SEHEMU YA KUMI NA MOJA
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI: Wakati hayo yanaendelea jijini Dar es salaam, huko kijijini Malangari, mambo yalikuwa tofauti kidogo, afya ya mzee Sinyagwe ilikuwa inazidi kudhoofika siku baada ya siku, mke wake akaihia kumchemshia dawa za mitishamba, ambayo aikusaidia kititu, siyo kwamba mitishamba aitibu, hapana, ila akuna aliekuwa anafahamu tatizo la mzee Shinyangwe, kilichokuwa kinafanyika ni kuhisia, au kumpatia dawa kutokana na maumivu anayo yasikia siku ile, ila kiukweli ilikuwa ni hatari kwa mzee huyo, baba wa mschana. .…. endelea….
Ilifika wakati wakampeleka kwenye dispensal, ya kijiji, ambayo licha ya kumpima vipimo vyote vidogo, ambavyo vinapatikana pale dispensal, lakini awakuona chochote, zaidi wakampatia dawa, za UTI, ambazo alianza kuzitumia mala moja, kitu ambacho uwezi amini, ni kwamba, siyo mama Masoud, au baba Masoud, yani mzee Kizinge, alie enda kumtembelea mzee Sinyangwe kama mgonjwa, akuna aliejuwa sababu.
Licha ya yote Arianna ambae, bado akuwa na simu wala mawasiliano yoyote, na mpenzi wake zaidi kudowea simu kwa mama mkwe, aliendelea kufanya kazi kwa juhudi, akitunza fedha, huku fedha chache akinunua dawa za baba yake na kugharamia matibabu, na pia kununua vifaa vya shule vya wadogo zake, pasipo kusahau kwenda kwa mama mkwe nyaati za jioni, kwaajili ya kusaidia kazi za pale nyumbani kwa wakwe zake.
Lakini wakati hayo yanaendelea, ghafla Masoud akabadirika, siyo kwamba alimweleza Anna kwamba amtaki, au alimsemea vibaya, hapana, ila ghafla Masoud akaacha kupiga simu na kuomba uongea nae, hivyo ata fedha akuomba tena, na pale Anna alipo amua kujiongeza, na kuazima simu kwa mama mkwe, iliaweze kuongea na mume wake mtarajiwa huyo, alipewa jibu ambalo lilimkosesha raha, japo aliliona lina ukweli na maana kubwa sana katika maisha yao ya baadae kati yake na Masoud, “ebu mwache mwenzio asome ujuwi kama sasa ni karibu na likizo, ni kipindi cha mitihani, utaongea nae akirudi” jibu ilo lilimfanya Anna atulie na kusubiri mpenzi wake afunge chuo na kurudi. japo ukiangalia kwa ukaribu, nikama mama Masoud, akuwa anauzingatia urafiki wa mtoto wake, na mschaa huyu nyenyekevu, na mwenye nidhamu ya hali ya juu.*******
Week ya pili toka Masoud aanze kufanya kazi pale kiwandani, tayari alikuwa amesha unga chuo, hivyo akaona nivyema kama akiendelea na kazi, kwa kuongezea kipato, na kuwa jilani na mtoto mzuri, ambae licha ya kujitamburisha kuwa ni mchumba wa mtu, lakini bado kuna dalili alizionyesha, zilizo mvutia kijana Masoud.
Mfano ukiachilia kujichekesha mala kwamala mbele ya kijana huyu, pia, kwa siku hizi ambazo alikuwa anakuja kila siku hapa kiwandani, alikuwa anampatia fedha nyingi, kuliko malipo ya elfu ishilini, aliyokuwa anapewa kwa siku moja, pia tabia ambayo aliianza ijumamosi ya leo, ya kumpeleka kwenye chakula cha mchana, huku wakiongea na kufurahi pamoja.
Katika siku zote hizo, Masoud akuwai kumwona mchumba wa Salma, ambae, licha ya kwamba uwa ajiusishi sana na kiwanda kile cha samani za majumbani, pia mchumba wake huyo ambae ni mtoto wa tajiri mzee Kiguru, tajiri mkubwa, alikuwa anasimamia biashara zake nyingine, ila kwa week kadhaa sasa alikuwa ameenda japan, kununua mashine mpya za kuzindika, na kutengeneza juice ya maembe.
Ila alivutiwa na offer alizokuwa anapewa na maschana Salma, ambae ni boss wake, ukiachialia mbali, kuambatana na Salma kwenda kwenye chakula cha mchana, pia mala kadhaa Salma amekuwa akimpatia fedha za ziada, yani pale ambapo angepewa elfu kumi na tano au ishilini, yeye angeongezewa tena ishilini au therasini zaidi, kitu ambacho kilizidi kumfanya Masoud, asifikilie kwenda likizo nyumbani kwao Malangari, huku tamaa juu ya penzi la mschana uyu, ambae ukiachilia offer ya fedha na chakula, pia alionyesha dalili za wazi zawazi za kuweka ukaribu na yeye.
Kitu ambacho Masoud akukizingatia, ni tabia ya Salma, kuwa busy na mawasiliano ya simu, kama siyo kuongea, basi ni kutumiana sms, na mtu ambae mwanzo ,asoud alizania kuwa ndie mchumba wake, ambae ndie mmiliki wa Kiguru Industry, maana maongezi yalionekana wazi kuwa ni mawasiliano ya kimapenzi, sababu maneno kama “niambie baby….. huko poa baby…. nimekumiss sana…… vipi leo tutaonana?” na ata wakati wa kukata simu ungesikia, “nakupenda sana mpenzi baby mmmhmmwaaaa!! by by” ukweli ilikuwa inapendeza sana, ilimia wivu Masoud, na kutamani kama yeye ndie angekuwa nafasi ya mwanaume wa Salma.
Lakini kitu ambacho uwezi amini, ni kwamba, baadae Masoud akaja kugundua kuwa, Salma akuwa anawasiliana na mpenzi wake ambae kwa sasa yupo Japan, ukiachilia kupanga mihadi za mala kwa mala, alizokuwa anapeana kwenye simu, pia siku moja ikiwa ni siku ya ijumaa, mida ya saa kumi saba mchana, muda ambayo wafanyakazi wa pale kiwandani, walikuwa wanajiandaa kwenda kupata chakula cha mchana, Masoud akawa anajipitisha pitisha ofisini kwa Salma, ilikuona kama anaweza upata offer ya chakula cha mchana ule, ndipo alipomwona Salma akiwa anaongea kwa simu, katika hali ya kukosa maelewano, ukiachilia mwonekano wa Salma usoni mwake, pia ata maneno yake yalionekana kuwa katikama ugomvi flani, “si ungeniambia ukweli, yani mimi najitoa kwako, alafu unakuja kunifanyia hayo unayo nifanyia” alisikika Salma akiongea kwa hasira na uchungu, niwazi alikuwa ame salitiwa katika mausiano ya kimapenzi,
Masoud ambae alikuwa amesimama karibu kabisa na mlango wa ofisi ya Salma, akiaka aonekane na pengine kukumbukwa juu ya chakula cha mchana, akaendelea kumsikia Salma akilimbana kwenye simu, “bwanaeee mimi naona yaishie hapo we endelea na huyo mtu wako” alisema Salma na kukata simu, kisha akaiweka mezani, huku anaehema haraka haraka, na mvululizo, akionnyesha kuwa amekasilishwa na jambo flani.
Hapo Masoud akajifaidisha, kwa kuchukuwa hatua ya kujikooza, kujikooza ambako kulizaa matunda, ni baada ya Salma kugeuka na kumwona kumwona Masoud, aliekuwa anamtazama huku anatabasamu, “Hooo! Masoud, kumbe hupo hapa, ebu kajiadae, kuna sehemu nataka unipeleke, sijisikii kukaa ofisini” alisema Salma, huku anakusanya vitu vyake mezani na kuviweka kwenye mkoba wake. .…. endelea….
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA MOJA: Hapo Masoud akajifaidisha, kwa kuchukuwa hatua ya kujikooza, kujikooza ambako kulizaa matunda, ni baada ya Salma kugeuka na kumwona kumwona Masoud, aliekuwa anamtazama huku anatabasamu, “Hooo! Masoud, kumbe hupo hapa, ebu kajiadae, kuna sehemu nataka unipeleke, sijisikii kukaa ofisini” alisema Salma, huku anakusanya vitu vyake mezani na kuviweka kwenye mkoba wake. .…. endelea….
Maagizo ya Salma yalimpendeza sana Masoud, ambae alijibu haraka haraka, nipo tayari” jibu ambalo lilimfanya Salma amtazame Masoud huku anatabasamu, aya tangulia pale kwenye kituo cha dara dara, nikukue hapo sitaki watu waone kama tumetoka wote” alisema Salma, japo ilishangaza kidogo, lakini Masoud ambae kuhudumiwa na wanawake kwake ni jambo la kulipa kipaumbele, pasipo kujari kuwa ni mchumba wa mtu, au ni mschana masikini, alifurahi na kuondoka mala moja, kuelekea kule alikoelekezwa, yani Kinyelezi mwisho, huku Salma akionekana kuwa katika utulivu wa hasira, kutokana na jambo lililomkuta kwa mpenzi wake.
Masoud alitembea kwa haraka, kuelekea kinyelezi mwisho, huku kichwani mwake anawaza juu ya Salma, “dah! mtoto mkali huyu, yani akikaa kwenye njia yangu nabutua sijari kama demu wa mtu wala nini” aliwaza Masoud, ambae aliumia dakika kama saba, hivi kufika kituoni, alikoelekezwa na Salma.
Pale kituoni azikupita ata dakika tatu, Masoud akaliona Toyota IST, likisimama pembeni yake, ni gari ambalo analifahamu, gari analotembelea mwana dada Salma, na pasipo kusubiri aitwe Masoud akaingia mala moja kwenye gari na safari ya kimya kimya, ikaanza kuelekea upande wa tabata Segelea, kupitia malamba mawili.
Wakiwa ndani ta gari wawili awa, hali ilikuwa tofauti kidogo na siku nyingine wanapo kuwa pamoja uwa wanaongea na kusimuliana story zao za zamani, ambazo, kwa upande wa Salma hadithi zake nyingi, uwa zimejaa simulizi za raha na furaha katika maisha yake, na kwa upande wa Masoud yeye uegemea katika kuelelezea maisha ya kwao na jinsi anavyo pendwa na wa wazazi wake na jinsi alivyo kuwa kijana wapekee kuweza kumaliza kidato cha sita pale kijiji kwao malangari.
Ila leo ilikuwa ni kimya kimya, mpaka walipo kuwa wanapandisha melemko wa kuelekea kipando cha gelezani, “Masoud tutafute sehemu tukale kwanza” Salma kwa sauti tulivu, iliyojawa kila dalili ya kutoka kwenye maudhi fu jambo baya ambalo akulitegemea, huku safari ikiwa inaendelea, “hapo umenena, maana dah! nina njaa ya kufa mtu” alisema Masoud huku akiachia tabasamu, na kumfanya Salma acheke kidogo, ikiwa dalili ya kuondokewa na hali aliyokuwa nayo mwanzo, “yani ulivyoongea utazani unanjaa ya mwaka mzima” alisema Salma, huku anajichekesha, wakati huo wanapandisha segelea gelezani.
Niwazi Salma alikuwa anajiaidi kusahau kile kilichomtokea, muda mfupi uliopita, kule ofisini, kwenye maongezi ya simu, “nina njaa kweli unazani utani Salma” alisisitiza Masoud, kwa sauti ambayo ilikuwa inaegemea kwa utani, “basi mimi nina hamu na bia, yani kuna mtu ameniudhi sana, wacha nilewe tu kisha nikalale zangu” alisema Salma, akionyesha kuanza kuzidi kuchangamka.
Maneno ya Salma yalimfurahisha sana Masoud, ambae kiukweli alijuwa kuwa kwenye pombe chochote kinaweza kutokea, asa wanapokunywa mwanamke na mwanaume, “dah! week yako itakuwa nzuri sana, unaanza na bia mida hii?” aliuliza Masoud, kwa sauti flani ambayo ilijaa sifa za kijinga, “sema week end yetu siyo yangu peke yangu” alisahihisha Salma, masahihisho ambayo yalimfanya Masoud atamani kuruka ruka kwa furaha, “utanifanya ninenepe kwa raha” alisema Masoud, na wote wakacheka kidogo.
Naam safari yao iliishia tabata bima, ambapo walisimamisha gari leo Toyota ist, kwenye maegesho ya bar moja iliyopo pembezoni mwa barabara, ambayo ilikuwa na watu wengi kiasi, ambapo waliagiza chakula, na kuanza kula, huku wakiongea ili nalile, na wakicheka na kufurahi kwa pamoja, wakati huo mala kwa mala simu ya Salma ilikuwa inaita, na yeye akawa anaitazama na lipoona jina la pigaji, akaikata na kiweka ena mezani.
Walipomalizakula wakaagiza bia na kuanza kunywa, huku maongezi yakiendelea, “hivi Masoud kwanini sijawai kusikia ukizungumzia kuhusu mpenzi wako, au ndio jongoo apandi mtungi?” aliuliza Salma, wakati flani wakiendelea kunywa bia, ambazo zilishaanza kuwakolea vichwani mwao, wote wakacheka, “mh! apandi mtungi, yani hap anime tulia tulia tu, ila ungenikuta….” alisema Masoud ambae alisia ghafla, akichelea kuropoka maneno ambayo yange mkosesha mambo mazuri ya baadae, “ningekukua wapi Masoud wewe, nimaneno ya wanaume wengi ila ukifika kitandani mambo hovyo kabisa” alisema Salma kwa sauti ya kubeza, huku anainua grass yake na kuipeleka mdomoni, “mh! nihatari Salma, sema nini achana na hayo mambo” alisema Masoud akiepusha kuaribu mambo, “sasa kwanini sijawai kumwona demu wako, ata kukusikia ukimzungumzia?” aliuliza Salma, ambae muda mwingi alikuwa anamtazama Masoud usoni, kwa macho malegevu, nazani kwaajili ya pombe alizokuwa anakunywa,
Swali ilo lilikuwa gumu kidogo, kwa Masoud ambae kiukweli, ukiachilia Arianna, akuwa na mwanamke mwingine ambae anaweza kumwita mpenzi wake, maana akuna mwanamke alie dumu nae aa kwa mwezi mmoja, lakini kutokana na wepesi wake wakufikilia, akapaa jibu la haraka, “ni sory ndefu Salma, sema kwa kifupi nimeachana nae, maana amenienda” alisema Masoud, ambae alizania kuwa ingekuwa ndiyo mwisho wa maswali, lakini alijidanganya, “ilikuwaje uka mwacha” aliuliza Salma, kwa sauti makini, iliyoushinda ulevi wake.
Nahapo ndipo Msoud akaanza kusimulia hadithi yenye ukweli, iliyogeuzwa, “nilikuwa na mpenzi wangu anaitwa Arianna, kwao ni masikini wakuupwa, yani ulikuwa marafiki toka utotoni, sasa alipomaliza form four akaferi, kwakuwa nilikuwa na nia ya kuishi nae, na ata wazazi wetu walikuwa wanafahamu ilo, na walikuwa wakiisaidia familia ya wakina Arianna, kwa chakula mavazi, ata wakiumwa walikuwa wanawapeleka hospital kwa ghalama za wazazi wangu, na wakati mimi naenda form five, Anna wakampeleka chuo cha uhuguzi pale Mafinga, walimpatia kila kitu, kuanzia fedha zamatumizi, chakula, ata mavazi, sasa alipojiona amependeza ndio akaanza kutembea na wanaume wengine, akirudi likizo, anajifanya yupo busy, ata wazazi wangu akuaka kwenda kuwasalimia, hapo nikaanza kufwatilia kwanini anafanya hivyo, nikagundua kuwa alikuwa, kule mafinga anatembea na wanaume wengi sana, ndio nikaamua kuachana nae” alimaliza usimulia Masoud kwa sauti ya kinyonge sana. .…. endelea….
SEHEMU YA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA MBILI: Anna wakampeleka chuo cha uhuguzi pale Mafinga, walimpatia kila kitu, kuanzia fedha zamatumizi, chakula, ata mavazi, sasa alipojiona amependeza ndio akaanza kutembea na wanaume wengine, akirudi likizo, anajifanya yupo busy, ata wazazi wangu akuaka kwenda kuwasalimia, hapo nikaanza kufwatilia kwanini anafanya hivyo, nikagundua kuwa alikuwa, kule mafinga anatembea na wanaume wengi sana, ndio nikaamua kuachana nae” alimaliza usimulia Masoud kwa sauti ya kinyonge sana. .…. endelea….
Hadihi hii ilimhuzunisha kidogo Salma, ungeona ata usoni, kwake jinsi alivyo shikwa na simanzi, “pole sana best” alisema Salma, na hapo ukapita ukimya mfupi, kabla Salma ajaachia tabasamu, lililoashilia kuwa kua utani unakuja, “sasa wewe ulikosea wapi, mpaka Anna, akakusaliti, au ulikuwa umfikishi?” aliuliza Salma huku anajichekesha kidogo, na Masoud nae akacheka kidogo, “ni tamaa zake, ila kama ni kumfikisha tu, yeye mwenyewe alikuwa anakubari mziki, yani nilikuwa na piga mambo mpaka akalalamika kisima kinakauka” alisema Masoud kwa sauti ya kujiamini.
Kwakusikia hivyo kulimanya Salma aache kuche ghala na kuachia tabasamu la huku macho yakizidi kumlegea, “mhhhh! unasema kweli Masoud?” aliuliza Salma, kwa sauti ambayo ilionyesha kama vile anaitaji uthibitisho, “tuachane na hayo mambo, ila kama ingekuwa inawezekana kukuthibitishia ninge fanya hivyo” alisema Msoud, huku anainua grass yake na kuipeleka mdomoni, “kwanini usiweze kunithibitishia, au unaogopa utaumbuka” Kauri hii ya Salma, ilimsisimua sana Masoud, ambae alitamani kama ingeongeewa wakiwa chumbani, kwa kuona muda unachelewa.
Naam kwa kifupi ni kweli wawili awa walienda kuthibitishiana, kwamana usiku ule walilala pamoja, huku wakinyanduana, na huo ndio ukawa mwanzo wa mausiano mapya kati ya Masoud na Salma, mapenzi ambayo yalifana kweli kweli, huku Salma akimpatia Masoud kila alicho itaji, na kuwa hakikisha anamshika mwanamke huyu mwenye fedha, Masoud alihakikisha ana mganda na kumbebisha, kitu ambao kilimfanya Salma azidi kuzama kwenye penzi la kijana Masoud, na kuambatana nae kila sehemu, huku kila siku wakilala pamoja, kwenye nyumba za wageni.
Haikuishia hapo, kwanza kabisa Masoud alighairi kabisa kwenda likizo kwao Malangari, na miezi miwili baadae, wakati chuo kikifunguliwa, Salma aliamua kumpangia Masoud chumba kimoja, kwenye nyumba moja nzuri, maeneo ya sinza karibu kabisa na mtaa ambao Salma alikuwa anaishi na shangazi yake, alifanya hivyo ili iwe lahisi kwa yewao wote kuwa pamoja na kulala pamoja, bila kutoa mashaka yoyote kwa watu wengine.
Penzi lilizidi kukolea, na wawili awa wakipendaa zaidi, Salma akamshawishi Masoud aache kazi, nae akampa ajira ya kuwa msimaizi mkuu upande wa mafundi pale kiwandani, huku akipaiwa mshahara mnono, na mkurugenzi wa kiwanda hicho, ambae ni Salma, hayo yote yalifanyika bila nyumbani kwao kufahamu.******
Naam mkasa kamili unaanzia miezi sita baadae, tuanze kijijini Malangari, usiku wa saa sita, nyumbani kwa mzee Sinyangwe, panzia chakavu la mlango wa chumba cha Arianna, ikiwa ndiyo mlango pekee, lilifunuliwa, na mama Anna akaingia ndani akiwa amevaa uapnde wa kanga, “Anna amka baba yako amezidiwa sana, amka tumpeleke hospital” aliongea mama Anna, yani mke wa mzee Sinyangwe, kwa saurti iliyojaa wasi wasi, na kuchanganyikiwa, “sawa mama waamshe wakina Tino tusaidiane” alisema Anna huku anajiinua kitandani, akuonyesha kuchangakiwa, maana anafahamu kuwa baba yake ni mgonjwa, tena mgonjwa toka siku nyingi, japo awakuweza kufahamu tatizo lake ni nini, kutoka na kukosa fedha ya kumpeleka Mafinga, kupata vipimo zaidi.*********
Sasa twende dar es salaam kwa Masoud, ambae mida hii ya saa mbili, usiku alikuwa ndani ya chumba chake, huko Sinza, akiwa amekaa juu ya kochi lake la watu wawili kochi pekee lililopo mle ndani ya chumba, huku mbele meza ndogo ya mbao ya kisasa, iliyo sheheni vyuma kadhaa vya bia, huku nyuma yake kukiwa na kitanda kimoja kikubwa, cha kisasa, hivyo vyote vikiwa ni bidhaa kutoka kwenye kampuni ya kiguru, huku nacho yake akiyaelekeza kwenye simu yake mkononi, japo TV ndogo ya nchi kumi na nne, ilikuwa inaendelea kuuguruma mbele yake, juu ya meza maalumu ya kuwekea television, mala kwa mala Masoud alibofya simu yake, kuperuzi kwenye mitanao ya kijamii, akijibu comment za marafiki zake, aliowai kusoma nao iwe chuo au kule Iringa, walio Comment kwenye picha zake, wakiwepo waschana ambao aliwai kupita nao siku za nyuma, Masoud aliyafanya hayo, huku akishushia bia zilizojaa mezani, ni wazi akuwa pake yake kwa mzigo ule wa bia, lazima kunamtu alikuwa anamtarajia, usiku ule. .…. endelea….
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Write your comment