Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Alhamisi, 22 Mei 2025

𝐇𝐚𝐝𝐢𝐭𝐡𝐢: 𝐔𝐊𝐈𝐌𝐀𝐋𝐈𝐙𝐀 𝐅𝐔𝐍𝐈𝐊𝐀 𝐄𝐏 56_60




Mpya
UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA HAMSINI NA SITA
MTUNZI @MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA TANO: Ilimfrahisha sana, maana akuna kitu alikuwa anaogopa au akutaka kitokee, kana kushindwa kuwa huru na Salma, sababu ya ujio wa Sebastian,  “poa usisahau ile ela ulimwahidi baba” alikumbusha Masoud, huku akijuwa fika kuwa fedha hiyo, itatoka kwa mwanaume mwenzie, “hooo! nakumbuka, Masoud, wacha kwanza Seba aje, nianipe hiyo laki tano, alafu ashughurikie na swala la kadi” alisema Salma kwa kujiamini, akijuwa wazi kuwa anatarajia kucjukuwa fedha kwa mwanaume huyu na kupeleka kwa mwanaume mwingine. …….endelea….

Waliongea mawili matatu, ya nayohusu mapenzi yao ya wizi, kisha wakaagana na kukata simu.******

Ilikuwa imepita dakika kumi na tano toka mwana dada Saphia mpemba, mwenye umri wa miaka therasini na nne, afungue saloon yake, pale mikochen, saloon ambayo kiukweli aikujificha kuwa ni yenye hadhi ya juu, na sasa aliliona gari moja zuri jipya, la gharama, aina range rover, likisimama karibu na Saloon yake.

Mwanzo akujari kuhusu lile gari, lakini baada ya kumwona mtu anae shuka toka kwenye gari, ikamlazimu atoke nje ya saloon yake na kumuwai kijana huyu, ambae kuna wait flani, kama mwaka mmoja hivi uliopita, kijana huyu alikuwa anamleta mpenzi wake kila week end maali hapa, kwaajili ya kufanya sclub za kulainisha ngozi, pia kutengeneza nywele zake na kununua mafuta mazuri ya ngozi.

Licha ya kwamba  dada Saphia mwenye uzuri wa hasiri unao nongeshwa na umbo zuri la rangi yake ya kiarabu, kuwa na wafanyakazi watatu wakike pale saloon, lakini inapokuja swala la kijana huyu tajiri mwenye mwonekano mzuri, uwa anapenda kumhudumia yeye mwenyewe, “karibu Seba ni muda mrefu sasa sijawaona wewe na wifi yangu” alisema Saphia kwa sautiyake ya kipemba, huku tabasamu likiwa limetawala usoni mwake, “mambo mengi tu, lakini leo nime kukumbuka” alisema .Sebastian na yeye akiachia tabasamu afifu, “hoooo! au umeshaamia kwenye nyumba yako, hapo nyuma ya tanesco?” aliuliza Saphia Mpemba, “hapana ila nitaamia hivi karibuni, ila leo nimekuja kuna kazi nataka unifanyie” alisema Sebastian, 

Nahapo akamweleza kuwa aende na baadhi ya vifaa yake, aende pale kwenye nyumba mpya, “kuna mwanamke yupo pale, naitaji umweke sawa, ni mgeni wangu toka nyumbani Iringa” alisema Sebastian, ambae alimweleza pia Saphia, mwangalie mgeni huyo, ni mafuta gani ya ngozi ambayo yatafaa kuweka ngozi yamgeni hoyo vizuri, hakikisha nywele zake zinakuwa safi, gharama zote utanitumia kwenye simu yangu, pia kuna chumba cha Saloon, kina vifaa karibia vyote, kasoro mafuta na mapambo mengine” alisema Sebastian kabla ya kuondoka zake.*******

Naam siku ile ya juma mosi, mama Anna na mzee Mdemu walikuwa katika hali ya amani mioyoni mwao, baada ya kuona mgonjwa wao ameamka akiwa anajitambua na kuongea vizuri, hal ambayo iliwafanya ata wakina mzee Mwaisaka waondoke pale Mafinga kuelekea kijijini Malangari, wakiwa weye furaha na amani, japo vichwani mwao walikuwa wanajiuliza nini kimetokea, na kupekelekea Anna afanikiwe kupata zile fedha nyingi, ambazo zime wasaidia ata wao kupata nauri ya kurudia kijijini.

Mzee Sinyangwe akiwa tayari anajisikia vyema, na sasa alikuwa kitandani anapata chakula laini, ambacho ni mzee Mdemu, na mke wake pekee ndio walio fahamu kuwa, kililetwa na yule bwana alie waletea fedha jana jioni. “nikama tulikuja na Anna yupo wapi, au amerudi kijijini, na mme pata wapi fedha za matibabu, maana na kumbuka tulikuwa, tulikuwa tuna zungumzia laki nane?” aliuliza mzee Sinyangwe aliekuwa amelala kitandani anasaidiwa kulishwa na mke wake, ambae pia alimsimulia kila kitu kilivyo kuwa, kuanzia pale walipo nyimwa msaada na mzee Kizinge, na wao kuamua kutembea kwa mguu, wakisaidiwa na mzee Mdemu na vijana wake.

Pia mama Anna alieleza juu ya maamuzi ya Ana kwenda dar es salaam, kukutana na Masoud, ambae tayari imesha thibitika kuwa, amesha acha shule na sasa anafanya kazi kwenye kiwanda, japo awa kueleza mambo ya ndani ya mausiano ya Masoud na mchumba wa boss wake, ila pia walisimulia jinsi Ana alivyo mfumania Masoud na mwanamke ambae ni mfanyakazi na ni mchumba wa mtu.

“lakini bahati nzuri Ana akapaya msaada, toka kwa boss wa kiwanda hicho, na mpaka sasa yupo kwake, na ndie alie mpatia msaada wa fedha hizo, kupitia mtu ambae ni mwenyeji wa hapa mafinga, ndie anae hakikisha kila kitu hapa tulipo” alimaliza mama Anna, na kumfanya mzee Sinyangwe aachie tabasamu la furaha, “bwana Mdemu si unavocha kwenye simu yako, naomba niongee na Anna?” aliuliza mzee Sinyangwe, akionyesha kuwa na mashaka flani juu ya swala la binti yake Ana kwenda Dar es laam, “tutanunua vocha tukitoka nje….” akumaliza kuongea tayari simu ya bwana Mdemu ikaanza kuita, “bahati nzuri Ana mwenyewe huyoooo anapiga” alisema mzee Mdemu, huku anapokea simu na kumpatia mzee Sinyangwe.********

Naam! sasa twendeni kiwandani, kule kinyerezi, ambako tuna mwona Salma akiwa ofisi kwake, ana jaribu kuweka sawa hesabu zake, kwenye daftari za kutunzia kumbu kumbu, huku kichwani mwake anawaza na kuwazuwa, sababu ya kadi za benk kukataa kufanya kazi, huku moja ikimezwa kabisa, ngoja aje nimbembeleze aende akanichukulie ile moja haraka, maana vinginevyo, maisha ya Masu yatakuwa magumu” aliwaza Salma, huku kichwanike anapanga namna ya kuhawa  muda wake vyama, na kuzidisha usiri, wa penzi lake, na Masoud, akizingatia kuwa, pengine hivi karibuni, yeye na Seba, wangeweza kutangaza, kuanza kwa vikao vya harusi yao, “sasa inabidi nimfungulie biashara yoyote, ili aondoke hapa kiwandani, maana akiendelea kuwa hapa, tunaweza kushtukiwa, na mimi nikaachika, aliwaza Salma, ambae kiukweli, ukiachilia mchezo mchafu anaofanyiwa na kichaja huyo wa kuingiliwa kinyume na maumbile, mchezo ambao yeye mwenyewe Salma ndie alie mfundisha Masoud, hakukuwa na nachochote ambacho Masoud alimfikia Sebastian, yani kuanzia utanashati, umbo, fedha, elimu, ata ujuzi wa kulea nakutunza mwanamke, iwe kwa huduma za nje, na kitandani kwenye kupeana dudu. …….endelea….



UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA HAMSINI NA SABA
MTUNZI @MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA SITA: “sasa inabidi nimfungulie biashara yoyote, ili aondoke hapa kiwandani, maana akiendelea kuwa hapa, tunaweza kushtukiwa, na mimi nikaachika, aliwaza Salma, ambae kiukweli, ukiachilia mchezo mchafu anaofanyiwa na kichaja huyo wa kuingiliwa kinyume na maumbile, mchezo ambao yeye mwenyewe Salma ndie alie mfundisha Masoud, hakukuwa na nachochote ambacho Masoud alimfikia Sebastian, yani kuanzia utanashati, umbo, fedha, elimu, ata ujuzi wa kulea nakutunza mwanamke, iwe kwa huduma za nje, na kitandani kwenye kupeana dudu. …….endelea….

Wakati Salma anawaza hayo, pasipo kujuwa kuwa kuna mambo mazito yanafwatia mbele yake, mala akasikia mlango wa ofisi yake ukigongwa taratibu, “nani?” aliuliza Salma kwa sauti ya ukali kidogo, lakini akukuwa na jibu lolote zaidi ya mlango kugongwa tena.

Hapo moja kwa moja Salma akahisi kuwa, gongaji atakuwa ni Sebastian, “nani wewe unajifanya bubu” aliuliza Salma kwa sauti ya juu kidogo, huku anajiweka sawa, kuanzia nguo mpaka kilemba chake cha kichwani, pia akafuta namba ya Masooud, katika namba zilizopigwa siku ile.

Safari hii mlango akugongwa tena, ila baada yake, mlango ulifunguliwa, na Salma ambae alishakuwa amejiweka sawa, akatazama mlango, huku amekunja uso kwa hasira, ambayo tunajuwa fika ilikuwa ni yakuigiza, maana alijuwa wazi kuwa anaeingia ni Sebastian, ambae aikuwa na haki ya kuingia mle muda wowote, tena bila kuulizwa na mtu yeyote.

Nikweli Sebastian ndie alie ingia ndani, “hoooo!! jamani baby” alipiga kelele  Salma huku anainuka na kumkukimbilia Sebastian, kisha akamkumbatia kwa nguvu, kisha akampa busu la mdomo, “jamani baby karibu” alisema Salma, kwasauti ya kujidekeza, iliyojaa mahaba, akiwa anajitoa kifuani kwa Sebastian, nakubakia amemshika mikono, “pole baby, yani unaonekana umepooza, vipi umeshaenda hospital, aunikupeleke?” aliuliza Salma kwa sauti ambayo inafaa kutuliza homa.

Ukweli Sebastian moyoni mwake, alikuwa anajitaidi kujizuwia kuongea anacho kifahamu, sijuwi alikuwa amepanga nini kijana huyu, “nimeshaenda, sema kuna mambo lazima niyashugulikie ndio niende nikapumzike” alisema Sebastian kwa sauti tulivu, kama vile akuwa anaitaji kuongea sana kwa wakati ule, “jamani sinunge niambia tu nikusaidie, ujuwe japo atuja funga ndoa, lakini sisi ni sawa na mke na mume, hivyo ni muhimu kusaidiana majukumu” aliongea Salma, maneno yenye busara, kwa sauti, yenye kubembeleza na kusisitiza, “ni wazo zuri Salma, ila usijari” alisema Sebastian, ambae alionyeesha wazi kutokuwa sawa kabisa kwa siku ile.

Naam waliongea mawili matatu, wakiulizana habari za siku nyingi, kuhusu safari na mambo mengine, wakati wote alikuwa anawaza namna ya kumweleza Sebastian juu ya card za benk, lakini baadae akakaza moyo, “alafu baby nimekumbuka” alisema Salma, huku anamtazama Sebastian, kwakuusoma usowake, kwamba anheweza kumsikiliza vyema au ingekuwa kazi bule, kutokana na jinsi hali yake ilivyo, “umekumbuka nini tena?” aliuliza Sebastian ambae sasa alikuwa mbioni kuondoka zake, “wenzio jana wacha card za benk zinifanyie uhuni, yani zote zimegoma, na moja imemezwa kabisaaaa” alisema Salma kwa sauti ya kujidekeza, 

Hapo Sebastian alijitabasamulia moyoni, “ho! kumbe, basi niitaenda kufwatilia” alisema Sebastian, kwa sauti ambayo usinge zania kama alikuwa anaambiwa kwa mala ya kwanza, maana akuwa na mshangao wala wasiwasi, kisha akakageuka na kutaka kuondoka lakini akasita kidogo, na kugeuka tena, kumtazama Salma, “alafu kuna kitu nilitaka nisahau, kwa sasa inabid i uachane na majukumu ya ofisi” alisema Sebastian, kwasauti tulivu pasipo kupepesa macho.

Hakika Salma alishtuka sana, na kuhisi kwamba, labda Sebastian amesha gundua anachokifanya na Masoud, “he! kwanini baby, kwani kuna kitu nimekosea” aliuliza Salma huku macho yamemtoka, “hapana Salma kwanini unasema hivyo, mimi nataka upate muda wa kujiandaa na tukio muhimu, ambalo naamini ata wewe ulikuwa unatamani litokee, maana umelipigania kwa moyo wako wote na kwa nguvu zako zote” alisema Sebastin ambae kichwani mwake ilikuwa inamjia picha ya tukio la Salma kushika meza na yule kijana mfanyakazi akiwa nyuma yake anapita kwenyenjia yenye madimbwi ya tope, kitu ambacho yeye mwenyewe Sebastian asiyo akutamani kujaribu, pia akuwai kufikiria kufanya kitu kama hicho.

Hapo kidogo moyo wa Salma ukatulia, “hooo! kumbe hivyo basi akuna shida, najuwa ela za matumizi utanipatia mume wangu” alisema Salma kwa sauti yenye kujawa furaha na unafuu, “usiwe na shaka, we chukuwa mkoba wako, twende zetu, mimi naenda kalia koo, baadae nitaenda mwenge, kisha niende nyumbani, alafu tuatawasiliana” alisema Sebastian, kwa sauti ile ile ambayo ilimtambulisha kuwa ni mgonjwa, “sawa baby, twende zetu” akiwa hana ili walalile, Salma alichukuwa mkoba wake pamoja na simu, ambayo aliiweka mkobani.

“Sasa hapa atakaa nani?” aliuliza Salma huku anaushika mkono wa Sebastian, kama wapendanao wengine wafanyavyo, nakuanza kutembea kutoka nje, wakipitia sehemu ya mwauzo, ambako kulikuwa na wafanyakazi kadhaa, waliokuwa wanawahudumia wateja, “ofisini atakaa Khasim” alijibu Sebastian, huku wakiendelea kutembea, kuelekea nje, wakiwapita wafanyakazi wengine, walio kuwa wanawatazama kwamacho ambayo yalitoa tafthiri mbaya, nikama mioyoni mwao walikuwa wanajisemea “dah! huyu boya ange juwa anacho fanya huyu kahaba” nikama Salma pia alisha juwa wanacho kiwaza wafanyakazi wale, nae akajisemea kimoyo moyo, “acheni kutoa macho, au mnataka awatomb.. nyie”

“Lakini baby Khasim ataweza kweli?” aliuliza Salma ambae alionyesha wazi kuto kulizia wazo la Sebastiam kumweka huyo Khasim pale ofisini, “kwanini ashindwe, maana naona yeye ndie afadhari kidogo, anaweza kumudu ofisi” alijibu Sebastian, ambae alikuwa ameona jinsi wafanyakazi wake walivyokuwa wanamsimanga kwa macho, “bora tungemweka mfanyakazi mmoja hivi, yeye amemaliza chuo VETA, anaitwa Masoud” alisema  Salma kwa sauti ya kubembeleza. …….endelea


UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA HAMSINI NA NANE
MTUNZI @MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA SABA: “Lakini baby Khasim ataweza kweli?” aliuliza Salma ambae alionyesha wazi kuto kulizia wazo la Sebastiam kumweka huyo Khasim pale ofisini, “kwanini ashindwe, maana naona yeye ndie afadhari kidogo, anaweza kumudu ofisi” alijibu Sebastian, ambae alikuwa ameona jinsi wafanyakazi wake walivyokuwa wanamsimanga kwa macho, “bora tungemweka mfanyakazi mmoja hivi, yeye amemaliza chuo VETA, anaitwa Masoud” alisema  Salma kwa sauti ya kubembeleza. …….endelea….

Ilimuuma sana Seba, yani siyo tu kumthariti, lakini bado anajaribu kulitaja jina la mwanaume huyo mbele yake, lakini Seba akakaza moyo, “achana nae lazima tuwe na mzoefu, maana awa wafanyakazi wengine, unaweza kushangaa kuwa alikuwa hapa kwa michongo yake, mwishowe anatuibia na kukimbia zake” alijibu Seba, akiwa anafahamu fika kuwa jibu ilo linge muumiza Salma, sababu Masoud ndie yule jamaa aliekuwa ananyanduana nae ndani ya ofisi siku iliyopita, na ndie mwanaume alie mtelekeza Arianna, licha ya kumsaidia katika elimu na afanikio yake.

“hapana baby, nikijana mstaarabu tu, alafu amesoma mpaka form six, ndio akaenda chuo” alitetea Salma, pasipo kujuwa anavyo ukolokocha moyo wa Sebastian, ambae alikaza moyo, “sawa ebu nimwone kwanza huyu kijana” alisema Sebastian kwa sauti tulivu, ambayo kiukweli ilificha hasira na chuki, akitaka kuona kama kweli Salma anaweza kusimama mbele ya wanaume wawili wanao mchungulia utupu wake, “hooo! baby, leo ajafika kazini, amesema anaumwa” alijibu Salma akijichekesha chekesha, “ingekuwa bora kama ningemwona, atahivyo isitoshe form six na VETA, aiwezi kumfanya awe mzuri ofisini, labda kiwandani” alisema Sebastian, huku wanazidi kkusogelea maegesho ya magari, bado wafanyakazi walikuwa wanamtazama.

Naam walipofika kwenye magari yao, wawili awa waliagana na kwa ahadi ya kuwasiliana baadae, kisha kilammoja akaingia kwenye gari lake, na safari ya kuelekea mjini ikaanza.*******

Naam kule mikocheni A, Anna alifurai sana kusikia sauti ya baba yake, ambae aliongea nae kwa kirefi, akimsimulia jinsi Masoud alivyo mkataa, na kwamba wameshachana siku nyingi, pia alimweleza jinsi alivyopata msaada kwa kijana ambae pia ni mhanga wa Masoud, baada ya kutembea na mchumba wake, “nimepata nguo mpya, na baadae ananipeleka kutembea kalia koo, lakini huku kote ni mjini tu” alisema Anna akionyesha kuwa mwenye furaha, kitu ambacho kiliondoa wasiwasi wa wazazi wake, juu ya uwepo Anna huko Dar es salaam, ambako kiukweli katika kumbukumbu zao, apakuwa na mjomba babu wala shangazi ambae angeweza kuwa mwenyeji wa Ana, endapo angeitaji msahada.

“nivyema kaama umegundua jambo ilo, wewe mwenyewe, maana kama ungeambiwa na mtu mwingine kuwa Masoud awezi kukuoa, usinge amini” alisema mzee Sinyangwe, japo sauti yake ilikuwa ya taratibu, kama wangonjwa wengine, asa wale watokao kwenye operation, lakini alionekana kuwa mwenye furaha.

Naam, aliongea mengi na baba yake asibakishe ata moja, alimsimulia ata uzuri wa chumba alicho alicho lalia, na vyakula alivyo kula usiku, ata chai ya asubuhi ile.

Na wakati Ariana anamaliza kuongea na baba yake, ndipo alipo kuja kuitwa akaingie kwenye chumba cha saloon, ambacho kiliandaliwa kwaajili ya Salma, ambae ndie mkusudiwa wa kuwa mama mwenye nyumba ile, baada yake Anna anakuwa wakwanza kuitumia Saloon ile binafsi, ambako bi Saphia alikuwa ameshafika.******

Ingefaa kuuzunika baada ya kucheka, kwa kile kilicho kuwa kinaendelea kijijini Malangari, kwenye familia ya kina Masoud, nawakusudia mzee Kizinge na mke wake, ya mama yake Masoud, ambao mala baada ya kusikia taalifa ya Masoud, kutuma kiasi cha Tanzania shilingi millioni moja na laki tano, kwaajili ya matibabu ya mzee Sinyangwe, mzee Kizinge mwenyewe, alipiga toka pale nyumbani na kuanza kupita kwa marafiki zake wakubwa, na pia kwa wale watu alio amini waliuzunishwa na kitendo cha yeye na mke wake kuto mpeleka wala kutokwenda hospital, kumwona mzee Sinyangwe, “aya sasa siwalisema sina msaada wowote” angesema hivyo, mala tu baada ya kuwa kuta walengwa wake , au watu wowote walio kaa kijiweni mfano wale vijana wa pale kijijini, wafanyao shuguri zao za kibiashara kati kati ya kijiji yani senta.

Nao kwa kuwa walisha pata ile habari, lakini kwajuwa sifa za mzee Kiainge wange mpambisha moto, ili waskie tambo zake, “kuna nini mzee Kizunge, kwani kuna  mtu amekukorofisha tena mzee mwenye mji wake” na hapo mzee Kizinge angeongea kwa masjisifu na majingambo, “ujuwe bwana, sisi watu wenye akiri zetu, uwa atukurupuki, wao wanataka wote tukimbilie hospital kwa nini sisi ni waganga, lazima wabakie watu wa kufaya mipango ya fedha, sasa kikowapi Masoud amesha watumia millioni moja na laki tano, ayasasa endeleeni kuongea, alisema Kizinge, nakuondoka zake, huku watu wakimsindikiza kwa macho, aibu zime washika, na ujiona wenye hatia.

Wakati hayo yanaendelea kwa mzee Kizinge ambae aliamini angetumiwa fedha muda wowote, toka kwa kijana wake Masoud, kwaajili ya kutengeneza trekta lake, mke wake nae alikuwa njiani anaelekea nyumbani kwa mzee Sinyangwe, “yani mimi nakaa na vyombo vichafu, wakati nyie mpo, alafu mwanangu anawatumia maela mengi hivyo, atamimi mwenyewe ajawai kunitumia” maneno hayo yaliyotamkwa kwa sauti ya wazi ilio jaa hasira yalikuwa kama wimbo, mdomoni mwa mama Masoud, wakati wote alipokuwa anatembea, mfano wa wanajeshi waliokatika zoezi la matembezi, yani rout in martch.

Sasa isitokee ata bahati mbaya, mtu akamsemesha, “vipi mama Msoud, safari yapi tena” hapo mama Masoud angefunguka mwanzo mwisho, “yani sisi tunawasaidia lakini bado wanatusema, etu atuna msaada, atuendi hospital, ebu ona ela iliyomwokoa ametumiwa na Masoud, millioni moja na laki tano, wao wangeweza kweli, au ndio wangetuacha tufie hospital” aliongea mama Masoud kwa sauti ya kusimanga, hapo kwa asie na havari ya utumwaji wa fedha hiyo, angeshangaa, na yule mwenye taarifa angebakia macho chini, kwa aibu, maana idadi kubwa ya wanakijiji, waliisimanga sana familia ya mzee Kizinge, …….endelea


UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA HAMSINI NA TISA
MTUNZI @MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA NANE: Sasa isitokee ata bahati mbaya, mtu akamsemesha, “vipi mama Msoud, safari yapi tena” hapo mama Masoud angefunguka mwanzo mwisho, “yani sisi tunawasaidia lakini bado wanatusema, etu atuna msaada, atuendi hospital, ebu ona ela iliyomwokoa ametumiwa na Masoud, millioni moja na laki tano, wao wangeweza kweli, au ndio wangetuacha tufie hospital” aliongea mama Masoud kwa sauti ya kusimanga, hapo kwa asie na havari ya utumwaji wa fedha hiyo, angeshangaa, na yule mwenye taarifa angebakia macho chini, kwa aibu, maana idadi kubwa ya wanakijiji, waliisimanga sana familia ya mzee Kizinge, …….endelea….

Mama huyu anapofika nyumbani kwa mzee Sinyangwe, anakuta akuna dalili ya uwepo wa mtu yoyote, pale nyumbani, japo mazingira yalikuwa safi, yakionyesha kuwa kuna watu wanaishi, tena wanao zingatia usafi, tofauti na kwake, ambako kunatisha kwa uchafu, kuanzia ndani sakafuni, vyombo jikoni, ata uwanja wa nyumba yake, “wameenda wapi awa watoto, na leo ni jumamosi” alijiuliza mama Masoud, huku anatazama kushoto na kulia, akaona kundi la watoto linacheza nyumba ya tatu toka kwa mzee Sinyangwe.

Pasipo kuuliza, mama Masoud akaanza kutembea kuelekea kwenye lile kundi, “nitawapata tu nyie watoto, lazima mkaoshe vyombo, na mfagie pote pale na kudeki ndani, si mmeshapata shemeji mliekuwa mna mtaka” alisema mama Masoud, huku anazidi kuisogelea ile nyumba, ambayo ni mali ya mzee Mdemu.

Nikweli mama Masoud aliwakuta wadogo zake Anna wote watatu, pale nyumbani kwa mzee Mdemu, wakiecheza na wenzao, “aya nyie wote tuondoke twende nyumbani, kuna kazi za kufanya” alisema mama Masoud, kwa sauti iliyojaa ukali, huku akiwa ameshika kiuno, na macho ameyakaza kwa Stive, ambae ndie mkubwa kuliko wengine.

Ukweli watoto wale awakushangaa wala kushtuka, maana walikuwa wanafahamu kuhusu utaratibu ule, ambao dada yao alikuwa anaufanya, miaka na miaka, hivyo akawasomba wote watatu, nakuondoka nao kama, kuelekea nyumbani kwake, huku wakina Kelvin wakitangulia mbele,  vichwa chini, kama vile wanakondoo wanaoelekea machinjoni, sijuwi wenyewe waliichukuliaje, lakini kwakweli iliuzunisha sana, ata watoto waliokuwa eneo lile walisitisha michezo yao, na kumtazama Stive, na wadogo zake wawili.

Lakini kama ujuwavyo watoto, aikupita ata dakika  tano, mke wa bwana mdemu akatoka nje, aya ebu ingieni ndani, mkanywe chai..” alisema mke wa mzee Mdemu, ambae kabla ajamaliza akasita kidogo, “hivi wakina Stive wapo wapi?” aliuliza mke wa Mdemu, ambae akuwa na watoto wadogo, zaidi ya wale wakubwa, ambao mida hii walikuwa wamesha enda shambani, “wamekuja kuchukuliwa na mama Masoud, amesema waende wakafanye usafi nyumbani kwake, alisema mmoja kati ya watoto waliokuweepo pale nje ya nyumba ile, “ananini huyu mwanamke lakini, au sababu ya hizo ela zao ambazo wametoa kwa matibabu ya mzee Sinyangwe” alisema kwa sauti ambayo ilionyesha wazi kuwa, ajapenda kabisa jambo lile, japo alionyesha kuwa ameshaoata ile taarifa ya fedha zilizotumwa kwaajili ya matibabu ya baba wawale watoto.

“Kuna nini shemeji” mke wa mzee Mdemu, alisikia sauti toka upande wa kulia wa nyumba yake, nae akageuka na kuwaona wakina mzee Mwaisaka na Sanga, wakiingia pale nyumbani kwake, “mama Masoud amekuja kuwa chukuwa wadogo zake Ana, amewapeleka nyumbani kwake wakamsaidie kufanya usafi” alisema mke wa Mdemu, na kuwafanya wakina Mwaisaka, washtuke kidogo, “eti, anaenda kuwafanyisha kazi kama nani, yani licha ya yote waliyo wafanyia, bado anawachukuwa na kutaka kuendelea kuwatumikisha” alisema mzee Sanga, huku ananaanza kutembea kuongoza upande wa nyumbani kwa kina Masoud, ambako mama Masoud na wakina Stive wameelekea dakika chache zizilizopita.

“Sanga ebu nisubiri kidogo” alisema Mwaisaka, huku anaingiza mkono mfukoni na kutoa noti nne za elfu kumi kumi, “shemeji amenipatia bwana Mdemu, nije nikupe, na kule hospital hali ya mgonjwa inaendelea vizuri, pengine mpaka jumatatu anaweza kuwa amesha luhusiwa” alisema mzee Mwaisaka, huku anampatia mke wa Mdenu, “lakini shemeji, mbona mbio mbio mnaelekea wapi?” aliuliza mke wa Mdemu, huku anapokea zile fedha, kwa lengo la kuwazuwia, ili wasikutane na aibu ya mwaka, “shemeji atuwezi kuwaacha waendelee kuwatumia watoto awa wakati kila kitu kipo sawa” alisema mzee Mwaisaka huku anaondoka kumuwai mzee Sanga, ambae alikuwa amesha piga hatua nyingi tu, “lakini muende mkijuwa kuwa wenzenu ndio wametoa hayo mamilioni ya matibabu” alisema mke wa mzee Mdemu, kwa sauti ya kutupia, yani ile ambayo mtu ongea na mtu anae enda, “nani kasema, hao washenzi awajatoa ata shilingi mbovu” alijibu Mwaisaka na kumfanya mke wa Mdemu, atoe macho ya mshangao.*******

Naam kijana Tino akiwa ndani ya gari dogo aina ya Toyota stallet, yupo njiani, nyuma ya gari la Salma, ambalo lilikuwa limetanguliwa na magari mawili, kabla ya gari la Sebastian, niwazi Tino akutaka Salma amwone anawafwatilia, japo lengo ni kufwatilia mienendo ya Sebastian ambae wazazi wake walikuwa na hofu ya matokeo yafumanizi, lakini pia kama Salma angemwona angeshtuka kuwa anwafwatilia, sababu anamfahamu.

Mala akaona simu yake inaita, nae akatazama kuona nani anaempigia simu, “Seba, au amesha juwa kuwa ninamfwatilia” alijiuliza Tino, huku anapunguza mwendo, na kuipokea ile simu, “ndiyo braza Seba, mambo vipi?” alisema Tino mala baada ya kuweka simu sikioni, poa tu Tino, pane zipi mida hii?” aliuliza Seba akionyesha kuwa ajuwi kama Tino yupo nyuma yake, “nipo mitaa ya buguruni kuna mishe nazifanya, vipi kunainshu kaka” aliuliza Tino, “ndiyo, nataka uende umfwatilie Salma kila hatua, na uchukue video n a vicha za matukio yote machafu, na huyu jamaa yake, sasa Salma anaelekea Sinza” alisema Sebastian, “aina shida kaka, naelekea huko” alisema Tino, na Sebastian akasisitiza, “hakikisha ajuwi kama unamfatilia”.********

Naam sasa tunamwona mama Masoud, akiwa amekaa kwenye kiti, pembezoni mwa ukuta wa nyumba yake kubwa, huku mbele yake watoto watatu wa mzee Sinyangwe wakiwa wamejigawa kila mmoja na jukumu lake, wakati mdogo kabisa wakike, mwenye miaka nane, akiwa ameshika ndoo, anaenda kuchukuw amaji bombani akadeki ndani, wakati huo huo Stive alikuwa amesimama mbele ya lundo moja kubwa sana languo, ambazo ziliitaji kufuliwa, na huyu mwingine wakike wa kati, yeye alikuwa anakinga maji, ili akaoshe lundo la vyombo, ambavyo vilikuwa vina nuka kama mzonga wa fisi, kutokana na kukaa muda mrefu na mabaki ya chakula. …….endelea….

UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA SITINI
MTUNZI @MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA TISA: Naam sasa tunamwona mama Masoud, akiwa amekaa kwenye kiti, pembezoni mwa ukuta wa nyumba yake kubwa, huku mbele yake watoto watatu wa mzee Sinyangwe wakiwa wamejigawa kila mmoja na jukumu lake, wakati mdogo kabisa wakike, mwenye miaka nane, akiwa ameshika ndoo, anaenda kuchukuw amaji bombani akadeki ndani, wakati huo huo Stive alikuwa amesimama mbele ya lundo moja kubwa sana languo, ambazo ziliitaji kufuliwa, na huyu mwingine wakike wa kati, yeye alikuwa anakinga maji, ili akaoshe lundo la vyombo, ambavyo vilikuwa vina nuka kama mzonga wa fisi, kutokana na kukaa muda mrefu na mabaki ya chakula. …….endelea…

Hakika ilitia simanzi, kila mmoja alijiuliza atamalizaje zile kazi, leo ndio waligundua kwanini dada yao alizeeka kwa haraka kuliko wanawake wengine wa umri wake, “fanyeni haraka bwana, yani mimi nifanye kazi nyie mpo, na huduma zote mnapata” alisema mama Masoud akioongezea kuwa, “na ole wake mtu alipue, atanitambua” kama ulikuwa ujuwi, basi nakudokeza kuwa mama Masoud nikama alikuwa amekasirishwa na kitendo cha kusikia kuwa, kijana wake Masoud ametuma fedha, kwa mama Anna kwaajili ya matibabu ya mzee Sinyangwe, “mnazani millioni moja na laki tano mchezo, sisi wenyewe ajawai kututumia ela kama hizo, ebu fanyeni kazi huko, tena mmalize haraka” alisema mama Masoud kwa sauti ya ukali kiasi cha kuwafanya wale watoto, asa yule mkubwa aone kuwa sasa ile imekuwa ashabu, na siyo kusaidia kazi kama dada yao anavyofanya.

Wakati watoto wanaangaika kukinga maji, ili waanze kazi, mala akaingia mzee Kizinge akaingia, “we mwanamke ni hatari sana, ume watoa wapi awa wakwe zako?” aliuliza mzee Kizinge huku anacheka, kicheko cha sanifu, “nimewakuta wacheza cheza tu, wakati kunakazi za kufanya, si wanataka dada yao aolewe, sasa akuna ndoa ya bule bul…” kabla ajamaliza akakatishiwa na sauti toka kwenye upande wa kulia wa jiko lao la nje, “ndoa hipi unaizungumzia shemeji, ambayo awa watoto wanaitaka” asiyo tu, Kizinge na mke wake, ila pia ata wale watoto wakina Stivin, waligeuka upande huo, kutazama nani alie ongea maneno hayo kwa sauti kali iliyojaa jazba.

Hakuwa mtu mmoja, ila walikuwa ni watu wawili yani mzee Sanga alie tangulia mbele, na mwaisaka alie fwatia nyuma, huku wite wawili nyuso zimekujamana kwa jazaba, “henheee!!! mme jileta wenyeweeee” alisema mzee Kizinge, ambae sasa aligeuka mzima mzima na kuwatazama wazee wale wawili, ambao walishangazwa na kujiamini kwa mzee Kizinge, “aya sasa kiko wapi, mlisema eti hooo sina ubinadamu, simsaidii mgonjwa, aya sasa ongeeni, bila masoud mgonjwa siangewafia huku mnamwona huyo” alisema mzee Kizinge, kwa sauti yenye kusimanga.

Hapo mwaisaka na Sanga wakatazama, kwa mshangao mkubwa zaidi ya ule wa mwanzo, na kumfanya mke Kizinge acheke kicheko kikali cha dharau, “lime washuka, wanazani sisi masikini kama wao” alisema mama Masoud, “Kizinge Masoud amefanya nini?” aliuliza mzee Sanga kwa sauti yenye kushangaa, “msijifanye hamjuwi, kwa taharifa yenu hapa kjijini, kila mtu anafahamu kuwa Masoud ametuma fedha nyingi za matibabu ya huyo mgonjwa wenu anae tuletea lawama kila kukicha” alisema mzee Kizinge, kwa dharau, huku mke wake akiendelea kuachia kicheko cha chake cha kuchukiza, “ebu nyie acheni kusikiliza mambo ya huku, choteni maji muanze kazi” alisema mama Masoud, na hapo nikama walizidi wakuwatibua wazee awa wawili.

Mzee Sanga aliwageukia wakina Stivin ambao sasa walikuwa wamesmama bombani, wakisubiri ndoo ya kwanza ijae, na wao wakinge nyingine, kisha akamtazama mama Masoud, kwa macho yenye kujaa hasira kali sana, “hivi we mama umesahau uchungu wa watoto, mpaka unawafanyia hivi watoto wamwenzio namna hii?” aliuliza Sanga, na Mwaisaka akadakia, “eti kisa sijuwi mtoto wenu ametuma ela kwa mama Anna, nani amewadanganya kuwa Masoud ametuma millioni moja na laki tano, kwa mama Anna?” aliuliza mzee Mwaisaka kwa sauti yenye hasira na uchungu, Kizinge na mke wake wakatazama, na kujikuta wakicheka kwa dharau, “wanazani atujuwi” alisema mzee Kizinge uku yeye na mke wake wakiendelea kuangua kicheko, na kuwafanya wakina mzee Sanga nao watazamane, kwa mshangao wakushangaa akili za mzee Kizinge na mke wake.

Hapo ghafla wakajikuta baada ya kukasirika, sasa wakaangua kucheko kikubwa cha masikitiko, kicheko ambacho kilizima kicheko cha mtu na mke wake, ambao waliwatazama wakina mzee Mwaisaka kwa macho yenye viulizo, “labda bwana Kizinge ufahamu, kuwa wewe na mwanao Masoud, roho zenu ni sawa kabisa, hamkumbuki wala kuthamini kile familia ya Sinyangwe ilicho wafanyia, labda nikubaliane na wewe kuwa bwana Sinyangwe alitumiwa million moja na laki tano, nabado anapata maitaji yote, anatibiwa kama mtu maalumu, mke wake anakula vizuri, lakini fedha hiyo aijatoka kwa Masoud, alie kuambia amekudanganya” alisema Mwaisaka, na hapo Kizinge achama mdomo kwa mshangao, huku wakina Stivine waki watazama wazee awa, na kuwasikiliza kwa umakini, “ata sisi tulijuwa hivyo mwanzo, maana Anna alienda dar kufwata fedha kwa masoud, baada yake Masoud amekataa Ana na kumfukuza kama amjuwi” alisema Mwaisaka, na kuzidi waduwaza Mzee Kizinge na mke wake.

Hapo Sanga akamgeukia Stivin, aliekuwa amesimama pale bombani na wadogo zake, “Stivin wachukuwe wadogo zako nendeni mkanywe chai, kwa mama Mdemu, namsije mkamsikiza tena huyu mama, kuja kufanya kazi hapa kwake, dada yeni siyo mchumba wa masoud tena” alisema mzee Sanga, kwa sauti yenye hasira, na hapo kama vile wamefunguliwa toka jela, Stiven na wadogo zake walikimbia mbio, kuelekea wakipita ile njia waliyojia wakina mzee Mwaisaka, wakisahau ata kufunga bomba la maji.

“kwanza nilijuwa tu, Masoud awezi kuwa na binti mchafu kama yule, yani aache wanawake wazuri aje kuwa na mwanamke asie eleweka, kama huyu” alisema mama Masoud, kwa sauti aliyoamini ni yachini, lakini iliwafikia wakina Sanga, ambao waliangua kicheko kikubwa sana, cha kumcheka mama huyu, ambae alishangaa pia, “we mama we, labda nikuambie kitu, kaa tayari kwa makubwa zaidi” alisema Mwaisaka, huku anageuka na kuanza kutembea, huku Sanga akimaliza kwa onyo kali, “na ole wenu muwatumikishe tena awa awa watoto tuna wapeleka polisi” alisema Sanga kisha nae akaanza kutembea kumfwata mwenzie, wakaondoka zao kuwafwata wakina Stivin kule walikoelekea. ENDELEA…. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu