Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Jumamosi, 8 Machi 2025

Ukimaliza Funika 38_39


 


SEHEMU YA THERASINI NA NANE


ILIPOISHIA SEHEMU YA THERASINI NA SITA: “hivi unavyomwona huyu mwanamke, ni mzima kweli” aliuliza Sebastian akiwa anamtazama Anna alikuwa anazidi kusogea upande wao, “yupo fresh kabisa, yule mwanamke, ena nimekumbuka, huyu ndie alie mpigia jana simu, pale mgahawani, na Masoud akamzimia simu” alijibu yule kijana, na wakati huo tayari Anna alikuwa amesha fikia usawa wao. ……. endelea….


Nikama Anna aliwakumbuka wawili awa, maana aliwafwata mpaka walipo na kuwasalimia tena, “habari za saa hizi” alisema Anna, ambae sasa alikuwa anajitaidi kuficha hali ya kilio, “salama vipi umesha mwona mchumba wako?” aliuliza Sebasian ambae alisha shuhudia kila kitu, “we acha tu kaka yangu, yani sijuwi ata nitaenda kuwaeleza nini nyumbani, mimi naomba minielekeze njia ya kwenda stendi ya kwenda mafinga” alisema Anna, pasipo kujuwa kuwa kijana huyu, Sebastian, ni mwenyeji wa huko mafinga, barabara ya Mufindi, “unaenda mafinga sasa hivi?” aliuliza Sebastian kwa mshangao, “ndiyo sina cha kufanya huku, nilikuja kuchukuwa ela nikamtibu baba, mtu mwenyewe kube alisha amua kuniacha” alisema Anna kwa sauti yenye kutia huruma, “mh! kwanini usilale, uondoke kesho mapema” aliuliza yule kijana, “niendelee kukaa hapa dar, kwa uwezo gani, hapanina elfu tano miambili tu za nauri” alisema Anna akiitaja nauri ambayo alikuja nayo jana, toka mjini Mafinga, pengine aliamini kuwa ndiyo nauri yake.


Mpaka hapo tayari waliguneua kuwa mschana huyu, alikuwa katika wakati mgumu, hivyo ingefaa wakamwelekeza sehemu sahihi ambayo angepata usafiri ata kwa msaada, “Ok! kwa kukusaidia, nenda hapo stendi, panda magari ya mbezi, ukifika mbezi panda gari la kibaha ukashukie mzani, hapo utapata magari ya mizigo yanayoenda njombe mbeya au nje ya nchi” alisema yule kijana, na hapo Arianna akawashukuru na kuondoka zake.


Dakika tano baadae wakati Sebastian anajiandaa kuondoka zake, mala akaliona gari la baba yake linaingia, akasitisha safari na kushuka toka kwenye gari, akalifwata gari la baba yake ambalo lilikuja kusimama nyuma ya gari lake, ndani ya gari la baba yake kulikuwa na watu watatu, yani baba yake mama yake, na dereva wa baba yake, yani Doto.


Kadiri alivyowasogelea ndivyo aliweza kuona sura zao, zilivyo kuwa katika hali ya tahadhari, ata macho yao yalimtazama kwa tahadhari pia, na yeye alizunguka upande aliokaa baba yake, na alipofikia mlango tu, Doto akashusha kioo, cha upande wa mzee Kiguru, ambae alionyesha wasi wasi, juu ya hali aliyokuwa nayo kijana wake, baada ya kuwa amesha shuhudia tukio la kutisha, maana walisha pigiwa simu muda mrefu na yule kijana, “baba na mama, sijuwi niwashukuru vipi kwa surprise yenu, maana imenifumbua macho na kuniondoa katika tatizo kubwa sana, ambalo nilikuwa naelekea kulipeleka nyumbani” alisema Sebastian, na kuwafanya baba na mama yake ata Doto pia, watabasamu, “ukweli leo nimeshuhuia kwa macho yangu kwamba huyu mwanamke siyo kama tunavyo mchukulia, ni mwanamke asiefaa atakidogo” alisema tena Sebastia kwa sauti tulivu kabisa.


Kwakusikia hivyo sura za wazazi wake zika changamka, “haa! umewaona wanafanya nini?” aliuliza mzee Kiguru kwa sauti yenye shahuku, Sebastian akacheka kidogo, “nikikusimulia nitakudanganya, maana siwezi kukusimulia ata kidogo, “uwezi kusimulia kwanini, sababu umewaona wanafanya mapenzi ofisini?” aliuliza mzee Kiguru, kwa namna ya utani, nazani leongo lilikuwa ni kumchangamsha, kijana wake ilikumtoa katika unyonge wa kufumania, “zaodi ya unavyo fikilia baba” alisema Sebastian, ambae pia aliwasilimulia kisa cha mwanamke Anna toka Mafinga.


Habari ya Anna iliwasikitisha sana wazazi wa Sebastia, “yupo wapi huyo mwanamke, inabidi tumsaidie, maana kuwasaiia wenye uitaji, ni sawa na sadaka” alisema mzee Kiguru, huku akiazama upande wa kiwandani, “alisha ondoka anarudi Mafinga” alisema Sebastian, ambae sasa aliweza kukumbuka kuwa, siyo tu kukosa fedha ya kumtibia baba yake, ukweli ni kwamba tsh elfu tano, isinge mfikisha ata morogoro, Sebastian alihisi mwenye hatia, kumwacha yule mwanamke bila kumsaidia, wakati anajuwa fika yupo katika mazingira magumu, “sasa baba, mimi naondoka zangu, nitakuwa kule nyumbani kwangu, tutaonana jioni” alisema Sebastian, na kabla ajaondoka mama yake akamuwai, “sasa aujatuambia unaamua nini baada ya kujione mwenyewe” alisema mama Sebastian, na hapo Seba akainamisha kichwa chini, kama anatafakari jambo.


Alifanya hivyo kwa sekunde kadhaa, kisha akainua uso wake na kumtzama mama yake alie onekana kupitia uwazi wa katikati ya seat za mbele, “sababu nililianziasha wacha nilimalize taratibu, cha msingi msimweleze wala kumwonyesha dalili zozote kwamba, tumwngundua tabia zake harisi” alisema Sebastian, kisha akatoka na kuelekea kwenye gari lake, ambalo aliliwasha na kuondoka zake, akielekea upande wa segere, akimwacha yule kijana akiungana na wakina mzee Kiguru, ambao walikuwa wanamsindikiza Sebastian kwa macho, mpaka gari lake lilipotokomea upande huo wa segerea..



SEHEMU YA THERASINI NA TISA


ILIPOISHIA SEHEMU YA THERASINI NA NANE: “sababu nililianziasha wacha nilimalize taratibu, cha msingi msimweleze wala kumwonyesha dalili zozote kwamba, tumwngundua tabia zake harisi” alisema Sebastian, kisha akatoka na kuelekea kwenye gari lake, ambalo aliliwasha na kuondoka zake, akielekea upande wa segere, akimwacha yule kijana akiungana na wakina mzee Kiguru, ambao walikuwa wanamsindikiza Sebastian kwa macho, mpaka gari lake lilipotokomea upande huo wa segerea………. endelea….


Na hapo mzee Kiguru akamgeukia yule bwana mdogo, “sikia dogo, ebu twende hotelini, ukachukue lile gari dogo, karibu na kibanda cha fire, kisha kuanzia sasa hivi, fwatilia nyendo zote za Sebastian, asa kwa kipindi hiki ambacho ametoka kumfumania huyo mwanamke wake, pia hakikisha hakuna mtu anafahamu kama tumesha gundua uchafu wa yule binti” alisema mzee Kiguru, na baada ya hapo yule bwana mdogo, akaingia kwenye gari, kwaajili kuondoka pamoja kuelekea hotelini.**********


Hali iliwa mbaya, huko kijijini Malangari, maana licha ya fundi kufika kwa mzee Kizinge, mpaka saa nane za mchana, bado trekta lilikuwa alijawaka, licha ya kuwa alisha badiri pump ya mafuta, na kusafisha tank, lakini aikusaidia kitu, walikagua nozel na kukuta waya zote nane za nozel zimeungua.


“sina fedha ya kununulia nozel nyingine”, akiba yote nimemaliza kwenye tank na pump” alisema mzee Kizinge, kwa sauti yenye kudhihilisha uchovu wawazi kabisa, “aina shida boss, ukiwa tayari utanishtua” alisema fundi, ambae pia alitegemea kupewa fedha ya ufundi, na kufidia gharama ya mafuta aliyo yatumia kutoka mjini, “umesema kweli fundi” alisema kizinge, huku anaingiza mkono mfukoni, na kutoa wallet yake, “nitawasiliana na kijana wangu, yupo mjini anafedha nyingi sana, nitakupigia kesho mapema, alisema mzee Kizinge huku anafungua wallet ambayo inaokena ikiwa na elfu hamsini tu, anatoa elfu alobaini, na kumpatia fundi, “usijari, mzee ukiwa tayari utanipigia tu” alisema fundi, huku anapokea fedha toka kwa mzee Kizinge, ambae alibakia na not mja tu ya Elfu kumi.


Mzee Kizinge ambae leo akufanya kazi yoyote na trekta lake, ya kuingiza fedha, zaidi ya kutoa fedha nyingi sana, kulinganisha na kiasi alichokuwa nacho, na sasa alibakia na elfu kumi tu, alimtazama yule fundi mpaka alipotokomea upane wa mjini, na yeye akatoa simu na kuchagua namba ya Masoud, kisha akaipiga.


Simu iliita sana bila kupokelewa, akukata tamaa akapiga tena, lakini aikupokelewa, akatulia kidogo, na kuipiga tena, lakini hali ilikuwa ile ile, hapo akaanzisha mtindo, akawa anakaa kaa dakika kumi anapiga tena, simu aipokelewi, dakika kumi anapiga tena, aipokelewi “mpuuzi wewe nitapiga maka upokee”.********


Hali ilikuwa mbaya zaidi, huko Mafinga, ambako mpaka saa tisa, siku hii ya ijumaa, bado wakina mzee Mdemu, na mke wa mzee Sinyangwe, wakiwa bado awaja pata fedha kwaajili ya mzee Sinyangwe mwenyewe, ambae tumbo lilikuwa limeanza kuvimba, huku maumivu yakianza kurudi kwa kasi, “inabidi asizidi masaa mawili kabla ya kufanyiwa upasuaji, zaidi ya hapo kua hatari kubwa ya kumpoteza mgonjwa” alisema mganga mkuu, na kuzidi kuwachanganya wakina mzee Sanga, “Doctor kwani aiwezekani kumtibu, alafu tulipa fedha baadae?” aliuliza mzee Mwaisaka, na jibu la Doctor liliwavunja moyo, “hiyo ingewezekana, tatizo ni kwamba, dawa na vifaa vya matibabu, tunachukuwa kwenye duka la mzabuni, ambako tunatoa cash” alisema doctor, na hapo wazee wakatazamana.******


 Yaap! wakiwa awana ili wala lile, Masud na Salma mida hii, walikuwa wanatoka ofisini, wakiwa tayari wamesha malizia walicho kifanya, walisha ongea mengi wakimsimanga Anna na kumwita majina yote mabaya, ata muda huu wa saa kumi kasoro, walipoamua waende yumbani wakabadiri nguo, ili wavute muda kidogo, kisha waende club kujiachia jidogo, siunajuwa mambo ya week end.


Walioka pale nje wakaelekea kwenye gari la Salma, huku washangaliwa na wafanyakazi wenzao, wakaingia kwenye gari na kuondoka zao, kuelekea mjini, na ndio wakati ambao, Masou alisikia mlio wa simu yake toka kwenye dash oard ya gari lile, “dah! unajuwa sikukumbuka kabisa kama nimesahau simu kwenye gari, aliichukuwa simu na kutazama aliekuwa anampigia.


Alikuwa ni baba yake, “mzee huyo sijuwi anataka nini” alisema Masoud Kizinge, huku anaitazama simu yake, “usikute yule chizi wako amesha piga simu huk kijijini kuwasimulia kilicho mtokea, ndoa maana baba yako anakupigia simu” alisema Salma alie kuwa anaenesha gari, “mh!! ataanzia wapi kumpigia simu baba, au mama awampendi kama nini” alisema Masoud alie ittazama simu mpaka ilipokatika.


Naam hapo akapata nafasi ya kuona miseed call, iliyoandika iadi ya namba, 99 na alama ya kujumlisha, ikinyesha ilikuwa ni zaidi ya tisini na tisa, “duh! aakuwa na tatizo siriazi” alisema Masoud, huku anapiga simu kwa baba yake, simu ambayo kama iliita basi ata alie pokea akusikia mlio, maana tiii!! twap! ikapokelewa, “inamaana kazi za ofisi zinakubana kiasi kwamba upokei ata simu?” ilikuwa ni sauti ya mzee Kizinge, iliyo jawa na matumaini, “hapana baba, nilisahau simu kwenye gari” alisema Masoud, Kizinge, kwa sauti yenye tambo za kitajiri. “hooo! ndio uzuri wa kuwa na gari lako mwenyewe, maana ungekuwa umesahau kwenye daladala usinge ipata” alisema mzee Kizinge ….endelea…



SEHEMU YA ALOBAINI


ILIPOISHIA SEHEMU YA THERASINI NA TISA: alisema Masoud, huku anapiga simu kwa baba yake, simu ambayo kama iliita basi ata alie pokea akusikia mlio, maana tiii!! twap! ikapokelewa, “inamaana kazi za ofisi zinakubana kiasi kwamba upokei ata simu?” ilikuwa ni sauti ya mzee Kizinge, iliyo jawa na matumaini, “hapana baba, nilisahau simu kwenye gari” alisema Masoud, Kizinge, kwa sauti yenye tambo za kitajiri. “hooo! ndio uzuri wa kuwa na gari lako mwenyewe, maana ungekuwa umesahau kwenye daladala usinge ipata” alisema mzee Kizinge ….endelea….


 huku akimalizia kwa kicheko cha nguvu, “hivi umesikia kilichotokea huku, mzee Sinyangwe anaumwa, sasa eti wakina Sanga wamekuja hapa wanaanza kuomba ela ya nauli ya kwenda mafinga, unajuwa niliwashangaa sana” alisema mzee Kizinge kwa namna ya kustaajabu kwa kitendo hicho, japo alijuwa fika kuwa ni ungo, maana wakina Sanga walimpti kwenda kumtazama mgonjwa, nasiyo kuomba nauli.


Hapo ndipo Masoud alipoanza kupata picha ya kile ambacho, Anna alikuwa anajaribu kusema, “mh! anasumbuliwa na nini mzee Sinyangwe?” aliuliza Masoud, “anaumwa tumbo, yeye alizania akila maharage yalio aribika kitamtokea nini, lakini atushangai, maana kwa masikini akuna chakula kinachooza” alisema mzee Kizinge na wote wakacheka kwa pamoja.


Masoud alitamani kumweleza baba yake juu ya ujio wa Arianna pale kiwandani, lakini akashindwa kufanya hivyo, maana wasinge weza kuongea kwa mapana juu ya jambo ilo, “tuwaachie wenyewe na mabalaha yao, bwana ninashinda kidogo, chombo kimeloga hapa” alisema mzee Kizinge, na kuanza kumwelezea mwanae tatizo la tractor lake, mwisho akimaliza kwa kutaja gharama, “nikipata laki tano kwaajili ya nozer na vifaa vingine vidogo vidogo, itakuwa safi sana” alisema mzee Kizinge, ambae alionekana wazi kujivunia kuwa na kijana huyo, japo hicho kilikuwa ni kiiasi kikubwa cha fedha kuwai kumwomba kijana wake huyo, alie amini kuwa anakazi nzuri na nafisi nzuri katika kazi yake.


Ila kwa upande wa masoud mwenyewe, ilikuwa ni mstuko mkubwa sana, maana yeye kama yeye akuwa na uwezo wa kutoa laki tano kwa ghafla hivi, “he! baba laki tano nitaitoa wapi ghafla hivi?” aliuliza Masoud kwa mshangao na mshtuko mkubwa, huku Salma alie kuwa anaendesha gari akisikiliza maongezi yale, “mh! bwana usiseme hivyo, tutamtumia jioni” alisema Salma, na hapo Masoud akaunga juu kwa juu, “poa, usiwe na wasi wasi, nitakutumia baadae, sasa hivi nipo busy kidogo” alisema Masoud kwa sauti ya kujinasib, kama usingejuwa undani wake ungezania kuwa ni boss flani, mwenye kazi kubwa sana mjini.


Basi waliongeamawili matatu kisha wakaagana na kukata simu, kisha wao wakaendelea na safari yao, “tukifika home tupumzike kidogo, alafu mida ya saa moja moja tuanze kujiandaa, ili saa mbili twende zetu, magomeni kwenye taarab” alisema Salma, ambae akukuwa na na habari kuwa tayari Sebastian amesha rudi nchini, na ameshaona kila kitu.*******


Naam  baada ya kufika mbezi, na kusimama muda mrefu akitafuta, akiwaza kile kilicho mtokea, yani akuamini kabisa kuwa Masoud, alie msaidia kwa hali na mali, licha ya umasikini wake, na familia yake, lakini walipambania elimu yake, mpaka kupata kazi, lakini leo hii anamwambia kuwa wamesha achana, na kama aitoshi amemkuta anafanya mapenzi na mwanamke mwingine ofisini, na vipi kuhusu hali ya baba yake kule hospital mafinga, akiwa mmoja kati ya watu walio pambania Elimu ya Masoud, ambae sasa memkataa, atapataje matibabu, vipi kuhusu Elimu na huduma alizo wazulumu wadogo zake, vipi maisha aliyo jidhurumu yeyemwenyewe, ambapo aliacha kila kitu, kwaajili ya Masoud, akuvaa nguo nzuri, wala akujipaka mafuta mazuri kutunza ngozi yake, ambayo kila mwanamke alitamani kuwanayo, akakubari kupoteza uzuri ambao, ulifanya kila mwanaume pale kijijini atamani kuwanae.


Ayo yote aliyafanya kwaajili ya kumsaidia mwanaume, ambae alimini kuwa mwisho wasiku, watakuwa pamoja kwenye mafanikio, baada yake, Masoud, anajiona kuwa ni watofauti na kwamba awezi kuwa na yeye, na mbaya zaidi yeye na mwanamke wake, wanamwita kichaa, ameshindwa ata kumpatia fedha za matibabu, ya baba yake, baba abae siyo tu kumluhusu binti yake msaidie kijana huyo fedha za kwenda chuo, ila pia alishiriki kwa kutoa mashamba yake, na pia ata kufanya kazi, ilikupata fedha ambayo ilienda kwa kijana huyo, kama fedha ya matumizi, wakati wa masomo yake, wakiamini kuwa, ni mume mtarajiwa wa binti yao, ambae pia waliamini kuwa angewasaidia watoto wao watatu, na pengine kufanya maisha ya familia yao yamwe yenye unafuu.


Hapo ndipo Arianna alijiona mkosaji namba moja, kwa kusababisha imani yake ichangie familia yao kuishi maisha magumu, kuvaa kwa shida kula kwa shida na ata wadogo zake kuishi kwa shida, wakiota ndoto ya maisha mazuri kupitia yeye dada yao, Ariana alikumbuka fedha walizo tumia kumsomesha, Masoud, kama zingetumika katika maisha yao binafsi, wangekuwa na maisha mazuri sana.ata wadogo zake wangesoma kwa raha, na ata baba yake angekuwa amesha tibiwa, toka zamani, isingefikia kiasi cha kuletwa Mafinga na kuitaji kufanyiwa operation.


Baada ya kuwaza kwa muda mrefu, huku machozi yakimtoka, Arianna anakumbuka kuwa anasafari ya kurudi Mafinga, hapo Anna, anatazama kushoto na kulia, licha ya uyaona magari mengie ya abiria na watu wengi sana, lakini alijina kama vile yupo peke yake, kutokana na kile kilicho mtokea, njaa inamuuma lakini awezi kununua chakula, anaofia kuwa elfu nne na mia saba iliyo bakia, inge pungua zaidi, na yeye kukosa nauri ya kurudia mafinga, ambako alijuwa fika anaena kumshuhudia baba yake akiendelea kuteseka, kwa maumivu makali ya tumbo, pasipo kupata msaada wowote, maana awakuwa na fedha yoyote ya kulipia matibabu.


Anna aliulizia gari linaloenda  mzani wa kibaha, kule alikoelekezwa na wale vijana wawili, anapnda gari la mlandizi, huku Kondakta akiahidi kumshusha, mala watapofika mzani, maana ilionyesha wazi kuwa mwanamke huyu mwenye mwonekano wa hali ya chini ya maisha, alionekana mgeni hapa mjini.


Muda mfupi baadae safari ilianza, Anna akiwa amekaa seat ya karibu lkabisa na mlango, baada ya gari kuondoka pale stendi, Anna akatoa simu yake na kumpigia, mzee Mdemu, lakini simu aikuita, baada yake akasikia sauti ya mwanamke, “aina salio la kutosha kupiga simu hii, tafahari ongeza salio na ujaribu tena” hapo Anna akakumbuka kuwa alikuwa ameshiwa muda wa maongezi….…. 


Maoni 1 :

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu