Mpya
Taji la ubaya 36-40
TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"
Sehemu 36.
"Mungu wangu!!!!" Jacob baada ya kuingia tu getini alishika kichwa mpaka askari pale nje walishituka na kuingia ndani.
Mule ndani ya geti Jacob aliona gari moja, na gari zote hakuziona, yaani zilikuwa gari zaidi ya 7 ambazo ziliachwa na mzee wake, hakuona kitu zaidi ya ile moja.
"Kijana vip mbona unashika kichwa? Kuna kitu hakipo sawa??" Askari aliuliza baada ya kuona Jacob kashika kichwa
"Afande huyu mpuuzi kakomba kila kitu, sijui kama humo ndani mupo salama" Jacob aliongea huku akiwa anaingia ndani kuangalia usalama.
Baada ya kufika ndani hakuamini maana, kulikuwa hakuna kitu, yaani ilikuwa kama nyumba ndo imejengwa na watu bado kuhamia.
"Kijana usihofu huyu mjinga tutamkamata tu popote alipo na atarudisha kila kitu chako alicho chukua" Askari wale waliongea maneno ya kumtia moyo bwana Jacob.
Baada ya hapo waliondoka na Jacob alirudi nyumbani wanako kaa na Fatuma, na muda huo Fatuma alikuwa bado yupo chuo maana huo ndo ulikuwa mwaka wake wa mwisho.
Baada ya fatuma kurudi Jacob alisimulia kila kitu kilichotokea kule, Fatuma alishauri wawaachie maaskari wafanye kazi yao.
Baada ya kama mwezi Jacob na Fatuma walihamia kwenye nyumba ambayo alikuwa anakaa Mr Derick, yaani ile nyumba ya akina Jacob na walijitahidi kuiboresha na kununua vitu vingine mbalimbali mpaka ikawa inapendeza tena.
Mr Derick aliacha kuonekana mjini hovyo hovyo, kwa sababu alikuwa yupo kwenye mipango mizito ya kuja kupambana na Jacob.
Mr Derick alihamia uswahilini ambako huko kuna nyumba alikuwa kamununulia mchepuko wake bila wake zake kujua, baada ya Sekeseke lile aliamua kutimua ule mchepuko na kubaki na wake zake, ila Vicky kutokana na ni mwanamke wa garama baada ya kuona Mr Derick kayumba kiuchumi, alihamia kwa mzee mwingine ambaye alikuwa anafahamika kwa jina la Mzee mapesa, na tukikumbuka huyu mzee alikuwa amewahi kumpa lifti Jacob kule porini wakati Jacob anaparangana na akina Mr Derick.
Kwa hiyo Mr Derick alibaki na Mama Jacob kama mke wake na walikuwa wanaishi maisha mazuri tu, ila yalikuwa tofauti na ya mwanzo na zile gari zote walizo kimbia nazo kule waliziuza na kubakiwa nayo moja tu, na baada ya kuuza walifungua baadhi ya miradi ambayo ndo ilikuwa inawaweka mjini kipindi chote, na kipindi chote hicho walikuwa wanasuka mipango kabambe ya namna ya kumkabili Jacob maana waliona ni kama kawazaririsha mjini.
Jacob naye maisha yalikuwa yanamuendea vizuri na alikuwa ashasahau kila kitu kilicho tokea na pia alikuwa ashamusahau mpaka shaifa kwamba kuna mwanamke kama huyo.
Kutokana na Jacob kuwa na maisha mazuri na pesa za kumwaga alianza kidgo kidgo starehe za hapa na pale.
Siku moja Jacob alipata pisi kali tena ilikuwa ya kihindi kabisa na ilikuwa pisi pisi kweli mpaka Jacob mwenyewe alichanganyikiwa, Jacob alikubaliana na ile pisi kali na baada ya kuelewana Yule mrembo alimpeleka Jacob mpaka kwao anako kaa na wazazi wake na bahati nzuri wazazi wa huyo mrembo wa kihindi walikuwa wamesafiri.
Jacob baada ya kufika na yule mrembo nyumbani kwa hao kina binti, walipitiliza moja kwa moja chumbani na kitu cha kwanza ilikuwa ni kuanza kupeana mate.
Kutokana na uzuri wa yule binti Jacob mwili ulikuwa unamsisimuka ni hatari yaani alikuwa anaona ni kama anacheleweshwa.
Punde si punde walianza kucheza mechi ya kikubwa kule chumbani, yaani ilikuwa ni mtanange wa kufa mtu, kutona na ufundi wa mrembo huyo Jacob aliapa kumuoa binti huyo bila kujua nyumbani kamuacha fatuma ambaye ndo anaishi naye kama mke wake.
Baada ya mechi Jacob aliona yule mrembo kazima gafra, Jacob alijaribu kumtikisa lakini hakuinuka, baada ya kumchunguza vizuri aligundua yule binti tayari kakata roho.
Jacob hapo kijasho chembamba kilianza kumtoka, alikumbuka yule Mama wa kwanza aliyekufaga kwa staili hiyo hiyo, alikumbuka na maneno ya Fatuma kuhusu mila za kina Fatumah, hapo ndo alianza kuamini na muda huo alikuwa haelewi afanye nini.
Akiwa kule chumbani Jacob alisikia honi ya gari inapigwa nje ya geti, hapo Jacob ndo alichanganyikiwa, yaani mkojo ulikuwa unakuja unarudi unakuja unarudi na ilibakia kiduchu utoke kabisa, na mapigo ya moyo yalikuwa yanaenda speed ya 5G.
Itaendelea......
Usikose sehemu ya 37.
TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"
Sehemu 37.
Akiwa kule chumbani Jacob alisikia honi ya gari inapigwa nje ya geti, hapo Jacob ndo alichanganyikiwa, yaani mkojo ulikuwa unakuja unarudi unakuja unarudi na ilibakia kiduchu utoke kabisa, na mapigo ya moyo yalikuwa yanaenda speed ya 5G.
Jacob alitoka haraka mule chumbani, moja kwa moja mpaka nje ya geti, na uzuri wa nyumba hiyo ilikuwa haina mlinzi wa getini.
Jacob baada ya kutoka nje alisikia kama kuna mtu anafungua geti kwa nje, hapo Jacob pressure ndo ilizidi kupanda, Jacob ilibidi azunguke nyuma ya nyumba na kujificha kwenye maua ili aone itakuwaje kama ana bahati au hana maana alikuwa hana namna nyingine.
Walikuwa ni wazazi wa yule binti ambaye Jacob kamuacha kule ndani amekufa, baada ya wazazi hao kuingia na gari humo ndani walienda kulipaki, Bahati mbaya kwa Jacob sehemu alipo kuwa amejificha palikuwa karibu na eneo la kupaki gari, ila Jacob katika kujificha hakuzingatia hilo maana kichwa kilikuwa kimevurugika na alikuwa anawaza akikamatwa ni kwenda kunyea debe kwa mara ya pili.
Wale wenye mji walipaki gari na kushuka, mapigo ya moyo ya Jacob yalikuwa yanadunda kiasi kwamba alianza kuhofia kama sauti ya mapigo ya moyo yanaweza kuwashitua wenye mji huo.
Bahati nzuri kwa Jacob wale wazazi baada ya kushuka waliongoza ndani moja kwa moja hawakugeuka nyuma kuangalia, maana wangegeuka upande wa pili Jacob alikuwa anaumbuka.
Baada ya wale wenye mji kuingia ndani Jacob alitoka speed mpaka getini, alifungua geti na kutoka speed ya kufa mtu maana siku hiyo alikuwa hana gari.
Jacob alifika nyumbani kwake akiwa haelewi kafikaje fikaje maana speed aliyo kuwa anakimbia siyo ya kitoto mpaka watu wanaomfahamu njiani walikuwa wanamshangaa kwamba kapatwa na nini.
Baada ya kufika kwake alikuta fatuma Naye ndo anafika kutoka chuoni, Jacob hakutaka mazungumzo alipitiliza moja kwa moja chumbani akiwa haamini kama kapona.
"We Jacob wew ndo nini hivyo sasa" Fatuma baada ya kuona vile alilalamika
Fatuma aliamua kumfuata Jacob huko huko chumbani ili ajue nini tatizo.
"We Jacob ndo tabia gani hiyo sasa? Alafu nakuita ndo unaendelea tu? Inakuwaje tunapishana kama magari bila hata salamu??" Fatuma baada ya kuingia chumbani aliwaka
"Fatuma naomba niache kwanza kichwa changu hakipo sawa kabisa" Jacob akikuwa hataki makelele
"Jacob naomba amuka unisimulie kila kitu la sivyo naenda kukuumbua mtaani, muuaji mkubwa wewe"Fatuma tayari alikuwa ashajua kile alicho kifanya Jacob.
Jacob baada ya kuambiwa hivyo alishituka alibaki katumbua macho tu
"Fatuma unasemaje? Inamana unajua" Jacob aliuliza swali ambalo ndo lilikuwa linamfunga na alionekana kuna kitu kakifanya
"Unatumbua macho nini sasa ndiyo najua we unatakaje??"; Fatuma naye alijibu jeuri
"Fatuma wewe ni mchawi au??" Jacob alianza kumhisia Fatuma vibaya, maana ni matukio mengi ambayo yalikuwa yanamtia hofu juu ya Fatuma na hili la leo ndo liliongeza wasi wasi mkubwa juu ya Fatuma.
"We unatakaje? Mi ni mchawi ndiyo we unatakaje au huo ujinga unao fanya unaona ndo usalama?? Huo ndo uchawi tosha kuliko huu nilio nao" Fatuma Aliongea kwa hasira mno.
Jacob alibaki kimya huku mambo mengi yakiwa yanazunguka kichwani mwake yaani akiwa haelewi kipi ni kipi.
"Jacob baada ya hilo tukio nadhani umeanza kujua shaifa ni nani si ndo maana yake? au bado unajiuliza kwamba kwa nini yeye hakufa??" Fatuma Aliongea maneno ambayo yalimfanya Jacob ashituke maana alikuwa ashaanza kusahau mambo ya shaifa ila leo alikumbushwa gafra na Fatuma.
Kutokana na maneno ya Fatuma, Jacob alianza kuumiza kichwa kumhusu shaifa, ila bado majibu yalikuwa hayasomi.
"Fatuma please nipo chini ya miguu yako, leo ndo nimeamini kweli mila zenu zinafanya kazi, maana nimeua binti wa watu bila hatia na sielewi nini kitatokea Mungu wangu, Fatuma naomba nisamehe kwa mara nyingine Mama" Jacob alianza kumwaga machozi na kumbembeleza Fatuma maana alijua asipo fanya hivyo Fatuma anaweza akamwaga siri nje alafu jamaa akaenda kunyea debe jera.
"Jacob tafadhali naomba usinichulie hapa, tena upumbavu sitaki kabisa, kwa hiyo uliona mi nakudanganya?? Na kulikuwa na faida gani endapo mimi ningekudangaya?? Mpuuzi mmoja wewe huo msamaha usiniombe mimi muombe Mungu wako kwa kuua watu wasio na hatia" Fatuma alikuwa kachachama kama mbogo
Jacob hakuelewa aongee nini tena maana maneno yalimuishia yalibakia machozi tu ndo yanamtoka.
"Tena Jacob mshukuru Mungu wako damu yako na ya shaifa zinaendana la sivyo heeee!!" Fatuma alizidi kumpasha Jacob
"Fatuma habari za shaifa zishaishaga bana mi sitaki kuzisikia" Jacob alikuwa hataki kusikia jina shaifa masikioni mwake.
"Unasemaje!!?? Zishaishaga!? Kumbe ndo unavyo jidanganya ee? Hivi wewe unamjua Shaifa vizuri au bado huelewi kitu? Kwa taarifa yako shaifa hawezi kukuacha kizembe hivyo na kibaya zaidi ushawahi kulala naye heeee!! Baba kwa kiburi chako we usharikoroga toka mwanzo, yajayo yanafurahisha japo sijui itakuwa lini na itakuwaje omba Mungu tu shaifa akupende toka moyoni" Fatuma alizidi kumpa Jacob habari yake maana tayari kwa ubishi wake ashayakorogaga mambo na Fatuma alimshanga Jacob anavyo sema habari za shaifa zishapitaga.
"Fatuma naomba usinitishe mwenzako, tena sitaki kabisa alafu naomba uniambie kumhusu shaifa, yule ni nani haswa na wewe ulimujuaje shaifa na kwa nini yeye hakufa kipindi kile nimelala naye? Na pia wewe unajuaje kila mimi ninacho kifanya huko nje??" Jacob aliuliza maswali mfululizo kwa Fatuma na yote alikuwa anataka majibu hapo hapo.
Itaendelea......
Usikose sehemu ya 38
TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"
Sehemu 38.
"Fatuma naomba usinitishe mwenzako, tena sitaki kabisa alafu naomba uniambie kumhusu shaifa yule ni nani haswa na wewe ulimujuaje shaifa na kwa nini yeye hakufa kipindi kile nimelala naye? Na pia wewe unajuaje kila mimi ninacho kifanya huko nje??" Jacob aliuliza maswali mfululizo kwa Fatuma na yote alikuwa anataka majibu hapo hapo.
"Jacob kwa kuwa umeshindwa kung'amua mwenyewe acha nikupe maelezo japo kidogo mengine utaelewa mwenye" Fatuma alikuwa yupo tayari kumuelezea Jacob.
"Fatuma siyo maelezo kidogo we nielezee kila kitu unacho kijua, na nina imani kama unanipenda utanambia kila kitu" Jacob naye baada ya kuambiwa na fatuma kwamba atapewa maelezo machache alianza kama kulazimisha.
"Jacob Mbona kama unanitisha au unataka niache? Unafkri hiyo ni kazi yangu mimi kukwambia??" Fatuma naye alitishia Kususa
"Haya we nambie basi mpaka pale utakapo ishia" Jacob ilibidi awe mpole.
"Jacob kitu cha kwanza we umeishi na mimi muda mrefu kidogo ila ujinga wako hujawahi kuniulizia hata historia yangu? Hata familia yangu yaani mwanaume upo upo tu, hiyo ni dalili ya kwanza inaonesha wewe haupo serious na Mimi, bali upo na mimi kwa sababu ya matatizo ambayo wewe ulikumbana nayo, kitu cha pili Jacob wew ni mgumu mno kushaurika tena sana, maana nilikupa onyo kuhusiana na shaifa wewe hukutaka kusikia na uliona wewe ndo mjuaji sana"
"Fatuma mbona unaanza kuniongelea na kunisimanga badala ya kusema shaifa ni nani? Acha kuzunguka bwana" Jacob alimkatisha Fatuma, aliona kama anachelewesha mambo maana Jacob yeye alikuwa na shauku ya kujua kile ambacho yeye amekuwa akijiuliza kila siku.
"Jacob kuwa mpole, na ukianza ubishi wako mi nakuacha sawa eee" Fatuma Naye alikuwa hataki kuharakishwa
"Haya nimeacha Mama we endelea tu"
"Jacob narudia tena ubishi wako ndo umekufikisha hapa, kwanza inatakiwa ujue shaifa siyo binadamu kama ulivyo wewe na ndio maana baada ya wewe kulala na shaifa yeye hakufa, shaifa ni nusu mtu nusu jini, yaani Mama yake na shaifa alikuwa ni Jini ila Baba yake na shaifa alikuwa ni binadamu wa kawaida na huyo Baba yake na shaifa ndiye aliye nilea mimi baada ya wazazi wangu kuuawa,
Mimi baba yangu alikuwa ni mganga wa kienyeji na mama yangu pia alikuwa mganga wa kienyeji kiufupi koo yetu yote ilikuwa na vimelea vya uganga, kuna seke seke lilitokea kijijini kwetu kipindi cha nyuma mimi nikiwa darasa la tano, kuna shutuma wazazi wangu walishutumiwa na wana kijiji, baada ya hapo kilichofuata imebaki ni historia katika maisha yangu maana nikiwa shuleni wazazi wangu walichomwa ndani ya nyumba yetu.
Baada ya wazazi wangu kufariki ukoo wetu ulianza kunilazimisha mimi nirithi mikoba ya wazazi wangu angali nikiwa mdogo kwa sababu nilionekana kwenye ule uko mimi ndo nimebarikiwa nyota nzuri kuliko wengine wote japo wote walikuwa ni wana asili ya uganga.
Kutokana na mimi lengo langu lilikuwa ni kusoma na hayo mambo mi sikupenda kabisa, ilibidi nikatae amri yao na baada ya hayo maamuzi yangu ukoo mzima ulinitenga Mimi na waliahidi kuniangamiza endapo nitaendelea kukaa pale kijijini.
Hapo ndo niliamua kutoroka na kuja huku mjini, na bahati nzuri nilipo fika tu mjini nilikutana na mwarabu mmoja ambaye baada ya kuona nadhurura tu aliamua kunichukua na kunipeleka kwake, baada ya mimi kumuelezea kila kitu aliahidi kunisomesha.
Basi hapo ndo nilianza maisha mapya na yule mwarabu alikuwa anaishi na mke wake na hapo tayari alikuwa amezaa Naye mtoto mmoja ambaye ndo shaifa, na yule mwarabu aliishi na yule mwanamke miaka zaidi ya kumi na kitu bila hata kugundua kwamba anaishi na jini japo kuna mambo yule mwarabu alikuwa hayaelewi vizuri mule ndani ila ndo hivyo alipotezea na hakuhisi chochote kuhusu mke wake.
Baada ya mimi kufika mule ndani kutokana na mimi kuwa na asili ya uganga na uwezo wa kujua mambo mengi ambayo yapo nyuma ya pazia kuna vitu nilianza kugundua kwa yule mke wa mwarabu na mtoto wake.
Mke wa mwarabu Naye kutokana na uwezo wake aligundua kwamba mimi nina uwezo fulani wa Ziada hapo ilibidi anionye kwamba nisimwambie yule mwarabu na nikisema maisha sina.
Basi kweli mi mwenyewe sikusema, maisha yaliendelea kama siku zote japo mi mambo mengi nilikuwa nayashuhudia ila ndo hivyo nilikuwa navumilia kwa sababu nilikuwa sina pa kwenda.
Baada ya kama miaka miwili kupita yule mwarabu alizaa mtoto mwingine wa kike na mwanamke mwingine tofauti na mama yake shaifa, na huyo mtoto ndo Sharifa kama unamjua na huyo Sharifa ni binadamu kama wewe tu.
Baada ya Mama shaifa kugundua kwamba mumewe kazaa na mwanamke mwingine hapo hasira ilimpanda, alicho amua alimuua yule mwarabu kwa hasira. kutokana na kitendo hicho Majini wenzie na Mama shaifa walikasirika kwa kile kitendo alicho kifanya kwa sababu huyo mwarabu walikuwa wamepanga kumtumia kwenye kazi zao maalumu ambazo hazikujulikana ni kazi gani, baada ya hapo Mama shaifa Naye alipewa adhabu ya kuteketezwa kabisa.
Hapo sasa ilibidi mimi nianze kuishi na shaifa, uzuri Mama shaifa aliziacha pesa za kutosha, maisha yaliendelea kama kawaida japo Mimi na shaifa ilikuwa kama panya na paka maana shaifa aliona namzuia mambo yake mengi na kuna ibada yeye na watu wake walitaka waihamishie pale nyumbani mimi nilikuwa sitaki hapo ndo ugomvi ulizidi kupamba moto, na shaifa aliingia kwenye mahusiano na wanaume kama watatu na kila mwanume ambaye alikuwa anaingia naye kwenye mahusiano alikuwa hamalizi mwaka, kutokana na ugomvi ambao mimi nilikuwa nao na shaifa ilifika kipindi anawinda kuniua, ila kufatana na kinga ya mila zetu toka tukiwa wadogo alishindwa kuniua, hapo ndipo alipo chukua uamuzi wa kunifukuza pale na kwenda kumchukua mdogo wake Sharifa ili ndo waishi Naye, na mimi kipindi hicho ndo nilikuwa nimemaliza form six.
Baada ya pale nilianza kufanya kazi ya kumsaidia Mama mmoja Kazi ya mgahawa na mshara wangu ilikuwa kulala na chakula.
Itaendelea......
Usikose sehemu ya 39.
TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"
Sehemu 39.
Baada ya pale nilianza kufanya kazi ya kumsaidia Mama mmoja Kaz ya mgahawa na mshara wangu ilikuwa kulala na chakula.
Baada ya majibu kutoka na kuonekana nimefauru vizuri ndo hapo ilibidi niombe mkopo na baada ya kupata nilianza chuo na muda wote huo shaifa tulikuwa hata hatuonani, nilikuja kumuona shaifa kwa mara nyingine baada ya wewe kuanza kujisogeza kwake na ndo maana nilianza kukuonya mapema kwamba yule mwarabu achana Naye kwa sababu Mimi nilikuwa namjua vizuri.
Sasa nadhani Saiz umeelewa Mimi ni na nani, na shaifa ni nani, na mimi nilimjuaje shaifa, na kifupi mimi nimebarikiwa kujua kile mtu ambacho katoka kukifanya hasa kama ni cha hatari japo siyo vyote ambavyo naweza kuvijua" Fatuma alimaliza kusimulia na alielezea kila kitu hakubakisha hata kimoja yaani alisimulia hata vitu ambavyo Jacob hakuulizia.
Jacob baada ya kusimuliwa alibaki kaganda huku akiwa haelewi aongee nini
"We Jacob wewe mbona hivyo?? Ulikuwa unanisikiliza kweli wewe??" Fatuma ilibidi amushitue
"Aaaa! Fatuma yes mimesikia kwa hiyo unamanisha shaifa anaweza kunirudia tena??" Jacob hofu kubwa ilikuwa kwa shaifa
"Jacob kwa ninavyo mjua shaifa atarudi tena cha msingi ni kujipanga na kuwa na misimamo na uombe shaifa akupende toka moyoni maana ikiwa tofauti muda wowote anakutoa sadaka" Fatuma alizidi kuongea maneno ambayo yalikuwa yanamfanya Jacob aogope sana na kutetemeka.
"Daaaaa!! Fatuma ebu nishauri nafanyaje sasa maana mi nahisi nina mikosi kila kona, " Jacob kilio kilianza upya maana aliona kila akipumuzika hili linakuja mara lile yaani ili mladi tabu tupu.
"Jacob kwa Saiz sina ushauri, alafu wewe huna mkosi bali hiyo mikosi umejitakia mwenyewe maana tamaa zimekuzidi mno" Fatuma aliongea na kuondoka ila kabla hajatoka kule chumbani alikumbuka kitu
"Jacob muda natoka kwenda chuo nimemuona Mr Derick na watu fulani kama watano wanaiangalia hii nyumba na inavyo onekana Mr Derick kuna maelezo alikuwa anawapa kuhusu hii nyumba" Fatuma baada ya kukumbuka alimwambia Jacob baada ya hapo alitoka nje.
Jacob baada ya yale maneno ndo alizidi kuvurugwa Zaid, alitamani anywe hata pombe ili mawazo yapotee ila ndo hivyo huo uwezo alikuwa hana.
Jacob baada ya kufikiria sana alipitiwa na usingizi mkali, na ndoto alizo ota baada ya kupitiwa na usingizi zilikuwa za kutisha na ilikuwa siri yake.
Alikuja kushituka saa tatu usiku hapo alitoka sebuleni,alikuta fatuma anaangalia TV.
"Duuuuuu Fatuma hata huniamshi bana mwenzako nimelala muda wote huo naota mandoto ya ajabu we umekaa huku" Jacob aliongea kichovu baada ya kukaa
"Bana eee, yawezekana ningekuamusha ungeanza tena kulalamika, kwa hiyo niliamua nikuache"
"Daaaaa?! Vipi lakini hakuna taarifa yoyote huko??" Jacob bado alikuwa na wasi wasi na yule binti wa watu aliye kufa kule.
"Sijaona chochote bana we nenda kajipakulie chakula huko ule acha uoga mwanaume" Fatuma Aliongea huku akiwa anacheka
"Fatuma uwe na heshima, chakula yaani nijipakulie mimi wakati wewe upo? Kweli?" Jacob alitaka heshima yake kama mwanaume
"We umerogwa nini? Umenioa? nakuuliza umenioa? We jana asubuhi ulijibuje au umesahau? nikikwambia tufunge ndoa unaingilia huku mara unatokea kule, Saiz unaanza kunielekeza ujinga, Baba we mpaka unioe hapo ndo utajua Mimi ni wife material ama laa, ila kwa Saiz utangoja sana kwanza hata hicho chakula nakupikia ni huruma tu" Fatuma alicharuka baada ya kuambiwa maneno ya kijinga na Jacob.
Jacob alibaki tu kimya bila kuzungumza maneno yoyote, ila akiwa hajakaa sawa alisikia simu yake inaita, alipo angali ilikuwa ni namba ngeni, kutokana na bwana Jacob kuwa na matatizo mengi aliogopa kupokea ile simu, maana machale yalimcheza.
Ila Fatuma alimsisitiza kwamba apokee tu ile simu, baada ya kupokea alisikia
" Unaongea na Afande mushi kutoka kituo cha Juu, tunaomba ufike kituoni mwenyewe bila shuruti kuja kujibu tuhuma zilizo letwa hapa dhidi yako" hiyo ilikuwa ni sauti nzito kutoka kwenye simu.
Jacob hapo alikuwa ashaanza kuchanganyikiwa maana alijua tayari kashagundulika kwamba kaua na hofu kubwa ya Jacob ilikuwa inaongezeka mara dufu akikumbuka suruba ya kule gerezani.
"Jacob Cool down tuliza munkari kwanza, mbona mwanaume unakuwa mwoga hivyo, kwani wamekwambia una kosa?? Si unaenda tu kujieleza?" Fatuma alikuwa anampa matumaini Jacob
"Fatuma we hujui,kujieleza huko unafikiri kupoje? Si unajieleza tayari ukiwa chini ya ulinzi huoni kama ndo dalili za mimi kwenda kunyea debe tena" mwanaume alikuwa anaogopa jera siyo kitoto.
Wakiwa bado wanaendelea na mazungumzo ya hapa na pale, kuna vitu Fatuma alianza kuhisi na mwishowe kuna kitu cha hatari aligundua.
Itaendelea......
Usikose sehemu ya 40.
TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"
Sehemu 40.
Wakiwa bado wanaendelea na mazungumzo ya hapa na pale, kuna vitu Fatuma alianza kuhisi na mwishowe kuna kitu cha hatari aligundua.
"Jacob huyo mpuuzi anasema anaitwa afande nani??" Fatuma aliuliza kwa kushituka
"Eti afande mushi" Jacob alijibu
"Jacob huo ni mtego huyo siyo afande, na kile kituo cha juu maafande wote wa pale nawajua kwa sababu nilikuwaga nawapelekea chakula wakati nafanya kwenye mgahawa hakuna afande anayeitwa mushi pale" Fatuma alishituka
"Fatuma labda ni mgeni kaja hivi karibuni?" Jacob bado alikuwa anaamini kama aliye mpigia simu ni afande
"Jacob tumia akili walau kidogo, kesi ya mauaji ulisikia wapi mtu anapigiwa simu eti uje kituoni?? Alafu pale hakuna afande yeyote mpya wote ni wale wale, amini ninacho kwambia huyo ni Mr Derick na watu wake" Fatuma alikuwa ashajua kila kitu.
"Duuuuuu!! Hii hatari na nilisikia huyo mzee ana bonge la bunduki!! Alafu we si ulisema asubuhi jana ulimuona mazingira ya hapa nyumbani" Jacob aliogopa sana baada ya kuambiwa atakuwa Mr Derick alipo kumbuka na maneno ya bwana Ediga kuhusu ukubwa wa bunduki ya Mr Derick hapo ndo alizidi kuogopa zaidi
"Jacob nina uhakika asilimia 💯 huyo ni Mzee wako, sasa ukiwa kama mwanaume fikria cha kufanya" Fatuma alisubiri maamuzi ya Jacob
"Fatuma mi naona hapa nyumbani tuhame kwa Muda, ili tupambane na watu hawa vizuri maana tukizidi kuwaogopa watatutesa mno" hilo lilikuwa wazo la Jacob
"Mi kivyovyote utakavyo sawa tu, ila Jacob kabla ya yote nilikuwa naomba tufunge ndoa kabisa ili tuwe tunafikiria mambo mengine kabisa" Fatuma kwenye swala la ndoa ndo alikuwa hataki kubaki nyuma maana alijua chelewa chelewa utakuta mwana siyo wako na alikuwa akifikiria kwamba kuna mwanamke anaitwa shaifa ndo alikuw anapata wasi wasi zaidi.
"Fatuma we vip kwani? badala ya tumalize kwanza hili la bwana Derick we unang'ang'ana na vitu ambavyo vipo tu kila siku hiyo ndoa si tutafunga muda wote tuu" Jacob kwa muda huo alikuwa hayupo tayari kuhusu mambo ya ndoa
"Jacob mi nilikuwa nakumbusha tu kwa sababu nataka kuwa huru na wewe, yaani Saiz sina mamlaka yoyote juu yako"Fatuma Aliongea kinyonge
"Mamlaka gani bana acha ujinga, tumalize Kwanza hili alafu ndoa itafuata, we unafikiri hiyo ndoa itakuwa na raha gani ikiwa maadui zetu wanatuwinda kila kona?" Jacob bado alitia Ngumu.
Basi akina Jacob walifanya uamuzi wa kuhama pale wanapo kaa na waliamua warudi tena kwenye ile nyumba ya Mr jomo kwa sababu kule kulionekana angalau kidogo kuna usalama kwao.
Lakini wanavyotoka pale nyumbani tayari kuna mtu alikuwa anawafuatilia nyuma na baada ya kuona walipo elekea hapo simu ilipigwa kwa Mr Derick haraka.
Mr Derick aliandaa kikosi chake cha kutosha, na usiku wa Siku hiyo alikuwa amepanga kumaliza kazi kabisa.
Jacob na Fatuma usiku huo walikuwa hawana wasi wasi kabisa na walikuwa wametulia kwenye sofa huku wakiangalia mpira na juice zikiwa mkononi.
Wakiwa wamekaa pale Fatuma alianza kuhisi jambo la hatari
"Jacob tupo kwenye danger" Fatuma alisimama huku akiwa kama kachanganyikiwa
"Fatuma mbona sikuelewi unaongea nini wewe??" Jacob alikuwa anashangaa
"Jacob hapa tutafute njia ya kukimbia la sivyo tunafia humu ndani, nakwambia tupo hatarini we umekaa" Fatuma alikuwa anashika nywele zake mara mbili mbili
"Fatuma unaongea nini? Kwani we umejuaje?" Jacob bado alikuwa analeta ubishi
"Jacob umesahau mara hii nilicho kusimulia juzi" Fatuma ilibidi amkumbushe
"Duuu!! Fatuma inama..." Kabla Jacob hajamalizia walisikia mlango unagongwa kwa nguvu
"Jacob tukajifiche" Fatuma Aliongea kwa sauti ya chini, kweli Jacob na fatuma walienda kujificha kwenye kale kachumba kadgo ka Siri aliko katengenezaga bwana jomo.
Baada tu ya kujificha, akina Mr Derick walivunja mlango na kuingia ndani.
"Nasema watafutwe kila sehemu walipo jificha, hakuna kuondoka mpaka wapatikane na nina uhakika wapo humu humu ndani" hayo yalikuwa ni Maneno ya Mr Derick akiwaambia vijana wake, hata akina Jacob walisikia maneno hayo wakiwa wamejificha kule ndani.
Msako ulianza chumba kwa chumba, yaani walikuwa wanarusha vitu hovyo hovyo na kila sehemu walikuwa wanaangalia, walitumia kama lisaa lizima wakiwa wanatafuta bila mafanikio.
"Boss labda watakuwa wamekimbia maana kila sehemu hawapo" ilisikika sauti ya Kijana mmoja akimwambia Mr Derick, ila Jacob alivyo isikia ile sauti kule chumbani waliko jificha aligundua ile ni sauti ya bwana Ediga
"Duuuuuu!! Huyu mpuuzi kumbe kanisaliti" Jacob mapigo ya moyo yakiwa yanaenda speed alijiwazia.
"Ediga acha ujinga hawa watu wapo humu ndani, we huoni hizi juice kwamba walikuwa wanakunywa mida hii, tafuteni kila sehemu najua wapo tu" Mr Derick alikuwa haamini kama wamekimbia.
Msako ulianza upya tena, Mr Ediga aliingia kule chumbani ambako ndo huko kuna kachumba ka siri, Ediga alipo angalia vizuri kabati aligundua lile kabati limesogea mbele alafu limekaa upande, inaonekana akina Jacob wanavyo ingia kwenye chumba cha siri kutokana na haraka kabati hawakulirudiha vizuri kwa sababu mlango wa kuingilia kwenye hicho chumba ulikuwa nyuma ya kabati.
"Boss njoo huku kuna kitu" ediga baada ya kugundua hilo alimuita bwana Derick kwa sauti kubwa na hiyo ilifanya vijana wote kukimbilia kule chumbani.
Jacob hapo alijua siku yake ya kufa ndo ishafika, yaani alikuwa kalowana kwa jasho mpaka basi myoyo ya Jacob na Fatuma ilikuwa inadunda kama sabufa.
"Ediga kulikoni" baada ya Mr Derick kufika kule chumbani aliuliza kwa pupa
"Boss angalia kabati hilo lilivyo kaa hapo inaonesha nyuma ya hilo kabati kuna kitu walikuwa wanaficha" Ediga alitoa maelezo ambayo akina Fatuma kule ndani walijua hapo ndo mwisho wao
Itaendelea.........
Usikose sehemu ya 41.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Write your comment