UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA ALOBAINI NA SABA
MTUNZI @MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI NA SITA: “yah! siunajuwa mida yangu baby, tayari nipo kitandani, sina pakwenda bila wewe” alijibu Salma kwa sauti ile ile ya mtu anae toka usingizi, “hooo!! basi poa tutaonana kesho kiwandani, maana nimesha rudi, nimeigia jioni hii” alisema Sebastian, na kukata simu, na ndio wakati ambao, Salma alipoiona simu ya shangazi yake inaingia, akajuwa kwa vyovyote anaka kumpa habari ya kurudi kwa Sebastia, hivyo akaipokea mala moja, “mwenzangu tumeumbuka” ilo nlo lilikuwa neno la kwanza toka kwa shangazi, ambae aliongea kwa sauti iiyo jaa wasi wasi na kihoro. …….endelea….
Hapo Salma akashtuka sana kiasi cha kushindwa kusikia honi za magari yanyuma yake, yaliyomtaka andoke, na wao wapite, “shangazi kwanini unasema hivyo?” aliuliza Salma kwa sauti yenye wasi wasi mwingi, huku Masoud akimshtua Salma kwamba aondoe gari, nae akakanyaga mafuta, huku simu bado ikiwa sikioni, “hivi unajuwa kama Seba amesharudi?” aliuliza shangazi na hapo Salma akazidi kushanganyikiwa, kwanini shangaziyake amejuwa mapema kuwa Seba amerudi, “ndiyo najuwa, “sa kama ulijuwa kama amerudi kwanini uliondoka na huyo sharobaro wako?” aliuliza shangazi kwa sauti yenye kushangaa, “hapana shangazi mimi ndiyo nimejuwa jioni hii” alijibu Salma, kwa sauti yenye tahadhari.
Ukweli ilimchanganya sana Salma, ambae siyo kwamba alikuwa anatembea tembea na Masoud kwa kuwa masoud alikuwa na kiti cha ziada kuliko Sebastian, hapana, Masoud akuwa na chochote cha kumfikia Sebastia kuanzia upendo, matendo ya upendo, ata kufikishana kitandani, Sebastian alikuwa anauwezo mkubwa kuliko Masoud, ukiachilia fedha ambayo Sebastian alikuwanazo, Masoud, akuwa na mwonekano mzuri kama Sebastian, kuanzia sura na mavazi. “shangazi kwani kimetokea nini mbona usemi, au alikuja hapo nyumbani?” aliuliza Salma ambae sasa alikuwa anakaribia kuingia mtaani kwao, huku Masoud akifwatilia maongezi yao, “ndiyo alikuja, tena amendoka sasa hivi, ila usiwe na wasi wasi, nimesha weka sawa nimemwambia umeenda kimara kwenye sherehe” alisema shangazi yake Salma, kwa kujiamini.
Wakati shangazi akizania kuwa ameondoa wasi wasi kwa Salma, kumbe sasa alikuwa ameonyesha wazi mambo yalivyo aribika, “nimekwisha…. shangazi nimekwisha… kwanini huku niambia kama umeongea nae, yani nimetoka kuongea nae sasa hivi, nikamwambia nipondani nimelala” alisema Salma kwa namna ya kupagawa, wakati huo anakata kona kuingia nyumbani kwao, akaenda kusimama, huku anakata simu, “Masu, Seba amerudi na alisha kuja hapa nyumbani, nenda kwako tutaongea baadae” alisema Salma, huku anashuka toka kwenye gari, kama siyo Masoud kumshtua, hakika angeacha gari bila kufunga milango ya gari.
Baada ya hapo Salma akachizi akakimbilia malango wa nyumba yao, huku Masoud anamtazama kwa macho yenye maswali mengi sana, kama kuna jambo alikuwa analitafakari kichwani mwake, wakati huo tayari Shangazi yake alikuwa amesha fungua mlango wa nyumba, “shangazi kwanini hukuniambia kama Seba amekuja, ona sasa nimemwambia nipo ndani nimelala, wakati wewe umemwambia nimeenda kimara” alilalamika Salma kwa sauti ya kuchanganyikiwa, na kupagawa, “lakini Salma nimekupigi ukawa unatumika” alisema shangazi na hapo Salma akagundua kuwa Seba aliwai kupiga simu kabla ya shangazi, “sasa tunfanyaje shangazi” aliuliza Salma, huku akionekana mwnye hofu kubwa sana, “wala usijari jibu litapatikana tu, awezi kutushinda yule, kwani anaonekana mambo ya mjini ayajuwi” alisema shangazi, kisha wote kwa pamoja wakaanza kujadiri chakufanya.*******
Naam mala baada ya kumaliza kuongea na simu, waliendelea na safari yao, huku wakipitia kwenye maduka kadhaa, wakinunua nguo chache, pamoja na maitaji muhimu ya Anna, kaa vile mafuta ya kujipaka, viatu, mswaki na dawa yake, pia awakusahau, vitu muhimu kama kanga kandambili na vingine ambavyo Ariana, alina aibu kuvitaja, “mbona sijaona ukinunua chupi” alikumbusha Sebastian, na kumfanya Anna atabasamulie chini, maana nguo hiyo alikuwa nayo moja tu, aliyo ivaa, na ilikuwa na siku ya pili mwili mwake.
Baada yakuona Ana anashindwa kujibu, Sebastian nie alie amua kununua nguo hizo, kwa mkadilio wa nje, kisha safari ikaendelea, wakikamata barabara ya mikocheni, licha ya Sebastian kuonekana mwenye mawazo na machungu mengi, lakini bado alijitaidi kumsemesha Anna, ambae safari hii, akuwa na maswali ya wazi zaidi ya kujiuliza mwenyewe kichwani, juu ya lengo la kijana huyu, “hapo tumeiacha sinza, hiyo barabara inaenda kinondoni, mpaka poster au kalia koo, na huku tunaenda mikochen, alisema Sebastian, huku safari ikiendelea, “kamasitoondoka kesho nitatembea tembea kuangalia itaa, nasikia kuna manzese buguruni, mbagara ata kaliakoo” alisema Anna, ambae alimaansiaha kutembea kwa miguu, kitu ambacho kilimfanya Seba acheke kidogo.
“usijari kesho nitakutebeza sehemu nyingi sana, cha msingi ufike uongee na mama, asiwe na wasi wasi juu yako” alisema Sebastian, na hapo nikama Anna alikumbuka kitu, “tena nimekumbuka, naomba ukiona duka usimame ninunue vocha” alisema Anna, kwa sauti iliyochangamka, huku macho yake yakipepea kushoto na kulia kuangalia mandhari yajiji hili la dar, nyakati za usiku, “wala usiwe na wasi wasi, nitakuwekea vocha kwenye simu yako” alisema Sebastian, na hapo Anna akamtazama kwa macho yaliyo jawa na mshangao, “kaka ujuwe nashindwa ata kusema asante kwa yote uliyonifanyia, maana sijuwi unafanya hivi kwaajili gani” alisema Anna, huku bado anamtazama Sebastian.
Hapo Sebastian akatabasamu kidogo, huku macho yake yakiwa bado yapo mbele yanatazama barabara, “nafanya hivi kwaajili yako, kwa nililoliona leo pale kiwandani, najuwa umepitia wakati mgumu sana, angalau ukirudi Mafinga, uwe katika hali nzuri ya kumsaidia mgonjwa na mama pia” alisema Sebastian kwa sauti tulivu, “sawa lakini nitalipaje hizi ela zote unazo ninunulia vitu, na ulizo watumia wakina mama?” aliuliza Anna, ambae alionyesha wasiwasi wa wazi kabisa. …… Endelea
UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA ALOBAINI NA NANE
MTUNZI @MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI NA SABA: Hapo Sebastian akatabasamu kidogo, huku macho yake yakiwa bado yapo mbele yanatazama barabara, “nafanya hivi kwaajili yako, kwa nililoliona leo pale kiwandani, najuwa umepitia wakati mgumu sana, angalau ukirudi Mafinga, uwe katika hali nzuri ya kumsaidia mgonjwa na mama pia” alisema Sebastian kwa sauti tulivu, “sawa lakini nitalipaje hizi ela zote unazo ninunulia vitu, na ulizo watumia wakina mama?” aliuliza Anna, ambae alionyesha wasiwasi wa wazi kabisa. …….endelea….
Seba ambae kiukweli alikuwa anachekesha kichwa juu ya uanganyifu wa Salma na Shangazi yake, huku maswali ya Anna yakijaribu kupunguza mawazo yake, kwa kuona amekutana na mwanamke wakipekee, ambae asie sahau utu wake kwa shida alizonazo, hakika mwanamke wasasa, asingeuliza maswali kama hayo, zaidi engejipigisaha story, kujiweka katika mikao ya kumtamanisha, tofautina huyu, anae ulizia namna ya kulipia gharama anazo gharamiwa, baada ya kufikilia kulipia kwa kutumia mwili wake.
Wakati anaendelea kutafakari jibu la kumpatia mwanamke huyu, ambae ameamua kumsaidia tu! mala simu yake ikaanza kuita, akaitazama na kuona mpigaji alikuwa ni Salma, nikama alitaka kughairi kuipokea, baada ya sekunde kadhaa kupita akaamua kuipokea, “hallow vipi usingizi umeisha” aliuliza Sebastia kwa sauti tulivu, iliyoficha hasira na chuki zidi ya mwanamke huyu, ambae leo ameshuhudia kwa macho yake siyo tu akiingziwa dudu, ila aliingiziwa dudu sehemu ambayo siyo sahihi kwa matumizi ya dudu, “haaaa! mmmmh! baby, wenzio samahani… yani niliogopa kukuambia kuwa nimeenda kwenye shrehe bila kukuambia, ila nimesha rudi nyumbani, yani shangazi amenigombeza sana kwa nini sikukuambia” alisema Salma kwa sauti iliyojaa wasi wasi.
Sebastian akatikisa kichwa kwa masikitiko, huku akijiaii kuzuwia hasira zake, “hooo kumbe, basi aina shida, niponjiani naendesha gari, baadae basi” alisema Sebastian, “sawa mume wangu, ila nimemiss kukuona jamani baby, uwezi kugeuza nije nikuone?” alisema Salma safari kwa sauti yenye kujidekeza, sauti ambayo ilimchukiza zaidi Sebastian, ambae alitumia nguvu kubwa kujizuwia, “wala siwe na wasi wasi mimi nipo tu, tutaonana kesho ofisini” alisema Sebastian, akijitaidi kuweka sauti yake katika hali ya kawaida, iliyochangamka, “jamani baby, uwezi ata kuja mala moja, au ujanimiss” kiukweli licha ya kwamba ilikuwa ni kupima kama kweli Seba amelizika na uongo wake, ila pia Salma alikuwa anatamani kukutana na Sebastian.
Ukweli toka moyoni kwa Salma Sebastian ndie mwanaume wake wa pekee ambae ni kama mkombozi wa maisha yake, mwanaume ambae amemwonyesha mapenzi ya hali ya juu sana, kiasi kwamba, sasa anaonekana mwanamke mbele ya wanawake, hiyo ni mja ya sababu ya Salma kumchukulia Seba kama mwanume wakipekee kwake, “Salma vumilia mpaka kesho asubuhi, tutakuwa wote mamaaa” alisema Sebstian huku akijitaidi kuzuwia hasira zake, ili kuepusha kumjibu Salma vibaya, na kuaribu alichopanga kukifanya, juu ya Salma na Masoud, ambae ni mfanyakazi wa kiwandani kwake, “sawa baby, basi usichelewe kuja kazini, mwenzio nimekumiss sana” alisema Salma kwa sauti ya kujidekeza, sauti ambayo Seba aliona kuwa ni utapeli mtupu, “poa basi usiku mwema” alisema Sebastia na kabla ajakata simu, Salma akasisitiza, “aya baby, lakini usisahau weka ratiba yako vizuri, kesho nakuitaji” alisema Salam, kwa sauti ya kujideza.
Hapo Sebastian alitazama mbele kwa hasira, huku anauma meno, “tutaangalia maana ninaakiwa kuzungukia miradi yote, siunajuwa sikuwepo kwa muda mrefu” alisema Sebastian, ambae kiukweli akuitaji kabisa, kupitisha mwiko wake kwenye chungu cha mwanamke yule, ambae amegundua kuwa siyo mwema kabisa kwake, “haaaa baby, ata jioni jamani” alisema Salma kwa sauti ya kujibembelezesha, “jioni kuna kuna watu ninaenda kukutana nao, nataka nitangaze tarehe ya kuanza vikao vya harusi yetu” alisema Sebastian na hapo akasikia ukelele wa shangawe, toka kwa Salma, kabla simu aijakatwa, Sebastia akaachia msonyo mrefu, “mpuuzi wewe subiri uone mchezo unavyokuwa” alisema Sebastian huku anweka simu kwenye dash board.
Anna ambae muda wote alikuwa kimya akisikiliza maongezi, ya yule mwenyeji wake, akashindwa kuelewa kwa kuowa nisha mambo mawili, yani sauti ya Sebastian, iliyojaa upendo, na urafiki, na sura ya mwanamume huyu, iliyojaa chuki na hasira kwa yule alie kuwa anaongea nae, “we kaka, huyo uliekuwa unaongea nae si mchumba wako?” aliuliza Anna kwa sauti ya upole yenye tahadhari, “yes, ila usiwe na shaka nazani sasa unaweza kunieleza juu ya mwanaume wako na kile ulichokiona kule kiwandani” alisema Sebastian, na Anna akaanza kueleza hadithi yake na Masoud, huku safari ikiendelea, kuelekea mikocheni.*******
Masoud akiwa chumbani kwake, amejilaza kitandani, aliwaza mambo mengio sana, aliwaza jinsi Salma alivyoonekana kuchachawa pale aliposikia kuwa, Sebastian amerudi, “wanawake watu waajabu sana, yani mambo yote tunayofanya, alafu ananionyesha wazi wazi, jinsi alivyo chachawa kwa huyo boya wake” alijisemesha Masud, kwa sauti ya chini iliyojaa chuki, “yani anamshobokea yule boya, utazani nani sijuwi” alisema Masoud, akisahau kuwa fedha anazotumia na kupendezeshwa ni za huyo huyo anaemwita boya, “alafu demu anaona ela ndiyo kila kitu” aliwaza Masoud..... Endelea
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Write your comment