Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Jumatano, 14 Mei 2025

Hadithi: MAJARIBU 21-23 MWISHO


Mpya
Hadithi: MAJARIBU

Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)

Sehemu: 21

"Afande Nadhani kapaniki huyo hasira zikiisha Mimi ntakuja asije akanimeza, ila mwambieni nampa Siku mbili sitaki kumuona kwenye nyumba Yangu, kwenye hilo Sina msamaha!" Majaribu akiwa serious aliongea maneno ambayo yalizidi kumpandisha Sumu Mr Luka.
Baada ya hapo Majaribu alianza kuondoka huku akiwa kaongozana na kina Liam!.
Mr Luka akiwa na Hasira alimkimbilia Kwa nyuma!.

"Dogo naona Sasa kama unanipima unataka ujue mashetani Yangu yalipo lalia Siyo!" Baada ya kumfikia Majaribu, Bwana yule alianza kumwaga mkwara!.

"Hahaa Kwani Mzee mashetani umeanza Leo! Sikiliza kila Mtu afanye mambo yake kiufupi kila Mtu achange kadi zake anavyo weza! Muda wote ulikuwa unaniandama nilikuwa nimekaa kimya, imefika dhamu yako mishipa inakutoka! Jikaze pambana!" Majaribu aliongea maneno yaliyo mchoma Mr Luka kuliko kawaida, baada ya hapo dogo huyo na machawa wake waliingia kwenye Gari na kuondoka!.

Basi zilipita Siku kama mbili! Mama mchungaji alikuwa haamini kama anaweza kutimuliwa kwenye mjengo ule! Yaani Siku alizo pewa zilikuwa zimeisha! Siku Hiyo Majira ya Jioni kama utani hivi, Mama mchungaji alishangaa kundi la vijana wanakuja pale kwake kumhamisha kinguvu.
Yaani Mama mchungaji alitolewa nje Yeye pamoja na Revina tena bila hata kitu chochote maana walikuwa wamepewa Muda wa kubeba Chochote wanacho kitaka Lakini walipuuzia!.

Mageti yalifungwa kama Utani Huku Mama mchungaji akiwa Nje na Revina, Hata mlinzi alitimuliwa Kazi!.
Mama mchungaji akiwa anaona haiwezekani alielekea kituoni kutoa taarifa Lakini badala ya kusikilizwa alipigwa sero Kwa sababu ilionekana yeye ndo mwenye makosa, yaani yeye na Revina wote walitupwa ndani!.
Majaribu alihamia kwenye mjengo ule rasmi, na watu Wake, awamu hii Majaribu alikuwa na Walinzi kama Kumi hivi, yaani alikuwa hataki masihara kabisa!.
Siku Iliyo fuata ilikuwa dhamu ya Mr Luka! Kama alivyo fanyiwa Mama mchungaji pia Mr Luka alifanyiwa vile Vile yaani alitolewa kwenye nyumba yake aliyo ijenga mwenyewe, tena alitolewa kama mwizi au Kibaka.

Kila sehemu ambayo Mr Luka alikuwa anakimbilia kuomba msaada, Majaribu tayari alikuwa katanguliza Pesa Kwa Hiyo Mr Luka alijikuta anapoteza nyumba yake akiwa anajiona! Yeye na familia yake ilibidi wapange nyumba!.
Mama mchungaji hakuwa na pa kwenda pia Pesa ambayo alikuwa nayo ilikuwa kidogo Muno kiasi kwamba iliishia kwenye kupanga nyumba na kununua baadhi ya Vitu vichache 

Maisha yaligeuka Miguu Juu! Kila Mtu aliye husika kwenye Kifo Cha Nemeke na kujipatia Mali Kwa Njia Isiyo Halali Majaribu alikuwa anakula naye sambamba! Baada ya miezi kama mitatu wale wote walio husika walikuwa wameisoma namba, yaani walikuwa wamefirisika vibaya Muno na Yote ilikuwa Kazi ya Majaribu!.

Kutokana na maisha ambayo Mama mchungaji alikuwa anaishi baadhi ya watu wanao mfahamu wengi wao wakiwa waumini walianza kupaza Sauti kwamba haiwezekani Mama huyo afukuzwe kwenye nyumba Zake ambazo aliachiwa na Mumewe! Yaani Kelele zilikuwa nyingi kiasi kwamba mpaka baadhi ya washirika pale kanisani ambao walikuwa wapo upande wa Mama mchungaji waliandamana!

Bahati mbaya kipindi hicho Majaribu alikuwa ashapoteza ushahidi wote, yaani zile flash zote za video zilikuwa zimepotea Katika mazingira ya kutatanisha! Kwa Hiyo alikuwa hana uwezo wa kumfungulia Mama mchungaji Kesi ya Mauaji tena! Japo kuwa Majaribu alitamani afanye hivyo ili amalize Kazi kabisa lakini ndo hivyo alikuwa hana ushahidi Tena.
Basi kelele zile za waumini zilifika mpaka Kwa viongozi wa Juu wa Serikali baadhi yao wakiwa mawaziri! Na chombo kinacho simamia Haki ilibidi kipewe maagizo ya kumpatia Mama mchungaji Haki Yake!.
Pamoja na kwamba hati ya mjengo alikuwa nayo Majaribu iliamuriwa kwamba mjengo urudi mikononi mwa Mama yule na hati akabidhiwe, pia baadhi ya kampuni apewe kama Mke Halali wa marehemu!.

Majaribu hakuwa na hiyana kufanya hivyo Japo kuwa ilimuuma Muno!.

Mama mchungaji alirudishiwa mjengo na kupewa makampuni kama mawili! Hapo walau Mama mchungaji Nuru ilianza kuonekana tena, ila moyoni alikuwa na machungu haswa na kijana Majaribu!.
Mr Luka kutokana na Hali ile naye alikuwa ni Mtu wa kuhaha na kutegemea ndugu zake, maana walau kidogo ndugu zake walikuwa wanajiweza kiuchumi kidogo!.
Ila Mr Luka baada ya kupata taarifa za Mama mchungaji kwamba karejeshewa baadhi ya Mali, bwana huyo aliona ndo Muda mwafaka Sasa!.

Mr Luka aliamua kumuendea Mama mchungaji na kumshawishi, kwanza aliingilia kwenye gia ya Mapenzi, yaani Mr Luka alikuwa kama kasomea swaga na ushawishi! Hakika Siku hiyo alimpiga Swaga Mama mchungaji mpaka Mama Huyo alijikuta analainika na ukichukulia ni Muda ulikuwa umepita tangia ashiriki tendo, Kwa hiyo alikuwa na ugwadu kama Wote!.
Siku Hiyo Hiyo Mr Luka alilala pale Kwa Mama mchungaji na alihakikisha anapeleka Moto mpaka Mama wa Watu anapagawa!.
Na kweli Siku Hiyo Mama mchungaji alipagawa! Yaani ilipo Fika asubuhi Mama Huyo alikuwa anacheka Cheka tu!.

Miezi kama mitatu ilipita Mahaba ya Mama mchungaji na Mr Luka yalianza kukolea kidogo kidogo, tetesi zilianza kuzagaa mitaani kuhusu mahusiano yale, baadhi ya watu walikuwa hawaamini kama Mama mchungaji anaweza fanya ujinga ule haswa wale waumini pale kanisani!.
Ila baada ya miezi kama Sita kupita haikuwa Siri tena Mahaba yalikuwa hadharani, Kwani hata kanisani Mama mchungaji aliacha, Kwa Jinsi Mahaba yalivyo mchanganya Mama mchungaji aliamua kumpatia Mr Luka kuwa ndo msimamizi mkuu wa kampuni Zake mbili!.
Ilikuwa ni kampuni ya kutengeneza na kusambaza nguo, pamoja na kampuni ya kusambaza vyombo vya majumbani!.

Baada ya Mr Luka kuhakikisha kwamba makampuni Sasa yapo mikononi Mwake na Yeye ndo mkubwa, aliamua kumpa Melisa naye kitengo, Mara nyingi Mama mchungaji alikuwa Mtu wa Nyumbani Kwa Hiyo hata makampuni Yake alikuwa hafwatilii Sana!.
Waumini na Watu baadhi ambao walikuwa wanampambania Mama mchungaji mpaka kurejesha baadhi ya Mali, hakika walibaki wanajilauma Kwa kile ambacho walikuwa wanajionea, maana Mama huyo alibadilika kabisa awamu hii alikuwa anazitwanga Bia Kwa kwenda mbele Huku Mahaba ya Mr Luka yakiwa yamemchanganya!.

"Sasa Mr Luka mbona kama umenogewa tena na Mahaba ya Yule mwanamke Wakati tuliongea vizuri unajipenyeza kwake baada ya hapo tunamumaliza tunapata Mali" Siku hiyo Melisa akiwa na Mr Luka aliuliza!.

"Melisa subiri! Mimi siwezi kunogewa na mwanamke kama yule! We mwenyewe unajua fika katika dunia hii mwanamke ninaye muelewa ni Wewe tu, hata Mke Wangu hakufikii Sasa wasiwasi wa nini!?" Mr Luka aliongea!.

"Mr Luka nauliza Kwa sababu nimeona kama Hakuna dalili! Jana nilikuwa naangalia TV Jinsi mlivyo kuwa mnazindua ule mtindo Mpya wa nguo pale, yaani Jinsi mlivyo kuwa mnashikana ujue iliniuma!" 

"Dear mambo matamu hayahitaji haraka, nikikurupuka ntashitukiwa lazima niende Kwa utaratibu"

"Basi Sawa ndo nasubiri Sasa ili niaze kutamba kwenye ule mjengo si unajua tena Nilivyo na Hamu ya kuitwa Mama mjengo!"
Hayo yalikuwa mazungumzo ya Melisa na Mr Luka, hapa ndo tunajua kwamba mipango ya Mr Luka Siyo mizuri kabisa dhidi ya Mama mchungaji!.
Siku zilizidi kusogea hatimaye Mr Luka alifunga Ndoa ya kiserikali na Mama Mchungaji na vyombo vya habari mbali mbali vilichapisha kuhusu taarifa Hiyo!.

"Aliye kuwa Mke wa marehemu mchungaji Nemeke Sasa afunga Ndo na Mr Luka!" Hivyo ni vichwa vya habari ambavyo vilikuwa vimetapakaa kwenye magazeti, kila Mtu aliye Iona taarifa ile alikuwa anashangaa kwamba imekaaje hiyo, kitu Cha kushangaza Mke wa Mr Luka na watoto Wake Wala hawakushituka huwenda walikuwa wanajua mpango wa Mr Luka!.

"Daaa Baba Tino ujue Japo kuwa tulikubaliana ila inaniuma" basi ikiwa ni usiku Siku hiyo Mr Luka akiwa na Mke wake aliye zaa naye watoto kadhaa, Mama huyo alianzisha maada!.

"Mke Wangu Mama Tino hakuna mafanikio yasiyo na maumivu, kama ulinivumilia kipindi kigumu utashindwaje saizi, nimesema Siyo Muda yule mwanamke anaenda kuaga dunia na Mtu mwenye Haki ya kurithi Mali zake ntakuwa Mimi!" Mr Luka alitoa maelezo!
"Haya Mume Wangu nimekuelewa, ila usije fanikiwa pale kwenye mjengo ukampeleka yule Malaya wako Melisa Haki ya Mungu ntatoboa Siri Zako zote!"

"Usijali Mke Wangu pale kwenye mjengo wa Mama mchungaji ni Wewe na Wanangu mtaenda kuishi" Mr Luka aliongea maneno matamu basi yeye na Mkewe walicheka na kugonga!.

Je Mr Luka atafanikiwa kumuua Mama mchungaji!? Na Je kipi kitajiri, maana Melisa kaahidiwa kupelekwa kwenye mjengo, pia Mama watoto kaahidiwa hivyo hivyo!?

Tukutane sehemu ya 22





Hadithi: MAJARIBU

Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)

Sehemu: 22

"Usijali Mke Wangu pale kwenye mjengo wa Mama mchungaji ni Wewe na Wanangu mtaenda kuishi" Mr Luka aliongea maneno matamu basi yeye na Mkewe walicheka na kugonga!.

Maisha yaliendelea huku Rasmi Mr Luka akiwa na Wake wawili wanao tambulika kisheria, na pia akiwa na mchepuko wake Melisa ambaye alikuwa anamtumia na kusaidiana naye kwenye shughuli zake zote chafu!.
Baada ya miezi Kama Sita ya Ndoa ya Mama mchungaji na Mr Luka kupita, Siku hiyo Mama mchungaji alikuwa anasafiri kuelekea Nchi Jirani ambako alikuwa kaalikwa kama mkurugenzi na mmiliki wa kampuni kubwa ya nguo na inayo fanya vizuri!.

Siku Hiyo Mama mchungaji alimuomba Mr Luka amsindikize uwanja wa ndege na Gari, Lakini Mr Luka alitoa visingizio vya hapa na pale, Kwa maana hiyo alipendekezwa binti Revina ndo amsindikize mwanamama huyo uwanja wa ndege!.
Ni kweli Mr Luka alielekea kazini, Revina alimsindikiza Mama mchungaji na Gari uwanja wa ndege!.

Safari ilianza vizuri tu! Lakini baada ya kufika kwenye kamteremko kidogo ambapo mbele yake kulikuwa na Njia zimepishana, Revina akiwa Kasi alijikuta anajaribu kuminya breki ili Gari isimame Lakini breki zilikuwa hazifanyia Kazi!.

"Mama Hizi breki vipi mbona hazishiki" Revina akiwa kaanza kutetemeka aliongea! Maana Kwa mbele taa zilikuwa zimeonesha kwamba asimame kupisha Magari upande wa pili yakatize!.
"Heeeee!! Revina acha Masihara shika breki!" Ma mchungaji macho yakiwa yamemtoka aliongea Lakini ndo kwanza Gari ilikuwa inaseleleka!

"Mama breki hazifanyi kazi!" Revina alijibu tena!.
Revina baada ya kuona Sasa ajali mbaya inaenda kutokea, aliamua kuingia mtaroni kuliko kwenda kuyavaa Magari mengine mbele!?

Gari ile ilienda kujigonga vibaya mtaroni na matairi yalipinduka na kuwa Juu! Yaani ajari mbaya ilitokea tena mbele ya askari ambao wlikuwa wapo pale kwenye mataa!.
Haraka haraka watu ambao walikuwa Karibu walikimbilia eneo la tukio na kwenda kuangalia kinacho endelea!.
Baada ya kuwatoa wahanga ndani ya Gari lile, na kuwachunguza! Mama mchungaji alikuwa kapoteza maisha pale pale! Yaani habari yake ilikuwa imeisha!.
Revina alikuwa bado anapumua Kwa mbali japo naye Hali yake ilikuwa mbaya kuliko Kawaida!

Miili Yote miwili ilikimbizwa hospital, Huku Mama mchungaji akipelekwa mochwari na Revina akipelekwa chumba Cha Dharura!.
Muda huo huo taarifa zilianza kutembea Mitandaoni, kama tujuavyo Mambo ya utandawazi taarifa zinasambaa ndani ya sekunde! Yaani kila Mtu alishitushwa na ajali ile!.

Moja ya Mtu ambaye alishitushwa vibaya Muno na ile ajari alikuwa ni kijana Majaribu, Muda huo alikuwa kakaa nyumbani na kina Liam wanacheza gemu!.

"Duuuuuu kudadeki nilijua tu yule Baba hawezi kumuoa yule Mama bila sababu ona Sasa, oya Fred sikia chukueni Timu nenda kwenye Hiyo hospital kachunguze kila kinacho Endelea, nina uhakika kama yule Binti hajafa basi Mr Luka atataka kumuua, nenda kafanye jambo!."baada ya kuona taarifa ile inapita kwenye video Majaribu aliwaambiwa watu wake!.

"Lakini Majaribu una uhakika kwamba atakuwa ni Mr Luka!?" Liam aliuliza!.

"Namjua vizuri yule bwana hii ajari ya kutengeneza! Eneo lile hapajawahi tokea ajari iweje itokee kizembe hivi!, Nyie nendeni!" Majaribu alitoa Maelezo na kweli Vijana walielekea waliko agizwa!.
Upande wa Pili Mr Luka alikuwa kakaa na Melisa kama kawaida wanajadiliana huku wakiwa wanapeana mawazo!.

"Mr Luka lazima lifanyike Jambo, yule Binti akipona ataeleza ajari ilitokeaje na maelezo yake tatafanya watu waanze kujiuliza na kutakuwa na ualakini!" 

"Melisa hilo nalijua ndo maana Muda huu nimewasiliana na Watu Wangu wafanye juu Chini leo isipite, pia hata Yule Daktari Wangu pale hospital inabidi niongee naye vyema kabisa!"
Mr Luka na Melisa walijadiliana na kupeana mawazo!.
Masaa yalisogea hatimaye ilitimia Mida ya Saa Tano za usiku!.

Mida Hiyo kuna vijana kama watatu walio valia mizuhura usoni walionekana wakiwa wametulia kwenye chumba Cha daktari mmoja pale hospital, baada ya Muda kama Nusu Saa daktari alikuja Mule ndani akiwa na haraka!.
"Okay nendeni mazingira yapo vizuri! Hakikisheni mnatoa ile mirija ya kupumlia, msimkabe maana itagundulika! Haya kazi kwenu kazi iishe ndani ya dakika kumi!" Daktari yule alitoa maelezo!.
Na kweli Wale vijana watatu walio valia mizuhura baada ya kupewa maelezo yale waliondoka Kwa mwendo wa kuangaza huku na kule mpaka chumba ambacho kilikuwa kimeandikwa 'Emergency' Juu ya mlango! Baada ya hapo walizama ndani!.

Lakini kitu Cha kushangaza Mtu waliye muendea kumumalizia hakuonekana mule ndani, walitafuta mpaka kwenye vyoo Lakini hawakuona Mtu! Walirudi Kwa Daktari kutoa maelezo, basi ilibidi daktari awaongoze akiwa anaamini wamekosea mlango! Lakini baada ya kufika ni Kweli Mule ndani hakuweo Mtu!.
Walimsaka karibia hospital nzima Lakini hawakuona kitu.

Siku Hiyo ilipita! Ikiwa ni Siku nyingine taarifa ya kupotea Kwa Revina pale hospital ilisambaa kila kona, askari walijaribu kufanya upelelezi Lakini hawakugundua wala Kupata dodoso zozote kuhusu Revina alipo!.
Mr Luka alikuwa kachanganyikiwa kuliko Kawaida, wengi walikuwa wanadhani kachanganyikiwa Kwa sababu Mke wake kafariki Lakini kumbe alikuwa kachanganyikiwa endapo Revina atakuwa hai!.

Wakati msiba unaendelea, vijana wa Mr Luka walikuwa wanaendesha operesheni ya msako Chini Kwa Chini Lakini wala hawakufanikiwa!.
Basi mazishi ya Mama mchungaji yalifanyika na msibani uliisha, Japo kuwa ni mengi yalizungumzwa, ila baada ya Siku kadhaa maneno yalipotea na Mr Luka alibaki anatamba na mjengo! Rasmi zilikuwa ni Mali Zake Kwa sababu Mke alikuwa kafariki na hakuacha mtoto yeyote zaidi ya Mume.

Siku, Wiki na miezi vilizidi kusogea, hatimaye miezi kama Nane ilipita Pasina mafanikio yoyote ya kumsaka Revina, mpaka hapo Mr Luka alimini Binti huyo alifariki, maana kuna tetesi zilisambaa mitandaoni miezi kadhaa ya nyuma kwamba mwili wa Binti Huyo ulionekana ufukweni na tena ukapotelea kusiko julikana huku wengi wakisema huwenda umeliwa na wadudu!.

Melisa akiwa na shauku na Hamu ya kuhamia kwenye mjengo Ambao ulikuwa wa Mama mchungaji, alishangaa anapata taarifa kwamba Mr Luka na familia yake nzima wamehamia pale kwenye mjengo! Kwanza Siku hiyo palikuwa hapatoshi, Melisa aliamua kwenda pale pale kwenye mjengo kuleta vurugu!.

"Mr Luka unanifanya Mimi kama dekio eee, kwamba nafanya kazi ya kusafisha alafu mwishowe unakuja kunikanyaga, yaani kazi yote niliyo fanya kushirikiana na Wewe leo hii unanifanyia hivi!?" Baada ya kufika pale nyumbani Melissa alianza kufoka!.

"Melisa sikiliza! Ningekuleta wewe hapa watu wangeshitukia Kwa Hiyo kuna nyumba nyingine nimekununulia ntakupeleka!" Mr Luka alijitetea tena mbele ya Mke wake!.

"Hujanishawishi Mr Luka hapa kuna machaguo mawili, either tubanane hapa hapa, au niende nikamwage Siri Zako zote mitaani na mitandaoni kote!" Melissa alikuwa hataki masihara! Yaani Kwa Jinsi Melissa alivyo kuwa anatishia, ilibidi Sasa Mr Luka na mkewe Mama Tino wakubaliane tu kwamba aishi pale, maana mjengo huo ulikuwa wa kifahari kuliko Kawaida!.
Siku zilizidi kusogea, Sasa Mr Luka alikuwa amekuwa Mtu mkubwa na maarufu tena Tajiri maana makampuni yake yalikuwa yanakuwa Siku mpaka Siku!.

Upande wa Pili kwenye Moja ya nyumba ambayo mmiliki wake alikuwa ni Majaribu ambayo ilikuwa katikati ya Mji! Kwenye chumba kimoja ambacho kilikuwa kimejaa dripu na mitambo ya hospital Haswa ya kupumlia, alionekana Binti Revina akizinduka rasmi!.
Ni Mwaka ulikuwa umepita Binti huyo akiwa kwenye koma bado, basi baada ya kuzinduka daktari ambaye alikuwa anamsimamia kisiri alipiga Simu sehemu kutoa taarifa!.

Baada ya Muda wa kama Nusu Saa Majaribu akiwa na Watu wake walionekana wamefika pale wakiwa na kimuhe muhe huku wakiwa kama hawaamini Hivi!.
Ni kweli Revina alikuwa kazinduka huku akiwa anashangaa tu mazingira na watu waliopo mbele yake!.

Matibabu Kwa Revina yaliendelea Kwa kasi Muno, baada ya mwezi kama mmoja tu Revina alipona na kuwa vizuri kiafya, baada ya kusimuliwa kila kitu Binti huyo alibaki akilia tu, kwanza alikuwa anamuonea aibu Majaribu isivyo kawaida, maana kipindi Cha nyuma amewahi toa ushahidi wa uongo kumhusu Majaribu!.
Upande wa Mr Luka baada ya kujiona Sasa yupo vizuri kiuchumi na ana connection za kutosha na Watu wazito, aliaona Sasa ndo Muda mwafaka wa kuanza kumshambulia Majaribu na kulipa kisasi!.

Kwanza kabisa Majaribu alikuwa na Biashara yake kubwa ambayo ilikuwa inahusu kutengeneza na kusambaza mbolea nchi nzima na Nje ya Nchi, kitu alicho kifanya Mr Luka alituma vijana na kwenda kutekeleza madawa ya kulevya ili ionekane kampuni hilo linasambaza madawa ya kulevya kisiri!.
Na kweli Siku Hiyo Majaribu akiwa kwake na Jamaa Zake alishangaa anapigiwa Simu kwamba kampuni yake inahusika na usambazaji wa madawa ya kulevya na meneja Wake ambaye anasimamia kakamatwa!.
Kwanza Baada ya taarifa hizo Majaribu alibakia kaacha mdomo wazi Huku macho yakiwa yamemtoka, na kengere ilikuja kichwani kwamba vita imerudi tena!.

Je Ipi hatima ya Vita hii!??

Tukutane sehemu ya Mwisho ya Hadithi Hii!




Hadithi: MAJARIBU

Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)

Sehemu: 23 (Mwisho)

Kwanza Baada ya taarifa hizo Majaribu alibakia kaacha mdomo wazi Huku macho yakiwa yamemtoka, na kengere ilikuja kichwani kwamba vita imerudi tena!.

"Huyu mpuuzi naona Sasa nilikuwa nimekaa kimya kaanza Vita eee! Au anadhani nimelala" Majaribu akiwa na hasira alijiongelesha!.

"Vipi hivi unaweza ukawa mchezo wa Mr Luka huu au yule meneja hii biashara anaifanya kweli!?" 

"Fred acha maswali ya kipuuzi wewe unashindwa kujiongeza, hapa Nadhani ni kujipanga mpaka huyo Mtu anaanzisha Vita upya maana yake kajipanga" Majaribu akiwa kama kapaniki aliongea!
Kwanza kampuni nzima ya Majaribu ilifungwa Kwa Muda kupisha uchunguzi! Na baadhi ya wafanyakazi walikamatwa kwa ajili ya uchunguzi, pia mmiliki ambaye ni Majaribu aliitwa kituoni kwenda kutoa maelezo!.

"Kiukweli ndugu Zangu Mimi sielewi kitu huwenda ni kweli baadhi ya wafanyakazi Wangu wanafanya hizo biashara ila hata mimi hii taarifa imenishangaza kama ilivyo washangaza nyie Nadhani mkifanya uchunguzi mtajua tu" hayo yalikuwa ni Majibu Ambayo Majaribu aliyajibu!.
Basi uchunguzi ulianza kufanyika kuhusu kile kiwanda Huku lile kampuni la mbolea likiwa limefungwa!.

Siku Hiyo Majaribu akiwa na Jamaa Zake kama kawaida waliamua kumfuata Mr Luka uso Kwa macho pale kwenye mjengo wake ambapo alikuwa anatamba!.

"Dogo vipi kipi kimekupalia mpaka unakuja Kwangu au umekuja kunipigia magoti" Kwa dharau Mr Luka aliuliza baada ya kumuona Majaribu pale kwake.

"Mzee Wangu nimekufuata kukupa tu onyo usije ukaanza kutia huruma, Vita unayo anzisha Mimi nishaimaliza Muda, alafu pamoja na ndevu Zako hata kwenye kiganja changu hujai nakupa Wiki Moja kampuni Langu lote la mbolea naomba lifunguliwe Wewe utajua Namna gani unasafisha kile ulicho kichafua" Majaribu akiwa serious alizungumza!.
Basi Mr Luka Siku hiyo alicheka Muno baada ya kuona Majaribu ni kama kaanza kupata kiwewe!.

"Dogo huu mchezo hauhitaji hasira ndo kwanza tunaanza , ebu naomba uondoke Kwangu Mara Moja!!" Mr Luka akiwa anajiamini alizungumza!.

"Kwako wapi unataka niondoke! Nimekwambia hii Vita huwezi achana nayo narudia mchezo wote nishaumaliza! Kitu Cha mwisho Japo Siyo Kwa umuhimu hii nyumba ni Mali ya Baba Yangu pia ni Mali Yangu Kwa Hiyo jichunge nimekuacha ukae humu kama msaada! Na ukileta mdomo hutaamini!" Majaribu alipiga mkwara baada ya hapo aliondoka!.

"Mr Luka ujue huyu dogo anatumia akili Muno usikute anaongea hivyo Kumbe hati ya nyumba ashaiba umeangalia vizuri!" Melisa ilibidi amkumbushe Mr Luka, ila Mr Luka hakuwa na wasiwasi kutokana na sehemu ambayo alikuwa anaficha hati zake, yaani ilikuwa ni ngumu Muno Kwa Mtu kuiba!.
Kiushahidi tu alielekea kucheki pale alipo ficha na alikuta zipo salama salmini!.

Mara Mr Luka akiwa amekaa pale sebuleni na Mke wake, pamoja na Melisa ambaye naye alikuwa anaishi pale pale Mara Simu ilipigwa, alikuwa ni Majaribu kapiga!.

"Mr Luka nakuheshimu pia nakuonea huruma, tuishi kindugu! Narudia tena ukifanya tukio jingine tena utajuta maisha yako Yote! Kuhusu tukio ulilo fanya nimeshauriana na vijana Wangu tumeamua tukusamehe!" Majaribu aliongea Kwa msisitizo baada ya Mr Luka kupokea Simu.
Basi Luka na Wake Zake walicheka kweli wakiwa wanaona Majaribu kaanza kuogopa na kuingia ubaridi!.

"Mume Wangu shikiria hapo hapo, maana yule mtoto alicho tufanyia kwenye nyumba yetu na kufanya tukapange sitasahau! Yaani hakikisha unampukutisha kila kitu!" Alikuwa ni Mama Tino akimjaza mumewe na kumtia mizuka na hamasa!.
Basi Siku kadhaa zilipita kuna tukio la uvamizi lilitokea sehemu na baadhi ya watu walijeruhiwa ilikua ni sehemu kuna parking ya Magari, baada ya uvamizi ule Magari kama matatu yaliibiwa!.
Ilipo Fika Siku nyingine katika harakati za kupeleleza na msako, Gari Mbili zilikutwa Kwenye nyumba ya Majaribu, ilikuwa ni nyumba ambayo Majaribu alikuwa kajenga kifahari na alikuwa bado hajahamia japo ilikuwa imekamilika!.
Gari jingine lilikutatwa limefichwa kwenye nyumba Moja ambayo ilikuwa ipo nje kidogo ya Mji na ilikuwa nyumba ambayo ni kama pagala, baada ya upelelezi kufanyika iligundulika hata lile Pagara ni Mali ya Majaribu, maana Majaribu alikuwa kapanunua Kwa ajili ya kujenga Shule!.

Moja Kwa Moja kesi ilimdondokea Majaribu! Hakika Pesa nyingi Muno ilimtoka Majaribu kuzima ile Kesi! Yaani alitumia Pesa ya Kutosha!.
Mr Luka alikuwa anajiona ameshikilia mpini na alikuwa anafurahi kweli kweli!.
Siku mbili zilipita, ikiwa ni Jioni Mr Luka alishangaa askari wa kutosha wakiwa wameambatana na Majaribu wanafika pale kwake! Kwanza hakuelewa kafanya nini alibaki kashika kiuno!

"Jamani kuna tatizo mbona mmekuja kishari!?" Mr Luka aliuliza akiwa anahisi imegundulika kwamba yeye ndo aliiba Magari!.

"Mr Luka tumekuja kuhakikisha usalama maana Majaribu anasema alikupa Siku mbili uwe umehama kwake anaona Bado upo tu Kwa hiyo tumekuja kuhakikisha unahama Muda huu!" Askari kiongozi alitoa maelezo!.

"Aaaaaa askari hapa Kwangu jamani! Niliachiwa urithi na Mke Wangu! Hati orijino ninayo na inasoma Jina Langu" Mr Luka alijitetea!
Basi aliambiwa akalete hati, bwana huyo alienda pale anapo tunzaga hati ni Kweli aliikuta kama alivyo iwekaga, basi Meno yakiwa Nje alitoka nayo na kuja kumpatia askari!.

"Mr Luka usituigizie! Kwanza kufoji hati ni Kosa jingine la jinai kabla hatujakuingiza kwenye Kosa hilo beba familia Yako muondoke!" Askari baada ya kuangalia ile hati aliongea Kwa Kufoka!.
Mr Luka ilibidi aichukue ile hati na kuangalia vizuri! Mwili mzima ulipata ubaridi baada ya kugundua ile hati kumbe ni feki!, Kwanza Mr Luka alimkata jicho Baya Muno Majaribu!.

"Mr Luka nilikwambia mchezo unao cheza nishamaliza kitambo muno Sasa umechokoza ni Muda wako wa kujuta!" Majaribu aliongea Kwa nyodo huku akiwa anakaa kwenye sofa!.
Mr Luka Kwa aibu na familia yake ilibidi waondeke pale kwenye mjengo wakiwa Chini ya askari!.

Mr Luka baada ya Kutoka pale alimpigia mhasibu wake Simu, yaani mhasibu wa makampuni yake ili aweze kuingiza Pesa kwenye akaunti yake binafsi zitakazo muwezesha kununua nyumba ya kuishi!.

"Mr Luka mmiliki wa kampuni kasema tuzuie miamala yote kwenye kampuni na Muda huu akaunti zote zipo chini ya uangalizi wake!" Hayo ni maneno ambayo Mr Luka aliambiwa na mhasibu wake, kwanza Mr Luka hakuamini aliona wanamchezea Sasa!.
Akiwa na hasira Moja Kwa Moja alienda mpaka ofisini! Lakin hata Getini hakuruhusiwa kuingia, yaani kiufupi alikuwa hatambuliki kama Mmiliki tena!.
Kwanza Mr Luka machale yalimcheza! Pale pale alienda kuangalia hati na mihuri ya kampuni! Mwanaume huyo alibaki kalowa Huku mapigo ya Moyo yakiwa yanaenda kasi baada ya kugundua kila kitu alicho nacho ni feki!.
Yaani kumbe mchezo wote Majaribu alikuwa ashacheza Muda, kipindi ambacho iliamuliwa Mama mchungaji apewe nyumba na baadhi ya kampuni, Majaribu hakuwa mpumbavu kiasi hicho, kitu alicho fanya alitengeneza nyaraka feki na mihuri feki na alikula Dili na baadhi ya wasimamizi wa makabidhiano yale, bila kujua Mama mchungaji alikabidhiwa kila kitu feki!.
Kwa Hiyo mpaka Mama mchungaji anafariki alikuwa hakuna anacho kimiliki.

Mr Luka kiukweli aliishiwa pozi alijikuta ameanza kujutia maamuzi yake muda ule ule, alitamani masaa yarudi nyuma ili ayasikilize maneno ya Majaribu!.
Siku Hiyo Hiyo Mr Luka akiwa anahaha kuitafutia familia yake sehemu ya kuishi alikamatwa na polisi Kwa tuhuma za kuuwa!.
Baada ya kufika kituoni Mr Luka alibaki katumbua Macho baada ya kumkuta Revina yupo hai.

Kiukweli Mr Luka alijikuta kwenye Wakati Mgumu Muno, yaani Kwa Namna ambavyo Majaribu alikuwa kasuka ushahidi Mr Luka ilikuwa ngumu Muno kuchomoka!.
Baada ya kesi kuendeshwa Kwa miezi kadhaa huku familia ya Mr Luka ikiwa inaishi Kwa ndugu tu, hatimaye Mr Luka alipatikana na Kosa la kusababisha kifo kimakusudi kabisa, ambapo alipigwa nyundo ya Miaka ishirini Gerezani!.

Mwanamama Melisa alibaki ni Mtu ambaye hana mbele wala nyuma, maisha yalikuwa yamemuendea kombo kweli kweli, alijikuta ameanza kuuza mboga za majani mtaani huku akiwa anaona hata aibu kukutana na watu ambao alikuwa anajuana nao!.
Majaribu alibakia anaendeleza Mali za Baba Yake Huku akiwa haachi kutembelea kaburi la mjomba Yake Mr Jedi!

Huo ni mwisho wa Hadithi Hii kutoka Kwenye mikono ya Mwaki Ze Done, tukutane kwenye hadithi nyingine hapa hapa story line usisahau kushare hadithi hii Kwa watu wako. Asante 

********Mwisho********”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu