Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Jumamosi, 8 Machi 2025

Ukimaliza Funika 19_20


 


SEHEMU YA KUMI NA TISA


ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA NANE : Naam mzee Kiguru na dereva wake wakiwa wanakaribia njia ya kuingilia nyumbani kwa kina Salma Dereva akapunguza mwendo, ili kupita kwenye bar moja kubwa ya mtaani hapo, kabla awajakata kona ya kuingia kwenye barabara ile afifu, ndipo wote wawili walipo waona wakina Salma na shangazi yake wakiwa kwenye bar ile, wanaweka chupa za bia kwenye mfuko, “Doto, hivi yule si Salma yule, anafanya nini bar usiku kama huu?” aliuliza mzee Kiguru, kwa sauti ya mshangao, huku wote wakitazama upande wa mapokezi ya ile bar, ambako alionekana Salma akiwa endelea kuweka chupa za bia kwenye mfuko, ulioshikiliwa na shangazi yake. …….…. endelea….


Kilicho mshtua na kumshangaza zaidi mzee Kiguru, ni kijigauni chepesi kama cha kulalia na kanga moja aliyoifunga kiunoni, kwa mtindo wa kata kei, na kufanya makalio yake yaonekana vyema pale alipokuwa ameinamana anaweka chupa kwenye mfuko, “lakini yupo na shangazi yake, unawasi wasi na ilo boss” aliuliza Doto, huku ambae anapunguza mwendo zaidi, kwalengo la kusimama gari, “hapana Doto, endesha gari mpaka pale mbele, nawasi na awa wawili, maana ninachojuwa nikwamba uwa awatumii kilevi chochote, sasa bia zote zile wanazipeleka wapi usiku huu, tena alkhamis, na wakijuwa kabisa kesho kazi zinaendelea” alisema mzee Kiguru, alieonyesha kuwa katika mshangao mkubwa sana, kama siyo mshtuko.


Naam Doto akafanya kama boss wake alivyo weleza, akaena kusimamisha gari mbele kidogo ya bar, yani upande ule ule, ambako kuna nyumba ya kina Salma, wakiwa wameiacha barabara ya kwenda kwa kina Salma kama mita ishilini, kisha akazima kabisa gari kabisa, “kama nihivyo boss pengine wanakuandalia wewe” alisema Doto, ambaenikama alileta utani pasipotakiwa kutaniana na boss wake huyo, ambae siyo tu kufanya nae kazi muda mrefu, ila pia walikuwa ni kama marafiki, kutokana na kufanya kazi huko kwa muda mrefu, “Doto, acha upuuzi, kwani ujuwi kuwa atuja wataarifu kama tunakuja huku kwao” alisema mzee Kiguru, kwa sauti iliyo onyesha wazi kuwa alikuwa amekasirika.


Hapo Doto, ambae anamfahamu vizuri boss wake, akiwa amekasirika, akaona itakuwa vyema akimtuliza hasira, “nikuambie kitu boss, ukiacha hasira ikutawale, utaharibu kila kitu, ni vyema kama utatulia, na kuangalia mwisho wa kila kitu” alisema Doto, na hapo Mzee Kiguru, akageuza uso wake na kumtazama Doto, “eti hen?” aliuliza mzee Kiguru, huku anashusha sauti yake, kisha akatazama kule bar, ambako sasa waliweza kuwaona Salma na shangazi yake wakitoka pale bar, na kuja uswa wao, huku Salma amebeba mfuko wawenye chupa za bia, shangazi yake akiwa ameshika chupa ya pommbe kali mkononi, pombe ambayo upendwa na watu ambao, awawezi kunywa bia au wine, wakidai kuwa aziwaleweshi haraka, “mh! kama najiona nivyoshindwa kudhibiti hasira zangu, kumbe awa watu niwalevi na washenzi namna hii?” alisema mzee Kiguru, kwa sauti iliyoonyesha wasi kasiriko lake, huku wanaendelea kuwatazama wakina Salma, “yani nikimaliza huu mzinga, usingizi huooooo, ata siangaiki” alisema shangazi huku ana isongeza ile chupa ya konyagi mdomoni wake, na kuikiss, kisha wote wanacheka, huku wanaifikia ile njia ya kuelekea kwao, ambapo lichepuka na kuelekea upande wa nyumbani kwao.


Ile wanapotea tu, mzee Kiguru alikuwa wakwanza kufungua mlango na kushuka chini, “ngoja nikawafumanie, lazima wajuwe kabisa kuwa, ninafahamu kuwa ni walevi” alisema mzee Kiguru, japo sauti ilikuwa ni yachini, lakini ilikuwa na hasira ya wazi, “mzee punguza hasira kama kama nilivyo kueleza” alisema Doto, kwa msisitizo huku anashuka haraka na kumuwai mzee Kiguru, “nisubiri nini sasa wakati tumesha waona bwana?” aliuliza mzee Kiguru, huku akionekana kutuliza hasira zake, “we subiri mpaka waingie ndani, ndio ukawagongee mlango” alisema Doto, ambae ndie mtu ambae mzee Kiguru alikuwa anamwelewa kwa haraka, “aya twende sasa” alisema Kiguru, huku anaanza kutembea, “tusipite njia hiyowatatuona, twine tupite kwenye uchochoro ule pale” alisema Doto, akionyesha uchochoro wakwaza toka kwenye ile njia.


Wakakubariana hivyo, na kupita kwenye ile chochoro, kwa haraka, mpaka mwisho wa chochoro, na kujibanza wakichungulia kule kwenye njia, ambako pia nyumba ya kina Salma aliyopangiwa na Seba, ilikuwa inaonekana, wakiwa wamewatangulia wakina Salma na shangazi yake.


Dakika chache baade Salma na shangazi yake wakaibuka na kusimama karibu na nyumba yao, waliyopangishiwa, “sasa shangazi kesho mapema basi, kama utakuwa umelala sitokuamsha” alisema Salma, akionekana kuaga kwa sangazi yake, kama vile kunasehemu anaenda, “sawa msalimie mkwe” alisema Shangazi, huku kila mmoja akishika uelekeo wake, yani wakati shangazi anaufwata mlango wa nyumba ile kubwa, ambayo Sebastiani alikuwa amewapangishia, Salma alikuwa anafwata uelekeo wa upande ule ambao wao walikuwa wamejibanza.


Hakika ilikuwa wazi kabisa, kuna sehemu anaenda kulala, “pumbavu anaenda kuto..” alisema mzee Kiguru, huku anatakakupiga hatua kujitoa mafichoni, Doto akamdaka, na kumziba mdomo, “tulia boss, utaaribu, nivyema ukijuwa anaelekea wapi kufanya nini, tukikurupuka atauzidi maarifa na hakuna atakae kuamini kuwa huyu mschana anatabia za hovyo, siunajuwa jinsi anavyo juwa kuigiza ustaarab” alishauri Doto, aliekuwa amemshikilia mzee Kiguru, kisha akamwachia mdomo, “unazani ni lahisi hivyo Doto, kushuhudia mambo ya ajabu kama aya, unazani anaenda wapi zaidi ya kwenda kufanya ufuska?” aliuliza kwa sauti ya kunong’ona mzee Kiguru, ambayo ilionyesha hasira za wazi kabisa, “ndiyo boss, lakini ata ukiona utafanyaje, unazani Seba atakuelewa na kukubariana na wewe, kuwa umemwona mchumba wake katika mazingira aya?” aliuliza Doto, huku wote macho yao yakimtazama Salma, ambae akwenda mbali sana, alisimama na kutoa simu yake, kisha akaipiga naflani, ambayo aikuchelewa kupokelewa, 


Naaam muda mfupi tu baada ya kuweka simu sikioni akasikika akiongea, “hallow baby, nimesha karibia njoo basi unipokee, mwenzio mikono imechoka” alisikika Salma akiongea kwa sauti ya kudeka, huku akiwa anaanza kutembea tena akiulenga mlango wa nyumba ya tatu tu, toka kwenye ile nyumba aliyopangiwa na mchumba wake.


Naam ilizidi kutia hasira kwa mzee Kiguru, ambae aliweza kusuhudia mlango wa ile nyumba mbayo Salma alikuwa anaisgelea ukifunguliwa, na akaibuka kijana mmoja mdogo mwenye umri wa Sebastian, mwenye mwonekano wa tabasamu, “umeniweka sana, ilibakia kidogo nilale, nilijuwa utokuja” alisema yule kijana, ambae alikuwa amevalia bukta, pasipo shati wala tishert, huku anapokea ule mfuko wenye chupa za bia, “naachaje kuja baby, iliuingize kademu kengine” alisema Salma, huku anaongoza kuingia ndani, akifwatiwa na yule kijana, aliebeba mfuko wa bia….…. endelea…. 


SEHEMU YA ISHILINI


ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA NA TISA : Naam ilizidi kutia hasira kwa mzee Kiguru, ambae aliweza kusuhudia mlango wa ile nyumba mbayo Salma alikuwa anaisgelea ukifunguliwa, na akaibuka kijana mmoja mdogo mwenye umri wa Sebastian, mwenye mwonekano wa tabasamu, “umeniweka sana, ilibakia kidogo nilale, nilijuwa utokuja” alisema yule kijana, ambae alikuwa amevalia bukta, pasipo shati wala tishert, huku anapokea ule mfuko wenye chupa za bia, “naachaje kuja baby, iliuingize kademu kengine” alisema Salma, huku anaongoza kuingia ndani, akifwatiwa na yule kijana, aliebeba mfuko wa bia….…. endelea….


Mala baada ya kuona wawili wale wamesha ingia ndani, hapo mzee Kiguru akakaanza kutembea kueleleka kwenye ule mlango wanyumba ambayo Salma alikuwa ameingia na yule kijana, ambae kwa macho yao wamemwona akiwa tumbo wazi, lakini Doto akamaka mkono, “boss eu tulia kwanza, ujiulize kabla ya kwenda kufumania” alisema Doto, aliekuwa amemzuwia boss wake, “nijiulize nini Doto, wakati tumeona kwa macho yetu?” aliuliza mzee Kiguru, japo sauti ilikuwa ya chini, lakini yenye hasira, “boss, uwezi kuona kuwa tutavuruga mambo, huyo ni mchumba wa mwanao siyo mkeo, wala siyo binti yako, akuna fumanizi la mkwe” alisema Doto, na wakati huo huo wakaonekana waschana wawili wakitokea upande wa barabarani, na kuingia mtaani.


Hapo wakina Kiguru, wakajaribu kujikausha kidogo, ni wazi awakutaka kuonekana sura zao mbele ya wanawake wale, sababu ni kwamba mzee Kiguru alikuwa maarufu sana, na mwenye kujulikana, kutokana na kuonekana mala kwamala kwenye vyombo vya habari, “mambo jamani” alisalimia mmoja wawale wanawake, huku wakiwatazama wakina mzee Kiguru kwa macho ya mashaka, “salama habari zenu” alisalimia Doto, ambae nikama alipata wazo flani, “salama tu, vipi kunamtu mnamtafuta” aliuliza yule mwanamke alie salimia, huku wote wanasimama mita kadhaa pembeni yao, “ndiyo, tunamtafuta dada mmoja anitwa Salma, anaishi mitaa hii” alisema Doto, huku Mzee Kiguru, akiwa ametulia kimya, katika, giza akificha uso wake, “hoooo! yule dada mwenye kigari kidogo, anaishi nyumba ile pale” alisema yule mwanamke, na mwenzie akadakia, “anaishi nyumba ile paleeee,  lakini mida hii sijuwi kama mtamkuta, lazima atakuwa kwenye nyumba hiyo hapo, kwa mpenzi wake” alisema huyo mwanamke mwingine, huku anaonyesha ile nyumba aliyoingia Salma na yule kijana.


Hapo Doto akamtazama kwa haraka boss wake, kuona kama ameshtuka vipi baada ya neno lile, akamwona akiwa ametulia, Doto akawatazama tena wale wanawanawake, “ni mpenzi wake muda mrefu?” aliuliza Doto, akijifanya kushangaa, “sanaaaaa, miezi sita sasa, toka alipo mchukulia chumba, atujuwi huko waliko toka” alisema mmoja kati ya wale wanawake, na mwenzie akaakia, “lakini Salma anamchumba wake tajiri, alafu handsome, sijuwi ata kwa huyu kijana amefwata, mpaka ajiingize na gharama ya kumpangishia” alisema yule mwingine, kwa sauti yenye msikiko wa lawama kwena kwa Salma.


Mzee Kiguru, ambae alikuwa amesimama gizani zaidi aliendelea kusikiliza maongezi ya Doto na wale wanawake, ambao pia uvaaji wao, aukuwa mzuri sana, “lakini uwezi ujuwa, labda yule mchumba wake kuna sehemu afiki, sasa anaona aibu kumweleza ndio maana ameamua kumweleza anae juwa michezo hiyo, maana kuna dada moja wa huko kwao tanga, alisema Salma ni hatari, siyo kama tunavyo muona sasa hivi, akuna tundu asilo tumia” alisema yule mwingine ambae kama ungemsikiliza, ungesema lile jambo wanalichukulia kimasiala.


Ukweli iliuchoma moyo wa mzee Kiguru, yani aliumia aswaaaa, ata Doto mwenye alijuwa kuwa lazima mzee Kiguru aumie maana ata yeye aliumizwa na taarifa ile, “mh! huyo kijana anaitwa nani na anafanya kazi wap..” kabla Doto aja maliza kuuliza swali lake, wale wanawake wakamuwai, “baba nyumba ile pale, kaulize mwenyewe, sisiwenyewe wageni kama wewe” alisema mmoja kati ya wale waschana, huku mwingine anadakia, “labda kama unajingine, maana mpo wawili na sisi wawili” alisema mwanamke huyo, “hapana tulitembelea Salma, lakini kwakuwa ndiyo hivyo wacha tuonoke zetu” alisema Doto, na kabla ata awajaanza kuondoka tayari wale wanawake walishaanza kuondoka zao.


Naam kwa kifupi wote wawili yani mzee Kiguru na Doto walionekana kuumizwa sana na jambo lile jipya, waliloligundua kwa Salma na shangazi yake, waliondoka pale huku wakiwa awajuwi wataanzaje kumweleza Sebastian, ambae muda wote anajuwa kuwa yupo na mwanamke mrembo mstaarabu mwenye nihamu na kujiheshimu, alie lelewa kwa maadiri mazuri na shangazi yake, “kummbe ameingia kwa wahuni ambao awafugiki ata kwa dawa” alisema mzee Kiguru wakiwa njiani wanarudi nyumbani.******


Naaam giza lilikuwa zito, baridi kari, watu sita mmoja akiwa juu ya baskeri, walionekana wakikatika kwenye vichaka na misitu mirefu ya mashamba yamiti ya mbao, sauti za ndege waendao usiku zilisikika, michakato ya wadudu wanao tambaa ilisikika kwenye nyasi kavu ndani ya vichaka vya mashamba ya miti. .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu