Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Ijumaa, 7 Machi 2025

Ukimaliza Funika ep 8_10


 UKIMALIZA FUNIKA

SEHEMU YA NANE

MTUNZI @MBOGO EDGAR

ILIPOISHIA SEHEMU YA SABA: Hakuishia hapo kijana Masoud, Fedha hiyo hiyo ilimfanya aanza kunywa pombe na kujipatia waschana, ambao walitambua kuwa Masoud ni mtoto wa tajili mmoja mkubwa huko Iringa, Masoud ambae akudumu na mwanamke mmoja japo kwawiki moja, alifikia hatua akaanza kusaka wanawake kwenye kumbi za starehe, wazo alilolipata toka wa marafiki zake, wa chuo, na wamtaani. … .…. endelea….


aliendelea na katabia hako, ambapo kila siku alikuwa anabadiri mwanamke mwingine, ambae angekutana nae mshana, na inapofika nyakati za usiku, angehakikisha ana fanya jambo lolote litakalo mwondoa Arianna pale nyumbani kwao, kisha yeye anaenda kumchukuwa mwanamke alie kusudia kulalanae siku hiyo, Masoud bila kujari kuwa, fedha anayo tumia kuonga kwa wanawake awa anaotembea nao, alifanya hivyo akitumia fedha hiyo ambayo pia, alitakiwa aifanye kama nauri ya kurudia, sababu malipo ya awamu ya pili ya kodi ya shamba, yangefanyika miezi miwili baadae.


Siyo kwamba mama na baba yake awakulijuwa ilo, walilihuwa vyema lakini awakuthubutu kukemea, maana walimwona kijana wao yupo sahihi kabisa, ukizingatia, mschana Arianna alikuwa amechokwa kuanzia mwili sura ata mavazi, “mh! hivi mke wangu, Masoud atamuweka wapi huyu binti wa Sinyangwe?” aliuliza Mzee Kizinge, siku moja, akiwa na mke wake, wakati Masoud akiwa likizo, huku wanamtazama Arianna kupitia dirishani, alie kuwa anaosha vyombo, “kwanini unauliza hivyo?” aliuliza mama Masoud, huku bado wanamtazama Anna, ambae akuwa anajuwa kama anazungumziwa huko ndani, “mh! ebu mwone alivyo kongoroka, yani ata wewe unamshinda kwa uzuri” alisema mzee Sinyangwe, na kumfanya mke wake acheke kwanguvu.


Kicheko kile kilimfikia Anna, lakini akujuwa kinausu nini, maana kiliokea ndani, “unazani Masoud mjinga, we uoni anavyo angaika na wanawanawake wengine” alisema mama Masoud, kwa sauti ya chini, ambae alisisitiza kuwa awezi kukubari, “yani mwanangu asome kwa juhudi, apate kazi nzuri alafu amwoe mwanamke wa ovyo kama huyu, tena ona familia yake ilivyo masikini, sindio itakuwa mzigo kwa mwanangu” alisisitiza mama Masoud, ambae kkweli alikuwa anamtumikisha Anna kama ile mfanyakazi wake, ilihali ata chakula akuwa anapata pale nyumbani wa wakwe, na yeye ndie alie kuwa anamsomesha kijana wao.


Zikiwa zime baki siku chache kufungua chuo, Masoud ambae ata kupendeza kwake, kulitegemea fedha zinazotokana na jasho la Arianna na familia yake masikini, Masoud alijikuta amesha maliza akiba yote ya fedha ambazo zinge msaidia kwa nauri na ile ya kuanzia pindi atakapofika dar, lakini swala ilo alikumsumbua akili yake, maana alijuwa mfafadhiri wake wa masomo, ata mpatia fedha za kuendea chuo, na fedha za kuanzia, kwakujuwa kuwa Arianna akuwa na ujanja wa kumkatalia kile anachoitaji, angefanya lolote ata kwa kuweka dhamani nyumba yao wanayoishi.


Nikweli Masoud alipewa fedha na Arianna, na yeye pasipo kufikilia mala mbili juu ya malengo yake kwa mschana huyo, akaipokea na kuondoka zake kuelekea Dar es salaam, kuendelea na masomo.*******


Naam siku ilisonga miezi ilikatika, Masoud akifanya matumizi kama mtoto wa kitajiri, huku akiendelea kujipatia wanawake, akitumia fedha nyingi na wanawake hao mavazi na ulevi, kiasi kwamba ikaikia hatua akawa anaomba, fedha toka Mlangari, kwa mshana Arianna, huku akimpa moyo kuwa mala atakapo maliza chuo na kupata kazi, atamchukuwa na kuja kuishi nae huku dar, mschana ambae, licha kwamba kila anapoenda likizo, utegemea fedha za kurudia toka kwake, lakini akiika dar asingejisumbua ata kuomba kuogea nae kupitia simu ya mama yake, na kila Arianna alipofanya juhudi za kuazima simu kwa majilani, au mama Masoud, lakini Masud ambae upokea simu mala moja, ila mala baada ya Arianna akujitambulisha kuwa ni yeye, ungesikia, “nipo busy Anna, nitakutafua” kisha angekata simu.


Ukweli angekaa ata miezi sita ya muhula bila kuongea na mpenzi wake na ata anapokuja likizo, uonana mala chache sana, na lilipokuja swala la kuomba edha, ambayo alianza kuomba kwa baba yake, na kuambiwa kuwa akukuwa na fedha ndipo alipoamia kwenye kibubu chake, ambacho ni Arianna. 


Ilikuwa karibu na mwezi wa tano, karibu na msimu wa kufunga kufunga vyuo, mwaka wapili tangu Masoud ajiunge na chuo hicho cha ufundi, hapo Dar es salaam, siku hiyo Arianna alikuwa ametoka kwenye vibarua vyake, ukweli alikuwa amechoka sana, lakini hiyo isingekuwa sababu ya yeye kuto kwenda nyumbani kwa kina Masoud, maana anajuwa lawama za mama mkwe, pale anapokosa kwenda kwake, japo jioni moja tu, hivyo hakuwa na budi kujitaidi kwenda kwa mama mkwe pasipo kusikilizia uchovu wake.


Mida ya saa kumi, ndio wakati ambao Arianna, alifika nyumbani kwa kina Masoud, kwanza akapokelewa juu juu, “hivi siku nyingine unashindwa kubadiri hiyo ratiba yako ya kuja jioni, ona sasa mwenzio amepiga simu toka jana usiku, anaitaji kuongea na wewe, akikosa kukupigia unalalamika, sasa anakupigia uonekani, bola ununue simu yako” alisema mama Masoud, kabla ata ya salamu.


Japo ilimfanya Arianna atabasamu kwa raha aliyo ipata, baada ya kusikia mpenzi wake amempigia simu, lakini ilimshtua kidogo, maana aikuwai kutokea ata mala moja, kwa miaka miwili ambacho Masoud ameenda chuo, kuwai kupiga simu kuitaji kuongea na yeye, “kweli mama alikuwa anasemaje?” … .…. endelea…. 


UKIMALIZA FUNIKA

SEHEMU YA TISA

MTUNZI @MBOGO EDGAR

ILIPOISHIA SEHEMU YA NANE: Japo ilimfanya Arianna atabasamu kwa raha aliyo ipata, baada ya kusikia mpenzi wake amempigia simu, lakini ilimshtua kidogo, maana aikuwai kutokea ata mala moja, kwa miaka miwili ambacho Masoud ameenda chuo, kuwai kupiga simu kuitaji kuongea na yeye, “kweli mama alikuwa anasemaje?” … .…. endelea….


aliuliza Arianna kwa shahuku, huku tabasamu, likiwa lime mtawara usoni mwake, “nitajuwaje anachotaka kusema, wakati yeye anataka kuongea na mchumba wake, yani anapiga simu kila saa kukuulizia kama umesha fika, ametoka kupiga sasa hivi, we kaendelee na kazi akipiga nitakuletea simu” alisema mama Masoud, huku anaingia ndani, na kumwacha Anna anaelekea kwenye kalo la kuonshea vyombo, lililosheheni vyombo vya toka jana usiku.


Nusu saa baadae Arianna akiwa anaendelea kuosha vyombo, mala mama Masoud akatoka nje, akiwa na simu mkononi, Anna, simu yako hii, nibola ata ukinunua simu yako, awe anakupigia moja kwa moja” alisema mama Masoud huku anampatia Arinna simu, “Hallow mambo” alisalimia Anna, mala baada ya kuweka simu sikioni, “poa Anna mambo?” ilikuwa ni sauti iliyochangamka ya Masoud, “poa tu Masoud, yani leo ndio umenikumbuka” aliongea Anna ka sauti ya kudeka, uku anatembea taratibu kuelekea ubavuni mwa nyumba ile kubwa ya wakwe zake, “Anna ukweli nimekukumbuka sana mpenzi wangu, yani toka jana napigasimu lakini mama anasema haupo” alisema Masoud kwa sauti ambayo ungesema kuwa, ni kweli alimkumbuka sana mpenzi wake huyu, “jamani, pole sana, aya niambie wanasemaje huko” alisema Anna kwa kujiachia, akijuwa kuwa mpenzi wake alimkumbuka sana, “huku poa tu, lakini maisha ya chuo ni magumu sana, siunajuwa tena kila kitu kujitegemea tofauti na shule, yani hapa nimeishiwa kila kiu, nadowea chakula kwawenzangu” alisema Masoud kwa mtindo flani, ambao usingezania kuwa alikuwa anaomba fedha, “jamani Masoud, sasa kwanini ujapiga simu nikutumie ela kidogo?” aliuliza Arianna kwa sauti iliyojaa uzuni.


Hapo ndipo Arianna alionekana kuotoa nafasi ya timu pinzani kutundika gori, “mpenzi ningejuwaje kama unaweza kuwanayo, yani ningejuwa mbona ningekuwa nimesha kueleza” alisema Masoud, mfano wa mtu anae jari na kuzingatia sana, kuhusu mpenzi wake, “lakini ulitakiwa unieleze tu, mi nitajuwa la kufanya, najuwa unasoma kwaajili yetu, utakiwi kuteseka Masoud” alisema Arianna kwa sauti ya kulalamka iliyojaa huruma upendo wa hali ya juu, “sawa Anna nimekuelewa, nitakuwa nakujulisha” alisema Masoud, ambae nazani wakati huo alikuwa anafurahi kimoyo moyo.


Naam ulifanyika utaratibu Anna akaenda kutuma fedha kwenye kibanda cha wakara, na huo ndio ukawa mwanzo wa vizinga vidogo vidogo, ambavyo vilimfanya Anna azidi kufanya kazi kwa juhudi na kujituma ili aweze kumhudumia Masoud, pasipo kujari kuwa alikuwa anazidi kuchoka kimwili na kisura, Anna akujari mavazi, wala urembo, akiamini kuwa anaandaa maisha ya familia yake, na msaada wa baadae kwa wazazi wake na wadogo zake.


Arianna alizidi kujituma kwa kuzingatia yeye ndiyo msaada kwa Masoud, kama ilivyokuwa mwanzo, akujari kujipodoa kama wafanyavyo waschana wengine wapale kijijini, ambao kama ungekutana nae Mafinga au Njombe mjini, ungesema ni mwenyeji wa pale, na siyo kutoka kijijini Malangari, yeye alichojari anafua nguo zake chakavu, na anaoga vizuri, anapaka mafuta vizuri, pasipo kujari, kuwa ni mafuta ya kupikia, na nyuda wote ungeona kandamili zae zikiwa safi kabisa, japo swala ilo la usafi, alikuweza kuficha ufukara wake wakujitakia.


Arianna akujuwa sababu zinazo mfanya Masoud ashindwe kuwa na hamu nae wakati anapokuwa likizo, licha ya kuwa alikuwa anawasilina nae mala kwa mala na kuomba edha, lakini cha kushangaza akirudi likizo, Masoud anaoneana kuwa busy, akujari kama Arianna alikuwa na hamu nae sasa alikuwa anatimiaza mwaka wapili pasipo kupata haku ya uchumba, zaidi kumhudumia mchumba wake huyo ambae akuwa ametolewa barua wala mahali.******* 


Naam siku moja wakati Masoud akiwa mwishoni mwa mwaka wapili, wa mafunzo yake ya  ujuzi huo wa kutengeza vifaa vya majumbani, furniture, kijana wetu Masoud akiwa nawenzake wanaongea ili na lile, ndipo alipo sikia habari za day worker, wao wakiita ndondo, kwamba unatumia mudawako wa ziada, asa siku za mwisho wa week, kufanya kazi kwenye viwanda vya watu binafsi, na kujipatia fedha, za matumizi na starehe. … .…. endelea…. kufwatilia mkasa huu, wa #UKIMALIZA_FUNIKA, inayo kujia hapa hapa kwa @HADITHI ZA MBOGO EDGAR, kwa hisani ya @kingelvis mbogo, wa @mbogo land


UKIMALIZA FUNIKA

SEHEMU YA KUMI

ILIPOISHIA SEHEMU YA TISA: Naam siku moja wakati Masoud akiwa mwishoni mwa mwaka wapili, wa mafunzo yake ya  ujuzi huo wa kutengeza vifaa vya majumbani, furniture, kijana wetu Masoud akiwa nawenzake wanaongea ili na lile, ndipo alipo sikia habari za day worker, wao wakiita ndondo, kwamba unatumia mudawako wa ziada, asa siku za mwisho wa week, kufanya kazi kwenye viwanda vya watu binafsi, na kujipatia fedha, za matumizi na starehe. … .…. endelea….


Jambo lile lilimpendeza sana, Masoud, ambae wenzake walikuwa wanajuwa kuwa ni kijana toka kwa familia bora yenye uwezo mkubwa wakifedha, ni kutokana na jinsi alivyokuwa anajiweka, na kujisifu kwa wanawake, kiukweli alikuwa anaitaji sana zile kazi za muda, maana kukweli fedha ya malipo ya kodi ya shamba la kina Anna ilisha maliza mkataba wake, kwamaana alisha lipwa yote, na fedha alizokuwa anatumiwa na Arianna azikutosha kwa starehe za pombe na wanawake na mavazi yake ya kisasa, lakini wenzake watamchukuliaje, endapo ataenda kufanya day worker.


Baada ya kuwaza kwa muda mrefu, Masoud akapata jibu, kwamba akatafute Day worker katika kiwanza ambacho, kipo mbali na maeneo ya buguruni anapoishi na wenzake, wazo ambalo alilifanyia kazi, na baada ya kusaka kiwanda kwa muda mfupi akabahatika kupata kiwanda kimoja cha mtu binafsi, huko maeneo ya sinza, ambako alienda kukutana na manager wa kiwanda kile maarufu cha KIGURU FERNITURE INDUSTRY, ambacho kilikuwa kinaongoza kwa kuuza samani za majumbani, jijini dar es salaam na mikoa yote ya Tanzania, na wakati mwingine walisambaza nchi za jilani, “karibu anko nikusaidie tafadhari” alikaribisha mschana mrembo, alie jawa na tabasamu pana usoni mwake, ambae ndie Manager mwenyewe.


Ukweli licha ya kuduwaa mbele ya mschana yule mrembo, akisaajabia urembo wake, alimtazama kwa umakini na macho ya tamaa, kiasi cha mwanamke yule kuachia kicheko laini, “naitwa Masoud” alisema Masoud huku anampatia mkono yule mwanamke mrembo, ambae uvaaji wake wa mavazi viatu, ata hearing na mkofu wake, vilionekana kuwa vya hamani, “naitwa Salma, ni mkurugenzi wa hapa, KIGURU FERNITURE INDUSTRY, karibu sana” alisema tena yule mschana mrembo, huku anampatia mkono kijana wetu Masoud, ambae nae aliushikamkono ule laini, wenye pete kwenye ndogo nzuri kwenye kidole chanda chake.


Masoud aliushikilia mono ule kwa sekunde kadhaa, kiasi cha mschana yule kuutioa mkono ule, huku anacheka kidogo, “karibu kaka yangu, tuna bidhaa nying nzuri na zakisasa” alisema yule mschana mrembo Salma, ambae tabasamu alikukauka mdomoni mwake, “asante sana, dada yangu, mimi siyo mteja, ila nimekuja na ninashida na wewe pekee ndie wakunisaidia” alisema Msoud kwa sauti ya upole, yenye swaga flani za kubembeleza, kwa namna ya pekee, “mh! shida gani hiyo kaka yangu, mbona unanitisha?”  aliu;iza yule mwanamke, kwa sauti iliyojaa utani, huku anaachia tabasamu laini.


Hapo Masoud, akasoma jambo flani kwa huyu mschana mwenye kujichekesha, “wala usiwe na wasi wasi, ni inshu ndogo kwako, ndio maana nimekufwata” alisema Masoud, huku anamkazia macho yule mwanamke alie jitambulisha kwa jina la Salma, ambae bila kupenda alikuta akishindwa, kuimili kumazama kijana huyu, na kujikuta akijitabasamulisha, bila sababu ya msingi, “kaka unavisa wewe, si unimbie tu, nione kama naweza kukusaidia” alisema Salma, kwa sauti iliyoanza kujilegeza, mfano wa mschana anae zungumzia mapenzi, na mpenzi wake.


Mpaka hapo, kijana Masodu mototo wa mzee Kizinge, tajiri wa Malangari, aliona dalili zote za kufanikiwa kwa ombi lake, na pengine, anaweza upata kitu cha ziada, pasipo kujari kama mschana huyu, alikuwana pete, katika chanda chema chake, “dada yangu mimi ni mwanafunzi wa waka wa pili wa chuo cha VETA, nachukuwa mafunzo ya utengenezaji wa vitu vya ndani, kama ambavyo nyie mnafanya hapa kiwandani kwenu, nimekuja kuomba nafasi ya kufanya mzoezi ya vitendo, pengine nitajiongezea na kipato kidogo, siunajuwa maisha ya chuo, siwezi kuwa na naomba ela ya bata wazee kila siku” alisema Masoud kwa sauti flani ya taratibu, huku akilamba lamba midomo yake.


Hapo Salma akatulia kidogo, akiwaza juu ya ombi la kijana Masoud, japo akuacha kutabasamu, “mmmhh! bila shaka unaweza kuja kufanya kazi, panga mipango yako vizuri, na utaeleza siku ambazo utakuwa unakuja kufanya kazi” alisema Salma, ambae siyo tu kijitabasamulisha, pia alikuwa aachi kujichekesha, huku anamtazama Masoud kwa macho ya kumkagua, “sawa maadam, nitaandika kila kitu, cha msingi nipate namba zako za simu” alisema Masoud ambae kiukweli, tayari alisha mpenda sana mschana huyo, pasipo kujari kama atakuwa mke au mchumba wamtu.


Ukweli, tofauti na vile ambavyo ungezania, kuwa mschana huyu, mwenye kusimamia kiwanda kikubwa kama hiki cha utengenezaji wa viaa majumbani, ange kuwa mgumu kidogo kutoa namba zake za simu, “ok! andika namba hizi hapa” alisema Salma ambae alionekana kufurahi sana kuombwa namba za simu, na kijana huyu Masoud, “hiyo namba naomba uitunze sana, ni yakwangu binafsi, uwa siitoi ovyo ovyo, ata wewe nimekupa tu” alisema Salma, kwa sauti flani ambayo ungesema ni kwei kijana Masoud alikuwa ni mwenye bahati ya pekee, “usijari maneger, namba yako hipo sehemu salama” alisema Masoud kwa sauti iliyojaa mbwembwe.


Nikama wawili awa walitokea kuzoweana kwa haraka sana, japo nikawaida asa kwa vijana wasasa, asa wanapo fikia atua ya kupeana namba binafsi, “ukikiika nijulishe” alisema Salma wakati wanaagana, “samahani dada yangu, nisije kukusababishia matatizo kwa mumeo, ni vyema kama ungenieleza muda sahii wa kupiga simu, maana ….” alisema Masoud, kwa sauti flani ya kuchombeza, huku akijuwa kuwa jibu la swali lile linge weka wazi juu ya jibu la ombi lake la pili, ambalo angelitoa usiku wa siku hiyo, “wewe ni mwelewa sana, we piga muda wowote, mchumba wangu ni mwelewa, ata hivyo atuishi pamoja, siunajuwa atujafunga ndoa” jibu la Salma lilimvunja nguvu, japo akuonyesha wazi wazi kuvunjika nguvu kwake.


Hivyo ndivyo Masoud alipoanza kufanya kazi za ziada, na kujipatia fedha, ambazo zilifanya apunguze kuomba fedha kwa Arianna mschana ambae, kiukweli alikuwanae sababu ya mazowea tu, yani alikuwa anamchukulia kama ndugu wakaribu, na isitoshe, ni sababu tu alikuwa msaada wake kifedha.*******


Wakati hayo yanaendelea jijini Dar es salaam, huko kijijini Malangari, mambo yalikuwa tofauti kidogo,  afya ya mzee Sinyagwe ilikuwa inazidi kudhoofika siku baada ya siku, mke wake akaihia kumchemshia dawa za mitishamba, ambayo aikusaidia kititu, siyo kwamba mitishamba aitibu, hapana, ila akuna aliekuwa anafahamu tatizo la mzee Shinyangwe, kilichokuwa kinafanyika ni kuhisia, au kumpatia dawa kutokana na maumivu anayo yasikia siku ile, ila kiukweli ilikuwa ni hatari kwa mzee huyo, baba wa mschana. .…. endelea..

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu