Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Jumamosi, 8 Machi 2025

Ukimaliza Funika 14_15


 


SEHEMU YA KUMI NA NNE

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TATU: japo TV ndogo ya nchi kumi na nne, ilikuwa inaendelea kuuguruma mbele yake, juu ya meza maalumu ya kuwekea television, mala kwa mala Masoud alibofya simu yake, kuperuzi kwenye mitanao ya kijamii, akijibu comment za marafiki zake, aliowai kusoma nao iwe chuo au kule Iringa, walio Comment kwenye picha zake, wakiwepo waschana ambao aliwai kupita nao siku za nyuma, Masoud aliyafanya hayo, huku akishushia bia zilizojaa mezani, ni wazi akuwa pake yake kwa mzigo ule wa bia, lazima kunamtu alikuwa anamtarajia, usiku ule. .…. endelea….


“nipe siri ya mafanikio kaka maana umekuwa vizuri” ilisema moja ya comment, nae akajibu kwa kujiamini, “mbona kawaida kaka tunaendelea kupambana” hakika ilikuwa raha sana, kwa kijana huyu toka marangari, kuja mjini, na kukutana na maisha kama aya, inaitaji moyo mgumu sana kukumbuka ulikotoka, japo safari na ujio wake wa dara es salaam, ilichangiwa kwa kiasi kikubwa na msaada toka kwa mschana wafamilia duni na masikini.*******


Naam sasa tuelekee Mikocheni Dar es salaam, ni mikocheni A, maeneo ya chama, nyuma ya jengo la Tanesco, ndani ya jumba moja kubwa sana la kifahari lililozingukwa na ukuta moja mkubwa sana, kwa jinsi jumba ili lenye viunga vya kupendeza lilivyo onekana usiku huu, ungesema ni moja ya hotel kubwa zenye utulivu hapa Dar es salaam, usingezania kuwa ni nyumba binafsi ya mtu, asa ukizingatia mpangilio mzuri wa viunga na bustani mbele ya jumba lile, lenye kupendezeshwa na nyasi za koka, mauwa ya akila aina yaliyopanwa katika mpangilio mzuri, pia bwawa la kuogelea yani swimming pool, lile tengenezwa vizuri, na lenye kuvutia, kushoto yalionekana magari manne ya kifahari, kati yao lenye thamani ndogo kuliko yote, lilikuwa ni Range Rover new model.


Licha ya kuwepo kwa walinzi wawili, waliovalia sale za kampuni flani ya ulinzi, lakini ghfla tuonaona gate linafunguka lenyewe, na linaingia gari moja aina ya RANGE ROVER, la kisasa kabisa, na la gharama kubwa, la langi ya kijivu, ambalo liliingia na kusimama mbele ya jengo ilo pembeni ya magari mngine yakifahari yaliyokuwepo hapo, kisha akashuka mzee mmoja wa makamo alie valia kaptura ndefu mpaka magotini, na tishet nyepesi chini akivalia sendo, na wakai huo uhuo mlango wa jumba kubwa ukafunguliwa wakatoka waschana watatu, waliovalia magani ya blue ya kufanana, na vitambaa vyekundu viunoni mwao, yani epron.


Kama aikutosha, wakaonekana vijana wawili wakiume wakitokea upande wa kulia wa jumba lile, wakiwa, na wakati wale waschana wakiwa wamesimama, mbele ya kibaraza kizuri chajumba lile, huku wavulana wawili walionekana wakienda moja kwa moja, mpaka lilipo lile gari la kifahari kuliko magari yote pale ndani, “kazi nzuri vijana, naona ata wenyewe akirudi, atafurahi sana kukuta nyumba yake hipo katika mwonekano huu” alisema yule mzee, huku huku uso wake ukionyesha tabasamu, “pia mkesho mtaenda kununua vitu kwaajili ya sherehe ya jumamosi kwaajili ya kusurprise mchumba wake, ambae aijuwi hii nyumba” alisema mzee yule, huku na wakati huo huo, likaingia gari jingine, ambalo ni Toyota V8, na kusimama nyuma ya range lover, “naona Dereva amenifwata, mimi naonika zangu” alisema yule mzee, kisha akaanza kutemmbea kulifwata lile V8, akiwaacha wale wafanyakazi wanashangaa, kwanini analiacha lile gari la kifahari.


Nikama yule mtu mzima, aligundua mshangao wa wale wafanyakazi wa jumba lile, “hoo! nilisahau, ilo gari jipya ni la Sebastian, nimelitoa airport sasa hivi, baada ya kumaliza taratibu zote za malipo ya kodi na usajiri, hivyo mliangalie vizuri, maana nigari lathamani kubwa sana” alisema mzee huyo na kuondoka zake, kuingia kwenye gari, kisha gari likatoka nje ya geti, “Dotto, utunaelekea sinza kwa kina Salma, inabidi nika mjulishe Shangazi yake, juu ya hafla ndogo ya jumamosi” alisema mzee huyo.


Naaam hapo Dereva aitwae Doto, akashika uelekeo wa Sinza kama alivyoagizwa, “unajuwa Seba, anampenda sana Salma, amepanga kumfanyia Surprise ya gari jingine, baada ya IST, ana mpayie lile toyota Caldina, nalo ni jipya, na pia katika siku hiyo Seba atatangaza tarehe ya ndoa, pamoja na kumwonyesha hii nyumba, ambayo wataishi baada ya kufunga ndoa, maana pia mchumba wake aijuwi” alisema mzee huyo, mwenye mkadirio wa umri wa miaka alobaini na nane.


Huyu anaitwa mzee Kiguru, ni mwenyeji wa mkoa wa Iringa, wilaya ya Mufundi, kilomita chache toka mafinga mjini kwenye kijiji cha Kinyanambo, kiukweli, mzee huyu, mwenye utajiri kubwa ali upata kupitia biashara ya mbao, toka huko mufindi, kuleta dar es salaam na baadae kuongeza miradi mingine kama vile kufungua hotel kubwa sana, maeneo ya poster na fukwe za kunduchi, alifungua mradi wa hotel maeneo ya mwenge na kigamboni, na sasa anamradi mwingine wa usafirishaji, ambao unamagari mkubwa ishilini ya mizigo, pia alimfungulia kijana wake wa pekee Sebastian, maduka ya makubwa tatu, ya spare za magari na pikipiki, mala tu baada ya kumaliza Elimu yake ya chuo cha biashara, pale CBE, moja likiwa mwenge, moja kaliakoo, na jingine temeke.


Hiyo ilikuwa ni kama anatazama umkini au majaribio ya kuwa kijana wake, kuona kama anauwezo wa kusimamia biashara, maana baada ya miaka mitatu, akamfunguli mradi mwingine mkubwa, wa vifaa vya majumbani, vinavyo tumia umeme, biashara ambayo yeye mwenyewe alilazimika kwenda nchi za china  japan, kufunga mzigo, na kuja nao Tanzania. .…. 



SEHEMU YA KUMI NA TANO


ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA NNE: Hiyo ilikuwa ni kama anatazama umkini au majaribio ya kuwa kijana wake, kuona kama anauwezo wa kusimamia biashara, maana baada ya miaka mitatu, akamfunguli mradi mwingine mkubwa, wa vifaa vya majumbani, vinavyo tumia umeme, biashara ambayo yeye mwenyewe alilazimika kwenda nchi za china  japan, kufunga mzigo, na kujano Tanzania. .…. endelea….


Katika vitu ambavyo mzee Kiguru alikichukulia kama alama, ya kuwa kijana wake amekomaa kiakili na uwezo wa kibiashara, ni pale Sebastian alipofungua biashara ya utengenezaji na uuzaji wa feniture, za majumbani mashuleni na maofisini, na kumweka Salma kama msimuizi wa biashara hiyo, ni biashara ambayo ilikuwa inaingiza faida kubwa sana, na ukiachilia magari, kadhaa, madogo madogo yamizigo, yasiyozidi tani tatu, yaliyo milikiwa na kiwanda hicgo chenye mashine za kisasa na mafundi wazuri wenyeuwezo mkubwa, pia Sebastian alipatia mchumba wake Salma, gari dogo aina ya Toyota ist, kwaajili ya kutembelea, pamoja na kumpagia nyumba nzima maeneo ya sinza, ambako sasa anaishi na huko, na Shangazi yake.


Nasasa kijana huyu mwenye upendo mkubwa wa kustaajabisha, alieamua kubadirishia mchumba wake gari, licha ya yeye mwenyewe kujinunulia range lover, tayari pia alisha mnunulia mchummba wake, gari jingine jipya kabisa, aina ya Toyota Caldina ambalo alipanga amkabidhi atakaporudi toka Japan, ambako alienda kwaajili ya kununua mashine mpya kabisa, kwaajili ya kiwana kimpya cha kusindika matunda kungeneza juice, alichopanga kukiweka miembe saba, kule kibaha.******


Naam, akiwa bado yupo sebuleni, anatazama music video za wasanii mbali mbali toka ndani na nje ya nchi, kupitia television ndogo ya ukutani,  pia kijana Masoud aliendelea kusoma na jibu maoni (comment) za rafiki zake, katika picha yake, aliyo ipost siku ile kwenye mtandao wakijamii.


Wengi walio toa maoni katika picha ile, walikuwa ni marafiki alio soma nao sekondari, yani walikuwepo wa kidato cha kwanza mpaka cha nne, pia kulikuwa na walewakidato cha tano mpaka cha sita, usisahau wa chuo cha ufundi, na wale alioihina mtaani, kule malangali, ambao wengine walikuwa katika miji mbali mbali, wakisaka maisha, huku anaendelea kunywa bia zake, “pande zipi kaka, naona maisha umeyapatia” ilikuwa ni Comment toka kwa mtu alieitwa Emmanuel Mdem, “hooo kaka hupo nichek in box” alijibu Msoud, ambae alifurahi kwa kuona mabadoroko yake, yanaonekana kwa wenzake, maana kila alie comment, alionekana kushangazwa na mwonekano wake kwenye ile picha aliyo post, “poa kaka” alijibu Emma.


Hapo Masoud akaendelea kusoma Comment za watu wengine, na kujibu kila iliyoitaji jibu, asa zile za wanawake wake wazamani, ambao wengi wao, walitoa comment fupi fupi, “hupo kijana” mwingine angecomment “umenisusa” mwingine angekumbusha jambo, “jibu sms zangu” na vutu kama hivyo, yeye alisoma huku akijibu baadhi na nyingine akizipoezea, mpaka alipo ona sms imeingia in box ya face book, Masud akaifungua mala moja, na kuona kuwa ilikuna mtumaji alikuwa nani, 


Huyo alikuwa ni Emanuel Sanga, kijana ambae alisoma nae shule ya msingi malangari, wakaja kupisha sekondari, “kaka tupeane ramani, wenzio tunapigika tu bushi” ndivyo ilivyosomeka ile sms, kwanza Masoud akaachia tabasamu la furaha, maana akuna kitu anakipenda, kama kuona vijana wenzake wa pale kijijini, wakikosa uelekeo, ukweli ni kwamba, alitaka kuona anakuwa juu ya wenzake, ata kifika kijijini awe tofauti na wenzake, na hivi alisha fundishwa kuendesha gari, na kupanga kuwa siku ya kurui kijijini, ata enda na Toyota ist la Salma, ndio usiseme.


“Kawaida tu kaka, siuna juwa mjini hapa, atukai bule, nimejishikiza kwenye kampuni moja kubwa sana, ya feniture, inaitwa Kiguru Feniture campuny, nipo kama meneja” alijibu Masoud, akidanganya kwa mwenzie, huyo kwakujuwa kuwa awezi akafika ar na kugundua uongo wake, kabla ya kusubiri ujumbe mwingine, toka kwa Emanuel, yeye akaandika ujumbe mwingine, “vipi wewe unamishegani siku hizi?” kisha akaiuma kwa Emmanuel, na akika moja baadae jibu likaingia, akaufungua haraka sana, “kaka mimi nipo afinga nafanya kazi za ulinzi siunajuwa nilipitiaga mgambo, baada ya kumaliza shule” jibu ilo lilimfanya Masoud acheke kwa sauti kubwa sana, huku anaandika ujumbe, kwenda kwa Emanuel, “dah, pole sana, mimi nakaa Sinza, ofisi zipo Kinyelezi,  sema nini kaka, muda wowote nita timba huko bush” kisha akaituma kwa Emma, na hapo hapo akaona ujumbe ukiingia whatasapp.


Masoud akaachana na chat yake na Emma, kisha aka fungua ile sms, ilikuwa inatoka kwa Salma, akaifungua, “baby, usilale, nitakuja baadae, bado shangazi na rafiki zake, wanapigisha story nashindwa atakuondoka” nivyo ulivyosema ujumbe huo, ambao Masoud aliujibu mala moja, “dah! sindio mpaka saa saba za usiku sasa” ilikuwa ni namna ya kulalamika, aikupita ata dakika ikajibiwa, “wala usijari naona wakaribia kuagam nakuja sasa hivi mpenzi wangu” hapo Masoud akajibasamulia kidogo, huku anaanika ujumbe “poa, ila usisahau kupitia chupa kaa nne hivi, maana karibu nakaukiwa” kisha akautuma kwenda kwa mpenzi wake, ambae alijibu mala moja, “wala usijari, ata mimi mwenye nina kiu na bia mpaka najihisi homa” ujumbe huo ulimalizia na vikaragosi vya kicheko…

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu