SEHEMU YA ISHILINI NA MOJA
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI : Naaam giza lilikuwa zito, baridi kari, watu sita mmoja akiwa juu ya baskeri, walionekana wakikatika kwenye vichaka na misitu mirefu ya mashamba yamiti ya mbao, sauti za ndege waendao usiku zilisikika, michakato ya wadudu wanao tambaa ilisikika kwenye nyasi kavu ndani ya vichaka vya mashamba ya miti. .…. endelea….
Safari ilitawaliwa na ukimya, hakuna ata mmoja kati yao alieongea, zaidi zilisikika sauti za michakato ya viatu vya mikanda miwili, yani ndala, sambamba na ming’ito ya maumivu, toka kwa yule alie kaa kwenye baskeri, ambae ni mzee Sinyangwe, huku askeri hiyo ikikokowa na vijana wawili wa mzee Mdemu, moja akiwa ameshika kiongoza baskeri, yani mshakanio, na mwingine meshika mwishoni mwa kitako hicho cha nyuma cha baskeri, akiisukuma, kuipa nguvu, ya kusonga mbele, mzee mdemu na mke wa mzee Sinyangwe na binti yao Arianna, wakifwata nyuma.
Mama Anna alikuwa anatembea, huku anawaza atapata wapi fedha za matibabu, ya mume wake, maana watu ambao aliamini kuwa wangeweza kuwasaidia, wamekataa ata kuwapeleka hospital, achana na hiyo pia wameonyesha wazi kabisa, kuto kukubariana na uchumba au urafiki wa watoto wao, ambae walimsomesha wao, kwakukodisha mashamba yao, na kufanya vibarua, utazani ni mtoto wao.
wakati mawazo hayo yakiwa kichwani kwa mama Anna, kichwani kwa Anna, mambo yalikuwa tofauti kabisa, ukweliakuwa anawaza kile kilichotokea nyumbani kwakina Masoud, yeye alikuwa anawaza namna ya kupata fedha ambazo zingemsaidia kumtibu baba yake, ambae ni lazima huko anakoelekea, angeitaji vipimo na matibabu, ambavyo kwa vyovyote lazima vingeitaji fedha nyingi.
“Sidhani kama tunaitaji kuwa na wasi wasi, bwana Sinyagwe atatibiwa na kukaa sawa, hospital za mjini, zina matibabu mazuri,” alisea mzee Mdemu, baada ya kuona kiya kimetawara kwa muda refu.
Naam! mungu alikuwa upande wao, kama ujuwavyo, mwenye haki, uwa aachiwi njiani, maana baada yakutumia lisaa limoja, wwakitembea kilomita tisa, na kubakiza kumi kumi na moja, ili waifike barabara, ndipo walipo bahatika kupata gari moja la magogo, lililokuwa linapeleka magogo Mafinga, kwenye kiwanda cha mbao.
Mama Anna mzee Mdemu na Anna, walipanda kwenye gari pamoja na mgonjwa, huku wale vijana wawili wa mzee Mdemu wakirudi kijiji kwakitumia Baskeri, “naomba muwatazame wakina Stive” aliomba mama Anna, akiwaagiza wale vijana wakati wanaagana, nao wakaahidi kufanya hivyo, na aikuwa na shaka kwa Ana, wala mama yake, maana vijana awa ni moja kati ya vijana walio lelewa katika familia yenye upendo na nihamu ya ukweli.*********
Yap! njiani wakiwa wanaelekea upanga nyumbani kwa boss Kiguru, wawili awa yani Mzee Kiguru mwenyewe na dereva wake doto, waliendesha kikao cha dharula, wakijadiri wata mwepusha vipi Sebastian, toka kwenye ndoa na mwanamke huyo tapeli, “kiukweli Doto, japo mimi ni baba, na ninaumia sana, kwa jinsi mwanangu anajidanganya, kwa kile anachozania anacho na kile alichonacho, lakini siwezi kumweleza moja kwa moja kwamba, yule mwanamke anamsaliti” alisema mzee Sinyangwe, “boss pia kumbuka, namna yoyote utakayo tumia kueleza ukweli kwa Seba, jiandae na hali atakayokuwa nayo wakati huo” alisema Doto, huku wanasimamisha gari nje ya geti la jumba kubwa la mzee Kiguru, mita chache toka parm beach.
“ilo lipowazi Doto, lakini tunatakiwa kuzuwia haraka hii ndoa, na kama ujuwavyo, usiku wakesho alkhamis, Seba anaingia hapa nchini na juwa kwa vyovyote atataka akakutane na yule mwanamke, na kesho kutwa ijumaa inafanyika ile tafrija, ya kutangaza kuanza kwa vikao vya ndoa, nakumwonyesha nyumba yao” alisema mzee Kiguru, ambae alionekana kujawa na uzuni kubwa sana, juu ya kile alicho kiona kwa macho yake.
Mzee Kiguru, akiwa mwenye uzuni akaendelea kueleza kinacho msibu moyoni, “sasa wasi wasi wangu ni kwamba, Salma na shangazi yake wakisha juwa kuwa tayari Seba amesha rudi, watazidi kuficha uovu wao, ili waendelee kumdanganya Seba” alisema mzee Kiguru, ambae ni wazi alikuwa amekosa amani kabisa, “boss usiwe na wasi wasi, tuta fanya jambo, tumtafute mtu ambae ata weza kuchunguza mienendo ya Salma na hawara yake, na tukisha juwa ratiba zake, tuhakikisha Seba anawakuta sehemu ambayo itamfanya agundue kila kitu, hii itakuwa nikama surprise yako kwake” alisema Doto, akionyesha kuwa na uhakika na kile anachokisema
SEHEMU YA ISHILINI NA MBILI
Naam! sasa upo mafinga mjini, kwenye lango la hospital ya wilaya ya maufundi, ilikuwa ni saa saba za usiku, ni msaa manne yalisha pita, toka kijana Emmanuel amalize kuchat na kijana mwenzie, alie somanae kule malangari, kijana ambae kiukweli anafahamu fika kusoma kwake, na kukuwa kwake, kijana ambae maendeleo na mafanikio yake yalimpa msukumo wa yeye kuongeza juhudikatika kazi yake ya ulinzi, ili afanikiwe katika maisha.
Ukweli licha ya kutamani mafanikio, lakini aliweza kuona wazi ugumu wa kazi yake hii ya ulinzi, kiuhalisia mafinga hakuna mbu kabisa, ila sasa baridi, yani licha ya kuvaa koti kubwa, na kuwasha moto,, lakini akiota moto mbele, mgongoni anasikia baridi, “nitafute nauri niende dar nikapate kazi ya maana, lakini sinipe kazi ya ulinzi, maana nasikia kuna mbu sana huko” aliwaza Emmanule huku anageuka kutazam upande wa getini, ambako, kulisikika ngurumo ya gari kubwa la mizigo.
Mwanzo alizani linapita, lakini alishangaa baadae akaliona gari lile linazidi kusogelea lango la hospital, na kusimama kwa mtindo wa kwamba, halikuwa na mpango wa kuingia ndani, baada yake Emanuel akanawaona watu wanashushwa toka kwenye gari lile, wengine mbele wengine nyuma kwenye mbao, walioshuka toka mbele ya gari ilo, walishuka na mgonjwa, aliekuwa analalamikia maumivu, hii ni kawaida kwa sehemu hii kujiwa na wagonjwa mida kama hii, ila na pengine zaidi ya mida kama hii.
Naam baada ya kushuka toka kwenye gari, wale watu waatu na mgonjwa wao, wakaanza kuingia ndani ya lango la hospital, na ata wale watu wakati wakatiza mbele yake, nae akajikuta anainuka kwa haraka, “Anna, mzee Mdemu, mama Anna, mmemleta nnani usiku usku huu” aliuliza Emanuel, ambae alishangaa sana kuwaona watu toka kijijini kwo malangari, japo ilikuwa inatokea mala kwa mala , kwa yeye kukutana na watu toka kijijini kwao.
“tumemleta mzee Sinyangwe, ameziwa ghafla usiku huu, anajiskia maumivu makali ya tumbo” alisema mzee Mdemu, na hapo bila kuuliza malambili, akasogea na kumweka mzee Sinyangwe mgongoni, kisha akaanza kutembea kwa haraka kuelekea kwenye jengo la dharalu, huku nyuma yake wakina Anna wakimfwata kwa haraka.
Baada ya kumfikisha mapokezi, na kumkabidhi kwa mganga aliekuwepo huku akisisitiza kuwa ni mzee wake toka kijijini kwao, kisha yeye akarudi kwenye sehemu yake ya kazi, huku akitoa ahadi ya kuja kuwaona asubuhi kabla ajaenda kupuzika, maana atakuwa amemaliza zamu yake ya usiku.
Mgonjwa alipokelewa vyema kabisa, na kuanza kupewa huduma, ikiwa ni pamoja na kupewa dawa za kutuliza maumivu, kisha kupelekwa kwenye ward ya wanaume, ambako angepumzika mpaka asubuhi, ambapo angeandikiwa vipimo.********
Siku iliyofuata siku ya alkhamis, Mzee Kiguru aliamka mapema sana, na kumpigia Dereva wake, yani Doto, kwamba amfwate pale nyumbani, tofauti na siku zote ambapo Doto ndie uwa wa kwanza, kufika nyumbani hapa, na pengine umkuta boss wake bado amelala, baba Seba, mbona le mapema sana, au nio maandalizi ya kumpokea mwanao?” aliuliza mke wa mzee Kiguru, ambae bado alikuwa kitandani, “mama seba ebu nipe mapumziko ya kichwa kidogo, yani sipo sawa kabisaaaa” alisema mzee Kiguru, ambae tayari alikuwa amesha maliza kujiandaa, huku anafungua mlango wa chumba na kuelekea sebuleni, akiacha mke wake anaachia mguno wa mshangao, “ndio maana leo ujalala usiku kucha” alisema mama Seba, kwa sauti ya chini, huku anajiinua toka kitandani. akiwa amevalia gauni la kulalia, na kumfwata mume wake sebuleni, ambako alimkuta mume wake amesimama mbele ya dirisha, la upande wa getini, amekunja nne ya mikono kifuani kwake.
“Mume wangu mbona sikuelewi, jana umechelewa kurudi, alafu unaonekana unamawazo mengi, leo unawai kuamka, utaki kuongea lolote, kuna nini lakini, au kuna jambo lime mkua Seba?” aliuliza mama Seba kwa sauti ya kutilia mashaka, “limpate lipi wakati jana tumeongea nae, nivyema kama ukiwa mpole mpaka nipate jibu kwanza, ndipo niakueleza kila kitu” alisema mzee Kiguru, ambae kiukweli toka arudi jana usiku, alilala kimang’amu ng’amu, kwa hiyo unazani nitakaa kwa amani kwa hayo maneno yako, yani bora unieleze tu, kama kukushauri unikushauri tu” alisema mama Seba, akionekana wazi kuwa, atokaa atulie mpaka ajuwe kinacho msibu mume wake, “mbona ujasema kama kuchanganyikiwa tuchanganyikiwe wote?” aliuliza mzee Kiguru, na kuzidi kumshtua mke wake, “baba seba, ujuwe kunamuda wa utani, lakini siyo hii alfajili?” aliuliza mama Seba, kwa sauti ya juu kidogo, akionyesha wazi mshtuko wake, “nimekuambia mama Seba, ebu wewe ubakie wa akiba, wacha kwanza tuchanganyikiwe sisi, wewe ndio wa kututuliza” alisema mzee Kiguru, wakati huo huo wakasikia honi yagari toka nje ya geti, na kwa macho yao wakapata kumwona mlinzi anafungua geti. .…. endelea….
SEHEMU YA ISHILINI NA TATU
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA MBILI : “mbona ujasema kama kuchanganyikiwa tuchanganyikiwe wote?” aliuliza mzee Kiguru, na kuzidi kumshtua mke wake, “baba seba, ujuwe kunamuda wa utani, lakini siyo hii alfajili?” aliuliza mama Seba, kwa sauti ya juu kidogo, akionyesha wazi mshtuko wake, “nimekuambia mama Seba, ebu wewe ubakie wa akiba, wacha kwanza tuchanganyikiwe sisi, wewe ndio wa kututuliza” alisema mzee Kiguru, wakati huo huo wakasikia honi yagari toka nje ya geti, na kwa macho yao wakapata kumwona mlinzi anafungua geti. .…. endelea….
“ebu ona, sasa unazani nitakuacha uondoke kabla ujanieleza lolote?” alisema mama Seba, kwa sauti yenye msisitizo, “ok! kwakifupi ni kwamba, Seba ameuziwa chumvi kwenye mfuko wa sukari” alisema mzee Kiguru, huku anaanza kutembea kuufwata lango, maana ata gari lilionekana linaingia ndani ya geti, “unamaana gani, unataka kusema Seba ametapeliwa huko aliko?” aliuliza mama Seba, huku anamfwa mume wake, aliekuwa amesha ufikia lango, na sasa alikuwa anakolokocha funguo, ilikuufunguwa, “tena ametapaliwa na tapeli alie jitapelisha” alisema mzee Kiguru, kwa sauti iliyojaa hasira ya ghafla, “kivipi mume wangu mbona unanitisha, si usimulie tu, kama kuchanga nyikiwa tuchanganyikiwe wote” alisema mama Seba, huku anamshika mkono mume wake.
Hapo mzee Kiguru, akasimama na kumtazama mke wake, kisha akaua pumzi ndefu, na kushusha kwa nguvu, alafu kwa sauti tulivu kabisa akamweleza mke wake “mama Seba, sijuwi kaa utaamini nitakacho kueleza, Seba ame pewa shubiri kwenye chupa ya asari, yule mchumba wake ni kahaba” hapo mama Seba, akacheka kidogo, huku anauachia mkono wa mume wake, “unaona sasa, yani unaleta utani, ili niache kukuuliza, wakati nakuona kabisa jinsi ulivyo jawa na mawazo” alisema mama Sebastian, huku anamtazama mume wake usoni, akamwona jinsi alivyo nyongea, “eu we mzee, siuniambie kama unanitania” alisema mama Seba kwa sauti ya juu kidogo, huku anamtazama mume wake, ambae alionyesha wazi kuuzunishwa na jambo alilolisema, “mume wangu, ebu nieleze vizuri nini kimetokea, yani umejuwaje juu ya ilo?” aliuliza mama Seba, kwa sauti yenyekutetemeka, ambayo iliaonyesha kuwa mama huyo akutaka kuamini anachomaanisha mume wake.
Na hapo mzee Kiguru akaamua kumweleza jinsi ilivyouwa, jana usiku kule nyumbani kwa kina Salma, “Kama nilivyo kueleza mama Seba, yule mwanamke na shangazi yake ni makahaba wakubwa” alisema mzee Kiguru, ambae pia alimweleza mke wake mpango wake, na kumwomba mke wake awe mtulivu, ili yeye afanye utaratibu na mtego ambao utamwezesha Sebastian yeye mwenyewe kujionea kile ambacho Salma anakifanya, kitu ambacho kita mfanya Sebastian mwenyewe ajuwe uharisia wa mwanamke ambae anataka kumfanya kuwa mchumba wake.
Naam walikubariana hivyo, huku mama Seba akisisitiza kuwa jambo ilo lisichelewe, kiasi cha Seba kuendelea kuwa na mwanamke yule, japo ata kwa bahati mbaya moja, mala tu atakaporudi toka Japan.********
Saa nne asubuhi, huko Mafinga, pale hospital, kijana Emmanuel alikuwa tayari amesha kabizi lindo lake kwa mlinzi mwingine, ambae pia alikuwa amechelewa kulipoti kazini, na baada ya hapo Emmanuel alienda moja kwa moja kwenye ward, ambayo mzee Sinyangwe alikuwa amelazwa, ambako akumkuta mgonjwa wala wakina Anna, hivyo akaanza kutafuta kwenye vyumba vya vipimo.
Emmanuel, alitembea kwenye makolido ya hospital, huku kichwani mwake akijaribu kutafakari, jinsi alivyo iona hali ya Arina na mama yake, akilinganisha na mwonekano wa sasa wa mchumba wa mschana Ana, yani kijana Masoud, ambae yupo Dar kwa sasa, hivi kwanini mpaka sasa ajamchukuwa Anna akaishi nae huko dar?” alijiuliza Emma wakati anaendelea kutembea kwenye kolido, na kabla ajapata jibu la swali lake, akakutana na wakina Ana wakiwa na mzee Mdemu, wamesimama nje ya chumba cha doctor wa magonjwa ya ndani, wakionekana kujadiri jambo flani, lenye kuumiza kichwa, “lakini atakama tukienda kijijini nani ata tusaidia hiyo lakisita” aliuliza mama Anna, kwa sauti yenye masikitiko makubwa, ilionekana kuwa kuna kiasi flani cha fesha kinaitajika kwaajili ya matibabu, “siyo tatizo, kuna wale wakulima wana wakutoka Iringa wanakodi mashamba kwa bei nzuri sana,, unaweza kupata ata mbili tatu kwa mashabayako machache” alisema mzee Mdemu, na hapo mama Anna akatazama chini, “baba we, tulisha kodisha muda mrefu, yani huu ndio msimu wamwisho” alijibu mama Anna, akionekana kusikitishwa na jibu alilolitoa, aana alikumbuka kuwa feza za kodi ya shamba, alikuwa ameipeleka kwenye ada na matumizi ya Masoud, mtoto wa mzee Kisinge, ambae alitarajia, angekuwa mkwe wake, ambae angebadirisha maisha yao kwa ujumla, “imekuwaje jamani, mgonjwa amesha tibiwa?” aliuliza Emmanuel mala baada ya kuwafikia. .…. endelea….
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Write your comment