Mpya
Hadithi: MAJARIBU
Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)
Sehemu: 17
Basi ilipo Fika Jioni! Jedi alionekana anaelekea Gerezani! Na kwenye kile kipindi hakwenda na alitoa taarifa kwamba ana dharura imejitokeza!
Jedi baada ya kufika Gerezani aliomba kuonana na Melisa! Ni kweli mwanamama Melisa alikuwa kachoka Muno! Yaani alikuwa Siyo Melisa yule wa kutingisha wowowoo!! Mpaka kumdatisha Mr Luka!.
"Eheee we mwanaidhaya unataka nini, wewe si ndo ulishirikiana na yule mpuuzi kutufunga Sisi, ila kabla hujaongea lolote msiombe tukatoka hapa mtajuta!"! Melisa kwanza aliongea Kwa hasira baada ya kumuona Jedi!.
"Haina haja ya Yote hayo Mimi nataka tushirikiane! Nataka kesi Yote abebe Mama mchungaji na nyie muachiwe Huru, ila Sasa Kwa sharti Moja!" Jedi alizungumza, basi Melisa macho yalimtoka baada ya kusikia maneno yale matamu!.
"Unasema kweli!? Eheee kitu gani hicho Kwanza unataka nikusaidie!?" Melisa akiwa anaamini maneno ya Jedi aliuliza, hakika Jera Siyo kuzuri yaani Melisa alipo pewa fursa ile ya kuwa Huru uso wake gafla ulichangamka!.
"Sikiliza nataka unisaidie kumpata mtoto halisi wa mchungaji Nemeke!?" Jedi aliongea!
"Nikusaidie kivipi!? Na ili iweje!?" Kwanza Melisa aliuliza!.
"Unajua nataka tutengeze mazingira Mama mchungaji achukiwe na washirika wote pale kanisani, yaani tukimpata tutatangaza kwamba Nemeke alikubaliana na Mke wake kwamba wazae nje na kweli walizaa na hapo ndo itatakiwa tumuoneshe mtoto mwenyewe!" Jedi alitunga maelezo yaliyo enda Shule na ya uongo!.
Kwa maelezo yale Melisa aliamini kabisa Jedi anataka kufanya kitu juu ya Mama mchungaji, yaani hakufikiria tofauti!.
"Kiukweli niseme ukweli! Yule mtoto nilikuwa namlea Mimi kwenye nyumba Yangu ya Siri ambayo nilikuwa nimepewa na mchungaji Nemeke! Na Mimi pale nilikuwa sishindi Mara Kwa Mara Bali nilikuwa nimeajiri tu mdada wa Kazi ambaye ndo alikuwa anafanya kila kitu, ila kuna mambo yalitokea mpaka mtoto yule alitoroshwa na mdada wa Kazi!, Kipindi hicho Mr Luka alikuwa kapata mtoto na mdogo Wangu Naya, kwakuwa mchungaji Nemeke alikuwa hajawahi muona mtoto wake hata sura na hajui yupoje zaidi ya kutuma tu matumizi na Vitu Vingine! Mr Luka alinishawishi kwamba yule mtoto wa Nemeke tumuue alafu mtoto wake na Naya ndo achukue Nafasi, maana Mr Luka alikuwa hataki familia yake ijue kwamba kazaa nje, pia alikuwa anaona ni njia nzuri ya mtoto wake kuja kurithi Mali za Nemeke!.
Ila nilipo mpelekea wazo lile Dada wa Kazi yule alipinga kabisa, na Mimi nilimwambia ikifika Jioni kama hataki aondoke akatafute kazi kwingine Mimi ntatafuta Mtu mwingine!.
Kitu Cha kushangaza Dada yule aliamua kutoroka na mtoto, Bahati nzuri alikuwa hajui yule mtoto kama ni wa mchungaji Nemeke, maana huwenda angejua angepeleka taarifa Kwa Nemeke! Lakini yeye alipotea na mtoto Moja Kwa Moja mpaka Leo hii tunavyo zungumza wote sijawahi kumuona Huyo mtoto na baada ya hilo tukio tuliona ile ndo fursa ya kumpa mtoto wa Mr Luka na Naya nafasi ya kuwa mtoto wa Nemeke!." Melisa alitoa maelezo ambayo yalizidi kumchoma Jedi! Maana Huyo mtoto ambaye alikuwa anazungumziwa alikuwa ni mtoto wa Dada yake!.
"Kwani vipi huyo mwanamke unaye sema alikuwa mfanyakazi wako alikuwa anatokea wapi!" Jedi aliuliza! Na Melisa alimtajia Kijiji aliko mtoa huyo mdada na pia alimtajia Jina la mdada huyo kwamba alikuwa anaitwa Zoha!.
Jedi aliondoka pale Gerezani akiwa na machungu kweli kweli maana alikuwa anaona Jinsi mtoto wa Dada yake anavyo teseka na maisha!.
Muda huo upande wa Pili Kwa Mama mchungaji na Wale wengine ambao wote walikuwa wametoa Pesa za kutosha Kwa Jedi kutokana na vitisho vyake walikuwa wamekaa kikao kizito ndani ya Hotel Moja ya kifahari!.
Yaani kila Mtu alikuwa anaongea Kwa jaziba na hasira Kwa kitendo ambacho Jedi kawafanyia, maana ni dhahiri Kwa pesa ambazo walikuwa wamempa walikuwa wanaelekea kufirisika!.
Mama Mchungaji yeye alikuwa kabakiwa na mjengo tu na gari kama mbili tu pale nyumbani! Yaani Miradi yote alikuwa kauza na pesa kumpatia Jedi ili Siri iendelee kusimama!.
Kundi hilo walipanga mipango ya maangamizi, yaani ilikuwa ni mipango ambayo walikuwa wanataka wahakikishe kwamba Jedi haponi.
Siku kadhaa zilipita Huku Jedi akiwa anazidi kupeleleza kuhusu huyo mtoto wa Dada Yake!.
Aliamua kusafiri mpaka huko Kijijini ambako aliambiwa huyo Dada ndo alikuwa anatokea, yaani ambako Dada huyo alikutana na Melisa!.
Siku Hiyo Jedi aliuliza Sana Jina la Zoha pale Kijijini!, Ila wengi wao walionekana hawamjui Dada huyo!.
"Unamuuliza Zoha yupi, aliyekuwaga Mke wa Fudi Miaka Iliyo pita!?" Bahati nzuri katika kuuliza alikutana na Mama ambaye alionekana anamjua vyema Dada huyo.
"Mama kiukweli kisura simjui ila atakuwa ndo huyo Huyo!" Jedi alijibu!.
"Heeeee ni Muda Sana ila ni kama nilisikiaga tetesi kwamba amefariki! Unajua Zoha alikuwa ameolewa na Jirani yetu, wawili hao Sijui walishindwana nini baada ya hapo Zoha nilisikia aliondoka na mwanamke mmoja Hivi alikuwa ananunua nunua mazao na walienda wote Mjini, tangia Siku hiyo sijawahi muona tena!" Mama yule alitoa maelezo ambayo yalizidi kufifisha jitihada za Jedi!.
"Kwani huyo Zoha kwao ni hapa hapa Kijijini!" Jedi aliuliza, basi yule Mama alimtajia Kijiji anacho tokea Zoha kilikuwa ni Kijiji kama cha Tano kutokea pale Kijijini, ila Jina la Kijiji hicho Jedi alikumbuka kwamba amewahi kulisikia Kwa kijana Majaribu wakati anamhadithia Stori ya maisha yake!.
"Duuuuuu ningekuja na dogo Majaribu si ingekuwa rahisi maana alisema anatoka Kijiji hicho hicho, ila asingekubali napo maana alisema anawindwa vibaya Muno!" Jedi alijiongelesha mwenyewe, baada ya hapo alimshukuru yule Mama na alianza safari ya kuelekea huko Kijijini akiwa na pikipiki!.
Ulikuwa mwendo wa Nusu Saa tu na pikipiki Jedi alifika!.
Aliuliza watu wawili tu, Watatu alionekana anamjua huyo Zoha!
"Kiukweli Zoha unaye muuliza atakuwa Ndo Huyo huyo, ila bahati mbaya ashafariki Muda Sana" Jedi alipewa Maelezo ambayo yalifanya aanze kuhisi huwenda Siyo huyo anaye mtafuta!.
"Zoha alifariki! Kwani hajawahi kwenda Mjini huyo Zoha!?" Jedi aliuliza!.
"Mjini tena, huko si ndo alitoka na majanga! Yaani Zoha alitoka Mjini akiwa kamuiba mtoto Sijui wapi, sijui alikuwa wake sijui wa nani, ila Kwa maelezo ya wale Ambao walikuwa wanamuona Zoha Huko Mjini ni kwamba Yule mtoto alimuiba" mtoa maelezo alitia maelezo ambayo yalimkuna Jedi kidogo!
"Sasa Mama Huyo mtoto vipi bado yupo!" Jedi aliuliza!.
"Haaaa hata Sijui Yuko wapi! Yaani huyo mtoto alikuwa ni Mwizi balaa, alikuwa ni Mwizi viwango vya dunia, ujue baada ya Zoha kufariki, mtoto yule akiwa mchanga kabisa, alimuachia Bibi yake! Maana Zoha alilelewa na Bibi tu Kwa hiyo Bibi huyo ndo aliye mlea huyo mtoto!"
"Heeeee!! Bibi huyo vipi bado yupo!?" Jedi alizidi kuuliza maswali!.
"Kwani we unatokea dunia gani Baba, mbona unauliza watu ambao washafariki! Huyo Bibi Zoha aliuawa na wanakijiji Kwa hasira, baada ya kuwa mjukuu wake amehusika kwenye Wizi wa mifugo hapa Kijijini!" Mama yule alitoa maelezo ambayo yalifanya Jedi azidi kupagawa, maana alianza kuhusianisha ile Stori na Stori ambayo alikuwa kahadithiwa na Majaribu kule Mjini!.
"Mama swali la mwisho! Huyo mtoto wa Zoha alikuwa anaitwa nani na anafananaje, ujue Mimi nauliza Kwa sababu ni Baba wa Huyo mtoto!" Jedi aliuliza Kwa upole!.
"Ahaaa Kumbe! Si ungesema mapema Sasa, Kwa hiyo nyie kwenye ukoo wenu muna Damu ya Wizi! Maana tangia dunia iumbwe na nizaliwe nilikuwa sijawahi kuona mtoto Mwizi kama Majaribu, yaani alikuwa Mwizi pia ana machale alikuwa hajawahi kamatwa! Kama kweli we ni Baba yake, basi Baba hongera maana Wizi ule uuuuu!!" Mama yule alitoa maelezo ambayo yalifanya Sasa Jedi athibitishe kabisa Kwamba kumbe mtoto ambaye alikuwa anamtafuta Siku zote ni yule Yule ambaye anaishi naye kila Siku! Hakika Jedi hakuamini maajabu ya Mungu yalivyo! Na kweli alipo vuta picha ya jedi kichwani aliona kuna kaufanano kidogo na marehemu mchungaji Nemeke!.
Jedi kwanza ilibidi aulize na wengine kuthibitisha ile taarifa na Kweli kila Mtu alikuwa anatoa maelezo yale yale!.
Jedi alianza safari ya kurudi Mjini Huku akiwa na furaha Kweli kweli! Yaani kichwani Mwake alikuwa kapanga Bonge la surprise ya kwenda kumpatia Majaribu kama mjomba yake!.
Mida ya Saa Moja za Jioni ndo Muda Jedi Ndo alikuwa yupo na pikipiki yake Huku akiwa anarudi Mjini na earphones zikiwa masikioni anakula Mziki Kwa Mbali, Lakin Bahati mbaya kumbe alikuwa analiwa rada, Yaani Kwa Jinsi ambavyo Mama mchungaji na watu wake walikuwa wamejipanga walitafuta mpaka wataalamu wa kompyuta, walitrack Simu ya Jedi ni wapi ilipo, na waligundua kwamba ipo maeneo ya vijijini!.
Kitu walicho kifanya waliamua kumsubiri kwenye Moja ya kamsitu kadogo ambako Kalikuwa kapo Karibu na Mji walijua lazima apite tu pale!
Ni kweli ikiwa ni Mida ya saa mbili kasoro za usiku Jedi alionekana akiwa anakuja na pikipiki yake! Jedi akiwa anaendesha pikipiki Mara gafla Mtu alijitokeza mbele na kusimama!.
Jedi alipunguza mwendo na hapo ndipo alipo kosea stepu,
Jedi alisikia tu mlio wa Risasi baada ya hapo alihisi kama kitu Cha baridi kimepita kifuani mwake, pale pale nguvu zilimuishia na alidondoka kwenye pikipiki, huku pikipiki ikimfuata juu!.
Risasi nyingine ilipigwa, ilipita kwenye shingo ya Jedi! Muda huo mwanga wa gari ikiwa inakuja ulimurika na ulifanya wale magaidi wakimbie na kupotelea Porini!.
Ipi hatima ya Jedi!? Je atapona awamu hii!! Au ndo Bahati huwaga haiji Mara mbili!!?
Tukutane sehemu ya 18
Hadithi: MAJARIBU
Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)
Sehemu: 18
Risasi nyingine ilipigwa, ilipita kwenye shingo ya Jedi! Muda huo mwanga wa gari ikiwa inakuja ulimurika na ulifanya wale magaidi wakimbie na kupotelea Porini!.
Gari ile ilisimama baada ya kuona mwili wa Mtu Chini huku Damu zikiwa zinatapakaa Chini! Alikuwa ni Baba mtu mzima na Mke wake! Basi wawili hao walipiga Simu polisi kutoa taarifa ile!.
Ndani ya dakika ishirini tu askari walikuwa wamefika eneo la tukio Kwa sababu kutokea maeneo yale mpaka mjini ilikuwa Siyo mbali Sana!.
Askari baada ya kuchunguza waligundua Bado Jedi anapambana na nafsi yaani alikuwa hajafa kabisa!.
Haraka haraka walimkimbiza hospital ya rufaa pale Mjini!.
Yaani ndani ya dakika chache tu tayari taarifa zilikuwa zimeanza kuripoti mtandaoni na kwenye vyombo vya habari!.
Kijana Majaribu akiwa katulia nyumbani huku Jicho lipo kwenye TV Mara alishangaa breaking News! na taarifa zilikuwa zinahusu kushambuliwa Kwa Jedi huku ikielezwa Hali yake kuwa mbaya!.
Majaribu alijikuta Jasho jembamba limeanza kumtoka Muda ule ule! Kwanza alizama chumbani alichukua Simu maalumu ambayo ndo ilikuwa na ushahidi pia na flash disk kisha alitia kwenye begi la mgongoni, na aliondoka pale nyumbani, yaani Kwa Jinsi alivyo kuwa kachanganyikiwa alisahau mpaka kufunga milango na kuzima TV!.
Bahati iliyoje Kwa Majaribu wakati anatoka tu pale nyumbani! Nazo njemba kama Tano zilifika kumaliza Kazi, yaani Kwa Namna walivyo mpiga Jedi walikuwa wanaamini hawezi kupona Kwa Hiyo aliye kuwa kabakia ni Majaribu tu!!.
Majambazi wale walimsaka Majaribu nyumba nzima Bila mafanikio!, Muda huo Majaribu alionekana hospital ya rufaa huku akiwa anataka kuingia chumbani aliko pelekwa Jedi, Lakini askari walimzuia kwamba hawezi kuingia!.
Lakini Majaribu akiwa analeta vurugu mbele ya askari huku akiwa anazuiwa na kutulizwa, Mara daktari alitoka kwenye chumba kile Cha Dharura!.
"Vipi jamani kuna Mtu anaitwa Majaribu atakuwa kafika! Maana mgonjwa Hali yake mbaya Muno anamuhitaji huyo Majaribu Kwa Namna yoyote ile kama hayupo tusaidie tumpate!" Daktari yule alitoa maelezo! Basi Majaribu alijitaja kwamba ndo Yeye! Hapo ilibidi askari wamruhusu kuingia, ila askari mmoja naye aliingia na kukaa mlangoni akiwa anaangalia ilimladi Majaribu asije akafanya lolote Kwa mgonjwa, maana kwenye matukio ya Mauaji kama Yale hakuna Mtu anaye kuwa anaaminika!.
Baada ya Majaribu kufika pale kitandani! Jedi alimuonesha ishara ya kwamba amsogelee, na kweli Majaribu alisogea, Basi Jedi alimkumbatia Kwa hisia Muno!.
"Uuuu!! Uuuuu uncle!!!" Jedi akiwa kwenye hali mbaya alitamka maneno hayo na kumfanya Majaribu asielewe!.
"Bro unasemaje! Sijakusikia!" Majaribu aliuliza tena!.
"Ma!ma!ma! Majaribu! we!we!wewe Ndo mtoto wa Dada Yangu! Nili! nili! nilikuwa nakutafuta! Mimi!!mimi! Mjomba yako!!" Kwa taabu pumzi zikiwa zinakata Jedi aliongea! Kwanza Majaribu macho yalimtoka kama kaona sijui mdudu gani!.
"Heeeee inamaana unataka kusema Mimi ni mtoto wa Marehemu mchungaji Nemeke!?" Majaribu aliuliza! Lakin hakupata Jibu maana tayari Jedi alikuwa kapoteza maisha, yaani Kwa Hali ambayo alikuwa nayo hata yale maneno machache alijitahidi Muno kuyatoa!.
Majaribu alipiga ukunga,yaani Sauti ya Juu na alizimia pale pale Kwa presha, maana alikuwa kamzoea Jedi kuliko Kawaida pale Mjini! Na alikuwa hana Mtu mwingine anaye juana naye Zaidi ya Jedi!.
Askari na madaktari walizama Mule ndani na kumtoa Majaribu kumpeleka chumba kingine Kwa ajili ya huduma ya kwanza!.
Jedi baada ya kuthibitika kwamba kapoteza maisha, basi ilibidi wafanye mpango wa kumpeleka mochwari! Kwanza walichukua Vitu ambavyo alikuwa Navyo na kuvitunza!.
Ilikuwa ni Simu, kadi ya benki na Pesa kidogo ambazo walizikuta mfukoni!.
Majira ya Saa kumi na Moja alfajiri ndo Muda Ambao Majaribu aliziunduka! Kwanza baada ya kuzinduka kilio kilianza upya akiwa anamlilia Jedi , hakika kijana alilia Kwa uchungu Muno!.
Basi Majaribu alipewa ile Simu na Kadi ya benki ambavyo vilikuwa ni Vitu vilivyo kutwa Kwa marehemu, na walimpatia Majaribu Kwa sababu ilisadikika ndo ndugu yake pekee aliyepo!.
Hakika msiba ulikuwa mkubwa Muno Kwa Majaribu! Yaani machungu yake ulikuwa usipime, Haswa machungu yalizidi pale alipo kumbuka maneno ya Jedi kwamba kumbe yeye ndo mtoto ambaye alikuwa anatafutwa! Yaani Majaribu ilimuuma kumjua mjomba Yake Siku ya Mwisho!.
Basi kushirikiana na Jamii pamoja na Serikali na askari Jedi alizikwa Huku askari wakiahidi kuwasaka walio husika kwenye Kifo kile Kwa Jasho na Damu!.
Wiki Moja ilipita Majaribu akiwa anaishi Kwa mawazo na uoga mkubwa, Pesa kwake haikuwa Tatizo Kwa sababu kadi ya benki alikuwa nayo na Namba za Siri alikuwa anazijua vyema, tena akaunti ya benki ilikuwa na pesa ambazo Siyo za kuisha Leo wala Kesho, maana Mama mchungaji na wenzake walikuwa wameingiza Pesa za kutosha baada ya kutishiwa na Jedi!.
Miezi miwili iliisha Huku Majaribu akiwa anaishi Kwa mawenge yaani alikuwa hatulii sehemu Moja, Leo kalala hapa kesho pale na hiyo ilikuwa ni kutokana na Namna ambavyo alikuwa anasakamwa na watu wasio julikana, na alikuwa anajua watu wanao msakama ni kina nani!.
Siku Hiyo ikiwa ni mchana Majaribu akiwa kakaa kwenye Hoteli Moja huku akiwa anapata chakula kuna wazo lilimjia pale pale! Yaani gafla tu alipata wazo ambalo aliamini ni Bonge la wazo Kwa upande wake!.
Muda ule ule alienda kwenye kituo Cha Television! Baada ya kufika alielezea kile kilicho mleta, kwakuwa zilikuwa ni taarifa nyeti ambazo kituo hicho Cha TV kiliamini zitatrend waliamua kumpatia Majaribu nafasi ya kufunguka hewani!.
"Majaribu Karibu! Unaweza kuelezea kile kilicho kuleta ambacho unataka wanachi wakijue kutoka kwako!? Maana inasaidikika hapo awali ulisingiziwa kifo Cha Mchungaji Nemeke! Vipi kuna kitu kingine kipya ambacho unataka kukizungumza!?" Hilo lilikuwa swali la mtangazaji! Muda huo Mama mchungaji akiwa nyumbani kwake alitumiwa meseji na Mtu kwamba afungue TV!.
Kile alicho kiona Mama mchungaji alitamani TV ipasuke azame akamchomoe Majaribu, yaani alikuwa anaona dogo anaenda kuropoka kila kitu! Jasho jembamba lilikuwa linamtoka Mama Huyo kila sehemu!.
Upande wa huku Aliko Majaribu baada ya kuulizwa swali hilo kwanza alivuta pumzi!.
"Najua Watu wengi hawataamini, ila wachache wanao Jua wataamini! Mimi ni mtoto pekee wa marehemu mchungaji Nemeke!" Kijana Majaribu alifunguka, kwanza mtangazaji mwenyewe alishituka maana alikuwa anajua Nemeke alikufa pasina mtoto!.
Basi Majaribu ilibidi aanze kufunguka mwanzo mwisho! Yaani alielezea kila kitu Mpaka Namna alivyo singiziwa kuua!.
"Ujue baada ya Mkewe kugundua kwamba Mimi ni Mtoto wa Nemeke, Huku mchungaji Nemeke akiwa anataka kuuweka ukweli! Na Uchungaji aache! Mkewe na baadhi ya waumini wachache ambao walikuwa wanajua waliamua kumuua Baba Yangu na kunisingizia Mimi ili wanipoteze, na baada ya kufanya hivyo walimtafuta mtoto bandia na waligawana kundi zima Mali za Baba Yangu!, Jedi alikuwa ni mjomba Yangu kabisa na baada ya kugundua kwamba mjomba Jedi ana mpango wa kuanza kudai Haki Yangu! Ndo hapo waliamua kumuua na ni hao hao! Wakibisha ntaleta ushahidi, pia hata Mimi nawindwa muda wote Kwa sababu washajua kwamba naujua ukweli!." Majaribu alimwagika kila kitu akiwa anachanganya na uongo!.
"Una uhakika na maneno yako!? Upo tayari vipimo vya DNA vikafanyike endapo Wapelelezi watasema wakafukue Mwili wa mchungaji Nemeke!" Mtangazaji aliuliza swali!.
"Hata Sasa hivi nipo tayari! Mimi sitaki Mali ila nataka Haki, kama ni Mali ningekuwa nishadai Kwa sababu Baba Yangu alinipa nyaraka zote na hati Zote za Mali Zake, mpaka nyumba anayo kaa Mama mchungaji saizi ni Mali Yangu ila sina Shida ya kufuatili, mpaka Kadi za benki za Baba Yangu aliniachia na Mali zake zote za Siri na zisizo za Siri nazijua ila nipo kimya, Kwa Hiyo Shida Siyo Mali, bali ni ukweli!" Majaribu alikuwa anaelezea Kwa mpangilio tena Kwa hisia isivyo kawaida!.
Hakika Siku hiyo Mitandao ilichafuka! Yaani picha ya marehemu mchungaji Nemeke ambaye alikuwa maarufu nchi nzima, pamoja na picha ya Majaribu vilianza kulinganishwa, na kweli baada ya watu kuziweka pamoja ule mfanano wa Majaribu na Nemeke ulionekana Mpaka baadhi ya watu alianza kucomment kwamba haina haja Hata ya vipimo!.
Mtaani ndo ulikuwa usipime, baadhi ya waumini pale kanisani ambao walikuwaga wanasikia taarifa za Chini chini kwamba Nemeke kazaa nje, nao walianza Sasa kuthibitisha kwamba wamewahi kusikia!.
Mama mchungaji Maji yalikuwa yamezidi unga yaani alikuwa kachanganyikiwa isivyo kawaida, alikuwa anaona Sasa habari yake kwisha!.
Alikusanya baadhi ya Vitu vyake vya msingi baada ya hapo aliona Sasa ule ni Muda wa kukimbia Mjini, yaani alikuwa anataka aende mbali kabisa!.
"Revina Muda wowote ntakupigia Simu kuna maelezo ntakupatia Sawa eee! Wacha Mimi nikimbie kujiokoa Kwanza!" Akiwa kachanganyikiwa Mama mchungaji alitoa Maelezo Kwa Revina!.
"Sasa Boss Kwa nini usijiamini, hapo Wewe ni kutafuta mwanasheria mzuri unakanusha tu tuhuma za Yule mtoto! Wakati huo utakuwa unatafuta timing ya kumuua, mbona hujiamini!" Revina alitoa ushauri Ambao Mama mchungaji alipo upima aliona ni bonge la ushauri!.
Muda huo huo makele yalianza kusikika nje, yalikuwa ni makelele ya waumini wakiwa wanaandama kwamba Mama Huyo atoke nje! Yaani walikuwa wanataka atoke Nje aje aongee ukweli!
Je nini Mama mchungaji alisema!?? Ipi hatima ya Yote!?
Tukutane sehemu ya 19
Hadithi: MAJARIBU
Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)
Sehemu: 19
Muda huo huo makele yalianza kusikika nje, yalikuwa ni makelele ya waumini wakiwa wanaandama kwamba Mama Huyo atoke nje! Yaani walikuwa wanataka atoke Nje aje aongee ukweli!
"Rehema toka nje! Tunasema toka nje!"
Ilikuwa Sauti nzito ya Baba Mtu mzima!.
Basi ni kweli Mama mchungaji alitoka nje Huku mwili mzima ukiwa unatetemeka, ila kabla hajaanza kuelezea chochote Mara defenda ya askari ilifika pale nyumbani! Yaani Mama mchungaji alibebwa Juu Kwa juu na kutupwa kwenye defenda huku Watu wakiwa wanashangilia!.
Mama mchungaji alifikishwa pale kituoni! Alipo angaza Macho pembeni alimuona mtoto Majaribu yupo pale kituoni!.
Basi Mama huyo alianza kuulizwa maswali, kila kitu alicho ulizwa alikana kuhusika hata Majaribu alisema hajawahi kumuona Kabla na hajui kama ni Mtoto wa Nemeke!
Kwanza ilibidi Mama mchungaji afungiwe Kwa ajili ya mahojiano zaidi! .
Kijana Majaribu aliruhusiwa aondoke baada ya kutoa maelezo ambayo yalitakiwa kwamba ayatoe!
Ila kabla Majaribu hajaondoka aliomba azungumze kwanza na Mama mchungaji na kweli aliruhusiwa!.
"Kuna machaguo mawili either nitoe video zote uende ukafie Jera, au uthibitishe kwamba Mimi ni mtoto wa Nemeke alafu huo ushahidi nisitoe na wewe uwe Huru!" Majaribu alimnong'oneza Mama Mchungaji, baada ya hapo aliondoka hakutaka hata majibu ya Mama mchungaji kwamba kakubali au kakataa!.
Siku nyingine Mama mchungaji alibananishwa ili atoe maelezo yaliyo nyooka!.
"Jamani ngoja niseme ukweli!, Ni kweli Majaribu ni mtoto wa Nemeke wa kumzaa! Ila kuhusu kifo Cha Nemeke Mimi sikuhusika kabisa na kipindi anauawa Mimi nilikuwa India kutibiwa Mguu kila Mtu anajua hilo, na pia kama ni Kesi ya Mauaji, wauaji washapatikana na walikili wenyewe!" Mama mchungaji aliamua kufuata kile ambacho Majaribu alikuwa anakitaka!.
Basi kwakuwa Majaribu hakutoa ushahidi wowote ambao ulimuonesha Mama mchungaji kwamba ni Muuaji, ilibidi Mama huyo aachiwe Huru, ila ndo hivyo ukweli ulijulikana kwamba Majaribu ni mtoto wa Nemeke!.
Mama mchungaji baada ya kutoka tu alipo fika nyumbani kwake alimkuta Majaribu katulia kajiachia hana hata wasiwasi!.
"Kwa Hiyo kilicho kuleta huku nini!? Si tushamalizana!" Mama mchungaji baada ya kumkuta Majaribu pale kwanza ilibidi aulize!.
"Mimi nipo nyumbani! Kwenye nyumba za Mzee Wangu! Kwa Hiyo kila Mtu afanye Yake tusifuatiliane na ukileta ufukunyuku nakutimua Kwa sababu hati ninayo Mimi na ipo Kwa Jina Langu!" Majaribu alijibu Kwa kujiamini tena bila uoga wowote!.
"Okay unajifanya mjanja eeeee! Subiri Dawa Yako inachemka!" Mama mchungaji akiwa na hasira alitoa kitisho!.
"Okay!! Ila tayari nishaweka maelezo kituoni, najua nyie ndo mlimuua uncle Jedi, Kwa hiyo lolote litakalo nikuta nishawaambia askari kwamba ni nyiee mnahusika!" Majaribu akiwa kajimwaga kwenye sofa alitamba!.
Mabishano yale yakiwa yanaendelea Mara mlango uligongwa na Muda huo Revina ndo alikuwa anatoka chumbani, kwa Hiyo ilibidi yeye ndo apitilize kwenda kufungua mlango!.
Astakafrurahi! Yaani kila Mtu alibaki kakodoa Macho na kubaki anashangaa Kwa kile alicho kiona! Alikuwa ni Mr Luka na Melisa wamefika! Yaani walikuwa wapo Huru tena wakiwa wanatamba!.
"Heeeee hii inawezekana vipi!? Yaani inawezekana vipi mbona sielewi!?" Mama mchungaji akiwa kaacha mdomo wazi aliuliza huku macho yakiwa yameganda pale mlangoni!.
"Unashangaa Nini!! Ulijua tutafia Gerezani!? Pesa haishindwi na Jambo, Sasa Kwa taarifa Yako Vita inaanza upya, tunakupongeza Kwa kumuua Yule kijana ila Sisi na wewe hatujamalizana!" Mr Luka akiwa anaonekana ana kisasi ndani yake alichimba bonge la mkwara!.
Mama mchungaji alibaki kanywea huku akiwa mdogo kama pilitoni!.
"Dogo na Wewe kaa Makini! Na usikatize kwenye anga zetu lasivyo huu mwezi humalizi! Pia Mali zote ambazo zinashikiriwa na Serikali tusipo zipata inakula kwenu!" Mr Luka alizidi kuchimba mikwara!
Yaani Luka na Melisa walimwaga mikwara kama yote baada ya hapo waliondoka!.
Mama mchungaji kwanza ilibidi aende Moja Kwa Moja mpaka Gerezani ambako alikuwa kafungwa! Na taarifa alizo kutana nazo ni kwamba katika orodha ya walio samehewa na raisi basi na Majina ya Lukas na Melisa yalikuwepo! Kwanza Mama mchungaji alibaki anashangaa kwamba inawezekana vipi ikatokea hiyo, ila ndo hivyo ukweli ni kwamba walikuwa wapo Huru!.
Siku kadhaa zilipita kila Mtu mtaani alikuwa anajiuliza hao watu wametokaje tokaje wakati walipimiwa Miaka mitano na hata Miaka miwili hawajamaliza! Ila ndo hivyo kila Mtu alibaki kuguna hakuna ambaye alikuwa ana Majibu!!
Majaribu baada ya kugundua kwamba kumbe Pesa ndo kila Kitu na pesa Ina nguvu zaidi ya sheria na Pesa ndo Haki yenyewe aliamua Sasa naye kufanya Jambo!.
Majaribu alikuwa na zaidi ya billion Moja kwenye akaunti, Pesa ambazo Mama mchungaji na wenzake walikuwa wameingiza baada ya kutishiwa maisha na Jedi!
Majaribu alianza naye kutengeneza Timu yake, maana aligundua anawindwa Muno yaani alikuwa haishi Kwa Amani!.
Siku Hiyo Katika kukatiza katiza Majaribu alikutana na Wahuni kama watatu wakiwa wamembananisha Baba mmoja kwenye uchochoro wanampora!, Kwanza baada ya Majaribu kuwaona bila hata kuogopa alifika mpaka pale!.
"Oya dogo umejichoka eee! Ebu sogea hapa!" Basi kuna kijana ambaye Kwa makadirio ni kama Miaka 18 aliongea Kwa kukoroma huku akiwa kashika dispisi, maana waliona ni kama Majaribu anataka kuwaharibia!.
"Oya Wana Mimi nina michongo ya Pesa ndefu! Alafu Mimi ni Mwizi niliye pita viwango acheni kuiba miambili! Tuliza kende niwape michongo!" Majaribu akiwa anajikubali aliongea kihuni tena Kwa mizuka! Wale Majaa walitazamana, waliona kama dogo yupo serious hivi, kwanza ilibidi wamuachie yule Baba wa Watu! Hakika yule Baba alitoka mbio ambazo hazina mfano huku akiwa anamshkuru Mungu!.
"Dogo usilete madili ya kichoko Sasa maana watu wenyewe tushavurugwa na maisha!" Basi kuna Jamaa mmoja ambaye alikuwa anaitwa Feno aliongea, na alionekana ni kweli ana maisha magumu isivyo kawaida!.
"Vipi muna Roho ngumu Lakini na mpo tayari Kwa Kazi!?" Majaribu aliuliza!.
"Ilimladi isiwe Kazi ya magumashi, Wewe lete mchongo!"
"Okay kwanza mnaishi wapi!? Tunaanzia hapo kwanza!?" Majaribu aliuliza! Wale wahuni walikuwa hawana noma walimpeleka mpaka magetoni wanako ishi, ilikuwa ni uswahilini kuliko maelezo! Alafu ndani ya geto la wahuni hao ni mabox tu yalikuwa yametandikwa Chini kama Vitanda!.
Kitu Cha kushangaza Majaribu alipo angalia kwenye Kona aliona kuna kameza! Juu ya kameza kulikuwa na mavitabu alafu pia kulikuwa na cheti kipo juu ya madaftari yale!.
"Duuuuuu nyie kweli noma yaani mnapora mpaka vyeti!" Majaribu akiwa anakagua kile cheti alijiongelesha!.
"Oya hicho changu mhuni Wangu Usinione hapa nilipo! Nimepiga kitabu Sema michongo tu imegoma ajira zenyewe ndo kama hivyo!" Basi kuna Jamaa ambaye alionekana ni mkubwa Kwa wale wengine aliongea!.
Pia wale wengine Kwa maelezo yao walikuwa wanasoma ila katika mazingira magumu wakaishia njiani, mmoja akiwa kaishia kidato Cha Nne, mwingine kidato Cha Sita!.
"Oya dogo tupe mchongo Sasa maana naona unatupeleleza Sana yaani!" Basi kijana wa kuitwa Feno aliongea .
Majaribu aliona wale wanamfaa Sasa kwenye kazi zake! Yaani alikuwa anataka ale Jino Kwa Jino na kina Mr Luka, maana aliona unyonge hautasaidia chochote!.
"Okay twende zetu! Kama Mtu unaona kuna kitu Cha Mhimu Chochote beba kabisa! Maana hapa ndo tunahama hivi!" Majaribu aliongea! Kwanza wale Jamaa walikuwa hawaelewi kabisa! Walitazamana! Na kukonyezana kwamba huwenda ni Zari la mentali!.
Kila Mtu alichukua kile anacho ona kinamfaa safari ilianza!.
Kituo Cha kwanza Majaribu aliwapeleka shopping na kuwaambia wachague pamba zozote wanazo zitaka na wapendeze!.
Kwanza Wale Jamaa watatu Ambao alikuwa Feno, Fred pamoja na Liam walishangaa, walihisi kwanza Labda Majaribu anawafanyia mtego anataka wanaswe, yaani waliulizana Mara mbili mbili!.
Basi ilibidi waaanze shopping hakika walichagua pamba na walipendeze, baada ya hapo Majaribu aliwapeleka kwenye Bonge la Hoteli kula chakula! Yaani Siku Hiyo akina Feno walihisi wanaota!.
Ilipo Fika usiku walielekea mpaka pale kwenye nyumba ambayo ilikuwaga ya doctor Lameck na ni Muda Majaribu alikuwa hajakaa pale kutokana na kuogopa!.
"Oya mdogo wetu ebu tupangilie kabisa mazingira! Maana naona umetufanya tuonekane watu miongoni mwa watu Kazi ipi unataka kutupatia!" Fred aliuliza.
Majaribu kwanza ilibidi aanze kuwasimulia kuanzia Moja mpaka mwisho kila Kitu alisimulia!.
"Heeeee mbona kazi kitonga Hiyo! Kwa hiyo kifupi unataka tuwe Walinzi wako au machawa wako Siyo!?" Liam aliuliza Kwa mizuka!, Maana maelezo ya Kazi waliyo pewa ilikuwa tofauti na matarajio yao! Wao walihisi watapewa hata Dili la kwenda kuuwa!.
"Yes hiyo ndo maana yake!" Majaribu alijibu.
"Mdogo wetu hapo pigia mstari kuanzia Sasa Sisi ni familia hakuna mpuuzi atakaye kuzingua! Yaani mipango iwekewe mezani tuanze kazi!" Feno naye alidakia Kwa mizuka! Hakika Siku Hiyo wale Jamaa walifurahia kupita maelezo, walilala mazingira mazuri Haswa!.
Asubuhi na mapema Kwa umoja wao walitoka pale nyumbani Huku Majaribu Lengo likiwa ni kwenda kwenye shoo ya Magari ili anunue Gari Zuri, Lakin wakati wanatoka pale Getini kuna Gari nyeusi ilikuwa imepaki Kwa mbaali!.
"Oya wanangu mnaona ile Gari nyeusi! Bila Shaka wananiwinda, yaani wanatafuta kuniua na Mtu anaye fanya hivyo lazima ni Mr Luka na Siyo mwingine!" Majaribu aliongea
Je Ipi hatima ya Vita hii ambayo inaonekana inaenda kuwa vita ya uso Kwa uso!
Tukutane sehemu ya 20
Hadithi: MAJARIBU
Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)
Sehemu: 20
"Oya wanangu mnaona ile Gari nyeusi! Bila Shaka wananiwinda, yaani wanatafuta kuniua na Mtu anaye fanya hivyo lazima ni Mr Luka na Siyo mwingine!" Majaribu aliongea
"Majaribu tuliza mizuka wale mbona Cha mtoto tu, nyie tuiteni tax tuondoke Namna ya kuwanasa mbona rahisi tu!" Basi Liam alitoa wazo, na kweli walifanya hivyo waliita taxi na kuondoka!.
Ile gari ilianza kufuata nyuma!, Baada ya mwendo wa kama dakika ishirini Liam na Feno walishuka, kwenye taxi alibaki Fred na Majaribu! Na safari iliendelea! Ile Gari ilizidi kufuatilia nyuma!.
Liam na Feno walichukua taxi nyingine na kuanza kulifuata lile Gari Kwa nyuma, yaani kifupi lile gari liliwekwa kati!.
Majaribu na Fred baada ya kufika kwenye shoo room ya Magari walishuka na kuzama ndani! Ile Gari nayo ilifika pale Jamaa kama watano walishuka kwenye ile Gari na kuzama ndani!.
Liam na Feno baada ya kufika pale walikuta ile Gari imepaki na wale Jamaa wameshuka na kuwafuatilia kina Majaribu kule ndani, maana lilikuwa ni eneo kubwa!.
Liam na Feno walicho fanya ile Gari ya wale majamaa walitoboa tairi baada ya hapo nao walizama ndani! Basi walikuta wale Majaa watano wakiwa wanachungulia chungulia!
"Wahusika Vipi mbona Hawa majamaa hapa wanachungulia chungulia bila shaka watakuwa wezi!" Feno aliongea Kwa Sauti! Basi mabaunsa ambao walikuwa wanafanya Kazi maeneo yale walikuja!.
Wale Majaa baada ya kuona kimenuka walichoropoka Mule ndani na kuanza kukimbia, kufika kwenye Gari lao walikuta Gari limetoblewa tairi, yaani kifupi wale Jamaa walijishitukia wenyewe maana hata wasingekimbia walikuwa hawana kosa kubwa hivyo, ilikuwa ni kitendo tu Cha kubisha, ila wao ni kama walipaniki!.
Yaani kila Mtu alipita njia yake na Gari lao waliacha pale pale!.
Basi Siku hiyo Majaribu alinunua Gari Zuri la kutembelea na Mtu ambaye alikuwa anajua kuendesha Gari kati yao alikuwa ni Liam tu!.
Siku zilizidi kusogea ulikuwa ni mwendo wa kuwindana tu, Mr Luka na Melisa walikuwa wanataka wamalizane na Majaribu kwanza ndo wamgeukie Mama mchungaji ambaye waliamini hana maajabu yaani ni kama kumung'unya ubuyu!.
Majaribu naye alitafuta vijana wengine wawili Ambao nao aliwakuta katika mazingira ya kutatanisha, ila awamu hii walikuwa ni wadada tena wakiwa wadogo wadogo Miaka kama 18 tu!.
Majaribu na Timu yake baada ya mipango kukamilika waliona Sasa ni Muda wa wao kuanza kushambulia maana Muda wote wao walikuwa ni watu wa kusakamwa na kuwakwepa majamaa!!.
Siku Hiyo ilikuwa usiku majira ya Saa Saba za usiku! Majaribu aliondoka pale nyumbani na kijana Feno tu, maana katika wote Feno ndo alionekana walau mjanja na ana Mbinu tena anajiamini!.
Safari yao ilienda kuishia mpaka kanisani, lilikuwa ni kanisa kubwa Muno ambalo lilikuwa lipo Katikati ya Mji!.
Siku hiyo Majaribu aliona ndo Siku sahihi ya kwenda kuchukua Siri ambazo mchungaji Nemeke alikuwa kaziacha!.
Kanisa lilikuwa limejengwa kisasa kabisa tena vioo vilikuwa vinawaka waka kila sehemu! Milango ilikuwa imefungwa na kufuri nzito tena ile milango ya Chuma!.
Majaribu na Feno walitoa funguo zao ambazo zilikuwa funguo zaidi ya hamsini, yaani hakika walikuwa wamejipanga, kila Aina ya ufunguo walikuwa nayo, mpaka funguo za vitasa walikuwa Nazo!.
Majaribu alitekenya kidogo tu kufuri lilikubali na walifanikiwa kuzama ndani!.
Kanisa lilikuwa linatisha utafikiri Siyo kanisani! Feno na Majaribu walielekea mpaka madhabahuni, walivuta sofa ambazo zilikuwa zipo pale mbele!.
Ilikuwa ni ngumu kugundua kama Chini pale kuna Chochote kama huna wazo lolote, ila Kwa sababu Majaribu alikuwa anajua pale Chini kuna kitu baada ya kuona kuna sehemu kama papo tofauti na sehemu zingine alianza Sasa kupambana Namna ya kufungua pale, baada ya kushindwa ilibidi waanze kutindua Kwa nyundo, maana walikuwa wana kila dhana!.
Kwenye kutindua walifanikiwa maana kuna sehemu ilibonyea na pale palikuwa na kashimo ambako Kalikuwa kamewekwa bahasha kubwa!.
Majaribu alichomoa ile bahasha ambayo ilikuwa imefungwa vizuri! Ila kabla hata hawajarudishia yale masofa ili waondeke, Mara Sauti kutokea mlangoni zilisikika!.
"Leo nimekubamba! Nimekufuatilia Siku nyingi Muno Nadhani leo nimefanikiwa, hapo hapo mlipo wote mikono Juu!" Ilikuwa ni Sauti ya Mr Luka ambaye alikuwa kafika pale kanisani na vijana wake kama wanne pamoja na Melisa ambaye alikuwa anatembea naye kila sehemu, kasoro akiwa anaenda kwake!.
"Shiitiiii! Wamejuaje hawa wajinga!" Majaribu alijiuliza kwamba wamejuaje kama wao walikuwa wanakuja pale! Lakin Mara gafla wale mabinti wawili Ambao Majaribu aliwasaidia na kuwafanya vijana wake Mara nao walizama Mule ndani wakiwa wanacheka huku Meno yote yapo nje!.
Kumbe walikuwa ni Watu wa Mr Luka ambao walitumia plani ya mbele zaidi ili kujua hatua zote!.
"Heeeee hawa wajinga Kumbe ndo maana plani zetu zote zilikuwa zinafeli!" Feno alijiongelesha lakini ndo hivyo walikuwa hawana Namna, maana walikuwa wamekamatika tena!.
Mr Luka alikuwa anajiona Sasa kashinda mchana kweupe! Lakin kabla hawajafanya Chochote! Mara umeme ulizima eneo lote la pale kanisani na Giza Nene lilitawala!.
Gafla ving'ora vya polisi vilisikika vikiwa vinakuja maeneo yale ya kanisani!.
Mr Luka alikuwa kachanganyikiwa aliwasha Simu akiwa anataka kumuangaza Majaribu Yuko wapi ili achukue chake akimbie!.
"Boss tukimbie askari wanakuja!" Kijana mmoja wa Mr Luka alizungumza na kweli Mr Luka aliona wacha ajiokoe Kwanza!, Yeye na Watu wake walikimbia, baada ya hapo Majaribu na Feno nao walitoka kama mishare Mule kanisani!! Yaani wakati wanatoka tu nao askari ndo walikuwa wanafika waliona tu vichogo vya watu wanaishia vichochoroni!!.
Majaribu mapigo ya Moyo yalikuwa yanaenda Kasi Muno, yaani alikuwa anamshukuru Mungu Mara mbili mbili Kwa kupona kwenye mkasa ule!.
"Feno unadhani nani atakuwa katusaidia!?" Wakiwa njiani Majaribu alimuuliza Feno!.
"Uuuuu Sina uhakika Lakini watakuwa ni kina Fred!" Feno alijibu, na kweli walipo Fika nyumbani walikuta Liam na Fred wamekaa Mguu pande!.
"Wapuuzi nyie mngedakwa! Duuuuuu ujue Bora Sisi tulibakia hapa, maana ingekuwa msara!" Baada ya kufika tu Liam aliongea! Na alianza kuzungumzia Mkasa mzima!.
"Ujue mlivyo ondoka tu, tuliwaona wale mademu nao wanaondoka tena waliondoka mwendo wa kunyata, kiukweli tulipata mashaka ilibidi tuwafuatilie, walipo Fika nje walipiga Simu sehemu na kuanza kuondoka! Tulifuata nyuma tuligundua wanakutana na Yule Mr, baada ya hapo walianza kuja uelekeo wa pale kanisani na tuliwaona wakifika kabisa kanisani!.
Hapo ilibidi Sasa tufanye Jambo tulipiga Simu polisi kutoa taarifa maana tuliona Sasa Yule Jamaa atatuzidi na vile ulisema ana Mguu wa bata kiunoni ndo tulihofia!!.
Ila bado tuliona askari ni kama watachelewa kitu tulicho amua ni kukata waya ambao umeunganishwa na pale kanisani! Kwa Hiyo Ndo hivyo!."Liam alitoa maelezo!.
Basi walipongezana Kwa Kazi nzuri.
Majaribu baada ya kuangalia ndani ya bahasha kulikuwa na hatimiliki za biashara nyingi tu pale Mjini, mpaka zingine Majaribu alibakia anashangaa kama ni Mali za Mchungaji Nemeke! Kwa mfano kulikuwa na kampuni kubwa ya Michezo ya ubashiri na kamali ilikuwa ni Mali ya Nemeke na ilikuwa Siri! tena ilikuwa ni kampuni kubwa tu!.
Pia kwenye bahasha ile kulikuwa na kadi ya Benki ambayo mchungaji Nemeke alikuwa anaweka Pesa zake ambazo alikuwa anazipata Kwa njia ambayo siyo ya Halali na maelezo ya akaunti yalikuwa yameandikwa kabisa!.
Siku Iliyo fuata Majaribu Sasa ndo alianza kutumia kufuru ya Pesa, maana hata kwenye ile kadi alikuta kuna Pesa za kumwaga, Kwanza hati zote na nyaraka zote aliweka Jina lake, Majaribu Nemeke! Kila hati ilikuwa inasomeka hivyo!, Baada ya hapo Majaribu alienda kituoni kulalamika kwamba anataka Mali za Baba yake zote zirudi mikononi Mwake na ili jambo lake liende Kwa uharaka alimwaga Pesa ya Kutosha!.
Siku Hiyo Mama mchungaji akiwa kajibweda pale pale kwenye mjengo anapiga Stori na Revina! Mara kijana Majaribu alifika akiwa kaongozana na Jamaa Zake!.
"Mama mchungaji Kwa heshima yako unapewa Siku mbili uwe umehama hapa Kwangu, na nakupa Ofa beba kila kinacho bebeka, unacho ona kinakufaa!" Hayo yalikuwa maneno ya Majaribu, Mama mchungaji kwanza alicheka Kwa dharau akiwa anataka aanze kumjibu Majaribu, kijana Majaribu alioondoka wala alikuwa hataki kusikia Majibu ya Mama Huyo yapoje kikubwa alikuwa katoa Siku mbili!.
Majira ya usiku yalipo wadia Majaribu akiwa na vijana wake pamoja na Vijana wengine wa kuwakodi tu walivamia nyumbani Kwa Mr Luka, tena Kimya Kimya! Bahati mbaya Siku hiyo Luka alikuwa Kalala Kwa Melisa akiwa kamdangaya Mke wake kwamba amesafiri!.
Baada ya uvamizi pale nyumbani Kwa Mke wa Mr Luka, pale nyumbani walifanikiwa kuwakuta watu kama watano, mmoja alikuwa mdada wa Kazi wawili watoto wa Mr Luka mmoja Mke wake na mwingine mdogo wa Mr Luka!.
Vitisho Ambavyo Majaribu alivitoa Kwa Mke wa Mr Luka huku akitishia kumuua mtoto wake mmoja, vilifanya mwanamke Huyo akimbie chumbani kwenda kuchukua hati ya nyumba yao na kumpatia Majaribu! Na ni nyumba Moja tu Mr Luka alikuwa nayo na ilikuwa ya kifahari kupita maelezo!.
Baada ya kupewa hati Majaribu aliondoka na Watu wake, yaani kijana Majaribu alikuwa kaamua kama mbwai na iwe mbwai! Yaani ni ubaya ubaya tu!.
Asubuhi Mr Luka alipo Fika nyumbani taarifa alizo kutana Nazo zilifanya aende kituoni kupeleka taarifa ya uvamizi wa Majaribu pale kwake!.
Na kweli kijana Majaribu aliitwa, awamu hii Majaribu alikuwa anaheshimika Kwa sababu askari karibia wote walikuwa wamekula Pesa yake, Kwa hiyo walikuwa hawaendi kumkamata bali walikuwa wanampigia na kumuomba aje kituoni! Yaani kifupi Pesa zilikuwa zinaongea! Mpaka Mr Luka alishangaa kwamba kapeleka malalamiko mazito kama yale ya uvamizi alafu mharifu haendi kukamatwa Bali anaitwa tena Kwa kuombwa!.
Majaribu ni kweli alifika kituoni, zile shutuma zote aligoma!.
"Ujue Afande Huyu bwana akili hana na anahisi huo ujanja ujanja wake utamsaidia Mimi nisipate Mali Zangu, kifupi ile nyumba anayo ishi ni Mali Yangu kihali, na nilimpatia Siku mbili awe amehama, Sasa kutapa tapa anaona atumie hiyo plani!" Majaribu aligeuza maelezo ambayo yalifanya Mr Luka abaki katokwa na Macho!.
"Dogo naona unanipanda kichwani! Ntakuuwa we mjinga Wewe! Hunijui eeee ntakumaliza mjinga Wewe yaani nyumba Yangu unasema Mali zako tena usije rudia huo ujinga wako na hati Yangu naitaka!" Mr Luka Sasa alijikuta kaanza kutumia hasira huku akiwa amepaniki.
"Afande Nadhani kapaniki huyo hasira zikiisha Mimi ntakuja asije akanimeza, ila mwambieni nampa Siku mbili sitaki kumuona kwenye nyumba Yangu, kwenye hilo Sina msamaha!" Majaribu akiwa serious aliongea maneno ambayo yalizidi kumpandisha Sumu Mr Luka.
Mambo yashaanza kumpalia Mr Luka je ipi hatima yake!??
Tukutane sehemu ya 21
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Write your comment