Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Jumamosi, 8 Machi 2025

Ukimaliza Funika 45_46

 



SEHEMU YA ALOBAINI NA TANO


ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI NA NNE: Bwana Lubava aliwapatia ile bahasha, ambayo ndani yake kulikuwa ma bunda mawili ya fedha, yaliyofungwa na mpira mdogo maalumu ya kufungia fedha, raba bend, “nitakuja kuwa tembea mala kwa mala, ila kama kuna dharula, basi namba yangu hii hapa mtanipigia” alisema bwana Lubava, huku anampatia mama Ana, karatasi ndogo ngumu yenye namba za simu. …….endelea….


Toka hapo ulianza mjadara wa uliotawaliwa na staajabiko, “wapo walio tilia shaka ukubwa na heshima ya Masoud, mpaka mambo yaende vile, na kama amefikia hatua ile kwanini ata siku moja akuwai kurudi kijijini, akamwonyesha Ana mafanikio yake, napengine kumchukuwa kabisa, kwena kuishi nae, baada yake amemficha mpaka sasa ambapo Anna ameenda mwenyewe, “cha kushukuru amemsaidia, tofauti na tulivyo zania” alisema mzee Mdemu, na Emanuel akadakia, “ulikuwa wasi wasi wenutu, yani niliwaambia Masoud sasa hivi ni boss.


Mjadara huu ulidumu kwa muda mrefu, huku mama Anna akigharamia mchele na mboga, kwaajili ya chakula cha jioni, ambacho kilipikwa nyumbani kwa Emanuel, mpaka mida hii walikuwa wamesha kula, na mgonjwa alisha toka kwenye upasuaji, ambao ulimalizika salama, na pia mganga mkuu aliagiza kuwa mgonjwa amashiwe katika war ya VIP daraja la kwanza, ambako sasa alikuwa amepumzika.


kwa kujuwa kuwa sasa walikuwa miongoni wa watu wanao fahamiana na watu wakubwa, wenye fedha zao, mganga mkuu, aliagiza wale wanne wakaonyeshe vyumba viwili, ambayo vilikuwa tupu, ambapo walipewa madoro matatu, moja alipewa mama Anna katika chumba kimoja, na yale mawili walipewa wakina mzee Mwaisaka, kwenye chumba kingine, ambapo waliya tandika chini, kwaajili ya kulalia, lakini sasa walikuwa wamekaa pale mapokezi, wakiongea ili na lile wakivuta muda wakulala.****** 


Mida hii ya saa mbili na nusu, Anna na Sebastian wakimwa mwenge, karibu na njia panda ya kawe, wanaelekea upande wa makumbusho, safari ilikuwa ni ya kimya kimya, ni kama kila mmoja alikuwa anawaza la kwake moyoni mwake, wakati Sebastian akiwa anawaza juu ya usaliti wa mchumba wake, huku Anna alikuwa anawaza juu ya msaada alipewa na kijana huyu ajiri, ambae alikutana nae leo tu, pale kinyerezi, karibu na kiwanda anachofanyia kazi Masoud, “lakini huyu kijana ni mzuri awezi kunifanya chochote, kwanza awezi ata kunitamani, nahivi nilivyo sifai ata kuwa house girl wake” alijisemea Ana komoyo moyo, na kujikuta akijicheka mwenyewe, kwa kuachia tabasamu, tabasamu ambalo ata Sebastian aliliona, na kujikuta na yeye akitabasamu, “vipi umeipenda dar es salaam?” aliuliza Sebastian, na Anna akaiikia kwa kichwa, kuonyesha kuwa ni kweli amependa Dar ilivyo.


Wakati wakiwa wanakaribia maeneo ya njia panda ya bamaga, mala ujumbe ukaingia kwenye simu ya Sebastian, ambae alisogeza gari pembeni, na kusimama, kisha akafungua ule ujumbe, akausoma kwa sekunde chache na kuujibu, kisha akamtazama Anna, “tayari baba yako alisha fanyiwa operaion, anaendelea vizuri” alisema Sebastian, na Ana alishindwa kushangiria kwa nguvu, akaachia tabasamu pana, huku anashukuru, “asante sana kaka yangu, ata sijuwi nita kulipa nini, ungekuwa na mashamba ningelima ata mwaka mzima” alisema Anna ambae sasa machozi yalianza kumdondoka, “usijari Anna, maisha ndivyo yalivyo, tena ibabidi tupitie hapo Sinza ukapate nguo za kubadiri, maana naona auna ata begi” alisema Sebastian huku anaondoa gari


Nakuingia njia panda, ambako alikata kona kulia kuelekea sinza, na baada ya kuvuka miataa miwili mitatu akakata kona na kuingia mtaani zaidi, Ana alitarajia kuona gari likisimama mbele ya duka flani, lakini baada yake akaliona linavuka maduka yote na kuendelea mbele zaidi, likivuka bar moja iliyopo ndani kabisa ya mtaa, na baadae kukakata kona kushoto, kisha gari likaenda kusimama mbele ya nyumba moja kubwa, ya kisasa, “nisubiri kidogo kuna mtu naenda kumtazama” alisema Sebastian, ambae alishuka toka kwenye gari pasipo kulizima.


Sebastian alitembea kwa haraka kuelekea kwenye ile nyumba kubwa, ambapo alienda akaenda moja kwa moja, kwenye mlango wa nyummba ile na kusimama mbele yake, akashusha pumzi ndefu, kisha kama mwenye kujiuliza jambo kichwani mwake, akatulia sekunde kadhaa, alafu akapiga moyo konde na kugonga hodi, “nani tena majumbani kwa watu usiku huu” ilisikika kali isiyo itaji ukorofi wala usumbufu, toka ndani ya nyumba ile, ikifwatiwa na vishindo vyepesi vilivyokuja mlangoni, kisha mlango ukafunguliwa, na akanekana, mwaname mtu mzima, alie shilia grasi yenye maji ya rangi ya mkojo mkononi mwake “he! baba… mwanangu.. niwewe… umekuja lini, mbona ghafla…” aliongea mama huyu kwa kubabaika, huku mkono wenye grass ya pombe ukitetemeka kwanguvu .


Hapa ni kwakina Salma, na huyu ni shangazi yake Salma, ambae anafahamu fika kuwa Salma ayupo nyumbani na mbaya zaidi ametoka na mwanaume wake wapembeni, hiyo aikuwa tatizo kwake, maana angesingizia chochote, lakini hii grass ambayo ilikuwa mkononi mwake, ambayo ina kinywaji chenye kilevi kikubwa, toka kwenye chupa iliyopo mezani ndani ya nyumba ile, “shangazi ulinimiss sana, naona unaanza kunihoji hapa hapa mlangoni” alisema Sebastian kwa sauti iliyojaa utani, ungesema kuwa akuwa anajuwa lolote linaloendelea pale nyumbani.


Hapo shangazi akalazimisha tabasamu, ambalo ungebahatika kuliona, ungeng’amua kuwa ni tabasamu lazimishi, lililogubikwa na aibu, debe zima, huku anatazama nani, nazani ata wewe msomaji umejuwa kuwa alikuwa anatazaa ile chupa mezani.


“nime ingwa mkwe, maana imekuwa ghafla sana….hivi …kuna… kuna…usalama kweli, hivi ata Salma anafahamukama kama umerudi” aliuliza shangazi, ambae bad akuwa amemkaribisha Seba kuingia ndani ya nyumba ile, ambayo inalipiwa kodi na huyo huyo Sebastian, ambae alitabasamu kidogo, “nime mfanyia surprise siunajuwa tena, inabidi tutangaze siku ya harusi, pia sikuwai kumwonyesha nyumba yetu, ambayo tutaishi baada ya kuunga ndoa” alisema Sebastian, ambae bado alikuwa amesimama mlangoni, “ndio tatizo lenu vijana, sasa mwenzio ameenda kwenye sherehe ya rafiki yake, hukooo kimara” alisema shangazi, aliekuwa bado ametanda mlangoni, 


Seba ambae alijuwa kuwa anadanganywa, akatabasamu kiogo, huku akificha hasira na chukizo moyoni mwake, “hooo! kama nihivyo basi sina aja ya kuingia ndani, nikuache uendelee na kinywaji” alisema Sebastian na hapo shangazi nusu ushuzi umtoke kwa kihoro, “siku moja moja mkwe… tuna kumbuka ujana” alisema shangazi huku ana, mtazama Sebastian aliekuwa anabofya bofya simu yake kama vile kuna namba ya mtu alikuwa anaitafuta, “basi shangazi mimi naenda, akija utamwambia nilikuja, niaonana nae kesho kazini” alisema Sebastian kisha akageuka na kuondoka zake huku anaweka simu sikioni, ni wazi alikuwa anampigia mtu flani. …….endelea…. 



SEHEMU YA ALOBAINI NA SITA


ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI NA TANO: “hooo! kama nihivyo basi sina aja ya kuingia ndani, nikuache uendelee na kinywaji” alisema Sebastian na hapo shangazi nusu ushuzi umtoke kwa kihoro, “siku moja moja mkwe… tuna kumbuka ujana” alisema shangazi huku ana, mtazama Sebastian aliekuwa anabofya bofya simu yake kama vile kuna namba ya mtu alikuwa anaitafuta, “basi shangazi mimi naenda, akija utamwambia nilikuja, niaonana nae kesho kazini” alisema Sebastian kisha akageuka na kuondoka zake huku anaweka simu sikioni, ni wazi alikuwa anampigia mtu flani. …….endelea….


Shangazi alimsindikiza kwa macho mkwe wake huyo, ambae amewafanya kuonekana watu, kati ya watu wenye maisha bora hapa jijini dar es salaam, mpaka alipoingia ndani ya gari, na kuonoka zake, ndipo na yeye alipo ingia ndani haraka na kufunga mlango, “tumeumbuka jamani, we mtoto kwanini ukujuwa kama mwenzio anarudi leoooo” alisema shangazi huku anakimbilia simu yake, iliyokuwepo juu yameza, “jamani jamani bora ata usiwe kwenye kelele” alisema shangazi huku anabofya simu yake kuipiga namba ya mmtoto huyu wa kaka yake, ‘simu unayopiga inatumika kwa sasa, tafadhari jaribu tena baadae” ilisikika simu ya shangazi ikimpatia maelezo hayo, akakata na kuipiga tena lakini maelezo yakawa yale yale, ata aliporuia mala ya tatu, akasikia ujumbe ukionhezeka, “namba ya mtumia wa simu unempigia anaongea na mtu mwingine, tafadhari subiri au jaribu tena baadae” jamani we mtoto, unaongea na nani huyo, ebu pokea simu yangu” alisema shangazi ambae alichagua kusubiri.****


Yap! mzee Kiguru na mke wake wakiwa nyumbani waliendelea kupata taarifa za kijana wao, kwa kila hatua aliyo piga, na sehemu alizo zungukia, na sasa waliambiwa kuwa ameshaenda kwa kina Salma, naakumkuta, baada yake amemkuta shangazi akiwa na grass ya pombe kali, pia walisha pewa taarifa kuwa Sebastian alisha mchukuwa Anna, bao aijajulikana anampeleka wapi, kufanya nini, “ bado nawafwatilia, nitawajulisha kila kitu” alisema yule dogo.


Ukweli akuna ata mmoja kati ya mzee Kiguru na mke wake, waliojilahumu kwa kumgundulisha Sebastian uchafu wa Salma, zaidi walijipongeza kwa kuona wamemwepusha kijana wao toka kwa mwanamke mwovu, na taperi, bahati nzuri Sebastian mwenyewe amejionea, “chamsingi sasa atulie, atafute mwanamke mwenye heshima zake, alisema mama Sebastian, wakiwa chumbani kwao, wanapaa grass ya #mbogo_land coco wine, mabayo sifa yake kubwa, uleta hali ya joto na kiu ya uji wa naza kwa bagia za kunde, kwa jinsia zote, hakika usije ukanywa ata jilani ya dada yako.****** 


Yap,! Salma akiwa na Masoud, wanavuka naeneo ya njia panda ya mabibo, yani mahakama ya ndizi au BBA (big brother afrika) huku wote wawili wakiwa wamekosa amani kwa, ukosefu wa fedha za kwenda kutumia kule taarabuni, vichwa vyao vikisongwa na maswali mengi, wakati Salma anajiuliza ni kwanini card zote zisumbue kwa pamoja, wakati walikuwa na uhakika account zilikuwa na fedha, huku Salma japo akualalishwa kibenk, lakini alikuwa na luksa ya kuchukuwa fedha kwa card za ATM machine hizo.


Masoud alikuwa anawaza jinsi baba yake anavyo subiria feha kwa hamu, na kama nitatizo litakalo chukuwa muda mrefu, basi mzee wake lazima atambuka, maana kwa jinsi anavyo mfahamu kuwa ni mpenda sifa, mpaka mida hii tayari atakuwa amesha tangaza kijiji kizima cha malangari, juu ya kutumiwa fedha na kijana wake huyo, hakika ilimtia simanzi sana Masoud, kwa kuona anazikosa fedha za kmtumia baba yake, akujari kuwa fedha anazo zisimanzia, nijasho la mwanaume mwenzie.


Wakiwa katika mawazo hayo, mala simu ya Salma ikaita, ebu tazama nani anapiga simu, “alisema Salma, aliekuwa anasimama kwenye taa za urafiki, akisubiri kuingia upande wa shekilango, “ni Seba” alisema Masou, huku anampatia simu Salma, ambae moyowake ulilipuka vibaya sana kusikia jina ilo, akaidaka simu haraka, na kuitazama.


Nikweli alikuwa Seba, yani kifupi cha Sebastian, aliandika hivyo kutokana na ombi la Masoud, lakubadiri jina ilo, kwenye simu yake, ikiwa ni baada ya Masoud kutokupendezwa na jila mwanzo, ambalo ni Husband to be, “amesha rudi, mbona amenipigia kawaida?” aliuliza Salma huku anapunguza sauti ya redio, kisha akaweka sauti yake vyema, kwa kujikooza kidogo, alafu akapokea simu, “hallow’ ilikuwa nisauti ndogo tulivu, yenye kama viji mikwaluzo ya sauti ya mtu alitoka usingizini, “hallow mambo vipi, mbona kama umelala” ilisikika sauti ya Sebastian toka upandde wa pili wasimu.


Ukweli sauti ya Seba ilisikika wazi alikuwa nani yagari, tena linalotembea, “yah! siunajuwa mida yangu baby, tayari nipo kitandani, sina pakwenda bila wewe” alijibu Salma kwa sauti ile ile ya mtu anae toka usingizi, “hooo!! basi poa tutaonana kesho kiwandani, maana nimesha rudi, nimeigia jioni hii” alisema Sebastian, na kukata simu, na ndio wakati ambao, Salma alipoiona simu ya shangazi yake inaingia, akajuwa kwa vyovyote anaka kumpa habari ya kurudi kwa Sebastia, hivyo akaipokea mala moja, “mwenzangu tumeumbuka” ilo nlo lilikuwa neno la kwanza toka kwa shangazi, ambae aliongea kwa sauti iiyo jaa wasi wasi na kihoro...

Maoni 1 :

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu