Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Jumapili, 18 Mei 2025

Hadithi: A CROWN OF BADNESS EP 16-20


Mpya

TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 16.

"Eheee ebu malizia kwanza huo ujinga wa mila Zenu kwamba kwa mfano nisipotekeleza nini kitatokea??" Jacob alikuwa haamini maneno ya Fatuma

"Mimi nasema kile ambacho tumekuwa tunaambiwa toka tunakuwa na ikitokea mmojawapo akakiuka mila hizo kitakacho tokea itakuwa ni haki yake, ila mimi siju nini kitatokea na nimekwambia hivyo ili ujue na tusije laumiana baadae na mimi naamini kwa vile umekubali kwamba unanipenda najua huwezi nisaliti" Fatuma alimalizia kusimulia na alionekana kile alichokisema ana manisha.

"Bora hata usingenisimulia tu mi nikajua unataka kuongea vitu vya maana kumbe ujinga tu, unaacha tuzungumzie kwamba tutaishije we unanza kusimulia paukwa pakawa, sasa mila zenu mi zinanihusu nini sasa??" Jocob yeye aliona kile alicho simulia Fatuma ni uongo tena wa grade za juu na aliamini kwamba wazee walisema hivyo ili kuwaepusha watoto wao wasiwe na tabia za hovyo

"Jacob nilichosema ni ukweli mtupu, nakuomba usije ukaenda kinyume maana majanga ya hapo mimi hayatanihusu na kuhusu mila zetu kukuhusu, zinakuhusu sana kwa sababu tayari ushashiriki mapenzi na mimi na wewe ndo mwanaume wangu wa kwanza na utakuwa wa mwisho pia" Fatuma alikazia swala.

Ila Jacob mwenyewe hakuamini hata kimoja, basi maisha yaliendelea Jacob na fatuma walianza kuishi pale kama mume na mke na Jacob alikuwa hatoki ovyoovyo pale nyumbani. 
Fatuma ndo alikuwa kama kichwa cha nyumba maana yeye ndo alikuwa anatoa kila kitu japo Naye alikuwa anategemea sana mkopo wa serikali, na mapenzi yao yalikuwa yamenawili hakuna mfano na walipendana kuliko kawaida.

"Alafu Fatuma, ujue hujawahi nisimulia kuhusu yule mwanaume niliye mkutaga siku ile pale nyumbani??" Wakiwa wapo kwenye matembezi mida ya jioni Jacob alikumbuka na kumuuliza Fatuma
"Jacob bana hata husahau, bana siku zile mi nilisafirigi sasa rafiki yangu nilimuachia getto kama siku tatu ili anilindie maana yeye anakaa hosteli, sasa yeye nilipo ondoka aliamua kuleta mwanaume kabisa" Fatuma alijitetea na kuelezea jinsi ilivyo kuwa.
Wakiwa bado wanaendelea na mazungumzo Jacob alishituka baada ya kumuona mrembo mwarabu aliyekujaga siku ile na kuchukua kitana pale nyumbani.

"Jacob unashangaa nini?? We si ulisema huyo mwarabu humjui mbona kama unamkodorea macho" Fatuma hakupendezwa na ile tabia na wivu ulimjaa
"Fatuma ujue huyu mwanamke sielewi elewi maana siku ile amekuja kuna maneno alizungumza mimi hata sikumwelewa" 
"Bwana huna lolote sema tu umemutamani, turudi tu nyumbani maana sikuelewi" Fatuma aliongea kwa wivu, na kweli waligeuza na kuanza kurudi nyumbani.
Wakiwa wanatembea uso kwa uso walikutana na Vicky akiwa anatokea kwenye hoteli moja ya kifahari na siku hiyo hakuwa na gari.

"Hahhhaaa Fatuma siku hizi naona umeanza kutembea na sound Brown? Au ni ninja?" Vicky Aliongea kikejeri baada ya kumuona Fatuma yupo na Jacob na bahati nzuri Jacob alikuwa kapiga mzuhuru unao zuia uso wake.

"Hayakuhusu, ila kuna siku yatakuhusu" Fatuma aliongea kifupi na waliendelea na safari na Jacob moyo ulikuwa una dundia kulia badala ya kushoto maana alijua akishitukiwa maisha yatakuwa magumu upande wake.

Vicky alicheka kwa zarau maana aliona Fatuma ni kikaragosi kama vikaragosi vingine.

Basi Jacob na Fatuma walifika nyumbani, ila Jacob bado moyo wake ulikuwa unataka kujua yule mwarabu ni nani haswa, basi walipo fika nyumbani alimuzuga Fatuma kama anapunga upepo nje fatuma alipo ingia tu ndani kupika yeye aligeuza na kurudi kule kule walikotoka nia na madhumuni ilikuwa ni kutaka kujua yule mwarabu ni nani wake na Mr jomo.

Basi alipo fika maeneo yale waliyo muona yule mwarabu alisimama na kuangaza kule na kule, mara gafra alimuona yule mwarabu anaingia ndani ya gari moja la kifahari na kuliwasha, Jacob hakukubari kabla gari halijaondoka alikimbilia na kusimama mbele ya gari

"We Nan unazuia gari langu huko mbele??" Yule mwarabu aliuliza kistaarabu akiwa ndani ya gari
"Samahani nina mazungumzo na wewe?" Jacob alikuwa hata haogopi
"Mi huwaga sizungumzi na watu ambao siwaoni toa kwanza hilo limuzuhura lako nijue we nani?" 

Basi Jacob alivua mzuhura wake na kusogea kwenye dirisha la gari, yule mrembo alipo muona Jacob alitabasamu,
"Ingia kwenye gari" yule mrembo aliongea kwa sauti laini iliyo changanyika na tabasamu mwanana.
Jacob wala hakutaka kuichezea hiyo fursa aliingia ndani ya gari Fasta.
Baada ya Jacob kuingia yule mrembo aliwasha gari na kuanza kuondoka
"Heeee!! We dada wew wapi tena mi nataka tuzungumzie Hapa hapa??" Jacob alishangaa yule Dada kuliwasha gari

Je nini kitatokea?? Jacob anapelekwa wapi na mrembo huyo?

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 17.



TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 17.

"Heeee!! We dada wew wapi tena mi nataka tuzungumzie Hapa hapa??" Jacob alishangaa yule Dada kuliwasha gari

Yule mrembo hakuongea kitu chochote zaidi ya kutabasamu na aliendesha gari mpaka kwenye nyumba moja ya kifahari, Jacob bado alikuwa haelewi lengo la huyo dada ila kufuatana na urembo wa huyo dada Jacob alikuwa anaona kama bahati kwake.
Basi waliingia kwenye jumba hilo la kifahari
"Hapa ni kwako??" Jacob aliuliza baada ya kuingia mule ndani na kukaa kwenye sofa na alikuwa anashanga shanga mazingira ya mule ndani yalivyo mazuri.

"Eheee ebu nambie hicho ulicho taka kunambia??" Yule mrembo aliuliza

"Mi nataka kujua wewe ni nani na kwanini siku ile ulikuja pale??" Jacob aliuliza kwa kifupi kabisa

"Mimi ni Shaifa na nilikuja pale kuchukua kitana changu nilichoibiwa kwenye gari langu" yule mrembo aliyejulikana kwa jina la Shaifa alijibu

"We ulijuaje pale ndo kitana chako kilipo kama uliibiwa na uliingia mpaka kwenye chumba cha siri kabisa??" 
"Hakuna sehemu ambayo siijui kwenye hii dunia" Hilo lilikuwa jibu tata kwa Jacob
"Kivipi yaani mbona sijakwelewa??"
"Ni hatari sana kwa maisha yako endapo utanielewa na naomba iwe mwanzo na mwisho kunifuatilia mimi na nione kama nilivyo na usitake kujua kama nilivyo hiyo itakusaidia sana, maana kunijua mimi kufana faida asilimia 10 na hasara alimia 90 nakuomba unyanyuke uende" Shaifa alijibu majibu tata na alinyanyuka kuingia chumbani.

Jacob bado hakumwelewa mrembo Shaifa alikaa pale kama nusu saa baada ya kuona binti haji tena aliamua kurudi nyumbani na huo ulikuwa ni usiku wa kama saa tano, cha kushangaza Jacob wakati anatoka pale getini hakuona hata gari walilokuja nalo.

"Duuuuuu!! Inamana hii nyumba ina milango mingi kiasi kwamba huyu mrembo katoka bila kumuona?? Au wanaishi wengi humu ndani?" Jacob alikuwa anajiuliza maswali baada ya kutoona gari pale nje.

Basi Jacob alirudi mdgo mdgo mpaka kule wanakokaa na Fatuma na mawazo yake yote yalikuwa kwa Shaifa maana alikuwa amepagawa na uzuri wa mrembo huyo na aliapia moyoni mwake kwamba lazima ampate.

Basi alifka nyumbani na kumkuta Fatuma anasomasoma,

"Eheee nambie ulikuwa wapi? Na wakati ulisema upo nje unapunga upepo??" Fatuma aliacha kusoma na kumuuliza Jacob na inaonekana alimsubiri sana kwa hamu
"Aaaaaaaa!!! Aaaa! Kuna mtu nilikuwa namfuatilia" Jacob alibabaika kujibu

"Nani huyo??" 
"Aaaaaa!! Si nilimuona Mother kwa hiyo nikaanza kumfuatilia ili nipeleleze" Jacob aliamua kudanganya
"Hahaaaa eti mother!!?" Fatuma alicheka sana kiasi kwamba ni kama anajua anadanganywa
"Kwa hiyo huamini ama??"
"Jacob hakuna mtu anayeweza akaamini ujinga kama huo, hivi wewe katika uongo wote umeona huo ndo unafaa eeee??" Fatuma alishitukia
"Heeeee yamekuwa hayo tena, basi sema ukweli wew" 
"Jacob mchuma majanga hulia na wakwao, nakuonya tu Yule mwarabu achana Naye, litakalo kuja kukutokea usije ukanishirikisha wala kuniomba ushauri maana mtu una matatizo chungu nzima unaamua kuyatafuta mengine wakati hayo uliyo nayo hujui hata namna ya kuyakabili" Fatuma aliongea na alionekana ana uhakika na anachokiongea.
Jacob alinywea kwa aibu maana kilicho zungumzwa na Fatuma ni ukweli mtupu, ila Jacob alikuwa anajiuliza Fatuma kajuaje kama yeye katoka kwa mwarabu ila hakupata jibu.

Basi maisha yaliendelea kwa wawili hao na Jacob hakuchoka kumtafuta yule mwarabu alijaribu hata kutafuta lile jumba waliloendaga siku ile ila hakujua ni wapi na hakuona maana siku ile ilikuwaga usiku alafu walikuwaga kwenye gari.

Siku moja jioni Jacob aliamua kwenda ufukweni kupunga upepo na siku hiyo hakuambatana na Fatuma, akiwa ufukweni alimuona yule mrembo mwarabu shaifa akiwa katulia pekee yake ufukweni ana punga upepo, moyo wa Jacob ulilipuka kwa furaha baada ya kumuona yule mrembo tena.
Jacob alianza kumsogelea yule mrembo taratibu taratibu akiwa siku hiyo amedhamiria kumwaga sera zake zote ambazo anazo mpaka kieleweke, ila wakati hajafika kwa yule mrembo gafra alimuona Mr Derick na Vicky wanafika ufukweni hapo wakiwa wameshikana viuno.

"Kudadeki huuu uchawi hawa wajinga wametoka wapi tena aaaaaa!!" Jacob alikasirika sana baada ya kuona wale wajinga wamemharibia, ila Jacob hakutaka kumpoteza yule mrembo aliamua kwenda kutulia sehemu ambayo yeye hawezi kuonekana na akina Vicky ili asubiri mpaka wao waondoke ndo amfuate Shaifa.
Jacob alikuwa katulia zake sehemu anamwangalia kwa mbali jinsi shaifa alivyo umbika na alikuwa anavutia kweli kweli alianza kujiwazia mengi mno

"Daaaa!! Hivi chombo ukinikubalia tu naitangaza ndoa, ila fatuma atachukuliaje? Aaaa! Kuhusu fatuma sijali, ila yule mzee Derick akiona hii chombo anaweza kuniharibia maana wazee wengine sijui wanatumia dawa, uuu!! Ila huyu lazima nimpate iwe isiwe" hayo yalikuwa ni mawazo lukuki ya Jacob akiwa katulia sehemu.
Ila Jacob alishangaa hamuoni tena shaifa pale alipo kuwa amekaa na hakuelewa kaelekea wapi maana ni dakika moja tu alikuwa anamuona binti huyo, siku hiyo Jacob alikasirika kweli kumkosa binti huyo na alitukana matusi ya kila rangi.
Kwa kuwa giza lilikuwa lishaanza kuingia aliamua kurudi zake nyumbani, ila alikuwa kakasirika kweli kweli.

Alifika nyumbani, kutokana na hasira alizo nazo kwa kumkosa yule mwarabu hakumsalimia hata Fatuma.
"Jacob siku hizi hatusalimiani eee??" Fatuma alishangaa
"Ahaaaaa!! Nilikuwa nimesahau bana vipi lakini za jioni??" Jacob alikuwa kama mtu anaye lazimishwa.

"Jacob mi narudia tena achana na huyo mwarabu, litakalo kuja kukupata mi sitahusika kabisa na kama unahisi nakuonea wivu sana we endelea kumfuatilia huyo mwarabu uone yatayo kupata" Fatuma Aliongea kana kwamba ni mtu ambaye kamuona Jacob ni wapi alipo toka, mpaka Jacob alishangaa na hakuelewa Fatuma kajuaje na aliamini Fatuma anamfuatilia.

"Fatuma mimi na wewe ni wapenzi tu na hatujafunga ndoa mambo ya kunifuatilia nyuma nyuma kila ninako enda yaishie leo" kwa mawazo ya Jacob aliamini kwamba Fatuma anatumia njia ya kumfuatilia.

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 18.



TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 18.

"Fatuma mimi na wewe ni wapenzi tu na hatujafunga ndoa mambo ya kunifuatilia nyuma nyuma kila ninako enda yaishie leo" kwa mawazo ya Jacob aliamini kwamba Fatuma anatumia njia ya kumfuatilia.

Fatuma hakujibu kitu chochote zaidi ya kusikitika tu, na aliingia jikoni kwenda kupika chakula cha jioni.
Jacob alikuwa amechanganywa na mrembo shaifa kiasi kwamba alisahau mpaka maswala ya kulipa kisasi na kuzirudisha mali za baba yake mikononi mwake, wakati huku upande wa pili kwa mzee Derick yeye alikuwa anapambana kubadili jina la mali zote na kuandika jina lake na ugumu ulikuwa unamjia kwamba lazima Jacob athibitishe na kama amekufa kweli inatakiwa cheti cha kifo kikiwa na mashahidi watano pamoja na sababu za kifo.
Mr Derick kufuatana na masharti hayo ndo alikuwa yupo kwenye mpango wa kukipata cheti cha kifo cha Jacob bila hata kujua Jacob mwenyewe yupo hai.

"Jacob ivi una mpango gani kuhusu Mr Derick?? Maana naona umekazana na vitu vya ovyo alafu umesahau lengo Mama au umejisahaurisha hapa kwa kuwa nakulisha msosi wa bure??" Fatuma alimkumbusha Jacob, siku hiyo wakiwa wametulia nyumbani kwao wanapiga story

"Fatuma kwa hiyo umeanza kunisimanga eee? Au kisa mi sina pa kuishi na sina kazi??" Jacob alikasirika kwa kupewa makavu yake.
"Jacob siyo nakusimanga nakwambia ukweli, alafu usiseme huna pakuishi we pakuishi papo ila wewe ndo haupo serious kupafanya uishi na kuwaachia wale wapuuzi wajibwede, sasa hapo mjinga nani??" Fatuma alizidi kumchana makavu.

Kutokana na maneno ya Fatuma Jacob alikasirika na kuondoka kwa hasira pale nyumbani, alienda kutulia ufukweni ili apunguze hasira na mawazo.

Jacob akiwa katulia kule ufukweni gafra alimuona Yule mrembo mwarabu anakatisha mbele yake na siku hiyo alikuwa kanoga kuliko Siku zote ambazo Jacob amewahi kumuona.

"Shaifa! We shaifa wewe?" Jacob alianza kumuita na kumukimbilia, Jacob alifika na kumzuia shaifa mbele ili walau wazungumze mawili matatu
"We kijana kwa hiyo huniogopi??" Shaifa aliuliza kwa kutabasamu

"Aaaa!! Naanzaje kukuogopa mrembo kama wewe sasa??" Jacob alijibu kikamanda

"Eeeee!! Sasa mbona mkeo ananiogopa kwa nini wewe??" Shaifa alizidi kumuuliza maswali Jacob

"Dada mi sijaoa bana au ndo unataka kuninyima?? "Jacob naye hakukubali
"Jacob nilishakwambia kaaa mbali nami, siyo kila chakula ni chakula vingine ni sumu ujue"
"Heeeee!! Wanijua mpaka jina langu, sitaki kujua umenijuaje ila mimi sijali kama wewe ni sumu ama laaa ! Mi ukweli shaifa nipo tayari kufa kwa ajili yako na sipo tayari kukukosa" Mwanaume Jacob alijilipua na kutupa ndoano, ila hakutaka kuhoji shaifa kalijuaje jina lake wakati yeye hajawahi kumwambia.

"Jacob nisikilize mimi nishakupenda toka siku ya kwanza nakuona na ni zaidi ya mwaka sijawahi tongozwa na mwanaume na natamka kwamba nakupenda kuliko kawaida ila tatizo mi nakuonea huruma wew na mkeo na ndo maana nakukwepa mno" Shaifa aliongea maneno ambayo yalimfanya Jacob atabasamu maana hakuamini kama ataabiwa na mrembo kama yule maneno yale.

"Shaifa mi nipo tayari kwa lolote lile hata ukisema niachane na Fatuma saa hii naachana naye ili mradi tu niwe na wewe" Jacob alijikuta anaropoka kwa kuchanganyikiwa
"Mi sitaki uachane na mkeo, ila niaahidi utakuwa tayari kwa lolote??" Shaifa aliuliza akiwa serious
"Ndiyo dear ntakuwa tayari kwa chochote" Jacob aliaapa
"Ok nakupenda pia na hili busu nakupa ni mkataba wangu kwako wa kukupenda" shaifa aliongea na kumpiga busu la maana Jacob mpaka mwili wa Jacob ulisisimuka kwa namna ambayo haujawahi kusisimuka tangu azaliwe, na baada ya hapo shaifa alianza kuondoka

"Dear nipe namba basi jamani" Jacob alikumbuka namba baada ya kuona mrembo anaondoka

"Sina simu na situmiagi simu" shaifa akiwa anaendelea na safari alijibu
"Sasa shaifa mi ntakupataje dear si unajua mi siwezi kuishi mbali na wewe??" Jacob akiwa anafuata nyuma nyuma alizidi kuuliza

"Utanipata any time ukinihitaji usijali" shaifa alijibu na kuingia kwenye gari lake ambalo alikuja nalo kisha akasepa maeneo hayo ya ufukweni.
Siku hiyo Jacob alikuwa na raha kupitiliza alisahau hata yale maneno ya kejeli kutoka kwa fatuma masaaa machache yaliyopita.
Basi Jacob alianza kurudi nyumbani akiwa na furaha, Astakafurulah ile Jacob anakatiza kona uso kwa uso na Mama yake mlezi na bahati mbaya siku hiyo Jacob hakuvaa hata Mzuhura wake wa kuzuia uso.

"Heheeee hivi wew ni Jacob au naota!!!??" Mama Jacob baada ya kumuona Jacob mbele yake kwanza aliganda kama kapigwa na shoti alafu alishituka na mavi yalikuwa yanagonga chupi maana kwa asilimia kubwa aliamini ule ni mzimu wa Jacob.
Jacob hakuelewa ajibu nini, ila alimcheki Mama yake na kugundua anatetemeka vya kutosha, Jocob hapo alianza kuigiza kama mzimu alianza kucheka kwa sauti kubwa huku akiwa anamsogelea Mama yake na alikuwa anatoa mate.

Mama yake Jacob mapigo ya moyo yalizidi mwili hatimaye alianguka na kuzimia, baada ya Jacob kuona hivyo alikagua mkoba wa Mama yake alikuta kiasi cha pesa kidogo alikichukua na kukimbia zake.
Mama Jacob aliokotwa na wasamaria wema na kumkimbiza hospitalini.

Jacob naye alikuwa haamini hofu kubwa ilimjaa moyoni, alifika nyumbani akiwa anahema mno.

"We Jacob Mbona unahema hivyo kulikoni??" Fatuma aliuliza baada ya kuona Jacob anahema mno

"Fatuma huwezi amini, leo nimekutana na mother uso kwa uso na ninavyokwambia muda huu nimemuacha kazimia huko maana niliigiza kama mzimu" Jacob alieleze

"Kwa hiyo ndo kinacho kufanya uheme?? Mwanaume mwoga wewe sijawahi kuona na najilaumu kweli kwa nini moyo wangu uliamua kupenda mwanaume mpumbavu namna hii" Fatuma Aliongea kama mtu mwenye kisirani na Jacob

"Heeee! Fatuma sasa hilo ndo limekukasirisha hivi mbona kama ugomvi??" Jacob alishangaa maana aliona ni kitu cha kawaida ila alipo mwangalia fatuma aligundua ni mtu mwenye makasiriko

"Jacob hivi wewe unahisi mimi nina shida sana na wewe si ndo maana yake?? Au unaona mimi mupumbavu kukung'ang'ania wewe na umeona mwarabu ni bora kuliko mimi?? Au umeangalia sura?? Ivi wewe unamjua shaifa vizuri au unafikiri wewe ndo mwanaume mwenye bahati pekee yako kwenye hii dunia kumpata mrembo kama yule?? Sasa nakwambiaje matatizo yako yawe yako usinihusishe na omba maombi damu yako na damu ya shaifa ziendane la sivyo umeyakanyaga" Fatuma aliongea kwa uchungu huku akiwa anatoa machozi na kuingia chumbani.

Jacob hakuelewa maneno ya Fatuma na kilicho mshangaza ni fatuma kamjuaje shaifa?? Na pia kajuaje kama yeye na shaifa washamalizana? na shaifa na urembo ule ana uhatari gani ambao unazungumziwa?, Jacob alijiuliza maswali ila hakupata jibu kamili.

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 19



TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 19.

Jacob hakuelewa maneno ya Fatuma na kilicho mshangaza ni fatuma kamjuaje shaifa?? Na pia kajuaje kama yeye na shaifa washamalizana? na shaifa na urembo ule ana uhatari gani ambao unazungumziwa?, Jacob alijiuliza maswali ila hakupata jibu kamili.

Basi Jacob alibaki katulia pale sebuleni akiwa anajiuliza maswali mengi na hapati majibu.

Basi zilipita kama siku tatu Jacob akiwa hajakutana na shaifa na alikuwa na hamu kweli ya kukutana na shaifa ili amuulize baadhi ya mswali, akiwa ametulia kwenye kochi anawaza namna ya kumpata shaifa na Siku hiyo Fatuma alienda chuoni Jacob alisikia mtu anagonga mlango, alipo fungua uso kwa uso na mtoto mrembo shaifa.

"Heeeeeee!! Shaifa umejuaje kama nakaa hapa??" Jacob alishangaa kumuona shaifa
"Jacob mi nilikwambia hakuna sehemu nisiyo ifahamu kwenye hii dunia hilo likae kichwani mwako" Shaifa aliongea huku akiwa anatabasamu
"Tuondoke kwanza hapa asije Fatuma akatukuta" Jacob alikuwa na wasiwasi kweli
"Hawezi na haji Saiz huyo ni mpaka jioni" Shaifa aliongea kama ni mtu mwenye uhakika.

Basi siku hiyo Jacob na shaifa walipiga story za kila rangi japo kuwa majibu mengi ya shaifa yalikuwa ya utata ila Jacob hakujali.
Basi siku hiyo Jacob alienjoy penzi tamu kutoka kwa mrembo shaifa na aliahidi kutokumuacha mrembo huyo.
Basi baada ya mechi nzito walikaa sebuleni na kuanza kushikana kichokozi na story za hapa na pale na Jacob aliahidiwa mambo mengi mazuri na mrembo huyo.
"Jacob fatuma anakuja saaa hii" wakiwa wanashikana shaifa alishituka na kumwambia Jacob
"We umejuaje anakuja?"
"Jacob mi nishakwambia hakuna kitu nisichokijua kwenye hii dunia" shaifa aliongea kwa msisitizo.
Wakiwa wanaongea hivyo mara walisikia mlango unagongwa kwa nje.
"We nenda kamfungulie tu" shaifa alimwambia Jacob, shaifa baada ya kumwambia Jacob yeye aliingia chumbani.
Jacob hakujali na alijizira liwalo na liwe kama nikufumaniwa na wafumaniwe tu, alienda kufungua mlango alikuwa ni Fatuma.

Fatuma baada ya kuingia alipitiliza chumbani maana alihisi kitu, Jacob mapigo ya moyo yalikuwa yanaenda speed maana alijua shaifa yupo chumbani na huo ndo muda wa famanizi.

Fatuma alifika chumbani huku Jacob akiwa anafuata nyuma nyuma, ila cha kushangaza ambacho kilimuacha hata mdomo wazi Jacob ni kwamba kule chumbani hakuwepo mtu yeyote.

Fatuma baada ya kuto ona mtu alirudi sebuleni na kutulia

"Fatuma mbona sikuelewi? Yaani umetoka huko unapitiliza chumbani bila hata salamu mara unakaa kwa kununa kulikoni??" Jacob alikuwa anajipendekeza maana alijua kashitukiwa tayari ila hakuwa na uhakika kama Fatuma kajua.

"Jacob ivi unanichukuliaje mimi?? Yaani nalipia kodi yangu, chakula changu?? Kila kitu changu unamuleta huyo mjinga wako humu ndani mnafanya ujinga wenu?" Fatuma aliongea kwa hasira kama ni mtu mwenye uhakika na kilichotoka kufanyika

"Fatuma unaongea nini mbona sikuelewi?" Jacob kwa aibu alizuga eti hajui kinachoendelea

"Eeeeee!!! Naongea nini eeeee?? Kwa hiyo we hlujui naongea nini?? Jacob unajitia mjanja sana eee?? Sasa mi nakwambia huyo shaifa mi namjua kuliko wewe unavyo mjua na nilianza kumjua kabla yako! Nakupa home work shaifa si aliingia kule chumbani kujificha nenda kamtafute ukimpata huko chumbani utaendelea kukaa hapa ila usipo mpata ndugu yangu tafuta kwa kwenda mi sitaki ugomvi na mtu kwa sababu inaonekana wewe unakuwa mwema kwenye matatizo tu" Fatuma Aliongea kwa userious na kutulia.
Jacob moyo wake ulikuwa unaenda speed ya helicopter za pakistan zikiwa vitani maana alikuwa haelewi mchezo unao endelea, kwanza alikuwa hamuelewi fatuma ni nani pia alikuwa ashaanza kumtilia mashaka shaifa maana kitendo cha kuingia chumbani na kupotelea huko kilikuwa siyo cha kawaida kabisa kwake.

Jacob aliingia chumbani, alitafuta kila sehemu anapo pajua ila hakuona mtu,hapo Jacob kichwa kilianza kusoma namba za kiebrania maana alikuwa haelewi, aliamua kutoka sebuleni.

"Fatuma naomba uniambie wew ni nani? Na huyo shaifa ni nani na mnajuaje na shaifa mbona kama sielewi??" Jacob aliuliza swali akiwa anatetemeka midomo yake

"Jacob mi sina mengi, si nishakupa home work kama unaona umeshindwa naomba beba kila kinacho kuhusu uondoke mi sina cha kukusaidia maana nilikuwa nakuonya ila ulikuwa unajitia ubabe, na kitu ninacho kuomba usiendelee kuharibu zaidi ya hapa ulipo haribu" Fatuma akiwa kajilaza kwenye kochi aliongea kwa kujibweda na alikuwa hana hata shida ya kumwangalia Jacob usoni.
"Fatuma mbona mi sielewi kinachoendelea??"
"Jacob usitake kunikela eee nimekwambia beba kila kilicho chako uondoke na nakupa dakika kumi la sivyo ntakuitia uwizi" Fatuma alikuwa yupo serious ni hatari.

Jacob alibeba kibegi chake kidgo kutokana na kuvurugwa alisahau hata kuvaa mzuhura wake wa kuzuia sura.

Jacob akiwa njiani haelewi aende wapi, uso kwa uso alikutana na Vicky na ilikuwa haina kukwepana maana kulikuwa hakuna njia nyingine zaidi ya hiyo moja, Jacob alibaki kaduwa haelewi afanye nini, Vicky hakutaka kuzembea alivua sendo zake na kuanza kula speed maana alihisi mwisho wa dunia umefika.
 (mpenzi msomaji hata kama ni wewe, chukulia mtu unajua alikufa na ulithibitisha kabisa kwa kuuona mwili wake, alafu unakuja kupita sehemu unakutana naye we utafanyaje??)
Jacob hapo alijikuta anaanza kupata mashaka maana tayari wale adui zake washaanza kumuona na je wakija kugundua jamaa bado yupo hai hapo ndo itakuwa hatari zaidi kwake.

Jacob akiwa anawaza gafra kuna gari la kifahari lilifika na alikuwa ni shaifa, alimwambia Jacob aingie ndani ya gari waondoke.
Jacob aliona msaada ndo huo, ila alipo kumbuka kile kitendo cha shaifa kupotea kule chumbani kuna kauoga kalianza kumuingia Jacob maana alianza kumshitukia shaifa.
"Shaifa ilikuwaje ukapotea pale chumbani? Mbona sikuelewi na wewe ulijuaje kama Fatuma anakuja muda ule??" Jacob aliuliza huku akiwa anatetemeka.

"Jacob usiwe na wasiwasi utanijua taratibu taratibu mimi ni nani, ila ungemuuliza Fatuma yeye ananijua vizuri mi nani, kwani hajawahi kusimulia kunihusu??" Shaifa alikuwa anaongea huku anatabasamu.

Jacob alitulia mpaka walifika wanapoelekea lilikuwa ni jumba la kifahari sana mpaka Jacob moyo wake ulishangilia kwa furaha kuingia katika jumba hilo.

"Jacob karibu sana" yule mrembo alimkaribisha Mara tu baada ya kuingia
Jacob alishukuru, Jacob aliulizwa atatumia chakula gani Jacob alitaja chakula atakacho tumia yule mrembo alimwambia ngoja niende jikoni nikakupikie, basi shaifa aliingia jikoni, ila Jacob kuna wazo lilimjia sijui lilitokea wapi?. 
Jacob aliamua aende jikoni ili akamsasidie mrembo huyo kupika ili ajiongezee maksi kwa bi dada huyo wa kiarabu, Jacob alipo fika jikoni hakukuta mtu yeyote na hakukuta dalili zozote za kupikwa chakula hapo alianza kushanga na moyo ulikuwa umeanza kumdunda na kwenda speed, alijaribu kuangaza huku na kule ila hakuona mtu, Jacob ilibidi awe mpole alirudi sebuleni na kutulia.

Baada ya kama dakika moja kupita tangu Jacob atoke kule jikoni alishangaa kuona shaifa kabeba chakula kwenye sinia na katokea kule kule jikoni ambako yeye hakuona mtu, hapo Jacob miguu yake ilianza kutetemeka aligundua shaifa siyo binadamu wa kawaida.

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 20.




TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 20.

Baada ya kama dakika moja kupita tangu Jacob atoke kule jikoni alishangaa kuona, shaifa kabeba chakula kwenye sinia na katokea kule kule jikoni ambako yeye hakuona mtu, hapo Jacob miguu yake ilianza kutetemeka aligundua shaifa siyo binadamu wa kawaida.

"Jacob Mbona kama una wasi wasi kulikoni??" Shaifa baada ya kufika na chakula pale sebuleni aligundua Jacob anatetemeka aliamua kuuliza

"Aaaaaa!!!!ahaaaa!! Kwani shaifa hicho chakula umepika wew??" Jacob aliuliza huku midomo ikiwa inatetemeka.
"Jacob Kwan vipi mi siwezi kupika ama?? Ndiyo nimepika mimi nilikuwa nasaidiana na mfanya kazi wangu??" Shaifa alijibu bila wasi wasi.
Jacob hakuamini majibu ya shaifa maana yeye alienda kule jikoni hakumuona mtu alafu yeye anadai katoka kupika, hapo Jacob alinyanyuka na kwenda kule jikoni kwa mara ya pili ili akajirizishe maana aliamini yawezekana alienda sehemu ambako siko.
Ila alipo enda sehemu ile ile aliyo enda kwa mara ya kwanza na hakuona mtu wala dalili za kupikwa kitu, alishangaa kukuta mazagazaga kibao kuonesha kwamba kuna kitu kimetoka kupikwa na alishangaa kumkuta na binti mwingine kule jikoni na ambaye ndo alionekana ni mfanyakazi, na binti huyo alikuwa mzuri ni hatari yaani hakufanana hata kuwa mfanyakazi.
Jacob alitumbua macho na mapigo ya moyo yalizidi mara dufu maana alikuwa haamini mazingaombwe anayo yaona, basi alirudi tena pale sebuleni huku mavi yakiwa yanagonga boxer.

"Kwa hiyo Jacob ulienda kujiridhisha kama kweli nilikuwa kupika ama kuna kitu ulitaka kujua??" Shaifa akiwa anatabasamu aliuliza maana alikuwa ashagundua wasi wasi wa Jacob unatokana na nini

Jacob hakujibu kitu, alizidi tu kutetemeka na mdomo wake ulikuwa mzito kama kafungwa mawe maana alikuwa hapo haelewi chochote.
Jacob hakutaka hata kula kile chakula, maana tayari alikuwa ashamshitukia shaifa.

"Shaifa naomba niondoke basi??" Jacob alijikaza kuongea na kutaka kuondoka maana tayari lile jumba la kifahari lilikuwa lishaanza kumtia mawenge.
"Jacob waweza kuondoka tu kama unapo pa kwenda mi nilikuonea huruma kwa kuwa hukuwa na sehemu ya kwenda" shaifa aliongea kana kwamba ni mtu ambaye hana shida yoyote.

Jacob alianza kuitafuta korido ya kutoka nje na alikuwa anakumbuka kabisa mlango walio ingilia wakati wanakuja, Jacob alizungunguka akiwa anautafuta mlango wa kutokea ila hakuuona yaani alikuwa kila akizunguka anajikuta anatokea sehemu ileile alizunguka Zaid ya masaa tisa akiwa bado anautafuta mlango mpaka alichoka, aliamua kukaa kwenye sofa na kusema liwalo na liwe na muda huo ilikuwa saa saba za usiku.

"Jacob vipi bado upo kumbe mi niljua umeondoka??" Shaifa aliongea akiwa akasimama mlango wa kuelekea chumbani na alikuwa anamtazama Jacob

"Daaaaa! Shaifa hii nyumba mi sijaelewa kabisa nimetafuta mlango wa kutokea sijaona na sielewi natokaje" Jacob alijikaza

"Jacob tatizo lako hukuomba nikuoneshe mlango, haya nifuate nikuoneshe mlango" shaifa aliongea huku akiwa anaongoza mlangoni.

Jacob baada ya kufikishwa mpaka mlangoni alishangaa na kujichekaa kimoyomoyo maana ni sehemu hiyo hiyo amepita zaidi ya mara 20 hajaona mlango, ila mlango ndo upo hapo hapo.
Jacob baada ya kutoka tu mlangoni kilichofanya kazi ni miguu, alikimbia speed za mtu aliyemuona Israel mtoa roho yaani hakukumbuka hata begi lake.
Na kibaya zaidi Jacob alikuwa anakimbia hata hajui anakimbilia wapi maana akili ilkuwa imevurugika kabisa, alikimbia mpaka kwenye jumba la kifahari na akili ilikuwa ishahama kabisa baada ya kufika kwenye jumba hilo aligonga mlango kwa pupa akiwa anaangalia nyuma mara mbili mbili kama Shaifa anakuja, maana aligundua shaifa siyo mtu wa kawaida.
Akiwa kasimama pale mlangoni akili ikiwa haisomi vizuri alikuja kushituka na akili kumrudia baada ya kugundua pale alipo gonga ni kwao yaani ndo pale mr Derick na mama yake wa kumlea wanaisha, maana alipo gonga mlango aliye fungua ni bwana Nguna yule mlinzi wa pale nyumbani.

Jacob baada ya kuona vile alianza kula speed kukimbia,
 pia naye bwana nguna huku nyuma kilikuwa kimeumana maana alimuona uso kwa macho Jacob ambaye aliambiwa kwamba tayari kashafariki

"We Nguna kulikoni usiku huu unapiga makelele unatushitua??" Baada nguna kupiga sana makelele Mr Derick na mkewe waliamka kwenda kujua nini shida maana ilikuwa siyo kawaida

"Boss huwezi amini Jacob kaja hapa, kagonga mlango alafu kakimbia" nguna akiwa anahema alisimulia

"We nguna wewe au ulikuwa unaota?? Jacob katoka wapi?? Ndo maana nakukatazaga kulala ovyo ovyo ukiwa kazini" Mr Derick aliwaka akiwa anajua masihara maana yeye mwenyewe kwa macho yake alimuona Jacob kule magerezani Siku ile akiwa kafariki.

"Boss siyo ndoto hii ni live ujue??" Nguna alisisitiza

"Derick juzi mi nilikusimulia kuhusu kukutana na mzimu wa Jacob we uliona masihara naona sasa huo mzimu umeamua kuja huku huku na unakumbuka hata leo Vicky naye kasema amekutana na Jacob?? Hilo inabidi mume wangu tufanye uchunguzi wa kutosha??" Mama Jacob alitoa ushauri kwa Mr Derick na kumshauli waingie ndani kwa muda huo

"Sawa tutafanya uchunguzi,ila mambo ya mizimu mi huwaga siamini kabisa kwenye maisha yangu, kama ni Jacob basi atakuwa ni yeye kweli na siyo mzimu wake" Mr Derick bado ilikuwa haimuingia akilini kuhusu mambo ya mizimu.

Basi waliingia ndani kuendelea na usingizi maana ilikuwa mida ya saaa tisa usiku kuelekea saa kumi na usiku huo bwana nguna ndo alianza kuichukia kazi ya ulinzi mawazo mengi ya kuacha kazi yalianza kumjia maana alikiona kifo kipo mkononi muda wote

"Au niache kazi, mi wakujikojolea kweli? alafu huyu mpumbavu namusimulia anasema mi naota! Duuu mpenzi wangu Naisa wa kule nyumbani ntamuachia nani nikifa?? Kwakweli hapa ntakufa, ni kuacha kazi kama mizimu imeanza kuninyemelea mwisho wa siku si yatakuja majini kabisa?? Na nasikiaga majini ndo yanapiga ni hatari, sasa hapa kesho nimwambie boss naacha Kazi, Uuuuu!! Kuhusu mshahara Wangu je? Au nimalizie haka kamwezi" hayo yalikuwa mawazo na maswali mengi ya bwana nguna akiwa pale getini usiku huo na moyo wake ulikuwa unaenda speed kali mno na tayari alikuwa ashajikojolea kwa hofu, ilibaki tu haja kubwa.

Huku kwa Jacob alikuwa bado anaendelea kukimbia na alikuwa haelewi wapi anaenda maana mitaa aliyo kuwepo zilikuwa nyumba za kifahari tupu, kiufupi ulikuwa mtaa wa matajiri.

Jacob akiwa anakimbia aliona gari mbele yake inakuja hapo alisimamisha ili aombe msaada na hakujali atakuwa nani, kweli gari lilisimama na Jacob alisogea ili aombe walau msaada, lakini cha kushangaza aliyekuwa anaendesha gari hilo ni mrembo shaifa na alikuwa anatabasamu vya kutosha, Jacob hakuamini alibaki katumbua macho kama kabanwa korodani na mkasi.

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 21.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu