KIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA KWANZA
Kabla hujaanza kuinjoy utamu huu, tafadhali kumbuka simulizi hii imeandikwa Kwa lengo la kuburudisha haina uharisia wowote. Lengo ni Kuburudisha TU.
Naam! safari hii kisa chetu kilichotokea mwaka 2009, kinaanzia maeneo ya Mbezi mwisho, barabara kuu iendayo morogoro na mikoa mingine ya Tanzania, ilikuwa ni mida ya saa kumi za jioni, siku ya ijumaa ya mwisho ya mwezi wa saba.
Ndani ya basi moja dogo, Toyota Coster linalofanya safari zake ubungo kwenda kibaha maili moja, walionekana abiria wengi wakiwa wamejaa ndani ya basi ilo dogo la abiria wa mjini, yani dala dala, waliokuwa wanatokea mjini katika pilika mbali mbali za kijamii, ni kawaida kwa mida hiyo magari kujaa kiasi hiki, asa kwa kipindi kile, ambacho usafiri aujawa lahisi kama ilivyo sasa.
Ndani ya gari ilo, seat ya karibu na mlango, anaonekana mschana mmoja, wa umri wa miaka ishilini na tatu, ambae kiukweli kwa haraka uwezi kusema ni mzuri kiasi gani, kutokana na jinsi alivyokuwa kwa wakati ule, alie kuwa ametulia kimya anatazama mbele kama mwanafunzi anae msikiliza mwalimu wa hisabati, huku mala kwa mala mala akipeleka mkono wake wa kulia usoni kwake usawa wa macho na kufuta machozi, yaliyokuwa yana karibia kutililika mashavuni mwake, japo kuna wakati mwingine aliyachelewa na kujikuta yakitangulia mashavuni.
Wapo waliomwona na kumshangaa, lakini kiukweli hakuna alie mwuliza kuhusu kinacho mtoa machozi, hayo ndiyo maisha harisi ya dar, kwa namna nyingine kila mtu anaishi maisha yake, akikuuliza kinacho kusibu, anataka umbea tu, pengine wewe ungependa kumwuliza kinacho mliza ili upate chakula cha sikio, na kwenda kusimulia mbele ya safari, kama mimi ninavyofanya.
Ukweli ni kwamba, mwanamke huyu alikuwa analia na mambo mawili makubwa, mambo ambayo yamefanya leo kwa mala nyingine tukutane hapa STORY LINE, kupeana mkasa huu ambao sidhani kama lengo ni kutoana machozi, au kuchafuliana nguo, ila naamini kuwa lengo ni kila mmoja ajifunze kutokana na jinsia yake, yani kama mwanaume jifunze kama mwanaume, na mwanamke ajifunze kama mwanamke, ikiwa pamoja na kuburudika pia.
Mschana huyu anaitwa Arianna, kama nilivyo kudokeza mwanzo, umri wake ni miaka ishilini na tatu, ni mtoto wa kwanza wa mzee mwenye kipato cha chini kabisa, kilichotegemea kazi ndogo ndogo za vibarua, vya ukulima wa mashamba, alie fahamika kwa jina la Mzee Sinyangwe, akiwatangulia wadogo zake watatu, wawili wakiume mmoja wakike, ambao walikuwa na umri wa kati ya miaka kumi na mbili kwa yule wakiume, alie fwatia miaka saba, na wa mwisho miaka mi nne, waliokuwa wanaishi na baba na mama yao huko Makete Iringa, kijiji cha Malangali, Arianna alibahatika kupata Elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Malangali, kabla aja pata nafasi ya kuaza kidato cha kwanza katika sekodari ya jumuiya ya wazazi ya Igafilo, hapo hapo mkoani Iringa.
Ariana alisoma kwa juhudi huku akipambana na vishawisho cya wanaume wa pale kijijini na shuleni, vilivyo sababishwa na uzuri wake, wa hasiri, wa umbo na sura, kiasi kwamba mpaka anafika kidato cha pili, mschana huyu, akuwai kutembea na mwanaume yoyote, japo tayari alikuwa katika urafiki na kijana mmoja Mtoto wa jilani yao, alie fahamika kwa jina la Masoud Kizinge, alie kuwa anasoma Mafinga sekondari, kidato sawa yeye na yeye.
Ulianza urafiki wakawaida mpaka kijana huyo, mtoto wa mzee Kizinge, ambae kidogo alikuwa na uwezo wa kawaida wa fedha, alizo jipatia kutokana na kukodisha mashamba ya maindi, mzee alie fahamika zaidi na kujizolea umaarufu kutokana na tabia yake ya majisifu, asa anapokuwa amelewa, maana upita njiani usiku wakati wakurudi nyumbani kwake, akitokea kunywa ulanzi, “nani mwingine zaidi ya Kizinge, panya wote wame lala” japo iliwakela majirani na wanakijiji kwa ujumla, lakini baadae wakaichukulia kawaida.
Mwishoni mwa kidato cha pili, wakiwa likizo ya mwezi wa kumili na mbili, ndipo wawili awa walipozindua penzi lao, na kuwa wapenzi kamili, kwamaana hiyo Arianna alitoa kitumbua kwa Masoud, ukweli penzi lao lilikuwa tamu, na lilimchanganya sana Arianna, ambae siyo tu kwamba alifurahi kuwa na mvulana pekee alie fauru kwenda kusoma nje ya Malangali, pia alifurahi kuwa na mwanaume mwenye mwonekano mzuri na mwenye kujipenda, ambae alikuwa anatamaniwa na waschana wengi wa pale kijijini ata vijiji vya jilani…. bila shaka unahamu ya kufahamu kinacho mliza binti Arianna, kama ni hivyo, basi endelea kufwatilia mkasa huu, wa #UKIMALIZA_FUNIKA, inayokujia hapa hapa Story line
UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA SEHEMU YA KWANZA: Mwishoni mwa kidato cha pili, wakiwa likizo ya mwezi wa kumili na mbili, ndipo wawili awa walipozindua penzi lao, na kuwa wapenzi kamili, kwamaana hiyo Arianna alitoa kitumbua kwa Masoud, ukweli penzi lao lilikuwa tamu, na lilimchanganya sana Arianna, ambae siyo tu kwamba alifurahi kuwa na mvulana pekee alie fauru kwenda kusoma nje ya Malangali, pia alifurahi kuwa na mwanaume mwenye mwonekano mzuri na mwenye kujipenda, ambae alikuwa anatamaniwa na waschana wengi wa pale kijijini ata vijiji vya jilani….ENDELEA….
Penzi lao lilishika kasi na kukolea moto, kiasi cha kwamba, kila mmoja alitambua penzi lao, tayari wazazi wao walisha fahamu juu ya penzi ilo, na kulibariki kisiri siri, kwamaana muda wowote Arianna alikaribishwa nyumbani kwa mzee Kizinge, na kupokelewa na mama yake masoud, ambae kiukweli alikuwa anampenda sana, mschana huyu, asa kutokana na tabia yake ya kujituma katika kazi, maana mala tu baada ya kufika pale nyumbani kwa kina Masoud ambako alienda ata kama massoud alikuwa shuleni huko mafinga, angefanya kazi zote ambazo angezikuta, ikiwa kufua kuosha vyombo, kufanya usafi wa ndani, na kazi nyinge zote ambazo wewe unazifahamu zinafanyika majumbani kila siku, kisha angerudi nyumbani kwao, ambako pia angeendelea na kazi pia.
Arianna aliyafanya hayo kutokana na ahadi aliyowekeana na Masoud, kwamba hapo baadae watakuja kuowana wafunge ndoa, na kuishi pamoja, ilifikia wakati Arianna alikuwa anajituma kwa kazi ndogo ndogo za vibarua kama wazazi wake, ili kupata fedha za kumtumia mpenzi wake, pale anapokosa fedha kutoka kwa wazazi wake, ambao licha ya majivuno ya mzee Kizinge, lakini kipato chao kilikuwa cha kawaida sana.
Kunawakati Arianna alijikita kwenye kazi ndogo ndogo za vibarua, huku akisahau majuku yake ya shuleni, na kuanza kushuka kimasomo, ata uzuri wake kuanza kuchujuka, na kupoteza nuru ya uzuri wake, kitu ambacho kilisababisha ata baada ya kumaliza mitihani yao ya mwosho na Masoud kurudi nyumbani, Masoud akaanza kitabia cha kuwa busy na marafiki zake, wengine kuliko kuwa na mpenzi wake Arianna, kama walivyo zoweshana siku za nyuma.
Hiyo aikumshtua Arianna, alijisema kuwa kwakuwa ajamtamkia kuwa wameachana, basi yeye ni wake tu, kilichokuja kumshtua zaidi ni tabia ya mpya ya Masoud ya kuto kula kitumbua chake mala kwa mala, kama ilivyokuwa zamani, ambapo kila siku wanapokutana iwe kichakani, iwe chumbani kwa Masoud au kwa Arianna, wangepeana kitumbua, lakini safari hii ndani ya week tatu, alikula mala moja tu.
Achana na hiyo ambayo pia, Arianna aliichukulia kuwa, wao ni wapenzi, na awana haja ya kufanya kila siku, kubwa kuliko pale Arianna alipoanza kusikia tetesi za kwamba Masoud alikuwa anatoka na baadhi ya waschana pale kijijini, lakini Arianna alipuuzia tetesi hizo, kwamaana alisema kuwa, kama Masoud angeamua kupenda mwanamke mwingine, basi angekuwa amesha mwacha, japo kuna wakati Arianna alikosa uvumulivu, na kuomba dudu kwa mpenzi wake Masoud, huku Masoud mwanazo akimpiga kalenda, na ata Masoud alipoona usumbufu wa Arianna umezidi, akaamua kummweleza jambo, “hivi Arianna unashindwaje kuvumilia kukaa bila kufanya mapenzi, kwani mimi nilipokuwa shule ulikuwa unafanya nanani, au ulikuwa una nisaliti?” swali ilo gumu, lilimfanya Arianna awe mpole, ili kumwaminisha mpenzi wake kuwa akuwa anamsaliti.
Naam matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, yalitoka, na Arianna alianguka vibaya sana, katika masomo, na kukosa sifa ya kuendelea na kidato cha tano, kama ilivyokuwa wa wanafunzi wengi wa pale kijijini, huku kijana Masoud akipata nafasi ya kwenda kusoma, shule ya sekondari ya elimu ya juu ya Tosamanganga, huko Iringa.
Maisha yakwa vile vile, Arianna akijitaidi kuangaikia vibarua, vidogo vidogo, hili kumsaidia mpenzi wake fedha za matumizi, akiamini kuwa anatengeneza maisha yao ya baadae, ambayo yangewasaidia yeye Arianna na ndugu zake pamoja na wazazi wake, ndio maana wazazi wa mschana huyu walikuwa radhi binti yao amsaidie mwenzao, huku wazazi wa Masoud, yani mzee Kizinge na mke waki wakifahamu na kuutambua msaada anao upata kijana wao toka kwa mke wake mtarajiwa.
Akiwa anahisikuwa anachokifanya ni sahihi, Ariana kuna wakati alimshirikisha mdogo wake Aidan, katika vibarua vyake, huku akimpa moyo kuwa, hipo siku atayaona mafanikio yaliyotokana kwa kazi anazo fanya.
Unajuwa kunakitu ambacho kinaitaji moyo sana kukifanya, kama ilivyomsinda bwana Sinyangwe, ambae siku moja akiwa amekaa nje ya nyumba yake, anaota jua la asubuhi, huku anasubiri uji na kande, ghafla yaka mjia mawazo ya tafakari, juu ya maisha ya mapenzi ya binti yake, na kijana wa jilani yao bwana Kizinge, maana licha ya binti yao kujituma katika vibarua, ambavyo alikuwa achagui kazi gani afanye, hipi asifanye, na kujipatia feza, ambazo alizituma kwa chumba wake, pasipo kujibakishia fedha yoyote, ambapo japo ange nunua ata kijinguo kizuri cha dukani, kitakacho, mpendesha kama waschana wengine, maana zaidi ya hapo yeye alikuwa ananunua nguo chache za mtumba, ambazo uzivaa mpaka zinapokaribia kusha, ndipo uenda kununua nyingine, huku wadogo zake wakati mwingine utembea makalio wazi kwa jinsi nguo zao zilivyo tukutuka, na wakati huo licha ya kazi zote hizo, lakini bado mschana wetu huyu, aliendelea kumtumikia mama mkwe mtarajiwa, kwa kwenda kufanya kazi za pale nyumbani, ikifikia wakati akikosa muda wakwenda kwa wakwe zake, basi angetumwa mtu, na mama mkwe angemsema sana Arianna, “yani hapo bado ujaolewa, umeshaanza uvivu, sasa ukiolewa itakuwaje, unazani Masou kwa usomi alionao awezo kupata mwanamke mwingine” hakika ilikuwa changamoto kwa Arianna, tena ni bahati mama yake akufahamu juu ya ilo.
Wakati kazi zikiendelea kumfubaisha Arianna, ilikuwa kinyume chake kwa Masoud ambae kila aliporudi likizo, alionekana kuzidi kunawili na kupendeza, haku habari za chini chini, kuhusu Masoud kutembea na waschana wengi wa sekondari pale kijijini, zikizidi kusambaa pale kijijini, ata zilipo mfikia Arianna, alizipuuzia na kuendelea na maisha yake na mpenzi wake, japo dudu alikuwa anaipata kwa mbinde, yani mpaka Masoud ajisikie kufanya hivyo, ambapo ungekuta likizo ya mwenzi mzima, wangefanya mala mbili, au mala moja tu….
UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA SEHEMU YA PILI: Wakati kazi zikiendelea kumfubaisha Arianna, ilikuwa kinyume chake kwa Masoud ambae kila aliporudi likizo, alionekana kuzidi kunawili na kupendeza, haku habari za chini chini, kuhusu Masoud kutembea na waschana wengi wa sekondari pale kijijini, zikizidi kusambaa pale kijijini, ata zilipo mfikia Arianna, alizipuuzia na kuendelea na maisha yake na mpenzi wake, japo dudu alikuwa anaipata kwa mbinde, yani mpaka Masoud ajisikie kufanya hivyo, ambapo ungekuta likizo ya mwenzi mzima, wangefanya mala mbili, au mala moja tu…. endelea…….
Huku mzee Sinyangwe na familia yake, siku zote wakitegemea ule msemo wa baada ya dhiki ni faraja, wakiendelea kula kwa tabu na kufanya kazi kwa juhudi kumsaidia mkwe wao mtarajiwa, wakati huo familia ya mzee Kizinge ikiendelea kulewa kila siku, na kutoa matambo yake nyakati za usiku, “nani kama Kizinge, kila siku nakunywa pombe, na jembe linasoma form six” hakika kauri hiyo, ilimtesa sana mzee Sinyangwe, aliichukulia kuwa, wakati mzee mwenzie anakunywa pombe na kulewa kila siku, huku yeye na familia yake inaangaika kusomeshea mtoto.
Uweli bwana Sinyangwea akuweza kukaa kimya, akamweleza mke wake yani mama Arianna, ambae pia alisema kuwa alikuwa na mashaka kama hayo, hivyo wote kwa pamoja, wakamwita binti yao, na kuliongelea swala lile, “lakini baba mimi naandaa maisha yetu na Masoud, siyo maisha ya baba yake” ilo lilikuwa jibu la Arianna, jibu ambalo liliwalizisha wazazi wake, ambao awakuacha kumuunga mkono binti yao, juu ya kile alichokuwa anakifanya, wakitegemea kufaidika hapo mbeleni.
Naam mambo yalizidi kupamba moto, na ujio mpya wa penzi moto moto, la Masoud kwa Arianna, kipindi ambacho Masoud alikuwa amemaliza kidato cha sita, na kueleza kuwa amepata nafasi ya kwenda chuo kikuu cha dar es salaam, ambapo wazazi wa kijana huyo walisema awakuwa na uwezo wa kumsomesha kijana wao, nayeye kuamua kukaa chini na mpenzi wake Arianna na kujadiri juu ya jambo ilo, bahati nzuri jambo ilo, lilikuja kipindi ambacho penzi lao lilikuwa limeshamili upya, na kuwa kama ilivyokuwa mwanzo, “yani Anna, tumekula ng’ombe mzima, tunashindwa kumaliza mkia, maana nikifanikiwa kumaliza chuo, napata kazi nzuri, huko dar, nyumba nzuri na gari pia” alisema Masoud kwa sauti ya kinyonge, “mh! nikaishi dar bora ata Iringa mjini, nitawaacha na nani wakina baba?” aliuliza Arianna kwa sauti ya kudeka, “unazani tutaweza kuishiwenyewe kwenye jumba kubwa kama ilo, lazima tutawachukuwa wazazi wako, pamoja na wadogo zako, tukaishi nao dar, lakini ndiyo hivyo sasa, baba amekosa fedha ya kunipeleka chuo” alisema Masoud kwa sauti yenye kukosa amani kabisa, “sasa jamani Masoud tutafanyaje?” aliuliza Arianna ambae kiukweli sasa alikuwa ameshaanza kumwonea huruma mpenzi wake huyo.
Hapo kikapita kimya kifupi kama vile wote walikuwa wanatafakari jambo, kabla Masoud ajainua kichwa ghafla huku uso wake ulikuwa umejawa na tabasamu, “nimepata wazo Anna” alisema Masoud, huku akipeleka mkono wake mgongoni kwa Arianna, na kufanya kama anampapasa hivi, na kumfanya Anna atabasamu, kwa raha, maana sasa penzi lao lilikuwa limerudi kama mwanzo, tena lilionekana kuwa moto moto, “wazo gani ilo Masoud?” aliuliza Anna huku anamtazama Masoud kwa jicho legevu la kusinzia, “mimi naona tutulie kila mmoja atafue njia ya kupata ela ata kwa kuanzia, au kuweka bond kitu, alafu mimi nikipata mkopo wangu wakwanza wa chuo, tutalipa” alisema Masoud, huku akimvuta Anna ubavuni kwake, nae anajilegeza na kujilaza ubavuni kwa mpenzi wake huyu, amae siku zote, aliamini kuwa ndie mume wake mtarajiwa.
Wazo la Masoud Kizinge, ulipokelewa kwa mikono miwili na Arianna, ambae aliaidi kumsaidia mpenzi wake huyo bega kwa bega, mpaka wafanikiwe malengo yao, maana aliminikuwa kufanikiwa kwa Masoud ndio kufanikiwa kwake yeye, sababu kama Masoud angemaliza chuo na kupata kazi, basi wangeweza kuishi pamoja na kuweza kuwasaidia wazazi wake ambao kwakifupi walikuwa na maisha duni.
Kitu ambacho siyo Arianna wala wazazi wa masoud walikuwa awakijuwi ni kwamba, Masoud alikuwa ameanguka vibaya kwenye mitiani yake ya mwisho, na kupata division tatu ya kidato hicho cha sita, japo katika masomo aliyo fauru, ni masomo ya biashara, lakini ukweli ni kwamba, Masoud ambae siku za hivi karibu ni alikuwa amekosa amani moyoni mwake, kutokana na kukosa fedha za kwenda chuo, lakini siyo chuo kikuu cha Dar es salaam kama, alivyo wadanganya wazazi wake, na mchumba wake Arianna, ukweli ni kwamba, aliomba nafasi katika chuo cha biashara cha CBE, chuo ambacho kiliitaji fedha nyingi sana ili aweze kujisomesha, maana akuwa na ufadhiri wa serikali.
Siku tatu baadae, mida ya asubuhi, Masoud akiwa na baba yake wanakagua Trektor ambalo lilikuwa linaitajika kwenda kubeba mazao kwenye shamba la mzee Mdem, alie likodisha kwa siku hiyo, ndipo mzee Kizinge alipo mtandika swali kijana wake, ambae siku zote amekuwa akijivunia, “hivi umeishia wapi, kuhusu maswala ya chuo?” aliuliza mzee Kizinge, “yani baba, mpaka sasa sijuwi iakuwaje, maana hakuna mpango wowote wakupata fedha, ila wewe kama baba inatakiwa ndio ungaikie swala ili” alisema Masound, akimweleza baba yake, ambae mpaka hapo, mzee huyo alisha sahau kusomesha mtoto kunafanana naje, maana jukumu lote lilikuwa ni la Arianna na familia yake, ambao walimsomesha Masoud kwa tabu na kwajasho.
Mzee Kizinge alitabasamu kidogo, “inamaana mchumba wako amesha ghairi kukusaidia, lakini ukipata kazi yeye ndie atakae faidi, na siyo sisi” alisema mzee Kizinge, huku anaendelea kufunga nati za kwenye bomba za maji ya kupoozea mashine ya trector lake, “lakini baba wakina Anna, wana uwezo gani wakupata million mbili, maana ukiachia ada inabidi nipate nyumba ya kulala, na pia niwe na ela ya kula, na usafiri, na ia dhararula yangu mwenyewe” aifafanua Masoud, ambae nikama alisha kata tamaa ya kwenda chuo, na pengine angebakia hapa hapa kijijini kitu ambacho akutaka ata kukisikia, maana alishaonja maisha ya mjini, “atizo lako utumii hakiri zako Masoud, mbona ilo swala lahisi sana kwa bwana Sinyangwe” alisema mzee Kizinge, kwa sauti ya kujiamini, na yakujitapa, kama kawaida yake. …. endelea….
UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA SEHEMU YA TATU: maana ukiachia ada inabidi nipate nyumba ya kulala, na pia niwe na ela ya kula, na usafiri, na ia dhararula yangu mwenyewe” aifafanua Masoud, ambae nikama alisha kata tamaa ya kwenda chuo, na pengine angebakia hapa hapa kijijini kitu ambacho akutaka ata kukisikia, maana alishaonja maisha ya mjini, “atizo lako utumii hakiri zako Masoud, mbona ilo swala lahisi sana kwa bwana Sinyangwe” alisema mzee Kizinge, kwa sauti ya kujiamini, na yakujitapa, kama kawaida yake. …. endelea….
Hapo Masoud akatabasamu kidogo, maana tumaini jipya lilianza kuingia moyoni mwake, maana anamfahamu vyema baba yake, asa anapo ongea katika mtindo huu, ujuwe lazima kuna matokea mazuri yanakuja, “baba bwana, unazani aafanya nini Anna, ikiwa sisi wenyewe tumeshindwa?” aliuliza Masoud kwa maana ya kuchokoza baba yake aseme anacho kifikilia, “sikia Masoud kama kweli Anna anataka kukusaidia usome, anaweza kukusaidia bila shaka yoyote, maana jana nikiwa kwenye ulanzi, nimesikia habari ya mtu mmoja anae itaji kufungua mashamba ya viazi mvilingo hapa kijijini, hivyo anatafuta mashamba ya kukodi” alisema mzee Kizinge, huku akimweleza kijana wake kuwa mzee Sinyangwe anamashamba makubwa sana ambayo kutokana na hali yake duni ya kiuchumi, ameshindwa kuendeleza.
Mwisho wa amelezo ya mzee Kizinge, Masoud alikuwa amenyongea, “nini ujaelewa hapo, mbona kama umenyongea tena?” aliuliza mzee Kizinge baada ya kugundua hali ya mwanae, “sasa baba kukodi shamba ni elfu hamsini kwa ekari moja, shambalao ni heka kumi na tano tu, sawa na laki saba na nusu, sasa millioni moja laki mbili na nusu tutatoa wapi?” aliuliza Masoud kwa sauti ya kulalamika, “sikia Masoud hayo ni malipo ya mwaka mmoja, una washawishi wachukue malipo ya miaka mitatu’ alisema mzee Kizinge nikama alikuwa mwenye kuangalia faida yake mwenyewe, na siyo kila ambacho kinge mtokea mzee mwenzie, ambae kwa muda wote amekuwa akimsomeshea mwanae.
Mpaka hapo Masoud alikuwa ameachia meno wazi, kwa tabasamu, baba ungesoma wewe, ungetusumbua sana” alisema Masoud na wote waacheka, kwa pamoja, “we unazani hizo hakiri umrithi kwa nani?” aliuliza mzee Kizinge, kwa sauti ya majisifu, ‘kuna mwingine basi zaidi yako, ila nikiwa rais nitakuchagua kuwa waziri wa mipango” alisema Masoud wote wawili wakicheka kwa pamoja, huku wakigongeana mikono.
Naam, ukweli ni kwamba, ikuwa kazi nyepesi sana, kwa Masoud kumshawishi Anna, juu ya wazo lile la Masoud, Anna nae akaenda kwa baba na mama yake, na kuwaeleza mpango ule, ambao ulikubalika mala moja, mbele za wazazi wake, ambao kiukweli walikuwa waaamini kuwa mafanikio ya masoud ndio mafanikio ya binti yao, na mafanikio ya binti yao, ndiyo mafanikio ya familia nzima, hivyo basi kwa msaada wa mzee Kizinge yani baba yake Masoud, mzee Sinyangwe na bini yake Arianna, wakakutana na mwakilishi wa tajiri mmoja toa dar es salaam, alieitaji shamba ilo, ambapo waliweka mkataba wa malipo ya Tsh million mbili lakini mbili na elfu hamsini, ambazo ni malipo ya kukodisha shamba kwa miaka mitatu, na fedha hizo zingeingizwa kwenye accout ya Masoud, kwa hawamu tatu.
Yap! malipo hawamu ya kwanza yalifanyika na Masoud akaenda chuo, akiagana vizuri na mpenzi wake wa utotoni, ambae alisha muahidi kumuoa mala tu akimaliza chuo na kupata kazi, na kwamba watausaidia familia ya mpenzi wake huyo na kuwafanya waishi maisha mazuri.********
Naam, Arianna aliendelea na maisha yake kama ilivyo kawaida, huku akifanya kazi ndogo ndogo, za vibarua vilivyo mwingizia fedha ambazo zilimwezesha yeye na familia yake kupata chakula cha kila siku, pasipo kusahau kwenda kwa mama mkwe kumsaidia kazi, kila siku baada ya kutoka kwenye vibarua, ambavyo alikuwa anasaidiana na ndugu zake, pamoja na wazazi wake, huku kila siku zilivyoenda ndivyo alivyozidi kufubaa mwili na ngozi yake, ata alipotimiza miaka ishilini na moja, ungezania kuwa ni mama wa miaka therasini na saba, kiasi cha kuto kutamaniwa na mwanaume yoyote, zaidi ya wale wenye tamaa ya kuonja onja.*******
Miezi mitano ilitimia, pasipo mawasiliano yoyote, ukweli Arianna akuwa na simu, na ata siku moja alipo omba kwa mama mkwe mtarajiwa kuwasiliana na mume wake mtarajiwa, mama mkwe alibofya namba za mwanae masoud na kupiga, ilikuwa ni mida ya jioni, simu nayo ikaanza kuita, huku mama Masoud, yani mke wamzee Kizinge, na aikuchukuwa muda mrefu upokelewa, “shikamoo mama” ilikuwa ni sauti iliyochangamka ya Masoud, ambae alikuwa na miezi minne ajawasiliana na mke wake mtarajiwa, huku Arianna akisikia kwa uwazi maongezi hayo, “marahaba mwanangu, nipo na Arianna, anaaka akusalimie” alisema mama Masoud, huku anacheka cheka.
Hapo wote wawili wakatulia kusikia jibu la Masoud kukubali kuongea na Anna…..…. endelea….
Kalibu
JibuFuta