Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Jumamosi, 17 Mei 2025

Hadithi: A CROWN OF BADNESS EP 1-5


Mpya
TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 1.

Katika nyumba moja ya kifahari walionekana watu watatu wakiwa wananyata kuingia ndani na walikuwa nyuso zao wamezifunika na maski, hao watu walikuwa makini kuliko kawaida kwa sababu kila hatua wanayopiga walikuwa wanaangalia nyuma kama hakuna mtu yeyote anaye waona, watu hao waliruka geti na kuingia ndani bila hata mlinzi kuwaona japo ilikuwa ni mchana ila mlinzi bado hakuwaona watu hao, baada ya kama dakika tano watu hao walitoka kupitia njia ileile waliyo ingilia na haijulikani lengo lao ilikuwa nini.

Katika gari la kifahari aina ya V8 tunamuona kijana ambaye alikuwa wa kishua anakula muziki taratibu huku akiwa anarudi kutoka chuo, huyu kijana alikuwa anaitwa Jacob na alikuwa anasoma chuo mwaka wa kwanza, kijana huyo alifika nyumbani kwao alipiga honi geti lilifunguliwa na akaingiza gari ndani na kushuka

"Helloo Nguna hakuna mtu yeyote aliyekuja kunitafuta hapa??" Baada ya kushuka alimuuliza mlinzi kama kuna mtu amekuja kumtafuta wakati yeye yupo chuo

"Boss hakuna aliyekuja" mlinzi alijibu huku akiwa anafunga geti

"Vipi mshua amerudi yumo ndani??" Kijana Jacob liuliza huku akiwa amenyosha kuingia ndani

"Aaaaaa!! Leo mzeee hajatokapo kabisa yaani!!" Mlinzi alijibu

Jacob baada ya kuambiwa hivyo alishangaa kusikia eti baba yake hajatokapo wakati asubuhi mzee alimwambia anaenda kwenye kikao maana yeye ndo alikuwa kiongozi wa kikao hicho,basi Jacob alijua kama kweli mzee wake hajatoka atakuwa anaumwa

Jacob aliongeza speed kuelekea ndani, Jacob ile anaingia tu mlangoni, Mungu wangu!! Alishika kichwa alikuwa haamini anachokiona
"Babaaaaaa!!" Jacob alipiga kelele kwa sauti kubwa baada ya kuona baba yake kalala Chini huku damu zikiwa zimetapakaa kwenye sakafu na Jacob alipoangalia pembeni aliona kisu kimejaa damu, Jacob alikiota kile kisu huku akiwa anamtikisa Baba yake na alikuwa haelewi afanye nini.
Ile jacob anapata akili ya kufanya na kujianda kunyanyuka pale chini alisikia sauti nyuma yake

"Upo chini ya ulinzi" ilikuwa ni sauti kutoka nyuma yake

Jacob alipo geuka kuangalia nani anaongea maneno hayo ya kipuuzi wakati yeye yupo kwenye mtihani mzito, hakuamini macho yake aliona kundi la maaskari wakiwa wamemnyoshea siraha na wengine walikuwa wanapiga picha kama ushahidi, Jacob hakuamini macho yake alibaki ameganda na kisu mkononi.

"Kijana upo chini ya ulinzi kwa mauaji" Askari mmoja aliongea huku akiwa anatoa pingu kwa ajili ya kumfunga jacob

"Kijana una akili kweli wewe yaani unamuua baba yako mzazi kweli??" Afande mwingine aliongea kwa hasira

"Jamani mi hata sijaua mi ndo nafika kutoka chuo, kama hamuamini muulizeni mlinzi" Jacob alijitetea lakini haikusaidia

Mlinzi aliitwa atoe maelezo kwa ufupi naye alitoa kama anavyo jua na kwa maelezo ya mlinzi ilionekana hakuna mtu mwingine aliyeingia mule ndani zaidi ya Jacob mwenyewe.

Jacob alijaribu kutoa maelezo hata kwa kutumia vitendo lakini hakueleweka maana yeye ndo kakutwa kwenye tukio tena kashika kisu kabisa kuonesha kwamba katoka kuua.

Jacob alifungwa pingu na kupakizwa kwenye defender mpaka rumande kwenda kutoa maelezo vizuri na mlinzi alichukuliwa kwa ushahidi zaidi.

Jacob baada ya kufungiwa rumande kama lisaa limoja Mama yake wa kambo aliye mulea jacob toka mdogo alifika Kupata maelezo maana naye wakati tukio linatokea alikuwa safarini na alipo rudi ndo alikuta hali kama aliyo ikuta
"Jacob mwanangu kwa nini umemuua Baba yako??" Mama yake ambaye ndo kamulea jacob toka utotoni na alikuwa mke wa baba yake na Mama huyo tangu aolewe na baba Jacob yeye hakubahatika kupata mtoto kwa hiyo alimuchukulia Jacob kama mtoto wake na Jacob alikuwa mtoto wa pekee kwa baba yake, alimuuliza swali jacob baada ya kufika pale rumande na kuruhusiwa kuongea na Jacob

"Mama mimi sijaua, nimekuta mzeee kauawa" jacob alikuwa anajitetea huku akiwa anatoa machozi kama bomba la maji

"Jacob kimya sitaki maelezo yoyote kila kitu nimeoneshwa ushahidi wote nimeona na mlinzi Nguna katoa maelezo yote kwamba hakuna aliyeingia mule ndani zaidi yako na inaonekana baada ya wewe kuingia tukio ndo lilifanyika" mama mlezi aliwaka alikuwa hataki maelezo yasiyo na kichwa wala miguu

Jacob hakujibu kitu kwa mama yake kwa sababu alikuwa hana njia yoyote ya kuthibitisha kwamba yeye hajaua, ila ukweli alikuwa anaujua mwenyewe.

"Jacob nimekulea vizuri kweli,ila kwa hili nakuapia utafia gerezani" mama mlezi aliongea kwa hasira na kuondoka.

Jacob alirudishwa ndani akiwa analia mno, naye alikuwa haelewi nani kafanya vile.

Zilipita Siku nne Jacob hata hakucheleweshwa alipandishwa mahakamani alisomewa shitaka lake la kuua kwa makusudi na lengo la kuua likiwa ni kujipatia mali za baba yake, Jacob alikana shitaka hilo na hapo kesi ili ahirishwa na kila upande uliambiwa uje na ushahidi wiki lijalo.

Jacob alirudishwa rumande huku akiwa anashangaa shitaka alilo somewa eti ameua kwa lengo la kujipatia mali.
"Hapa kuna kitu haiwezekani, mbona sikumbuki kama mzee alikuwa na bifu yeyote na mtu"hayo ni maswali ambayo Jacob alikuwa anajiwazia akiwa rumande.

Ilifika tarehe ya kesi Jacob alikuja kuchukuliwa na kupelekwa tena mahakamani, kesi ilianza kusikilizwa pande zote, kwa upande wa jamuhuri ilitoa ushahidi wake na kwenye huo ushahidi kulikuwa na sms kabisa iliyo tumwa kwa maaskari kutoka kwenye simu ya baba yake na Jacob na ilikuwa inasomeka kwamba "naomba mje mnisaidie mtoto wangu anataka kuniua kisa anataka mali" hiyo ni sms ambayo maaskari walidai kwamba waliipokea kutoka kwa marehemu na walipoenda kutoa msaada pale ndo walikuta mtuhumiwa anamalizia kuua na walionesha picha za Jacob akiwa kashika kisu huku katapakaa damu na pia mlinzi alithibitisha kwamba ni Jacob pekee ambaye alikuwa ameingia mule ndani kwa muda ule.

Kwa ushahidi huo Jacob hakuwa na cha kujitetea
(Mpenzi msomaji hata kama wewe ndo hakimu kwa ushahidi huo unamwachaje mtu)

Kwakuwa Jacob alishindwa kujitetea na kutoa ushahidi unao eleweka kwamba yeye hajafanya hivyo alisomewa kfungo cha miaka 30 jera na viboko juu.

Je nini kitatokea? Je Jacob ataenda kutumikia kifungo kama alivyo somewa au kuna muujiza utajitokeza??

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 2


TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 2.

Kwakuwa Jacob alishindwa kujitetea na kutoa ushahidi unao eleweka kwamba yeye hajafanya hivyo alisomewa kfungo cha miaka 30 jera na viboko juu.

Jacob alipelekwa gerezani kwenda kutumikia kifungo chake na alipelekwa kwenye lile gereza la watukutu haswa maana kitendo cha kuua kilikuwa siyo cha mchezo.
Jacob alianza kutumikia kifungo chake kwa mateso makubwa maana kutokana na upole wake wafungwa wenzake walimpokea kwa kumfanyia vitendo vya unyanyasaji, kiufupi Jacob alipelekwa gereza ambalo ni over size kwake, maana hilo gereza lilikuwa halina mnyonge.

Baada ya muda wa kama mwezi mmoja kupita baba yake mkubwa na Jacob alikuja kumuona Jacob na kuulizia kwamba ilikuwaje mpaka Jacob kafanya vile maana inaonesha wakati tukio linatokea yeye alikuwa kasafiri.

"Jacob ivi kwa nini uliamua kufanya kitendo cha kikatili vile huoni kama umejiharibia maisha??" Baba yake mkubwa na Jacob alianza kumhoji Jacob baada ya kuruhusiwa kuzungumza naye

"Daaaa!! Mzeee haina haja ya kuelezea maana hata nikikuelezea mpaka kesho huwezi kunielewa" Jacob alikuwa hana maneno mengi
"Jacob kwa nini unasema hivyo huoni mimi ndo mtu wa pekee ambaye naweza kukusaidia??"

"Mzeee hapa cha kunisaidia hamna kwa sababu kama ni kifungo nishapimiwa na kama ni muda wa rufaa ushaisha kwa hiyo hakuna ambacho unaweza kunisaidia kwa sasa" Jacob alikuwa ashakubaliana na yote.

"Jacob achana na yote ila mi mwenyewe siamini kama wewe ndo unaweza kufanya hivi, ebu niambie hakuna mtu yeyote unaye mhisi labda ili tuanze kumfanyia upelelezi??"
"Mzee kama ni upelelezi anza na mlinzi wa pale nyumbani yule nina wasi wasi naye kwa asilimia 💯" Jacob aliongea na baada ya hapo alikuja kuchukuliwa na kurudishwa ndani maana muda wa kuongea na mgeni ulikuwa umepita.
Basi baba yake mkubwa na Jacob aliondoka na alikuwa hajamaliza kumhoji Jacob ila ndo muda ulikuwa ushakata, na huyu baba yake alikuwa ni pacha na baba yake na Jacob, yaani maana yake baba yake na Jacob yeye kwao walizaliwa wawili tu nao walikuwa ni mapacha kwa hiyo huyu aliyekuja kumhoji Jacob alikuwa ni kurwa na baba yake na Jacob alikuwa ni doto.

Basi maisha yaliendelea kwa Jacob na taratibu taratibu alikuwa ashaanza kukubaliana na mazingira ya kule gerezani japo kwake ilikuwa ngumu kuyazoea mazingira yale maana yeye tangu azaliwe hajawahi pitia shida za ovyo ovyo wala kulala sehemu ya ovyo ovyo na hiki kitu ndo kilimfanya Jacob apate shida zaidi gerezani na alikuwa kakonda kwa mawazo maana ni mengi mno aliyo kuwa anayawaza.

Jacob siku moja akiwa katulia alikuwa anamwaza mchumba wake wa chuo ambaye walikubaliana kwamba watafunga ndoa baada ya kumaliza chuo na Jacob alishangaa huyo mchumba wake hakuja hata kumjulia hali kule gerezani, Jacob akiwa anawaza hayo alikuja kuitwa na kuambiwa kuna mgeni wake, Jacob alijua atakuwa ni mpenzi wake maana walikuwa wanapendana mno.

Jacob alipofika sehemu husika hakuamini maana alimuona Fatuma ambaye naye walikuwa wanasoma chuo kimoja na huyo Fatuma alikuwa anampenda sana Jacob ila jocob yeye mawazo yalikuwa kwa mwingine na Fatuma alijaribu kila njia kumshawishi na kumuonesha upendo lakini Jacob alikuwa anampiga chini.
"Heeee!! Fatuma ni wew??" Jacob aliuliza kwa kushangaa maana yeye alijua ni mpenzi wake Vicky kaja kumuona, anakutana na sura ya fatuma tena
"Jacob ni mimi Kwan kuna ubaya mimi kuja kukuona jamani??"
"Aaaaaa! Hakuna sikutegemea kama utakuja ndo maana nashangaa, nashukuru kwa upendo wako"
"Haina shida Jacob mi kitu kimoja ambacho nimekuja kukuulizia hivi ni kweli uliua? Nahitaji ndio au hapa na nataka jibu lako litoke moyoni"
"Fatuma mi sijawahi kuua maisha yangu yote"
"Basi poa mi nilitaka kujua hilo tu, na nakuahidi ntakusaidia kila uhitajipo msaada wangu"
"Fatuma asante kwa upendo wako?? Vip lakini kuhusu Vicky" Jacob uzalendo ulimshinda aliamua kumuulizia mpenzi wake maana ni miezi mitatu imepita yupo gerezani hajawahi kutembelewa na Vicky.
"Jacob some time naogopa kukwambia nahisi ntaonekana mnafiki na mchonganishi na nakumbuka nimewahi kukwambia kuhusu Vicky we ukanitukana"
"Aaaa! Fatuma hayo yashapita we nambie tu unachojua au kuna kitu unanificha??"
"Jacob sikiliza ukiwa hutumii akili hii dunia ni kubwa mno na ukitumia akili hii dunia ni ndogo mno mi sikwambii kwa mdomo, kwa sababu utaniona mnafiki ila nikipta ushahidi ndo ntakwambia na nahofia unaweza fia gerezani kwa mawazo ndo maana sitaki kukwambia" Fatuma aliongea maneno ambayo Jacob hakuelewa maana yake na Jacob alipo taka kuuliza nini maana ya yale maneno tayari muda walio pewa ulikuwa umekwisha.

Huku uraiani katika pub moja ambayo ilikuwa ni maarufu kwa watu maarufu alionekana binti mmoja mrembo ambaye alikuwa ana kila vigezo vya kuwa mrembo alikuwa kakaa na baba yake mkubwa na Jacob ambaye alijulikana kwa jina la Mr Derick na kwa jina la utani alijulikana kama 'Mzeee wa pisi kali' maana alikuwa anapenda sana mabinti wadogo wadogo na warembo.

Na kwa jinsi baba yake mkubwa na Jacob alivyo kuwa amekaa na yule mrembo alionekana ni mpenzi wake maana walikuwa wanakiss na kubadilishana mate, mara wanashikana yaani ili mladi raha tu.
Na katika hiyo hiyo pub alionekana Fatuma akiwa anawarekodi watu hao kwa siri maana alikuwa kakaa nje ya ile pub kwenye dirisha.

Je nini kitatokea?? Je kwa nini Fatuma anawarekodi hawa watu?

Itaendelea......




TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 3.

Na katika hiyo hiyo pub alionekana Fatuma akiwa anawarekodi watu hao kwa siri maana alikuwa kakaa nje ya ile pub kwenye dirisha.

Baada ya kumaliza kurekodi aliweka simu yake kwenye mkoba na kupotea maeneo hayo.
Zilipita kama siku mbili siku hiyo ilikuwa jumapili Fatuma akiwa anaenda kanisa katika pitapita yake alimuona baba yake mkubwa na Jacob Mr Derick akiwa na Mama yake mlezi na Jacob ambaye alikuwa kama Mama yake tu maana ndo alimulea toka utotoni, aliwaona watu hao wakiwa wameshikana viuno wanaingia super market na walikuwa wanatiana makiss njiani bila hata kuhofia.

"Daaa!! Dunia imekwisha yaani huyu mzee ni balaaa na atakuja kufa vibaya hataamini, na huyu mother Naye nilikuwa namchukulia ana akili kumbe naye ni hamnazo"
Fatuma alijisemea mwenyewe akiwa anaendelea na safari na hii ilitokana na kuwaona wale watu wakiwa kwenye hali ile.

Baada ya kama wiki moja Fatuma kuna vitu aligundua ambavyo yeye alikuwa hapendezwi navyo kabisa hasa kumhusu Mama yake na Jacob maana aligundua Mama yake na Jacob anaishi na Mr Derick kama mke na mume, yaani mr Derick aliamua kumiliki mtambo wa ndugu yake mazima.

Ulipita muda Jacob kule gerezani akiwa hajaja kutembelewa na mtu yeyote na alikuwa amemiss walau hata kusikia habari za kitaa kwamba zinaendaje, bahati nzuri kwake siku hiyo akiwa mtu mwenye mawazo mengi alikuja kuchukuliwa na kuambiwa kwamba kuna mgeni wake na alipotoka tu alikutana na sura ya Fatuma ikitabasamu japo Jacob alikuwa hamkubali Fatuma ila alifarijika sana kumuona

"Eheee Fatuma vipi kitaa kuna mapya??" Jacob alikuwa na hamu sana ya kujua nini kinaendelea huko mitaani
"Aaaa!! Kitaaa mambo mazuri tu ila kwa wenye maisha yao"
"Kwani vipi Fatuma mbona unaongea kwa mafumbo na siku ile uliniacha na fumbo kubwa mno"
"Jacob we ni mwanaume ambaye unatakiwa kupambana na siamini kama unasitahili hili taji ulilovikwa"
"Fatuma muda unaisha nyoosha maelezo nikwelewe" Jacob aliongea kama mtu mwenye kukasirika na mafumbo ya Fatuma.
Basi baada ya hapo Fatuma hakuongea neno alitoa simu na kumuonesha ile video aliyo rekodi kule pub.
Jacob alitumbua macho kama kapigwa na kitu kizito kichwani, maana aliona mpenzi wake Vicky akiwa kwenye mahaba mazito na baba yake mkubwa mr Derick, kabla hajauliza swali lolote Fatuma aliichukua simu yake na kuiweka kwenye mkoba alafu aliongea maneno ambayo yalimwacha Jacob mdomo wazi
"Mr Derick kamrithi Mama yako" baada ya hayo maneno alinyanyuka na kuondoka na Jacob alikuja kuchukuliwa na kupelekwa ndani.
Siku hiyo ilikuwa ngumu sana kwa Jacob maana kile kitu amekiona kwenye video ndo kilimchanganya kabisa na mbaya zaidi mchumba wake alichukuliwa na baba yake mkubwa bora angekuwa mtu mwingine.
Kitu kingine kilicho mchanganya ni kusikia eti baba yake mkubwa karithi Mama yake, yaani Jacob hapo ndo alichoka kabisa, machozi yalikuwa yanatiririka kama maji
(Maumivu yaliyoje yaan baba yako anamchukua mchumba wako, anamchukua na Mama yako alafu ana rithi na mali zako)

Yaani Jacob alitamani aridhi ipasuke azame maana alikuwa kachoka na mambo ya dunia, 

"Mwanaume halii lii ovyo bali anapambana we unafikiri Sisi hatuna machungu tuliyo pitia acha unduva huo, mwanaume gangamala" Jacob akiwa analia alisikia hayo maneno kutoka kwa njemba moja ambayo ilikuwa ipo pembeni yake, baada ya Jacob kusikia maneno hayo alijikaza na kukaa kiwanaume japo alikuwa anaumia mno.

Huku kitaani yaani mr Derick ilikuwa full kula bata maana mali zote za ndugu yake zilikuwa chini yake, yaani mpaka mke wa ndugu yake ilikuwa ni mali yake.
Vicky naye alikuwa kanunuliwa nyumba ya kifahari na bwana Derick yaan alikuwa anaishi kama yupo paris kila siku kwake ilikuwa sherehe mpaka ilifika kipindi akaanza kusahau chuo maana raha alizokuwa anazipata kwa Derick zilipitiliza.

"Ivi dear tangia mtoto afungwe kule gerezani umeendako kumuona??" Bwana Jacob alimuuliza Mama yake na Jacob wakiwa wamekaa mezani wanakula chakula maana walikuwa wamebakia kama mme na mke sasa

"Achana naye bana yeye si mpumbavu kama wapumbavu tu wengine kwani we ulitakaje" Mama mlezi wa Jacob aliongea kwa chuki, akionesha ni mtu ambaye hatamani hata kumuona Jacob.
Basi watu hao wawili waliendelea na mazungumzo yao na walikuwa na furaha kweli kweli, wakiwa wanaendelea na mazungumzo yao walisikia mlango unagongwa na hapo mama Jacob alienda kufungua ili aone ni nani anagonga, alipo fungua tu alikutana na njemba mbili zimenuna ni hatari.

"Ivi mr Derick unatuona sisi wajinga eeee??" Njemba moja iliongea baada ya kuingia mule ndani na ilikuwa imekasirika kweli.
"Aaaaaaa!! Mr Jomo Cool down haya ni mambo madogo tu kwani milioni 10 kitu gani??" Mr Derick Aliongea kwa kujichekesha
"Ni mwezi mmoja umepita unatuzungusha pesa zetu, sasa tunakupa siku mbili utachagua moja, either utumalizie pesa yetu au tuyumbishe antena" hizo njemba ziliongea zikiwa serious na baada ya hapo zilisepa.

Baada ya njema hizo kuondoka kizaa zaa kilihamia kwa bwana Nguna ambaye ndo alikuwa mlinzi wa getini na alilaumiwa kwamba kwa nini karuhusu zile njemba kuingia mule ndani bila ruhusa ya maboss wake.
Nguna alijitetea lakini hakueleweka na aliambiwa anakatwa mshahara kwa uzembe alio ufanya.

"Sasa tunafanyaje kuhusu hawa watu??" Mama Jacob alimuuliza mr Derick baada ya wao kuingia ndani

"Hapa kilichobaki hawa watu watatusumbua ni kuwapoteza kwenye uso wa raia either wafe au wakafie jera, maana tukiwachekea wanaweza yumbisha antena alafu channel zikakata" mr Derick aliongea akiwa serious na mama Jacob alimwelewa nini anamanisha.

Je nini kitatokea?? Je hizo njemba kwa nini zinawadai akina mr Derick??

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 4





TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 4.

"Hapa kilichobaki hawa watu watatusumbua ni kuwapoteza kwenye uso wa raia either wafe au wakafie jera, maana tukiwachekea wanaweza yumbisha antena alafu channel zikakata" mr Derick aliongea akiwa serious na mama Jacob alimwelewa nini anamanisha.

Basi maisha yaliendelea kama kawaida huku akina mr jomo na akina mr Derick wakiwa wanaliana timing na haikueleweka ni kwa nini watu hao wanawindana.
Ila baada ya kupita mwezi kama mmoja hivi, mr jomo alipata taarifa za rafiki yake kipenzi kuuawa na aliaambiwa mauaji yametokea usiku wa kuamkia leo 'pub ya watu maarufu' mr jomo hakuamini taarifa hizo kwa sababu yeye usiku walikuwa na rafiki yake pale pub na wote waliondoka kwa pamoja iweje tena aambiwe kwamba rafiki yake kafia pale pub, hiyo haikumwingia akilini.
Mr jomo akiwa anajiandaa ili aende kwenye eneo la tukio ambako anaambiwa rafiki yake kauawa ili akashuhudie kama ni kweli, Mara alishitukia anawaona maaskari mbele yake na walikuwa wamemnyoshea siraha.

"Kuna nini kwani??" Mr jomo aliuliza kwa mshangao maana alikuwa hajategemea hicho kitu

"Maelezo utapata kituoni ila cha kujua kwa Saiz ni kwamba upo chini ya ulinzi kwa kosa la kuua" askari mmoja aliongea huku akiwa anamsogelea mr jomo na pingu mikononi.

Siku zote mr jomo aliamini kila anapo tembea yeye ni mharifu maana kazi walizokuwa wanadili nazo na yule rafiki yake ambaye ndo anaambiwa kauawa zilikuwa ni kazi za uharifu siku zote, na kwao walimuona askari kama sumu.
Basi bwana jomo hakuulizia ni mauaji gani kafanya kwa sababu mpaka hapo alipo alikuwa kazi za mauaji amefanya za kutosha kwa hiyo aliona kweli ana kosa, na alicho kuwa anakipigia mahesabu akiwa chini ya ulinzi ilikuwa ni namna gani anachomoka maeneo hayo.
Basi yule askari polisi akiwa anasogea na pingu, Mr jomo alifyatuka mule ndani kwake na kuanza kukimbia, ila kabla hajafika mbali maaskari walimfyatulia risasi ya mguu na jamaa ilibidi awe mpole maana maumivu aliyo kuwa anayapata aliyajua yeye na malaika wake.

Basi mr jomo alifikishwa rumande, na kitu kilicho mshangaza bwana jomo ni baada ya kuambiwa yeye ndo kafanya mauaji ya rafiki yake, hicho kitu alikikataa kwa nguvu zote ila aliambulia kipigo tu toka kwa askari maana wao walikuwa na uhakika ni yeye na ukichukulia askari walikuwaga wanawalia timing ya muda mrefu na huyo rafiki yake aliyefariki.
Basi kama ilivyo sheria mr jomo alipelekwa mahakamani na kesi ilianza kusikilizwa, baada ya mr jomo kuyakana hayo mashitaka alirudiswa gerezani mpaka tarehe nyingine.
Basi siku nazo zilikimbia hatimaye tarehe ya kesi iliyopangwa kwa mara ya pili ilifika na kesi ilianza kusikilizwa.
Kwanza ushahidi ulimuonesha Bwana jomo akiwa na yule rafiki yake pale pub usiku ule kitu ambacho jomo alikubali ni kweli, na baada ya kutoka pale pub walionekana bwana jomo akiwa na marehemu kitu ambacho jomo alisema kweli, na baada ya hao watu kuondoka baada ya dakika tano marehemu alikutwa tayari ashauawa na mtuhumiwa mkubwa alikuwa bwana jomo kwa sababu ndo alionekana anatoka Naye maeneo hayo hapo mr jomo alikataa na kusema yeye walipo achana na rafiki yake alienda moja kwa moja nyumbani kwake na rafiki yake Naye alienda nyumbani kwake pia sasa iweje waseme tena yeye aliua na kibaya zaidi kwa jomo alijitokeza mpaka shahidi ambaye alithibitisha kwamba alimuona bwana jomo akiwa anamchoma visu rafiki yake huyo.
Jomo alijaribu kujitetea lakini kwa kuwa hakuwa na ushahidi wowote tayari kesi ilikuwa ishamuelemea.

Basi hakimu hakutaka kumung'unya maneno kwa kuwa kila kitu kilionesha jomo ana hatia basi alimpimia bwana jomo kifungo cha miaka 30 na viboko juu.
Bwana Jomo alikuwa ashakamatika na muda wa kwenda kunyea debe ulifika na kibaya zaidi naye alitakiwa kupelekwa kwenye lile gereza la watukutu ambako Jacob alikuwa Naye kafungwa huko.

Mr jomo akiwa anatolewa pale mahakamani kwenda magerezani kutumikia kifungo chake alimuona mr Derick na Mama Jacob wakiwa maeneo hayo ya mahakani na walipo muona jomo akipandishwa kwenye gari walitabasamu na kumpungia mkono, hapo tayari mr jomo alikuwa ashajua kila kitu kinachoendelea.

Basi kila mtu na taji lake, taji la bwana Jomo lilikuwa lishapatikana na alitakiwa kwenda kujifunza gerezani, Mr Jomo alipofikiswa tu gerezani alikutana na kizaa zaa.

Je nini kitatokea?? Kizaa zaa gani Me jomo alikutana macho??

Itaendelea......




TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 5.

Basi kila mtu na taji lake, taji la bwana Jomo lilikuwa lishapatikana na alitakiwa kwenda kujifunza gerezani, Mr Jomo alipofikiswa tu gerezani alikutana na kizaa zaa.

Kitendo cha Mr jomo kutua tu mule ndani alikutana na wahuni waliopinda walimpokea kwa kichapo na kibaya zaidi kwenye gereza hilo maaskari gereza walikuwa hawaingilia ugomvi wa wafungwa, maana wafungwa kwenye gereza hilo walikuwa hawaoni shida kuua mtu hata kama ni askari kajilengesha walikuwa wanapita naye.

Basi Mr jomo alichezea kichapo kutoka kwa wababe wa hilo gereza ila yeye alitulia na alikuwa anawaangalia sura za wale wanao mpiga na kuzi kalili vizuri, kwenye hilo hilo gereza kuna watu walikuwa wanamjua mr jomo na habari zake walikuwa wanazijua vizuri hao hawakudiriki hata kusogea maana walikuwa wanajua moto wa Mr Derick.

Basi dakika na masaa yalisogea hatimaye ikawa siku nyingine, Mr jomo akiwa ametulia alimuona mmoja wa wale wababe waliokuwa wanampiga jana anaenda toilet, hapo bwana jomo aliamua kumfuata kule kule toilet na kilichotokea kule toilet sisi hatukuwepo ila malaika wetu walikuwepo.
Baada ya dakika kama kumi kupita kuna mfungwa mwingine alikuwa anaenda kulekule toilet, kilichosikika huko ni kilio cha huyo mfungwa, basi wafungwa wengine na manyampara walikimbilia kule toilet kuangalia yale makelele yametokana na nini walipofika tu walikutana na mwili wa mfungwa ambaye ndo alikuwa anaogopeka katika gereza hilo mpaka maaskari walikuwa wanaogopa kumusogelea ovyo ovyo, ukiwa umetapakaa damu na meno yalikuwa yamezagaa chini na walipomwangali vizuri waligundua jama kafa.
Nakwambia siku hiyo wengine walitetemeka kwa kuogopa maana aliye uawa ndo alikuwa kamanda wao na alikuwa anawafanya wavimbe mule gerezani, wengine walio kuwa wanaonewa na huyo mbabe walifurahi na kushangilia.

Basi maaskari gereza walipewa taarifa na walikuja kuuchukua ule mwili, na haikujulikana nani kamuua ila tayari wafungwa walikuwa washaanza mumtilia shaka Mr jomo maana jamaa tangia aingie siku ya kwanza na kula kichapo alikuwa hajawahi zungumza na mtu.
Basi maisha yalisonga mr jomo akiwa gerezani na siku moja kuna mhuni humo ndani alijichanganya kwa mr jomo, jamaa alipigwa ngumi nzito mbili za uso jamaa meno yote yalidondoka chini na alizimia kama dakika kumi hivi, kitendo alichofanyiwa yule mfungwa kilibaki ni story ya siku kwa mule ndani na wafungwa wote mule gerezani walianza kumhusudu mr jomo na baada ya kupita kama mwezi mule gerezani mr jomo alipewa cheo cha nyampara mkuu wa gereza.

Mr jomo alianza kujenga urafiki na Jacob na ilionekana Mr jomo ndo alikuwa anajipendekeza kwa Jacob, kutokana na ukaribu ule Jacob alianza walau kuishi maisha ya kujiachia mule ndani maana aliacha kuonewa ovyo ovyo na chakula alikuwa anakula anashiba hiyo hali ilimfanya Jacob naye kuukubali sana urafiki na mr jomo.

Siku moja ilikuwa ni jumapili ambayo angalau wafungwa walikuwa wanakuwa free kidgo Jacob na mr Derick walikuwa wametulia zao wanapiga story

"Hivi we dgo Jacob we ulifikaje fikaje huku??" Mr jomo alimuuliza Jacob swali na alionekana kuna kitu anataka kujua juu ya Jacob

"Brother Jomo bana eti nilifikaje!! Nilifika kama ulivyo fika wewe, we huoni hili gereza kwamba ni la watu watukutu"

"Jacob nimekuuliza hivi kwa sababu wewe huendani na kuwa hapa yaani huna huo utukutu na inaoenekana wewe ni mtoto wa mama" 
"Bro Jomo acha hizo, niliua mtu ujue sasa unavyoniita mtoto wa wa mama sijui unataka nikueleweje bro??" Jacob hakutaka kuonekana mnyonge, alijipaisha ili naye aonekane sio wa kawaida.
"Ulimuuwa nani na kwa sababu ipi??" Jomo alikuwa bado anapeleleza
"Bro mpona kama tunapelelezana kwani we unataka kujua nini?? We sema niliwaua akina nani unafkri nilimuua mmoja, tunavyosema sisi ni watukutu tuelewe bro" Jacob bado alikuwa anajifagilia na alikuwa anaongea huku anacheka

"Jacob mtukutu hacheki cheki ovyo kama wewe na sura yako inaonesha kabisa wewe haujawahi uwa mtu" Jomo alikuwa anachoma kwenye kidonda maana alikuwa anaongea ukweli mtupu
"Heee basi bro we chukulia unavyo chukulia ila ndo ujue mimi so wakawaida sema tu some time naamua kuwa Cool kuepusha mashari yasiyo na tija" Jacob swala la kukubali kwamba yeye ni mtoto wa Mama ndo alikuwa halitaki kabisa.
"Jacob nimekuuliza maswali yote niliyokuuliza kwa sababu mtu uliye muua wewe namjua mtu aliye muua yeye" mr Jomo Aliongea kwa mafumbo

"Heeeee!! Usasemaje bro??" Jacob alitumbua macho kwa mshangao baada ya kusikia kauli ya mr jomo

"Nasemaje tena we si ndo muuaji bana mbona unashituka sasa??"

"Bro ujue kuna point umeongea hapo sijaelewa ebu ifafanue vizuri"Jacob alitaka kusikia kinaga ubaga maana alikuwa hajamuelewa nini Mr jomo anakimanisha.
"Jacob bwana we unataka kujua nini sasa wakati umesema wewe uliuwa watu kibao, ila mimi nakwambiaje aliye muua Mr Deus namjua, ila uliye muua wewe ndo simujui" bwana jomo aliongea kitu ambacho kilimfanya Jacob asimame kwa mshituko maana kitu alichokisikia kilikuwa ni zaidi ya kupata taarifa za mke/mme wako kufumaniwa.
Kitu kilicho mshitua Zaid Jacob ni kusikia jina la baba yake likitajwa na hakujua huyo Mr jomo kalijulia wapi jina la Mr Deus ambaye ndo baba yake.

"Bro wewe ni nani kwanza?? Na umelijuaje jina la baba yangu??" Akiwa kasimama Jacob aliuliza swali kwa kutetemeka mdomo maana alikuwa ashakumbushwa machungu ya nyuma.

"Jacob Cool down Kwanza, swala la kumjua baba yako siyo issue kubwa kwani baba yako alikuwa ni mtu mkubwa ila issue kubwa ni huyo mtu aliye muua baba yako" Mr jomo ndo alizidi kumchanganya Jacob kabisa.

Wakiwa wanaendelea na mazungumzo tayari kengele la kwenda kufanyiwa ukaguzi na kwenda kulala lilikuwa lishagongwa na Jacob hakupata muda wa kumuuliza swali lolote Mr jomo.

Je nini kitatokea?? Je Mr Jomo ni nani?? Na kwanini anamjua aliye husika na kifo cha baba yake na Jacob


Itaendelea......

Usikose sehemu ya 6

Maoni 1 :

  1. 𝐖𝐞𝐤𝐚 𝐌𝐚𝐨𝐧𝐢 𝐘𝐚𝐤𝐨 𝐘𝐚 𝐧𝐢𝐧𝐢 𝐊𝐢𝐟𝐚𝐧𝐲𝐢𝐤𝐞 𝐚𝐮 𝐤𝐢𝐨𝐧𝐠𝐞𝐳𝐰𝐞 𝐤𝐰𝐞𝐧𝐲𝐞 𝐛𝐥𝐨𝐠

    JibuFuta

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu