Mpya
Hadithi: MAJARIBU
Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)
Sehemu: 13
"Baba usifanye hivyo, Siyo Kwamba Mimi simuonei huruma huyo mtoto ila Sasa ushahidi huo mlio nitumia unatufunga wote! Ntawezaje kuwakata!!?" Mama mchungaji alikuwa anaongea Huku anatetemeka, Kama ni Maji yalikuwa yamefika shingoni!.
"Sikiliza Ninavyo Sema Wewe hutahusika nina maana Yangu, nina ushahidi Ambao haikuhusu wewe na unawaonesha tu Luka na mwenzake kwamba ndo wanahusika!" Jedi aliongea na alimuonesha Mama mchungaji video fupi na baadhi ya Audio ambazo yeye alikuwa hahusiki!.
Walau kidogo baada ya kuona hizo video alijua Kumbe inawezekana na aliona pia ule ndo Muda wa kulipa kile ambacho Luka na mwenzake wamemfanyia, yaani aligawana Mali na mtoto ambaye Siyo Damu ya Nemeke!!.
Basi wote Kwa pamoja walipanga mipango yao na waliweka ile iwe Siri baina ya watatu! Mipango Mingi waliizungumza.
Basi Jedi na Majaribu walirudi mpaka pale nyumbani Kwa Lameck kimya kimya, ila bahati mbaya Siku Hiyo kumbe Watu walikuwa wameandaliwa kuja kuwachukua kija Jedi pale nyumbani na kuwapeleka maeneo ya maficho ili wakafanywe ndafu!.
Jedi na Majaribu walipo fika tu waliona kuna Gari kama mbili zimepaki pale getini!.
Kwanza ilibidi wajifiche ili kuangalia kinacho endelea!.
Baada ya kama dakika Kumi njemba kama Kumi zilitoka ndani zikiwa zimetuna Kwa hasira huku Lameck akiwa anawasindikiza!.
"Daaaah!! Sijui wameenda wapi!, Yaani Sijui wamegundua ila sidhani kama wamegundua kitu! Wakirudi basi tutawasiliana!"Lameck aliwasindikiza Wale Jamaa na maneno ya kuwatia Moyo!, Wale Jamaa waliondoka na Lameck aliingia ndani!.
Masaa yalisogea Huku Lameck akiwa hana usingizi kabisa yaani alikuwa anawasubiri kina Jedi Kwa Hamu Muno pale sebuleni!.
Baada ya Masaa kadhaa kukiwa kunakaribia kucha! Jedi na Majaribu ndo walifika pale nyumbani tena wakiwa hawana hata wasiwasi kama hawajui lolote vile!.
"Kwa Hiyo Wanangu mpo kwenu au Siyo mnajitokea tokea tu usiku, haya mmetoka wapi!? Au ndo nafuga magaidi Humu ndani!?"Lameck akiwa na hasira aliuliza.
"Aaaaaa si unajua Sisi mchana kutembea Jau Kwa Hiyo usiku ndo tunajiachia kidogo! Mwanangu nilikuwa kutembelea sehemu ambayo demu Wangu alikuwa anaishi nilitaka nijue yupo au hayupo!" Jedi alitoa maelezo!.
"Yaani nyie wapuuzi kweli Kwa hiyo mnataka kila Mtu ajue mpo hai Sasa, kama mademu washaanza kujua" Lameck aliongea Kwa kulalamika na ukali ila Jedi na Majaribu walitulia kinyonge, maana Siku zote wanasema Mtu kwake!.
Basi kwakuwa kulikuwa kunakaribia kukucha Lameck aliona haina haja ya kuwaita wale Jamaa waje pale nyumbani.
Hatimaye palikucha na ilifika mchana huku pirika pirika pale mjini zikiwa zinaendelea huku na Kule, Muda huo Mama mchungaji alionekana akielekea kwenye Moja ya chombo kikubwa Cha habari, tena chombo Cha Serikali kabisa!.
Basi Mama mchungaji alielezea Shida yake na alipewa Nafasi Siku hiyo Hiyo maana waliona ile ni taarifa ya kuwapeleka Mjini!.
Basi ikiwa ni Mida ya Saa Tisa alasiri! Mama mchungaji alianza kufunguka alielezea Jinsi alivyo enda India na kukuta Mumewe kauawa, pia wasiwasi wake juu wa wauaji!, Na alitaja wahusika wa kifo Cha Mchungaji Nemeke kwamba ni katibu wa kanisa Melisa pamoja na katibu wa Jimbo, pia alienda mbali na kuwaumbua wawili hao kwamba ni wapenzi wa Siri Japo kuwa Mr Luka alikuwa na familia!.
Mama mchungaji aliplay baadhi ya Audio pale na kusisitiza kwamba anazo nyingi tu! Na yupo tayari kwenda kutoa ushahidi mahakamani!.
Na pia aliutumia Muda ule kuomba radhi Kwa Majaribu na familia yake huko waliko pia na watu wengine walio athirika na maamuzi yale ya kikatili Kwa mtoto Majaribu!.
Baada ya kumaliza kutapika maneno yote, kwanza Mama mchungaji alitoka pale studio Mwili mzima ukiwa unatoka Jasho, Yani alikuwa anaogopa isivyo kawaida, alikuwa anaona kama ndo kalikoroga zaidi!.
Mama yule hakwenda kwake Moja Kwa Moja bali alienda Hotelini Huku akiwa na hofu!.
Mtandao ulikuwa umechafuka kuhusiana na zile taarifa! Yaani kila Mtu alikuwa anaropoka lake mtandaoni! Wengine wakiwa wanasema mahakama walikula rushwa, wengine wakiwa wanasema wahusika wanyongwe! Kama tujuavyo mambo ya Mitandao!.
Upande wa Huku Kwa Mr Luka Moja ilikuwa haikai, mbili haikai yaani alikuwa anajamba Mara mbili mbili, alikuwa haelewi ashike lipi aache lipi, kwanza Mke wake na watoto wake walikuwa washamjua kwamba kumbe Malaya tu Kwa kuchepuka na Melisa, Kwa hiyo hata Nyumbani kulikuwa hukukaliki!.
Mr Luka alielekea nyumbani Kwa Melisa akiwa kachanganyikiwa, yaani nywele zilikuwa zinawasha, kufika Kwa Melisa kwanza alikuta mwanamama huyo kazimia huku mdogo wake Naya akiwa anampepea!.
"Heeeee Mama Habir vipi Dada yako imekuwaje tena!?" Mr Luka aliuliza!.
"Unauliza nini Sasa Kwani we huoni, ujinga wenu ona Sasa kinacho tokea, na Labda nikwambie Luka mwanangu Habir akipata matatizo yoyote haaa utanijua Mimi nani! Malaya mkubwa Wewe! Uliona Mimi sikutoshi ukaamua kumganda Dada Yangu! Ebu kwanza mpepee Malaya mwenzako hapo" Naya ambaye alikuwa mdogo wake na Melisa aliongea!.
Kifupi Naya alikuwa kazaa na Mr Luka mtoto anaye itwa Habir na wawili hawa walizaa kama bahati mbaya, yaani Mr Luka enzi hizo akiwa bado kaoa alikuwa na mahusiano na Melisa kama kawaida, na Siku Moja alienda Kwa Melisa na alikuta Dada Huyo kasafiri na aliye kuwepo nyumbani ni Naya tu! Basi kama tujuavyo Tamaa hazimuachagi Mtu salama! , Mr Luka alimtamani Naya na kulala naye! Siku ya kwanza tu Mimba iliingi!.
Wawili hao walianza mahusiano ya Siri mpaka pale ilipo kuja kugundulika Naya ana Mimba Mr Luka ndo aliamua kukata mahusiano!.
Baada ya Muda Dada Mtu alijua kila kitu na aliachana na Mr Luka, mpaka mtoto Habir anazaliwa Mr Luka alikuwa kaachana na wote wawili yaani Melisa na Naya! Ila baada ya Muda Melisa alijikuta anarudi kwenye mahusiano na Mr Luka mpaka majanga haya yanatokea walikuwa wapo kwenye mahusiano, ila Luka alikuwa kazaa na Naya!.
Nadhani mpenzi Msomaji tumeeelewana,basi baada ya Luka kukuta Melisa kazimia ilibidi aanze kusaidiana na Naya kumpepea mpaka mwanamama Yule alizinduka!.
"Jamani tumekwisha, Luka tumekwisha tunafanyaje Sasa!?" Melisa alikuwa anaongea huku analia na kutetemeka Mwili mzima!.
Mr Luka naye alikuwa haelewi Moja wala mbili!, Kwanza akiwa kapaniki Muda ule ule alishika Simu yake na kuanza kujirekodi huku akiwa anakanusha zile tuhuma za Mama mchungaji!.
Yaani alikuwa anaongea huku akijichanganya mwenyewe! Maelezo yake yalikuwa hayaeleweki kabisa yaani alikuwa anaenda mbele anarudi nyuma! Akiwa kapaniki vile vile alirusha ile video aliyo rekodi kwenye Mitandao!.
Ila Muda ule Ule askari kama saba Hivi waliingia ndani! Bila huruma walikamata kila Mtu pale ndani, yaani Melisa, Luka mpaka Naya naye alibebwa!!.
Mr Luka na wenzake walifikishwa kituoni, na Mr Luka alikuwa anajiamini Kwa sababu alikuwa anajua Mkuu wa Kituo ni Mtu wake Kwa Hiyo Mambo hayatakuwa mengi!.
Ila baada ya kufika pale kituoni alipo uliza kuhusu Mkuu wa kituo aliambiwa bwana Huyo kasimamishwa na kufunguliwa kesi kadhaa wa kadhaa, maana iligundulika ni Mtu anaye kula rushwa!.
Muda huo Lameck alionekana yupo sipidi anarudi nyumbani maana alikuwa kachanganyikiwa baada ya kuona zile taarifa! Yaani alikuwa anaona Naye atafikiwa tu! Maana Yeye ndo aliye kuwa kahusika na kifo Cha Jamaa pale hospital na Kesi kupewa Jedi!.
Lameck baada ya kufika nyumbani alikuta Jedi na Majaribu wanacheza zao karata huku wakiwa hawana wasiwasi, yaani kama hawajui lolote hivi!.
"Jedi nyie ndo mumempa Mama mchungaji zile Sauti na ushahidi mwingine!?" Baada ya kufika pale nyumbani Lameck alianza kufoka!.
"Lameck unaongelea Nini mbona hatukuelewi!?" Jedi aliuliza kana kwamba hajui lolote!.
Mambo yameanza kuchangamka, Kipi kitajiri!??
Tukutane sehemu ya 14
Hadithi: MAJARIBU
Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)
Sehemu: 14
"Lameck unaongelea Nini mbona hatukuelewi!?" Jedi aliuliza kana kwamba hajui lolote!.
"Naongelea nini inamaana Wewe hujui lolote!?" Lameck alijikuta anauliza maswali ambayo hayana Miguu wala kichwa, yaani Kwa alivyo paniki alijikuta hata Siri zake anataka kuzimwaga!.
"Ndo uniambie Mimi Sijui lolote"
"Huuu usenge! Ebu bebeni Vitu vyenu muondoke Kwangu, sitaki wanafiki Kwangu" Lameck akiwa haelewi lolote aliongea!.
"Lameck wanafiki Sisi au wewe!?" Majaribu aliona haina haja ya kujivunga vunga aliamua kuuliza tena Kwa Sauti kavu!.
"Dogo unasemaje! Yaani upo Kwangu unasema Mimi mnafiki!?"
"Ndiyo Wewe mnafiki, Wewe ulituleta hapa Kwa Ajili ya nini!? Ulituleta kama msaada au Kwa manufaa yako!?" Majaribu aliuliza!.
Kwanza Lameck lile Swali ndo lilizidi kumchanganya kabisa, yaani alijikuta haelewi hata aulize nini!.
"Ni!! ni! nini!? Unasema nini!? Manufaa kivipi!?" Lameck akiwa na kigugumizi aliuliza!.
"Lameck sikiliza Sisi tuna akili kuliko zako! Siyo kwamba hatujui kwamba yule Jamaa pale hospital wewe ndo ulimpa Sumu akafa tunajua vyema na ushahidi wa kila kitu upo mpaka ulipo kuwa unapewa kazi ya kumuua na Mr Luka, yaani mipango yenu Yote ushahidi upo, pia tunaweza kujitokeza hadharani tukaelezea Jinsi ulivyo tumia taaluma yako kututorosha Gerezani na pia ushahidi upo, Kwa hiyo kaa Kwa kutulia ukituchokoza tu unaenda kunyea Debe kama Mr Luka!! Bora utulie na ibaki Siri yako!."Jedi aliamua kufunguka kila kitu, yaani Lameck alijikuta anakaa kwenye kiti Kwa kuchoka, yaani alikuwa anajiona mjanja kumbe hamna lolote,
"Jamani naombeni mnifichie Siri Yangu nipo tayari kuwapa chochote kile mnacho taka" akiwa anatetemeka Lameck aliongea!.
"Lameck nina ushahidi wa madudu yako yote upo kwenye Simu Yangu na flash pia au unataka nirushe kwanza mtandaoni hata Moja ujue kweli ninao!?" Mr Jedi alizidi kumtishia Lameck! Na ukweli Jedi hata huo ushahidi hakuwa nao, ila kwakuwa Lameck alikuwa anajua ni kweli aliyafanya hayo aliamini ni Kweli!.
Kijana Lameck alikuwa muoga kupita kiasi, yaani Kwa Uoga tu alijikuta anajikojolea maana alikuwa analiona Jera lile pale!.
"Jedi ntawapa chochote semeni niwape Nini!?" Lameck akiwa anatetemeka aliuliza!.
"Haya unazo Pesa shilingi ngapi kwenye akaunti yako?" Jedi aliuliza!.
"Kiukweli zipo million Saba tu" Lameck alijibu, basi Jedi aliona Hizo zinatosha wakati anataka kumwambia awape hizo pesa, kijana Majaribu alidakia na kuropoka!.
"Tunacho taka ni hii nyumba ndo tutanyamaza na Wewe utapona, kalete hati za nyumba hapa " Majaribu aliongea Kwa userious mpaka Jedi mwenyewe alishangaa kwamba dogo kumbe mafia vile, yaani Majaribu alikuwa na Sifa ya Wizi haswa, maana Mwizi anapo chukua kitu chako huwaga haweki huruma mbele na kujiuliza Wewe utaishije!.
Kwa Namna ambavyo Lameck alikuwa kachanganyikiwa alikimbia haraka chumbani kwenda kuleta hati Miliki ya nyumba tena orijino kabisa, na alimkabidhi Majaribu, Muda huo Jedi alikuwa katulia anaangalia shoo za Majaribu!.
"Okay chukua kila unacho ona kinafaa hapa ndani hama na uende sehemu ambayo hatutaonana! Maana tukikuona tu hasira zitakuja upya, yaani hata ukituona wewe tukwepe na usije ukarudi tena hapa maana hapa Siyo kwako tena" Majaribu aliongea maneno ya kikubwa tena maneno makavu na Kwa herufi kubwa!.
Lameck akiwa kachanganyikiwa alikusanya Vitu vyake vya muhimu na nguo zake alitia kwenye begi kubwa, baada ya hapo alipakiza kwenye pikipiki na kuondoka zake, yaani alikuwa anaona afadhari, ila wasiwasi wake ulikuwa Mr Luka akimtaja itakuwaje, maana alikuwa anahisi Mr Luka atapewa kipigo mpaka ataje anao shirikiana nao!.
Ni kweli kama alivyo hisi upande wa Huku kituoni, Mr Luka na Melisa walikuwa wanakula kipondo isivyo kawaida!.
"Jamani naombeni niongee na Mkuu wa kituo" Mr Luka akiwa anapigika aliomba mkuu wa Kituo aitwe, maana bwana Huyo alikuwa anaamini katika rushwa!.
Muda huo upande wa nje ya kile kituo ikiwa ni Saa Moja Jioni watu walikuwa wameandamana na kujazana, Haswa wale waumini wa kanisa lile! Walikuwa wanataka haki itendeke ipasavyo!.
Kama alivyo mhitaji! Mkuu wa kituo alifika pale alipo karishwa Mr Luka kumsikikiza na Mkuu Huyo alikuwa yupo serious vibaya Muno, kwanza Sura tu ilikuwa inaonesha ni Mtu wa Kazi!
"Boss ningeomba tuongee faragha kidogo!" Mr Luka alimuomba mkuu huyo kwamba askari wengine waondeke!.
"Mr Luka naona unatengeneza mazingira ya rushwa, kwa taarifa yako Mimi sinaga tamaa ya Mali, nilizo nazo zinanitosha, maana hata mshahara ninao pokea huwaga natoa Kwa Yatima, Haki itafuata Mkondo!" Mkuu yule ambaye Sura yake ilikuwa na makovu na ngeu za kutosha alizungumza, yaani Sura yake ilikuwa inasadifu kwamba ni Mtu asiye na huruma Kwa mharifu!.
Kiukweli Melisa na Luka walipigwa Siku Hiyo!.
Melisa uvumilivu ulimshinda kipigo kilikuwa kikubwa kwake, alijikuta anaropoka kwamba nikweli waliuwa Lakini walishirikiana na Mama mchungaji! Yaani aliamua Sasa ni Bora wote wakose!.
Mr Luka kwakuwa mwenzake alikuwa kakubali naye alikuwa hana budi alijikuta anakili kwamba walimuua mchungaji Nemeke!.
Siku Hiyo ilipita! Ikiwa ni asubuhi na mapema kabisa! Askari wa kutosha Walifika nyumbani Kwa Mama mchungaji! Bahati mbaya walimkosa maana Mama huyo alikuwa kalala Hotelin Siku Hiyo!.
Revina naye Bahati mbaya hakuwepo yaani walimkuta tu mlinzi wa getini!.
Wakiwa wanataka kuondoka Mara Mama mchungaji alifika pale na Gari yake! Yaani alidakwa juu Kwa juu na wale askari! Moja Kwa Moja alipelekwa mpaka kituoni kutoa Maelezo vizuri!.
Hakika Mama mchungaji alikuwa kajipanga Kwa maelezo vilivyo, yaani Mr Jedi alikuwa kampamgilia Mama mchungaji maneno ya ushawishi, pia hata ushahidi ambao alikuwa nao ulikuwa unaonesha kwamba Yeye hahusiki kabisa!!.
Yaani Mama mchungaji aliwakataa na kuruka futi Mia Moja!.
Kwa Namna Melisa na Luka walivyo changanyikiwa walianza kutaja na Watu wengine Ambao walishirikiana, mmoja alikuwa Mzee wa kanisa, wengine ni watu wa busara tu pale kanisani, Yaani walitajwa watu kama watano!.
Mpaka inafika Jioni wote walio tajwa walikuwa wamekamatwa, lakini kati yao hakuna hata mmoja aliye kubali na wote walionesha kwamba wana wasiwasi na Luka!!
"Jamani ushahidi upo! Ushahidi tunao nyumbani tena ni video zinaonesha wote hapa kwamba tulihusika wasikatae Afande tunaweza kwenda kuchukua huo ushahidi!" Baada ya Mr Luka kukumbuka kwamba kuna flash Jofu aliwapatia zilikuwa na ushahidi wa videos zote na audio zote aliamua kuongea!.
Basi askari walimfunga Luka pingu na Melisa baada ya hapo waliongozana kwenda mpaka Huko nyumbani kuchukua hizo flash, yaani ilikuwa ni Jino Kwa Jino!.
Muda huo Mama mchungaji Mavi yalikuwa yanagonga chupi, alikuwa anaona basi kaisha habari yake kwisha!.
Pia hata wale wengine majasho yalikuwa yanawatoka maana ni ukweli kwamba walikuwa wamehusika!.
Melisa na Luka wakiwa Chini ya ulinzi walifika mpaka nyumbani pale Kwa Melisa, walikuta mlango upo wazi! Yaani Naya au Mama Habir baada ya kuponea chupu chupu na kuachiwa pale kituoni baada ya kugundulika hahusiki alivyo fika nyumbani tu alibeba kila kitu, yaani alisafisha nyumba nzima! Hata kabati ambalo walikuwa wameficha zile flash disk nalo lilikuwa limebebwa na hawakukuta kitu!.
"Afande tuliweka kwenye kabati mdogo Wangu atakuwa kahama nazo" Melisa alijitetea Lakini alikula Bonge la kofi zito kutoka Kwa askari!.
"Wajinga wakubwa nyie Kwa Hiyo mnatufanya watoto, mnataka kutoroka Siyo!? Sasa Kwa taarifa yenu tumewashitukia!" Askari aliongea Kwa jaziba baada ya kumuwasha Melisa na Kofi!.
Mpaka hapo Mr Luka alijua habari yake kwisha, yaani alikuwa hana ujanja mwingine tena!.
Walirudishwa kituoni, Mama mchungaji na wenzake waliachiwa Kwa sababu ilionekana Luka na Melisa wanatafuta wa kufa nao, na Kwa maelezo ya Mama mchungaji ni kwamba alikuwa na ugomvi na watu hao ndo chanzo Cha kutaka na yeye ahusike!.
Siku mbili zilipita kesi ilipelekwa mahakamani! Yaani Mr Luka na Melisa walikuwa hawaamini kama ndo wanaenda kuishia Gerezani!.
Upande wa huku Kwa Jedi na Majaribu wao walikuwa wanajibweda tu maana walijua lazima Mr Luka na Melisa wakikamatwa watataja wenzio, na kwakuwa wana zile flash walizo mpatia Jofu basi wote Kwa pamoja watakuwa wamechomana na wamekamatwa!.
Yaani Jedi alikuwa anajua Mr Luka ana ushahidi wa kutosha! Ila aliamua kumchochea Mama mchungaji na kumdanganya kwamba ushahidi wote Ambao unamuonesha na yeye ataufuta Kwa sababu upo kwake tu!.
Kwa hiyo Jedi alikuwa anajua hata Mama Mchungaji atanaswa tu , Lakini kumbe Bahati nzuri ushahidi Binti Naya alikuwa kahama nao! Na Binti huyo alikuwa kahamia mkoa mwingine kabisa yaani alikuwa hataki mabalaa!.
Upande wa huku Kwa Mama mchungaji Meno tu yalikuwa yanamtoka,na alikuwa anaamini huwenda Majaribu na Jedi ndo walio msaidia mpaka ushahidi ambao kina Luka waliuendea kutopatikana!.
Je ipi hatima ya Yote
Tukutane sehemu ya 15
Hadithi: MAJARIBU
Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)
Sehemu: 15
Upande wa huku Kwa Mama mchungaji Meno tu yalikuwa yanamtoka,na alikuwa anaamini huwenda Majaribu na Jedi ndo walio msaidia mpaka ushahidi ambao kina Luka waliuendea kutopatikana!.
Basi Siku zilizidi kuhesabu Huku Mr Luka na Melisa wakiwa wanaendelea kunyea Debe na Kesi yao ikiwa ipo mahakamani!.
Mr Luka alikuwa na watoto wakubwa pia na ndugu Zake Ambao walikuwa na uwezo pia, wale ndugu wa Mr Luka walikuwa wanahaha kuhakikisha Mr Luka anakwepa kwenye ile Kesi!.
Kesi ilianza kusikilizwa mahakamani! Mama mchungaji alikuwa Shahidi pia alitoa na ushahidi wake pale mahakamani, pia katika Hali ya kushangaza mtoto Majaribu alijitokeza Siku hiyo pale mahakamani!.
Na Siku hiyo mahakama ilikuwa imefurika watu, Haswa waumini wa kanisa lile!
Kila Mtu alibaki anakodoa macho akimshangaa Majaribu! Kwanza ilibidi Kijana Majaribu akamatwe na askari mpaka kituo Cha polisi ili akatoe maelezo Vizuri ilikuwaje mpaka akafa!.
Majaribu alitoa maelezo yaliyo changanyikana na uongo! Na lawama zote alikuwa anazipeleka Kwa Mr Luka na Melisa kama kawaida!.
"Wale ndo walikuwa na Lengo la kutuua! Kwa sababu walijua kwamba Mimi kuna Siri marehemu aliniambia Kabla hajafa, Kwa Hiyo walifanya Mbinu ya kunitorosha Gerezani ili waje wanibane niwaambie Siri na baada ya hapo waniue, tena Mimi na brother Yangu wote walitufanyia hivyo, hata hivi naongea brother Jedi sijui Yuko wapi ila tulipoteana akiwa kwenye hali mbaya!" Hayo ni baadhi ya maelezo ambayo Majaribu aliyatoa, askari walizidi kushangaa baada ya kugundua na Jedi naye yupo hai.
Upelelezi wa Kesi zote mbili yaani kesi ya Jedi na Majaribu ulianza upya! Na Wapelelezi wa awamu hii walikuwa wanajua na wafuata Haki!.
Baada ya mwezi mmoja ukweli ulijulikana kwamba Jedi hakuuwa Bali marehemu alikufa Kwa Sumu, maana mpaka mwili wa marehemu ulienda kufukuliwa japo kuwa ni kama mifupa tu ilikuwa imesalia Lakini walipima na waligundua kwamba Sumu ndo iliyo muua Mtu yule!.
Yaani Mr Luka na Melisa rundo la Kesi lilizidi kuongezeka kiasi kwamba Ingekuwa ngumu kuchomoka!.
Doctor Lameck baada ya kugundua kwamba anatafutwa Kwa kosa la kuuwa kutumia Sumu akiwa kama Daktari, aliamua kutoroka na kupotelea kusiko julikana, yaani hakuna aliye Elewa kwamba Bwana huyo ni wapi kapotelea maana aliacha kuonekana kabisa!.
Kesi ile iliendeshwa Kwa Mwaka mzima! Yaani danadana zilikuwa nyingi na kona kona nyingi Muno, baada ya kugundulika kwamba Hakimu anaye endesha kesi ile ana mpango wa kuwaachia akina Mr Luka Huru, Hakimu alibadilishwa na kuletwa mwingine!
Yaani ilifika kipindi mpaka watu mtaani walisahau kabisa kuhusu ile Kesi, maana ni zaidi ya Mwaka na Nusu ulikuwa umepita tangia kesi ile ianze kusikilizwa japo kuwa palikuwa na ushahidi!.
Hakimu mpya aliye ingia aliamua kutoa hukumu! Kitu Cha kushangaza hukumu yake ni kwamba Melisa na Mr Luka walifungwa Gerezani Miaka Mitano kila Mtu, yaani Hukumu ile ilikuwa na ualakini kiasi kwamba hata Ambao walikuwa wanaifuatilia walishangaa Muno kuona watu wauaji wanapewa hukumu ndogo vile!.
Maisha yaliendelea huku Melisa na Mr Luka wakiwa wamefungwa Miaka mitano tu.
Jedi na Majaribu walikuwa washajimilikisha ile nyumba ya Lameck hata hati waliamua kuzibadilisha Majina waliandika ya kwao!.
"Majaribu kama Nilivyo kwambia! Hapa kuna mipango miwili kwanza nataka nianze kumtafuta Mtoto wa Dada Yangu ni wapi alipo, pili nataka Mama mchungaji apukutike yaani Mali zote zije mikononi mwetu!" Hayo yalikuwa maneno ya Jedi Siku hiyo wakiwa wamekaa na Majaribu wanapanga mipango.
Basi walikubaliana kushirikiana kila hatua ili kufikia malengo yao!.
Wiki Moja ilipita, Mama mchungaji akiwa na Revina pale nyumbani Mara mlango uligongwa na ulipo funguliwa Jedi na Majaribu walionekana kuingia Mule ndani!.
"Hahaaaaaa! Jamani Karibu! Karibu" mama mchungaji akiwa anajichekesha aliwakaribisha! Maana alikuwa anajua wale ndo wasiri wake! Wakisema tu Suu! Basi anaenda kunyea Debe!.
"Mama usijichekeshe kama hujui! Unajua Nusu ya Mali ambazo Nemeke alikuwa anamiliki zilikuwa ni Mali za wazazi Wangu na alizipata Kwa njia ya uhuni!" Jedi akiwa na Sura ngumu alizungumza!.
"Kwa Hiyo Kijana Wangu unasemaje maana hapo sijaelewa!" Mama mchungaji mapigo ya Moyo yakiwa yameanza kwenda kasi aliuliza!.
"Siyo nasemaje! Mali zote unazo Miliki tunagawana Nusu Kwa Nusu! Pia hata hao ulio gawana nao baada ya kumuua mchungaji Nemeke ntamfuata mmoja baada ya mwingine wanazirudisha! Na kingine ambacho hamjui nyaraka zote za Mali tunazo Sisi!" Jedi aliongea maneno ambayo yalifanya Mama mchungaji ahisi joto linapanda Mwilini!.
"Hiyo haiwezekani yaani tugawane nusu Kwa Nusu! Labda nikupe pesa kidogo na Wewe ukafungue mradi wako" mama mchungaji aliongea!
"Usijifanye umesahau, Bora uishi na kichache kuliko kwenda kunyea Debe Gerezani!" Jedi alianza kutoa vitisho, yaani Kwa vitisho Ambavyo Jedi aliendelea kuvitoa pale vilifanya Mama mchungaji akubali matakwa ya Jedi!.
Siku hiyo Jedi alipita Kwa kila Mtu aliye husika na Kifo Cha Nemeke na kupewa sehemu ya Mali! Yaani kila Mtu aliambiwa arudishe Mali alizo pewa lasivyo atawaambua!
Vitisho vile vilikuwa vikubwa ukichukulia na video ambazo Jedi alikuwa nazo zikionesha kundi zima wapo kwenye kikako Cha kujadiliana mgao basi kila Mtu alibaki Mnyonge na alikubali kurudisha kile alicho kichukua!.
Lakini Mama mchungaji na wenzake walionekana Bado hawajaridhika kumuacha Jedi atambe vile, baada ya Siku kama Tatu waliitana na kukaa kikao! Basi waliazimia Kwa umoja wao kwamba watafute mamafia wawaue Jedi na Majaribu!.
Ni kweli baada ya Wiki kama Moja kuna vijana walio zoea kazi ya Mauaji walitafutwa na walikuwa mamafia kweli.
Siku Hiyo Mida ya Saa Tano usiku Jedi na Majaribu walikuwa wamekaa sebuleni wanaangalia mpira wa ulaya huko, huku wakiwa wanabishana.
Wakiwa pale Sebuleni Mara walisikia mlango unagongwa nje, bahati Nzuri Jedi alikuwa mjanja nje ya mlango alikuwa ametegesha camera alafu kaunganisha na Simu yake!.
Kabla ya kwenda kufungua Jedi aliangalia kwenye Simu yake, aligundua watu waliopo pale mlangoni Siyo watu wema kabisa!
Walikuwa ni Watu wanne wakiwa wamevalia mizuhuru ya kuziba uso Huku mmoja kati ya wale wanne akiwa ameshika bunduki tena zile bunduki zenyewe!.
"Duuuuuu dogo Majaribu hapa tumekwisha naona hapo nje kuna vidume wanataka kutuua bila shaka Mama mchungaji atakuwa kawatuma!." Jedi akiwa anafikiria Cha kufanya aliongea!
"Kwa Hiyo brother tunafanyaje Sasa!" Majaribu ilibidi aulize!.
"Sikiliza Majaribu hapa inabidi tufanye Jambo lasivyo tunakufa, maana inaonekana Jamaa wapo serious Muno" Jedi akiwa anapiga mahesabu aliongea, Muda huo huo Mara walianza kusikia nje kitasa kinavunjwa na wale Jamaa!.
Je ipi hatima ya Jedi na Majaribu!??
Tukutane sehemu ya 16
Hadithi: MAJARIBU
Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)
Sehemu: 16
"Sikiliza Majaribu hapa inabidi tufanye Jambo lasivyo tunakufa, maana inaonekana Jamaa wapo serious Muno" Jedi akiwa anapiga mahesabu aliongea, Muda huo huo Mara walianza kusikia nje kitasa kinavunjwa na wale Jamaa!.
Kwakuwa nyumba ile ilikuwa na mlango mmoja tu wa kutokea nje, ilibidi Sasa wakubaliane kwamba Majaribu alipite dirishani! Yaani Majaribu alikuwa ni kijana mwembamba na mtundu Muno, japo kuwa madirisha yalikuwa na nondo zimebanana kupita kiasi lakini alipita, baada ya Majaribu kupita dirishani haraka haraka alikimbia kwenda kuita majirani ili waje Sasa wanase wale majambazi!, Na wale majirani baada ya kuambiwa majambazi Wana bunduki ilibidi wapige Simu kituoni na wao waliogopa kuingia Mule ndani!.
Wakiwa nje ya geti Mara mlio wa bunduki ulisikika ndani! Yaani hapo hakuna hata aliye sogea, Lakini dogo Majaribu alijiamini alifungua geti na kuzama ndani Huku akiwa anapiga makelele!.
Dakika mbili nyingi wale magaidi baada ya kusikia nje kuna makelele haraka haraka walitoka sipidi mpaka nje, na waliona Raia kama wangapi pale nje! Hakuna aliye jaribu kuwasogelea Kwa sababu walikuwa wameshika Bonge la bereta! Basi walikimbilia pale walipo ficha pikipiki zao, waliziwasha na kuondoka, Muda huo huo askari nao ndo walifika pale nyumbani!.
Majaribu aliingia ndani alikutana na Damu za kutosha Chini ! Baada ya kupiga Macho mbele alimuona Jedi akiwa Chini!.
Katika Hali ya kupambana na wale Jamaa Jedi alikuwa kapigwa Risasi mbili, yaani risasi ya Mguu na Risasi ya mbavu! Yaani Jedi alikuwa yupo Chini hali yake ikiwa mbaya alikuwa kazimia kabisa!.
Askari nao waliingia mule ndani na baadhi ya majirani! Haraka haraka Jedi alibebwa na kukimbizwa hospital!, Majaribu kitu alicho hakikisha anaondoka nacho pale nyumbani zilikuwa ni zile flash disk na Simu ya Jedi maana hivyo ndo vilikuwa na Siri!.
Jedi alikimbizwa hospital akiwa Chini ya uangalizi wa askari! Yaani hali yake ilikuwa mbaya kuliko Kawaida!.
Upande wa pili Mama mchungaji alionekana kachanganyikiwa isivyo kawaida maana taarifa zilikuwa zimerudi kuhusu kile kilicho tokea, yaani hapo ndo alikuwa anajiona kama kaharibu kabisa!.
Zilipita Siku mbili Jedi akiwa bado yupo pale hospital, ila Mama mchungaji alikuwa anahaha na kupambana ili aweze kuhakikisha kwamba Majaribu na Jedi wanakufa Kabla Mambo hayajaharibika!.
Basi Siku hiyo Usiku Jedi alizinduka na Majaribu alikuwa yupo pembeni, yaani alikuwa habanduki!!
Baada ya kuzinduka tu Jedi aliomba Maji, basi haraka haraka Majaribu alikimbia nje kwenda kutafuta Maji!.
Ila akiwa anakimbia kwenye korido! Gafla alimuona Mama mchungaji na wababa wawili wakiingia kwenye chumba kimoja! Na juu ya mlango kwenye chumba kile palikuwa pameandikwa, mganga Mkuu!.
Majaribu aligairi hata kwenda kufuata Maji alirudi Mule ndani kumpelekea taarifa Jedi!.
"Majaribu tuondoke Muda huu huu! Humo Kwenye Simu Yangu kuna Pesa utazitoa! Nipeleke hospital nyingine!," Jedi akiwa anahisi maumivu huku anaongea Kwa taabu kutokana na jeraha ambalo lilikuwa lipo kwenye mbavu aliongea!.
Muda ule ule Majaribu alimshikilia Jedi walianza kutoka nje, tena walitoka mpaka nje ye geti kabisa, Mlinzi wa pale Getini alionekana kuleta upinzani, Majaribu alichomoa shilingi elfu kumi na kumpatia, basi Mlinzi yule alibaki katulia!.
Pale nje kuna taxi zilikuwa zinakesha! Basi walikodi taxi mpaka hospital nyingine!.
Masaa yalizidi kusogea! Ikiwa ni Mida ya Saa Tisa! Daktari Mkuu kwenye hospital ile alionekana kuwatuma vijana wake ambao walikuwa ni madoctor pale na aliwapatia maelezo ambayo alikuwa anajua yeye!.
Ila wale madoctor baada ya kwenda kwenye chumba ambacho Jedi alikuwa kalazwa hawakukuta Mtu, walitafuta kila kona ya hospital Lakini hakuonekana.
Ilipo Fika asubuhi askari kama kawaida walikuja pale hospital kuangalia Maendelea ya Jedi, lakini walikutana na taarifa ya kwamba mgonjwa huyo katoroka pale hospital!.
Muda huo Jedi alikuwa anazidi kupata matibabu kwenye Moja ya hospital za binafsi na tena aliomba iwe Siri kwamba Yeye yupo pale!.
Siku mbili zilipita Jedi alitafutwa bila mafanikio, pia hata Majaribu naye hakuonekana.
Jedi alionekana afya yake inaimarika kidogo, Siku Hiyo Jedi aliamua kushitua Kwanza kitu alicho kifanya alishika Simu yake alifungua ile video ambayo inaonesha kikao Cha watu kama saba ,kukiwa na Mr Luka, Melisa Mama mchungaji na wengine wanne ambacho walikuwa wanajadiliana Namna ya kugawana Mali za Nemeke baada ya kifo Cha Mchungaji Huyo.
Kwanza Nemeke aliscreen shot ile video na kufanya iwe picha ambayo inawaonesha watu wale wakiwa kwenye kikao!.
Baada ya hapo ile picha aliituma mtandaoni huku akiweka maneno!
"Je wajua kipi kinajadiliwa hapo! Aibu kwakweli Soon itajulikana!" Hayo ni maneno ambayo aliyaweka juu ya ile picha na kuitupia mtandaoni!.
Siku Hiyo upande wa Huku Kwa Mama mchungaji alikuwa anaenda Mara mbili mbili chooni! Yaani alikuwa kapatwa na matumbo ya kuhara gafla.
Akili ya kukimbia Nchi ilianza kumjia kichwani mwake maana alikuwa anaona video zile zikitumwa mtandaoni basi kaisha.
Siku Hiyo ilipita, ikiwa ni Siku nyingine mchana, Jedi baada ya kuona anaendelea vizuri aliamua kuomba aruhusiwe pale hospital, Japo kuwa madaktari walimsisistiza kwamba Bado hajapona ila yeye alikuwa anataka kuondoka, maana ni Mambo mengi Muno ya kufanya yalikuwepo!
Basi ni kweli waliruhusiwa, baada ya kutoka pale hospital safari ya wawili wale ilienda kuishia mpaka nyumbani Kwa Mama mchungaji!.
Muda huo Mama mchungaji alikuwa ana mawazo haelewi kitakacho mpata! Yaani alikuwa anaona kila anacho fanya ni kama anakosea!.
Akiwa kwenye lindi la mawazo huku usingizi nao ukiwa unampitia Mara gafla alishitushwa na Sauti ya mlango kugongwa!.
Alibaki kaacha mdomo wazi baada ya kumuona Majaribu na Jedi wanazama pale ndani, japo kuw Jedi Bado alikuwa na bandeji Mguuni na ubavuni!.
"Nakupa nafasi ya Mwisho! Ukishindwa kuweka million 500 Leo kwenye akaunti nikatayo kupa basi Kesho asubuhi utakuwa upo ndani unanyea Debe!" Jedi akiwa serious aliongea Kwa ukauza, baada ya hapo aliandika namba ya akuanti na Jina!.
Jedi hakuongeza Neno, alianza kuondoka huku Majaribu akiwa anafuata nyuma.
"Ndugu Yangu Basi tufanye million 200 ujue Hizo 500 nyingi Muno yaani hapo ntakuwa nimefirisika kabisa ujue!" Basi Mama mchungaji alijiongelesha, lakini kijana Jedi alirudia na Kwa msisitizo kwamba anahitaji 500 lasivyo ajiandae Kwenda kunyea Debe na kula ugari wa bure!.
Jedi aliwatembelea wote ambao alihisi wanahusika na kila Mtu Alikuwa anahaha kivyake!.
Mama mchungaji alikuwa kachanganyikiwa, aliona ni Bora afanye hivyo kuliko kwenda Jera na kuumbuka!.
Mama huyo kwenye akaunti yake alikuwa na million 200 tu, Basi ilibidi Sasa aanze kuuza baadhi ya Vitu anavyo Miliki!.
Aliuza Gari zake za kifahari mbili, aliuza Duka lake kubwa la pembejeo ambalo ndo lilikuwa kubwa katika Miradi yake!.
Baada ya kuuza na Miradi yake mingine midogo midogo, Mama mchungaji alienda kuweka ile Pesa kwenye akaunti.
Mama mchungaji alijua kufanya hivyo walau atapumua! Lakini akiwa ndo katoka kuweka tu Mara alipokea ujumbe!.
"Hilo la kwanza tumemalizana, bado kesi ya ulivyo jaribu kuniua ili nayo iishe malizia na million 200!" Huo ulikuwa ni ujumbe ambao ulifanya Sasa Mama mchungaji aanze kupiga makelele hovyo na kujiongelesha mwenyewe!.
"Aaaaaa hapo haiwezekani! Hiyo sitoi tena narudia sitoi Pesa nyingine!" Mama mchungaji alikuwa anajiongelesha mwenyewe hovyo!.
Siku Iliyo fuata kuna kituo Cha TV kilitoa matangazo kwamba Jioni watakuwa na Jedi kijana ambaye kapitia mengi Huku ikisadikika kijana huyo kwamba ana mengi ya muwaelezea wanachi!!.
Mama mchungaji baada ya kuona hilo tangazo hapo ndo alichanganyikiwa alijua lazima Jedi ataenda kuanika Siri zao!.
Yeye mwenyewe bila kulazimishwa alimpigia Simu Jedi na kumwambia anatoa ile Pesa, ili kijana asije akaropoka!.
"Umechelewa Mama! Kama unataka nisiende kwenye hicho kipindi ni million 300 Siyo 200 tena kama mwanzo!" Hayo yalikuwa maneno ya Jedi na hakutaka kuongea Sana baada ya hapo alikata Simu!.
Hakika Mama mchungaji alichanganyikiwa! Yaani alijikuta Miradi yale Yote iliyo Salia anaipiga mnada wa haraka haraka na Pesa zote aliziweka kwenye akaunti ya Jedi, na Mama Yule alikuwa na Imani kwamba akifanikiwa kumuua Jedi kila kitu chake kitarudi!.
Mama mchungaji alikuwa kabakiwa na nyumba tu ambayo alikuwa anaishi! Yaani Miradi yote alikuwa kauza Kwa Bei za Hasara!.
Basi ilipo Fika Jioni! Jedi alionekana anaelekea Gerezani! Na kwenye kile kipindi hakwenda na alitoa taarifa kwamba ana dharura imejitokeza!
Je Kipi Jedi kaenda kukifanya Gerezani!??
Tukutane sehemu ya 17
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Write your comment