Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Jumapili, 11 Mei 2025

Hadithi: MAJARIBU EP 1-2


Mpya
Majaribu 1-4


Hadithi: MAJARIBU

Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)

UTANGULIZI: Ni hadithi inayomzungumzia kijana mdogo wa kuitwa majaribu. Wakati akijaribu kuyakimbia matatizo yake akakutana na majaribu menyewe Sasa Alijikuta akikabiliwa na kesi ya mauaji ambayo hakuyafanya ilipelekea kupelekwa gerezani je kijana Huyu atafanyaje ili kuthibitisha hana hatia. Ongozana nani Katika kigongo hili mwanzo mwisho. Mtunzi wa Hadithi hii anaitwa Mwaki Ze Done wasiliana naye Kwa whatsapp yake Kwa namba hizo hapo juu.

Sehemu: 1

Ni Majira Ya Usiku kwenye Moja ya Jengo la kifahari katikati ya Jiji ambalo lilikuwa limechangamka Haswa, kwenye Moja ya chumba ndani ya Jengo Hilo alionekana mdada wa Miaka kama 17 akiwa anaperuzi mtandao wa FB huku akiwa anakenua Meno Kwa furaha, Bila Shaka kile ambacho alikuwa anakifuatilia kilimfurahisha Sana.
Ila Mida hiyo ya Saa Saba za usiku akiwa bado kazama kwenye Mitandao kiasi kwamba usingizi uliogopa hata kumnyemelea Mara gafla Dada huyo alianza kusikia kukuru kakara upande wa pili ndani ya nyumba hiyo hiyo!.

Dada huyo taratibu aliweka Simu yake kitandani na kutoka kule chumbani ili kuona nini kinaendelea!.
Kwanza alienda mpaka sebuleni na kutulia ili kusikilizia zile kukuru kakara alizo zisikia ni wapi zimetokea.

"Msaadaaaa!! Nisaidieni......uuuuu!!!.." Dada Yule akiwa pale sebuleni alisikia Sauti Kwa mbaali ya mwanaume akiwa anaomba msaada! Haraka haraka Dada yule alipanda ngazi mpaka gorofa ya juu ambako Sauti hizo zilikuwa zinatokea! Kwa mwendo wa taratibu na umakini mkubwa Dada yule alisogea mpaka kwenye mlango ambao ulioneka upo wazi!.

"Mungu Wangu....!!" Dada Yule Kwa kile alicho kiona alijikuta anaropoka Kwa Sauti ya Chini huku akiwa anajiziba mdomo, Mapigo ya Moyo yalionekana kwenda Sipidi Muno Mwili mzima wa Dada Yule ulikuwa unatetemeka Kwa kile alicho kiona, Haraka haraka alitoka pale mlangoni na kukimbilia chumbani kwake!.
Dada Yule alianza kukusanya vitu vyake kule chumbani Kwa ajili ya kuondoka huku Mapigo ya Moyo yakiwa yanamuenda sipidi, ila baada ya kukusanya na kufunga begi lake vyema, baada ya kufika mlangoni ni kama kuna akili ilimjia kwamba usiondoke!.

"Uuuuu!! Nikikimbia Hii kesi si itakuwa Yangu hii! Siendi kokote!" Dada yule alijiongelesha mwenyewe, baada ya kuwaza na kuwazua aliamua kurudi kitandani na kukaa!.
Simu Ya Dada huyo ilikuwa haishikiki tena yaani Moja ilikuwa haikai Mbili haikai Jasho tu ndo lilikuwa linamtoka Japo ilikuwa usiku.

Dada huyo akiwa katulia chumbani alisikia vishindo vya watu walionekana Sasa wanashuka ngazi kutokea gorofa ya juu! Dada yule ambaye bado hatujamjua ni nani, akiwa na Moyo wa kijasiri aliamua kutoka kule chumbani kwake taratibu na kwenda kuchungulia.
Dada Yule aliona Njemba kama Nne zikiwa zimebeba furushi zinatoka kule chumbani huku nyuma yao kukiwa na Mama Mtu mzima Miaka kama arobaini na kitu akiwa anafuata nyuma tena Kwa ujasiri!.

"Heeeee!! Mbona maajabu jamani! Wamefanana au ni Yeye!?? Mama Mchungaji si yupo India!?? aaaaaa hii haiwezekani!??" Dada yule baada ya kuona hali ile alijiuliza maswali ambayo hayana Majibu Huku akiwa anachungulia na Mwili mzima ukiwa unamtetemeka!.

Usiku huo huo kwenye Moja ya kijiji ambacho kilikuwa hakipo mbali Sana na Jiji lile ilikuwa ni kama mwendo wa masaa matatu na Kitu Hivi ukiwa na usafiri kutokea Mjini mpaka kwenye Kijiji hicho.
Ndani ya kijiji hicho Walionekana wanakijiji wakiwa wamechafukwa Haswa Usiku huo wa manane kwenye Moja ya nyumba ya nyasi ambayo alikuwa anaishi Bibi wa Miaka kama 70 na mjukuu wake wa kiume Miaka kama 16, wakiwa wamelala usiku huo Mara walisikia makelele ya wanakijiji wakiwa wanaonekana wanakuja pale nyumbani.

"Tumechoka!! Tumechoka!! Tumechoka!!" Hizo zilikuwa nyimbo za Mizuka kutoka Kwa wanakijiji, yaani nyimbo hizo zilifanya hata wale Ambao walikuwa wamelala usingizi wa pono waamuke na kwenda kuungana na wenzao katika kutimiza Jambo lao!.
Umati ule wa wanakijiji walifika mpaka kwenye nyumba ile ya nyasi ambayo alikuwa anaishi Bibi huyo kikongwe na mjukuu Wake!.

"Bibi Zoha Tumechoka! Tumekuchoka wewe na mjukuu wako! Wizi nyie! Uchawi nyiee! Kwa usalama wenu kabla hatujachoma hiki kinyumba chenu tokeni nje!" Basi umati ule baada ya kufika nyumbani Kwa Bibi yule kuna Jamaa aliongea Kwa mizuka na kweli watu waliripuka Kwa shangwe.
Upande wa ndani Bibi Yule na mjukuu wake walikuwa wanatazama huku wakiwa Hawaelewi kipi ni kipi!.

"Majaribu Hivi umeiba tena!? We mtoto upoje Lakini!?" Huku ndani Yule Bibi alianza kumlaumu mjukuu wake huku Moyo ukiwa unaenda mbio!.

"Bibi Mimi nimeiba Saa ngapi wakati tupo wote Muda wote, isitoshe hao wanasema uchawi siyo Wizi! Bibi wewe ni Mchawi na ndo wamekufuata!" Basi kijana yule naye akiwa na uoga alimjibu Bibi yake!.

"Majaribu acha ujuaji, sikiliza hapa hakuna usalama ebu tokea dirishani kimbia tena kimbia uende mbali, hata ukisikia nimekufa usirudi Hapa!" Bibi Yule akiwa anajiandaa kwenda kufungua mlango alimjibu mjukuu wake, lakini Kabla hata hajanyanyuka kwenda mlangoni Mara walianza kusikia mlango ukivunjwa Kwa kutumia vitu Vizito maana wanakijiji walikuwa wamevurugwa mpaka Siyo vizuri.

"Au kama Vipi tuchome nyumba mbona watatoka wenyewe!" Basi kuna jamaa aliongea Kwa mizuka na kufanya watu waanze Sasa kutafuta kiberiti, wale wa Karibu na pale Kwa Jinsi walivyo kuwa na Roho ngumu waliamua kufuata viberiti majumbani kwao!.
Huku ndani kijana wa kuitwa Majaribu baada ya kuona Sasa Maji yamezidi unga aliamua kuchomokea dirishani, Japo kuwa dirisha lilikuwa dogo ila alijilazimisha na alitosha na ilionekana ni mzoefu wa kupita Madirishani.

Baadhi ya Watu walimuona kijana Huyo akiwa anakimbia na waliamua kumuungia Kwa kumfukuza maana huyo ndo walikuwa na Shida naye zaidi kuliko hata Bibi yake!.
Kijana majaribu pamoja na umri wake alikuwa ni mwizi haijawahi kutokea, yaani alikuwa ni kama kasomea shahada ya Wizi, na tangia aanze kuiba alikuwa hajawahi kukamatwa, yaani Watu walikuwa hawambahatishi kwenye matukio Japo kuwa walikuwa wanajua ni Mwizi!.
Bahati mbaya Siku hiyo pale Kijijini kuna Mtu alikuwa kaibiwa mifugo yake Yote na baada ya wanakijiji kuamushana Usiku waliamua Sasa kuelekea nyumbani Kwa Bibi yake na Majaribu wakiwa na uhakika kwamba huwenda kijana huyo ndo mhusika kuhusu mifugo hiyo kupotea.

(Kwakuwa kijana Majaribu ndo mhusika mkuu bado kuna mengi tutayajua kumhusu mpaka Yeye kuwa kwenye mazingira yale Je ni ipi Historia Yake!? Tutajua tu!.)

Basi baada ya Watu kumuona Majaribu akikimbia waliamua kumuungia na kuanza kumfukuza, yaani Kwa Jinsi alivyo kuwa anakula unyoya ndo kabisaa watu waliamini Yeye ndo aliye husika na Wizi wa mifugo kushirikiana na anao wajua Yeye!.
Majaribu pona pona yake ilikuja baada ya kukimbilia kwenye pori kubwa ambalo lilikuwa linapakana na Kijiji hicho!.

Wanakijiji baada ya kumkosa Majaribu Sasa Hasira walizihamishia Kwa Bibi Yake, yaani Bibi wa Watu Siku hiyo alipigwa kipigo cha uhakika na nyumba Yake ilichomwa Moto kabisa.
Bibi Yule alifariki Usiku ule ule Bila hata kusema neno lolote, yaani wanakijiji walikuwa wamechafukwa Haswa, maana walikuwa wamechoka na Wizi wa Majaribu.

Majaribu alikuwa anakimbia huku Mapigo ya Moyo yakiwa yanaenda sipidi, yaani alikuwa kachoka Lakini bado alikuwa anaendelea na mchaka mchaka maana alikuwa anajua akikamatwa basi Hana Bahati, alikuwa analikata pori lile huku akiwa hajui hata anako kimbilia!.

Ikiwa ni majira ya kama Saa Kumi za usiku Majaribu akiwa anaendelea kusonga mbele ndani ya pori lile! Mara alishituka kuna mwanga mkali unamurika Kwa mbali kuja maeneo aliko.

"Heeeee ni Majini au watu Gani!? Nani yupo Porini huku Usiku huu!" Majaribu akiwa kajibana kwenye Mti alijiongelesha Kwa uwoga!.
Majaribu alitulia kuangalia ule mwanga unaelekea wapi, basi akiwa kabana kwenye Mti aliona watu kama watano wakiwa wanasogea kwenye upande aliko huku wakiwa wamebeba furushi!.

Baada ya watu wale kuhakikisha kuna usalama lile furushi walilirusha huku wakiwa Makini!.

"Sasa Jamani! Mimi nasubiriwa na ndege maana nimekodi! Narudi India! Hakikisheni kila kitu kinakaa Sawa!" Hayo yalikuwa ni maneno ya mwanamke mmoja ambaye ndo alikuwa mwanamke pekee yake kwenye kundi lile, maneno Hayo pia kijana Majaribu aliyasikia Vyema akiwa kajibana kwenye Mti!.

Basi watu hao walianza kuondoka kuelekea njiani ambako walikuwa wameliacha Gari lao!.
Kijana Kwa uoga hakutaka hata kuangalia kwenye furushi lile lililo rushwa na Wale Jamaa kuna nini, mdogo mdogo alianza kuzipiga hatua kuondoka yale maeneo maana aliona ni nuksi!.
Ila baada ya kupiga hatua kama Tatu hivi Majaribu alisikia kikohozi kikiwa kinatoka kwenye furushi lile, yaani kikohozi kilikuwa kinatoka Kwa taabu kweli kweli

"Heeeee!! Nini tena!? Mtu!!!!??" Majaribu kwanza aliganda kama kanaswa na sumaku alafu alijiuliza ni nini tena hicho!
Majaribu Kwa ujasiri na kujiamini alisogea mpaka pale kwenye furushi, alifungua Huku mapigo ya Moyo yakiwa yanamuenda kasi, hakika Siku hiyo Majaribu aliamini Watu wana Roho mbaya!.

Ndani ya furushi lile alionekana mwanaume wa makamo kidogo Miaka kama 50 na kitu akiwa kachomwa vibaya muno na visu, yaani alikuwa amekatwa katwa hovyo kila sehemu ni dhahiri mwanaume huyo alikuwa anapambana na uhai wake wa mwisho, yaani kama ni Israel mtoa Roho alikuwa tayari kavunja kufuri imebakia tu kuingia ndani kuchukua kilicho chake!.

"Heee! Mzee upo hai! Kwani umetokea wapi na Kwa Nini wamekutupa hapa!?" Kijana Majaribu aliuliza maswali mfululizo huku akiwa mguu Sawa maana aliamini huwenda hata yule Mtu akawa ni Jini, maana Kwa visu ambavyo vilikuwa vimepita mwilini Mwake ilikuwa ni ngumu kuamini kama yupo hai!!.

"Aaaaaa!! Ehuuu! Kijana naomba nisaidie Vitu Viwili tu na Mungu atakubariki!" Baba Yule akiwa anakohoa Damu aliongea Kwa taabu kweli kweli!.

"Vitu gani hivyo!? " Majaribu akiwa anajua tu ataombwa msaada aliuliza huku kichwani akiwa anajijibu mwenyewe kwamba atawezeja kumbeba Mtu yule kumtoa kule porini!.

"Mimi ni mchungaji ila nakiri kwamba ni mkosefu mbele za Mungu! Naomba Hii Dhambi utanitubia mbele ya Watu wote, kitu Cha Pili ndani ya kanisa Langu Mazabahuni Chini ya Viti vya Mazabahuni kuna Siri Zangu, naomba kamtafute Mtu anaitwa Melisa ni katibu wa kanisa kampe Hii Siri na mwambie kila Kitu ampe mwanangu na ndo urithi Wangu wa Pekee kwake, chonde chonde naomba hizo Siri usimwambie Mtu yeyote zaidi ya Melisa, Kitu Cha mwisho Mke Wangu Siyo Mtu mzuri" Baba yule akiwa anaongea Kwa taabu huku pumzi zikiwa zinamuishia alitoa maelezo ambayo kijana majaribu hakuelewa Hata Moja!.

"Mzee ebu toa maelezo Vizuri nikuelewe basi, kanisa la wapi na Siri gani hizo mbona unaongea Mambo sielewi!??" Majaribu akiwa kama kapaniki aliuliza, Lakini hakuambulia Jibu lolote maana tayari Baba yule alikuwa kaaga dunia baada ya kutoa maelezo!.
"Heeeee! Kafariki!?? Jamani hili Jina ntabadilisha Sasa naona linaniletea majaribu ya kweli! Haya si majaribu Sasa!!? Haya hilo kanisa Mimi ntajua la wapi!?" Kijana majaribu alibaki anajilalamisha pale porini!.

Huu ni mwanzo mzuri wa Mkasa huu wa kusisimua Naamini hutojutia kuifuatilia hadithi hii, Je ipi safari ya Majaribu!.

Tukutane sehemu ya 2


Hadithi: MAJARIBU

Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)

Sehemu: 2

"Heeeee! Kafariki!?? Jamani hili Jina ntabadilisha Sasa naona linaniletea majaribu ya kweli! Haya si majaribu Sasa!!? Haya hilo kanisa Mimi ntajua la wapi!?" Kijana majaribu alibaki anajilalamisha pale porini!.

Ulikuwa ni usiku mbalamwezi ikiwa inaangaza na kufanya kila sehemu ionekane vyema, kijana Majaribu Alisimama Huku Jasho jembamba likiwa limeanza kumtoka! Gafla radi nazo zilianza kupiga na wingu zito la mvua kutanda Juu!.

"Ujinga sitaki kila Mtu atabeba mizigo Yake!" Kijana Majaribu alijiongelesha mwenyewe na kuanza kuzipiga hatua, Huku manyunyu ya Mvua yakiwa yameanza kushuka! Majaribu alitembea mpaka aliikuta barabara ya Lami ambayo ilikuwa imekatiza katikati ya Msitu ule!.
Kijana Majaribu alijikuta Roho yake imeanza kuuma Muno, Yaani kuna akili ilikuwa inamwambia arudi porini tena aliko muacha Yule Baba!.

Baada ya Majaribu kuwaza na kuwazua aliamua kurudi porini tena, baada ya kufika kitu alicho kifanya aliamua kuukokota mwili ule mpaka Barabarani, Japo kuwa barabarani palikuwa mbali na pale ulipo tupwa ule mwili wa Yule Baba Lakini Majaribu alipambana na kuufikisha barabarani!.
Baada ya Majaribu kuhakikisha mwili kauweka sehemu ambayo aliamini ni salama aliangaza huku na Kule ili aone ni wapi aelekee, ilikuwa ni Majira ya Saa Kumi na moja alfajiri kuelekea Saa kumi na mbili kifupi kulikuwa kumeanza kupambazuka kabisa!.
Ila bahati mbaya kijana Majaribu akiwa anaukokota mwili na kuuweka pale barabarani kuna Gari ilipita maeneo Yale na ndani ya Gari lile alionekana Dada wa Miaka kama 30 Hivi akiwa anaendesha, kwanza baada ya kufika mbele kidogo Dada yule alisimama na kurudisha Gari kinyume nyume, Kisha alisimamisha na kushuka.

"We dogo Vipi unafanya Nini hapo!?" Yule Dada alimuuliza kijana Majaribu tena alionekana anaogopa Muno!.

"Aaaaaa! eeeeeee!! Nimemkuta kauawa katupwa porini!" Majaribu akiwa na kigugumizi alijibu
Yule Dada alirudi kwenye Gari lake, baada ya hapo alitoka na Simu yake alimpiga picha kama Tatu hivi Majaribu, na alimrekodi video fupi Majaribu, kijana Majaribu alikuwa haelewi hata kinacho fanyika, yaani alikuwa haelewi Dada yule anafanya nini Yeye alibaki kaganda pale pale huku Chini Mwili wa Yule Baba ukiwa umelala.

"Watu wengine bwana ndo nini Sasa! Aisee Mimi nishamaliza Kazi Yangu!" Majaribu akiwa na Hasira alijiongelesha na kuanza kuondoka Huku akiwa ameanza kula jaramba Kwa kukimbia!.
Dada yule naye baada ya kurudi kwenye Gari Moja Kwa Moja alipiga Simu kituoni kutoa taarifa ya tukio la Mauaji, maana alicho Amini ni kwamba Yule dogo huwenda ndo kaua.

Masaa yalizidi kusogea! Ikiwa ni kama Saa mbili kijua kikiwa kimeanza kuwaka Majaribu alionekana akiwa kanyosha barabara anaelekea Mjini, yaani alikuwa hataki kurudi Kijijini kwao Tena, ila akiwa anaelekea Mjini alipishana na Gari za Askari kama mbili zikiwa kasi kweli kweli kuelekea kule aliko tokea!.
Majaribu hakugundua haraka haraka kwamba Gari zile ni wapi zinaelekea yeye aliendelea kuzihesabu hatua tu kusonga mbele.
Baada ya kama lisaa Sijui Nini kilitokea huko ziliko elekea Gari za Askari, Majaribu alishangaa anasikia king'ora Cha Askari tena Gari zikiwa zinarudi Kwa Kasi, huku mbele ya Gari zile kukiwa na Gari nyeusi ambayo ilikuwa inaendeshwa na mdada yule yule aliye mpiga Majaribu picha!.

Gari zile zilipo fika pale alipo Majaribu zilisimama na Askari walishuka, Huku Majaribu akiwa kando ya Barabara anatumbua tu Macho.

"Dada vipi mbona tunasimama!??" Askari ambaye alikuwa kiongozi wa msafara alimfuata Yule Dada ambaye alikuwa yupo mbele na Gari yake!.

"Afande, kijana mwenyewe ndo huyo Hapo!?" Yule Dada akiwa anamnyoshea kidole Majaribu aliongea!.
Kwanza Majaribu alishangaa kumuona Yule Dada Kwa Mara nyingine, Macho yalikuwa yanamtoka huku akiwa haelewi kipi ni kipi!.

"Jamani mbona sielewi kuna nini!?" Kijana Majaribu aliuliza Kwa mshangao, lakini badala ya kupewa majibu alipigwa Bonge la Kofi mpaka mate yalimruka mdomoni pasina kupenda, ilibidi Majaribu atulie kama kamwagiwa maji.
Bila hata huruma alirushwa kwenye defenda kama gunia vile, yaani alidondokea Mkono vibaya Muno kiasi kwamba Mkono wake uliteguka na kuumia, Lakini Majaribu ilibidi abaki anagugumia maumivu ndani Kwa ndani!.

Askari wale walirudi Eneo la tukio walibeba mwili wa Yule Baba ambaye alikuwa kauawa baada ya hapo safari ya kuelekea kituoni ilianza!.
Ni ndani ya sekunde tu picha ya Baba Yule akiwa kakatwa katwa vibaya na visu ilianza kusambaa Mitandaoni na kufanya kila Mtu ambaye alikuwa anamjua Baba huyo kushika kichwa, haieleweki ni Mtu gani alikuwa kampiga picha zile Baba Yule na kusambaza mtandaoni.

Turudi ndani ya Jumba la kifahari ambako tulimuona Yule Dada akishuhudia tukio la kutisha usiku.

Asubuhi na mapema kabisa Dada yule aliamka Huku Bado Mwili wake ukiwa unatetemeka! Yaani kile alicho kiona usiku bado kilikuwa kinampa kiwewe!. 
Dada Yule alishika Simu yake na kuwasha Dada, kwanza baada ya kuwasha tu data, ujumbe ulianza kutiririka kwenye Simu Yake Kwa upande wa Whatsapp! Dada Yule alifungua Whatsapp yake alikutana na SMS kama 10 mojawapo ilikuwa ni Video ambayo alikuwa katumiwa na Namba iliyo seviwa "Boss Mama mchungaji ".

Video hiyo Dada yule aliifungua, ilikuwa ni video ambayo alikuwa katumiwa na Boss wake ambaye Kwa muda huo alikuwa yupo India, na ilikuwa ni salamu tu za Asubuhi!.

"Revina Haiii, Hamjambo Huko Home!? Huku India Sisi tupo poa as You see!!" Hayo yalikuwa ni maneno ambayo Mama yule alikuwa kayazungumza kwenye video!.
Kwanza Dada yule Kwa Jina la Revina alishangaa Muno, yaani ilikuwa Mara ya kwanza Kwa Boss wake huyo kumtumia video ya kumtakia Hai, Boss wake huyo alikuwa ni Mtu wa Roho mbaya Muda wote Kwa upande wake na kila Siku ilikuwa ni kuoga matusi na kipigo japo kuwa mwanamke Huyo alikuwa Mke wa mchangaji!.

Basi Revina aliachana na ujumbe Ule huku akiwa anataka kusoma na ujumbe mwingine, ila kabla hajafungua ujumbe mwingine Mara alisikia ni kama kuna makelele getini!.
Revina alitoka mpaka nje alikutana na Nyomi ya watu pale nje!.

"Eheee Revina Bora umekuja!? Ni kweli Mchungaji Nemeke kauawa!! Na Jana alirudi nyumbani au hakurudi!?" Hilo lilikuwa ni swali kutoka Kwa Baba Mtu mzima ambalo Dada yule alikutana nalo baada ya kutoka nje!
Revina Macho tu yalikuwa yanamtoka alikuwa haelewi hata kinacho endelea, yaani kila alipo kumbuka kile alicho kiona usiku mwili wake ulibaki unasisimuka tu!.

Kabla Revina Hajajibu swali lile Mara kuna Gari ya Askari ilifika pale nyumbani! Na Muda huo idadi ya Watu ilikuwa inazidi kuongezeka, maana Bwana aliye uawa alikuwa ni Mtu maarufu pale Mjini, ukiachana na uchungaji Wake pia alikuwa mfanyabiashara mkubwa.

Revina alichukuliwa na askari waliingia mpaka ndani Kwa ajili ya kumhoji baadhi ya maswali!.

"Binti, mchungaji Nemeke Jana Usiku alilala Hapa nyumbani au hakulala!!?" Hilo lilikuwa ni Swali la kwanza ambalo Revina aliulizwa!.

"Alilala hapa nyumbani!?" Revina akiwa anatetemeka alijibu!.

"Eheee baada ya kulala nini kilitokea!?? Au usiku kuna Hali yoyote Isiyo ya kawaida ilitokea!??" Revina aliulizwa tena, Lakini Binti huyo mdomo wake Ulionekana kutetemeka yaani alikuwa haelewi ajibu Nini!.

"Okay afande Mika Huyu tunaondoka naye inaonekana kuna Vitu anajua!" Basi askari kiongozi wa msafara aliongea baada ya kuona Revina kashikwa na kigugumizi, baada ya hapo askari walielekea mpaka chumbani ambako ndo ilisadikika marehemu alikuwa analala yeye na Mkewe!.
Ndani ya chumba hicho palikuwa Safi kabisa na palikuwa pametandikwa vizuri kiasi kwamba hakuna kilicho tokea!.
Ila katika askari wanne walio ingia kule chumbani, kuna askari mmoja aliona madoa kama mawili ya Damu ukutani, Askari huyo aliamua kuvunga na wala hakuwashirikisha wenzake kitu alicho kiona!.

"Inaonekana Huyu Mtu hakulala hapa, Huyu Binti kuna Vitu kadanganya!" Baada ya ukaguzi basi askari kiongozi aliongea na kweli askari waliondoka pale nyumbani huku wakiwa wameambatana na Revina kuelekea naye kituoni.
Upande wa huku kituoni kijana Majaribu alikuwa anachezea kipigo cha maana huku akiwa anaulizwa maswali!.

"Kwa nini umemuua mchungaji Nemeke!?? Ulitumwa na Nani au ulishirikiana na nani!?" Hayo ni miongoni mwa maswali ambayo Majaribu alikuwa anaulizwa! Kijana Majaribu alijaribu kutoa maelezo Lakini swali zito lilikuwa ni kwamba alikuwa anafanya nini Porini Usiku ule!?.

"Kijijini kwetu walitaka kuniua wakidai Mimi ni Mwizi Kwa hiyo Katika Hali ya kukimbia Usiku ndo nilikutana na watu wanatupa Mwili Porini!" Majaribu alitoa maelezo Lakini badala ya kujiokoa ndo alijikuta anaongeza Matatizo!.

"Afande Gozi unaona, nimesema Huyu dogo anahusika! Ona anasema yeye ni Mwizi! Yaani huyu dogo muhuni kuna kitu anajua!" Basi kuna afande aliongea Kwa mizuka!.
Muda huo huo Revina naye alifikishwa pale kituoni Kwa ajili ya mahojiano zaidi!.

Lakini ilikuwa tofauti badala ya askari upelelezi kumhoji Revina kwenye chumba Cha upelelezi iliamuliwa kwamba Binti huyo apelekwe kwenye ofisi ya Mkuu wa kituo ndo akahojiwe huko tena na Mkuu!
Revina baada ya kufikishwa kule ofisini baada ya kutishiwa kidogo na Yule mkuu wa kituo, Revina alianza kuropoka kila kitu alicho shuhudia usiku! Yaani mpaka Yule mwanamke anaye fanana na Boss wake alimuelezea huku akiwa anahisi huwenda ni Boss wake.

"Binti Sikiliza ukitaka kuwa Salama hayo maelezo usije ukatoa sehemu yoyote utaenda kufia Jera au kufa kabisa, Nakuandikia maelezo Hapa chochote utakacho ulizwa hayo ndo Majibu itabidi uyatoe na huo ndo usalama wako!" Hayo yalikuwa maneno ya Mkuu wa kituo Cha polisi!.
Ni kweli Revina aliandikiwa maelezo kwenye karatasi na kuanza kuyameza kama yalivyo baada ya kama lisaa limoja alitolewa na kuruhusiwa arudi nyumbani!.

"Kwa maelezo ya Huyu Binti, kijana Huyu kuna Namna anahusika kwenye mauaji, maana Binti anasema kijana Huyu alikuja mchana pale nyumbani Kwa mchungaji!" Basi Mkuu wa kituo baada ya kutoka kumhoji Revina hayo ni maelezo ambayo alitoka nayo!.
Hapo kesi ilizidi kuwa kubwa na ngumu Kwa kijana Majaribu!.

Yule Dada ambaye alikuwa kampiga picha alikuwa kathibitisha kwamba alimuona Majaribu akikokota mwili na kuuleta barabarani! Hakika Majaribu alikuwa kapatikana yaani kila maelezo aliyo yatoa alionekana ni Muongo tu.

Mitaani taarifa ilikuwa ni Moja tu kuuawa kwa mchungaji Nemeke, yaani kila Mtu alikuwa anaongea lake!.

"Yaani nasikia mchungaji Nemeke alikuwa kwenye maombi huko milimani ndo alikutana na wauwaji!"

"Masikini Mke wake ndo kwanza yupo India nasikia anafanya matibabu ya mguu!"

"Nasikia muuaji ni Chali tu aisee! Hii noma!"

"Sema tuache yote kinacho niuma mwamba kafariki Bila hata kuwa na mtoto, yaani hajaacha chata yoyote kitaa"

"Hivi ni kweli Hana mtoto! Ujue kuna Kipindi nilisikiaga mchungaji kazaa na mwanamke wa Nje!?"

"Aaaaaa huo ulikuwa uvumi tu wa kumchafua Mchungaji, si unajua Mti wenye matunda ndo hupigwa Mawe!" 
Hayo yalikuwa ni mazungumzo ya baadhi ya vijana kwenye vijiwe wakizungumzia Kifo Cha mchungaji Nemeke.
Ilikuwa ni Siku ya kuuaga mwili wa mchungaji Nemeke kwenye Moja ya kanisa kubwa ambalo lilikuwa lipo pale mjini, na ndo kanisani ambalo lilikuwa linaongozwa na mchungaji Huyo, kila muumini wa kanisa Hilo alikuwa analia kilio Cha Aina Yake!.
Na hiyo ndo Siku ambayo Mke wa mchungaji alikuwa anarudi kutokea India, na alirudi Huku akiwa kafungwa mhogo na bandeji za kutosha mguuni, yaani Kwa Jinsi ambavyo mwana Mama huyo alikuwa anajitirisha huruma kila Mtu alijikuta anamuonea huruma pale kanisani na ndo vilio vilizidi zaidi na zaidi.

Je Ipi hatima ya Kijana Majaribu!?? Je kijana Majaribu ni nani!? Na ipi Historia Yake!? Vipi kuhusu Mauaji ya Mchungaji itakuaje? Na Sababu za kuuawa ni zipi!? Usipange kukosa miendelezo ya simulizi hii Tamu.


Maoni 2 :

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu