Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Jumapili, 18 Mei 2025

Hadithi: A CROWN OF BADNESS EP 6-10


Mpya

TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 6.

Wakiwa wanaendelea na mazungumzo tayari kengele la kwenda kufanyiwa ukaguzi na kwenda kulala lilikuwa lishagongwa na Jacob hakupata muda wa kumuuliza swali lolote Mr jomo.

Basi siku hiyo Jacob alilala akiwa na maswali mengi mno kumhusu Mr jomo na kuyatafakari maneno ya Mr jomo kwa kweli siku hiyo usingizi hakupata kabisa mpaka kunakucha.

Huku uraiani Mr Derick kila siku kwake ilikuwa party alikuwa anaongeza tu idadi ya warembo anao miliki kitendo hicho kilifanya waanze kupishana na Mama Jacob maana alikuwa hafurahishwi kabisa na kitendo anachokifanya Mr Derick.
Siku moja katika pitapita zake Mr Derick alikutana na Fatuma na kama kawaida yake alitupia maneno yake huku yakiwa yameambatana na burungutu la pesa maana ndo ilikuwa mbinu aliyo tumia kuwanasa warembo wengi.
Fatuma baada ya kutongozwa na mzee wa pisi kali hakukata, alikubali ila alikuwa na plani zake maana alikuwa ashaichoka tabia ya Mr Derick.
Basi kama kawaida Mr Derick na Fatuma walienda pub na siku hiyo Fatuma alizuga tu kama hatumiagi kilevi chochote kumbe ni mtu wa tungi, wakati Mr Derick anaagiza vinywaji vikali Fatuma yeye aliaagiza soda.
Basi glass ziliendelea kutembea pale na mwishowe Mr Derick alikuwa yupo hoi kwa pombe na alikuwa hata haelewi kinachoendelea maana siku hiyo alikunywa pombe kuliko siku zote alizo wahi kunywa pombe na haijulikani why.
Basi baada ya kulewa kama kawaida walielekea chumbani na Fatuma, walipo fika chumbani tu Fatuma alimvua nguo zote Mr Derick na kuanza kumrekodi, bila kujua lolote mr Derick alikuwa anaongea maneno ya shombo na alikuwa anajishikashika sehemu zake za siri bila kujua anarekodiwa, basi Fatuma baada ya kuhakikisha amerekodi vizuri alimuacha mule ndani Mr Derick na kuondoka.

"Yaani huyu mpuuzi asipopunguza huu ushenzi wake kwa njia hii, kifuatacho ntatafuta wahuni wapasue mirinda alafu nimrekodi nione kama hataacha"hayo ni maneno aliyokuwa anajisemea Fatuma akiwa njiani kurudi kwake.
Na kitu kilicho kuwa kina muumiza Fatuma ilikuwa ni kuona mzazi wa mtu anaye mpenda toka moyoni anafanya vitu ambavyo hata jamii ilikuwa haivipendi.
Basi baada ya Siku hiyo kupita Mr Derick aliamuka asubuhi akiwa haelewi kipi kilitokea jana yake ila alicho kumbuka tu ni kwamba alienda na mtoto mzuri pale pub ila kilichotokea baada ya hapo ndo hakuelewa.
Basi jamaa aliamua kurudi nyumbani, ile anafika tuu alikutana na Mama Jacob kanuna ni hatari, alipojaribu kumsemesha Mama Derick hakujibu kitu bali alimupa simu ajionee mwenyewe, Mr Derick alipo iona ile video alitumbua macho akiwa haamini

"Dear hii video umeitoa wapi na nani amenirekodi??" Jamaa aliuliza kwa pupa akiwa anashangaa ile video ambayo sisi tunajua ni Fatuma ali rekodi kule pub.
"We malaya mkubwa wewe eti nani alirekod" Mama Jacob alibana pua moja kuonesha anachoongea bwana Derick ni upuuzi
"We mjinga usinibanie pua au unataka tuanze kutiana mateke asubuhi yote hii??" Bwana Derick hakufurahishwa na kile kitendo cha yeye kubaniwa pua
"Unifanyeje we mjinga? Sasa kama hii video hujaikuta mitandaoni thubutu, na nakwambiaje ukirudia huo umalaya wako hii video inaruka kwa mitandao hiyo ndo habari na aliyenitumia hii video ni binti msamalia mwema amenambia hivi wakikuona tena unachakarika na mabinti za watu huko njiani yajayo yanafurahisha siyo hii video kusambazwa tu bali kuna zito zaidi ya hili hiyo ni message sent Baba upo" hayo yalikuwa ni maneno ya Mama Jacob mwenda kwa Mr Derick na inavyoonekana ile video alitumiwa na Fatuma na yale maneno yalitoka kwa Fatuma.

Siku hiyo bwana Derick hakuwa na ujanja alibaki mdgo kama piliton maana aliogopa kwa umaarufu alio kuwa nao kwa kipindi hicho video ile kusambaa ingekuwa aibu kwake.

Huku gerezani, maisha yaliendelea na zilikuwa zimepita Siku tatu Jacob akiwa bado hajapata muda wa kuzungumza na Mr jomo tena ili angalau ampeleleze mawili matatu.
Siku zilisogea wakiwa hawajapata muda wa kukaa kupiga story maana kila siku ilikuwa ni kaazi baada ya kazi, baasi ilifika jumapili nyingine ambayo ndo ilikuwa siku ya wafungwa wote kurelax na kufanya usafi na siku hiyo ndo Jacob aliisubiri sana kwa hamu kama mtu anayesubiri msichana ambaye ndo wameahidiana kukutana naye kwa mara ya kwanza.

Basi Jumapili hiyo Jacob alimfuata Mr jomo na kuomba wazungumze na bwana jomo alikuwa anajua kitu gani Jacob anataka wazungumzie
"Bana eeeee ni Saiz nataka nifanye mpango nitafute sabuni nifue nguo" mr jomo alijifanya anadeka maana alijua dogo ana kimuhe muhe cha kuongea Naye kweli.
"Bro we usijali sabuni ninayo ntakupa na kama ni kufua ntakufulia" Jacob alijipendekeza ili tuu walau amuhoji bwana jomo yake maneno aliyoyasema siku ile.

Basi bwana jomo baada ya kusikia kwamba sabuni atapewa na atafuliwa nguo aliona hayo ndo mambo sasa walienda kutulia sehemu na kuanza kupiga story.

"Bro jomo mi sitaki kuzunguka naomba uniambie kila kitu unachojua kama ulivyo nidokezea siku ile??" Jacob alienda direct

"Jacob bana eti kila kitu, mi hapa nilipo najua vitu zaidi ya milioni sasa ukisema kila kitu si ntakusimilia wiki nzima, we nenda kwenye swali specific" Jomo alikuwa bado anajimwambafai kwamba yeye anajua mengi

"Basi bro ebu nambie aliye muua Mr Deus ni na nini??" Sasa hapo Jacob ilibidi awe specific

"Aliuemuua Mr Deus ni Mr Derick Na Mrs Deus" naye mr jomo hakupindisha inaonekana aliamua kuyumbisha antena ya Mr Derick na Mama Jacob.

Je nini kitatokea?? Je Jacob atachukuliaje taarifa ambazo amepewa na Mr Jomo??

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 7




TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 7.

"Aliuemuua Mr Deus ni Mr Derick Na Mrs Deus" naye mr jomo hakupindisha inaonekana aliamua kuyumbisha antena ya Mr Derick na Mama Jacob.

"Whaaaaaat!!! Unasemaje we fala!!!" Jacob aliinuka na kumkunja Mr jomo maana yale aliyoyasikia haikumwingia akilini hata kidogo

"Kama huamini niachie niondoke maana naona wewe upo kama wale wazee wazamani waliokuwa wanaamini mzungu ndo kila kitu" Mr jomo alizidi kumchanganya Jacob na maneno yake

"Bro ivi nilicho sikia ni unamaanisha au ulitaka tu unitest kwamba nita react vipi??" Bado Jacob alikuwa haamini eti kusikia Mama yake na baba yake mkubwa Mr derick ndo wamehusika na kifo cha baba yake

"Jacob tatizo lako we umekaa kifara fara, yaani nchi yetu ina watu Zaid ya milioni 50 umeona mi ni kichaa kuwachagua hao watu wawili??" Jomo aliongea kwa ukali na ilioneka ni mtu aliyekuwa serious na kile anacho kiongea

"Ebu nieleze kwa nini wafanye hivyo kwa mzee wangu sasa??" 
Jacob bado ilikuwa haimwingii akilini maana alikuwa akikumbuka ule upendo wa mama yake japo alikuwa ni mama yake wa kambo ulikuwa ni upendo mkubwa mno.
"Jacob tatizo lako mawazo yako yapo enzi za ujimaa, we nielewe sina haja ya kumsingizia mtu, na mimi unaniona hapa gerezani ni kwa ajili ya hicho kifo cha huyo mzee wako" Jomo alizidi kushindilia mambo juu ya mambo

"Eeeeee!! Mbona unanichanganya bro ebu elezea kifupi maana hapa sielewi nishike lipi" Jacob alikuwa dillemma
"Nisikilize kwa makini, Mimi na rafiki yangu ambaye kwa sasa ni marehemu tulipewa Kazi ya kumuua baba yako na mr Derick akishirikiana na mama yako na kuna kiasi cha pesa ambacho tulikubaliana kwamba baada ya Kazi tutalipwa tulipewa nusu ikabaki nusu, kweli kama ilivyo kuwa kauli mbiu yetu mimi na rafiki yangu kwamba 'Kazi hailali' na kweli siku hiyo alikuja kutuchukua Mr Derick mchana kwamba tukafanye tukio na tukishafanya kesi upewe wewe na tulipohoji kwamba mbona ni mchana hatuwezi kushitukiwa alisema kila kitu kakiweka sawa na alisema alimupanga demu fulani hivi ambaye wewe ulikuwa unatoka naye akuzugezuge huko chuoni ili uchelewe kurudi ukute kila kitu tayari, na kweli siku hiyo tulienda watu watatu tukiwa mimi na rafiki yangu pamoja na Mr Derick mwenyewe na tulipo fika pale tulikuta mzee anajianda kutoka na kweli tulifanya kilichotupeleka pale na baada ya kumaliza kazi tulichukua simu ya mzee na kuwaandikia sms polisi ndo kilicho fanya wewe ukakamatwa, sasa baada ya kazi hiyo Derick alianza kutuyumbisha pesa zetu, jamaa alipo ona tushaanza kumzonga ndo aliamua kumuua rafiki yangu na kesi nimebebeshwa mimi Ndo maana waniona hapa" Mr jomo alisimulia bila hata kuogopa.

Ila Mr jomo alipo maliza kusimulia alimuona Jacob anatetemeka mwili mzima na baada ya dakika moja Jacob alidondoka Chini na kuzimia maana mambo aliyokuwa ameambiwa yaliuzidi moyo uzito.

Basi waliitwa maaskari gereza, na kumchukua Jacob kumkimbiza hospitali kupata huduma maana alikuwa ashaanza kupoa kama mtu ambaye yupo karibu na Israel mtoa roha.
Mr jomo wala hata hakujali kwamba baada ya kumusimulia yale Jacob yeye atamchuliaje maana yeye aliamini kwamba alikuwa kazini na ile ilikuwa ni kazi kama zilivyo Kazi nyingine (Ama kweli duniani kuna watu na viatu).

Basi matibabu yaliendelea kufanyika kwa Jacob na hali yake ilikuwa siyo nzuri, ilionekana mapigo ya moyo yanaenda kwa speed ndogo sana na ilikuwa ili azinduke lazima waya boost mapigo ya moyo, ilibidi Jacob ahamishwe hospitali na bahati nzuri hospitali aliyo pelekwa Jacob ndo hospital aliyo kuwa anafanyia field Fatuma maana yeye alikuwa anasomea udaktari.

Basi matibabu yakiendelea kwa Jacob akiwa chini ya ulinzi, na Fatuma alikuwa karibu sana kumhudumia Jacob, na baada ya wiki moja Jacob alizinduka na bado Fatuma alionekana sana kumjali Jacob mpaka maaskari walio pewa kazi ya kumlinda Jacob walianza kushitukia ukaribu kwamba hawa watu wana ajenda za siri, sana sana wao walifikiria kwamba wanapanga mbinu ya kutoroka.
Jacob baada ya kukumbuka kila kitu alicho simuliwa na Mr jomo naye aliamua kumsimulia Fatuma japo alimwambia iwe siri yake.

" Jacob nakuhakikishia siwezi mwambia mtu na mimi hicho kitu nilikuwa nakitilia sana mashaka kuhusu mienendo ya hao watu sema siku ile nimekuja kukuona kule gerezani niliogopa kukuambia" baada ya Fatuma kusimuliwa kila kitu naye alifunguka.
Basi Jacob na fatuma walipanga mipango mingi mno ambayo haikueleweka ni mipango gani na wakiwa wanaendelea kumalizia mazungumzo yao mara aliingia askari
"We Doctor samahani kwa kukuingilia kazi, mbona tunaona mazungumzo yamekuwa mengi mno na mtu wetu wakati ulisema unaingia tu kumuulizia hali yake kwamba anajisikiaje, vip imekuwaje tena??" Askari alitilia mashaka maana aliona ni zaidi ya nusu saa bado Doctor fatuma amekaa tu kwenye chumba cha mgonjwa.

Basi maneno hayo yalimfanya Fatuma atoke mule chumbani na askari waliamua kumchukua mtu wao bila hata kuruhusiwa na Doctor maana waliona yanaweza kutokea ya kutokea alafu vibarua vyao vikaota nyasi na wakaenda kunyea deba.

Je nini kitatokea?? Ni mpango gani Fatuma na Jacob wamepanga na je utafanikiwa??

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 8




TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 8.

Basi maneno hayo yalimfanya Fatuma atoke mule chumbani na askari waliamua kumchukua mtu wao bila hata kuruhusiwa na Doctor maana waliona yanaweza kutokea ya kutokea alafu vibarua vyao vikaota nyasi na wakaenda kunyea deba.

Basi Jacob alirudishwa magerezani na alikuwa angalau hali yake imerudirudi japo siyo kivile, ile anafika tu mtu wa kwanza kumpokea alikuwa ni Mr jomo kweli watu wamepinda yaani mtu umemusimulia kwamba umeua baba yake alafu tena unamfuata fuata.

"Oya mwanangu Jacob daaa!! Nilikuwa na hofu sana kichaa wangu bora umepona yaani" baada ya Jacob kuingia tu, Mr jomo alianza kujipendekeza na kujikeshachekesha.

"Kwa hiyo ndo umenuna ama?, Oya fanya basi mpango unipe hiyo sabuni yangu si unajua siku ile hukunipa eee??" Kweli kuna watu vichaaa yaani Mr jomo kujipendekeza kote huko kumbe alikuwa anataka akumbushe sabuni yake.

"Bro we kausha mi sipo poa kabisa, alafu sina mudi na wewe wala nini na hiyo sabuni sikupi, maana ulicho nisimulia hakiendani na kupewa sabuni" Jacob naye hakuogopa alijibu jeuri

"We si fala kama mafala wengine tu unafkri nina shida sana na sabuni!!?" Jomo naye hakujali maneno ya Jacob
"Basi kama huna shida vunga" 
"Ila mwanangu eeee!! Vip sasa kwa nilivyo kusimulia yule mzee tunadili naye vipi maana nina hasira naye au ndo hukuniamini ninacho ongea??"
"Bro si nimekwambia niteme kwani we unatakaje??" Jacob aling'aka baada ya kuona bado Mr jomo amemuganda

"Oya dgo acha upimbi mtu hawezi kuwa anatumbua maisha huko uraiani na mali zako alafu we unasotea huku wakati yeye ndo alifaa kuwa huku hiyo haiwezi kuwa kweli kamanda wangu, yaani yule fala ale bata sisi tuwe tunakula msoto hata sikubali" Mr jomo aliongea kwa uchungu maneno ambayo hata Jacob yalimwingia na hapo akili ndo ilifunguka kwamba kumbe wale wapuuzi wamemuua baba yake kisa mali.

"Kwa hiyo brother Jomo we hapo unatakaje??" Jacob aliuliza kwa upole baada ya kugundua Mr jomo anaongea pointi

"Dgo mi nakwambiaje hapa lazima tutoroke, hata kama mimi sitafanikiwa lakini kwa jasho na damu lazima wewe utoroke ukapambanie haki yako, mi hata nikifa au nikibaki huku ni sawa maana kwa mengi mabaya niliyofanya nastahili kuwa huku ama kufa kabisa ila kijana mtiifu kama wewe inaniuma kukuona upo huku kwa makosa ambayo siyo yako, hiyo kamanda wangu iweke kichwani lazima tutoroke ama nikutoroshe wewe na kesi ntabeba Mimi" Mr Jomo aliongea kwa machungu mpaka machozi yalimtoka na ilionekana anajutia kile alichokuwa anakifanya nyuma na kilicho kuwa kinamtoa machozi ni kumuona kijana mdogo mwenye ndoto nyingi za maisha anaharibu maisha yake kwa kosa la mwingine.

Basi siku hiyo waliongea mengi na tayari kengele ya kwenda kwenye ukaguzi ilikuwa ishalia.

Huku uraiani harakati ziliendelea kama Kawaida na mzee wa pisi kali, Mr Derick baada ya kupigwa zile picha za utupu alipunguza speed kidogo, ila baada ya miezi miwili alirudia tabia yake tena kwa kasi kubwa yaani alikuwa kama anafidia.

Baada ya kurudia ile tabia yake basi Fatuma hakutaka masihara alizisambaza picha za Mr Derick kwenye mtandao, picha hizo zili trend kwenye mtandao mwezi mmoja tu zikapotea na ilionekana Mr Derick hazikumshitua sana maana tabia yake ya kutembea na mabinti ovyo ovyo aliizidisha mara mbili na pesa ndo zilikuwa zinampa kiburi.
Fatuma baada ya kuona ile mbinu haijasaidia chochote aliamua kuja na mbinu nyingine kabambe ila tatizo kubwa kwake lilikuwa ni uchumi maana fatuma alikuwa anatokea kwenye familia ya kimasikini na chuo alikuwa anasomeshwa na mkopo wa serikali tu.

Basi siku moja kama ilivyo kawaida ya Fatuma kumtembelea Jacob gerezani, siku hiyo alienda kumtembelea Jacob gerezani na alienda kwa ajili ya mazungumzo maalum, ila anapoingia mlangoni alikutana uso kwa uso na Mr Derick akiwa anatoka mule gerezani kwa mawazo ya Fatuma alijua labda katoka kumuona Jacob, Fatuma hilo hakuzingatia sana aliingia kumuona Jacob na aliruhusiwa kuongea naye na siku hiyo waliongea mengi mno na Fatuma alimisimulia kila kitu kuhusu tabia za Mr Derick mtaani na jinsi anavyo tapanya mali na alimusimulia zile plani alizojaribu kuzitumia ila hazijafanya kazi na plani zingine kafeli kwa ajili ya uchumi wake.

Kitu kilicho mshangaza sana Fatuma na kumfanya afikirie baada ya kutoka pale gerezani ni baada ya Jacob kusema kwamba ni zaidi ya miezi sita Mr Derick hajajapo kumuona gerezani wakati yeye amekutana naye mlangoni na Mr Derick akitokea ndani ya gereza.

Je nini kitatokea?? Je Mr Derick alienda kumuona nani gerezani na je mpango wa Mr Jomo utafanikiwa??

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 9




TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 9.

Kitu kilicho mshangaza sana Fatuma na kumfanya afikirie baada ya kutoka pale gerezani ni baada ya Jacob kusema kwamba ni zaidi ya miezi sita Mr Derick hajajapo kumuona gerezani wakati yeye amekutana naye mlangoni na Mr Derick akitokea ndani ya gereza.

Basi Fatuma alilipotezea hilo swala na kuondoka zake kurudi nyumbani.
Huku nyumbani kwa Mr Derick alionekana anapanga mipango mizito na mke wake na walionekana ni watu wanaopishana kauli

"Mr Derick bwana uwe na huruma hata kidogo, mtoto tumembebesha kesi nzito namna ile bado unata vya kutaka nini lakini??" Mama Jacob alionekana kulalamikia maamuzi ya mr Derick

"Nyie wanawake huruma yenu inawaponza na siku zote ukicheka na nyani utavuna mabua, ivi we unafikiri kwa mfano akitoka kule na akajua hiki tulicho mfanyia we unafikiri itakuwaje au unawaza tu leo huwazi kesho??" Mr Derick aliona mawazo yake ndo ya maana kabisa

"Hata kama dear, yule si kafungwa miaka 30 ivi unafkri kutoka ni leo" Mama Jacob bado aliona kile anachotaka kufanya Mr Derick ni kujiongezea uwingi wa mazambi huko mbinguni.

"Unaona sasa mawazo yenu wanawake yalivyo finyu, yaani ndo maana mlidanywa na nyoka enzi hizo kula tunda mkafanya hadi maisha yawe mafupi duniani wakati muda huu tungekuwa tunaponda raha milele, eti miaka 30, kwa hiyo unafkri wote huwa wanamaliza hiyo miaka?? Huoni kama kuna kutoroka?? Huoni kama kuna kusamehewa? Je kwa mfano akasamehewa leo anatoka unafkri itakuwaje?? Au unawaza tu ndani ya box?? Acha uvivu wa kufikiria we mwanamke" Mr Derick Aliongea kama anapiga kampeni mpaka Mama Jacob alianza kujicheka mwenyewe kwamba alikuwa hajatumia akili kufikiria.

Basi walikubaliana kufanya jambo na walipanga mipango yote kama inavyotakiwa na haikujulikana ni mipango ipi ila kwa walivyoonekana tu ilionekana ni mipango juu ya Jacob.

Huku gerezani Mr jomo walikuwa wanapanga mbinu gani watatumia kutoroka gerezani, ila walikuwa hawaioni maana gereza hilo lilikuwa linalindwa ni hatari na kila kona ya gereza zilitegeshwa camera kwa ajili ya usalama zaidi hiyo ilitokana na utukutu wa wafungwa waliopo kwenye gereza hilo.
"Jacob hapa inabidi tufanye mpango tuhonge maaskari ikiwezekana maana sioni njia nyingine" hilo lilikuwa wazo la Mr jomo siku hiyo wakiwa wamekaa wawili wanajadili mipango

"Bro na wewe uwe unafkri vizuri bana we unahonga nini wakati unaona wote tupo humu ndani au wewe una connection huko nje??" Jacob alishanga lile wazo la Mr jomo la kuhonga

"Siyo kwamba nina connection, pesa ninazo za kutosha ila tatizo nani ataenda kuzichukua ndo tatizo, maana nyumbani kwangu nilikuwa naishi pekee angu na sina ndugu labda kwamba wanaweza kwenda kukagua nina uhakika pesa zipo salama" Mr jomo aliongea maana alikuwa ashakumbuka kwamba nyumbani kwake alikuwa na akiba ya pesa kabla hajakamatwa.

Basi siku hiyo walikubaliana kwamba watamutumia Fatuma akija na maelekezo yote atapewa na waliahidiana kwamba yeye ndo ataongea na Mkuu wa magereza ili waone ni jinsi gani wanaweza kufanya.
Basi kweli kama mipango ilivyo pangwa baada ya Fatuma kuja kumuona Jacob, alienda Mr jomo badala ya Jacob na fatuma alishangaa kwa nini imekuwa hivyo ila Mr jomo alimwelekeza kila kitu Fatuma kuhusu zile pesa na ile nyumba yake na wapi atapata ufunguo, yaani alimupa maelezo yaliyo nyooka Fatuma.

Basi siku hiyo ilipita na ilikuwa ni siku nyingine mpya kabisa, ila siku hiyo Jacob alishangaa kutokumuona Mr jomo maana haikuwa kawaida, kwa sababu ilikuwa kila asubuhi lazima mr jomo apite kukagua wafungwa wote kama wapo kabla ya askari kupita maana yeye ndo alikuwa nyampara mkuu.
Basi masaa yalizidi kusogea bado Jacob hakumuona bwana jomo, na hatimaye ilifika siku nyingine bado rafiki yake alikuwa haonekani, zilipita siku mbili Mr jomo alikuwa haonekani.

"Kwa hiyo huyu mjinga ndo kaamua kutoroka pekee yake wakati tuliahidiana mambo matamu tu au ndo alikuwa ana ni enjoy tu?" hayo yalikuwa mawazo ya Jacob kumhusu bwana jomo, ila akiwa amekaa anawaza mara alianza kusikia minong'ono na tetesi za wafungwa wenzake kwamba bwana jomo kafa.
Hizo habari zilimshitua mno, ila jinsi muda ulivyokuwa unazidi kusonga ndo taarifa za kifo cha bwana jomo zilikuwa zinaenea, na Jacob alikuja kuthibitisha kwamba kweli, mwamba wake bwana Jomo kafa baada ya kauli ya askari magereza mmoja siku hiyo

"Sasa nyie jifanyeni wababe, kuna mwenzenu humu alijifanya mbabe wa gereza leo ni marehemu sasa nyie leteni domodomo na kujifanya mmepinda mtanyooka tu" hayo yalikuwa ni maneno ya kuropoka ya askari mmoja baada ya kuja kuamulia ugomvi ambao kuna wafungwa walikuwa wanataka kuzichapa, hapo ndo Jacob alijua rafiki yake kwisha habari.

Hapo wasiwasi ulizidi kumjaa Jacob maana yule aliye kuwa anamtia moyo wakiwa gerezani ndo huyo kachukuliiwa na Israel mtoa roho na ndo huyo huyo alikuwa anmlinda zidi ya uonevu humo ndani.
Kweli kutesa kwa zamu, baada ya wahuni mule ndani kusikia kwamba Mr jomo kafa walianza kumutesa Jacob yaani kama ndo walikuwa wanamuonesha kwamba sasa utaona, yaani alikuwa anaonewa kwa kila kitu ukichukulia na upole wa Jacob.

Huku uraiani kwa Mr Derick alionekana akiwa na Vicky pamoja na Mama Jacob kwenye pub wanakula raha kana kwamba ni watu waliofanikiwa jambo fulani.
"Sasa na wewe Mama Jacob kwa kazi anayofanya Vicky si uniruhusu tu awe mke mdogo jamani, We unafikiri yule mjinga kufa ni masihara?" Mr Derick akiwa anapiga glass ya pombe alilopoka kwa mke wake

"Aaaa!! we mke mdogo mara ya ngapi? We unafikiri sijui kwamba ni mtu wako? Si ushampa hadi nyumba ya kule juu unafikiri sijui ama??" Mama Jacob aliongea

"Sasa mke wangu si ndo nataka iwe lasmi" Mr Derick pombe ilikuwa ishaanza kusoma kichwani
"Mi sina neno cha msingi Vicky uwe na heshima sawa eee na kazi kama hizi tutakuwa tunasaidiana" Mama Jacob alikubali Vicky kuwa mke mwenza

"Alafu Vicky umetumia njia gani mpaka bwana jomo kafa kizembe vile??" Mr Derick aliuliza, hapa ndo tunajua kwamba kumbe kifo cha Mr jomo hawa ndo wahusika na walikuwa wapo hapo pub kwa ajili ya kupongezana

Basi Vicky aliwasimuliwa njia aliyo tumia, hapo walimpongeza, na walikubaliana kwamba amebakia mmoja ili kazi yao iwe imemalizika.

Basi baada ya kumaliza maongezi hao watu walianza kuondoka maeneo hayo, ila baada ya kuondoka tu Fatuma naye aliingia mule ndani na alinyoosha moja kwa moja kwa muhudumu wa ile pub, ilionekana anapewa kifaa fulani kama sound recorder na baada ya kupewa kile kifaa, Fatuma alitoa pesa kama elfu 50 na kumpa yule mhudumu kisha akaondoka.

Je nini kitatokea?? Fatuma ana mipango gani??

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 10.



TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 10.

Basi baada ya kumaliza maongezi hao watu walianza kuondoka maeneo hayo, ila baada ya kuondoka tu Fatuma naye aliingia mule ndani na alinyoosha moja kwa moja kwa muhudumu wa ile pub, ilionekana anapewa kifaa fulani kama sound recorder na baada ya kupewa kile kifaa, Fatuma alitoa pesa kama elfu 50 na kumpa yule mhudumu kisha akaondoka.

Fatuma alienda kujifungia magettoni kwake aliko panga na kuanza kusikiliza kile kilicho rekodiwa na mhudumu wa kule pub.
Baada ya kusikiliza mwanzo mpaka mwisho hapo ndo alikumbuka Siku wamepishana na mr Derick kule gerezani, na alishangaa sana maongezi ya wale watu wakimanisha kwamba bwana jomo kafa na Fatuma ndo alikuwa anazijua hizo habari na Fatuma aliiona hatari iliyo mbele ya Jacob.

Kitu alichokifanya alienda nyumbani kule aliko elekezwa na Mr jomo, kweli alifika maeneo hayo alikuta ile nyumba imechafuka na majani yameanza kuota njiani maana ilionekana hakuna mtu anaye kaa maeneo hayo.
Kama alivyo elekezwa, alifanya vile vile na kweli aliingia mpaka kwenye chumba cha siri cha mr jomo na kwenye chumba hicho Fatuma alikuta kuna siraha za kila aina yaani bunduki zilikuwepo, visu vya kutosha, mapanga na mikuki ndo usiseme, basi Fatuma alifungua begi alilo elekezwa alikutana na maburungutu ya fedha yamefungwa.
Fatuma ilikuwa inamuuma kuchukua hizo pesa kwa sababu alijua zimetokana na uharifu ila ndo alikuwa hana namna maana yeye alikuwa hana pesa za kumsaidia Jacob.

Baada ya Fatuma kuchukua zile pesa hakutaka kuchelewa alienda moja kwa moja kwa Mkuu wa gereza na kumwelezea shida yake na alitaja kiwango cha pesa atakacho toa.
"Binti sasa hapa nimepata akili na nahisi ungechelewa kidgo tu huyu mtu wako angekufa maana kuna watu tayari wameongea na ngazi za juu zaidi na Mimi nimeletewa maelezo kwamba huyu mtu kufika kesho awe amekufa, sasa hapa cha kufanya njooo tutumie hiyo fursa kwa huyo mtu wako kutoroka na hii itasaidia kwa sababu itaaminika amefariki na kwenye mafaili ya magereza jina lake litafutwa kwa hiyo hatatafutwa tena, kwa hiyo kazi yako itafanyika" mkuu wa magereza alimweleza kila kitu Fatuma na walikubaliana kila kitu na walipanga jinsi mpango utakavyo endeshwa.

Basi huku uraiani kwa upande wa Mr Derick walipokea taarifa kwamba tayari Jacob kafariki na kwa kuwa wao ndo walikuwa ni ndugu wa pekee ilitakiwa wakauchukue mwili wa marehemu baada ya kuthibitisha kwamba ni kweli kafa.
Kweli kama ilivyo ada Mr Derick akiwa na mama Jacob walienda gerezani kuchukua mwili wa Jacob na walipo angalia walithibitisha kwamba yule ni Jacob kweli hapo mioyoni mwao walikuwa wanasherekea maana tayari vikwazo vyote walikuwa washaviondosha.

Basi akina mr Derick walituma watu wakanunue jeneza na waliwapa maelekezo yote mpaka sehemu ya kwenda kuzika, hao vijana kweli walikuja na jeneza na walikabizi maaskari ili waingie ndani wautie mwili kwenye jeneza, basi maaskari walipoingia ndani walibadilisha maiti yaani kwenye jeneza waliweka maiti ya mtu mwingine alafu Jacob wakamtia kwenye box kubwa.
Basi wale vijana walikabidhiwa jeneza lenye maiti ambayo wao waliamini ni Jacob, baada ya akina mr Derick kushuhudia kila kitu na kuhakikisha wale vijana waliopewa kazi ya kwenda kuzika wamebeba jeneza basi wao waliondoka na kurudi nyumbani kwenda kula bata maana kazi ilikuwa Isha Isha kwa upande wao.
Jioni na kigiza kwenye nyumba ambayo alikuwa anaishi Mr jomo kabla hajakamatwa na kufa, alionekana Fatuma amebeba box kubwa na ilionekana ni box zito maana alikuwa anatembea kama mtu ambaye anataka kuanguka.

Baada ya kuingia ndani alifunga milango na kulifungua lile box, alikuwa ni Jacob ambaye ndo aliwekwa kwenye lile box na alionekana amezimia muda mrefu, basi baada ya Fatuma kumtoa mule kwenye box alichukua dawa fulani ya maji na kumpitisha Jacob puani, baada ya ile dawa kupita puani tu, Jacob alianza kupiga chafya mara mbili mbili tayari alikuwa ashazinduka.

Basi usiku huo Fatuma aliutumia kumhudumia Jacob mpaka Jacob alianza kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

"Daaaaa Fatuma ubarikiwe mi siamini kama nipo uraiani na nipo huru"
"Jacob kwa sasa bado hauko huru maana ukijichanganya alafu baba yako akajua bado haujafa anakulima chuma, kwa hiyo inatakiwa uwe makini kuliko kawaida"
"Fatuma mpaka hapa nilipo nakushukuru sana ila huko kwingine niachie mimi ntamalizia"
Hayo yalikuwa ni baadhi ya maongezi ya Fatuma na Jacob kulipo kucha asubuhi, na waliahidiana kwamba watasaidiana kila hatua.

Huku kwa mr Derick baada ya kuwa na uhakika kwamba tayari Jacob ashafariki alianza kufanya mpango wa mali zote kuzibadilisha majina na kuandika jina lake maana mali zote za mzee Deus ambaye ndo alikuwa baba yake na Jacob zilikuwa zimeandikwa kwa jina la Jacob.

Huku upande wa pili Jacob naye alikuwa anajipanga na anaanda mbinu mbalimbali namna ya kuzirudisha mali zake mikononi mwake tena.

Je nini kitatokea?? Mr Derick amepanga kubadili jina la mmiliki wa mali, pia Jacob naye anataka kurudisha mali zake je nani atafanikiwa??

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 11

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu