mzimu wa Jacob.
Jacob naye baada ya kuwaona wanashuka kwenye gari alishituka sana, alijua pale watakuwa wamemfuata ni yeye ili wamnase, Jacob alinyanyuka Fasta pale chini alipo kuwa amekaa na kuvaa shati ili aanze kula speed.
Akina Derick nao baada ya kumuona Jacob ananyanyuka pale chini na kuvaa shati huku akiwa anawakodolea macho hapo ndo walijua wanaenda kunyonywa makamasi kabisa, Mr Derick na ubabe wote moyo wake ulianza kudundia chini ya matako, naye Vicky na urembo wake wote alikuwa tayari ashalimwaga kojo, hapo akina Derick hawakutaka kusubiri tena walipanda kwenye gari na kutoka nduki kituo cha kwanza kilikuwa ni nyumbani kwao.

Jacob naye alianza kuwashanga akina mr Derick baada ya kutoka nduki
"Uuuuu!! Hawa watu mbona kama nao wananikimbia na kuniogopa? Au wanahisi mimi ni mzimu nini? Uuuu hapa kuna kitu itabidi nifanye jambo maana..!!" Jacob alianza kujiwazia na kujiuliza maswali mengi baada ya kuona baba yake mkubwa na wake zake wametoka nduki ya kufa mtu baada ya kumuona.

Upande wa kina Derick walifika nyumbani huku wakiwa wanahemeana ni hatari
"Nyie wanawake ni wapumbavu kweli mumeona sasa wazo lenu la kwenda kwa sangoma lilivyo ongeza matatizo? Yaani Saiz mzimu wa Jacob ndo umeanza kutufuata kila Sehemu" Mr Derick baada tu ya kufika nyumbani lawama zilianza kwa wake zake maana wao ndo walikuwa wanamshawishi ili waende kwa mganga wa kienyeji na yeye aliamini hilo wazo ndo limepelekea mzimu wa Jacob kukasirika zaidi.

"Sasa Mr Derick lawama za nini? Sisi tulitoa hilo wazo tulijua labda ndo tutaondoa hilo tatizo" Vicky alijitetea

"Nyie wapumbavu kweli, haya sasa hapo mumeondoa au mumeongeza? Mnajua ilibakia kidgo tu ule mzimu unimeze kule porini?? Maana pale tulipo kimbia nilikutana tena na ule mzimu mbele yangu yaani ilikuwa imebakia kiduchu tu yaani, haya oneni sasa tumekimbia na gari tumeuacha kule porini tunaukuta ubatusubiri mjini, nyie fikirieni sasa maisha yataendaje na tayari tusha uchokoza??" Jacob yaani alikuwa kapaniki ilikuwa ni full lawama.

"Mr Derick kama unaona sisi mawazo yetu tulikosea na tumeongeza tatizo basi tusamehe na sasa ni muda wako wa wewe kutoa mawazo yako ambayo ni sahihi sasa?" Mama Jacob alimuachia mpira wa kufikiria ili Mr Derick ndo aucheze.
 

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 25.



TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 25.

"Mr Derick kama unaona sisi mawazo yetu tulikosea na tumeongeza tatizo basi tusamehe na sasa ni muda wako wa wewe kutoa mawazo yako ambayo ni sahihi sasa?" Mama Jacob alimuachia mpira wa kufikiria ili Mr Derick ndo aucheze.
 
"Alafu wewe acha ujinga!? Ujinga sipendi kabisa yaani nyie mmeharibu kila kitu kwa mawazo yenu ya mgando mnataka mi ndo niboreshe eeee?? Au ndo mnataka mnisakizie??" Jacob naye hakutaka uzembe aliwaka vya kutosha, aligundua kwamba wake zake wanataka kumsakizia yeye

"Derick kwani we unatakaje? Na kwa nini hukuja na mawazo ya maana mwanzo? Yaani unaona kila kitu kimeharibika wewe ndo unaaza kutulaumu, kama vipi acha tuvune tulicho kipanda maana hili ndo taji letu, si unakumbuka nilikwambia Jacob tusimuue wewe ulijitia ubishi" Mama Jacob naye alipandwa na hasira maana damu ilikuwa bado inachemka kutokana na mbio walizo kimbia kule porini.

Baada ya hayo maneno ilibidi Mr Derick akae kimya maana aliona wanako elekea wataanza kuvumbuana siri zao na hatimaye kupigana ngumi kabisa.

"We Vicky nenda kaoge huko hujioni kama una nuka mkojo pumbavu" Mr Derick baada ya kutulia kama dakika kumi alihisi harufu ya mkojo na alipo chunguza aligundua ni Vicky, sasa ukichukulia na hasira aliyo nayo kwa Vicky kumshawishi na mawazo ya kipuuzi aliamua kumuoshea Vicky.

Vicky naye alikuja kujitazama alikumbuka kwamba ni kweli alijikojolea katika harakati za kuparangana kule waliko kuwa wanamkimbia Jacob,hapo Vicky alinyanyuka kwa aibu na kwenda bafuni, na kibaya Vicky alikuwa hakai hapo maana hapo palikuwa ni kwa bi mkubwa yaani Mama Jacob kwa hiyo hata nguo za kubadilisha hakuwa nazo na kwa hasira ya Mama Jacob aliamua kumnyima Vicky hata nguo ya kubadilisha, yaani ukisikia kuvurugwa siku hiyo kila mtu alikuwa kavurugwa kivyake.

Jacob naye huku pub aliamua kuondoka na alikuwa hajui aelekee wapi maana tayari kwa fatuma ndo alikuwa ashayakoroga.
Ila Jacob alifikiria kwa muda mrefu aliona hakuna sehemu nyingine ya kwenda Zaid ya pale kwa fatuma na alipanga kabisa maneno ya kwenda kumpanga Fatuma mpaka amwelewe na amsamehe.

Kweli Jacob alifika pale anapo kaa Fatuma na aligonga mlango, ila badala ya fatuma kutoka alitoka mtu mwingine na alionekana ni Mama mtu mzima kidogo

"Karibu mwanangu" yule Mama baada ya kumuona Jacob alimkaribisha

"Asante mama, samahani namuulizia Fatuma??" Jacob aliulizia
"Uuuuuuu!! Fatuma!!? Mbona mi simjui" mama yule alikana na alisema hamjui Fatuma kitu kili fanya Jacob anyong'onyee na kukaa chini
"Mama kuna mdada Siku ngapi zilizo pita alikuwa anakaa hapa ina maana humjui kweli!!?" Jacob bado alikuwa haamini maneno ya mama
"Kijana mi simjui bana mi hapa nimehamia tu jana na ndo nimepangishiwa hii nyumba na dalali, ila kuhusu aliye kuwa anakaa hapa mi simjui kwani vipi??"
Jacob ilibidi aanze kumuelezea matatizo yake yule Mama na kwa nini anamtafuta Fatuma, yule Mama ilibidi amwambie Jacob kwamba atamusaidia na atakaa naye pale kwake mpaka atakapo pata sehemu ya kukaa, basi Jacob alifurahi alijua walau atapata ahueni kidogo.

Maisha mengine Jacob akiwa anakaa kwa yule Mama ambaye kiumri alikuwa ni mkubwa kama Mama yake na Jacob tu, Jacob alikaa na Mama huyo kama wiki mbili hivi na Jacob alikuwa hatoki hapo nyumbani ovyoovyo maana aliamini akitoka tu anaangukia mikononi mwa shaifa.
Majaribu mengine yaliibuka kwa Jacob kwa sababu yule Mama aliye kuwa anakaa na Jacob alianza kumtaka Jacob kimapenzi, na Jacob alianza kukosa tena amani ya moyo wake maana alikuwa anamheshimu Mama huyo kama Mama yake wa kumzaa ila huyo Mama alianza kumletea Jacob pigo ambazo siyo kabisa.

Yule Mama ilibidi amupe Jacob masharti, na masharti yenyewe yalikuwa ni either Jacob akubali kulala na yule Mama au aondoke pale nyumbani aende anako kujua yeye.
Huo ulikuwa mtihani mgumu kwa Jacob kwa sababu alikuwa hajui akitoka kwa mama huyo ni wapi ataenda kuishi na vile hajui ni wapi fatuma alihamia, na mbaya zaidi Jacob kwenye kitaa chake aliko zoeleke ilikuwa inajulikana kama yeye ashafariki kwa hiyo ilikuwa ni ngumu hata yeye kwenda kuomba msaada angalau kwa watu anao wajua na alihisi akifanya hivyo itakuwa ni hatari kwa maisha yake.

Jacob hakuwa na chaguo lingine, alikubali kulala na yule mama, yaani kufanya naye mapenzi, na yule Mama baada ya kuambiwa maneno hayo na Jacob siku hiyo alifurahi ni hatari hata chakula alicho kipika siku hiyo kilikuwa ni tofauti na vyakula vya siku nyingine kabisa, yaani kilikuwa kimekaa ki VIP Zaid.

Basi siku hiyo ilikuwa jioni Jocob na yule mama
Walikuwa wamekaa sebuleni, yule Mama alianza kumshika Jacob kichokozi na kuamsha hisia za Jacob, kweli kama mwili ulivyo umbwa kwa hisia Jacob naye alijikuta mwili unatamani kufanya kazi inayo takikana.

Basi wawili hao waliingia kwenye mtanange mkali pale pale kwenye kochi, ila Jacob alishangaa baada ya kumaliza tu mechi na kufunga bao kama tatu hivi safi kabisa, alishangaa yule Mama amekata pumzi na hakuelewa tatizo nini, Jacob alijaribu kumtikisa yule Mama ila bado hakushituka, Jacob alipo cheki vizuri aligundua yule Mama tayari kasha fariki.

Hapo Jacob mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio, na tayari alikuwa ashaua bila hata yeye kuelewa huyo Mama amekufanyaje, Jacob jasho jembamba lilikuwa likimtoka na hakuelewa afanye nini kwa muda huo, Jacob akiwa anazunguka zunguka mule ndani na kukuna kichwa kwa kuchanganyikiwa alisikia mlango unagongwa kwa nje.
Hapo mapigo ya moyo wa Jacob yalianza kuseleleka kwa speed ya juu kabisa na alikuwa haelewi afanye nini, na huku mlango uliendelea kugongwa kwa nguvu.


Itaendelea........

Usikose sehemu ya 26.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu