Mpya
Hadithi: MAJARIBU
Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)
Sehemu: 3
Na hiyo ndo Siku ambayo Mke wa mchungaji alikuwa anarudi kutokea India, na alirudi Huku akiwa kafungwa mhogo na bandeji za kutosha mguuni, yaani Kwa Jinsi ambavyo mwana Mama huyo alikuwa ananitirisha huruma kila Mtu alijikuta anamuonea huruma pale kanisani na ndo vilio vilizidi zaidi na zaidi.
Pale kanisani vilikuwa ni vilio hata ibada haikufanyika ipasavyo, kitu ambacho kilikuwa kinawaliza wengi mchungaji Nemeke alikuwa ni Mtu anaye toa Muno na kusaidia watu maana alikuwa na Mali za kutosha, Pia alikuwa kajitolea kulea baadhi ya Watu wasio jiweza, kifupi Alikuwa anasaidia watu Muno Japo kuwa naye alikuwa na mapungufu Yake n madhambi yake ambayo ilikuwa Siri yake.
Basi baada ya Ibada Mwili wa mchungaji Nemeke ulipelekwa kwenye uwanja wa wazi , yaani hapo ilikuwa kama mafuriko Ya Watu walio jitokeza kumuaga!.
Siku Hiyo ilipita, Siku nyingine ilifika ikiwa ni Siku ya kupumzisha Mwili wa Nemeke! Yaani Mke Wake alikuwa analia anazimia na kuzinduka huku akiwa anashikiriwa na Watu!.
Binti Revina alikuwa anamkata Jicho Muno Boss Wake yaani yule Mke wa mchungaji, ni dhahiri Binti huyo alikuwa kaanza kubaini kitu!.
Revina akiwa Makaburini ambako Mwili wa marehemu ulikuwa unazikwa kuna Sura aliona pale makaburini, ilikuwa ni miongoni mwa Sura aliyo ishuhudia Usiku wa tukio pale nyumbani, Mtu huyo alionekana yupo mbele mbele kushugurikia maswala mbali mbali pale msibani!.
"Samahani Mama yule Baba aliyevaa suti ya Kijivu na tai nyekundu unamjua!?" Binti Revina aliamua kumuuliza Mama ambaye alikuwa kakaa naye Karibu!.
"Yes Yule ni katibu wa Jimbo Kwa hiyo ni mhusika mkubwa hapa maana mchungaji aliye fariki alikuwa kwenye Jimbo lake" Mama Yule alijibu kistaarabu, Revina hakuongeza Swali jingine lolote alitulia Huku akiwa na mawazo mengi Kweli kweli.
Binti Revina alikuwa ni mdada wa Kazi ambaye alikuwa kaajiliwa pale nyumbani Kwa Mchungaji, Binti Revina alikuwa hajawahi kuwajua wazazi wake maana alikuwa amekulia kwenye kituo Cha watoto Yatima na baada ya kufikisha Miaka 12 aliingia mtaani na kuwa mtoto wa mtaani mpaka pale alipo saidiwa na mchungaji Nemeke na kumfanya mtoto wa pale nyumbani anaye saidia kazi ndogo ndogo, mchungaji Nemeke alikuwa anamchukulia Revina kama mwanae tu, Lakini ilikuwa tofauti na Mke Wake ambaye alikuwa anamtesa Muno Revina, yaani ule upendo Ambao Revina alikuwa anaoneshwa na Mchungaji Nemeke ulikuwa unamkera Muno Mama mchungaji.
Basi Siku hiyo mazishi yalifanyika na Historia ilisomwa kwamba marehemu hajaacha mtoto yeyote! Ni watu wachache Sana Ambao walikuwa wanajua Siri ya mchungaji Nemeke na baada ya Historia kusomwa walibaki kucheka tu Chini kwa Chini.
Zilipita Siku kama mbili Huku kituoni Mambo yalikuwa yanazidi kuwa mazito Kwa kijana Majaribu, tayari kesi Yake ilikuwa imepelekwa mahakamani! Huku yeye akiwa ndo anaonekana kama muuaji!.
Baada ya Wiki Tatu kupita huku Majaribu akiwa ananyea debe Gerezani kama mtuhumiwa hatimaye Siku ya Kwanza kusikiliza kesi ilifika, Majaribu alikuwa haelewi chochote Kwanza alikuwa hana hata Mtu wa kumtetea! Alivyo fikishwa kizimbani na kuulizwa kama ana wakili yeyote Majaribu alibaki anatumbua Macho tu, maana alikuwa hajui hata wakili ni nani!.
"Jina Langu naitwa Majaribu, huyo wakili simjui" kijana Majaribu akiwa serious alitoa Jibu ambalo lilifanya Watu waanze kuchekea Chini ya meza, maana kucheka mahakamani ni mwiko, hata Hakimu alitamani kucheka!.
Baada ya kuonekana Majaribu hana Hata wakili Basi alianza kuulizwa maswali baada ya kusomewa mashtaka yake!.
Majaribu aligoma kabisa kuhusika na kifo Cha Mchungaji Nemeke, lakini Kwa Namna ambavyo alikuwa anaulizwa ni kama alikuwa analazimishwa kukubali makosa kwamba yeye ndo kaua.
Siku hiyo kesi iligairishwa, kijana Majaribu alirudishwa rumande, baada ya Siku kama mbili kuna askari alikuja kumtembelea Majaribu pale Gerezani!.
Alikuwa ni Askari ambaye Kwa Mara ya mwisho tulimuona kwenye upelelezi akificha Siri baada ya kushuhudia madoa ya Damu ukutani! Alikuwa anaitwa Afande Jedi!.
"Dogo nataka kukusaidia! Nambie ukweli kutoka moyoni wewe uliuwa au hukuuwa!?" Basi baada ya afande yule kukaa faraghaa na Majaribu alianza kumuuliza maswali!.
"Haki ya Mungu naapa, Mimi sijaua bro! Yule Mtu alitupwa na watu fulani usiku Porini na Mimi niliona!"
"Okay Vipi walivyo mtupa Wewe ulichukua hatua gani!? Na je uliwaona sura hao watu! Na walikuwa wangapi!?" Majaribu aliulizwa tena!.
"Kiukweli Mimi nilijificha mpaka walipo ondoka, Lakini nikiwa nataka kuondoka niligundua yule Baba bado hajafa nilienda kumfungua kwenye kile kiroba, ila kabla hajafa kuna Maneno aliniambia!" Majaribu alizidi kutoa maelezo!.
"Eheee! Alikwambiaje!??" Afande yule aliuliza, kijana Majaribu kwanza aliwaza alikumbuka Jinsi alivyo sisitiziwa na marehemu kwamba ile Siri asimwambie Mtu yeyote zaidi ya huyo aliyemtaja kwamba ni katibu wa kanisa!
"Aliniambia kwamba Mke wake Siyo Mtu mzuri!" Kijana Majaribu aliamua kuongea maneno machache miongoni mwa mengi aliyo ambiwa, mengine aliamua kuyaacha.
"Vipi walio utupa Mwili ukibahatika kuwatambua na ukiwaona unaweza kuwajua!?" Afande Yule aliuliza huku akionekana kuna Vitu ashaanza kuvijua!.
"Japo ulikuwa Usiku ila kutokana na mbalamwezi niliwaona vyema, walikuwa wanaumme wanne na Mwanamke mmoja, Tena nimekumbuka mwanamke yule nilismikia anasema anarudi India Kwa ndege ya kukodi!" Majaribu alitoa maelezo ambayo yalifanya afande yule atikise kichwa, kwanza alitoa Simu yake na kuingia Instagram alitafuta Jina la Rehema Nemeke, baada ya kuipata akaunti hiyo alitafuta picha mojawapo ambayo amewahi Post huyo Rehema!.
"Hii sura umewahi kuiona!?" Yule afande baada ya kufungua ile picha alimuonesha kijana Majaribu.
"Ndo Huyu Huyu mwanamke nilimuona Usiku ule, afande Mimi Macho Yangu yapo vizuri hata kuwe Usiku naona vyema ni Huyu huyu mwanamke tena alikuwa kavaa miwani!" Kijana Majaribu aliongea Kwa mizuka Huku akiwa anaona kama anaenda kupona hivi kwenye ile kesi!.
Ila mahojiano Yale yakiwa yanaendelea kuna askari magereza alionekana anasikiliza Kwa Siri, kifupi Alikuwa mkuda!.
"Sasa dogo sikiliza Hii kesi ni nzito kwako!? Hii Siri hatakiwa Mtu yeyote kuijua mpaka Siku ya kesi, na Siku hiyo Mimi ntakuletea mawakili, Wewe kazaa usimwambie Mtu yeyote sawa dogo!?" Afande Jedi aliongea Kwa msisitizo haswa, baada ya hapo aliondoka zake kurudi kituoni ambako alikuwa anafanyia Kazi!.
Afande Jedi baada ya kufika tu kituoni kabla hajaingia ndani alipo fika mapokezi tu alikutana na Barua ya kufukuzwa Kazi! Kwanza jicho lilimtoka huku akiwa haamini kama kibarua Cha uaskari kimeota nyasi!.
Afande Jedi akiwa na hasira alizama mpaka Kwa mkuu wa kituo hicho kuuliza sababu za yeye kufukuzwa Kazi!.
"Afande Jedi!?? Wewe umekuwa fukunyuku Muda mrefu Sana, yaani unapenda kufuatilia kesi ambazo hazikuhusu, Wewe Hii kesi ya kifo Cha mchangaji Nemeke haikuhusu hata kidogo na walio pewa kuipeleleza ni wengine, kinacho kuwasha na kuanza kuifuatilia ukaacha kesi zako ulizo pangiwa ni nini!!!?, Kwa mantiki Hiyo unadharau mamlaka inayo panga majukumu, mpaka hapo una Kosa la kudharau Mamlaka ambalo adhabu yake ni kufukuzwa kazi, kama ni onyo tushakupa Mara nyingi tu!" Hayo ni majibu ambayo afande Jedi alipewa na Mkuu wa kituo!.
Kwakuwa afande Jedi alikuwa anajua kinacho endelea aliamua kuondoka Kwa hasira, pamoja na hasira zake ndo hivyo kazi alikuwa hana tena!.
Siku zilizidi kusogea hatimaye mwezi mmoja ulikatika, Siku ya kurudi mahakamani ilifika tena!.
Kijana Majaribu aliulizwa kama anaye wakili, Lakini kila Mtu akiwa anaamini Majaribu Hana wakili Mara kuna Mzee wa makamo kidogo alisimama na kudai Yeye ndo mwanasheria atakaye msimamia Majaribu!.
Kesi ilianza kusikilizwa, Kwanza baadhi ya mashahidi waliletwa akiwemo Revina na yule Binti aliye Ona Majaribu akikokota Mwili kule porini.
Binti Revina alitoa maelezo ambayo alikuwa kamezeshwa, yaani aliyatoa kama yalivyo!.
"Ndugu hakimu napinga Maelezo ya huyo Binti, Kwa Upelelezi nilio ufanya ni dhahiri Kifo Cha Mchungaji kilifanyika pale nyumbani, na Kwa ratiba ya Mchungaji Siku hiyo ilikuwa siyo Siku ya maombi kwake!! Je tunaomba Shahidi athibitishe wakati anaenda kulala marehemu alikuwa kaondoka au alikuwa bado hajaondoka!?" Mwanasheria ambaye anamuwakilisha Majaribu alikuwa ni mzoefu kweli kweli yaani alikuwa na maswali ya mtego isivyo kawaida.
"Eeeeeee!! aaaaaa! Ninavyo Enda kulala Baba alikuwa eeee eeee! Alikuwa ameondoka!" Binti Revina akiwa anatetemeka alijibu!.
"Okay Wewe ulilala Saa ngapi na mchungaji aliondoka Saa ngapi!!?" Revina alipigwa Swali tena!.
"Nililala Saa Nne Baba aliondoka Saa Mbili Usiku!" Revina alijibu huku Mapigo ya Moyo yakiwa yanaenda kasi!.
"Mheshimiwa hakimu Huyu Binti anadanganya, Kwa maelezo ya Mlinzi wa getini amesema mchungaji aliondoka Jioni, Kwa Nini yeye anasema aliondoka Usiku!??" Mwanasheria Yule akiwa anazidi kusokomeza maswali! Hakimu aliamua kuahirisha kesi gafla baada ya kuona Binti Revina kaanza kupaliwa na maswali!.
Kijana Majaribu alifurahi na alianza kuona dalili za yeye kuokoka kwenye ule Msala!.
Basi Majaribu alirudishwa rumande, upande wa Afande Jedi naye akiwa kafukuzwa Kazi alizidi kufanya upelelezi wake Chini Kwa Chini, na kila kitu anacho kibaini alikuwa anamshirikisha mwanasheria aliye mtafuta yaani Yule Mzee.
Mpaka Siku ya kesi inafika Mr Jedi na Yule mwanasheria walikuwa wamebahatika kujua vitu vingi Muno! Jedi alikuwa anajua kabisa Kwa ushahidi walio ukusanya lazima kijana Majaribu ataachiwa! Haieleweki Kwa Nini afande Jedi alikuwa kachagua kumsaidia Majaribu!.
Siku Zote Pesa inaweza kubadili hata welekeo wa Maji mtoni! Mr Jedi hakuamini macho yake Siku ya Kesi ilipo wadia, yule mwanasheria wake alimgeuka, yaani badala ya kuwa upande wa Majaribu yeye alikuwa anamsokomeza na kumfanya Majaribu aonekane ni mharifu zaidi!.
"Ndugu Hakimu, mteja Wangu alikiri mbele Yangu kuhusika na tukio hilo ila anacho dai mchungaji Nemeke ndo alikuwa mwanzilishi wa ugomvi Kwa Madai kwamba alienda kufanya maombi Porini kwao!" Hayo ni maelezo ya yule mwanasheria ambayo yalifanya Mr Jedi na Majaribu mwenyewe wabaki wameacha midomo wazi pale mahakamani!.
Je ipi hatima ya Majaribu ambaye anaonekana kuwa kwenye wakati mgumu!??
Tukutane sehemu ya nne
Hadithi: MAJARIBU
Mtunzi:Mwaki Ze Done (0653814440)
Sehemu: 4
"Ndugu Hakimu, mteja Wangu alikiri mbele Yangu kuhusika na tukio hilo ila anacho dai mchungaji Nemeke ndo alikuwa mwanzilishi wa ugomvi Kwa Madai kwamba alienda kufanya maombi Porini kwao!" Hayo ni maelezo ya yule mwanasheria ambayo yalifanya Mr Jedi na Majaribu mwenyewe wabaki wameacha midomo wazi pale mahakamani!.
"Muongo! Muongo Mimi sijawahi kuzungumza naye anaongea uong, kwanza simjui" Kijana Majaribu akiwa kapaniki huku akiwa yupo kizimbani aliropoka Kwa Sauti ya juu tena bila utaratibu wala kuruhusiwa na Hakimu!.
Kwanza Hakimu alipiga nyundo kwenye meza na kufoka!.
"Wote tutulie ni Muda Sasa wa kutoa hukumu!" Hakimu akiwa na Sura ya Kazi aliongea,na Kwa Jinsi Hakimu alivyo kuwa anaendesha Kesi ile alionekana ni kama ana Maelezo kabisa, yaani baada ya maelezo ya Yule wakili hakutaka kusikiliza maneno mengine tena.
"Majaribu Majaribu! Amepatikana na kosa la kumuua Mchangaji Nemeke kimakusudi kabisa Kwa kutumia siraha! Adhabu yake ni kifungo Cha maisha Gerezani na Kazi ngumu!" Hakimu akiwa anamaanisha alitoa hukumu baada ya hapo aligonga nyundo na kusimama kisha aliondoka!.
Mr Jedi alibaki kaacha mdomo wazi akiwa haamini kama dogo ndo anaenda kunyea Debe, pia kijana Majaribu alikuwa anaona kama ndoto, yaani alikuwa anaona Dunia nzima inamzomea!.
"Mbona sielewi naota au ni laivu imekaaje kaaje mpaka tunafikia huku aisee!" Kijana Majaribu alikuwa anajiuliza maswali ambayo yalikuwa hayana Majibu.
Kijana Majaribu kabla ya kupelekwa Huko Gerezani kwenda kuanza kutumikia adhabu hiyo kwanza aliomba akutane na katibu wa kanisa ili kama anaweza amuelezee Siri ambayo alikuwa kaambiwa na marehemu!.
Basi Muda ule ule taarifa zilimfikia Katibu wa kanisa, alikuwa ni Mama Mtu mzima kidogo.
Majaribu alipelekwa pale Gerezani kwa ajili ya kuanza Sasa kutumikia kifungo Chake huku ikiwa imepangwa kwamba baada ya Wiki Moja ahamishwe Gereza na kupelekwa gereza analo stahili kutokana na makosa yake.
Ikiwa ni majira ya Jioni Katibu wa kanisa alionekana kaambatana na Baba Mtu mzima wakiwa ndani ya Gari na safari yao ilienda kuishia mpaka pale Gerezani!.
Majaribu aliitwa Kwa ajili ya kwenda kuzungumza na katibu wa kanisa kama alivyo agizwa na mchungaji! Kabla hajakata kauli!.
Baada ya Majaribu kufika kwenye chumba Cha mazungumzo alishangaa kumuona Mama Mtu mzima akiwa kaambatana na mwanaume ambaye Sura yake ilikuwa siyo ngeni machoni pake!.
Majaribu alivuta kumbukumbu vizuri, ile Sura aliikimbuka kwamba ni miongoni mwa Sura alizo ziona pale porini Siku ya tukio!.
"Samahani Mama Wewe ndo Katibu wa kanisa au Huyu Baba!?" Majaribu macho yakiwa yamemtoka Huku akiwa anajiuliza maswali mengi Muno aliuliza!.
"Mini ndo Katibu wa kanisa na nimepokea ujumbe kwamba kuna Siri unataka kunipa!"Yule Mama alijibu!
"Okay tunaweza tukabakia wawili kwani!?" Majaribu aliuliza!.
"Usiwe na wasiwasi Wewe ongea tu huyu ni Mume Wangu wala usiogope!?" Yule Mama aliongea maneno ambayo yalifanya kijana Majaribu ashituke Muno!.
"Kijana usiwe na wasiwasi Mimi ni Mtu mwema! Ongea tu kila Kitu!" Yule Baba ambaye alikuwa ni Katibu Mkuu wa Jimbo aliongea, na alikuwa ni Baba ambaye alikuwa na familia Lakini alikuwa na mchepuko na mchepuko wake alikuwa ni yule katibu wa kanisa ambaye alikuwa anajulikana Kwa Jina la Melisa.
"Okay kitu ambacho marehemu aliniambia kabla ya kufariki aliniambia nikupe ujumbe kwamba mtunze mtoto wake na pia Mali Zake zote umsaidie mtoto wake azipate!" Kijana Majaribu baada ya kuona huwenda kuna kitu kipo nyuma ya pazia kinaendelea aliamua kuficha Siri ambayo aliambiwa na Mchungaji, aliongea tu maneno ya juu juu, yaani Majaribu Roho tu iligoma kumpa Yule Mama Siri.
"Kwani Vipi ndo hicho tu alicho kwambia!? Hakuna kingine!?" Mama yule Kwa Jina la Melisa au Katibu wa kanisa aliuliza huku akionekana kukerwa na taarifa nyepesi kama zile!.
"Ndiyo Mama ndo hicho tu nilitaka nikwambie!" Majaribu alijibu!, Basi Mama Yule na bwana yule waliondoka pasina kuongea Neno lolote wala kutoa asante Kwa Majaribu Kwa ile taarifa!
"Inawezekana Vipi Mtu aliye husika na kifo yupo na Mtu niliye ambiwa nimpe Siri!? Au Huyu Mama ndo aliwatuma na yule Baba hakujua!?? Uuuuu!! Mbona sielewi hii Siri ntabaki nayo Mimi mwenyewe mpaka kufa Kwangu!" Kijana Majaribu alijikuta anapata mawazo mengi Muno!.
Basi Siku hiyo ilipita! Zilipita Siku nyingine kama Tatu hivi!, Mr Jedi alionekana ni Mtu anaye dhurura huku na kule kutafuta taarifa ili kujua ukweli kuhusu Kifo Cha Mchungaji Nemeke!.
Mr Jedi alikuwa ni Mtu mwenye kipaji Cha pekee linapo kuja swala la upelelezi kitu ambacho alikuwa hajajaliwa ni elimu kubwa ambayo alikuwa hajaipata, yaani alikuwa na Elimu ya kawaida kiasi kwamba hata pale kituoni alikuwa ni askari asiye na cheo Chochote mpaka anafukuzwa, ila Mr Jedi alikuwa ni Mtu mwenye kipaji Cha kupeleleza Jambo na akajua ukweli, yaani kuna Muda alikuwa anatumia mpaka hisia kwenye kupeleleza na hakosei!.
Haieleweki ni Kwa Nini Mr Jedi alikuwa kaamua kulivalia swala lile njuga na kulifuatilia kiundani.
Baada ya Mr Jedi kupeleleza Kwa Siku kadhaa kuna Vitu Vingi alivigundua na Siku hiyo aliamua kwenda Gerezani kuonana na kijana Majaribu ili aone Namna ya kumsaidia maana alikuwa na asilimia zote kwamba Majaribu hajauwa!.
Kijana Majaribu baada ya kuitwa na kuambiwa kwamba kuna mgeni wake alitembea haraka Muno kwenda kuona mgeni aliye mtembelea, ila baada ya kuiona Sura ya Mr Jedi Majaribu alinyong'onyea maana alikuwa anaamini Yule ni miongoni mwa watu walio fanya yeye awe pale!.
"Bro kuna Nini tena!?? Wewe na yule Mzee wako si mliamua kkkunichoma!? Eheee umefuata nini hapa!?" Majaribu akiwa na Hasira aliuliza!
"Hakuna Mtu atakaye kusaidia zaidi Yangu! Napambana usiku na mchana Wewe utoke, nilipambana hata mwanzo ila Yule Mzee pesa zilimpumbaza na hatimaye mahakamani alitugeuka" Mr Jedi alitoa maelezo ambayo yalifanya walau kijana Majaribu akae kusikiliza kile alicho itiwa!.
"Eheee kilicho kuleta ni kipi!?" Majaribu aliuliza!.
"Sikiliza kuna Vitu kadhaa nimevijua kuhusu marehemu, kwanza nimegundua mkewe wa Ndoa ndo aliye husika na kifo Chake kushirikiana na baadhi ya watu na sababu ya mkewe kumuua mchangaji Nemeke Sina uhakika nayo Saana ila nahisi ni baada ya kutambua mumewe ana mtoto Nje ya Ndoa! Japo bado nazidi kulifuatilia!" Mr Jedi aliongea maneno ambayo yalimgusa kidogo Majaribu na alikumbuka hata maneno ya mchungaji kwamba kuna Dhambi aliifanya!!
"Heeeee inamaana yule Baba, mtoto ambaye alikuwa anamzungumzia ni mtoto wa Nje ya Ndoa!!!??" Kijana Majaribu akiwa kajisahau alijikuta anaropoka!.
"Unasemaje!? Marehemu alizungumzia kuhusu mtoto!? Ebu dogo eleza kila kitu alicho kwambia marehemu kabla hajafarika ili tujue tunatatua vipi hili tatizo!"
"Aaaaaa!! eeee!! Hapana bro hakuniambia kitu chochote! " Majaribu baada ya kugundua kazingua aliamua kupotezea, ila Mr Jedi aligundua kwamba kuna Siri lazima kijana Majaribu anazijua kuhusu marehemu na huwenda aliambiwa na marehemu kabla ya Kifo Mambo mengi tu.
"Okay sikiliza Kijana ngoja nikupe maelezo kifupi nilicho kibaini kuhusu marehemu, na Wewe utaniambia unacho kijua kumhusu ili Lengo letu la wewe kuwa Huru litimie, marehemu Nemeke na Mke Wake anaye fahamika Kwa Jina la Rehema walifunga Ndoa Miaka kama ishirini na kitu iliyo pita,
Kwa maelezo niliyo yapata wawili hao walidumu kwenye Ndoa Karibu Miaka nane pasina kupata mtoto, na walipotembelea hospital iligundulika mwanamke hana uwezo wa kubeba ujauzito, hapo ndipo uvumilivu ulimshinda mchungaji Nemeke aliamua kuchepuka na kwenda kuzaa Nje!.
Ila swala la yeye kuzaa njee inasadikika ilikuwa ni Siri kubwa Muno Ambayo ni baadhi ya watu wachache tu ndo walikuwa wanaijua, mchungaji Nemeke inasemekana alikuwa anatuma matumizi Kwa Siri Kwa Mtu ambaye alikuwa anamlea mtoto wake, na baadhi ya Miaka kumi na kitu kupita baadhi ya watu walianza kuijua Siri ambayo mchungaji alikuwa hataki ijulikane Kwa kuhofia Sifa Yake Kuvunjika!.
Ila Kwa Upelelezi kidogo nilio ufanya inasadikika Hivi punde Siku za hapa Karibuni Mke wake Rehema aligundua Siri ya Mumewe kuwa na mtoto nje, kitu ambacho Bado sijakipatia Jibu ni je Kwa Nini Mke wa mchungaji aliamua kumuua mumewe! Na je huyo Mtu ambaye anamlea mtoto wa mchungaji ni nani!? Kifupi ipo hivyo, Sasa Kijana kama kuna Siri unajua naomba nambie!" Mr Jedi Kwa Upelelezi wake ulio Shiba Ambao alikuwa kaufanya Kwa njia anazo jua yeye hayo ni machache ambayo alikuwa kayabaini.
Kijana Majaribu hapo kuna kitu alikibaini kichwani Mwake japo hakutaka kumshirikisha Mr Jedi, maana ni dhahiri kwamba Bado alikuwa hamuamini hata kidogo!.
Kwanza Majaribu alimwangalia Mr Jedi Kwa makini machoni pake, aligundua Bwana huyo kuna uongo kaongea kuhusu yale maelezo yake!
"Kwanza brother Kwa Nini wewe unataka kunisaidia!?" Majaribu aliuliza
"Majaribu Siku zote Mimi napenda Haki, sipendi Mtu anaye onewa?" Mr Jedi alijibu!,basi Majaribu aliitikisa kichwa kuonesha kakubali Japo alikuwa hajamuamini Kwa asilimia zote Mr Jedi.
"Bro kuna Mtu Mama Mtu mzima kidogo ni Katibu wa kanisa la marehemu, mtafute Yule au mfanyie upelelezi Nadhani utajua kitu kuhusu mtoto wa marehemu, maana mchungaji kabla hajafa alimtaja huyo Mama kwamba amtunze mtoto wake vyema!!" Kijana Majaribu alitoa maelezo ambayo yalifanya Mr Jedi apate Kazi nyingine ya kufanya!.
Mr Jedi alitoka pale Huku kazi inayo fuata ikiwa ni kumpeleleza Katibu wa kanisa na kujua kila kitu kumhusu!, Yaani Lengo la Mr Jedi alikuwa anataka kabla ya kukataa rufaa ya Kesi ya Kijana Majaribu basi awe na ushahidi ulio shiba!.
Upande wa Huku nyumbani Kwa marehemu mchungaji Nemeke, Binti Revina alikuwa Siyo mfanyakazi wa ndani tena, yaani baada ya Mke wa Mchungaji kugundua kwamba kuna Siri Revina anazijua kumhusu basi alimfanya Binti huyo mfalme pale ndani kila anacho kitaka alikuwa anapata, na alianza kumtuma kwenye baadhi ya mambo yake ya Siri, yaani kifupi tunasema Revina aligeuka chawa wa Mama Mchungaji.
Siku Hiyo pale nyumbani Kwa mchungaji kikao kizito kilikuwa kinaendelea, Mabishano makubwa yalikuwa yameshika kasi, ni kundi la Watu kama Saba Hivi walikuwa wamekaa wanabishana!.
"Rehema huo ni uzembe Siku zote Hizo unashindwaje kupata nyaraka zilipo, haya Sasa utajuaje Mali zote za Mchungaji ikiwa Mali nyingi alikuwa anaziweka Siri!? Au kuna Namna unataka kutuzunguka tusipate share!?"
"Siyo hivyo jamani nimejaribu kutafuta nyaraka hapa nyumbani sijaona, nyaraka zote ambazo nilikuwa najua ni nyaraka kumbe ni kopi tu! Yaani mpaka sielewi Nemeke alikuwa kaficha wapi Siri Zake!
"Uuuuu!! Haya tunafanyaje Sasa bila kuwa na nyaraka!?"
"Jamani Labda mpigieni Simu Melisa muulize maana inasadikika yeye ndo alikuwa Mtu wa Siri anaye jua mtoto wa Nemeke anako lelewa!?"
"Mrisho unaona Ninavyo sema tunafichana Siri!? Kumbe nyie mlikuwa mnajua kwamba Nemeke ana mtoto!? Na huyo Melisa ndo mpanga mipango, Sasa naomba Melisa aje hapa ajibie huyo mtoto yuko wapi maana huwenda huyo ndo alipewa nyaraka zote na Mume Wangu" Mama mchungaji aliongea Kwa jaziba.
"Rehema tuliza jaziba kila kitu kitakaa Sawa!"
"Siwezi kutulia! Mume Wangu alikuwa anataka aache Uchungaji kisa huyo mtoto unahisi angeshindwa kumuachia kila kitu kama alivyo niropokea!?" Mama mchungaji alikuwa anazidi kuuwasha Moto kwenye kikao kile, yaani mabishano yalikuwa makubwa, inaonekana Bado kuna Siri zilikuwa zipo Chini kwa Chini.
Je Siri Gani zipo Chini Kwa Chini!? Kwa nini Nemeke aliuawa!? Ipi hatima ya Kijana Majaribu!?? Mr Jedi Kwa nini anafuatilia Sana swala hili!?
Tukutane sehemu ya 5
Share hadithi hii Kwa watu wako
JibuFuta