Mpya
UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA ALOBAINI NA TISA
MTUNZI @MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI NA NANE: Masoud akiwa chumbani kwake, amejilaza kitandani, aliwaza mambo mengio sana, aliwaza jinsi Salma alivyoonekana kuchachawa pale aliposikia kuwa, Sebastian amerudi, “wanawake watu waajabu sana, yani mambo yote tunayofanya, alafu ananionyesha wazi wazi, jinsi alivyo chachawa kwa huyo boya wake” alijisemesha Masud, kwa sauti ya chini iliyojaa chuki, “yani anamshobokea yule boya, utazani nani sijuwi” alisema Masoud, akisahau kuwa fedha anazotumia na kupendezeshwa ni za huyo huyo anaemwita boya, “alafu demu anaona ela ndiyo kila kitu” aliwaza Masoud.
Ambae alisha sahau kuwa ata yeye yupo pale kwaajili ya fedha hiyo hiyo, ambayo ndiyo inayomweka mjini, nakusahau kurui kwao Malangari, ngoja nimchek, lazima mambomengine yaendelee bwana” alijisemea Masoud, huku anachukuwa simu yake na kuingia sehemu ya whatsapp, kwaajili ya kutuma ujumbe.*********
Naam mafinga mjini bado wakina mzee Mdemu walikuwa wamekaa na kijana Emanuel pale mapokezi, wakiongea ili na ili, huku maongezi yao yakiegemea sana kumpa sifa kijana Masou, jambo ambalo mama Ana akuwa na imani nalo, ndio maana wasi wasi, aukumtoka moyoni mwake.
Wakati naongezi yanendelea Emanuel akaaga na kuelekea kwenye lindo lake, maana saa tatu ilikuwa imeshaingia, na baaa ya kuwaaga wakina mzee Mdemu, Emanuel akaondoka zake, huku anaandika ujumbe kwa Masoud kumpa pongezi kwa kile alichokifanya, kusaidia matibabu ya mzee Sinyangwe, pasipokujuwa kile ambacho Masoud alikifanya kwa Anna.********
Ana alisimulia kila kitu, kuanzia kusaidia masomo ya Masoud, mpaka kutumikishwa na mama yake Masoud, matendo yote yakisaliti abayo Masoud alikuwa anayafanya, wakati walikizo, lakini yeye na familia yake, awakuacha kufanya kazi kwa juhudi, kusamsaidia Masoud, wakiamini kuwa alikuwa anampenda kweli Anna, nakwamba mwisho wasiku wataishi pamoja katika mafanikio.
Ana alimweleza Sebastian jinsi wazazi wa Masoud walivyoshindwa kuwasaidia kumkimbiza mginjwa hospital, pia jinsi walivyosumbuka kwenda Mafinga usiku, ata walipopata taarifa juu ya maisha ya Masoud, na yeye kuja huku, ambako alikutana na kitu ambacho akutegemea kukutana nae.
“huyo mwanamke wake anaitwa Salma, nie mwanake niliekuwa naongea nae, muda mfupi uliopita” alisema Sebastian huku na yeye akianza kumsimulia mkawa wake na Salma, mpaka alipoenda kujionea mwenyewe kule ofisini.
Sestian alimaliza kusimulia wakati wanasimama nje ya lango la jumba kubwa la kifahari kule mikocheni, lango ambalo licha ya kulindwa na walinzi wawili, lakini pia lilikuwa na uwezo wa kufunguka lenyewe, ndivyo lilivyofanya sasa, na kumfanya Anna atoe macho kwa mshangao, kwa uzuri wa mle ndani, ya uzio wa jumba lile, ambalo siyo tu akuwai kuliona kule kwao, pia akuwai aya kufikilia kama kuna nyumba kama ile, anamiliki mtu binafsi, ambapo mwanzo alizania kuwa hapa ni kwa wazazi wa kijana huyu, mwenye sura nzuri, kuliko wanaume wote aliowai kuwa nao karibu.
Mshangao wa Anna aukuishia hapo, ilikuwa ni zaidi ya mshangao alipoingia nani ya jumba ilo, lenye vitu vizuri na vya thamani, kiasi kwamba, mschana huyu toka malangari, alipofika mlangoni, alivua ndala zake na kuzishika mkononi, kwa kutaka kuingia nazo ndani, bahati nzuri alikuwepo mmoja wawafanyakazi wa kike, ambae aliwai kumpokea, “ziache tu hapo aunaaja ya kuzibeba” alisema yulemfanya kazi wa kike, ambae alizania kuwa huyu mwanamke ni mfanyakazi mpya, anaeongezwa pale nyumbani.
“dada Sia, mwonyeshemgeni chumba cha kulala” alisema Sebastian, huku anatembea kuelekea upande wa ngazi, za kuelekea ghorofani, “sawa kaka atalala na kile chumba kingine dada mage, alafu kesho tuta mwandalia chumba chake” alisema yule mfanyakazi wakike, alie iwa Sia, ikiwa ni kifupi cha jina Siamini.
Hapo Sebastian akasimama na kugeuka, “unazungumzia chumba gani Sia?” aliuliza Sebastian, ambae akuwa katika hali ambayo siku zote waliizowea, kwamba ni mtu wa tabasamu muda wote, “kile cha dada Mage, mwenyewe aliondoka toka juzi, mama yake anaumwa” alisema Siamini, akimaanisha moja kati ya vyumba sita, vilivyopo upande wa nyuma ya jumba lile, vyumba ambavyo utumiwa na wafanyakazi wa nani, pamoja na chumba kimoja cha walinzi, “nani alikuambia mgeni wangu anafikia kwenye chumba cha nje?” aliuliza Seba, kwa sauti kavu yenye ukali kidogo, “samahani kaka.. nili.. nilijuwa mfanyakazi mpya” alisema Sia, kwa sauti yenye uoga na unyenyekevu, “mwonyeshe chumba kule ghorofani, mwelekeze bafu, akisha oga aje kupata chakula” alisema Seba, kisha akaondoka kueleka ghorofani, akimwacha Sia anamazama Anna kwa macho ya mshangao.*******
Naaam masoud anapomaliza kuongea na simu, mala anaona ujumbe umeingia kwenye simu yake, unatoka kwa Emanuel, Masoud anapawa na hasira, anakumbuka kuwa Emmanue, ndie mtu pekee wa kule kijijini, alie mweleza kuhusu kufanya kazi kwake Kiguru, anapanga kumtumia ujumbe, kwa hasira, kukomesha tabia yake ya kusambaza habari zisizo mhusu. …….endelea….
UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA HAMSINI
MTUNZI @MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI NA TISA: Naaam masoud anapomaliza kuongea na simu, mala anaona ujumbe umeingia kwenye simu yake, unatoka kwa Emanuel, Masoud anapawa na hasira, anakumbuka kuwa Emmanue, ndie mtu pekee wa kule kijijini, alie mweleza kuhusu kufanya kazi kwake Kiguru, anapanga kumtumia ujumbe, kwa hasira, kukomesha tabia yake ya kusambaza habari zisizo mhusu. …….endelea….
Lakini anapoufungua ule ujumbe anakutana na kitu kizito, “safai sana kaka yani huku wazee wanakusifu kwa kile ulichokifanya, millioni moja na laki tanosiyo mchezo, nifanyia mpango na mimi nije huko kaka” ndivyo ulivysomeka ule ujumbe, ambao ulieleza kuwa Masou aetuma fedha hiyo kwaajili ya matibabu ya mzee Sinyangwe, “eti Million moja na laki tano” alijiuliza Masoud kwa mshangao, “mh! mbona mimi sijatuma hizo ela kwanza nitazitoa wapi?” alijuliza tena Masoud huku ameshikilia simu mkononi mwake, akisahau kujibu ujumbe wa Emanuel.********
Naam sasa turudi mikocheni dar es salaam, nyumbani kwa Sebastian, ambako sasa tunamwona Anna akiwa amekaa kwenye meza kubwa ya chakula amekodoa macho akitazama mabakuri makubwa ya kuifadhia chakula, yaliyo jipanga mbele yake, huku kila bakuri likiwa na chakula chake, kama siyo kachumbali basi nyama ya kukaanga, kama siyo mboga ya majani, basi jingine lina mapaja ya kuku, kama akiona ndizi za kuchemsha, basi bakuri jingine lina wali mweupe, na la pembeni yake ndizi za kukaanga, likiwa karibukabisa na bakuri lenye pilau, na jingine rost ya maini, ya ng’ombe.
Japo mwanamke huyu alishaambiwa karibu, lakini bado alikuwa amekaa anaodoa macho kutazama vyakula vile, huku sasa akiwa anaisikia jaa vyema kabisa, ni njaa ya kutwa nzima, ebu fikilia, licha ya yote yaliyomtokea lakini aliweza kusikia njaa, ni kutoka na mwonekan wa yakula vile, ukweli ni vyakula ambavyo siyo kwamba akuwai kuviona, hapo mwanzo, ila ukweli ni kwamba akuwaikutemea kwamba, kuna siku at aula vyaula hivi kwa pamoja, yani wenye mlo mmoja.
“Anna mbona auanzi kula” aliuliza Sebastian, ambae alikuwa anakatiza sebuleni, huku ameshika grass yenye kimiminika cha rangi nyeupe ndani yake, ilikuwa ni wine iliyotengenezwa kwa nazi, maarufu kaa #mbogo_land coco wine, na mkono mwingine ameshikilia simu yake, akiwa amevalia tishert jepesi, na chini alivalia kaptula, “nawasubiri wengine” alisema Anna, alionyesha wazi kuwa, anaamini ya kwamba, chakula kile kilikuwa cha familia nzima.
Sebastian akacheka kidogo huku anasimama, na kumgeukia Anna, “akuna mwingine atakae ula hapo nivyema ukala na ukaenda kupumika, labda kama utaiaji kunywa wine kidogo” alisema Sebastian huku anafwata Anna pale mezani, ana akatoa macho kwa mshangao, “weeee ikichakula na kula peke yangu, mbona ….?” aliuliza Ana kwa sauti iliyojaa mshangao mkubwa sana, huku anatazama yale mabakuri makubwa ya vioo yaliyoifadhiwa vyakula, moja baada ya jingine, asijuwe aanzie wapi.
Anna ulisema utaitaji vocha, kwaajili ya kuongea na mama, nitajie namba yako nikutumie, alisema Sebastian huku anaweka sawa simu yake kwaajili ya kutuma salio, “sifuri saba…..” Anna alitaja namba za simu yake, huku akili yake ikiwa kwenye chakula kile, ambacho sasa alibaki amekitazama kama vile anaona kitu cha ajabu.
Sebastian alimaliza kuamisha salio kwenye simu ya Anna, kisha akaondoka zake, huku akimwacha Anna anaaza kupakuwa chakula alicho kichagua kwenye sahani yake, akujuwa kuwa Anna alikuwa katika wakati mgumu sana, maana alikumbuka shida zao kule kijijini, akujuwa wadogo zake watatu wanaishije, kwa sasa ambapo yeye na mama yake awapo kijijini, alikumbuka shida zinazowakuta wanakijiji wengine kule Malangari, ambapo wange shindia viazi mvilingo vya kuchemsha, siyo kama hii anavyo viona mbele yake vikiwa vimelostiwa vizuri, hivyo vingekuwa vilivyo chemshwa kwa maji na kuwekwa mafuta kwambali huku kiungo kikubwa kikiwa chumvi na kinguu, au majani ya kitunguu, ambacho ingekatiwa kwa juu, msimu wa nyanya wange katia na nyanya, ilikunogesha zaidi, vinginevyo ungekuwa ni chemsho wa maji na chumvi pekee.
Ukweli japo Anna alikula chakula kile, lakini kwa mala ya kwanza akukifurahia sana, maana alikula huku moyo ukiwa unamchoma kweli kweli, anapokumbuka hali ya familia yake kule kijijini, “yani watu wanaishi vizuri wakati wengine huko kijijini, tunaishi kwa kuujuwa mlo wa leo tu” aliwaza Anna ambae alikumbuka mwonekan wa sasa wa Masoud, mwanaume ambae yeye na familia yake, wamejitolea kwa moyo mmoja, kwa hali na mali, awakujali kula yao, awakujari mavazi yao, wala awakujali wanaonekanaje mbele ya wanakijiji wenzao, walich hakikisha ni kwamba, asoud anapata Elimu aliyokuwa anaitafuta, ili kuja kuwa mkombozi wao.
Anna alivuta picha jinsi alivyowakuta mle ofisini na yule mwanamke anaesemekana kuwa ni mchumba wa Sebastian, wakifanya ngono ambayo, ata yeye Ana akuwai kufikilia kama Masoud anaweza kuifanya, “hivi Masoud amemlaghai nini dada wa watu, mpaka akamwacha huyu mwanaume mzuri, na kuwa na yeye” alijiuliza Anna, ambae kwa dalili hizi unaweza kugundua kuwa, tayari alisha anza kumtoa Masoud kichwani mwake, kwa kukubariana na ukweli kwamba, Masoud akuwa anampenda.
Ana aliwaza mengi sana, akiwa mezani, ata alipoenda chumbani kwake, ambako akuzania kama ataweza kupata usingizi, maana alijiona kama anaenda kulala dukani, kutkana na kuwa na vitu vingi vya kupendeza, meza TV ambayo akuwa na uwezo wakuiwasha, sei ya music, meza ndogo yenye kitu mbali mbali, pia kabati, na meza ndogo ya kujipamba, alafu kuliwa na koochi dogo la watu wawili, ukiachilia kitanda kikubwa sana, ambacho Ana mpaka sasa, akuamini kuwa alikuwa anatakiwa kulala juu yake, “ebu ona mama yake, alivyokuwa ananinyanyasa, mivyombo yote ile, mingu michafu, kudeki nyumba” aliwaza Anna.. …….
Itaendelea
UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA HAMSINI NA MOJA
MTUNZI @MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI: Ana aliwaza mengi sana, akiwa mezani, ata alipoenda chumbani kwake, ambako akuzania kama ataweza kupata usingizi, maana alijiona kama anaenda kulala dukani, kutkana na kuwa na vitu vingi vya kupendeza, meza TV ambayo akuwa na uwezo wakuiwasha, sei ya music, meza ndogo yenye kitu mbali mbali, pia kabati, na meza ndogo ya kujipamba, alafu kuliwa na koochi dogo la watu wawili, ukiachilia kitanda kikubwa sana, ambacho Ana mpaka sasa, akuamini kuwa alikuwa anatakiwa kulala juu yake, “ebu ona mama yake, alivyokuwa ananinyanyasa, mivyombo yote ile, mingu michafu, kudeki nyumba” aliwaza Anna.. …….endelea….
ambae kuna mala zote alikuwa anapika pasipo kuweza kukaribishwa mezani, yani akimaliza kupika anaondoka zake, akiwaacha wanafamilia wanajumuika mezani, “sijuwi kwa nini sikugundua mapema kama natumiwa” alisema Anna amba alipokumbuka jinsi alivyokuwa analima kwenye ashamba ya watu kwaajili ya kutafuta fedha za kutuma kwa Masoud, ambae akuwa anasoma chuo kikuu, ila chuo cha ufundi, ambacho ameishia katikati, pasipo kupata cheti chochote, hakika machozi yalianza kulenga lenga, kwenye macho yake.
Ila mwisho wa yote, Ana akujuwa Sebastian amepanga nini, juu wasaliti wale wawili, maana mpaka mala ya mwisho alipo ongea na Salma, akumwonyesha chuki ya wazi, ila onekana akiigiza mapenzi kwa mwanamke huyo, akijifanya ajajuwa chochote kilichotokea, “ngoja nimpigie mama nimweleze kila kitu” alisema Anna huku ana, anza kubofya simu yake, kwaajili ya kuangalia salio alilotumiwa, iliaweze kujiunga kifurushi.
Naam picha linaanza salio ni vocha ya elfu kumi, mwanzo Anna alizania elfu moja, lakini amesoma vibaya, lakini kwa Elimu yake ya kidato cha nne, akaona sifuri moja imezidi kwenye elfu moja na kufanya sifuri kuwa nne, “elfu kumi” ilimshangaza sana Anna, ambae alijiunga kifurushi chenye dakika nyingi na kupiga simu kwa mzee Mdem kwa ajili ya kuongea na mama yake, akipanga kumweleza kila kitu.********
Twendeni Mafinga kule Hospital, ambako tunapofika langoni, tunakutana na kijana wetu Emanuel, akiwa amevalia koti lake kubwa jeusi, amekaa chini ya mti ulipo ita chache toka pale Langoni, ameshika simu yake, anapekuwa kurasa za face book, na kutazama marafiki zake, ili aweze kutoa maoni kwenye picha zao, nazani unafahamu Emmanuel, kuwa ni mpenzi wa kutoa maoni kwenye post za wenzake.
Wakati anapekuwa pekuwa kwenye mtandao huo wakijamii, huku akitarajia majibu, toka kwa Masoud, ambae alimsifia kwa kutendo anacho hisi yeye kuwa amekifanya cha kutoa million moja na nusu, ya matibabu ya mzee Sinyangwe, mala Emma anaona simu yake ikiwa inaita, akatazama simu yake, akaona mpigaji ni Festor, huyo ni kijana mwenzie, wa lika lake, aliepo huko kijijini Malangari, walisoma pamoja, kama ilivyo kuwa kwa wakina Masoud na Ariana, japo baadhi yao walipishana darasa moja au mawili.
Emmanuel akapokea simu haraka, “niambie Festor, mambo vipi, naona le umenikumbuka” alisema Emma mala baada ya kuweka simu sikioni, “poa tu Emma, mambo yanaendaje huko town?” alijibu na kuuliza Festor, ambae siyo kawaida yake kumpigia Emma, licha ya kuwa na namba yake, “huku fresh kaka, wanasemaje huko shamba?” aliongea Emma kwa sauti yenye swaga flani hivi za kimjini mjini, “huku tunakomaa na jembe, ebu nipe taarifa za mgonjwa, maana naona kimya kuna usalama kweli?” aliuliza Festor, kwa namna flani ya kuitaji habari ambazo anazitilia mashaka, “bwana Festor kiukweli ni jambo la kumshukuru mungu, mgonjwa amesha fanyiwa operation, na sasa amesha anza kupata fahamu” alisema Emanuel kwa sauti flani iliyopoa kidogo.
Nikama ilikuwa taarifa ya kushangaza kwa Festor, “weeee unasema kweli, wamewezaje kupata laki nane za matibabu?” aliuliza Festor akionyesha wazi kuto kuamini alicho kisikia, “unazungumzia lakini nane, watu wanaela bwana Festor, yani Anna ameondoka jana jioni, kwenda Dar kwa mchumba wake, ile na leo tayari imetumwa millioni moja na laki tano, alijibu Emanuel, akitoa sifa za hali ya juu, “mh! kwani Ana amepata chumba?” aliuliza Festor kwa sauti ya mshangao, “inamaana ujuwi kuwa Masoud na Ana ni wapenzi toka kitambo, au unajitoa ufahamu tu?” aliuliza Emma kwa namna ya kumshangaa Festor, “haaaa! Emma heee, wewe aupo hapa kijijini muda mrefu, yani hapa kijijini akuna asie fahamu kuwa Masoud sasa hivi siyo mwenzetu, ana kazi nzuri ana nyumba nzuri na anamwanamke mwingine mzuri, sasa Ana ametkea wapi tena, huyo alisha pigwa chini kitambo” alisema Festor na kumfanya Emma acheke kidogo.
Baada ya kumaliza kicheko chake, Emma akaanza kumweleza Festor, kile alichoamini kuwa ni ukweli harisi, “najuwa mzee Kizinge na mke wake ndi wanao tangaza hizo habari za kwamba, Masoud amemwacha Anna, ilifikia hautua ata mama yake Anna alitaka kumzuwia Ana asiende Dar, akiamini kuwa Ana aaenda kuzalilishwa na kukaaliwa mbele za watu, kisha kuangaika huko ugenini, lakini Anna aliofika Dar, mambo yalikuwa tofauti na walivyofikilia, maana leo jioni imeletwa millioni moja na laki tano, nakama aitoshi, mzee Sinyangwe amelazwa kwenye ward ya gharama, huku anapewa huduma nzuri kama boss, sasa hiyo cha mtoto, kikubwa ni kwamba wakina mzee Mdemu nao wamepewa sehemu nzuri za kulala” alisema Emma akinyesha kuamini kile anacho kifikilia.
Tuachane na maongezi ya simu ya Emma na Festor, sasa tuingie ndani zaidi ya jengo la hospital tunafika pale mapokezi, ambapo tuna wakuta wa;ewazee watatu yani wazee wawili wakiume na mzee mmoja wa kike, yani wakina mzee Mdemu, na mama Anna, ambao sasa walikuwa wanajiandaa kwenye kupumzika, ni baad ya kuwa wamesubiri simu ya Anna paka wakachoka.
Japo fedha zilifika na kusaidia matibabu, lakini bado mma Ana akuwa na imani na kule mwanae aliko, yani Dar es salaam, ambako katika familia yao akuna mingine ambae aliwai kwenda zaidi ya Anna, ambae zaidi ya Masoud, Ana akuwa na mtu mwingine anae mfahamu, ambae ange mshika mkono kama mwenyeji wake.
Lakini wakiwa wanatembea taratibu, kwenye jengo ambalo wange pumzika, mala wakasikia simu ya mzee Mdemu ikianza kuita, walipotazama wakaona kuwa ni Anna ndie liekuwa anapiga, “jamani Ana huyu anapiga” alisema mzee Mdemu, huku anaipokea simu, na kuiweka katika sauti ya wazi, kisha akampatia mama Anna, huku wenzake wote, wakisogelea simu, iliyoshikwa na mama Anna, “hallow Anna habari za huko mwanangu” aliongea mama Ana, yani mke wa mzee Sinyangwe, huku tabasamu pana likuwa limetawara usoni pake, “salama tu mama, shikamoo” ilisikika sauti ya Anna, ambayo ilikuwa tulivu, yenye kusikika vyema kabisa, ikitoka sehemu tulivu, “marahaba Anna, baba yako tayari amesha fanyiwa operation, na sasa anaendelea vizuri, na sasa tunapata huduma nzuri, utazania mabosi, vipi wewe unaendeleaje na huyo mwenzio” aliuliza mama Anna, kwa sauti ambayo siyo tukuwa na furaha, sasa ilikuwa na uhai wa matumaini, huku wakina mzee Mdemu, wanafwatilia maongezi ya mama na binti yake, ambayo yalifanyika wka sauti ya wazi.
Naam, hapo Anna, aliachia mguno mdogo, “nimekutana nae mama, lakini yale wanayo yafanya wazazi wake, ni afadhari, yeye mwenyewe amenikana adharani” alisema Anna kwa sauti ile ile tulivu, na hapo siyo mama Ana peke yake, ata wakina mzee Mdemu pia walitoa macho ya mshangao, wakitazama kwenye nyuso zao, kama vile awaamini kinachosikika toka kwenye speeker za simu ile ya mzee Mdemu, asimu ambayo inamsaidiaga sana kuangazia njia, nyakati za usiku, wakati anarudi toa kwenye ulanzi. …….endelea…
UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA HAMSINI NA MBILI
MTUNZI @MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA MOJA: Naam, hapo Anna, aliachia mguno mdogo, “nimekutana nae mama, lakini yale wanayo yafanya wazazi wake, ni afadhari, yeye mwenyewe amenikana adharani” alisema Anna kwa sauti ile ile tulivu, na hapo siyo mama Ana peke yake, ata wakina mzee Mdemu pia walitoa macho ya mshangao, wakitazama kwenye nyuso zao, kama vile awaamini kinachosikika toka kwenye speeker za simu ile ya mzee Mdemu, asimu ambayo inamsaidiaga sana kuangazia njia, nyakati za usiku, wakati anarudi toa kwenye ulanzi. …….endelea….
“we Ana, unamaana gani amekukataa adharani?” aliuliza mzee Mama Anna kwa sauti ya mfano wamtu anaeitaji habari kamili, “yani mama we acha tu, kosa kupata msaada sijuwi ingekuwaje, yani yeye na mwanamke wake wamenifukuza ofisini kwao, na mbaya zaidi niliwafumania kwa macho yangu, Maoud alinisukuma, kwa nguvu, nikaanguka chini, akunijari, wala akutaka kujuwa nimekuja vipi na ninarudi vipi, ataki kusikia kilicho nileta, ndio kwanza anamwambia mwanamke kuwa huyu ndie yule mwanamke niliekuambiaga” alisema Anna nakuzidi kuwashangaza awa wazee, ambao sasa walianza kuelelewa na kujifunza kuamini ile wanacho kiwaza, kwamba familia ya bwana Kizinge, aikuwa na lengo la kutengeneza familia pamoja na famili ya mzee Sinyangwe, bari lengo lilikuwa ni kuitumia familia hii, kwa kumsaidia Masoud, kupata Eimu yake ambayo wao walikuwa wanahisi ni Elimu ya chuo kikuu, cha pale mlimani, nasiyo Veta ya Keko Chuo alichosoma Masoud, “mama nili nalo kumbia sasa, aomba usimwambie mtu yoyote, we waachie weyewe” alisema Anna kwa sauti yenye tahadhari kubwa.
Hapo mama Anna, ambae akujuwa binti yake anataka kusema nini, akawatazama wakina mzee Mdemu, kwa awamu, akianza na Mzee Mwaisaka, mabae aliitikiakwa kichwa kukuubari kuwa amekubariana na Anna, kuwa itaendelea kuwa siri, na ikawaivyo kwa mzee Sanga na mzee Mdemu, wote wakampia ishala ya kukubari kwa vichwa vyao, “nini hicho mwanangu?” aliuliza mama Anna kwa sautiyenye wasi wasi, ma shahuku, maana mpaka sasa hakujuwa Anna amezipataje zile fedha, “masoud siyo bosi wala akuwa anasoma chuo kikuu, kama tulivyo zania” alisema Anna, na kuwafanya wale wazee washtuke kidogo, nakutazama, kama walivyofanya mwanzo, “we Anna unasema kweli sasa zile ela tulizo mpa amefnyia nini?” aliuliza mama Ana kwa sauti yenye mshangao wakuto amini, “alikuwa anasoma kwenye chuo cha kawaida tu cha ufundi, atahivyo na chuo chenyewe akumaliza akaomba kazi hapo alipo danganya kuwa ndio boss”
Ana alisimulia kilakitu kam kiilivyo kuwa, mpaka kuwafumania, na yeye kutimuliwa, “bahati nzuri. yule boss mwenye kiwanda ni mtu wa hapa mafinga, akaamua kunisaidia” alisema Ana ambae alieleza wasi wasi wake juu ya hatua ambayo Sebastian ataichukuwa kwa wawili wale ambao amewafumania bila wao kujuwa” alisema Anna pasipo kujuwa kuwa anasikilizwa na kikundi cha wazee, ambao kila mmoja alimfikilia mzee mwenzao Kizinge, jinsi atakvyo umbuka, kutokana na jinsi alivyo leta majivuno juu ya kazi nzuri gari na nyumba ya mtoto wao Masoud, “mwanangu hayo tuwaachie wenyewe, vipi kuhusu wewe unarudi lini?” aliuliza mama Anna.
Na hapo Ana akaonekana kubabaika kidogo, kama vile asie juwa hatima yake, “nipo hapa kwao, yani jumba zuriiiii, ata kulala kwenye kitanda chenyewe naogopa, ila naangalia kesho, kama atanipa kazi ya ndani, kama sipati kazi, kesho kutwa narudi” alisema Anna, na mama akamaliza kwa kumsisitiza Anna kuwa makini, na pia kesho angeomba kuongea na Sebastian, ili aseme asante, kwa ule msaada mkubwa alio patiwa, kwa matibabu ya mumewe na kwabinti yake.********
Yap! usiku ule pia ulikuwa na utofauti kwa wapenzi wawili, ambao penzi lao ni kama la wizi, yani Salma na Masoud, ambao kila mmoja alikuwa katika hali tofauti na mwenzie.
Wakati mwana dada Salma Ramadhan, akiwa anajilaza kitandani nyumbani kwao, yani pale alipo pangishiwa na mwanaume anampenda sana, mwanaume ambae alimpandisha hadhi na kuonekana mwanamke wa daraja flani la heshima, ambapo akipita barabarani, mwanaume yoyote ange jiuliza namna ya kuanza kumsemesha, “afadhari amerudi, maana ata sijuwi ningeishije, na hivi card za benk zote zime kataa” aliwaza Salma huku tabasamu pana likiwa usoni mwake, akujuwa kama tayari Sebastian amegundua uchafu wake.
Wakati salma anawaza ili na lile huku anajibu sms toka kwa Masoud ambae alikuwa anabembeleza aende japo akapate kimoja, na yeye akimweleza avumilie kwa leo, ila kesho wataendelea na mambo yao, ukweli nikwamba Salma aliofia Sebastian, angeweza kurudi tena ghafla, na kukuta ametoka, mala shangazi nae anafungua mlango na kuingia chumbani, akiwa ameshikiria grass yake ya pombe kali, toka #mbogo_land, “vipi leo uendi kwa kiben ten chako?” aliuliza shangazi, huku anakaa kwenye kitanda, pembeni ya Salma aliekuwa amejilaza kitandani kitandani hapo, “weeee niende akanilegeze, wacha kwanza leo nitulie ili kesho akiingia akute angalau mnato” alisema Salma na wote wakaachia kicheko cha kishangingi, “yani we mtoto leo ungeniumbua vibaya sana, yani shukuru umepata mume zuzu, mwingine pange waka moto hapa” alisema shangazi na wote wakacheka tena.
Naam walingea mawili matatu, kisha kisha wakaagana na shangazi akaenda chumbani kwake, huku akimwacha Salma anatafuta usingizi, huku anasubiri siku ya kesho, akakutane na mpenzi wake, ambae aliamini kuwa amembebea zawadi nyingi sana toka japan, kama ilivyo kawaida yake anapo kuwa ametoka safari kama hizo. …….endelea
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Write your comment