Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Jumamosi, 8 Machi 2025

Ukimaliza Funika 30_31


 


SEHEMU YA THERASINI


ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA TISA: “sikia Mdemu mme msumbua bule Anna, na tena uenda akakutana na kitu amacho kitamuumiza huko Dar” alisema mzee Mwaisaka, pia akawaeleza wakina mzee Mdemu, na mama Anna, kilicho tokea kijijini kati yao na mzee Kizinge, “mke wa bwana Kizinge ametueleza wazi kabisa, kuwa muda wowote Masou atarudi kijijini akiwa na mwana gari lake, na msije kusema kuwa anamchumba” alieleza Mwaisaka, huku mzee Sanga, akisisitiza kwa kueleza kile kilichosema na mzee Kizinge na mke wake. ….…. endelea….


Mpaka hapo tayari macho na masikio ya mama Anna na zee Mdemu yalikuwa yamefunguka, na kuona kuwa jambo linalofaa ni kwamba kumzuwia Anna asiende  Dar es salaam, “jamani naomba muwai stendi mkamzuwie Anna asiende huko…” alisema mama Anna kwa sauti ya kuombeleza, lakini akuwai kumaliza kauri yake, “tayari Anna ameshaondoka, amepata lift kwenye gari viazi toka Njombe, na sasa watakuwa wamepita Matanana” wote waligeuka kutazama kule ilikotokea sauti.


Wote kwa pamoja walimwona kijana Emmanuel, alikuwa amesha wafikia, “anabahati sana, wamemoza elfu tano tu, wamesema pia wata mwelekeza sehemu ya kupandia daradara za kweuendea huko kinyenyelezi, ambako Masoud anafanyia kazi” alisema Emma akizidi kuwachanganya hakiri wazee wale, aswa mama yake Anna.


Hapo kilipita kimya kifupi kidogo, wote wakionekana kuwa na sura zilizo jaa simanzi, “jamani kuna nini tena au…?” aliuliza Emanuel, ambae kwa haraka alizania kuwa, mzee Sinyangwe, tayari ameaga dunia, “jamani tusahau kuhusu Anna, akiyakuta ya huko, atarudi mwenyewe, na bahati nzuri anasimu, cha msingi tuangalie tunapata wapi fedha za matibabu” alisema mzee Mdemu, na wote wakaunga mkono hoja hiyo, kasoro mama Anna ambae alionekana kukosa amani kwa jambo lile.*******


Naaam masaa yalisonga, pilika zikiendelea kila kona, maana wakati Salma akiendelea kuponda raha na mpenzi wake Masoud, huku akijuwa fika kuwa, anamchumba wake, ambae amempatia maisha mazuri aliyo nayo, mzee Kiguru alikuwa anaandaa mpango ambao utamfanya Sebastian kugundua kuwa Salma akuwa mwanamke sahihi kwake, maana kuna ugumu wake kumweleza mtu kuwa, mwanamke anaemwamini na ambae alisha mgaramia vitu vingi, kuwa siyo mwanamke sahihi.


Mafinga wakina mzee Mwaisaka walikuwa wanaumiza kichwa na mna ya kupata laki nane, za matibabu ya mwanakijiji mwenzao, mzee Sinyangwe, ambae sasa alikuwa ndani ya chumba cha kupumzikia, akiishi kwa dawa za kutuliza maumivu, dawa ambazo kwa maelezo ya wauguzi, ni kwamba, zingefika ukomo wa matumizi, kwa kuacha kufanya kazi kwenye mwili wa mgonjwa, ata kama angezidisha dose.


Lakini licha ya mipango yote, walikuwa na shilingi laki moja na elfu albaini tu, ni baada ya wakina mzee mwaisaka kuongeza laki moja, fedha ambayo aikuweza kuwashawishi wauguzi na madaktari, kuingia katika chumba cha upasuaji.


Mpaka saa nne gari la mizigo lililobeba magunia ya viazi, ndio kwanza lilikuwa lina iacha mizani ya Mikumi, kuelekea upande wa Morogoro, safari ilikuwa nzuri kwa Anna, ambae ukiachilia mbali, kuwa hii ndiyo safari yake yakwanza ya mbali, ambapo aliweza kujionea kwa macho yake uzuri mazingira ya nchi yake.


Pia mschana huyo wenye uzuri uliofichika, alikuwa amefurahika moyoni mwake, kwa kujuwa anaena kukutana na mpenzi wake, ambae sasa ametimiza ndoto zake, za kumaliza chuo kikuu kama alivyo amini yeye Anna, na kupata kazi nzuri, kama ambavyo Masoud alimweleza Emmanuel, “baba akishapona na kurudi kijijini, basi nitarudi kuja ishi darn a wazazi wangu” aliwaza Anna aliekaa kwenye cabin, nyuma ya seat ya dereva wa gari ili aina mitsubish fuso, tayari alisha pata chakula cha mchana pale luaha Mbuyuni, mkononi alikuwa amebakiwa na shilingi elfu saba na mia tano, baada ya kulipia gharama ya usafiri na chakula, akujaribu ata kufumba macho yake kusinzia kidogo, maana kutaka kupitwa na chochote, iliakasimulie vizuri siku akirudi kijijini Malangari.********


Ukiachana na hao, wende maeneo ya uwanja wa ndege, wa kimaitaifa wa Mwalimu Julius Nyelele, ambako sasa liweza kuishuhudia ndege kubwa ya kampuny ya usairishani ya Ethiopian airline, ikiwa inagusa ardhi ya Tanzania, na kuseleleka kwenye barabara yake, huku akipunguza mwendo kadiri ilivyosogea, mpaka ilipoenda kusimama usawa wa eneo la kushukia abiria.


Dakika chache baadae abiria wakaanza kushuka, toka kwenye ndege, na kuelekea sehemu ya ukaguzi na nakisha kuelekea kwenye mlango wa kutokea, ambako kulikuwa watu wengi sana, ambao walikuwa wanawasubiria waheni wao.


Miongoni mwaabiria hao alikuwepo kijana mmoja mtanashati, mwenye umbo pana kidogo, mrefu kiasi, na uso wa tabasamu, alie valia suruali ya kitambaa, rangi ya silva, na shati jekundu, huku kosi la suit rangi ya silva, kikiwa kwenye mkono wake wa kushoto, wakati mkono wa kulia, akiwa ameshikilia sanduku dogo, la rangi ya silva, yani brifcace. ….…. endelea…. 



SEHEMU YA THERASINI NA MOJA


ILIPOISHIA SEHEMU YA THERASINI: Miongoni mwaabiria hao alikuwepo kijana mmoja mtanashati, mwenye umbo pana kidogo, mrefu kiasi, na uso wa tabasamu, alie valia suruali ya kitamaa, rangi ya silva, na shati jekundu, huku kosi la suit rangi ya silva, kikiwa kwenye mkono wake wa kushoto, wakati mkono wa kulia, akiwa ameshikilia sanduku dogo, la rangi ya silva, yani brifcace. ….…. endelea….


Yap! akiwa anategemea kabisa kuwa lazima baba yake atakuwa anamsubiri pale airport, alienda moja kwa moja mpaka kwenyekundi la wasubiriaji, ambako alimkuta baba yake, ambae leo ilikuwa tofauti kidogo, maana akuwa peke yake, ila alikuwa na dereva wake Doto, ambae siku zote ambazo baba yake mzee Kiguru, anapomfwata airport, umwacha nje kwenye gari, “imekuwaje leo, au leo alizani nitakuwa na mizigo mingi” alijiuliza Sebastian, uk anatembea kuwafwata baba na dereva wake, waliokuwa wamesimama kwa ukaribu, huku wakinong’ona jambo.


Sebastian akujari kule kunong’ona, maana anatambua wazi ukaribu wa muda mrefu wa mzee Kiguru na Dereva wake, ila kilicho mshtua ni tabasamu la bandia la baba yake, ambalo aliligunduwa mala baada ya kuwafikia, “karibu Tanzania Seba” alisema mzee Kiguru, huku anajaribu kuendelea kutabasamu, “asante baba shikamoo” alisalimia Aebasiani kwa awamu, akiwasalimia baba yake na bwana Doto, ambae umri wake umepishana kidogo sana na mzee kiguru, kisha wakaanza safari ya kutoka nje ya jengo lile.


“mambo yanaenda sawa kabisa, kila kitu kipo vizuri kwaajili ya tafrija yako na mchumba wako” alisema mzee Kiguru, akijitaidi kuondoa hasira na chuki iliyopo moyoni mwake, juu ya Salma, “lakini baba uonekani kuwa unacho kisema kipo sawa, vipi kuna tatizo huko nyumbani?” aliuliza Sebastian, huku wakiwa njiani wanaelekea nyumbani.


Ilimshtua kidogo mzee Kiguru, ambae akuitaji kijana wake, agundue mapema kuhusu tabia za mchumba wake, na shangazi yake, hapo mzee Kiguru akapata kigugumizi kidogo, na kujikuta akikosa jibu, “Seba, umeona boss amepoa kidogo, ni sababu ya uchovu mwingi, maana jana tulipotoka kupokea gari lako, moja kwa moja tukaanza kukuandalia surprise yanguvu” alisema Doto, na hapo nikama Doto alimpa mzee Kiguru, nafasi ya kuweka sawa mambo, “hivyo usikutane na Salma kabla mpaka tutakapo kuambia, tumeelewana Seba?” aliuliza mzee Kiguru, kwa sauti yenye msisitizo, “kwani Salma analijuwa ilo?” aliuliza Sebastian, kwa sauti iliyojaa shahuku, “ni surprise kwa nyie wote, na yeye pia ajuwi, atujamweleza yeye wala shangazi yake, hivyo utafwata kile utachoelezwa na Doto” alisema mzee Kiguru akisisitiza mala kwa mala.*****


Naam!!! siku iliyofwata ilikuwa ni ijumaa, huko Mafinga, wakina mzee Mwaisaka  ambao bado walikuwepo pale mjini, wakijibanza kwenye chumba cha kijana Emanuel, pamoja na mzee Mdemu, wakimwacha mama Anna, kule Hospital, ambae waliungana nae baadae, huku wakiwa awaja pata fedha yoyote, ya kumsaidia mzee Sinyangwe, ndio maana wakapanga leo hii mapema walijihimu kwa mganga mkuu wa hospital hii, kwaajili ya kuogea nae, kuhusu huduma ya matibabu kwa wazee wasio jiweza, japo mzee Sinyangwe akuwa amefikisha umri wa miaka sitini, ndio kwanza alikuwa na miaka alobaini na tisa, na mpaka mida hii bado walikuwa wamesimama nje ya ofisi ya mganga mkuu, wanasubiri amalize kikao, ili waingie wakaongee nae.


Siku hiyo hiyo ya ijumaa, ndiyo siku ambayo, ilipangwa kuwa na tafrija ya kushtukiza, ambayo itafanyika kwenye nyumba mpya ya Sebastian, siku ambayo ilikuwa na pilika nyingi sana, upande wa familia ya bwana Kiguru.


Maana ukiachilia mbali, Sebastian aliekuwa amekaa mbele ya meza yake kubwa, kwenye chumba maalumu, pale nyumbani kwao, ambacho utumika kama ofisi, akiwa anakagua baadhi ya nyaraka au karatasi zinazo elezea taarifa za baadhi ya biashara zake, hiyo ni baada ya kushindwa kuwenda kwenye baadhi ya miradi yake, ikiwa ni baada ya kuzuiliwa kutoka, kwaajili ya hiyo surprise, ambayo baba yake alidai ameiandaa kwaajili yake.


Huko ndani baba na mama yake walikuwa makini wakisiuiria simu, ilikupewa taarifa ya surprise, kama ingekuwa tayari, ili wamjulishe Sebastian aende eneo ambalo ilipangwa hiyo surprise,  “unazani hiyo itasaidia baba Seba, tusije kumuuwa mtoto kwa pressure?” aliuliza mama Sebastian ambae kiu yake kubwa ilikuwa nikuhakikisha kijana wake anaachana na Salma, hali hiyo ilikuwa imeongezeka zaidi baada ya kuzina zile video fupi fipi kwenye simu ya mumewe, zinazoonyesha mahaba niue ya mkwe wao Salma, na kijana ambae anaonekana wazi kuwa ni muajiliwa kwenye kiwanda cha kijana wao, “Seba bado kijana, awezi kudhurika kwa jambo ili, ila itabidi tumwache kwa muda flani, atulie akili yake, mala tu atakapo jionea ukweli kwa macho yake.*********


Siku hii ya ijumaa ilikuwa ni sikunzuri kwa wapenda nao wawili yani Masoud na Salma, ambao licha ya kujuwa kuwa wanacho kifanya ni uthaliti kwa Sebastian, ukiachilia kwa upande wa Masoud yeye alisha kataa kuwa na mpenzi, na kwamba alisha achana nae, kwamadai kuwa alimsomesha na mwisho kumthaliti, ila nao ulikuwa ni uthaliri mkubwa sana, pengine kuliko ule wa Salma kwa Sebastian, ambao kama Seba angekuwa amezijuwa mapema tabia harisi za Salma, achilia kugusa kitumbua chake kwa mwiko wake, hakika asinge thubutu ata kumsogelea, au kumwajili. ….…. Itaendelea…

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu