Mpya
Hadithi: MAJARIBU
Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)
Sehemu: 5
"Siwezi kutulia! Mume Wangu alikuwa anataka aache Uchungaji kisa huyo mtoto unahisi angeshindwa kumuachia kila kitu kama alivyo niropokea!?" Mama mchungaji alikuwa anazidi kuuwasha Moto kwenye kikao kile, yaani mabishano yalikuwa makubwa, inaonekana Bado kuna Siri zilikuwa zipo Chini kwa Chini.
"Ebu subirini Ngoja tumpigie Simu Melisa!" Mmoja wao aliongea, Basi ni kweli Muda ule ule Simu ilipigwa Kwa huyo Katibu wa kanisa ajulikanae Kwa Jina la Melisa na aliambiwa Aje Kwa mchungaji Muda ule ule!.
Ilipita kama Nusu Saa Mama Yule ambaye alikuwa Katibu wa kanisa alifika pale nyumbani kwa Mchungaji, baada ya kuingia ndani na kukuta watu wamekaa wamenuna alishituka kidogo!.
"Melisa ebu naomba nambie mtoto wa Nemeke yuko wapi!? Na unajua nini kuhusu nyaraka za Siri za marehemu Mume Wangu!?" Baada ya kufika tu Mama mchungaji aliuliza Kwa jaziba!.
"Haya ndo mambo sipendagi ndo maana nilikuwa sitaki kuja Mimi! " Mwanamama Melisa alijibu!
"Jamani tukae Kimya! Mbona ni Mambo madogo tu! tuende Hoja Kwa Hoja!" Basi Baba Mtu mzima ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Jimbo alizungumza, na Baba huyu naye alionekana ana mambo yake katika lile Swala!.
"Melisa ebu toa maelezo Yote kama marehemu alivyo kwambia hapa lazima tufikie muafaka!" Baba Yule alizungumza huku akionekana anamkonyeza Melisa Kwa Siri!.
"Okay, ni Kweli Nemeke alizaa mtoto na mwanamke mmoja hivi, ambapo mwanamke huyo alifariki Kwa ajali na mtoto alimuacha kwenye mazingira magumu, hapo ndipo mchungaji Nemeke aliamua kuniomba Mimi nisimamie malezi ya mtoto Yule, Basi ili nisitengeneze picha mbaya na kuendelea kuficha Siri Yule mtoto kuna sehemu ilibidi nimpeleke Kwa ajili ya malezi yake, Japo kika Siku nilikuwa namwangalia na mchungaji Nemeke alikuwa anatoa matumizi!.
Baada ya Miaka kadhaa kupita mtoto kuwa mkubwa mchungaji Nemeke alinipa maelezo kwamba mwanae inatakiwa ajulikanae rasmi maana ndo mrithi wake wa pekee na kama ni Uchungaji Bora aache kuliko mwanae aendelee kuishi kiyatima Wakati Yeye yupo.
Mchungaji alimtafuta mpaka mwanasheria na Sijui Vitu Gani aliongea na mwanasheria kuhusu mwanae! Mpaka mchungaji Nemeke anafariki hayo Ndo alikuwa kaniachia! Na juzi nilivyo enda Gerezani Yule mtoto aliye husika na kifo chake anasema kabla mchungaji hajafa alisema kila kitu chake ni Cha mwanae!." Mwanamama Melisa alitoa maelezo! Lakini maelezo yake asilimia kubwa yalionekana ni maelezo ya kutungwa!.
"Haiwezekani! Mr Luka unaona maelezo anayo toa Huyu Mwanamke! Yaani mtoto ambaye hajulikani eti ndo arithi Mali! Ebu kamlete mtoto huyo hapa!" Mama mchungaji aliongea Kwa kupaniki!.
"Jamani hapa inabidi tuyajenge Kwa Haki, Mtoto wa mchungaji Nemeke ana Haki Zake Pia Mke wake naye ana Haki Zake hatuwezi kumpuuzia mmoja! Hapa kilichopo ni ijulikane nyaraka ziko wapi then kila Mtu atapata asilimia zake!" Katibu wa Jimbo alitoa maelezo ambayo yalifanya Mama mchungaji agune Japo bado alikuwa hakubaliani na hilo ila aliona ni sawa tu Bora iwe hivyo!.
Basi kikao kile kilitamatika Kwa watu wale kukubaliana kumtafuta mwanasheria ambaye ilisadikika Mara ya mwisho aliachiwa maelezo na mchungaji Nemeke, pia wamlete na mtoto wa mchungaji Nemeke.
Basi Siku hiyo ilipita, Siku iliyo fuata kijana Mr Jedi alionekana nyumbani Kwa Melisa yule Katibu wa kanisa! Mama huyo alikua ni mjane, yaani tangia mumewe afariki miaka kadhaa iliyopita alikuwa hajawahi kuolewa tena!.
Mr Jedi baada ya kufika pale aliruka ukuta na kuingia ndani, ilikuwa ni Jioni Mida ya Saa Kumi na Moja, Mr Jedi alijua lazima Muda huo Mama huyo atakuwa yupo kanisani!.
Mr Jedi alikuwa na funguo za bandia, alifungua ndani na kuingia baada ya hapo alitegesha camera yake vizuri kabisa pape sebuleni, yaani ambayo ina rekodi Sauti na video na aliiweka sehemu ambayo alikuwa anajua hakuna Mtu anaweza kuona, baada ya kufanya hivyo aliondoka!.
Masaa yalisogea! Mida ya Saa Moja Jioni ndo Mida ambayo Melisa akiwa na mdogo wake pamoja na mdada wa Kazi walifika pale nyumbani!.
"Naya uache uzembe Sasa! Dili linaenda kufanikiwa wewe unaenda enda Shuleni Kwa Habir, unaenda kufanya nini Sasa!??"basi baada ya kufika pale nyumbani mwanamama Melisa alimuuliza mdogo wake!.
"Dada Melisa, Damu nzito kuliko Maji ujue, mwenzako najikuta tu nashindwa kuvumilia yaani namumiss mwanangu" Dada Yule Kwa Jina la Naya ambaye alikuwa mdogo wake na Melisa alijibu!.
"Sasa Wewe jishaue uje uharibu Dili wakati tupo mwishoni Mwishoni,na Luka akijua unaenda enda Shuleni Kwa mtoto Mara Kwa Mara sidhani kama atafurahi!"
"Eeeeeee Dada na wewe bwana na huyo Luka wako! Utafikiri sijui nani, Mtu mwenyewe Mume wa Mtu unavyo mpapatikia Sasa kama dhahabu!"
"We mtoto Wewe koma eee! Ulivyo kuwa unazaa naye hukujua kama Mume wa Mtu!"
"Eeeeeee Dada nawe! Haya yaishe basi!"
Hayo yalikuwa mazungumzo ya Melisa na Naya, na mazungumzo ya wawili hayo yalionekana yana Siri kubwa iliyo jificha ndani yake! Muda huo huo mlango uligongwa na Mtu aliye ingia alikua ni Mr Luka yule Katibu mkuu wa Jimbo!.
Basi Melisa na Luka walikumbatiana kimahaba na kupigana busu mbele ya Naya na Dada wa Kazi!.
"Eeeeeee!! Naya macho Gani hayo si muende Jikoni basi umbea tu!" Melisa aliongea Kwa Sauti ya wivu huku akiwa anamwangalia mdogo wake! Na inaonekana Naya kipindi Cha nyuma alikuwa Mtu wake na Luka mpaka wakazaa mtoto! Sasa nini kilitokea mpaka Melisa ndo yupo na Luka tutajua yote!.
Basi Naya akiwa anaumia ndani Kwa ndani alielekea chumbani kwake huku Dada wa Kazi akielekea Jikoni!.
"Uuuuu! Mr Luka ujue Jana ulinifurahisha Muno kipenzi!" Melisa aliongea!.
"Kuhusu nini Dear!"
"Si pale nyumbani Kwa Mama mchungaji! Yaani ulivyo mpangilia kuhusu mgao mpaka nilikuta ameanza kuregea! Ila Luka kipenzi kwenye hilo Dili nimekuamini! Kwenye mgao wa Habiri Nusu Yangu Nusu Yako! Isitoshe Wewe utapata Mara mbili maana hata Mama Mchungaji atakupa asilimia!" Melisa aliongea tena akionekana yupo serious!.
"Kuhusu hilo usijali! Ila wasiwasi Wangu ni huyu mdogo Wako Naya, ebu ongea naye atulize komwe lake asije akaharibu wakati Mambo yapo mwisho!"
"Dear kuhusu naya usijali hawezi fanya hivyo!"
"Basi kama ni hivyo vizuri! Kuhusu mwanasheria nimeongea naye kila kitu nimempangalia na amesema yupo vizuri katika Hilo ila amesema kabla ya Kazi lazima apewe kwanza laki mbili!"
"Okay haina Shida!"
Wawili hao waliongea mipango yao, baada ya hapo walitiana mabusu ya kiutu Uzima, baada ya kuona wamepandwa na midadi walibebana mpaka chumbani!.
Mr Jedi yeye alikuwa anaangalia tu kwenye laptop yake kile kinacho endelea nyumbani Kwa Melisa, yaani kila kitu ambacho kilikuwa kinatokea kilikuwa kinarekodiwa Haswa vinavyo fanyika pale sebuleni!.
Basi Siku zilizidi kusogea! Mwezi mmoja ulipita huku kijana Jedi akiwa Bado anafuatilia, na alionekana ana machungu kweli kweli Katika ile Kesi, Yaani alikuwa anafuatilia hatua Kwa hatua!
Basi Siku hiyo ikiwa ni usiku Mr Jedi akiwa mtaani alikutana na bango kubwa likiwa limebandikwa picha ya Mchungaji Nemeke yaani waumini waliamua kwenda kuiweka picha ya Mchungaji Nemeke kama kumbukumbu kwenye bango kubwa la barabarani!.
Mr Jedi aliangaza huku na kule baada ya kutoona Mtu, lile bango kubwa aliling'oa na kulivunja Kwa hasira!, Yaani alionekana ana hasira Haswa na Marehemu mchungaji Nemeke!.
Siku nyingine Iliyo fuata Mr Jedi alienda kwenye Moja ya shule za private pale mjini, na Kwa Namna alivyo ingia pale getini na kuchangamkiana na mlinzi ilionekana Siyo Mara ya kwanza kwenda pale!.
Ila Siku hiyo baada ya kufika pale Shuleni alishangaa anaiona sura ya Melisa na Mr Luka, kwanza ilibidi ajibane sehemu kuona kipi wamekifuata!.
Baada ya dakika chache aliwaona wawili wale wakitoka na kijana mmoja Kwa Jina la Habir, alikuwa ni mtoto anaye soma kidato Cha pili Katika Shule Hiyo!.
"Heeeee mbona bado sielewi! Huyu Habir ni mtoto wa mchungaji Nemeke au wa huyu Bwana!" Mr Jedi alijiuliza swali ambalo hata hivyo hakupata Majibu, Kwanza Siku hiyo aliamua kwenda mpaka ofisini pale Shuleni kuuliza Jina kamili la kijana Yule aliye toka pale!.
"Huyu anaitwa Habir Nemeke!" Mr Jedi alijibiwa hivyo na Mwalimu baada ya kuuliza!.
Muda huo Melisa na Luka walionekana wakifika pale nyumbani Kwa mchungaji Nemeke wakiwa na mtoto Habir! Huku na watu wengine kama watano wakifika pale Kwa mchungaji na ilionekana kuna kikao kizito kinaendelea! Lakin kijana Jedi alionekana hayupo Mbali na maeneo yale maana baada ya kutoka pale Shuleni na kuona wawili wale wametoka na mtoto aliamua kufuatilia nyuma, Mr Jedi alikuwa anapiga mahesabu ya kuingia Mule ndani baada ya kuona kundi la watu kadhaa wameingia.
Je ipi Siri ipo nyuma ya pazia!? Habir ni mtoto wa Nemeke!!? Itakuwaje!?
Tukutane sehemu ya 6
Sehemu: 6
Muda huo Melisa na Luka walionekana wakifika pale nyumbani Kwa mchungaji Nemeke wakiwa na mtoto Habir! Huku na watu wengine kama watano wakifika pale Kwa mchungaji na ilionekana kuna kikao kizito kinaendelea! Lakin kijana Jedi alionekana hayupo Mbali na maeneo yale maana baada ya kutoka pale Shuleni na kuona wawili wale wametoka na mtoto aliamua kufuatilia nyuma, Mr Jedi alikuwa anapiga mahesabu ya kuingia Mule ndani baada ya kuona kundi la watu kadhaa wameingia.
Basi baada ya Jedi kuhakikisha wote wameingia Mule ndani! Naye alisogea mpaka pale Getini na alimkuta Mlinzi akiwa kakauka koo mpaka Siyo vizuri!.
"Oya dingi kuna Laki Moja Hapa kuna Kazi nataka unisaidie!" Jedi alimshawishi yule mlinzi, kwanza mlinzi baada ya kusikia Laki Moja macho yalimtoka kama kaona dhahabu Chini imetelekezwa, maana mshahara wake wenyewe Kwa mwezi mzima ulikuwa haufiki hata hiyo Laki!.
"Kazi Gani hiyo mwanetu! Yaani hapa nina hamu na ugoro kuliko Kawaida ebu nipe niishi nayo Mimi napiga mishe yoyote!" Yule mlinzi aliongea Kwa mizuka!.
Basi Jedi alitoa kakifaa kadogo mithiri ya kifungo Cha sharti, Kalikuwa ni kadogo Lakini Kalikuwa na uwezo wa kunasa Sauti kuliko Kawaida!.
"Chuku hii kitu nenda mpaka ndani sebuleni pale walipo kaa hao Wageni walio ingia kadondoshe Chini au kaweke popote ambapo hakawezi kuonekana, yaani tumia njia yoyote ile!" Jedi aliongea baada ya kumkabidhi kale kakifaa!.
"Eheee dingilai baada ya hapo kingine nafanya nini!"
"Hakuna kingine, ukishafanya tu hivyo basi!"
"Heeeee masihara haya dingi! Yaani hivyo tu unanitia Laki!"
"Ndiyo!" Jedi alijibu
Basi yule mlinzi akiwa na mizuka na pesa aliyo ahidiwa alizama ndani kama hana akili vizuri!.
"We Yoctan! Umeanza lini kuingia ndani! Tena unaingia kama kirabuni, ebu toka nje umefuata nini humu!?"basi Mama mchungaji alifoka kweli kweli baada ya kumuona mlinzi kaingia ndani kichwa kichwa.
"Boss samahani kuna Jamaa yupo nje amekuja kuomba Kazi, nimemwambia ngoja nimuulize Boss Ndo maana nimekuja" Mlinzi yule aliongea uongo, ila tayari alikuwa kakiweka kile kifaa kwenye sofa!.
"Kwa Hiyo we huna akili ya kujiongeza, unataka ufukuzwe kazi yeye ndo aajiriwe Siyo! Ebu nitokee hapa kamwambie Kazi hamuna!" Mama mchungaji alimjibu Kwa hasira, na kweli mlinzi Yule alitoka huku akiwa haamini kama atapewa Hiyo Laki au laaa!.
"Daaaa akinipa hata Ten naishi nayo mbona!" Yule mlinzi akiwa fast kutoka nje alijiongelesha! Basi alifika pale getini alimkuta Jedi katulia!.
"Mwanangu tayari Kazi yako! Nigei Basi changu!" Mlinzi yule aliongea Kwa midadi! Basi Jedi aliweka earphone zake Masikioni huku akiwa kaunganisha kwenye Simu na kufungua program maalumu ambayo ilikuwa imeunganikana Moja Kwa Moja na kifaa kile, baada ya kuthibitisha mambo yapo vizuri alichomoa Pesa kama Laki mbili na kumkabidhi yule mlinzi!.
"Mwanangu ishi nayo Hiyo Laki mbili, kuanzia Leo utakuwa mwana kuna madili madogo madogo kama haya ntakuwa nakupa!" Jedi aliiongea baada ya hapo aliondoka!.
Yule mlinzi alikuwa anaona kama anaota kwanza alimwangalia Jedi Mara mbili mbili huku akiwa haamini!.
"Heeeee yule mwana Mwizi au jambazi, yaan kirahisi Hivi kanipa laki mbili, au lile ni bomu anataka kuripua hapa, au ni mtego!? "Yule mlinzi alibaki na maswali ambayo hata hivyo aliamua liwalo na liwe!.
Huku ndani mjadala ulikuwa ni mkubwa Muno! Mwanasheria alikuwa ameitwa atoe ufafanuzi ambao marehemu Nemeke alimuachia!!
"Jamani Mimi kiukweli mchungaji Nemeke hakuniambia mambo mengi! Kitu alicho nambia ni kwamba Mali Zake zote zitakuwa Mali za mtoto Wake, na alinionesha picha ya mwanake pia alinipa vipimo vya DNA endapo itatokea Mtu atapinga, na huyu ndo mtoto wake aliye nionesha ni hivyo tu" mwanasheria yule alitoa maelezo!.
"Haiwezekani jamani! Iweje museme alisema Mali zote za mtoto wake alafu mseme hati Miliki hakuacha, Mr Luka au Huyu Mwanamke kuna mchezo anataka kuufanya, alafu na Wewe unamtetea badala ya kuwa upande Wangu!"Mama mchungaji aliongea!.
"Jamani Mimi naona hakuna haja ya ugomvi tulikubaliana kwamba Mali zote hawezi kuchukua mtoto! Lazima agawane na Mama mchungaji! Kuhusu hati Miliki hiyo Siyo Shida Sana zitatengenezwa tu zingine kikubwa tuende kwenye Sheria mgawo ufanyike Sawa!" Mr Luka aliongea!.
Siku Hiyo walipanga mipango Mingi Muno na mwishowe walikubaliana kila Kitu.
Kijana Jedi alikuwa kakaa getoni kwake akiwa anasikiliza kila Kitu kilicho zungumziwa huku akiwa anarekodi.
Jedi alikuwa anaishi pekee yake kwenye geto la chumba kimoja na sebule, Na ilikuwa nyumba ya Kawaida. Jedi alikuwa na maisha ya kawaida Muno Haswa baada ya kufuzwa Kazi ndo kabisaa Maisha yalikuwa magumu! Pamoja na ugumu wa maisha alijikunja na kumpatia mlinzi Laki mbili kwa sababu alikuwa na maana Yake!.
Siku Nazo hazigandi, mwezi mwingine ulikatika! Upande wa Huku Kwa kijana Majaribu, kijana huyo alihamishwa gereza na kupelekwa gereza jingine ambalo waharifu wa Mauaji ndo walikuwa wanapelekwa! Japo kuwa Gereza hilo halikuwa mbali Sana na Mji, yaani ilikuwa ni Nje kidogo ya Mji!.
Maisha mapya Kwa Majaribu yalianza, mwanzo kijana Huyo alikuwa anaishi Kwa kuteseka Muno, yaani pale Gerezani Yeye ndo alikuwa mnyonge wa kila Mtu kutokana na udogo wake! Ila baada ya miezi kama mitatu kupita alijenga urafiki na mbabe mmoja wa pale Gerezani ambaye alikuwa anaitwa Nesto, mbabe huyo pale Gerezani alikuwa anaogopwa Haswa na alikuwa na vijana wake kama wawili.
Chanzo Cha urafiki ni pale kijana Majaribu alipo onesha kipaji Cha Wizi, yaani alikuwa anaibia wafungwa wenzake na kupeleka Kwa Nesto!.
Majaribu hakika alikuwa Mwizi, yaani ilifika kipindi alianza kuibia mpaka askari magereza! Yaani hata sehemu iwe nyembamba vipi Majaribu alikuwa anapita!, Pia pamoja na udogo wake Wote hakuna ukuta ulikuwa unamshinda kuruka!!
Siku Hiyo pale Gerezani kuna kiongozi mkubwa wa Serikali alikuwa anakuja kufanya ukaguzi na zaidi zaidi alikuwa anakuja kuwakagua askari magereza utendaji wao wa Kazi, na pia kuwakagua wafungwa kwamba wanaishije!!
Pale Gerezani kuna askari magereza alikuwa hapendwi na kila mfungwa, yaani alikuwa mnoko na pia alikuwa na Roho mbaya! Yaani alikuwa anachukiwa na wafungwa kuliko hata mavi, pia kutokana na unoko wake mpaka askari magereza wenzake walikuwa hawampendi!.
Basi Siku hiyo kiongozi huyo wa Serikali alifika pale Gerezani na Mkuu wa Gereza alimpokea Kwa heshima!.
Muda huo wafungwa wote pale Gerezani kila Mtu alikuwa anahaha kuficha kitu chake ambacho hakiruhusiwi kuwa nacho pale Gerezani! Haswa ilikuwa ni bangi! Lakini katika Hali ya kushangaza kila Mtu mzigo wake Haswa bangi zilikuwa hazipo pale anapo fichaga! Ilikuwa ni ndani ya sekunde mbili tu kila Mtu aliibiwa Bangi Zake!.
"Oya Wazee Mali Yangu mbona Sioni"
"Hata Mimi Sioni!"
"Kudadeki au yule afande mnoko kachukua!?"
"Sema poa tu hata hivi katusaidia! Wakija kuuliza ni kumkataa!"
Hayo yalikuwa mazungumzo baadhi ya wafungwa mule Gereza!, Muda huo kijana Majaribu alikuja akiwa anahema haswa!!.
"Oya dogo au Wewe ndo umeiba Mali!? Maana dogo Kwa Wizi hujambo!" Basi kuna Jamaa aliuliza!.
"Oya nyie tulieni Afande Pablo mtapata habari Zake!" Kijana Majaribu aliongea huku akiwa anahema, Na kweli hazikupita dakika hata Tatu wafungwa wote waliitwa kwenye paredi!.
Baada ya kufika paredi walikuta yule afande magereza mnoko yupo Chini ya ulinzi huku mifuko ya Bangi ikiwa pembeni yake!.
"Okay! Jamani tunataka kuuliza, huyu afande anadai kuna Mtu kamuwekea Hizi bangi, je mnakubaliana na Hilo!? Na je kuna taarifa yoyote mnaijua kuhusu huyu askari!" Basi kiongozi aliye kuja kufanya ukaguzi aliuliza!.
Ukisikia watu kumsagia Mtu kunguni , hakika Siku hiyo yule afande mnoko alichomekewa yaani alisagiwa kunguni kweli kweli! Na wafungwa wote waliropoka kwamba ndo huwaga anawauzia Bangi!.
Basi askari yule mnoko Siku hiyo hiyo kazi iliisha na alienda kupewa hukumu kama muuza bangi!.
Pale Gerezani kuanzia Siku hiyo kijana Majaribu aligeuka shujaa, yaani alikuwa anaishi kama yupo nyumbani, Siyo wafungwa wala askari magereza ambao walikuwa wanamkubali Kwa ushujaa alio ufanya!.
Baada ya miezi kadhaa kupita baadhi ya askari magereza wale wanao penda kufanikiwa kupitia njia za mkato walianza kumtumia Majaribu kwenye madili yao haswa ya Wizi! Yaani walikuwa wanamtoa Majaribu usiku Kwa njia za panya akifika mtaani wanamcholea Raman anaenda kuiba, alafu anarudishwa tena Gerezani!.
Majaribu alikuwa Master wa Wizi! Yaani mtoto alikuwa balaa zito kwenye Wizi!
Upande wa huku mtaani Mr Jedi alizidi kukusanya taarifa Zake kuhusu ukweli, na inaonekana Siyo tu kufungwa Kwa Majaribu ambako alikuwa anafuatilia Bali kulikuwepo na Vitu Vingine ambavyo alikuwa anafuatilia!.
Mwaka mzima ulipita! Siku Hiyo Mr Jedi akiwa mtaani Majira ya Saa Saba Usiku, Huku akiwa katokea kwenye upelelezi wake ambao alikuwa anafanya kila Siku! Mara alishangaa kuna pikipiki ilipita kasi, na pikipiki ile ilienda kusimama mbele.
Jedi ilibidi aisogelee ile pikipiki haraka haraka na kujibana sehemu!.
"Dogo unasikia! Unaona ile nyumba pale kama kawaida utazama ndani! Pale getini kuna Gari zimepita utafanya kama tulivyo kuelekeza ukishafanikiwa utatukuta Eneo lile lile" hayo yalikuwa ni maelezo ambayo Jedi aliyasikia Vyema Mtu akiwa anaelekezwa!.
Lakini Mr Jedi alipo chungulia vizuri aligundua Mtu anaye pewa yale maelezo ni dogo Majaribu!!.
"Heeeee! Huyu dogo vipi si yupo Gerezani!? Hapa tena imekuwaje!?" Jedi alijiuliza maswali ambayo hata hivyo hakuwa na majibu ya haraka haraka!.
Kwanza alijipa subiri ya kusubiria ili aone nini kitatokea.
Basi Watu wawili Ambao walionekana ndo wamemleta pale Majaribu, baada ya kumpa maelezo waliwasha pikipiki na kuondoka!, Kijana Majaribu aliangaza Huku na kule baada ya kutoona Mtu aliruka Fensi Kwa ufundi mkubwa na kuzama ndani!.
Kwanza Mr Jedi alibaki kaacha mdomo wazi, Kwa Namna Majaribu alivyo ruka ule ukuta na kuzama ndani!.
Bahati mbaya kuliko zote maelezo ambayo Majaribu alikuwa kapewa na wale walio mtuma yalikuwa siyo! Bila kujua lile Eneo kumbe ulinzi ulikuwa umeongezeka zaidi.
"Mwizi!! Jamani Mwizi! Mwizi!" Nduru za Mtu kuitiwa Wizi zilisikika upande wa ndani Huku Muda huo Jedi akiwa upande wa Nje, na zile nduru alizisikia vyema kabisa!.
Majaribu aliruka ukuta haraka na kuanza kukimbia Huku Jedi akiwa bado kakodoa macho anashangaa pale nje na alijithibitishia kwamba yule ni Majaribu baada ya kumuona Kwa Karibu zaidi!.
Walinzi wa Maeneo yale ambayo yalionekana ni parking ya Magari walitoka getini wakiwa wanapiga nduru za Wizi, bahati mbaya pale nje Mr Jedi alikuwa yupo na alikuwa anatumbua tu Macho huku akiwa anajiuliza maswali Yasiyo na majibu!.
Je kipi kilimkuta bwana huyu!?
Tukutane sehemu ya 7
Sehemu: 7
Walinzi wa Maeneo yale ambayo yalionekana ni parking ya Magari walitoka getini wakiwa wanapiga nduru za Wizi, bahati mbaya pale nje mr Jedi alikuwa yupo na alikuwa anatumbua tu Macho huku akiwa anajiuliza maswali Yasiyo na majibu!.
"Kamata Mwizi huyo! Mwizi huyo!" Jedi akiwa haelewi hili wala lile alikoswa na Rungu, mpaka hapo alijua akizembea kinamdondokea!.
Mbio Kwa bwana huyo zilianza na alikuwa anaelekea kule kule aliko kimbilia Majaribu! Bahati nzuri Eneo hilo watu walikuwa wavivu kujitokeza Usiku pindi wasikiapo kelele za Mwizi na hiyo ndo ilikuwa pona pona ya Mr Jedi maana wale Walinzi watatu ambao walikuwa wanamfukuza waliamua kukata tamaa baada ya kuona Jamaa anakipimbia kama ana mota miguuni.
Mr Jedi akiwa anakimbia Kwa mbali alimuona dogo Majaribu akiwa naye anakimbia huku akiwa hoi, yaani ilikuwa Siyo kawaida Majaribu kufukuzwa kwenye matukio au kushitukiwa!.
Mr Jedi alimfuata Majaribu nyuma Kwa nyuma! Mpaka Eneo la uwanja wa shule! Ambapo aliona kuna pikipiki imepaki!.
Basi Majaribu alifika mpaka pale ilipo pikipiki, walikuwa ni askari magereza wawili wanamsubiri!.
"Wote tulieni hapo hapo lasivyo nauwa Mtu!" Mr Jedi gafla alifika pale, Wale askari wakiwa wanataka kuondoka zao na Majaribu Mara walisikia Sauti Kavu kutoka Kwa Mtu wasiye mjua!.
Askari magereza Wale walijaribu bahati yao Kwa kumpiga Jedi, Lakini kidogo Jedi alikuwa kabarikiwa uwezo wa kupigana kuliko wao, dakika mbili nyingi kila Mtu alikuwa anaugulia maumivu Chini!.
"Majaribu Kwa Hiyo Siku hizi umeanza kutumika kwenye Wizi!? Huoni kama unaingia kwenye Matatizo zaidi!?" Jedi alimuuliza Majaribu, Basi Majaribu baada ya kugundua na kumfahamu bwana huyo walau alipumua kidogo!.
"Daaaa! Bro Kumbe Wewe ujue umenishitua unapiga kama kwenye video nikajua Mtu gani! Sema bro potezea tu!" Majaribu alijielezea Lakini Jedi userious uliongezeka alipo gundua kwamba wale ni maaskari Gereza.
"Sikilizeni! Nawapeleka kituoni Muda huu, haiwezekani askari ndo mnafanya huo ujinga!" Jedi aliwapiga mkwara.
Basi wale Jamaa walibembeleza kuliko Kawaida.
Kitu ambacho Jedi alikifanya ile pikipiki yao alichukua na ndo ilikuwa kusamehewa kwao! Baada ya hapo walianza kukanyaga Mguu mpaka gereza liliko, ilikuwa ni mbali kabisa nje ya Mji ila walitembea mpaka walifika! Huku kijana Jedi akijipatia pikipiki, na aliwaahidi kabisa itakapo fika Kesho yake anaenda kuchukua bluu kadi!.
Baada ya tukio hilo! Kijana Majaribu hakupewa tena yale madili ya kwenda kuiba mtaani Japo pale Gerezani kila Mtu alikuwa anamnyoshea Mkono Kwa kipaji Cha Wizi ambacho alikuwa nacho!.
Baada ya miezi miwili mingine mbele Mr Jedi alipata vithibitisho ambavyo aliamini vinaweza kumsaidia kwenye ile Kesi!.
Na kweli Mr Jedi alitafuta mwanasheria na walifanikiwa kukata rufaa ya Kesi ya Kijana Majaribu!
Siku iliyo fuata Mr Jedi alienda Gerezani kumtembelea Majaribu na kumpa taarifa ya ile rufa waliyo ikata!.
"Bro una uhakika Lakini kwamba tutashinda hii kesi!?" Majaribu aliuliza!.
"Kuhusu kushinda hilo tumwachie Mungu ila ushahidi wote ninao!"
"Samahani Lakini bro Hivi Kwa nini umeamua kunisaidia Mimi!!? Na sikujui hunijui!?"
"Najisaidia Mimi mwenyewe! Ila wewe umeingia tu kwenye njia Zangu Katika hali ya kujisaidia ndo maana unaona kama nakusaidia!"
"Njia Zako kivipi tena bro!?"
"Mchungaji Nemeke yule marehemu alikuwa ni adui Yangu na nilikuwa namfuatilia Mguu Kwa mguu na kuna Vitu nilikuwa nataka kuvijua toka kwake, bahati mbaya akawa amekufa ndo maana ikawa rahisi hata kufuatilia kifo Chake!"
"Hee bro mbona sikuelewi! Kwamba ulikuwa na ugomvi naye!? Mbona ni kama alikuwa Mtu poa Sana Kwa Nilivyo muona Mara ya mwisho!"
"Majaribu ujue wema wa Mtu hauonekani Kwa Macho!!.
"Heeeee haya Bwana kwamba alikufanyia vibaya hivyo mpaka ukawa unamufuatilia!!!??"
"Siku ikifika utajua! Ila mchungaji Nemeke alimuua Dada Yangu na kumdhurumu baadhi ya Mali"
"Heeeee Kweli!!? Ilikuwaje bro!?"
"Mchungaji Nemeke alizaa na Dada Yangu Kwa Siri mtoto, ila baada ya kuona Sasa Dada Yangu anataka kuitoa Siri ili kila Mtu aijue, kwakuwa alikuwa mchungaji hakutaka kuharibu Sifa zake na hicho ndo chanzo Cha kumuua Dada Yangu akishirikiana na baadhi ya watu!"
"Heeeee Jamani Kumbe yule bwana naye alikufa kihalali! Sema brother nikitoka Hapa kuna Siri ya mchungaji Nemeke aliyo niambia kabla hajafa ntakwambia!" Majaribu aliongea maneno ambayo yalifanya Mr Jedi awe na mizuka ya kujua ni Siri ipi, japo kuwa alikuwa anakisia tu!.
"Ebu nidokezee kidogo!"
"Kuna sehemu mchungaji Nemeke aliniambia alificha Siri zake na nyaraka na kuna Mtu aliniambia ndo nimwambie hiyo Siri, ila kabla sijamwambia niligundua yule Mtu niliye ambiwa nimpe Siri Siyo Mtu mzuri, maana kuna Siku alikuja kuniona akiwa na Mtu niliye muona kwenye mauaji!" Kijana Majaribu alizidi kuelezea, bahati mbaya wakati anatoa maelezo yale kumbe kulikuwa na askari magereza mnoko ambaye alikuwa ashapewa kazi ya kumchunga Majaribu na endapo kuna mgeni atakuja kumuona Basi ijulikane ni mgeni wa aina Gani na wanazungumzia kuhusu nini!.
"Mtu Gani Huyo uliambiwa umpe Siri" Jedi aliuliza!.
"Kuna Mama mmoja Hivi mrefu mweupe ni Katibu wa kanisa!" Majaribu alielezea!.
"Shiitiiii!! Dogo sikiliza tulia hivyo hivyo hao ndo wabaya wenyewe! Kibaya zaidi nilicho gundua wanazungukana wao Kwa wao kuna mchezo unafanyika! Ila subiri Muda Siyo mrefu naenda kugusanisha waya mbona watapigana wao Kwa wao, ila sikiliza kitu kimoja ni kwamba.....!!" Jedi aliongea ila wakati anazidi kutoa maelezo kabla hajamalizia aligundua kuna mpuuzi anasikiliza yale maelezo! na baada ya kugundulika kama anasikiliza aliamua kuondoka!
"Okay Majaribu zingatia kila kitu nilicho kwambia Siku Siyo nyingi utaenda kupandishwa mahakamani Kwa Mara nyingine!." Jedi aliongea baada ya hapo aliondoka!.
Siku Hiyo ilipita! Ikiwa ni Siku nyingine Majira ya usiku kama Saa nne Hivi Jedi akiwa getoni kwake anapangilia baadhi ya ushahidi Kwa ajili ya kesho yake kupeleka Kwa mwanasheria aliye mtafuta, Mara alisikia mlango unagongwa.
"Uuuuu!! Nani tena usiku huu" kwanza Jedi alijiuliza maana ilikuwa ni adimu Sana kugongewa usiku, kwanza alikuwa hana rafiki wa hivyo mpaka kuja kugongewa usiku, Pili alikuwa hana hata demu Labda kwamba atasema demu wake kaja!.
Kijana Jedi alisimama na kusogea mlango! Kisha alitulia kama dakika Moja bila kufungua!, Mara gafla alisikia minong'ono mlangoni, mpaka hapo alijua kimeumana!.
Jedi alitamani apige kelele za kuomba msaada Lakini aligundua hakuna msaada atakao pata! Maana mitaa hiyo ushirikiano ulikuwa sifuri, yaani ukivamiwa hata upige Kelele vipi watu walikuwa hawajitokezi kabisa!.
Jedi aliangaza huku na kule aliona Mule ndani kuna paint Spray ambayo ilibakia Mara baada ya kuwa amepulizia kwenye pikipiki ile aliyo jipatia kutoka Kwa askari magereza.
Kwanza Jedi alikusanya ushahidi wake wote zikiwemo flash disk ambazo zilikuwa na video pamoja na ushahidi mwingine, baada ya hapo alielekea sehemu ambayo palikuwa Kama ukuta!tu alisogeza kidogo, Basi kuna kashimo kalionekana pale ukutani alificha ule ushahidi wake, na alirudisha kama palivyo kuwa awali! Ilikuwa ni ngumu Muno kugundua kama pale ukutani kuna shimo linafunguka!.
baada ya hapo Kitu Alicho kifanya alichukua nondo ambayo alikuwa nayo mule ndani na hiyo spray!.
Jedi alisogea mlango na kufungua taratibu taratibu! Baada ya kufungua pale mlangoni aliona vijana wanne walio Shiba Huku mmoja wa mbele akiwa kashika Bastola!.
"Chini ya ulinzi! Ukifanya chochote Cha kipuuzi nakufyatua Risasi!" Basi Jamaa aliye shika bastola aliongea!.
Jedi wala hakuogopa bastola haraka aliwapulizia ile spray usoni, wakiwa wanahaha Jedi alitembeza nondo kama mbili baada ya hapo alitoka baruti!, Yaani Jamaa mmoja baada ya kupigwa nondo na Jedi alidondoka Chini na kuzima pale pape!.
Basi wenzake ilibidi wambebe haraka haraka na kuondoka naye.
Siku Hiyo ilipita ikiwa ni asubuhi ndo Jedi alirudi pale Getoni kwake, lakini wakati anafika tu nao askari ndo walikuwa wanafika pale kwake!.
"Jedi unashitakiwa Kwa kumvamia Mtu Usiku na kumpiga na nondo!" Hayo ni maneno ambayo Jedi aliambiwa na pale pale alikamatwa na kupelekwa kituoni!.
Siku Hiyo Hiyo upande wa Gerezani aliko fungwa kijana Majaribu! Alionekana mwanamama Melisa akifika pale Gerezani akiwa na wapambe wake wawili, basi kama Kawaida waliomba wazungumze na Majaribu na walitoa kitu kidogo!.
Yaani pale Gerezani ili uzungumze na Mtu wako mazungumzo ya Siri ilikuwa lazima utoe rushwa, lasivyo inabidi yawe ya wazi ambayo askari wanasikia!.
Kijana Majaribu aliletwa na baada ya kumuona mwanamama Melisa, Majaribu alibaki katumbua tu macho!.
"Okay kijana sitaki kupindisha maneno! Najua marehemu mchungaji Nemeke alikwambia Siri ya zilipo nyaraka zake zote, na alikwambia unambie mimi Hiyo Siri! Sasa nimekuja hapa Siyo kukuomba nataka uniambie Hizo nyaraka ziko wapi!?" Melisa akiwa na Sura ya ukauzu aliuliza!.
"Nyaraka Gani unazizungumzia!?"! Majaribu aliuliza kana kwamba haelewi kinacho zungumziwa!.
"Kijana usifikirie kwamba utaachiwa hapa kirahisi! Huyo uliye kuwa unamtegemea tayari kakamatwa Kwa kosa la kuuwa, Siku Siyo nyingi utakuwa naye hapa Gerezani!."Melisa aliongea maneno ambayo yalifanya Majaribu atokwe na Jasho, yaani matumaini Yote yalipotea tena Kwa Mara nyingine!.
Wakati huo huo upande wa hospital aliko pelekwa yule Jamaa aliye pigwa na nondo usiku na kijana Jedi alifariki, ila kuna daktari wa field ambaye alikuwa yupo pale hospital Kwa ajili ya mafunzo alijaribu kupima kifo Cha yule bwana aligundua kilicho muua Siyo kupigwa na nondo bali alikuwa amekufa Kwa Sumu Kali!, Inaonekana kuna Mtu alikuwa kamchoma sindano ya Sumu kwa makusudi ili afe Japo kuwa daktari huyo aligundua hilo Lakini aliamua kukaa kimya tu.
Yaani hapo Kesi ndo ilizidi kuwa ngumu Kwa kijana Jedi! Maana pale kituoni taarifa zilifika kwamba Jamaa aliye pigwa na nondo na Jedi usiku amefariki dunia, kwanza kijana Jedi zile taarifa zilimshangaza Kwa sababu hata nondo yenyewe alivyo piga alikuwa hajakaza Mkono Sana!.
Pia wale wenzake na marehemu nao walishangaa mwenzao kafaje kafaje maana alikuwa hajaumia kihivyo kufikia hatua ya kufa!!.
Wakati yote Hayo yakitokea huku Gerezani kijana Majaribu alikuwa kagoma kutoa Siri! Yaani alikuwa katishiwa Lakini kijana alimjibu Melisa kwamba hajui lolote, mwishowe Melisa alianza kutumia maneno mazuri kama ya kumtoa Gerezani na kumpa maisha mazuri Lakini napo Bado Majaribu alisimama kwenye mstari kwamba hana Siri yoyote aliyo ambiwa na marehemu!.
Siku Hiyo Melisa aliondoka kichwa kikiwa kinawasha, yaani ilibakia kidogo hata wigi alilovaa limtoke!.
Basi Siku kadhaa zilipita bwana Jedi alipandishwa mahakamani Kwa kosa la kuuwa! Yaani ushahidi na mashahidi wa uongo walikuwa wametengenezwa! Bahati mbaya Jedi alijichanganya pale alipo sema alimpiga jamaa huyo baada ya kuwa wamemvamia kwake na alikuwa anajihami.
Je Mr Jedi atafungwa Gerezani!? Baada ya kufungwa kipi kitatokea!??
Tukutane sehemu ya 8
Sehemu: 8
Basi Siku kadhaa zilipita bwana Jedi alipandishwa mahakamani Kwa kosa la kuuwa! Yaani ushahidi na mashahidi wa uongo walikuwa wametengezwa! Bahati mbaya Jedi alijichanganya pale alipo sema alimpiga jamaa huyo baada ya kuwa wamemvamia kwake na alikuwa anajihami.
"Kwa Hiyo Kijana baada ya kuvamiwa ndo ukaona Sasa una Haki ya kuuwa ukaamua kuua kabisa!!?" Wakili wa Serikali alimuuliza Jedi swali!.
"Mimi Sikuuwa na nilimpiga kidogo tu, sidhani kama kumpiga Kwangu ndo kumepelekea kifo Chake naomba kifo chake kichunguzwe upya!" Jedi alitoa maelezo na wasiwasi wake juu ya Kifo kile lakini alizidi kushindiliwa maswali mfululizo!.
Siku Hiyo kesi iligairishwa na Jedi akirudishwa tena rumande! Yaani Mambo yalikuwa yamegeuka gafla badala ya Jedi kufuatilia kesi ya Majaribu Sasa alikuwa anaparangana na Kesi yake!.
Wiki Tatu zilipita Tarehe nyingine ya kurejea mahakamani iliwadia! Siku Hiyo ndo ilikuwa Moto zaidi Kwa Jedi maana mashahidi kama wote walijitokeza pale mahakamani na wote walikuwa karibia na maelezo yanayo fanana wakiwa wanasema Jedi wala hakuvamiwa bali alimpiga Mtu huyo Njiani na Siyo kwake!.
Na kibaya walio kuwa wanatoa ushahidi walikuwa Siyo wale vijana ambao walikuwa na marehemu usiku, bali walikuwa ni watu wengi tu Ambao hawakuwepo hata Siku ya tukio!.
Mpaka hapo Kesi ilikuwa ngumu Kwa upande wa Jedi na Mwishowe Hakimu aliamua kusoma Hukumu!.
Kijana Jedi alihukumiwa Miaka 30 Gerezani kwa Kosa la kuuwa Kwa makusudi kabisa! Yaani Jedi alijaribu kujikanyaga Lakini ilishindikana!!.
Hakika kijana Huyo alikuwa anaziona Ndoto zinapotea taratibu taratibu, yaani kutoka kuwa askari mpaka kuja kuwa mfungwa!!.
"Dada Yangu Nisamehe! Nilijiunga na uaskari ili niweze kufichua maovu ya watu walio kusababishia kifo, Lakini Leo hii naishia Gerezani bila kulipiza kisasi chako!" Akiwa kwenye karandinga anapelekwa Gerezani kijana Jedi alikuwa analia huku akiwa anajiongelesha maneno ya huzuni!.
Siku Hiyo ilikuwa jmatatu wafungwa wakiwa wametoka kugonga Mawe huku wakiwa hoi bin taabani Mara kuna mfungwa mpya alionekana akiletwa!.
Majaribu alibakia kaacha mdomo wazi baada ya kumuona Jedi naye kaletwa Mule Gerezani, hapo ndo alianza kuamini maneno ya Melisa kwamba Yeye na Huyo Jedi wake watafia Gerezani!.
Maisha Mapya Kwa Jedi yalianza huku rafiki yake mkubwa akiwa ni Majaribu! Kutokana na umaarufu wa Majaribu pale Gerezani hiyo ilisaidia hata Jedi kutopelekeshwa Sana na Wahuni, pia Jedi mwenyewe naye alikuwa anajiweze kwenye upande wa kupigana!.
Siku nazo hazigandi hatimaye Mwaka mzima ulipita, huku mtaani Mama Mchungaji aligawana Mali Nusu Kwa Nusu na mtoto Habir ambaye ilisadikika ni mtoto wa marehemu mchungaji Nemeke! Mali zingine ambazo zilikuwa zimejificha ambazo hawakuweza kuzitambua zilipotea kimya kimya!.
Ila pamoja na kwamba Mama mchungaji alikuwa kagawana na yule mtoto Mali zote Lakini bado Mama mchungaji Yule alikuwa na wasiwasi kweli kweli kwamba yule ndo mtoto wa mchungaji kweli au kuna mchezo! Maana mtoto huyo na marehemu mchungaji Nemeke walikuwa hawafanani hata kidogo!!.
Upande wa huku Gerezani kijana Jedi aliona Siyo kweli kwamba yeye aendelee kusota Gerezani wakati kesi Siyo yake! Na Hiyo ilitokana na kwamba kuna Mtu alikuwa amekuja kumletea taarifa kwamba marehemu aliye fariki alipewa Sumu!.
"Ndugu Yangu Kwa saizi Mimi nimeajiliwa hospital ya mkoa, ila nimeona Siyo busara kukaa na Siri! Kipindi kile nafanya field kwenye ile hospital aliyo fia yule kijana! Kiukweli kila kitu nilishuhudia! Yule kijana alikuwa amepona kabisa! Ila kuna daktari pale hospital alimchoma sindano ya Sumu! Na ushahidi ninao! Pia vipimo vyote na aina ya Sumu Ninavyo! Kwa Hiyo ndo hivyo kaa ukijua ulisingiziwa!" Hayo ni maelezo ambayo Jedi aliletewa na yalifanya apate mizuka ya kutoka pale Gerezani!.
Jedi alikuwa anajua Kutoka Kwa njia ya kihalali ni ngumu bali lazima atoke Kwa njia za kiwizi Wizi!.
Kijana Jedi alianza kutengeneza mipango kushirikiana na baadhi ya askari wenye tamaa!.
"Hivi huo mpango una uhakika nao!? Na umewahi shuhudia wapi mpango kama huo? isije ikawa unaleta Mambo ya kwenye video!"
"Mimi si ndo nakwambia ndugu Yangu mbona simpo tu! Nyie kazi yenu ndogo itakuwa kutukimbiza hospital Mimi na Majaribu!"
"Uuuuu! Na ikithibitika hamjafa itakuwaje!?"
"Haiwezi kutokea, yaani tukitoka hapa tunapotea Mjini moja Kwa Moja!"
"Una uhakika Lakini Pesa uliyo isema baada ya kutoka tutapata!?"
"Aaaaaa million 100 kitu gani afande msijali hiyo mtapata!"
Jedi alikuwa anazidi kuwashawishi askari magereza pale Gerezani!.
Mpango wa Jedi alikuwa ameongea na Yule Daktari ambaye alimletea taarifa, na Lengo alikuwa anataka yeye na Majaribu wanywe Dawa, na zilikuwa ni Dawa maalumu ambazo zinasimamisha Mapigo ya Moyo Kwa Muda.
Baada ya kunywa hiyo Dawa ithibitishwe kwamba wamekufa na wafutwe kwenye faili la pale Gerezani Kisha wapotelee mitaani, yaani kifupi Jedi alikuwa anataka kutoroka Gerezani kwa njia ya kuwa kama mfu!.
Basi baada ya askari kupangiliwa vyema nao walipangika vizuri kabisa na walikubaliana kila kitu na Jedi, kijana Majaribu alipo pewa ule mpango yeye aliona noma tu maana alikuwa hana tumaini lingine lolote la maisha mbele yake!.
Basi Siku kadhaa zilipita Siku Hiyo Majira ya mchana Mara gafla Majaribu aliumwa ugonjwa wa ajabu, yaani alikuwa anatetemeka hovyo, wale wale askari walio kula dili na Jedi walimbeba haraka haraka dogo na kumkimbiza hospital ya mkoa na daktari aliye wapokea alikuwa ni yule Yule aliyepangana na Jedi!.
Siku inayo fuata asubuhi Jedi naye alipatwa na Hali kama aliyo patwa nayo Majaribu Jana yake! Pia naye alikimbizwa hospital!.
Baadhi ya askari magereza Ambao walikuwa hawaelewi mchezo unao endelea walihofia kwamba huwenda kuna ugonjwa wa mripuko umezuka pale Gerezani! Basi haraka haraka wataalamu wa kupuliza Dawa za kuuwa vidudu waliitwa na gereza zima Dawa zilipulizwa!.
Yaani Dili lile lilikuwa linapita Chini Kwa Chini kiasi kwamba hata mkuu wa gereza alikuwa hajui kinacho endelea aliamini ni ugonjwa tu!.
Basi Jedi na Majaribu walijikuta wapo hospital Kwa pamoja!.
Siku Moja ilipita! Yule Daktari aliye julikana Kwa Jina la Lameck aliamua Sasa kuwapa vile vidonge maalumu vya kusimamisha mapigo ya Moyo Kwa Muda na Daktari huyo tangu aajiriwe alikuwa na miezi mitatu tu kazini.
Jioni ilipo Fika ilithibitika wale wagonjwa wamefariki, taarifa zilifika mpaka Gerezani! Mpaka mkuu wa kituo taarifa zilimfikia kwamba wafungwa wawili wamefariki!.
Daktari mkuu wa hospital ya mkoa naye alithibitisha kwamba ni kweli wafungwa wale wamefariki, madaktari wazoefu nao walipima vipimo vyao waligundua wale watu wamefariki! Ila kuna Mzee mmoja alikuwa mzoefu aligundua kitu maana hata miili ya wawili wale ilikuwa ya Moto, Japo kuwa daktari huyo aligundua ila aliamua kuuchuna tu na kupotezea!.
Basi wawili wale Majaribu na Jedi walipelekwa mochwari ikiwa ni kama maiti!.
Majira ya Saa Kumi na Moja alfajiri bahati mbaya Majaribu na Jedi walizinduka maana vile vidonge Sasa vilikuwa vimeisha Kazi yake! Bahati nzuri doctor Lameck alikuwa analijua hilo mapema, alfajiri ile ile alifika pale mochwari! Alimhonga mlinzi wa mochwari Pesa ya pombe aliingia Mule ndani! Basi alifanya kile kilicho mpeleka alitoka tena!.
Majira ya Saa mbili asubuhi Mkuu wa Gereza na baadhi ya askari Walifika pale hospital kuthibitisha ni kweli Majaribu na Jedi walikuwa wamepoteza maisha, na Sijui doctor Lameck alikuwa kawamwagia Vitu Gani, maana walikuwa wananuka kama maiti kweli!.
Taarifa za vifo vya Watu hao zilifika mpaka mtaani! Watu walipata taarifa kwamba kijana aliye husika na Kifo Cha Mchungaji Nemeke amefia Gerezani kwa ugonjwa wa mripuko! Maana taarifa zilitangazwa mpaka kwenye vyombo vya habari!.
Bwana Luka na Melisa walishituka ila hawakuzingatia Sana wala kufuatilia kabisa Swala hilo kwamba inawezekana vipi Majaribu na Jedi wafe Kwa pamoja, Upande wa Mama mchungaji Yeye Ndo alionekana ameshituka Sana kuliko Hata kina Melisa, yaani hakuamini kabisa mpaka Mama Huyo alipo enda kujionea na kuthibitisha walau ndo aliamini Japo kuwa alikuwa anajiuliza maswali mengi Muno kwamba imekuwaje wafe wawili tu tena wanao Juana!.
Kwa Macho yake alijonea kabisa maiti ya Jedi na Majaribu tena zikiwa zinatoa harufu vibaya Muno ikiwa ni dalili ya kwamba zimeanza kuharibika!.
Basi ilitangazwa kwamba ndugu wa wawili hao wajitokeze wakabiziwe miili ya wapendwa wao wakaizike!.
Kuna vijana wawili, Baba mmoja na wamama wawili walijitokeza kama wao ndo wahusika Huku kila Mtu akiwa anataja ndugu yake! Na Watu hao Kwa maelezo yao walionekana wamepangwa.
Basi ndugu walienda mpaka Gerezani walisaini sehemu zinazo takiwa na walienda hospital kukabiziwa miili ya wapendwa wao tena walinunuliwa na majeneza kabisa!.
Hakika Njia ile aliyo ibuni Jedi ilikuwa ngumu Muno! Akiwa ndani ya Jeneza kijana Majaribu alizinduka Lakini baada ya kusikia maneno nje Watu wakiwa wanaongea kuhusu vifo hivyo huku wengine wakiwa wanalia aliamua kuvunga!.
Kwa mbwembwe kabisa na vilio juu Gari ya kubeba maiti ilikodiwa huku ikiwa inasemekana maiti Inasafilishwa kwenda mkoani, pia maiti ya Majaribu ilisadikia inapelekwa kijijini!.
Wafiwa bahati mbaya walikuwa hawataki kusindikizwa na Mtu yaani, lakini mkuu wa gereza alisema lazima atume vijana wake wakathibitishe kwamba Watu hao wanazikwa!.
Bahati nzuri Kwa Jedi na Majaribu wale wale askari walio kula nao Dili ndo walijipendekeza Kwa mkubwa na walitumwa wasindikize misafara!.
Basi yaliyo tokea yalitokea na askari magereza wale walirudisha ripoti kwamba wameshuhudia mazishi tena walikuja na picha za msibani kabisa, Sijui walikuwa wamezitoa wapi!.
Askari magereza wale kazi yao ilikuwa imeisha walicho kuwa wanasubiri ni million 100 Kutoka Kwa Jedi kama walivyo ahidiwa! Na Kwa mahesabu yao kila Mtu alikuwa anapita na million 25 maana walikuwa wanne!.
Siku zilizidi kukatika miezi kama mitatu ilipita huku Jedi na Majaribu wakiwa hawajaonekana kabisa! Kiasi kwamba hata wale askari magereza walianza kujiuliza watampatia wapi Jedi awape Pesa zao!.
"Daaaa Sema na Sisi Wazembe kweli! Yaani tulikubali Dili la hatari vile bila hata kujua tutakabidhiwa Pesa Kwa mfumo upi, Ona Sasa huyu msenge hatujui hata pa kumkutia!" Basi Siku hiyo wakiwa wanajadili askari mmoja aliongea Kwa malalamiko kweli kweli!
"Ndugu Yangu usijali hii dunia ndogo Muno! Ipo Siku tutamnasa ndo atajua kwamba Pesa ina maana Gani! Maana tutauza hata Figo yake Moja!" Basi askari mwingine akionekana ana hasira aliongea!!.
Je watafanikiwa kumpata Jedi!!? Na Je upi mpango wa Jedi na Majaribu baada ya kutoroka Gerezani!?
Tukutane sehemu ya 9
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Write your comment