SEHEMU YA ISHILINI NA NANE
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA SABA: Huku mama Anna akiwa anaumia rohoni kwa kuona kuwa, licha ya yote ambayo binti yake na familia yake, wamemfanyia Masoud, lakini yeye na familia yake, anawezaje kuficha, juu ya maisha yake mapya ya mafanikio, huku wao wakiishi katika hali ngumu ya ufukara, wakishindwa ata kukodisha mashamba yao, ambayo walisha ya kodisha hapo mapema, kwaajili ya kulipia gharama za masomo za kijana huyo, hakika mama Anna aliona wazi jinsi binti yake alivyo achwa kwenye mataa na kijana huyo mhuni asie na huruma wala mapenzi ya kweli kwa binti yake Ariana. ….…. endelea….
Ilikuwa hivyo kwa mzee Mdemu, ambae siyo tu alimwonea huruma Arianna peke yake, pia alimwonea huruma mama Anna, mzee Sinyangwe, kwa kupoteza nguvu zao na muda wao, kumsaidia Masoud, ambae ni wazi akuwa na mpango wowote na Arianna, siyo kwamba walimsikia akisema hivyo, au mefanya hivyo, ila dalili zilisha onyesha, ikianzia dalili ya kukatika kwa mawasiliano ghafla, pia ata mwonekano tofauti kati ya Masoud mwenyewe na mschana huyu, aliepo mbele yao, ndio maana amefikia hatua ya kuto mshirikisha katika mafanikio yake, katika maisha.
Wakati wengine wakiwaza hayo, ilikuwa tofauti kwa Ariana, ambae lionekana kuachia tabasamu pana, lenye kuonyesha furaha ya wazi iliyopo moyoni mwake, kiasi cha kuwashangaza wenzake, “mama natakiwa kwenda Dar, nikachukue ela kwa Masoud, ili tumtibu baba” alisema Anna, kwa sauti iliyojaa uraha na maumaini, ya mafanikio, mfano wa mfungwa alie maliza kifungo, “we Anna, una akili kweli, yani mtu amekukatia simu bado unataka kwenda dar kumtafuta, utaanzia wapi, unaijuwa dar wewe?” aliuliza kwa ukali mama Anna, akionekana amekasirishwa na hakiri mbovu ya binti yake.
“hapana mama usisema hivyo, Masoud ajanikatia simu, siumesikia kuwa anakazi nyingi” alisema Anna akionekana mwenye uhakika wakile alichokisema, “kwa nini mpaka leo ajakueleza chochote, wala kuja kijijini kukuchukuwa, wakati amesha maliza chuo na kupata kazi?” aliuliza mama Anna, huku Emma na mzee Mdemu, wakiwasikiliza kwa umakini, na kutamani kusikia jibu la Anna, “tulipanga hivyo mama, kwamba Masoud akimaliza chuo, atakaa kwanza huko akiandaa maisha yetu, ndipo aje kutuchukuwa” alisema Anna akionekana kuwa na uhakika mkubwa na mpenzi wake Masoud.
Ujibuji wa Anna, nikama ulianza kuwapa moyo Emma na Mzee Mdemu, ambao walikubariana kwa vichwa kuwa Anna yupo sahihi kwenda dar, “sihani kama ni wazo zuri mwanangu, Dar kubwa sana, kuna watu wanapoteaga huko” alisema mama Ana, akionyesha wazi kuwa akukubariana na binti yake, safari Emma ndie alie jibu, “Masoud anielekeza sehemu ya kumpata, ni kazini kwake, Anna awezi kupotea maana ni jina la mtaa kilipo kiwanda maarufu sana, isioshe kesho siku ya mwisho kufanya kazi, vinginevyo mpaka jumatatu, ndio mzee atapata matibabu, ni vyema ukimwachia aende akatafute ela tu” alisema Emma, ambae aliona kama vile Anna anauhakika na kile anacho kisema.
Naam baada ya mjadara mfupi, ikaonekana kuwa Anna alikuwa sahihi, kwamba nivyema akienda dar, kukutana na mwanaume ambae ni chumba wake, akamsaidie fedha za matibabu ya mzee Sinyangwe, “aya sasa nauri utaipatia wapi?” aliuliza mama yake Anna, ambae nikama bado akukubariana nao toka moyoni, bado mapema tutavizia magari makubwa yanayotoka zambia, au Kongo, anaweza kusafiri kwa bei nafuu, au tukiwaeleza shida yetu, anaweza kusafiri bule mpaka Dar, wengi ufanya hivyo” alisema Emmanuel, na Anna akadakia, “nita kuachia hii yote, nita bjia na elfu kumi, kwaajili ya njiani, najuwa nauri ya kurudia Masoud atanipatia” alisema hivyo Anna, akionyesha kuwa mwenye furaha kubwa, huku anatoa noti nne za elfu kumi kumi, na kubakia na moja mkononi mwake.
Mzee Mdemu aliekuwa amtulia kwa muda mrefu nae akatoa noti tatu za fedha, moja ikiwa ni mefu kumi, na mbili zikiwa elfu tano tano, akachambua ile moja ya elfu kumi, kumpatia mama Anna, hii ongezea kwenye hiyo ela ya matibabu, nahii moja nikuongezee Anna, katika safari yako” alisema mzee Mdemu, akimaliza kwa kumpatia Anna noti ya elfu tano, “asante sana” alisema Anna akipokea ile noti ya elfu tano, sambamba na kupiga nusu goti, “mungu akutangulie katika safari yako mwanangu” alisma mzee Mdemu, kwa sauti flani iliyopoa, nikama akuwa na uhakika wa mafanikio katika safari ya Anna, “Asante baba” alisema Anna, na wakati huo huo mama Anna nae akawa amekumbuka jambo, “mwanangu, mungu akutangulie, safari yako iwe ya mafanikio” alisema mama Anna, akitoa baraka zake kwa binti yake.
Labda nikujuze kidogo msomaji wangu, hizi baraka ni nzuri na muhimu sana, siyo tu zitoke kwa wazazi, ata kwa mtu yoyote yule, mladi zitokee moyoni, ni jambo jema sana, omba baraka pokea braka toa baraka siku zote, kwani atoa kwa jema, ulipwa zaidi kwa jema, “asante mama, naamini tutafanikiwa” alisema Anna, huku akipiga nusu goti mbele ya mama yake, kisha akainuka na kuanza kundoka akiongozana na kijana Emma, ambae siyo kwamba akutoa fedha, kwaajili ya kwamba ni mchoyo, ila tu kwa kuwa hakuwa nazo kabisa, na pengine alitamani kumweleza Anna, ampunguzie ile aliyokuwa nayo, ili aweze kujipatia chai asubuhi ile, “mzee Mdemu nakuja kukuchukuwa ili ukapige swaki nyumbani kwani, ngoja nimpeke Anna akapande gari” alisema Emma, wakati wanaondoka.******
Naam!!!! saa sita mchana, maeneo ya kinyelezi mwisho, mita hamsini toka kwenye kiwanda maarufu cha kutengeneza thamani za majumbani, yani feniture, cha Kiguru Feniture Campany, pembezoni mwa safu ya maduka yaliyopo pembeni ya barabara iendayo mbezi mwisho, maafuru kama barabara ya malamba mawili, lilionekana gari aina ya Toyota landcruize V8, likiwa limesimama huku badolina unguruma, kwamaana hiyo gari alikuwa lime zimwa. ….….
SEHEMU YA ISHILINI NA TISA
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA NANE: Naam!!!! saa sita mchana, maeneo ya kinyelezi mwisho, mita hamsini toka kwenye kiwanda maarufu cha kutengeneza thamani za majumbani, yani feniture, cha Kiguru Feniture Campany, pembezoni mwa safu ya maduka yaliyopo pembeni ya barabara iendayo mbezi mwisho, maafuru kama barabara ya malamba mawili, lilionekana gari aina ya Toyota landcruize V8, likiwa limesimama huku badolina unguruma, kwamaana hiyo gari alikuwa lime zimwa. ….…. endelea….
Ndani ya gari ilo la gharama kubwa, kulikuwa na watu wawili, ambao ni mzee Kiguru, baba wa mmiliki wa kiwanda cha Kiguru Faniture, pamoja na Dereva wake, mwenye jina la Pacha mdogo, yani Doto, waliotuliza macho yao kwenye njia inayotokea upande wa kiwandani, kiyoyozi kikiwanyunyizia hewa safi yenye ubaridi wa kupendeza, nikama kuna kitu au mtu walikuwa wanamsubiri, au kutarajia kukiona.
“Ina chukiza sana Doto, yani Seba, amemgharamia kiasi kile lakini mwanamke mwenyewe ni wa ajabu ajabu kama nini?” alisema mzee Kiguru huku bado wote wawili wametazama upande wa kiwandani, ambako watu wengi walikuwa wanapita, kwenda na wengine kurudi, “dah! yani uwezi kuegemea kama huyu mwanamke angekuwa waajabu hivi” alisea Doto, na sasa macho yao wakiwa yana mwona kijana mmoja, akiwa anakua kwa wendo wa haraka, akilielekea lile gari lao, “huyoooo! anakuja, atakuwa amesha pata kitu cha kuonyesha” alisema mzee Kiguru, “namwamini huyu dogo” alijibu Doto, huku wanamtazama yule kijana, ambae sasa alikuwa ameilkaribia kabisa gari la kina mzee Kiguru.
Kijana analifikia gari na kufungua mlango wa nyuma wa gari, na kuingia ndani, “boss nime fanikiwa, nime wachukuwa pale mgahawani, na pa ofisini” alisema yule kijana huku anata simu na kuweka video flani kisha akapatia mzee Kiguru, ambae pasipo kuongea lolote alikuwa amenyoonysha mkono kuipokea ile simu, na kuanza kutazama ile video, ambayo siyo tu, ilionyesha michezo ya kimahaba ya pale mhagawani, ila pia ilionyesha mahaba ya ofisini.
Mzee Kiguru, aliweza kuona video iliyochukuliwa dirishani, ikionyesha jinsi Salma, na kijana yule wasie mahamu, wakiwa wanafanyiana amb ya kimahaba ofisini, wakifia haua ya kupeana busu kimahaba, wakinyonyana ndimi zao kimahaba, wakijilegeza na kukaribia kupeana dudu, mle mle ofisini, “niache bwana jioni si tutalala wote” anasema Salma huku anajitoa kwa kijana yule, “shika uchafu wako” alisema mzee Kiguru, huku anampatia simu yule kijana, seat ya nyuma, nae akaipokea, “nitumie hizo video” alisema mzee Kiguru, na kumtazama Doto, “tuondoke turudi mjini” alisema Mzee Kiguru, na Doto akaondoa gari, huku yule kijana anatuma zile video fupi fupi zisizopungua sekunde therasini, nazisizo zidi dakika moja, kwenda kwenye simu ya mzee Kiguru, kupitia njia ya whatsapp.*******
Saa nane na nusu mchana, bado Emmanuel alikuwa ajarudi pale Hospital, toka stendi alikokuwa ameenda kumpeleka Ariana, mzee Mdemu na mama Arianna, walikuwa nje ya hospital, wamejilaza chini ya mti kubwa, kila mmoja amepitiwa na usingizi mzito, bahai nzuri walikuwa wamesha pata chakula cha mchana, kwenye vibanda vya mama ntilie, jilani na pale hospital.
Wakiwa wamelala usingizi wa maana, mala wote wawili wanasikia sauti ya kiume ikimwita mzee Mdemu, “bwana Mdemu, bwana Mdemu” woe wakafumbua macho, na kumtazama anaeita, ambae akuwa peke yake, maana mala baada ya kufuambua mcho, wakawaona mzee Sanga na Mwaisaka,, wakiwa wamesimama pembeni ya mzee Mdemu, “hooo jamani mmefika” alisema mzee Mdemu huku anainuka, toka pale alipokuwa amelala, na kujikalisha kitako, kama mama Anna aliekuwa amelala mita kama tano au sita hivi, toka alipo lala mzee Mdemu.
Naam baada ya kujiweka vizuri, wakasalimia vizuri, na wakina mzee Sanga wakatafuta sehemu za kukaa, na kuanza kupeana habari za mgonjwa na huduma alizopewa, mzee Mdemu akasimulia kila kitu, kuanzia walivyo pokelewa pale hospital, na kuanza kupaa huduma ya kwanza, “leo asubuhi, amepata vipimo, na ameonekana anavidonda vya Tumbo, ambavyo vinakaribia kuoboa utumbo wake, natba pekee ni kufanyiwa operation, ambayo inagharimu shilingi laki nane, hivi ninavyokuambia, Anna yupo stend anatafuta usafiri wa kuelekea Dar es salaam kwa Masoud, kufwata Fedha” alisema mzee Mdemu, na kuwafanya wale wazee wawili watazamane kwa macho ya mshangao.
Kisha kwa macho yale yale ya mshangao, wakamtazama mama Anna, baadae mzee Mdemu, “eti mnamaanisha huyu huyu Masoud mtoto wa Kizinge?” aliuliza mzee Mwaisaka, kwa sauti ambayo ilimfanya mama Anna atazame chini, huku mzee Mdemu, nae akiwatazama kwa macho ya mshangao, “kwani kuna tatizo, pale kijijini hakuna asie fahamu kuwa Masoud ni mchumba wa Anna, na isitoshe, kwa sasa amesha maliza chuo na ana maisha mazuri..” alisema mzee Mdemu, na kabla ajamaliza, mzee Mwaisaka akadaka juu, “pia anaishi kwenye nyumba nzuri, na anagari pia, lakini mnafahamu kuwa, lakini mnafahamu jinsi wazazi wake na wanavyo wachukulia nyie, itakuwaje kwa Masoud mwenyewe, bado atakuwa na binti yenu” aliuliza mzee Mwaisaka, kwa sauiti yenye kuwa shangaa wale wawili, yani mama Anna na mzee Mdemu.
Naam!!!! kauri hiyo iliwashtua sana, wakina mama Anna, “nyie mme ambiwa na nani juu ya jambo ilo?” aliuliza mzee Mdemu, akionekana kushangazwa na habari ile, ambayo yeye tayari alisha ifahamu, “sikia Mdemu mme msumbua bule Anna, na tena uenda akakutana na kitu amacho kitamuumiza huko Dar” alisema mzee Mwaisaka, pia akawaeleza wakina mzee Mdemu, na mama Anna, kilicho tokea kijijini kati yao na mzee Kizinge, “mke wa bwana Kizinge ametueleza wazi kabisa, kuwa muda wowote Masou atarudi kijijini akiwa na mwana gari lake, na msije kusema kuwa anamchumba” alieleza Mwaisaka, huku mzee Sanga, akisisitiza kwa kueleza kile kilichosema na mzee Kizinge na mke wake. ….….
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Write your comment