Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Jumatano, 21 Mei 2025

Hadithi: A CROWN OF BADNESS EP 31-35








TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Sehemu 31.

Mr Derick mambo ya waganga ndo alikuwa hataki kabisa, ila aliogopa kumbishia mama Jacob, kwa sababu angebishia angeanza kuonekana yeye ndo kalichukua lile box, kwa hiyo ilibidi awe mpole.

Huku Jacob na fatuma Naye walikuwa wanaumiza kichwa namna ya kuzitumia nyaraka zile ili kila kitu kiende vizuri, yaani uzuri kila kitu kilikuwa kipo kwenye lile box yaani kuanzia mihuri yoye ya mmiliki wa mali zote yakiwemo makampuni yote, mihuri ya kutolea pesa benki ilikuwepo na nyaraka zote ziliandikwa kwa jina la Jacob na uzuri picha za Jacob zilikuwepo kwenye nyaraka zote, ila walicho kuwa wanahofia ni kwamba Jacob akijitokeza hadharani atakamatwa tena kwa tuhuma za kutoroka gerezani na kuidanganya jamuhuri kwamba amefariki.

"Jacob ninacho omba kitu cha kwanza twende kwa waziri wa mambo ya ndani tukajieleze kila kitu na yule akikubali hapo tutakuwa tumepiga hatua kubwa mno" Fatuma alitoa wazo

"Fatuma huoni kama ndo hatari zaidi? Yaani we unafikiri upande mmoja tu je huyo waziri akikataa? Au unafikiri tu upande wa kukubali na je unafikiri anaweza kubali bila kumpa kitu chochote??" Jacob alikuwa kajawa na wasiwasi maana swala la kwenda kunyea debe tena ndo alikuwa hataki kabisa.

"Jacob tunaenda kujaribu tu, nina imani atakubali kuhusu kitu cha kumkabidhi we fikiria mwenyewe si unaweza kumuahidi hata kumuachia kile kiwanda chenu cha vinywaji unafikiri atakataa? ila ukiwa mgumu hapo ndo ujue ugumu utakuja" Fatuma alitoa wazo ambalo lilimfanya Jacob afikirie sana.

Kutokana na Jacob hakuwa na njia nyingine alikubaliana na wazo la fatuma, hapo ilibidi waanze michakato ya kumtafuta waziri, ilikuwa ni ngumu sana kwa upande wao kukutana na waziri moja kwa moja kwa sababu walikuwa ni watu wasio julikana kabisa.
Iliwachukua mwezi mzima wakiwa wanapambana kukutana na waziri, na muda wote huo Jacob alikuwa anajificha mno ili asionekane hovyo na alikuwa kila akitoka kwenda kutembea lazima avae mzuhura unao ziba uso wake.
Basi siku moja wakiwa pale nje ya geti kuingia ofisini kwa waziri na walikuwa wanabishan na walinzi maana kila siku walinzi walikua wanatia ngumu kuwaruhusu watu hao kuingia, sasa siku hiyo ilibidi akina Fatuma wawe wakali na yalikuwa ni makelele ya kufa mtu hapo nje, na bahati nzuri waziri mwenye ndo alikuwa anapita kuingia ofisini alipo kuta makelele hayo na sababu ya makelele aliwaruhusu kina Fatuma kuingia ndani na hiyo ndo ilikuwa bahati yao.
Baada ya kuingia ndani walienda moja kwa moja kwenye ofisi ya waziri mwenyewe kwa sababu ilikuwa ni order ya waziri kwamba waingie moja kwa moja.
Walipo ingia fatuma ndo alianza kuelezea kila kitu mwanzo mpaka mwisho na lengo la wao kwenda pale.
"Nyiee nyosheni maelezo yaani mnataka mi niwasaidie nini sasa??" Waziri alikuwa kama hawaelewi vile.

"Mheshimiwa tunachotaka kutoka kwako ni wewe kutulinda sisi na ikiwezekana kumtakasa huyu kwamba hakuhusika na hayo mauaji" Fatuma alizidi kuelezea

"Hivi nyie watoto mmechanganyikiwa eeeeee? Yaani mmenyosha kwangu kuja kueleza ujianga kama huo au mnaona ni kazi rahisi rahisi tu, sasa nawaambia mi si shughuliki na mambo ya ovyo kama hayo na nyie mtakuwa mfano mnaenda kuozea jera" Waziri alikuja juu baada ya kuona anaambiwa upuuzi.

Hapo Jacob na fatuma walianza kutetemeka maana waliona kila kitu kinaenda kuwa tofauti.
Jacob ilibidi atoe nyaraka zote na kuweka mezani na kutoa maelezo mengine na alimwahidi waziri kwamba endapo atawasaidia anaachiwa kiwanda cha vinywaji kinakuwa cha kwake.
Waziri alipo cheki zile nyaraka na kusikia maneno ya Jacob kwamba anaachiwa kiwanda, taratibu taratibu alianza kutabasamu na kuonesha meno yake.

"Sasa nyie vijana si mngeongea hivyo toka mwanzo, si unajua Sisi kazi zetu zinahitaji Zaid pesa, basi kuhusu hilo ondoeni shaka kabisa ila kikubwa mzingatie ahadi yenu, kwa hiyo kuanzia Saiz we kijana kuwa huru na mambo yako hakuna atakaye kubuguzi mengine yote niachie mimi ila wewe pambana na hao ndugu zako" waziri Aliongea maneno ambayo yaliwafanya akina Jacob nyuso zao zitabasamu.
Basi akina Jacob na waziri walikubaliana kila kitu na kazi ilibaki kwa akina Jacob kuikamilisha wao.

"Jacob kitu cha kwanza tufanye mpango twende benki tukafunge akaunti zote zenye jina lako arafu mambo mengine yatafuata" Baada ya kufika nyumbani, Fatuma alitoa wazo ambalo Jacob alikuwa hana upinzani.

Basi hawakutaka kuchelewa baada ya siku moja walienda benki, na walipo fika kutokana na swala lao kuwa zito kidgo ilibidi wapelekwe kwa manager wa benki ndo wakaongee naye, walitoa nyaraka zote na mihuri ambapo kweli ilionekana Jacob ndo mhusika haswa wa akaunti zote za benki.
Kiufupi Baba yake na Jacob alikuwa ni mtu tajiri na maarufu na alikuwa anamiliki makampuni kadhaa pamoja na kiwanda kimoja ambacho ndo hicho wameahidi kumuachia waziri na kila kampuni ambalo alikuwa kalifungua alifungua na akaunti yake benki, kwa hiyo makampuni matatu ambayo yaliku
Yanamalikiwa na Mr Deus pia kulikuwa na akaunti tatu benki ambazo kila kampuni lilikuwa na akaunti yake ukiachana na kiwanda.

Basi akina Jacob baada ya kutoa uthibitisho wote manager wa benki alikubaliana na wao kuzifunga akaunti hizo kwa muda mpaka pale watakapo amua vingine.

Huku upande wa akina Mr Derick walikuwa hawajui kinachoendelea wao walikuwa wamepanga kwenda kwa mganga kuagua nani aliye iba lile box la nyaraka na walikubaliana kwamba awamu hii wanasafiri mpaka mkoani kabisa.


Itaendelea......

Usikose sehemu ya 32.





TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     

Sehemu 32.

Huku upande wa akina Mr Derick walikuwa hawajui kinachoendelea wao walikuwa wamepanga kwenda kwa mganga kuagua nani aliye iba lile box la nyaraka na walikubaliana kwamba awamu hii wanasafiri mpaka mkoani kabisa.

Mr Derick aliwachukua wake zake wote wawili kama walivyo kubaliana na safari ya kwenda mkoani ilianza, kwa kuwa walikuwa na usafiri wao walitumia masaa kama sita kufika huko waliko kusudia na walienda moja kwa moja mpaka kwa sangoma waliko elekezwa.
Basi walifika kwa mtaalamu huyo ambaye alikuwa yupo kijijini kabisa na alikuwa kajitenga na makazi ya watu kabisa na huyo mtaalamu alikuwa anaaminika kwa mambo mengi mno.

Walipo fika walielezea shida yao iliyo wapeleka, baada ya yule mganga kuangalia kwa utaalamu wake badala ya kuwaambia alianza kucheka.

"Doctor vipi mbona unacheka tena kulikoni??" Ilibidi Mr Derick aulize maana alikuwa haelewi

Doctor alianza kutoa maelezo na aliwaelezea kuhusu Jacob, kitu walicho shanga wao na kuanza kumtilia mashaka yule mganga ni baada ya kuwaambia Jacob hakufa na yupo hai na ule siyo mzimu ni Jacob mwenyewe na yeye ndo kachukua kile kibox kwa kuwa ni mali zake.
hapo Mr Derick ilikuwa haimuingii akilini kabisa yaani alijionea mwenyewe Jacob kafa na walienda kuzika akiwa anashuhudia alafu huyo mganga anasema eti Jacob yupo hai, hapo Derick aliona ni upuuzi mtupu.

"Oya nyie mpeni hela yake tuondoke, huu ni ujinga" Mr Derick alipaniki na kuwaambia akina Vicky kwamba waondoke maana akikuwa haelewi kile kinachozungumzwa na yule mtaalamu.
Basi walimpatia pesa yake yule mtaalamu ila alikataa kuichukua maana aliwaambia matatizo yao yeye hawezi kuyatibia na aliwaambia washachelewa, ila wao hata hawakujali.

"We mwanamke umeona ujinga wako ninao kukatazaga kuhusu hao waganga wako? Umeona sasa ujinga anao twambia? Yaani Jacob tulimshuhudia wenyewe akiwa amekufa leo huyu mpuuzi anakuja kutwambia eti yupo hai??" Mr Derick baada ya kufika kwenye gari alianza kugomba maana alikuwa haelewi.
Hapo ilibidi wake zake wafanye kazi ya kumtuliza na walimshawishi waende kwa mtaalamu mwingine wakathibitishe waone.

Kweli walikubaliana na waliamua waende kwa mtaalamu mwingine ili walinganishe majibu, ila baada ya kwenda waliambiwa majibu yale yale kama waliyo ambiwa mwanzo na mtaalamu wa kwanza, walizunguka Zaid ya watalamu watano majibu yalikuwa ni yaleyale.

"Derick mi nahisi siku ile tumeenda kule gerezani kuangalia maiti basi kuna mchezo tulichezewa" Mama Jacob alianza kupata wasi wasi

"Uuuuuuu, ila hata kama kweli Jacob yupo hai basi atakuwa ni mchawi maana nakumbuka siku ile tulimuacha kule porini alafu tukamkuta mjini anatusubiri au nyie mshasahau??" Mr Derick bado ni kama alikuwa haamini vile.

Basi walikubaliana kwamba wakifika nyumbani inabidi waanze kufanya uchunguzi mara moja.

Walipofika mjini Vicky alienda kwake na Mr Derick na Mama Jacob nao walienda kwao.

Ila Vicky alipo fika kwake alikuta mazingira ya nyumbani yamebadilika na alikuta milango imefungwa na watu walikuwa wanalinda pale getini.
Vicky alipojaribu kuuliza aliambiwa mwenye nyumba kaifunga na kasema haruhusiwi mtu yeyote kuingia, Vicky alianza kuleta vurugu maana hakuamini na alikuwa anaambiwa mwenye nyumba wakati mwenyewe anajua mwenye nyumba ni Mr Derick na ndo walikuwa naye siyo muda sasa hao wanaosema mwenye nyumba kasema, kawaambia wapi, yaani Vicky hakukubaliana nao na aliomba wamuache aingie ndani.

Kutokana na ubishi wa Vicky alipigwa kipigo cha mbwa koko na hapo ujanja ulimuishia ilibidi ageuza na kwenda kwa Mr Derick kule anako kaa na Mama Jacob.

Baada ya kufika alitoa maelezo ambayo hata mr Derick na Mama Jacob walishangaa

"Vicky hivi unacho ongea wewe ni kweli ama? Nani kakufukuza" Mr Derick hakuamini maneno ya Vicky kwamba kazuiwa kuingia ndani.
"Bana eeeee, mi siwajui wanasema mwenye nyumba ndo kafunga na wamesema mtu haruhusiwi kuingia pale." Vicky akiwa analia alitoa maelezo

"Ebu twende huko huko upumbavu mi staki mwenye nyumba yupi wakati nyumba ni yangu" Mr Derick alinyanyuka kwa hasira huku akiwa anatema cheche maana aliona watu wameanza kumzoea.

Mr Derick na Vicky walifika mpaka pale nyumbani kwa Vicky bado walikuta nyumba inalindwa na watu.
Mr Derick kwa jaziba alishuka kwenye gari akiwa katumbua macho.
"Mpuuzi gani ambaye kawaweka hapa?? Na nani anayezuia mke wangu kuingia humu ndani??" Mr Derick alifika pale na kuanza kuongea kwa Jazba

"Mzeee tulia na uwe mpole kwenye nyumba za watu, hapa kwako we una uthibitisho??" Jamaa mmoja aliongea kwa sauti nzito na jicho lilikuwa jekundu na inaonekana alikuwa hataki masihara kabisa kwenye kazi.

Mr Derick baada ya kuambiwa ana vithibitisho vya kuonesha pale ni kwake alibaki kujing'ata tu maana alikumbuka kwamba nyaraka zote ziliibwa.
Ila Mr Derick alikuwa bado hakubaliani na watu wale kukaa pale kwake maana alikuwa hataki kukubali kunyang'anywa makazi kizembe vile.
Baada ya wale walinzi wa pale kuona Mr Derick ameanza kuleta vurugu walianza kumshushia kichapo, jamaa alichapika mpaka akawa anaona kama mvua inanyesha wakati bado kuna jua yaani dunia ilikuwa inazunguka.
Hapo ilibidi Mr Derick na Vicky wapande kwenye gari na kurudi kule waliko toka maana walikuwa hawana namna.

Jacob na Fatuma walikuwa wameanza opereseheni ya kuweka kila kitu kwenye himaya yao na walianza kutembelea yale makampuni yote, walianza kwenye kampuni linalo husika na uuzaji wa magari, pikipiki na vitu vingine vyote vya moto na walipo fika huko walisafisha wafanyakazi wote ambao walionekana wabishi na manager alitolewa na kuwekwa mwingine.
Yaani walifanya hivyo kwa kila kampuni ambalo lipo chini ya Jacob.

Mr Derick huku nyumbani alikuwa haelewi kile kinacho endelea na kila kitu kilianza kwenda tofauti maana alienda benki kutoa pesa ili amununulie Vicky nyumba nyingine ila alikuta akaunti zote zimefungwa, alijaribu kwenda kwenye kila kampuni lake analo miliki mambo yalikuwa yapo tofauti maana kila aliko enda alikuta wafanyakazi ni wapya na mambo yamebadilika.

Mr Derick baada ya kupeleleza kwa kina aligundua mtu anaye husika na yote hayo ni Jacob mwenyewe hapo ndo alipata uhakika kwamba Jacob ni kweli hajafa.


Itaendelea......

Usikose sehemu ya 33



TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     


Sehemu 33.

Mr Derick baada ya kupeleleza kwa kina aligundua mtu anaye husika na yote hayo ni Jacob mwenyewe hapo ndo alipata uhakika kwamba Jacob ni kweli hajafa.

"Duuuuuu!! Hapa kazi ipo naona Jacob ameamua kurudisha kila kitu chake yaani hapa tukizembea tumekwisha na tutaumbuka hapa mjini" Mr Derick alikuwa kakaa na wake zake wanajadili mambo yalivyo badilika

"Derick tatizo ubishi wako, hivi tungekubali mara ya kwanza tulivyo ambiwa Jacob bado yupo hai tungefika kote huku kweli?? Haya fikiria wakija kuchukua na hapa tutaenda kukaa wapi?? Maana kinyumba chako cha kule uswahilini ndo umepangisha chote" Mama Jacob ilikuwa full kulaumu tu

"Kitu cha kufanya inabidi tukamfungulie kesi Jacob, maana tayari ana hatia ya kuuwa na ukichukulia Katoroka gerezani, hiyo ndo njia pekee maana akikamatwa hapo tutapata nafasi nzuri ya kurudisha kila kitu, na huu mpango ukifeli hatuna namna inabidi tufanye kama tulivyofanya kwa Mr Deus na Mr jomo." Mr Derick kama mwanaume alitoa wazo ambalo halikuwa na upinzani wowote kwa wake zake maana tayari mambo yalikuwa yamewafika shingoni.

Jacob na fatuma Mambo yalikuwa yashaanza kuwaendea vizuri, ila bado walikuwa wanakaa kwenye nyumba ya Mr jomo maana waliona hayo ndo makazi salama kwao ila awamu hii waliongeza ulinzi pale nyumbani maana walikuwa wanamjua vizuri Mr Derick kwamba ni mtu wa roho mbaya anaweza kufanya lolote.

Siku moja Jacob na fatuma wakiwa wametulia nyumbani kwao walishanga kuona askari wanatimba na kuwaweka chini ya ulinzi.
Jacob aliwekwa chini ya ulinzi na sababu kubwa ilikuwa ni kutoroka gerezani na kudanganya jamhuri kwamba yeye amekufa.
Jacob hapo wasi wasi ulikuwa umemujaa na alijua anaenda kunyea debe na akilini mwao walijua Mheshimiwa waziri ashawasaliti, maana tayari walikuwa wamempa kile kiwanda.

Jacob baada ya kufikishwa, kituoni aliswekwa ndani moja kwa moja na akiwa hajakaa sawa kule mahabusu alimuona Baba yake mkubwa anaingia, hapo Jacob aligundua kwamba mhusika ni huyo mzee wake.

"Jacob si nilisikia umekufa imekuwaje tena?? Mbona hukuja nyumbani kama ulikuwa hai??" Mr Derick aliongea kama mtu anaye msanifu Jacob na alitaka kumpima Jacob kwamba anajua mangapi kumhusu yeye.

"Mzee no comments mshindi wewe basi." Jacob aliongea kifupi na maneno machache,Mr Derick alicheka kweli aliona kila kitu kinaenda kuwa vizuri siyo muda.

Jacob alikaa pale kituoni siku kama tatu akiwa bado hajapandishwa mahakamani, huku nje fatuma Naye alikuwa anaparangana kumtafuta waziri kwenye simu ili ajue imekuwaje tena ila ndo hivyo waziri alikuwa hapatikani kwenye simu.

Huku upande wa akina Mr Derick walikuwa wanacheka tu walijua kila kitu kinaenda kuwa sawa siyo muda mrefu maana waliamini Jacob akifungwa gerezani basi kila kitu kitarudi kwenye mikono yao Tena.
"Derick una uhakika lakini kwamba ataenda jera yule mpuuzi??" Vicky aliuliza wakiwa wamekaa nyumbani wanapata chakula, maana tangia Vicky atimuliwe kule walikuwa wanakaa pamoja wote watatu.

"Vicky yule hawezi kupona kesi yake ni nzito, hata hivyo akiponyoka kuna mpango tayari nisha uanda hata maliza siku mbili atakuwa asha kufa" Jacob alikuwa anajikubali na mipango yake haswa.

Huku sero fatuma alienda kumuona Jacob na ilikuwa imebakia siku moja Jacob kupandishwa mahakamani

"Jacob umeona huruma yako sasa? Nilikwambia hata pale wanapo kaa tuwatimue na tuchukue kila kitu, we ukadai unamuonea huruma mama yako atakosa pa kwenda? Unaona sasa yanayo tokea, waziri ndo huyo hapaatikana na kesho mahakamani we huoni kama utarudishwa tena gerezani??" Fatuma akiwa pale kituoni alikuwa anatoa lawama kwa Jacob

"Fatuma huu siyo muda wa kulaumiana, cha msingi we fanya kila njia mi niweze kutoka hapa" Jacob hofu yake kubwa ilikuwa ni kwenda gerezani maana hali ya kule alikuwa anaijua.

Fatuma alitoka pale kituoni, kichwa kikiwa kizito mno na alikuwa haelewi afanye nini.
Akiwa njiani kurudi nyumbani alikuwa anajaribu kumpigia waziri kiutani tu ila alishituka baada ya kuona simu inaita na haikuchukua muda simu ilipokelewa na aliye pokea alikuwa ni waziri mwenyewe.

Fatuma alitoa maelezo ya kile kilicho tokea, waziri alimjibu Fatuma kwamba alikuwa nje za nchi ila siyo muda atashughulikia hilo swala na aliuliza Jacob yupo kituo gani fatuma alimwelekeza, basi maongezi yaliishia hapo.
Fatuma alifurahi mno aliona sasa matumaini yanaanza kuja ya Jacob kuwa huru.

Jacob akiwa kule kituoni ilikuwa ni jioni alishangaa anakuja kuchukuliwa, na baada ya kufunguliwa kule aliko kuwa amefungwa alikabidhiwa vitu vyake na kuambiwa yupo huru, Jacob alibaki kaduwa alikuwa haamini kama yupo huru, alihisi labda ule ni mtego kwake ili wamuue.
Jacob alitoka pale kituoni akiwa makini sana na alikuwa anaangalia huku na kule ili kuona kama kuna mtu anamfuatilia.

Usiku Fatuma akiwa katulia anaangalia TV alishangaa kusikia mlango unagongwa na alipo enda kufungua uso kwa uso na Jacob

"Heeeee!! Jacob tayari ushaachiwa??" Fatuma alishangaa

"Fatuma mi sielewi kwa nini nimeachiwa nahisi labda ni mtego??" Jacob alikuwa na wasiwasi wa kufa mtu maana alikuwa haamini jinsi alivyo achiwa kilaini

"Jacob nimeongea na waziri, itakuwa ni amri yake na amesema haitajirudia tena na huu uzembe umefanyika kwa kuwa yeye alikuwa nje za nchi" Fatuma alimutoa wasi wasi Jacob.

Huku kwa akina Mr Derick walikuwa hawaelewi kitu kinacho endelea, wenyewe walikuwa wamejiandaa kwamba kesho asubuhi na mapema wanaamukia mahakamani kwenda kushuhudia jinsi Jacob anavyo somewa hukumu

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 34.





TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
    

Sehemu 34.

Huku kwa akina Mr Derick walikuwa hawaelewi kitu kinacho endelea, wenyewe walikuwa wamejiandaa kwamba kesho asubuhi na mapema wanaamukia mahakamani kwenda kushuhudia jinsi Jacob anavyo somewa hukumu.

Dakika na masaa yalisogea hatimaye ikawa siku nyingine, ilikuwa ni asubuhi na mapema akina Mr Derick kwa bashasha na furaha walijiandaa na kuondoka pale nyumbani kwenda mahakamani ili wakajionee wenyewe jinsi Jacob anavyo somewa hukumu
"Huyu mtoto awamu hii asipo somewa hukumu ya kunyongwa atakuwa na Mungu wake yaani anacheza na jamuhuri" Derick akiwa kwenye gari na wake zake alikuwa anaongea maneno ya kujifariji na kujitia matumaini na maneno hayo yalifanya wake zake wacheka kwa sauti na kugonga kabisa.
Akina Mr Derick walipo toka tu pale nyumbani kwao gari kama tatu zilifika na alikuwepo Jacob na fatuma, waliambatana na njemba za kutosha, baada ya kufika walimkuta Mr nguna getini, naye nguna baada ya kuwaona alibaki anashangaa shangaa tu maana alikuwa haelewi.

"Mr Nguna kwa kuwa unaishi na wauaji na wewe ni muuaji pia, kuanzia muda huu beba kila kilicho chako kazi imekushinda rudi kwenu, mwenye mji nimerudi" Jacob Aliongea kwa ukali na siku hiyo alikuwa serious hakuna mfano mpaka Fatuma mwenyewe alishangaa kumuona Jacob siku hiyo yupo serious kweli.
"Jacob punguza jazba baba, mbona unaongea kwa munkari hivyo??" Fatuma ilibidi aanze kumtuliza ili atumie tu ustaarabu

"Fatuma we hujui tu, huyu mpuuzi ndo alitoa ushahidi kwamba mimi nilihusika na mauaji ya mzee wangu, huoni kama naye alishiriki??" Jacob alikumbuka ushahidi ambao Nguna aliutoa hapo ndo hasira zilimzidi zaidi.

Ila kutokana na uoga wa bwana Nguna hakutaka maneno mengi, alichukua kila kinacho mhusu na kutimuka pale nyumbani.
Jacob ilibidi awaache walinzi pale nyumbani na alitoa amri kwamba haruhusiwi mtu yeyote kuingia pale ndani bila ruhusa yake na atakaye leta ubishi ale kipigo.

Baada ya maelezo hayo Jacob na fatuma waliondoka kwa speed kali maana siku hiyo walikuwa na mambo mengi ya kufanya.

Mr Derick na wake zake baada ya kufika mahakamani, walishangaa muda unazidi kwenda kesi ya Jacob haisomwi, zinasomwa kesi nyingine tu hapo ilibidi waanze kuulizana kwamba imekuwaje ila hakuna aliyekuwa anajua sababu ni nini.
Hapo iliwabidi waondoke mahakamani na kuelekea kule sero aliko kuwa amefungwa Jacob ili wakapeleleze sababu ya Jacob kuto fikishwa mahakamani.
Walipofika na kuuliza walishangaa kusikia eti Jacob kaachiwa, na walipo uliza sababu za kuachiwa waliambiwa kaachiwa kwa sababu hana kosa lolote, hapo bwana Derick akichoka aliona kitambi chake kinawaka moto maana alijua kazi bado ipo na yawezekana ndo ikawa ngumu zaidi.

"Sasa hapa inabidi plan B ifanye kazi la sivyo huyu mtu atatusumbua" Jacob ilibidi afikirie haraka haraka na aliona kitu cha kufanya ni kumuangamiza Jacob.

Basi iliwabidi wageuze kurudi nyumbani, ila walishangaa baada ya kufika mazingira ya pale nyumbani hayaeleweki maana waliona watu wamejazana pale getini na gari kama mbili zimepaki pembeni.
"Hey nyie vijana mbona mumeweka kambi nyumbani kwangu? Inakuwaje hamuheshimu miji ya watu kiasi hicho??" Mr Derick baada ya kufika tu pale na kushuka kwenye gari alianza kutema cheche maana aliona ni zarau kubwa watu kujazana nyumbani kwake bila hata tarifa yake
"We mzee tunaomba tuheshimiane, na inatakiwa unapo fika kwenye miji ya watu uwe mpole na uulize vizuri sawa eee" nao wale walinzi hawakubaki nyuma walimtolea uvivu.

Mr Derick baada ya kuambiwa hayo maneno, alitumbua jicho kama kadungwa sindano ya tako bila kutegemea na midomo yake ilianza kutetemeka kwa hasira

"Nyie vijana naona mumechoka kuishi eee?? Yaani nyumbani kwangu ndo mnaanza kuniletea masharti? Kwanza aliye waweka hapa ni nani??" Kwa hasira Mr Derick aliongea huku akiwa anatetemeka
"Mzee aliye tuweka hapa ni mwenye hii nyumba, kama unadai hapa ni kwako tupe uthibitisho tunakuacha uingie ndani na sisi tunaondoka" kwa jeuri kabisa wale walinzi walijibu bila hata wasi wasi.

Mr Derick Siku hiyo rangi yake ya asili ndo ilionekana vizuri maana hasira zilikuwa zimempanda mpaka kitambi chake kilianza kutikisika chenyewe, Mr Derick kwa kuwa kila sehemu anayoenda alikuwa kwenye gari anatembea na bastola kwa ajili ya kujiahami, hapo aliamua kurudi kwenye gari ili liwalo na liwe.
Wake zake nao walikuwa wanashangaa kwamba huyo bwana kwenye gari anakimbilia kuna nini? Maana nao walikuwa hawajawahi kumuona akiwa na bastola.

Baada ya Mr Derick kuingia kwenye gari, alitoka akiwa kashika bastola mkononi na hasira zilikuwa zimemupanda ni hatari.

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 35.



TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
    

Sehemu 35.

Baada ya Mr Derick kuingia kwenye gari, alitoka akiwa kashika bastola mkononi na hasira zilikuwa zimemupanda ni hatari.

We bunduki isikie tu, ukisikia wanakwambia kitu cha moto hakinaga mbabe, mwenye misuli au kifua hapo ndo uelewe, yaani zile njemba zote zilizokuwa zikilinda pale getini baada ya kumuona Mr Derick anakuja na bastola mkononi huku akiwa anaikoki hakuna aliyekumbuka kwamba walipewa kazi ya kulinda, yaani kila mtu ilikuwa anajali roho yake na nafsi yake kila mtu aliomba Mungu kivyake na pale ndo ilijulikana kwamba hii nchi ina wana riadha wengi maana speed zilioneshwa pale na vijana zilikuwa siyo za nchi hii, walikimbia kiasi kwamba walisahau na magari waliyo kuja Nayo.
Mama Jacob na Vicky baada ya kuona speed za wale majamaa walisahau kama wapo kwenye matatizo walianza kucheka
"Na nyie wajinga mnacheka nini sasa? Kitu cha msingi tuingie ndani tuhamishe kwanza kila kitu cha maana kiasi kwamba hata wakija kutuhamisha kibabe tuwe tumehamisha baadhi ya vitu" Mr Derick aliongea huku akiwa anahema kwa hasira

"Daaaa!! Mwenzangu acha tucheke tu, umeona yule jamaa mwenye kifua kikubwa alivyo kimbia mbio yaani kama yupo Marathon, Alafu mwenzetu kumbe unatembeaga na siraha kwenye gari na hujawahi kutwambia??" Mama Jacob alikuwa bado anacheka speed za wale majamaa

"Jamani acheni uzembe mambo ya siraha hayawahusu, nyie cha msingi ingine ndani muanze kukusanya kila kitu, nikatafute fuso hapo mbele lije libebe vitu, kwa ajili ya kujihami maana hatujui hao wajinga watarudi muda gani" Mr Derick alikuwa anatoa maelezo huku akiwa anaingia kwenye gari ili akatafute gari kubwa lije lisombe mizigo yote, maana waliona
Wakizembea wanaweza kosa kila kitu.
"Sasa we mwanaume hiyo mizigo tunasomba tunapeleka wapi sasa??" Mama Jacob alikuwa hata haelewi watakako enda??

"Bwana we mi si ndo mwanaume ama?? Mi najua wapi tutaenda nyie tekelezeni majukumu niliyo wapa" Mr Derick Aliongea na kupanda gari kisha aliondoka kwa kasi.

Akina Jacob wakiwa wametulia zao kule wanako kaa wakiwa hawana wasiwasi hata kidogo walishangaa mlango wao unagongwa kwa pupa kweli, Jacob alipo enda kufungua mlango alishanga kumuona yule mlinzi kiongozi aliyemuacha na wenzake kule ili walinde ule mji.
"Heeeee!! We Ediga wewe imekuwaje tena?? Mbona unakuja unahema??" Jacob alishangaa kumuona jamaa aliye julikana kwa jina la Ediga akiwa anahema siyo kitoto.
"Daa huwezi amini boss yule mjinga nusura atumalize na risasi, na sijui kama wenzangu wamepona huko, maana mi risasi ilipita kwenye sikio nikawa nimekwepa kwa kuruka sarakasi! We acha tu" Akiwa anaelezea kilicho tokea bwana ediga aliamua kuongeza na uongo ili aonekane yeye ni hatari
"Duuu!! Huyo mjinga ni wa kuogopwa, kumbe ana bunduki??" Jacob alishangaa
"Boss tena bunduki yake ndo zile za kivita kabisa, unazo zionaga kwenye movies za Vandame" Jamaa alizidi kuongea uongo, ambao ndo ulizidi kumchanganya Zaid Jacob.
"Basi ediga we rudi nyumbani tutaongea kesho" Jacob aliona jamaa kazidisha vitisho aliamua kumuaga na kufunga mlango akazama ndani.

Kesho yake Jacob na fatuma walienda kuchukua askari polisi ili kwenda kumhamisha Mr Derick kinguvu, walifika kwa Mr Derick waligonga kama kawaida na walimkuta Mr Derick hana hata wasi wasi.
Wale askari walimuamuru Mr Derick aondoke maana mwenye nyumba ndo kaamua, kwa kuwa Mr Derick alikuwa hana nyaraka yoyote ya kuthibitisha kwamba pale ni kwake ilibidi aondoke bila hata wasi wasi, alingia ndani aliwachukua wake zake na kutoka nao nje ya geti kabisa ambapo ndo maaskari walikwa wamesimama, maana muda wote askari wanavyotoa amri ya Mr Derick kuondoka walikuwa hawajaingia ndani.
Basi Mr Derick aliingia ndani ili achukue gari
"Unaingia tena kufanya nini??" Askari kiongozi ilibidi aulize maana Jacob alitoka vizuri tu alafu anarudi tena ndani
"Mheshimiwa nataka nitoe gari" Mr Derick alijitetea
"Huruhusiwi kuondoka na kitu chochote kwa sababu vyote ni mali za mwenye nyumba" yule askari alitoa maelezo

Mr Derick hakuwa mbishi alianza kuondoka taratibu taratibu kwa mguu akiwa na wake zake, na wanavyo ondoka walimwangalia Jacob kwa jicho kali, kama ndo wanamwambia kwamba utatukoma mpaka Jacob mwenyewe alishangaa na kuogopa.

Wakiwa washaondoka, Jacob machale yalimcheza alianza kufikiria,
"Uuuuuuu!! Huyu mzee na ubishi ule kaondoka kiwepesi hivyo? Huko ndani kupo salama kweli??" Jacob alipata mashaka hapo ilibidi azame getini Fasta.

"Mungu wangu!!!!" Jacob baada ya kuingia tu getini alishika kichwa mpaka askari pale nje walishituka na kuingia ndani.

Itaendelea.........

Usikose sehemu ya 36.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu