ILIPOISHIA SEHEMU YA NNE: ilikuwa ni mida ya jioni, simu nayo ikaanza kuita, huku mama Masoud, yani mke wamzee Kizinge, na aikuchukuwa muda mrefu upokelewa, “shikamoo mama” ilikuwa ni sauti iliyochangamka ya Masoud, ambae alikuwa na miezi minne ajawasiliana na mke wake mtarajiwa, huku Arianna akisikia kwa uwazi maongezi hayo, “marahaba mwanangu, nipo na Arianna, anaaka akusalimie” alisema mama Masoud, huku anacheka cheka. Hapo wote wawili wakatulia kusikia jibu la Masoud kukubali kuongea na Anna…..…. endelea….
lakini ilikuwa tofauti kabisa, maana Masoud alianza kugubeza, “khaaa! mamaaaaa nipo busy najisomea, sina muda wa kuongea nae, nitampigia siku nyingine” hapo kuna kitu kama msisimko wa simanzi ilisambaa mwilini mwa Arianna, ambae japo aliabasamu, lakini kiukweli alijisikia aibu kiasi flani, siyo kwaajili ya jibu alilo pewa a mchumba wake huyo, ambae ni mwanaume pekee alie mpatia kitumbua chake, toka mschana huyu alipovunja ungo, pengine ni kweli kijana wetu alikuwa busy na masomo, maana ata Arianna alishawai kusikia kuwa masomo ya chuo, yanalenga sana kwenye kwenye tafiti, hivyo mtu ungepaswa ujisomea kwa mudamrefu na kwa juhudi kubwa sana, “mwenzio amebanwa na masomo, uaongea nae siku nyingine” alisema mama Masoud, pasipo kufikilia kile kitendo cha kuguna, alicho kifanya mwanae.
Aikutumia siku nyingi kwa Arianna, kusahau mguno wa mbezo, wa mpenzi wake, maisha yaliendelea Arianna akimsubiri mpenzi wake kwa hamu kubwa, huku sikuzote wakati wakulala akitumia lisaa lizima kuwaza na kuvuta picha ya maisha mapya watakayo ishi na mpenzi wake, huko dar es salaam, hakika ilkuwa ni picha nzuri, picha yenye maisha mazuri yenye upendo na amani, maisha yenye watoto wachangamfu wenye afya, maisha yenye kutembelewa na wazazi na wadogo zake ambao sasa walikuwa wanasoma shule nzuri, na kuvaa mavazi mazuri ya kupendeza.
miezi mitatu baadae yani mwezi wa saba, week ya kwanza ya mwezi huo, Arianna alikuwa amebanwa na kazi nyingi sana, za vibarua, ilibidi apambane sababu, wadogo zake waliitaji sare mpya za shule, na vitabu, ubusy ambao, ulisababisha Arianna akae siku nne, pasipo kwenda nyumbani kwa mkwe wake, yani mama Masoud mke wa mzee Kizinge, lakini siku ya tano ambayo ilikuwa ni juma tano, mida ya jioni, Arianna alienda nyumbani kwa kina Masoud, ambako alimkuta mama mkwe wake mtarajiwa, akiwa anaangaika kuosha vyombo ya toka asubuhi, “we mtoto Siunge niambia kama nitafute dada wakazi, yani umetoweka kabisaaaa, uliposikia mwenzio kaja, ndio unakuja” alilalamika mama Masoud, bila ata kungoja salamu ya mkamwana wake, japo ilimshangaza kidogo Arianna, kwamba mwenzie kaja, “samahani mama, nilibanwa na kazi” alijitetea Arianna, huku ana sogea kwenye vyombo vichafu na kuanza kusaidia kuosha.
Pengine unaweza kuzania mama Masoud angekaa kimya, lakini aikusaidia, ndio kwanza lawama zika geuka masimango, “ yani mimi nakushangaa sana, ena ata sijuwi unajiamini nini, hapo bado ujaolewa umeshaanza jeuri, ukiolewa sindio utaniambia nikuandalie maji ya kuoga” alisema kwa sauti ya juu, mama Masoud, alie simama pembeni huku ameshika kiuno, hapo Arianna aliishia kucheka kidogo, kwa furaha aliyoipata baada yakusikia kuwa Masoud amekuja.
Lisaa limoja lilikatika, Arianna akimaliza kuosha vyombo, pasipo kumwona Masoud, kwakuwa ilikuwa mapema, akuwa na wasi wasi, zaidi aliingia chumbani kwa kijana huyu, ambako alikua kuguo na viatu vizuri vya kisasa, baadh yake vikiwa vichafu, akafua nguo zoe chafu, pamoja na viatu, mpaka mida ya saa moja, za usiku, tayari alikuwa amesha maliza kufanya usafii wa nguo na viatu vya mpenzi wake huyo pasipo kumwona, lakini hiyo aikumfanya Arianna aache kumsubiri mpenzi wake, ambae alikuwa anamuda mrefu ajamwona.
Arianna alikaa na mama mkwe akimsaidia kupika chakula cha jioni, chakula ambacho sikuzote kwao imekuwa kama ndoto, kwamba watakuja kula siku Masoud akipata kazi, “lakini ukiona anachelewa unaweza kuja kesho mapema, maana toka afike juzi, mida yae ya kurudi ni saa nne usiku” alishauri mama Masoud, wakati ambao tayari Anna alikuwa amesha maliza kupika, nikama utamadumi wa mala kwa mala, kwa mama huyu, linapokuja swala la chakula, Anna angepika na kuonsha vyombo lakini kwenye muda wa kukaa mezani, hapo angepewa vijimaneno vya kumfanya aage na kuondoka zake, pasipo kupitisha mdomoni kile alicho kiangaikia jikoni. “he! kumbe amekuja toka juzi?” aliuliza Anna kwa mshangao, maana akutegemea kama Masoud anaweza kufika hapa Malangari, siku tatu nyuma, bila kumtafuta wala kumjulisha.
Nikweli Msoud aliingia pale nyumbani kwao mida ya saa nne kasoro, wakati Anna anajiandaa kuondoka, kwenda nyumbani kwao, maana kesho pia angeitajika kuamka mapema, kwaajili ya kwenda kwenye vibarua vyake,ambavyo kwa sasa ndio kitu pekee cha kumwingizia fedha, “ho! Anna, mambo vipi?” alisalimia Masoud, ambae alikuwa amependeza na kuonekana kuwa ni kijana wakisasa usinge sema kuwa alizaliwa pale kijijini Malangari, “poa tu Masoud, yani umefika bila ata kuniambia” alilalamika Arianna, kwa sauti ya kujidekeza kwa mpenzi wake.
Ukweli nikama aliekosa jibu la maana, au kama vile akupenda uwepo wa mwanamke huyu, hapa nyumbani kwao, Masoud akamtazama Anna, kama anamtafutia jibu, “kama wewe mwenyewe auji hapa nyumbani unataka mimi nifanyaje?” ilo lilikuwa swali, lakini ndiyo jibu toka kwa Masoud ambae baada ya kuongea hivyo akaanza kutembea kuelekea chumbani kwake, “lakini Masoud hiyo siyo sababu ya wewe kushindwa kunitumia ata ujumbe kuwa umefika, kwa hiyo ningekuwa nina umwa ndio tusinge onana?” aliuliza Anna kwa namna ya kuo kukubariana na sababu ya Masoud kuto kumjulisha ujio wake, “swala la kuumwa ni jingine, ila lakuacha kuja home makusudi ilo la kwako mwenyewe” alijibu kikaudhu Masoud, huku anakaa kwenye kitanda na kuanza kuvua viatu vyake vya kisasa, vya gharama kubwa………..…. endelea….
UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA SEHEMU YA TANO: “lakini Masoud hiyo siyo sababu ya wewe kushindwa kunitumia ata ujumbe kuwa umefika, kwa hiyo ningekuwa nina umwa ndio tusinge onana?” aliuliza Anna kwa namna ya kuo kukubariana na sababu ya Masoud kuto kumjulisha ujio wake, “swala la kuumwa ni jingine, ila lakuacha kuja home makusudi ilo la kwako mwenyewe” alijibu kikaudhu Masoud, huku anakaa kwenye kitanda na kuanza kuvua viatu vyake vya kisasa, vya gharama kubwa………..…. endelea….
Hakika kijana huyu alionekana kuwa ni mwenye mwonekano wa kisasa kabisa, usingeweza kumfananisha na Arianna, ambae siyo tu kuzoofika mwili, kutokana na kazi ngumu, pia alionekana kuzeeka sura yake, kwahiyo kama nisingekuja na wewe usingekuja ata kuwasalimia wakina baba?” aliuliza Arianna, huku akiwa anakaa kwenye kitanda, yani pembeni ya Masoud, akitegemea kupata dudu ya mpezi wake usiku ule, “sasa kama wewe uaki kuja kwetu mimi ningefwata nini kwenu” alisema Masoud kwa sauti kavu, akionyesha wazi kutokuwa na shahuku na mwanamke huyu, “basi baba tuyaache hayo, nipe habari ya Dar, vipi uzuri hen?” alisema Arianna, huku anajiegemeza ubauni kwa Msoud, na kukutana na arufu nzuri ya manukato.
Miaka ya nyuma, hapo Masoud angejibu huku anamkumbatia Anna, lakini leo ilikuwa tofauti kidogo, “akuna jipya, kwa kawaida tu” alijibu Masoud huku anainuka na kuanza kuvua shati, wakati bado ata viatu akumaliza kuvua, “jamani, mbona watu wanasema ni kuzuri sana” alisema Anna, huku anamtazama mpenzi wake ambae alionekana kuwa na ngozi laini kuliko yeye ambae ni mwanamke, “kwani mimi nimeenda kushangaa jiji au kusoma?” lilikuwa ni swali la mkato, toka kwa Msoud alie kuwa Anna maliza kuvua shati na kuvaa tishert kisha aka vua viatu akiwa amesimama.
Kuna kitu Anna aliona akipo sawa, lakini akuwa na uhakika, na mawazo yake, kama Masoud amechoka na mizunguko yake, au kuna jambo linamtatiza, “nikuambie kitu Anna, twende nikusindikize, maana ninataka kulala mapema” alisema Masoud, pasipo kuonyesha uso wa uchangamfu wala tabasamu, “wala nisikusumbue baba, nikuache upumzike nitakuja kesho jioni” alisema Anna, akimwonea huruma mpenzi wake, ambae alionyesha kuchoka au kukosa aliflani ya uchangamfu.
Siku ya pili jioni, baada ya kutoka kwenye kazi zake za kila siku, Anna alienda nyumbani kwa kina Masoud, ambako akuona dalili ya uwepo wa Masoud, zaidi alimkuta mama mkwe wake, huku lundo la vyombo vya toka jana usiku vikimsubiri, Anna alifanya kazi zake, na alipomaliza alituia kumsubiri Masoud, ambae alirudi mida ya saa tatu, na kupitiliza chumbani, kama ilivyokuwa jana, japo leo ilikuwa na utofaui kidogo, maana dakika kumi baadae Anna alipoingia chumbani kwa Masoud alimkuta akiwa amesha lala, kama vile amelala lisaa lizima lililopita nae akutaka kumsumbua, akaaga na kuelekea kwao, huku njiai akijiuliza juu ya ubusy ambao unamkaba Masoud, kiasi cha kushindwa kutamani kuwa nae, hali ambayo iliendelea hivyo kwa muda wa week nne.
Ukweli limuumiza sana mschana Anna, ambae alimsubiri mpenzi wake huyu kwa hamu kubwa, alafu matokeo yake Masoud anakosa muda wa kuwanae, hali ambayo ilimfanya Anna awaze sana, japo alijitaidi kuyapuuzia mawazo yale ya kwamba mapenzi yao yameisha, ata hivyo wazazi wake ndio walio kuja kutilia shaka juu ya mwenendo wa mapenzi ya binti yao.
Hiyo ilikuwa ni mala baada ya, kusikia kuwa Masoud amekuja hapa kijijini tangu week nne zilizopita, “Anna kumbe huyu mwenzio yupo hapa kijijini na ameshindwa kuja kutusalimia?” aliuliza mama Arianna, walipokuwa njiani wanarudi toka kwenye vibarua, siku hiyo walikuwa wenyewe, maana baba yake alikuwa amelala nyumbani ajisikii vizuri kiafya, “amesema atakuja, ila kwa sasa kunamambo anafwatilia, alisema Anna akimtetea mchumba wake, “mambo gani anafwatilia kiasi cha kushindwa kuja kutusalimia, kwa aya yote tunayo mtendea” alisema mama Arianna, akionyesha wai kuto kuwa na imani na Masoud utokana na kitendo cha kuto kuja kuwasalimia.
Nikweli mashaka ya mama Anna, yaliugusa moyo wa Anna, lakini alijipa moyo, na kuamini kuwa Masoud akimaliza ubusy wake, ata kuja nyumbani kwao kuwasalimia wazazi wake, “Anna, leo naomba usiende kwa kina Masoud, bakia hapa nyumbani, tusaidiane kazi, mimi nitakuwa na mwangalia baba yako” alisema mama Anna, japo ilimshangaza Anna mwenyewe, maana baba yake akuwa anaumwa kiasi cha kuangaliwa kama mama yake anavyosema, ila akuwa na pingamizi.
Ukweli siku ile Arianna, alibakia nyumbani kwao, akifanya kazi za nyumbani, ata siku ya pili aliamkia kwenye kazi zake akiongozana na mama yake, huku moyoni mwake akiwa anawaza juu ya Masoud na mama mkwe wake, yani mama Msoud kwamba wange chukuliaje kwa yeye kutokwenda nyumbani kwao siku iliyopita, “naona baba yako anaendelea vizuri, ila ajapenda kitendo cha Masoud kutokuja kutusalimi” alisema mama Anna, wakati wakiwa njiani wanarudi nyumbani, “lakini mama nimekuambia kuwa ametingwa na mambo flani, atakuja tu” alisema Anna, ambae ukweli akuwa na uhakika wa kile anachokisema, “jambo gani muhimu huku kijijini, kama kila kitu wewe ndie unae msaidia, ada ya chuo mapaka nauri ya kuendea huko chuoni kwake, ssa yeye nngaika na nini kiasi cha kushindwa ata kuja kusalimia?” aliuliza mama Arianna.
Maneno ya mama yake yalionyesha kumwigia Arianna, ambae licha ya yote, akuamini kama Masoud anaweza kufanya tofutti kama walivyo panga juu ya maisha yao ya baadae, “jamani mama Masoud awezikufanya hivyo kwa mkusudi, atakuja tu” alisema Arianna, ambae kiukweli siyo tu, kumpenda Masoud ila “sawa najuwa hapo ulikosa kwenda jana, basi leo unatamani kwenda” alisema mama Anna, huku wanaendelea kutembea na majembe yao begani.
Arianna akuwa nalakujibu zaidi ya kucheka basi kabla ujaenda kwa mkweo, unisaidie kwanza kazi za pale nyumbni” alisem mama Anna, ambae wasi wasi wake juu ya Masoud ulikuwa ni wa wazi kabisa. “ndiyo mama” Anna ambae kiukweli alitamani sana leo kwenda mapema nyumbani kwa kina Masoud, maana aliofia sana lawama na masimango ya mama kwe huyo, na ukichukulia, jana yake akwenda kwa mama mkwe huyo.
Naam mcshana Arianna alifanya kazi kw haraka, huku mpango wake ni kuwai kwa kina Masoud, ambako pia angekutana na kazi zaidi ya hizi anzo pambana nazo pale kwao, lakini kila alipo maliza hii mama alimpatia nyingine, “nisaidie nahii, kabl ujondoka” na ilikuwa hivyo kila napomaliza kazi nyingine, muda wote mama yake na baba yake wliokuw wmekaa pl mbele ya nyumba yao, walikuwa wanamtazama, huku wakikonyezana ungesema kuna jambo walilikusudia.
Saa kumi na mbili nanusu, ndiyo mida ambayo Anna alikuwa amemaliza kazi za pale nyumbani, lakini kabla ata Anna aja aga ili aondoke zake kwenda kwa wakwe mala akamdogo wake mdogo kabisa, ambae alikuja mimbio mbio mpaka kwa dada yake, “dada… dada… Masoud yupo pale barabarani, amesema anakusubiri” alisema yule mtoto, mbe ni mdogo w mwisho wa Arianna, kisha akaondoka zake, “inamaana yeye ameshindwa kuja hapa nyumbani” aliuliza mzee Shinyangwe, huku yeye na mke wake wakimtazama binti yao ambae sasa alikuwa ananawa mikono haraka ili awai kule likoitwa…… .…. endelea….
UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITA: Saa kumi na mbili nanusu, ndiyo mida ambayo Anna alikuwa amemaliza kazi za pale nyumbani, lakini kabla ata Anna aja aga ili aondoke zake kwenda kwa wakwe mala akamdogo wake mdogo kabisa, ambae alikuja mimbio mbio mpaka kwa dada yake, “dada… dada… Masoud yupo pale barabarani, amesema anakusubiri” alisema yule mtoto, mbe ni mdogo w mwisho wa Arianna, kisha akaondoka zake, “inamaana yeye ameshindwa kuja hapa nyumbani” aliuliza mzee Shinyangwe, huku yeye na mke wake wakimtazama binti yao ambae sasa alikuwa ananawa mikono haraka ili awai kule likoitwa…… .…. endelea….
“Inamaana ndio ataishia huko huko” aliuliza mama yake Anna hapo Arianna ambae akuwa na lakujibu, akajichekesha huku anaondoka mbio mbio kukimbilia kule barabarani, ambako alimkuta Masoud akiwa amesimama anamsubiri.
Kwanza kabisa Arianna alitegemea lawama toka kwa Masoud ambae siku kwa sasa amekuwa na tabia ya kumnunia bila kosa, lakini alipofika tuakapokelewa na tabasamu la matumaini, usingese shindwa kubaini kuwa, kijana huyu alikuwa anashida kubwa ambayo inge tatuliwa na mpeni wake huyu, ambae ni sawa na mbachao, ambao unasahauliwa baada ya kupatikana kwa mswala mpya, “nilikuwa na wasi wasi sana, nikajuwa umepatwa na tatizo, mbona jana ujaja nyumbani, na ata leo sioni dalili yaw ewe kuja nyumbani?” aliuliza Masoud, huku anamsogelea Arianna, na kumshika viganja vyote vya mikono, kwa mikono yake miwili.
Hakika kitendo hicho, kilimfanya Anna ajisikie raha na msisimko, maana mala ya mwisho kushikwa hivi, na mpenzi wake huyo, ni zaidi ya miezi nane iliyopita, “mwenzio baba anaumwa ndio maana sikuweza kuja, ila leo nilipanga nije ata kama ingekuwa usiku” alisema Anna, huku anajitabasamulisha, “weeee unasema baba mgonjwa, mbona ukuniambia nije nimtazame?” aliuliza Masoud, kwa sauti iliyo jawa na mshangao, huku anapapasa vinja vya Arianna, swali ambalo lilimfanya Arianna binti wa Sinyangwe ajihisi kama amezaliwa upya, “tena alikuwa anakuulizia kila siku, nikamweleza kuwa umesema utaenda kumwona” alisema Anna, kwa sauti ya kujidekeza kwa mpenzi wake, ambae toka arudi likizo, leo ndiyo afadhari ameonyesha kuwa bado wapo pamoja, “ukweli Anna ujanitendea haki kabisa, yani unashindwa kunipa taarifa ya kuumwa kwa baba, utazani mimi na wewe siyo wachumba” alisema Masoud kwa sauti ya kulalamika, akiwa bado ameshikilia mikono ya Anna, “nisamehe Masoud, lakini ulikuwa busy sana” alijitetea Arianna, “lakini nisingeshindwa kuja kumwona mgonjwa” alisema Masoud kwa sauti ambayo ilionyesha wazi kuwa akupendezwa na kitendo cha kuto kupewa taarifa ya mgonjwa.
Basi waliongea mawili matatu, kabla Masoud ajaeleza kitu harisi kilicho mfanya amtafute Anna jioni ya leo, “alafu Anna nakaribia kurudi, chuo, niandalie kama laki mbili tu, yanauri na yakuanzia siku mbili tatu, baada ya hapo nitajuwa lakufanya” alisema Masoud wakati wanaagana mida ya saa moja na nusu, “wala usiwe na wasi wasi mpenzi wangu, na juwa jukumu langu” alisema Anna ambae alikuwa anajuwa anachokifanya kinafaida kubwa katika maisha yao ya baadae.
Kauri ilimfurahisha sana, Masoud, ambae ni tofauti na walio wengi, yeye anafadhiriwa masomo ya chuo, na mschana masikini, kuliko familia yake, “poa basi waambie wakina mama nitakuja kesho kumwona” alisema Masoud, wakati anaondoka zake, kueleka upande wa kwao kabla aja kata kona kuelekea upande wa kijiweni, huku Anna akielekea kwao moyo wake umefarijika kupita kiasi, na kuwaeleza wazazi wake ujumbe toka kwa Masoud, ambao wazazi wake waliupokea kwa mtazamo wa mashaka.
Baada ya kuwapa ujumbe huo wazazi wake, Anna akaingia chumbani kwake, moja kwa moja mpaka kwenye kopo aliloliweka uvunguni mwa kitanda, na kulifunua, kisha akazamisha mkono na kuibuka na noti kadhaa mchanganyiko wa elfu moja moja, elfu mbili mbili, elfu tano na elfu kumi, na kwa msaada wa kibatari akaanza kuhesabu, kwa kuzipanga mafungu kwa jinsi zilivyo, yani elfumoja kwa elfu moja nyenzie, elfu mbili hivyo hivyo na zote mpaka elfu kumi, idadi yake iliuwa ni tsh lakini mbili na therasini, “afadhari imetimia, baba mtarajiwa aende chuo, akatafute maisha ya baadae” alijisemea Anna, huku anarudisha zile fedha kwenye kopo, fedha ambazo amezitolea jasho kwa muda mrefusana, huku akijinyima kula vizuri, kuvaa vizuri, na mambo mengine muhimu.
Siku chache mbele Masoud aliondoka na kuelekea chuo, akiwa amekabidhiwa fedha na Arianna, lakini swala la kwenda kuwaona wazazi wa mchumba wake, lilikuwa ndoto hisiyo timia.******
Kitu ambacho Arianna akukijuwa ni juu ya maisha ya ua Masoud huko mjini, labda tutazame na upande wa kijana huyu, toka alipo fika chuo na kupokelewa, mpaka sasa anarudi shule katika muhula wa pili.
Wakati kule nyumbani Mlangari wanajuwa kuwa kijana yupo chu kikuu cha milimani, kumbe kijana wetu alikuwa chuo chaVETA, akicukuwa mafunzo ya utengenezaji wa vifaa vya ndani ya nyumba, yani furniture, ni baada ya kukosa nafasi katika chuo cha biashara, kutokana na marks zake za mihani, wa mwisho wa kidato cha sita, na kuona itakuwa aibu kurudi nyumbani ambako wangejuwa ukweli, juu ya maokeo yake mabovu, ya kidato cha sita.
Masoud kwa ushauri wa rafiki yake ambae walisoma wote Iringa, ambae alikuwawepo pale Veta, akachangia chumba kimoja na yule rafiki yake, kule buguruni malapa, ambako mwenzie alikuwa amepanga, na maisha ya chuo yakaanza, huku Masoud akijitaidi kuvaa vizuri, kwa kutumia fedha ambazo alikuwa analipwa, kwa awamu na mtu alie kodisha shamba, la wakina Anna.
Hakuishia hapo kijana Masoud, Fedha hiyo hiyo ilimfanya aanza kunywa pombe na kujipatia waschana, ambao walitambua kuwa Masoud ni mtoto wa tajili mmoja mkubwa huko Iringa, Masoud ambae akudumu na mwanamke mmoja japo kwawiki moja, alifikia hatua akaanza kusaka wanawake kwenye kumbi za starehe, wazo alilolipata toka wa marafiki zake, wa chuo, na wamtaani. … .…. endelea…
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Write your comment