Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Jumamosi, 24 Mei 2025

𝐇𝐚𝐝𝐢𝐭𝐡𝐢: 𝐔𝐊𝐈𝐌𝐀𝐋𝐈𝐙𝐀 𝐅𝐔𝐍𝐈𝐊𝐀 𝐄𝐏 61-65




UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA SITINI NA MOJA
MTUNZI @MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI : “kwanza nilijuwa tu, Masoud awezi kuwa na binti mchafu kama yule, yani aache wanawake wazuri aje kuwa na mwanamke asie eleweka, kama huyu” alisema mama Masoud, kwa sauti aliyoamini ni yachini, lakini iliwafikia wakina Sanga, ambao waliangua kicheko kikubwa sana, cha kumcheka mama huyu, ambae alishangaa pia, “we mama we, labda nikuambie kitu, kaa tayari kwa makubwa zaidi” alisema Mwaisaka, huku anageuka na kuanza kutembea, huku Sanga akimaliza kwa onyo kali, “na ole wenu muwatumikishe tena awa awa watoto tuna wapeleka polisi” alisema Sanga kisha nae akaanza kutembea kumfwata mwenzie, wakaondoka zao kuwafwata wakina Stivin kule walikoelekea. ENDELEA….

Mama na baba Masoud waliwasindikiza kwa macho, wakina mzee Mwaisaka, mpaka walipo toweka machoni pao, “aiwezekani, hii itakuwa ni njama yao ya kuficha aibu yao” alisema mzee Kizinge huku anatoa simu yake na kuipiga kwenda kwa Masoud, bahati nzuri ikaanza kuita.*******

Naam kijana wetu Sebastian, akiwa mwenye mawazo mengi, uchungu na hasira, alikamata njia moja kuelekea mikocheni, na akiwa njiani alipoke simu toka Mafinga, akipewa taarifa kuwa mgonjwa anaendelea vizuri, na huduma zinatolewa vyema kabisa, nae akasisitiza kuwa mgonjwa na mke wake watazamwe vyema.

Sebastian alipo kata simu hiyo, akapigiwa simu na bi Saphia kwamba tayari amesha maliza kazi yake, na pia akamweleza kuwa ata mtumia gharama kwa njia ya sms, “sawa nitumie nikurushie fedha yako” alisema Sebastian, na kukata simu, kisha akapiga namba flani, iliyo ifadhiwa kwa jina la Fundi Fred.

Simu iliita kidogo na kupokelewa, “niambie boss” ilisikika sauti toka upande wapili wa simu, “sikia fred, acha kila unacho kifanya, nenda sinza kwa Salma, kachukuwe gari, kisha uje nalo Mikochen” alisema Sebastian, akimweleza huyo Fundi Fred, “haaa kaka ndio unataka umkabdhi lile toyota wish?” aliuliza Fred ambae ni wazi alikuwa anafahamu mpango wa mwanzo wa Sebatian, wa kumbadirishia Salma gari, “we fanya hivyo hayo mengine aya kuhusu” alisema Sebastian akijitaidi kucheka, kwa lengo la kuficha asira, iliyopo moyoni mwake, “aya kaka kwahiyo niende sasa hivi?” aliuliza Fred, “nenda sasa hivi na ulilete mikocheni” alisisitiza Seba, kisha akakata simu.

Baada ta hapo akapiga simu kwa Salma, ambae pia alipokea, lakini alionekana kuwa alikuwa njiani, “vipi baby ushanimiss?” ilisikika saitu ya Salma, huku iliyojaa mahaba deke deke, sijuwi kwanini Sebastian alicheka kidogo, tena kicheko tulivu, “nimepiga kukuambia kuwa naelekea nyumbani, kwa jinsi navyo jisikia, kwakweli sitowezakuja huko, nitakutembelea kesho, nikiamka vizuri” alisema Sebastian, na hapo Salma akaongea kwa sauti moja yenye mbembelezo wa ajabu, “jamani baby, mbona nina bahati mbaya mimi, ningekuwa naluhusiwa ningekuja kulala kwenu” maneno ya Salma yalimfanya Seba tabasamulie pembeni, maana kila alichokifanya Salma, alikiona ni kama maigizo tu, “homa imeniaribia, nilikupania sana kipenzi” alisema Seba, kwa sauti tulivu, huku usowake ukionyesha wazi kuwa, alikuwa anamsanifu Salma, ambae aliachia kicheko cha raha, “usiwe na wasi wasi baby, mimi ni wako, kunywa dawa upone, maliyako hipo tu, kana wakuigusa” iloneno la Salma, nikama lilimtibua Seba, ambae alijizuwia kuonyesha hasira zake, “sasa anakuja yule fundi wetu Fred, ambae anatutengenezeaga magari yetu, mpatie gari akalilekebishe, mengine tutaongea” alisema Sebastian kisha wakaagana na kukata simu.*******

Naam mida ya saa nne za asubuhi, njaa ikiwa imeshaanza kumtekenya, Masoud aliekuwa amejilaza kitandani anaperuzi simu yake, anatazama post zake mtandaoni, na kujibu maoni ya rafiki zake, mala simu yake ikaanza kuita, kwa kuwa simu ilikuwa mkononi akaliona jina la mpigaji, kuwa ni baba yake, “khaa! huyu mzee anazani fedha inaokotwa au” alisema Masoud kwa sauti ya ukali, huku akiitazama simu inaendelea kuita, pasipo kuipokea.

Masoud aliitazama Simu yake pasipo kuipokea, mpaka ilipokatika, hapo ndipo kwa haraka sana, alipo bofya ile namba na kuleta mpangilio wa upangaji, na kukuboya sehemu iliyoandikwa, zuwia namba, alafu akaendelea na upekuzi wake kwenye mtandao wa kijamii, huku njaa ikiendelea kumchamanda.

Dakika kumi baadae, uzalendo ulimsinda Masoud, na kuinuka kitandani, kwa lengo la kwenda kujinunulia chochote kwenye magenge ya mama nitilie yaliyopo mtaa mbele yao, yani barabarani.

Lakini ile natoka nje tu, akaliona gari la Salma linasimama mbele ya nyumba yao, “yes amesha rudi” alisema Masoud, huku anarudi ndani na kupiga simu kwa Salma, ambae akuchelewa kuipokea, “niambie babyndio umesha nimiss tayari?” aliliza Salma kwa sauti ya chini yenye deko la mahaba, “yani mama hapa nimekumiss sana, mixer njaa, natamani nife” alijibu Masoud, “usiwe na wasi wasi baby wangu, ngoja nikutengenezee chai ya nguvu, ule upate nguvu, unishugulike aswaaaaa, maana leo ni siku yetu, Seba anaumwa, atokuja huku” maneno ya Salma yali mfanya Seba asisi kwena mwili, “vipi kuhusu ile ela ya mzee, Maana ananipigia simu kama ananidai” aliuliza Masoud, na hapo Salma akamweleza kuwa avute subira kidogo, Seba arekebishe Card za benk.********

Naam Sebastian alifika nyumbani, kwake mikocheni, nakuingia ndani moja kwa moja, akiwa na hamu ya kumwona mgeni wake, katika mwonekano wa baada ya kuingia saloon. ENDELEA….



UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA SITINI NA MBILI

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA MOJA : Naam Sebastian alifika nyumbani, kwake mikocheni, nakuingia ndani moja kwa moja, akiwa na hamu ya kumwona mgeni wake, katika mwonekano wa baada ya kuingia saloon. ENDELEA….

Sebastian alimkuta Ariana, sebuleni anatazama filam, ukweli akuwa amebadirika sana, ila angalau sasa angeweza ata kukaa nae kwenye gari na kutembea mitaani, achana na ngozi yake ambayo bado ilkuwa aijabadirika, ila angalau ilionekana kung’aa kidogo, na dalili ya kunyorolika, kama ngozi ya mwanamke inavyotakiwa kuwa, ila sasa upande wanguo japo zilimpendeza lakini siyo sana, “sante kaka Seba, nime jitazama kwenye kioo, nimekuwa mzuri” alisema Anna huku anacheka cheka, “usjari dada Ana, sasa endelea kujihudumia kila siku kama ulivyo elekezwa, asa utumiaji wa mafuta, na pia Saphia atakuwa anakuja kusaidia kila week end, nataka ukirudi Mafinga uonekane bomba, upate mume mzuri” alitania Seba, kabla ajamweleza Ana akaingie kwenye gari waende wakatembee, kama alivyoomba jana.******

Naam nusu saa baadae, tayari Sebastian alikuwa ndani kwa kina Salma yupo na Salma na shangazi yake, wanamalizia kupata chai, kwa sambusa za nyama, pasipo kujuwa kuwa, tayari Tino alikuwa anachukuwa picha na video fupi fupi. kupitia dirishani, “mambo yameia sasaaa. yani Seba ameamua ukae nyumbani ujiandae kwa harusi” alisema shangazi yake Salma, kwa sauti iliyo jaa ushambenga, “shangazi yani naomba nikisha olewa uwe unapiga simu kwa Seba unaniomba nije kulala huku, ili niweze kulala na Masoud wangu” alisema Salma kwa sauti ya kujidekeza, “ilotu mwanangu, wala usihofu, we ata ukitaka nikuite kila siku nitampiigia simu” alisema shangazi, huku Masoud akitabasamulia chini, kwa kufurahia maoongeszi ya Salma na shangazi yake.

Mangezi aya kudumu sana, Salma na Masoud wakatoka nje, tayari kueleke kwenye nyumba anayoishi Masoud, na wakiwa nje, ndipo walipo mwona Fred, akiingia pale kwa, akiwa amebebwa na boda boda, “hooo fundi karibu ndiyo ume fwata gari” alisema Salma, huku anageuka na kurudi ndani, “ndyo bwana ila naomba uongee na bro, mniuzie ili” alisema Fred, huku anajichekesha.

Zailipita dakika tatu, akabla Salma ajatoka nje akiwa na funguo mkononi, “unasema nikuuzie alafu mimi nitatembelea nini?” aliuliza Salma, huku anampatia Fred funguo za gari, “haaa shemeji bwana, kwani siri, au bro ajakuonyesha gari lako jipya, ambalo alipanga akirudi tu, akukabidhi” aliuliza Fredkwa namna flani ya kimbele mbele, “usiniambie, inamaana Seba anataka kunfanyia surprise” alisema Salma kwa sauti ya juu iliyojawa na furaha, “nimeliona kwa macho yangu, yani gari jipya kabisaaaa! sasa ndio utakuwa unaendesha kama mke waboss kweli” alisema Fred huku anafungua gari na kungia ndani, kisha akaliwasha na kuondoka zake, akimwacha Salma anapiga kelele za shangwe, “baby mambo yetu yanaenda kuwa supa, twende zetu ndani tukasherehekee” alisema Salma, aliekuwa amefurahi kwelikweli kwa taarifa zile za Fred, paspo kujuwa habari za Fred ni za siku za nyuma, tena kabla ya safari.********

Naam mzee Kizinge, alikuwa amekaa na mke wake kwenye kiambazacha nyumba yao kubwa, hiyo ilikuwa ni baada ya kupiga simu zaidi ya mala ishilini, kwa kijana wake, Masoud, na kuaambiwa kuwa inatumika, alimini kuwa mida hii yakazi, kijana wake atakuwa anapokea simu nyingi za za kikazi, hivyo itakuwa vyema kama atampigia baadae.

Hapo mzee Kizinge anamke wake waliokaa mita chache toka lilipo trekta, wakaanza kujadiri juu ya kile walicho sikia toka kwa wakina Sanga, kwamba, siyo tu kwamba zile fedha walizo zania zimetumwa na Masoud kwenda kwa mzee Sinyangwe, zilitumwa na mtu mwingine, ila pia waliambiwa wasubiri mambo mengine mzito, “wanamaana gani tusubiri mzito zaidi” aliuliza mama Masoud, huku anatazama vyombo vichafu, vilivyo lundikwa karibu na bomba la maji, “kwanza kama ingekuwa siyo masudi alie tuma hizo ela sisi tungejuwaje kama kuna ela imetumwa?” aliuliza mzee Kizinge, huku anatazama nguo yake chafu iliyojaa mafuta lainishi ya maungio yagari, (grice) iliyokuwepo katika fungu la nguo chafu, pale mbele yao, ambayo ilikudiwa ifuliwe na stive mtoto wa Sinyangwe, yani mdogo wake Anna, “ata mimi nashangaa, au wamepanga kufanya hivyo ili kutuzuwia tusi wachambe?” alisema mama Masoud, na hapo wote wakaangua kicheko cha nguvu, “yani walitufanya sisi wajinga sana, na bado, wata kiona cha moto, au imewauma Ana kukataliwa adharani” alisema mama Masoud, na mzee Kizinge akadakia, “kwanza umemwona mwanamke mwenyewe, amekomaa ata trekta langu lina subiri” alisema Kizinge na wote wakaongezea kicheko.******

Naam safari ya matembezi, kati ya Sebastian na Arianna, ilikuwa nzuri sana, walitoka mikocheni, wakaingilia kinondoni, alafu walipofika njia panda ya moroco, wakakona kushoto na kufwata barabara ya sarenda, ambapo waliambaa mbaa na barabara hiyo ata kuna wakati Anna, ambae ushangaaji wake ulikuwa kama burudani kwa Sebastian, aliweza kuiona bahari na kutoa macho kwa mshangao, “weeee mbona huu mto mkubwa sana, ndio maana huku maji yanatoka kila sehemu, kwenye ukuta, ata juu ya dari” alisema Anna, ambae alimwacha njia panda mwenyeji wake, “mh! we umeona wapi maji yatoka ukutani na darini?” aliuliza Sebastian kwa mshangao, “mh! kwani wewe ujaingia kwenye kile chumba nilicho lala mimi, choo cha kuoo alafu kina chemi chemi, (chem chem), alafu ukuta wake unatoa maji wameweka kibomba, ata juu ya dari pia wamechomeka bomba, maji yana wagika kama mvua, yani mjini raha sana” alisema Anna kwa sauti iliyojaa hisia kali toka moyoni, kiasi cha Seba kumtazama mwanamke huyu, kwa macho ya mshangao. ENDELEA….



UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA SITINI NA TATU

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA MBILI : “mh! kwani wewe ujaingia kwenye kile chumba nilicho lala mimi, choo cha kuoo alafu kina chemi chemi, (chem chem), alafu ukuta wake unatoa maji wameweka kibomba, ata juu ya dari pia wamechomeka bomba, maji yana wagika kama mvua, yani mjini raha sana” alisema Anna kwa sauti iliyojaa hisia kali toka moyoni, kiasi cha Seba kumtazama mwanamke huyu, kwa macho ya mshangao. ENDELEA….

Ukweli alimwona Anna alikuwa anamaanisha anachokisema, na kabla aja mwelekeza juu ya maji aliyo yaona, Ana akaongeza neno, “wenzio Nalangari, mabomba machache, vinginevyo maji mtoni, tena mito midogo, siyo kama huu wa dar es salaam, ona magari yanapishana kama ngombe wanaenda machungani, sisi kule kama ujaona gari la magogo au viazi, basi trekta la mzee Kizinge” alieleza Anna na kumfanya Sebastian ashindwe kujizuwia kuangua kicheko, ilifikiahatua akaamua kuweka gari pembeni na ili acheke vizuri.

Dakika tano zilipita Sebastian akuendelea kucheka maana kila alipo maliza kucheka na kutaka kumfafanulia ana juu ya mashaka yake, anajikuta anaangua kicheko, sasa ilifikia hatua Anna nae akaanza kucheka, akikicheka kicheko cha Seba, na kicheko cha Anna kilizidi kumchekesha Seba, hakika angepita mtu ghafla angezania wawili awa wameshikwa na uchizi wa ghafla, “Anna ebu acha tafadhari, utanivunja mbavu mwenzio” alilalamika Sebastian, huku anajishika sehemu za mbavu, “wewe siulisema umesoma mpaka kidato cha nne, sasa unasemaje maji yana toka ukutani” aliuliza Sebastian huku analazimisha kukomesha kicheko.

Hapo Anna akaonekana kushangaa kidogo, “kwani nyie huku dar, mnasoma mpaka maji ya kwenye ukuta na chemi chemi ya chooni, hapo akakimamsha tena kicheko cha Sebastian, ile siyo chem chem Anna, yale nimaji yanayotoka kwenye mabomba” alisema Seba ambae alikuwa amesha juwa Ana anazungumzia Chem chem hipi, yani yale maji yachoo cha sink, kule kijijini, uwa wanatumia vyoo vya shimo, “sasa mbona toka jana usiku mpaka sasa hivi tulivyo ondoka, maji bado ayajakauka” dah! siyo jambo la kucheka, ila inachekesha kwakweli.

Seba alicheka kiasi cha kufikia hatu sauti inakwamia kooni, “unajuwa zamani nilijuwa ni hadithi za mbogo edgar tu, kumbe ni kweli kuna vituko kama hivi” alisema Seba, huku anaendelea kuangua kicheko, “Anna nakuomba usiongee kwanza tumalize mizunguko, sasa ushangae kimya kimya nitakueleza kila tu” alisema Seba akionekana kuomba poo, “unazani sitamani kukaa kimya, natamani sana, ila ndiyo nakuta tu nimeongea” alisema Anna, na kusababisha kicheko kingine safarihii wakicheka wote.******

Wakati wawili awa waliopokonywa wapenzi, wakiwa wamegawana madaraka mmoja akiwa mshamba (alie toka kijijini kuja mjini) na mwenzie Mshambuzi, (mwelekezaji wa mshamba) hiki ni Kiswahili cha #mbogo_land, sidhani kama kuna aja ya kutafuta kamusi, wakiwa wanasahamu shida zao kwa vicheko, huku nako wapenzi wawili, walio ibana toka kwa wapenzi wao, wenye malengo mazuri na wao, walikuwa chumbani, uchi wa mnyama, wakibadiri shuka, ambazo zilikuwa azitamaniki kwa uchafu, chumba pia kilikuwa kina nuka ungesema ni chooni, sehemu zao zasiri ungesema ni kinu na mtwangio, wa kisamvu.

Hayo ni matokeo ya kushrehekea gari jipya, na kitutolewa ofisini, kitu ambacho Salma kama Salma, aliamini kuwa, ni dalili za kuanza kwa taratibu za kufunga ndoa, ukizingatia maneno ya Sebastian, yakwamba asubiri kitu ambacho yeye Salma amekuwa akikitegemea, kitu ambacho amekifanyia juhudi kitokee.

“Sasa Salma, pale ofisini atakuwepo nani?” aliuliza Masoud wakati wanaingia bafuni, kunguza uchafu ulio tapakaa maungoni mwao, “sjuwi mjinga gani yule, jina lime niitoka kidogo, ila mimi nimemwambia nataka ukae wewe, kama leo ungewai ofisini, basi mpaka sasa ungekuwa boss pale kiwandani” alisema Salma kwa mbwembwe za ufahari, “daah! kwahiyo nimekosa nafasi hiyo?” aliuliza Masoud, kwa sauti yenye kujilahumu, “walaaaa ujaikosa, Seba awezi kunikatalia, nitahakikisha una kuwepo pale ofisini” alisema Salma, ambae pia alionyesha kuwa na wazo jingine, “alafu Masoud, inabidi ifikie wakati ukae mbali na ile ofisini, ili tusi gunduliwe mapema” alisema Salma na hapo Sema akatia shaka, “mh! nitaishije hapa mjini, we siunaona mpaka nime mboack mzee Kizinge?” aliuliza Masoud, kwa sauti yenye mashaka.

Nahapo kwa macho ya mahaba, na tabasamu mwanana, Salma akamtazama Masoud, “sikia baby, wewe ni mwanaume tena unaujuzi wako, ngoja card zifunguliwe alafu nikupatie ela ufugue ofisi yako ya nguvu, au utashindwa kuisimamia?” aliuliza Salma, kwa sauti iliyojaa mahaba, “kwanini nishindwe, tena ilo wazo zuri sana” alisema Masoud, huku anamkumbatia Salma, pasipo kujari uchafu uliojaa makalioni mwampenzi wake huyo, sijuwi sababu yeye ndie alie usababisha.

Naam wawili awa walianza kuoga, huku wakifanyiana michezo ya kimahaba, pasipo kujuwa walikuwa wanafwatiliwa kwa karibu, huku wakichukuliwa video na picha za kila rangi, wakati mwingine ata vipande vya sauti, pale Tino alipoona kuwa awezi kuwapata kwa picha, ujuwe ata kuna wakati, Tino mwenyewe, aliogopa kwamba, kama zile picha zinaweza kuvumilika mbele ya macho ya Sebastian, maana wawili awa walikuwa wanajuwa kutifuana.********

Naam Safari ya matembezi aikuwa lahisi, kwa Sebastian na Ariana, japo ilikuwa tamu ya kuburudisha, kiasi kwamba, toka ile saa nne mpaka saa kumi na moja jioni, waliona ni kama nusu saa tu, kwa burudani walizo peana, japo aikuwa burudani, mgusano, au burudani ngono, kama ilivyo zoeleka kwa sisi watu masikini, ya kwamba burudani yoyote, isikose pombe vyakura na kunyanduana, au angalau kipatikane kimoja wapo, ila tofauti na wenzetu wenye fedha na wasio iwazia kesho, wao burudani ni moyo wake ufurahi tu, basi hiyo ni burudani tosha.

Safari ambayo mwanzo, Sebastian aliifanya kwa kumfurahisha Ana, ambae kiukweli alimini kuwa Ana ndie mwasirika mkubwa wa uthariti wa wakina Salma, ebu fikilia, akujari uzuri wake, akujari ulaji wake, alijitolea kufanyakazi na kukodisha shamba kwaajili ya Elimu ya mumewake wabaadae, lakini baada yake, mwanaume huyo anamkataa, na kumweleza kuwa walisha achana muda mrefu uliopita. ENDELEA…




UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA SITINI NA NNE

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA TATU: Safari ambayo mwanzo, Sebastian aliifanya kwa kumfurahisha Ana, ambae kiukweli alimini kuwa Ana ndie mwasirika mkubwa wa uthariti wa wakina Salma, ebu fikilia, akujari uzuri wake, akujari ulaji wake, alijitolea kufanyakazi na kukodisha shamba kwaajili ya Elimu ya mumewake wabaadae, lakini baada yake, mwanaume huyo anamkataa, na kumweleza kuwa walisha achana muda mrefu uliopita. ENDELEA….

Kiukweli safari ile siyo tu, ilikuwa burudani kwa Anna pekee, bari ata kwake yeye Seba, inakuwa burudani tosha kabisa, maana kumbuka kwamba, licha ya kuwa ni kijana alie kulia katika familia ya kitajiri, lakini akuwai kutoka nyumbani na gari, na kuanza kuzunguka jiji la dar, kwa minajili ya kuzurula kama leo, yanikila alipotoka alikuwa anaenda sehemu flani, kwaajili ya kitu flani, ata kama ni matembezi, basi angetoka nyumbani akiwa ameshapanga kabisa sehemu za kwenda.

Maana leo ikiachilia vicheko vya mala kwa mala, walizunguka sehemu nyingi za jiji la Dar, huku Sebastian akichukuwa jukumu la kumwelezea aku kumtambulisha mitaa na sehemu zote walizo pitia, “hii ni bahari, ya hindi” alisema Sebastian wakati flani wakiwa maeneo ya kivukoni, pale magogoni, “he! kumbe bahari ndiyo hii” alisema alisema Ana kwa mshanga mkubwa, “ndiyo hii, ni kubwa sana, imeanzia kule tunako kaa, mpaka huku, unaenda kenya mpaka huko msumbiji” alifafanua Sebastian, huku anamtazama Anna alieonekana kushangaa zaidi, kama vile kuna kitu amekiona upande wa kigamboni, “jamaniiii, kumbe ni karibu hivi?” alisema Anna, huku anatazama upande wa kigamboni, kwa mshangao mkubwa wa kustaajabu, Seba nae anatazama upande wa kigamboni, “yah! nikaribu, tena kuba barabara ya kuzungukia mbagara” anaeleza Sebastian, kwa ufafanuzi zaidi.

Hapo Ana anamgeukia Seba, na kumtazama kwa macho ya mshangao, “sasa nani muongo hapo kati ya wewe na walimu?” aliuliza Anna akionekaana akuwa na na utani ata kidogo, “kwanini uongo?” aliiuliza Seba stain ambae sasa mbavu changa zilikuwa zina muuma kwa kucheka, “si wanasema Zanzibar imezungukwa na maji kote kote, sasa hiyo barabara inapaje kwenye maji” alisema Anna na hapo Seba akatoa macho kwa mshangao, “nani kasema kuna barabara ya kwenda Zanzibar?” aliuliza Seba kwa mshangao, kabla ajagundua alichokuwa anamaanisha Anna, “Ana ahapana siyo sasa hivi, bwana watu watanishangaa, hahaha!” tayari Seba alishaponyokwa na kicheko, “pale nikigamboni wewe, siyo Zanzibar, hahahaha” alisema Sebastian akiendelea kucheka, lakini mbona naona meli ile pale una enda nawatu” alsema Ana ambae jina kigamboni siyo geni kwake.

Ukiachia ilo, pia, walienda sehemu nyingi kama Kaliakoo, ambako ana alipata nafasi ya kufanya manunuzi ya nguo viatu na vitu alivyoona vina faa, huku seba akiwa mshauri wake, muda wote walikuwa wakiongea na kucheka, ata wakati flani Seba alijikuta anafanya vitu ambavyo pengine kutokana na adhi yake asinge vifanya, kama kula vitafunwa vinavyouzwa njiani, kwaajili ya ushawishi wa Ana, ambapo walizinguka karibia mitaa yote ambayo ana alitamani kufika, ili ajione kama amefika Dar, kama vile magomeni manzese, buguruni, na kwingineko, ata kuna wakati Sebastian akimnunulia Ana simu mpya ya kisasa, ambapo Ana aliomba awekewe line nyingine, ambayo ingeweza kukaa kwenye simu ile, maana akuwa na kitambulisho cha kuweza kusajiri line ile katika umbo dogo, hivyo Sebastian akafanya hivyo, japo siyo vyema.

Hakika ilikuwa ni burudani kwao, “Anna sasa mpango wakoni nini baada ya kuachana na Masoud?” aliuliza Sebastian wakati wanarudi nyumbani, wakitoka kwenye matembezi ya kutwa nzima, “mh! kwakweli ata sjuwi nifanye nini, maana Masoud alichukuwa nafasi ya wadogo zangu, baada ya kusimamia Elimu yao wote tukasimamia Elimu ya Masoud, hapa sijuwi nifanye nini ili kufidia kile walicho poteza” maneno hayo yalimtoka Ana, kwa sauti iliyojaa tabasamu, akionyesha kuto kufikilia chochote, juu ya muda na vitu alivyopoteza.

Ilitia uchungu, kiasi kwamba ata seba aliezowea kucheka kwa kila neno la Ana, sasa alijihisi uchungu mkubwa moyoni mwake, “nishuguri gani kule kwenu ambayo inaweza kukupatia fedha?” aliuliza Seba kwa sauti tulivu, huku safari ikiwa inaendelea, “kazi ya vibarua vya kulima na kuvuna mashamba ya watu” alijibu Ana bila wasi wasi na kificho chochote, ilizidi kumtia uzuni Sebastian, “Ana mimi nataka upige hatua zaidi, usifanye tena vibarua, nataka wewe ndio uajiri watu wakufanyie kazi” alisema Sebastian, na kumfanya Ana amtazame usoni, tena kwa macho mduwao.

Ana alimtazama Sebatian kwa sekunde kadhaa, kabla akija mponyoka kicheko changuvu, kicheko kilicho dumu kwa nusu dakika, kiasi cha kumshangaza Sebastian, ambae alijizuwia kucheka, “sasa unacheka nini Ana?” aliuliza Seba, wakati huo wanakariba geti la kuingia nyumbani kwao, “yani mimi niajiri watu, hiyo ela ya kuwalipa nitaitoa wapi, kwanza kwa shamba gani?” aliuliza Anna, na kumfanya Seba atabasamu kidogo, “Ana siulisema yule mile mkodisha samba amesha maliza mkataba wake, na mnarudisha shamba lenu?” aliuliza Sebastian, “ilo shamba uwa atulimi lote, atuwezi kulihudumia” jibu la Ana lilikuwa sahihi kabisa.

Naam wawili awa waliingia ndani, huku wanaendelea kujadiri, juu ya mstakabari wa Ana, na familia yake kwa ujumla, “ujuwe nilazima ukubari mabadiriko, ambayo kila mmoja anayaitaji, kumbuka sasa mama sivyema ibabidi amwangalie baba yako, pia wadogo zako nivyema ukawaacha wasome, kuliko kuwausisha kwenye vibarua, kwamaana hiyo utakuwa peke yako katika vibarua, ambapo utalazimika kujiumiza zaidi ili uweze kufanya kazi ambayo itakupa fedha za kuilisha familia, ambayo kwa vyovyote aito tosha kwa matumizi yote, na kufanya maisha yabakie vile vile” alisema Sebastian wakiwa wanaingia ndani, wakati huo yalisha pita masaa saba, ajaiona simu toka kwa Salma, “sasa nitafanyaje wakati maisha yenyewe ndivyo yalivyo” alisema Anna kwa sauti yenye kukata tamaa, “mimi najuwa la kufanya chamsingi uniahidi kuwa hupo tayari kusongambele” alisema Subastian wakiwa sebuleni.

Hapo Ana akamgeukia Seba, aimtazama kwa macho yakuto kuamini, “weeee kaka wewe, unazani nitasema sitaki kuwa kufanya hivyo, kwani mimi napenda kuangaika hivi?” alijibu Ana, kwa sauti iliyochangamka, huku akimtazama Sebastian kuona ata fanya nini, “ok! ,simu wa kilimo unakaribia unakaribia, utasimamia shambalote likilimwa na kupandwa viazi, utaajili watu kwaajili hiyo, ila hakikisha unaendelea kujitunza, ili upate mume mzuri” alimaliza kwa utani Sebastian.. …. endelea …


UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA SITINI NA TANO

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA NNE: Hapo Ana akamgeukia Seba, aimtazama kwa macho yakuto kuamini, “weeee kaka wewe, unazani nitasema sitaki kuwa kufanya hivyo, kwani mimi napenda kuangaika hivi?” alijibu Ana, kwa sauti iliyochangamka, huku akimtazama Sebastian kuona ata fanya nini, “ok! ,simu wa kilimo unakaribia unakaribia, utasimamia shambalote likilimwa na kupandwa viazi, utaajili watu kwaajili hiyo, ila hakikisha unaendelea kujitunza, ili upate mume mzuri” alimaliza kwa utani Sebastian.. …. endelea ….

 kauri ambayo ilimfanya Ana atabasamu kwa aibu, “sawa nitasimamia” alijibu Ana, kisha wakapanda ngazi kuelekea ghorofani kila mmoja akienda chumbani kwake, “aya dada Ana ukaoge maji ya darini” alisema Sebastian wote wakacheka kwanguvu, kiasi cha kuwashangaza wafanyakazi wengine.*******

Naam saa mbili na robo za usiku, kijijini Malangari, nyumbani kwa mzee Kizinge, ambako mzee huyu na mke wake, walikuwa wamekaa mbele ya uwanja wa nyumba yao, wanaota moto magunzi ya maindi, huku wakiwa wameshiba viazi vya kuchemsha, maana leo apakuwa na chakula kingine, sababu bwana Kizinge alisha maliza fedha, siku iliyopita, kwenye matengenezo ya trekta, na elfu kumi iliyobakia alinywea ulanzi, pamoja na rafiki zake, akiamini leo angetumiwa laki tano na mwanae Masudi, ambae mpaka sasa anampigia simu, lakini inaonekana kuwa simu ile inatumika, “hivi mtandao mbovu, au simu ya Masoud, ndio mbovu, maana sizani kama anatumika masaa yote aya?” aliuliza mzee Kizinge, kwa sauti ya kutilia mashaka.

Ukweli mama Masoud akujibu chochote, maana alikuwa amechukizwa kwa kitendo chakula viazi chuku chuku, sababu mume wake alikuwa ameshamaliza fedha yote, “hii siyo bule lazima kuna mkono wa mtu, yani watu wakijiji hiki mimi nawafahamu awakubari kaa wakaona mwenzao anafanikiwa, lazima wafanye maujinga yao, inawezekaje simu ya ikawa busy muda wote huu” alisema mzee Kizinge, huku anajaribu tena kupiga simu, ambayo ilimweleza kuwa simu anayopiga inatumika” alisema mzee Kizinge ambae saa alianza kuamini kuwa, kuna mkono wa mtu katika jambo ilo, pasipo kuweka wazi anamlenga nani.

“Yani we acha tu, mtoto kupata kijikazi, na kununu hicho kigari tu, tayari wameshaanza vituko, sasa mtu gani huyo anaongea na simu toka asubuhi mpaka usiku kama huu?” alalamika mama Masoud, kwa sauti ya kukata tamaa, nkiona inazid na mimi nitaanza kuannkaika, we ngoja uone” alisema mzee Kizinge, kwa sauti iliyo onyesha kuwa anaamini kuwa, kunamkono wa mtu ulio sababisha simu ya Masoud kuwa vile.******

Mida hii nyumbani kwa mzee Kiguru, familia ilikuwa mezani inapata chakula cha jioni, tayari walikuwa wamesha pata taarifa za kijana wao Sebastian, ambae sasa alikuwa jilani sana na yule mschana toka Mafinga, japo akuonyesha dalili yoyote ya kumtamani kimapenzi, ila taarifa zinasema kuwa wawili awa walikuwa wanaongea wka furaha pasipo kuonyesha dalili za kwamba wamepigwa na vitu vizito, na wapenzi wao, pia walisha ambiwa kuwa sasa Tino anamfwatilia Salma, ambae ndio kama anazidi kupagawa na penzi la Masoud, “mzee hizi veideo naomba nisikuonyeshe, maana azifai kwa matumizi ya watu tunao heshimiana” alisema Tino, ambae pia alimweleza Sebatian juu ya ilo.********

Naaam usiku wa siku hiyo, ulikuwa mzuri kwa wezi wamapenzi, yani Masoud na Salma, ambao walikuwa na uhakika kuwa Sebatian asingeenda nyumbani kwakina Salma, walikuwa wamejifungia chumbani kwa Masoud, na sasa walikuwa wamekosa ata shuka ya kuutandika, maana zote walisha chafua, mle ndani akukuwa na harufu nyingine zaidi ya arufu ya choo, “kwahiyo Salma lile gari jingine utalifanyia nini?” aliuliza Masoud, ambae wazazi wake walikuwa wanazania kuwa amelogwa, kumbe anachezea makalio ya mtoto wawatu, huku namba ya baba yake ameibloack.

Ilikuwa ni raha kubwa kwao, achana na Masoud ambae aliamini kuwa mpaka wakati huo Ana, kama kutumiwa nauri amesha tumiwa, na amesha fika Mafinga, na amesha zimulia maisha mazuri anayoishi yeye, akujywa kuwa mwenzie bado yupo dar, anaishi kwenye jumba kubwa, huku akihudumiwa kama binti mfalme.********

Naaam ilipita jumamosi ikaja juma pili, nayo ikapita, hali ya gonjwa ikiendelea kuwa nzuri, na mzee Kizinge akizidi kufuria kiasi cha kuanza kupokea fedha toka kwa wateja wake wakubebewa mazao, wakati akijuwa fika kuwa mpaka dakika ile trector lilikuwa linaitaji laki tano ya matengenezo, fedha ambayo alitegemea ingetoka kwa kijana wake Msoud, ambae mpaka mida hiyo ya saa tatu, alikuwa ndani ya chumba, alicho pangiwa na mwanamke, kwa fedha za mwanaume mwingine, mfukoni alibakiwa na noti moja tu ya elfu kumi, shilingi ya kitanzania, ambayo alikuwa anaogopa ata kuitumia kwa madai ya kilinda mfuko huku akila na kunywa kwa nguvu za Sebatian kupitia Salma, ambae alikuwa anapikia nyumbani, kisha amawita wanakula pamoja, au wakiwa busy sana na kunyanduana, basi shangazi anapika na kuwapelekea ili wapate nguvu ya kuendele kupeana dudu, pengine hii ndiyo faida aliyoipata Salma, kwa kuchumbiwa na mwanaume mwenye fedha, ambazo alizitumia kumshawishi Masoud kuwa nae.*****

Jumatatu ndiyo siku ambayo, Sebastian alirudi nyumbani kwa wazazi wake, na kumwacha Ana kule nyumbani kwake, akiendelea kuhudumiwa kama binti mfalme, huku Saphia akielezwa kuwa awe anamtembelea Ana kila baada ya siku mbili, kwaajili ya club na massage, jumatatu ndiyo siku ambayo, mzee Sinyangwe aliluhusiwa kutoka hospital, ambapo licha ya kupelekwa mpaka kijijini Malangari, pia aliachiwa fedha kiasi cha laki nne, kwaajili ya matumizi, huku wakipatiwa simu, kwaajili ya mawasiliano. …. endelea ….

Maoni 4 :

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu