Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Jumanne, 13 Mei 2025

Hadithi: MAJARIBU EP 9-12


Mpya
Hadithi: MAJARIBU

Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)

Sehemu: 9

"Ndugu Yangu usijali hii dunia ndogo Muno! Ipo Siku tutamnasa ndo atajua kwamba Pesa ina maana Gani! Maana tutauza hata Figo yake Moja!" Basi askari mwingine akionekana ana hasira aliongea!!.

"Sema dogo hawezi kuzingua, tutulize mizuka maana Kwa Hali ilivyo kaa Sidhani kama dogo anaweza onekana kitaa haraka hivyo!" Basi askari mwingine aliongea kuwatoa shaka wenzake!.
Muda huo Jedi na Majaribu walionekana nyumbani Kwa doctor Lameck wakiwa mezani wanapata chakula Cha usiku!.

"Daaaa! Lameck Sijui usingekuwa wewe tungefanyaje ndugu Yangu, yaani nakushukuru Sana!"

"Jedi usijali ndugu Yangu! Ujue historia yako uliyo nisimulia pale Gerezani ilinigusa Muno Kwa sababu hata Mimi nimepitia kama uliyo pitia wewe, tena Mimi Mtu aliye nifanyia ubaya alikuwa Baba Yangu mzazi!"

"Uuuuu!! Pole ndugu Yangu walimwengu waache kama walivyo, zamani nikiwa mtoto nilikuwa naaminigi viongozi wa Dini hawanaga Dhambi lakini kumbe nilikuwa najidanganya!" Jedi aliongea!.

"Alafu ujue Jedi hukunifafanulia vizuri, unasema mchungaji Nemeke alimuua Dada yako yaani Ilikuwaje na chanzo haswa ni kipi!?"doctor Lameck aliuliza!.

"Ujue Mimi na Dada Yangu tuliachwa na wazazi wetu tukiwa wadogo! Wazazi wetu wote wawili Kwa pamoja walipata ajari na kufariki papo hapo!, Kiukweli lilikuwa ni pigo kubwa kwetu, Kwa kipindi kile hatukuteseka Sana Kwa sababu wazazi wetu waliacha Mali za kutosha! Kampuni na biashara kubwa kubwa! Na biashara zote bahati nzuri Baba alikuwa kaandika Majina yetu!.
Basi baada ya vifo vile tulianza kulelewa na Shangazi Yetu pale nyumbani ambaye ndo alikuwa ndugu yetu pekee aliye Salia, na Shangazi ilibidi ahamie na Mume wake pale nyumbani!.

Baada ya Miaka kama Mitatu kiukweli hatukuamini Shangazi na Mumewe waliiba baadhi ya hati zetu na waliuza karibia Nusu ya Mali zetu, baada ya hapo walikimbilia Sijui Nchi gani!.
Mimi na Dada Yangu tuliabaki tukiishi pekee yetu, uzuri Dada alikuwa kawa Mtu mzima anaye jitambua kidogo!.

Baada ya Miaka miwili biashara zetu zilikuwa zinaenda vizuri Japo Siyo Sana, Sijui Dada alidanganywa vipi na mchungaji Nemeke! Dada alijikuta anamwamini Sana mchungaji Huyo mpaka kumshirikisha kwenye biashara zetu na kuomba atusaidie baadhi ya Mambo, na Hiyo ilifanya mchungaji Nemeke kuzama kwenye mahusiano na Dada Yangu ambapo mwishowe ilipelekea wao kupata mtoto!.
Kipindi hicho Mimi nilikuwa kidato Cha kwanza na nilikuwa nakaa Shuleni, Kwa hiyo nilikuwa sielewi yale yanayo endelea!.
Mchungaji Nemeke Sijui alimlaghai vipi Dada Yangu! Yaani alimdanganya kwamba atampa taraka mkewe alafu atamuoa yeye! Na hiyo ilifanya Dada kumuamini Nemeke kupita kiasi mpaka ikapelekea kumpa hati zetu za Mali zote atunze Yeye!.

Mwishowe Dada alikuja kugundua hati zote Nemeke kabadili Jina na kuweka Jina lake badala ya kuweka Jina la mtoto kama walivyo kubaliana!, Hali Hiyo ilifanya Dada apate hasira na Lengo la Dada ilikuwa ni kutangazia kila Mtu Siri kwamba Yeye kazaa na mchungaji Nemeke, na mchungaji Huyo kamdhurumu Mali!.
Baada ya mchungaji Nemeke kuona Sasa ni kama anaenda kuumbuka aliamua kumuua Dada Yangu Kwa kushirikiana na baadhi ya watu, na Mtoto alimchukua na kumpeleka kusiko julikana!.

Kiukweli baada ya hapo niliishi Kwa kuteseka Muno, yaani niliishi kama Digi Digi, japo nilifanikiwa kumaliza kidato Cha Nne, Lakini Kwa taabu na misaada ya baadhi ya watu!.
Kwa hasira tu niliamua kuanza kupambana kutafuta nafasi ya Jeshi, bahati mbaya nilikosa na nilijijuta nimebahatika kupata uaskari Lengo Langu likiwa ni kulipa kisasi Kwa mchungaji Nemeke!.

Bahati mbaya Wakati sijalipa kisasi mchungaji Nemeke aliuawa kwenye mazingira ambayo Hata hayaeleweki, na hapo ndipo nilipo Anza kufanya uchunguzi!.
Hakika nimepata kujua mengi, kwanza niligundua Mtoto wa Dada Yangu Shule anayo Soma na nilianza kumfuatilia, ila mwishowe niligundua yule Siyo mtoto wa Dada Yangu bali kuna mchezo unafanyika wa kutaka kujipatia Mali za marehemu, Ambapo Mali nyingi za marehemu huyo zimetokana na Mali zetu!, Kwa kifupi ndo hivyo " Mr Jedi alimaliza kuelezea historia Yake ambayo ilifanya atilie mkazo Sana ile Kesi ambayo ilikuwa inamkabili Majaribu!.

"Bwana Jedi pole Sana! Kwa Hiyo mpaka saizi hujui mtoto wa Dada yako alipo!?"

"Hilo ntalifanya baada ya kuwa waharifu wapo mahali wanapo takiwa kuwepo!".

"Kwa hiyo inakuwaje! Yaani mchakato unaanzia wapi Mimi nipo tayari kuwasaidia kila hatua!" Lameck aliuliza,na kijana Lameck alionekana ni Mtu mpole na mwenye Moyo!.

"Hapa ndugu Yangu naomba nitafutie mwanasheria mzuri ambaye ana msimamo nimkabidhi ushahidi, maana kila kitu ninacho!" Mr Jedi alitoa maelezo!.
"Basi kuhusu hilo usijali na hiyo itakuwa njema, na Vipi kuhusu huyu dogo yeye ilikuwaje akaingizwa kwenye Kesi za mauaji!" Lameck aliuliza!.

"Uuuuu ni Stori ndefu! Ila Huyu dogo alisingiziwa! Na bahati nzuri aliwaona wauwaji na marehemu alimtaja kabisa kwamba Mkewe ndo Mtu mbaya!"

"Heeeee! Inaamana yeye ndo alishuhudia kifo Cha marehemu Nemeke, inaamana Nemeke hakumuelezea sababu za mkewe kumuua!" Lameck alizidi kuuliza!!

"Kwa Hali ambayo alikuwa nayo hakufanikiwa kuniambia yote hayo!" Kijana Majaribu ilibidi adakie na kujibu!.
"Uuuuu Mara nyingi Watu wakiwa wanakata Moto huwaga wanaropoka kila Kitu Kwa Jinsi Ninavyo jua katika taaluma Yangu, unataka uniambie hakuropoka kitu chochote Ambacho kinaweza kikafanya tukashinda hii kesi!?" Lameck aliuliza tena!.

"Kuna Siri aliniambia tu kuhusu maficho yake ya Siri yaani alipo ficha nyaraka zake na Siri zingine, ila tatizo niliye ambiwa nimpe taarifa niligundua ndo mhusika wa kifo Chake!" Majaribu alitoa Maelezo Kwa ufupi.

"Sasa hapo tunaweza shinda kirahisi hii Kesi! Yaani itakuwa rahisi maana ushahidi utakuwa wazi kwamba wewe hukuuwa mpaka anakupa Siri zake! Vipi umewahi fika hiyo sehemu aliyo kwambia na ni wapi!?" Lameck aliuliza!.
Kijana Majaribu kwanza machale yalimcheza, yaani alijikuta tu Moyo wake unakuwa mzito kuendelea kuropoka! Na Siku zote hakuna Mtu mwenye machale kama Mwizi!, Kwa Hiyo Majaribu alikuwa na machale ambayo Siyo ya Dunia hii!.

"Nadhani Majaribu huu ni Muda wa kufunguka kila kitu alicho kwambia marehemu Nemeke kabla ya kufariki, usimuogope Lameck ni Mtu mwema tu!" Mr Jedi alimsihi Majaribu atoe maelezo!.

"Jamani msijali Mimi ntawaambia tu ila Siyo saizi Nadhani inatakiwa tuanze na Mambo ya msingi kwanza!" Majaribu aligoma kutoa Siri Kwa Muda ule!.
Basi Lameck na Jedi walichukulia kawaida na walikuwa wanaamini Muda wowote Majaribu atawaambia!.
Siku Iliyo fuata Dr Lameck alitafuta mwanasheria, na alikuwa mwanasheria mzuri tena kijana Damu inachemka!.
Mwanasheria Yule alijinadi vyema kwamba yeye hajawahi feli kwenye Kesi na alinogesha maongezi vizuri Muno.

Basi baada ya makubaliano na Jedi kukubali kwamba atampa ushahidi, Lameck na yule mwanasheria waliondoka pale nyumbani huku Lameck akimsindikiza yule mwanasheria Kwa kutumia pikipiki yake.

"Bro Jedi hivi unamuamini Huyu brother! Mimi naona ni kama wale wale tu!" Majaribu aliongea point ambayo Jedi aliona ni ya kitoto!.
"Majaribu kama huna Hoja tulia, Mtu katusaidia kutoroka Gerezani, katupa hifadhi, katusaidia Kwa mengi na pia wazo la kutoroka Gerezani alinipa yeye alafu saizi eti humuamini, angekuwa Mtu mbaya si angetupa Sumu tufe Muda ambao tulikuwa tunazuga tumekufa pale hospital!" Basi Jedi aliongea Kwa kupaniki mpaka Majaribu aliogopa!.

"Kama kumuamini ni Wewe! Mimi simuamini na siwezi kumpa Siri za marehemu, isitoshe Mtu mbaya hapimwi Kwa wema alio fanya, na wala Sura! Anaweza akafanya wema kumbe ni chambo tu ya kuwanasa!" Majaribu aliongea Kwa hasira na kutoka nje!.
Mr Jedi alikuwa ni mtaalamu wa upelelezi na pia alikuwa na kipaji Cha kupeleleza, na Sifa ya mpelelezi mzuri ni kwamba usiamini kila kitu Kwa Macho na maneno!.

Siyo Kwamba Jedi alikuwa kamuamini Lameck Moja Kwa Moja ila alikuwa anafanya uchunguzi wake kimya kimya tena Kwa Siri Muno, ili kujua Bwana Huyo anawasaidia kutoka moyoni au ana jambo lake!.
Basi ilifika usiku Lameck alirudi, walipika vyema na kula, na Siku hiyo Jedi alikuwa amepanga kwamba ikifika usiku lazima aelekee kwenye geto lake la zamani kwenye kuchukua zile Siri zake ambazo alifichaga, na bwana Jedi alikuwa haelewi kama atakuta Mtu au laaa!.
Basi yakiwa ni Majira ya Saa Sita usiku Jedi alimshitua Majaribu ili waongozane! Maana alikuwa anajua Majaribu ni mtaalamu wa kupita Madirishani!.

Ila Wakati wanatoka walishangaa kuona milango ipo wazi, walitoka mpaka nje geti nalo lilikuwa lipo wazi na walisikia nje ya geti kama Gari inaunguruma Hivi!.
Jedi alichungulia taratibu pale getini, ili aone nje kuna nini!.

Je Jedi aliona Nini!??

Tukutane sehemu ya 10





Hadithi: MAJARIBU

Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)

Sehemu: 10

Ila Wakati wanatoka walishangaa kuona milango ipo wazi, walitoka mpaka nje geti nalo lilikuwa lipo wazi na walisikia nje ya geti kama Gari inaunguruma Hivi!.
Jedi alichungulia taratibu pale getini, ili aone nje kuna nini!.

Jedi alibaki katumbua Macho baada ya kumuona Lameck akiwa kasimama na Melisa yule Katibu wa kanisa, pamoja na bwana Luka yule Katibu wa Jimbo ambaye ni mchepuko wa Melisa, tena walikuwa wamesimama mbele ya Gari huku wakiwa wanajadiliana majambo, na taa ambayo ilikuwa ipo pale getini Kwa upande wa nje ilimsaidia Jedi kuona vyema kinacho endelea pale nje!.

"Machale mabaya yamenicheza ebu twende ndani dogo huko tutaenda Kesho!" Jedi ilibidi amzuge Majaribu na kweli walirudi ndani kimya kimya.
Majaribu hakuelewa kitu chochote, Lakini Jedi alikuwa ashajua doctor Lameck Siyo, alianza kuhisi Kwamba huwenda hata yule Bwana aliyefia hospital aliye daiwa kwamba kauawa na Jedi basi ni Lameck alimtia Sumu!.
Masaa yalisogea hatimaye palikucha na kuwa asubuhi, Kama kawaida Lameck alikuwa anawachangamkia Jedi na Majaribu! Pia nao hawakusita kuonesha ushirikiano walimchangamkia!.

"Jedi vipi ushahidi mwanasheria ameniuliza Muda Gani utamkabidhi akafungue Kesi!?"Lameck aliuliza, basi Jedi alimjibu kwamba ataenda kuuchukua na atamkabidhi!.
Kutokana na kwamba ilikuwa imesadikika kwamba wawili wale wamepoteza maisha, ilikuwa ni ngumu Kwa Jedi na Majaribu kutembea mchana!.

Usiku ulipo fika Jedi na Majaribu walienda mpaka pale Jedi alipo kuwa anakaa! Bahati mbaya sehemu Hiyo kuna Dada alikuwa kapanga na alikuwa anakaa hapo!.
Kama kawaida Majaribu alipitia dirishani, Japo kuwa dirisha lilikuwa na nondo Lakini Majaribu alipita kibishi, baada ya kuingia ndani alifungua mlango ili Jedi aingie!.

Wawili wale walisukuma mlango wa chumbani, walikuta mdada wa watu akiwa na Mtoto wake mdogo wamelala huku wamejiachia, yaani Dada huyo alikuwa kazalia nyumbani, baada ya kujipatia kimtaji ndo akaamua kwenda kupanga geto!.

"Weeee...." Dada Yule alikurupuka usiku ku na kutaka kupiga makelele ya kuitia Wizi! Lakini Jedi alimziba mdomo!.

"Dada Sisi Siyo watu wabaya! Mimi ndo nilikuwa nakaa humu kabla yako, kuna Vitu vyangu humu niliacha nimevifuata!" Jedi aliongea kistaarabu, basi yule Dada alitikisa kichwa Kwa uoga!!
Jedi alisogea ukutani, kuna Namna alibinua pale ukutani tobo lilionekana, baada ya hapo alichukua vitu vyake na waliondoka na Majaribu!.
Yule Dada alibaki kaacha mdomo wazi huku akiwa haamini kama ukutani pale palikuwa na tobo mpaka la kuweka Vitu!.

Basi Siku Hiyo ilipita! Ikiwa ni majira ya Saa Nne asubuhi Jedi alivaa vizuri alipiga na kepu yake mpaka puani, baada ya hapo alielekea kitaa.
Jedi katika ile sehemu yake aliyo kuwa kaficha ushahidi pia alikuwa anaficha Pesa zake za akiba,Kwa hiyo alichukua na zile pesa!.
Basi Siku Hiyo alielekea mpaka Library alinunua flash disk nyingine mpya kama mbili! Yake mafaili Yote aliyakopi kwenye flashi Mpya, maana alikuwa anajua akiwapa ushahidi lazima tu wataupoteza!.

Ilipo Fika Jioni mwanasheria yule alikuja pale nyumbani Kwa Lameck, alikabidhiwa ushahidi, alijaribu kuchomeka kwenye laptop yake! Hakika alibaki kaacha mdomo wazi! Yaani zilikuwa ni video za kutosha na Sauti za kutosha za wahusika, zikiwa zinaonesha mipango yao, mpaka mazungumzo yao Jinsi walivyo husika na kifo Cha Nemeke!.

"Ndugu Yangu hapa umeuwa! Kwani hizi video na audio wewe ulipataje, maana ni adimu Mtu kuwa na ushahidi wa maana kama huu, yaani Mtu hapa hawezi kukwepa!" Manasheria alimuuliza Jedi, basi Jedi alijibu kijanja tu kwamba kuna Mtu alimpatia ambaye ni miongoni mwa wale wale wahusika, maana yake anawasaliti wenzake!.

"Heeeee!! Vipi ndugu Yangu kwani kuna kopi zingine za ushahidi unazo au ndo hizi hizi!?" Mwanasheria yule aliuliza tena!.

"Sina kopi yoyote ndugu Yangu, na inatakiwa uwe Makini maana ukipoteza huo ushahidi ndo utakuwa umefelisha kila kitu!" Jedi alijibu, Muda huo Majaribu alikuwa anamkata Jedi Macho mabaya Muno huku Moyoni akiwa anajisemea kwamba Jamaa huyo mjinga kuwaamini watu hao na kuwakabidhi kila kitu kirahisi!.
"Yaani naona kabisa hawa Siyo watu wema Lakini brother Jedi anavyo waamini Sasa, Sijui huo anao sema upelelezi alisomea wapi!" Hayo yalikuwa mawazo Ambao Majaribu alikuwa akijiwazia!.

Mwanasheria yule aliondoka akiwa anakenua Meno njia nzima! Kwanza baada ya Kutoka pale alienda mpaka kwenye Hoteli Moja ya kifahari!.
Halikupita hata Nusu Saa Luka na Melisa walionekana kufika pale!

"Eheee! Jofu nambie umefanikiwa kupata huo ushahidi!?" Melisa akiwa na kimuhe muhe baada ya kufika pale Hotelin na kumkuta mwanasheria yule amekaa aliuliza Kwa pupa!.

"Boss nimefanikiwa na bahati iliyoje yaani wameniamini Moja kwa Moja, pia Lameck naye wamemuamini vibaya Muno! " Mwanasheria Yule akiwa anakenua Meno alikabidhi flash disk mbili Kwa Melisa!.
"Safi Sana jofu! Sàsa imebakia Kazi ya Lameck kumpeleleza Yule dogo mpaka tujue Nemeke alificha wapi nyaraka zote na vitabu vya benki!" Melisa akiwa na mizuka aliongea.
Basi waliagana na kuondoka Huku wakiwa wanajiona washindi!.

Huku upande wa kina Jedi! Majaribu muda wote alikuwa anazitupa lawama kwa Jedi Kwa kuwaamini wawili wale.
Ila Jedi alikuwa anatumia akili yaani alikuwa anatumia ule usemi wa mnafiki ishi naye Kwa akili na ukila na kipofu usimshike Mkono!.

"Majaribu Mimi naelewa kuliko wewe! Kitu ulicho nizidi wewe ni Mbinu za Wizi tu, ila Mambo mengi yote nimekuzidi!" Jedi Siku hiyo aliamua kumjibu Kwa akili!.

"Hata kama bro ndo uwaamini watu kirahisi hivyo!"

"Majaribu nikuulize Swali!?"

"Swali gani hilo!?"

"Okay Sisi tunaishi kama tumekufa, haya Lameck akasema atufukuze hapa kwake tutaenda wapi!?"

"Maswali Gani hayo bro anatufukuzaje Sasa!?"

"Umeona eee! Sasa unavyo sema tusimuamini unamanisha nini! Si unamaanisha tumkatae na hapa kwake tuondoke! Muda mwingine tumia akili" Jedi aliongea Kwa mafumbo, ila bado Majaribu yeye alikuwa haelewi na alimwambia kabisa Jedi kwamba Siri yake hawezi kuizungumza!.
Basi Siku zilizidi kusogea huku ile rufaa ya Kesi inayo mhusu Majaribu ikiwa bado haijakatwa! , Yaani yule mwanasheria alianza kuzungusha!.

"Lameck Jamaa yako mbona haeleweki, ujue huu mwezi unapita naona bado tu hajakata rufaa ya kesi na Pesa kidogo nilimpatia pamoja na ushahidi? "Basi Siku Hiyo Jedi aliamua kumuuliza Lameck!.
"Sema usijali, Jamaa juzi juzi alikuwa nje za Nchi Kwa hiyo kuna mambo anayaweka sawa! Ila Jamaa kapendekeza kwamba Ingekuwa vizuri Majaribu angeelezea kila kitu alicho ambiwa na Nemeke kabla hajafa ili kazi iwe nyepesi" Lameck aliongea!.

"Okay kuhusu hilo ntazungumza na Majaribu! Ila msisitizie Mtu wako afanye hima basi!" Jedi aliongea, basi Lameck alijibu kwamba Sawa!.
Ikiwa ni usiku Lameck aliamua kuanza kumpekenyua Majaribu tena kuhusu Siri alizo ambiwa na Nemeke kabla hajaaga dunia!.

"Ngoja niongee ukweli! Marehemu aliniambia nyuma ya nyumba yake kuna box la Kijivu alishalifukia hilo ndo lina kila kitu chake" kijana Majaribu akiwa serious aliongea, na inaonekana huo ni uongo ambao alikuwa kaelekezwa na Jedi kwamba auseme!.

"Kweli!!! Una uhakika alisema hivyo!!?" Lameck Macho yakiwa yanamtoka aliuliza mara mbili mbili!, Baada ya kuthibitishiwa na Majaribu kwamba ni kweli Muda ule ule aliamua kutoka huku Simu ikiwa mkononi, yaani taarifa zile zilikuwa za moto kwake mpaka zilikuwa zinamuunguza alitamani azifikishe sehemu nyingine Muda ule ule!.
Basi Siku hiyo ilipita ikiwa ni Siku nyingine, nyumbani Kwa marehemu mchungaji Nemeke, Mama mchungaji akiwa kakaa mchana kwenye bustani na shoga yake mmoja ambaye walikuwa wanaivana Haswa, alishangaa vijana kama wanne wakiwa wanaongozwa na Bwana Luka wanafika pale kwake tena wakiwa na mashine ya kuchimbi!..

"Katibu kulikoni mbona mnakuja na dhana za kuchimbia Kwangu kuna Nini!?" Mama mchungaji aliuliza Kwa mshangao maana alikuwa hajui lolote linalo endelea, kumbe harakati zote ambazo zilikuwa zinaendelea Mama mchungaji alikuwa hahusishwi!.
Jedi alikuwa anajua kwamba Melisa na Luka kuna Namna wanamuzunguka Mama mchungaji ndo maana aliamua kumpa plani Majaribu kwamba ataje pale pape nyumbani ili kuumanisha Mambo, maana alijua kitawaka!.

Mr Luka baada ya kuulizwa vile na Mama mchungaji, ilibidi amuite pembeni kumuelezea kile kinacho endelea!.

"Unasemaje Mr Luka! Kwa Hiyo nyie na huyo Melisa sijui na kina nani, munaona wajanja Sana eee, Mimi najua tupo pamoja kumbe nyie mnaendelea na mpango wa kutafuta nyaraka Chini Kwa Chini! Sasa nasemaje nyumbani Kwangu hachimbi Mtu! Labda niwe marehemu!" Mama mchungaji Siku Hiyo alikuwa anaongea mpaka mate yanamtoka, yaani alikuwa anaona naye ile ndo fursa yake ya kujipatia kila kitu, maana ilikuwa inasadikika kwamba kwenye hizo Siri ndo huko bwana Huyo alikuwa anaficha mpaka vitabu vya Benki!.
Yaani Kwa Namna ambavyo Mama mchungaji alikuwa anawaka na kuongea kwa kufoka, mpaka yule shoga yake ambaye alikuwa yupo pale nyumbani alibaki anashangaa kwamba Shida nini!.

Je Ipi hatima!? Mama mchungaji atakubali na je baada ya kuchimba nini kitatokea!??

Tukutane sehemu ya 11




Hadithi: MAJARIBU

Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)

Sehemu: 11

Yaani Kwa Namna ambavyo Mama mchungaji alikuwa anawaka na kuongea kwa kufoka, mpaka yule shoga yake ambaye alikuwa yupo pale nyumbani alibaki anashangaa kwamba Shida nini!.
Mr Luka alijaribu kumshawishi Mama mchungaji Kwa utaratibu lakini Mama huyo wala alikuwa haelewi, yaani aliwaka isivyo kawaida! Na Lengo lake alitaka achimbe mwenyewe!.

Basi Mr Luka na watu wake waliondoka huku wakiwa wanapiga mahesabu Namna ya kufanikiwa Jambo lao!.

"Shiitiiii yaani hapa pilau limeingia mchanga! Yule mpuuzi kajua kwamba Nyaraka zimefukiwa nyuma ya nyumba yaani hapa Sijui itakuwaje!" Baada ya Luka kufika nyumbani alijiongelesha Kwa hasira huku Melisa naye akiwa anakuna kichwa kivyake!.
Ilipo Fika usiku Mama mchungaji wala hakutaka kulaza Damu! Alitafuta vijana na baada ya hapo walianza kuchimba nyuma ya nyumba maeneo ambayo waliamini watapata kitu!.

Walianza kuchimba Saa Tatu Usiku mpaka inafika Saa Saba hakuna kitu walikuwa wamekipata, na walikuwa wanatumia mashine! Yaani walichimba kila sehemu Lakini ilikuwa hola, baada ya kuona hamna Kitu ilibidi waaanze kufukia mashimo yote!.
Mama mchungaji alikuwa na hasira isiyo ya kawaida, yaani alikuwa katumia gharama kuchimba Lakini hakupata kitu, kwanza wale vijana aliwalipa, Pili zile mashine alikuwa kakodi na kuweka mafuta ya Kutosha!.

Kufukia walimaliza alfajiri baada ya hapo wale vijana waliondoka, Mama mchungaji aliamua kulala huku akiwa na hasira!.
Siku hiyo ilipita palikucha na Kuwa asubuhi, Mida ya Saa nne asubuhi Mr Luka akiwa na Melisa na vijana wa kuchimba walifika pale nyumbani Kwa Mama mchungaji tena, Siku hiyo walikuja na Mbinu nyingine Mpya ambayo waliamini lazima Mama mchungaji atakubali wachimbue kule nyuma!.

Pale Nje walimkuta Binti Revina akiwa anaotea Jua la asubuhi huku anachati mtandaoni, maana Binti huyo tangia azijue Siri za Mama mchungaji alikuwa anaishi kiboss kabisa!.

"Revina vipi Mama mchungaji yuko wapi, ebu muite basi" Mr Luka aliongea!.

"Duuuuuu!! Mama mchungaji kalala alfajiri! Usiku kucha walikuwa wanachimba huko nyuma hata sielewi walikuwa wanachimba nini, Kwa hiyo kumuamusha saizi atanifokea Labda mpaka aamke mwenyewe!" Revina alijibu.
Kwanza Mr Luka Macho yalimtoka baada ya kusikia kwamba eti Mama mchungaji alikuwa anachimba usiku kule nyuma!.

Mr Luka na Melisa Macho yakiwa juu juu, walizunguka mpaka nyuma ya mjengo ule na kweli walikuta kila sehemu imechimbwa na kufukiwa vyema!.

"Shiitiiii Huyu Mwanamke hanijui eee!! Yaani Sisi tumefanya Kazi kubwa ya kupeleleza na kujua hizo nyaraka ziko wapi, yeye kirahisi tu anakuja kuzichukua! Hakika patachimbika!." Mr Luka aliongea Kwa hasira, baada ya hapo alizunguka na kuingia ndani Kwa hasira!.

"Mr Luka ndo Nini hivyo unaingia ndani Kwa vurugu, yaani kama kwako! Wewe una mamlaka kanisani Siyo kwenye majumba ya Watu!" Revina alimkimbilia Mr Luka na kuongea kwa hasira!.
Muda huo hayo Yote yanaendelea kumbe Mama mchungaji alikuwa kaamka Muda na alikuwa kaweka earphones 🎧 Masikioni mwake kuna video alikuwa katumiwa kutoka kwenye namba ngeni!
Baada ya Mama mchungaji kufungua video ile nusura azimie alibaki anatetemeka Kwa hasira, ilikuwa ni video ambayo ilikuwa inaonesha nyumbani Kwa Melisa na mazungumzo Yote!.

Mama mchungaji alijaribu kupiga ile Namba iliyo mtumia ilikuwa haipatikani!.

"Shiitiiii kumbe Luka na Yule mwanamke lao Moja wananizunguka eee! Hata yule mtoto Siyo mtoto wa Nemeke, huu ujinga Gani! Na Bado wanaona haitoshi wanataka wapate nyaraka zote!" Mama mchungaji akiwa kajilaza kitandani huku anarudia rudia kuangalia ile video alikuwa anajiongelesha Kwa hasira isiyo ya kawaida, kwanza alichomoa earphones masikioni huku akitamani kumeza Mtu!.
Akiwa na mawazo na hasira za kujaza Dunia nzima, Mara alisikia makelele sebuleni, ilikuwa ni mabishano Kati ya Revina na Mr Luka, maana Mr Luka alikuwa kaingia ndani bila utaratibu tena Kwa kupiga teke mlango!.

Mama mchungaji ilibidi atoke kwenda kujionea kinacho endelea!.

"Bora umetoka mwenyewe! Hizo nyaraka ulizo chimba huko nyuma zilete hapa, haiwezekani tutumie nguvu na gharama alafu wewe uje uchimbe kirahisi tu!" Mr Luka mishipa ikiwa inamtoka aliongea Kwa jaziba!.

"Hahaaaaaa!! Ebu nicheke mie! Hivi Mr Luka ujasiri wa kunifokea unaupata wapi!? Unazidai hizo nyaraka kama nani!? Kwa mamlaka ipi!? Au huo ukatibu wa Jimbo ndo umeamua kuuhamishia nyumbani Kwangu!?" Mama mchungaji aliongea Kwa nyodo na kujiamini huku naye akiwa na hasira za ndani Kwa ndani!.
Yaani kauli ya Mama huyo ilifanya Mr Luka na Melisa waamini kwamba Mama mchungaji alifukua na kupata Nyaraka!.

"Kama hutaki tuharibu mambo lete Hizo nyaraka lazima share ifanyike, mtoto wa Nemeke kwanza ndo mwenye Haki kuliko hata wewe, unafikiri tukimpelekea Hizi taarifa itakuwaje!?" Mr Luka alizungumza Kwa msisitizo!.

"Hahaaaaaa eti mtoto wa Nemeke! Kwa Hiyo mnanifanya Mimi mjinga Siyo!?" Mama mchungaji alizungumza huku akiwa anapekua kwenye Simu yake, aliingia Whatsapp na kufungua ile video Kisha aliwapatia wajionee!.
Mr Luka na Melisa baada ya kuona ile video kwanza walibaki wanatazamana Kwa aibu huku wakiwa hawaelewi hata wazungumze nini!, Walipo angalia pale juu namba ya Mtu aliye tuma ilikuwa haijaseviwa, ila Mr Luka Hata Melisa mwenyewe waliitambua vyema ile Namba!.

"Shiitiiii!! Jofu ! Jofu huyu mtoto kumbe mpuuzi! Hivi!" Mr Luka akiwa na hasira alijiongelesha Kwa hasira, huyo Jofu alikuwa ni yule mwanasheria ambaye Jedi alimpatia ushahidi wote!!.

"Haya ongeeni mniambie kwamba huyo mtoto ni wa Nemeke! Na najua mmenidanganya kwamba Nyaraka zimefukiwa nyuma ya nyumba huwenda hata mshazipata! Kwa taarifa yenu huko nyuma zijakuta kitu!" Mama mchungaji aliongea Lakini hakuna aliye Amini kwamba hajakuta kitu, wote walijua amezipata nyaraka ila sababu ni Kwa Vile kagundua kwamba yule Habir Siyo mtoto wa Nemeke.

Mr Luka na Melisa pamoja na Vijana walio kuja nao waliondoka Kwa aibu maana tayari Siri zao Mama mchungaji alikuwa kazijua! Yaani Mr Luka alikuwa na hasira isivyo kawaida huku akiwa na uhakika kwamba mwanasheria Yule ndo kamtumia video Mama mchungaji!.

"Huu ujinga! Madogo wengine wehu kabisa, yaani alitupatia zile flash disk kumbe amebaki na kopi! Mjinga Sana yule ona Sasa!" Mr Luka wakiwa njiani alikuwa analalamika Njia nzima!.

"Mr Luka Kwa Nini tusimtumie Yule Revina kuiba nyaraka pale nyumbani kwa Mama mchungaji, ujue Yule Binti ana Tamaa ya Pesa!?" 

"Hilo nalo wazo! Ila Kwa saizi ngoja tumalizane na Jofu kwanza haiwezekani tunafanya mipango tunampa Pesa ya kutosha yeye anatusaliti!" Mr Luka aliongea Kwa hasira!.
Muda huo Jedi na Majaribu Bado walikuwa wanaendelea kukaa Kwa Lameck, japo kuwa walikuwa wanakaa Mguu pande!.

"Heeeee bro Jedi! Ile video bado haijamfikia mlengwa Nini, mbona mwanasheria hajaja!"wakiwa wametulia pale nyumbani kwenye varanda Majaribu alimuuliza Lameck!.

"Majaribu we subiri tu si anatukwepa!!? Jana Lameck si alitwambia rafiki yake yupo Dubai kikiwaka huko lazima atakuja tu hapa!" Jedi alijibu, na hilo ni ushahidi tosha kwamba Jedi na Majaribu ndo walituma ile video iliyo mfikia Mama mchungaji, njia Gani waliitumia Mimi na Wewe hatujui.

Upande wa Pili kijana anaye itwa Jofu akiwa kwenye ofisi yake ya wanasheria ambayo alikuwa ameifungua Mara alishangaa pale ofisini kwake Mr Luka na Melisa wanafika tena wakiwa wamefula hasira isivyo kawaida!.

"Jofu Kwa Hiyo umeamua Sasa kutusaliti na kushirikiana na Mama mchungaji! Yaani mjinga wewe ndo wakutuharibia kiasi hiki!?" Mr Luka baada ya kufika ofisini alimkunja Jofu huku akiwa anaongea Kwa Hasira!.
Kwanza kijana Jofu alibaki katumbua Macho huku akiwa haelewi, maana yeye alikuwa hajafanya kitu!.

"Boss Mimi mbona sijafanya chochote, alafu hata huyo Mama mchungaji sina mazoea naye!" Jofu alijitetea!.
"We mpuuzi unafikiri kuna kitu utadanganya Kwa taarifa yako tumeona Kwa Macho yetu hatujaambiwa na Mtu ebu lete Simu yako hapa, toa password!" Mr Luka aliongea.
Kwakuwa Jofu alikuwa anajiamini na alikuwa anajua hajafanya kitu alitoa Simu na kumpatia Luka!.

"Hiki nini! Huyu uliye mtumia hii video nani alafu eti humjui, na umemsevu Boss Namba 1, yaani Alex Wewe wa kufanya hivi!?" Mr Luka baada ya kuingia kwenye upande wa Whatsapp ya Jofu alikuta ni kweli Bwana huyo alituma video, Majira ya Saa Tisa za usiku! Hata kwenyewe Simu yake alipo angalia mafaili ushahidi wote ulikuwa upo kwenye Simu!.

"Jamani mbona Mimi sijatuma! Yaani....." Jofu akiwa anajitetea alikula Bonge la Kofi zito kutoka Kwa Luka!.

"Mpuuzi wewe, yaani unaniuza, Wewe si ulisema hakuna kopi yoyote uliyo nayo Kumbe umesevu kila kitu kwenye Simu, kijana mbaya wewe! Sasa subiri ntakuonesha nguvu Yangu ilipo si unajifanya ndumila kuwili!" Mr Luka alichimba mkwara, baada ya hapo alichukua na Simu ya Jofu, Yeye na Melisa waliondoka!.
Jofu Moja ilikuwa haikai Mbili haiki, yaani alikuwa kachanganyikiwa isivyo kawaida, alihisi kabisa ule mchezo lazima Jamaa yake Lameck anahusika maana alijaribu kufikiria kama watakuwa ni kina Jedi aliona hapana, maana ni tangia apewe ushahidi alikuwa anawazungusha na alikuwa hajawahi kutana nao!.

Masaa yalisogea! Majira ya Jioni kijana Jofu aliona we usinichezee, aliamua kumfuata Lameck huko huko kwake, maana kama ni kumpigia Simu alikuwa hawezi tena maana simu yake alikuwa kapokonywa!.
Muda huo Lameck alikuwa kakaa nyumbani kwake na kina Jedi wanacheza karata pale sebuleni! Mara gafla walishituka Mtu anasukuma mlango na kuingia kama mvamizi!.

Je Kipi kiliendelea!? Majaribu na Jedi walifanyaje fanyaje mpaka video ikaenda na Namba ya Jofu.

Tukutane sehemu ya 12




Hadithi: MAJARIBU

Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)

Sehemu: 12

Muda huo Lameck alikuwa kakaa nyumbani kwake na kina Jedi wanacheza karata pale sebuleni! Mara gafla walishituka Mtu anasukuma mlango na kuingia kama mvamizi!.

"Oya Jofu mwanangu pigo Gani hizo Sasa unaingia ndani kama mvamizi, je ningekuwa nipo na Shemeji Yako nafanya Yangu je!" Lameck aliuliza Kwa kupaniki maana Jofu aliingia Kwa vurugu Kwanza aliwashitua!.

"Oya mwanangu Lameck usenge ulio ufanya najua, Kwa Hiyo unataka wewe ndo uonekane unapiga kazi Sana Siyo!?" Akiwa na jaziba Jofu aliuliza!.

"Mbona hueleweki Mzee! Umevuta Bangi au kitu gani!? Mambo gani nimefanya!" Lameck akiwa anashangaa aliuliza!.

"Au Siyo unajifanya hamnazo eeee! Au na Wewe unataka Siri Zako niwachane Hawa madogo!" Jofu aliuliza!.

"Jamani kuna nini!? Jofu ebu Njoo kwanza nje tuzungumze" Lameck ilibidi kwanza amvutie Jofu nje ili akina Majaribu wasiendelee kusikia!.
Basi Jedi na Majaribu walitazamana Kisha walichekeleana, maana walikuwa wanajua kimeumana!.

Huku nje ilikuwa ni balaa! Jofu alikuwa haamini kama Lameck hajafanya kama alivyo jitetea!.

"Sasa Lameck mwanangu kama Siyo Wewe ni nani, kama ni Hawa madogo Mimi sijawahi kutana nao, hata ninapo kaa hawapajui, Simu Yangu hawajawahi gusa Hiyo inaingia Vipi akilini!" Jofu Bado alikuwa haamini!!.

"Mwanangu Haki ya Mungu Mimi siwezi kufanya huo upuuzi!! Mimi na wewe tumetoka mbali tangia enzi hizo skuli, isitoshe Mimi ndo niliye kuunganisha Kwa Mr Luka ningewezaje kufanya hivyo Sasa!?"Lameck alijitetea Kwa hisia mpaka Jofu alishusha Hasira japo kuwa Bado alikuwa haamini kama Lameck hajafanya huo mchezo!!.
Lameck alianza kuwahisi kina Jedi Japo ilikuwa Siyo Sana! Basi Jofu aliondoka na Lameck alirudi ndani!.

"Oya Lameck Jamaa kaondoka! Mimi nikajua amekuja kwenye maswala ya Kesi unajua sikuelewi huyo jamaa yako, juzi tu mlisena yupo Dubai! Kama kashindwa Kazi basi arudishe ushahidi tutafute mwanasheria mwingine, maana ushahidi wenyewe ndo ule ule nao niliupata Kwa shida kweli!" Jedi akiwa serious aliongea Kwa Kufoka!.

"Mwanangu usijisahaulishe hapa upo nyumbani Kwangu, Kwa Hiyo punguza Sauti usinikoromee! Naweza nikwatimua na mkakosa pa kwenda! Isitoshe naweza kwenda kuwachoma Kwa wale askari magereza maana wanakusaka Sana wanataka Pesa zao ulizo waahidi!" Lameck alifoka na aliongea Kwa jaziba! Kifupi rangi yake ilianza kuonekana!.
Jedi ilibidi awe mpole wala hakuongeza neno! Pia Majaribu naye alitulia kama Hana mdomo!.

Masaa yalisogea ikiwa ni majira ya usiku wa Saa Sita Jedi akiwa na Majaribu, Bwana Jedi alitoa Simu ambayo alikuwa anaitumia kisiri na kuficha Lameck asije akaiona!.
Baada ya hapo Jedi aliingia kwenye Simu ile alichagua baadhi ya video na audio alafu alizituma Kwenye namba ambayo alikuwa kasevu Mrs Nemeke, na alisindikiza na ujumbe mrefu!.

Upande wa Pili Mama mchungaji akiwa kalala huku ana mawazo tele haswa baada ya kugundua kwamba Mr Luka na Melisa wanamzunguka Mara alisikia ujumbe unaingia, na alipo angalia ilikuwa ni upande wa Whatsapp, Basi Mama huyo alifungua ili aone kitu Gani katumiwa!.
Hakika Jasho lilianza kumtoka Mama Yule kule chumbani usiku ule, mapigo ya Moyo yalikuwa yanaenda Kasi isivyo kawaida, yaani mwili mzima ulikuwa unatetemeka!.

Ilikuwa ni video ambayo ilikuwa imerekodiwa pale kwake, Yeye na kundi Zima wakiwa wanajadiliana tena wakiwa wanahusisha na Jinsi walivyo shirikiana kumuua mchungaji Nemeke!, Pia Audio ambazo alikuwa katumiwa zilikuwa ni Sauti zake tena zikiwa zinadhihirisha laivu kwamba Mama huyo alihusika kwenye Kifo Cha mumewe!.
Alafu Chini yake baada ya zile video kulikuwa na ujumbe!.

"Kama hutaki hizo video ziende Mitandaoni naomba tukutane saizi Eneo la uwanja wa shule ya Azimio, na uje pekee yako Mimi ni Mtu mwema kwako, na kingine ambacho hukijui Mr Luka ana mpango wa kukuuwa Wewe!" Huo ni ujumbe ambao ulikuwa upo pale Chini!.
Kwa Jinsi mama mchungaji ambavyo alikuwa kachanganyikiwa, wala hakuhofia kama unaweza kuwa mtego, yaani aliamuka na kuvaa gauni lake bila hata kumuaga Mtu aliwasha Gari na kuelekea huko aliko ambiwa wakutane na Mtu huyo ambaye hata hamjui!.

Mama mchungaji aliendesha Gari Kwa vurugu usiku ule huku akiwa kapaniki! Na kichwani mwake alikuwa anajuta kumuua Mumewe! Na swala la Mama huyo kumuua mumewe ilikuwa ni ushawishi na uchochezi wa Mr Luka!.

Muda huo huo Jedi akiwa na Majaribu walionekana wapo uwanjani kwenye kona huku wakiwa wamejibana kuona kama Mama mchungaji atafika, maana wao ndo walikuwa wamemtumia zile video!.
Wakiwa wapo pale waliona kuna Gari inafika pale uwanjani Kwa vurugu na ilienda kusimama Katikati ya uwanja wa shule! Baada ya hapo Mama mchungaji alishuka huku mwili mzima ukiwa unatetemeka, alikuwa anaangaza huku na kule!.

Basi Jedi akiwa kavaa Kofia mpaka kwenye pua huku akiwa kajifunika uso baada ya kuthibitisha kwamba Mama Yule amekuja pekee yake naye alisogea pale Huku Majaribu akiwa anafuata nyuma!.
Mama mchungaji kwanza alipo muona Majaribu ilibakia kidogo akimbie maana aliamini ni mzimu, Jedi hakutambulika kwa sababu alikuwa kaziba uso!.

"Heeeee we mtoto si walisema umekufa na nilishuhudia kabisa mwili wako wewe nani kwanza!?"Mama mchungaji akiwa anatetemeka aliuliza!.

"Hicho sicho tulicho kuitia hapa Mama! Kitu tulicho kuitia ni Wewe kwenda mbele ya vyombo vya habari kusafisha Jina la Majaribu! Hicho ndo kitu kikubwa!" Jedi aliongea maneno ambayo yalifanya Mama mchungaji Macho yamtoke na aone kama Dunia inazunguka!.

"Heeeee kivipi mbona sikuelewi!?" Mama mchungaji akiwa na kigugumizi aliuliza!.

"Mama najua unajua kwamba Huyu mtoto hakumuua Nemeke, pia unajua nyie na wenzako ndo mlio husika na Kifo, Kwa taarifa Yako wenzako Wana mipango mibaya na Wewe wanataka wahakikishe kila kitu wanakichukua wao, Sasa Sisi tupo Tayari kusaidiana na Wewe na kuwaangusha akina Mr Luka, kikubwa inabidi uende mbele ya vyombo vya habari uelezee kwamba Majaribu hakuhusika na chochote Bali ni kina Mr Luka ndo walihusika! Wewe funguka kila kitu!" Jedi aliongea Kwa msisitizo!.

"Heeeee mbona Hiyo ngumu Kwangu! Kwanza Wewe Kwa Nini unataka nifanye hivyo!?" Mama mchungaji aliuliza!.
Kwanza ilibidi Jedi amsimulie Mama mchungaji kila kitu ambacho Nemeke alimfanyia Dada yake na pia alivyo wapora Mali, yaani alielezea kila kitu Mpaka kuhusu yule mtoto Habir!.

"Heeeee!! Kweli dunia kubwa jamani! Nimeishi na Nemeke zaidi ya Miaka ishirini na kitu sijawahi jua kama ana tabia za hovyo hivyo! Ila pamoja na Yote Mimi siwezi kufanya hicho unacho taka Kwa sababu Mr Luka akikamatwa hata Mimi ntakamatwa, maana huo ushahidi unanionesha na Mimi" Mama mchungaji alijibu!.

"Mama mchungaji hili Siyo ombi ni lazima, kama unataka Basi Wewe mwaga ugali Sisi tumwage mboga na Kesho ikifika Jioni hujatekeleza nilicho kwambia kila kitu kinaenda mtandaoni na Jina la Majaribu litajisafisha lenyewe maana watu wataona ukweli!" Jedi ilibidi Sasa aongee serious kama mwanaume!.
"Baba usifanye hivyo, Siyo Kwamba Mimi simuonei huruma huyo mtoto ila Sasa ushahidi huo mlio nitumia unatufunga wote! Ntawezaje kuwakataa!!?" Mama mchungaji alikuwa anaongea Huku anatetemeka, Kama ni Maji yalikuwa yamefika shingoni!.

Je Ipi hatima ya Mama mchungaji atakubali au liwalo na liwe!??

Tukutane sehemu ya 13



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu