Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Jumatatu, 19 Mei 2025

Hadithi: UKIMALIZA FUNIKA EP 53-55



Mpya.

UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA HAMSINI NA TATU
MTUNZI @MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA MBILI: Naam walingea mawili matatu, kisha kisha wakaagana na shangazi akaenda chumbani kwake, huku akimwacha Salma anatafuta usingizi, huku anasubiri siku ya kesho, akakutane na mpenzi wake, ambae aliamini kuwa amembebea zawadi nyingi sana toka japan, kama ilivyo kawaida yake anapo kuwa ametoka safari kama hizo. …….endelea….

Wakati huo nyumba ya tatu toka pale, kijana Masoud, alikuwa chumbani kwake, akitafakari, juu ya ujio wa Sebastian ambao umehasiri penzi lake, “ni ujinga huu, yani huyu boya tu anamzingua Salma, mpaka leo amegoma kuja huku”alijisemea Masoud, akimlaumu Sebastain Kiguru, kwa kumzuzua Salma, ambae siyo tu anamfahamu kuwa ni mchumba wa Sebastian, pia anafahamu kuwa, ata fedha anazo tumia kula kuvaa, ata kulipiwa kodi ya nyumba anaishi, pombe anazokunywa, gari analotembelea kila siku kwendakazini zinatokana na fedha ya mwanaume huyo, anae mwibia mwanamke wake.

Licha ya kuwaza hayo, lakini pia aliwaza juu ya Ana, ambae alitegemea kumwona akiwa amechakaa na kulala kwenye viambaza vya maduka ya watu, kutokana na kukosa sehemu ya kulala fedha ya kula au nauri ya kurudia Mafinga, baada yake anapewa hongera ya kutoa million moja na laki tano, kwaajili ya matibabu ya mzee Sinyangwe, “kwani mimi chizi mpaka ni toe fedha yote hiyo, mi mwenyewe nina elfu kumi tu” alijisemea Masoud, ambae aliamini kuwa wanafamilia wale fukara, wamejipatia fedha kwa kuuza mamshamba yao, na iwe isiwe lazima watamtumia Ana fedha ya ili aweze kurudi kijijini.

Licha ya kuwaza hayo yote, lakini Masoud akuwaza juu ya fedha ambayo aliahidi kumtumia baba yake, ambae aliitaji kutengeneza trekta lake, ambalo mo muhimu sana kwake, kitu ambacho kina mfanya ajitape kwa kuonekana mwenye fedha kulikowote pale kijijini.******

Naam saa kumi na moja na nusu, alfajili, ya siku ya pili, Sebastian aliamka mapema sana, hii nikutokana na kukosa usinngizi, maana licha ya kuchelewa kulala akinywa wine yake, huku kichwani mwake akiwaza ili na lile juu yakile alichofanyiwa na Salma, mwana mke ambae siyo tu kuweka imani yake kwake, ila pia alimfanyia kila kitu, kumpatia adhi ya kuwa mwanamke wa maisha ya juu, lakini mwisho wake mwanamke huyo huyo ana amua kupenda mwanaaume mwingine, na kutoa huduma kwa fedha yake mwenyewe, fedha ambayo aliitafuta kwa jasho lake mwenyewe, na kilicho muuma zaidi ni aina ya ngono waliyokuwa wanaifanya, “kumbe yule shangazi anajifanya kuwa Salma awezi kutoka nje ya nyumba zaidi ya saa mbili, kumbe Salma aanatoka kwenda kuzurula, alafu analala kwa mwanaume, shangazi mwenyewe ni mlevi” Sebastia analala saa nane usiku, na kushtuliwa saa kumi na moja, kwa maongezi ya mlinzi na Anna huko nje.

Sebastian anasogelea dirisha, anatazama nje upande wa chini, ambako anamwona Anna akiwa amevalia zile ngupo zake za jana, anaongea na mlinzi, “dada huu siyo muda wa kufanya usafi, isitoshe bado atujaambiwa kama wewe ni mfanyakazi hapa” alisikika yule yule mlinzi, “Anna unafanyanini huko nje, mapema namna hii?” aliuliza Sebastian ambae, tayari alikuwa amesha juwa kilichomtoa nje Ariana, mida ile, “nataka kusaidia kazi, lakini huyu kaka ananikataza” alisema Anna, kwa sauti ya upole lakini yenye kusemelea, “hapana ingia ndani, upumzike, umechoka na safari” alisema Sebastian, kisha aka fuunga panzia na kupotelea ndani, “nani kakuambia umekuja kufanyakazi hapa” alijisemea Sebastian, huku ana jilaza tena kitandani, baada ya kuona kuwa, kichwa chake bado kizito kwa usingizi.*******

Asubuhi, ya saa moja na robo asubuhi, kijijini Malangari, tayari taarifa za kufanikisha kwa matibabu ya mzee Sinyangwe, zilisha tapakaa kijiji kizma, huku sifa zikienda kwa Sebastian kuwa ndie alie tuma fedha hizo.

Mida hii mzee Kizinge alikuwa anapiga mswaki, pale kwenye matembele, “hivi umesikia hiyo arufu hapo jiko la ndani?” aliuliza mzee Kizinge kama kawaida yake, povu la mswaki likimtoka hovyo mdomoni, “yani baba Masu unazidi kunichanganya tu, achana na hiyo harufu ya vyombo, ume maliza ela yote jana kutengenezea trekta lako, ukasema Masoud atakutumia ela lakini mpaka sasa hivi bado, ndani akuuna cha sukari wala majani ya chai, hiyo mchana ni majani ya maboga tu, atuwezi kununua ata dagaaa”alisema mama Masoud kwa sauti ya manung’uniko, “wala usiwe na wasi wasi, nazani jana alikosa muda, ila leo atatuma mapema tu” alisema mze Kizinge, kwa sauti ya kujiamini.

“hivi ujawaona wadogo zake Anna, huko mtaani, waje wanionshee vyombo?” aliuliza mama Masoud, alikekuwa ameshika sufuria chafu lenye mwiko mchafu, “mh! watakubari sasa?” aliuliza mzee Kizinge, akimalizia kwa kutema povu la dawa za mswaki, kwanini wasikubari, kwani wao shida yao sidada yao aolewe na tajiri” alisema mama Soud, na kumfanya mume wake acheke kwanguvu na kupaliwa na povu la mswaki, na kuanzako kukooa kwa fujo. …….endelea…. 

UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA HAMSINI NA NNE
MTUNZI @MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA TATU: “hivi ujawaona wadogo zake Anna, huko mtaani, waje wanionshee vyombo?” aliuliza mama Masoud, alikekuwa ameshika sufuria chafu lenye mwiko mchafu, “mh! watakubari sasa?” aliuliza mzee Kizinge, akimalizia kwa kutema povu la dawa za mswaki, kwanini wasikubari, kwani wao shida yao sidada yao aolewe na tajiri” alisema mama Soud, na kumfanya mume wake acheke kwanguvu na kupaliwa na povu la mswaki, na kuanzako kukooa kwa fujo. …….endelea….

Kikoozi kiliendelea ata alipofika mzee Mwagoda Kagari, ambae alisubiri mpaka mzee Kizinge alipomaliza kukooa, kisha aka msalimia, “habari bwana Kizinge” hapo Kizinge bila kunawa wala kuondoa povu mdomoni, akamgeukia bwana Kagari, “hoooo bwana Kagari, karibu bwana” alisema Kizinge, akionyesha furaha kubwa sana, maana ukweli ni kwamba huyu ni mmoja wa marafiki zake wakubwa, urafiki ambao umedumu kutokana na tabia ya bwana Mwagoda, kumsifia sifia Kizinge, ambae anapenda sana kusifiwa kwa chochote anachosema au kufanya, “bwana Kizinge kweli nime kukubari, sasa kila mmoja anatakiwa kukuheshimu” alisema Kagari, kwa sauti yenye kusifia.

Hiyo ilimfanya mzee Kizinge ashangae kidogo, maana bado akuwa amezipata fedha alizo sema kuwa leo zinatumwa na kijana wake Masoud, “kwanini unasema hivyo Mwagoda, aliuliza Kizinge, kisha akaweka kombe la maji mdomoni nayabwiaa, “haaaa! bwana Kizinge, au mmefanya siri, kwa kijana wako kuwasia wakwe zake million moja na laki tano?” aliuliza Mwagoda, nakumfanya Kizinge ashtukwe kwangvu kiasi cha kualiwa na maji aliyoyajaza mdomoni mwake.

Kiainge anathema maji mdomoni mwake kisha haraka, “Eti! humjinga amefanya nini, yani mpaka sasa ajatuma ela ya kutengenezea trekta, alafu anawezaje kutumaela yote hiyo kwao?” aliuliza Kizinge huku anatembea haraka kuingia ndani ya ntymba, pasipo ata kumaliza vizuri au kuosha mswaki na uso wake.

Kizinge anaingia ndani huku anajisemesha peke yake, “huyu mjinga awezi kunifanyia hivi mimi, au ela yangu ndiyo kaituma kwa wale washenzi” hayo ni baadhi ya maneno ya Kizinge, ambae aliingia ndani, kisha dakika mbili mbele, akatoka akiwa na simu sikioni, ilyokuwa inaita.********

Naam mida hii ya saa mbili mwana dada Salma alie valia gauni lake refu na ijabu yake ya kupendeza, tayari alikuwa ofisini, kule kiwandani kinyelezi, akiwasisitiza wafanyakazi kuweka mambo sawa, kwamaana ya kwamba, akutaka Seb afike pale na kukuta vitu vipo hovyo.

Salma ambae leo mapema alijiandaa, na kuondoka nyumbani kwao pale Sinza, pasipo kumchukuwa Masoud, akicheleakumkuta Sebastian, kule ofisini, na kuzuwa maswali, ya kwamba kwanini yupo na mfanya kazi yule wakiume, aliingia ofisini ambako kulikuwa kumefanyiwa usafi wakiwango cha juu, kisha akakaa kwenye kiti chake.

Salma alitulia kwa dakika kadhaa, akitazama mazingira ya ofisi ile, ambayo siku za nyuma alikuwa anaitumia Sebaastian mwenyewe, lakini bahati mbaya kwake, kila alipokuwa anatazama, zilimjia kumbu kumbu za tukio la jana, la kufumaniwa na mwanamke anae itwa Anna, akiwa anaingiliwa kinyume na maumbile yalivyo, “hivi yule mwanamke mchawi, anawezaje kumfwata Masoud mpaka hapa, aliwaza Salma huku anachukuwa simu yake, na kuitafuta namba ya Masoud, “sijuwi ata kuwa wapi, maana mpaka sasa hivi ajafika kazini” aliwaza Salma, huku anataka kuipiga ile namba, lakini akasita kidogo, “ngoja kwanza nimpigie Seba nijuwe yupo wapi, alafu nitampigia Masoud, asije kunifuma naongea nae” alisema Salma, huku anaitafuta namba ya namba ya Sebastian.

Alipoipata namba hiyo. akaipiga mala moja, nayo ikaanza kuita kuita mala moja, nae akaisikilizia, huku anajiweka sawa kuongea kwa deko, ili kumpumbaza mpenzi wake huyo, ambae kiukweli akutaka kumkosa ata kwa bahati mbaya, maana amekuwa msaada mkubwa kwake na na wawazazi wake huko Mombo.********

Naaam wakati huo huo, mikocheni A dar es salaam, nyumbani kwa Sebastian, sasa kijana huyu alikuwa anatoka chumbani kwake akiwa amesha jiandaa vyema kabisa, amependeza kwa mavazi yake nadhifu, huku simu yake ikiwa sikioni, anaongea mtu flani, “hoooo! kumbe ushafika ofisini, basi mimi ndiyo natoka hapa, nika kuja hapo nimkuone, alafu nianze mizunguko” alisema Sebastian huku anatembea kuelekea sebuleni, ambako alimkuta Anna amekaa kwenye makochi anatazama television, huku akiwa amevalia gauni lake la zamani, yani lile alilotoka nalo mafinga, Sebastian anashangaa kidogo, “poa basi baadae kidogo” alisema Seba, huku anamtazama Anna, wakati huo akakata simu.

“Anna, kwanini umevaa nguo hiyo tena, kwani zile za jana akunaata moja uliyo ipenda?” aliuliza Sebastian, huku anamtazama Ana usoni, “hapana zile nzuri nitazivaa wakati wakwenda mjini” hapo Seba stain alitabasamu kwa udhuni, “sikia Anna, ebu kabadiri nguo, usiwe na shaka kuhusu nguo za kuendea mjini, nitakuja nazo, na baadae nitakupeleka mjini mimi mwenyewe” alisema Sebastian , kwa sauti ya kubembeleza iliyojaa urafiki, kama angekuwa mschana mwenye kujipenda Anna, basi tungesema Seba alikuwa analainisha, ili baadae ajinyakulie mwanamke huyu, lakini kwa maisha ya sasa, sidhani kama angekuwa na aja ya kufanya hivyo, na isitoshe wawili awa walikuwa tofauti kimwonekano, maana Ana wa sasa asingefaa kuwa ata kijakazi wa Sebastian.

Ana akainuka huku usowake umetawaliwa na tabasamu la furaha akaelekea ghorofani, huku Sebastian akimsindikiza kwa macho, siyo kwamba alikuwa anamtazama makalio au kitu flani kizuri sana, hapana, alikuwa anamtazama kwa kumwonea huruma, kwa jinsi kijana Masoud alivyo mpotezea nguvu, muda na uzuri wake, kisha kumtosa katika shida kubwa ya kuuguza wazazi wake. …….endelea….

UKIMALIZA FUNIKA
SEHEMU YA HAMSINI NA TANO
MTUNZI @MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA NNE: Ana akainuka huku usowake umetawaliwa na tabasamu la furaha akaelekea ghorofani, huku Sebastian akimsindikiza kwa macho, siyo kwamba alikuwa anamtazama makalio au kitu flani kizuri sana, hapana, alikuwa anamtazama kwa kumwonea huruma, kwa jinsi kijana Masoud alivyo mpotezea nguvu, muda na uzuri wake, kisha kumtosa katika shida kubwa ya kuuguza wazazi wake. …….endelea….

Baada ya hapo Sebastian, aliondoka zake huku akiacha maagizo yakinifu juu ya Arianna, kwamba apatiwe huduma zote kama ambazo angestairi mwanafamilia au mgeni muhimu wa familia, na pia hapo baadae angekuja mtu, kwaajili ya kumwandaa Ana, kwa safari ya kwenda matembezi mjini.

Ata wakati Sebastian akiwa anatoka na gari lake jipya lile Range lover nje ya geti, akasikia simu yake inaita, alipotazama simu, akaona kuwa mpigaji alikuwa ni Salma, kwanza aliiacha kwa sekunde kadhaa, huku akijitaidi kupunguza hasira, na alipoona amekaa sawa akaipokea, na hapo akadakwa juu juu, “jamani baby kwanini hivyo, yani auna hamu na mimi kabisa, ebu ona mpa saa hizi saa mbili aujafika kuniona” aliuliza Salma kwa sauti yenye kujilalamisha kwa kudeka, sauti ambayo kama ungebahatika kuisikia, ungese2ma kuwa Salma alikuwa mwenye mapenzi makubwa kwa Sebastian.

Lakini kinyume chake, sauti ile ilikuwa inakela na kuchefua masikioni kwa Sebastian, ambae ungemtazama muda huu, ungeona jinsi uso wake ulivyo kunja kwa hasira, “Salma uwezi kwanza kusalimia, au kuuliza hali yangu?” aliuliza Sebastian kwa sauti tulivu, tofauti na usowake ambao ulionekana wazi kujawa na hasira ya hali ya juu, “he! jamani baby, kwani nimefanya kosa kukumiss, ujuwe mwenzio nahamu na wewe, basi samahani kama nimefanya kosa” alisema Salma kwa maana ya kuwa ameonewa.

Kitendo hicho kilimfanya Sebastian azidi kuchafukwa, ila alijitaidi kujizuwia, kuonyesha kama amechaafukwa, “Salma unazani ilopekee linafaa kuombwa msamaha?” nazani swali la Sebastian lilimwacha njia panda Salma, ambae alishikwa na kigugumizi, “kwani… kwanini unasema hiyo, au ..” alibabaka Salma, ambae alionyesha wazi kutokuelewa maana ya swali la Sebastian, ambae alimuwai “nipo njiani nakuja, maana hapasijikii vizuri kichwa kina niuma sana” alisema Sebastian, ambae nikama alikuwa anaona kelo kuongea na Salma, “hoooo jamani mpenzi, pole sanaaaa, umeenda hospital, vipi dawa umekunywa, sasa unaendeshaje gari?” nimaswali mfululizo maswali ambayo Sebastian akujuwa aanze kujibu lipi, “nimesha tibiwa, usijari, poa baadae” alisema Sebastian na kukata simu, kisha akaachia tusi zito la nguoni, “kum…mak.. unaongea utazani unanipenda vile” alijisemea mwenyewe huku anaweka simu pembeni, wakati huo anaasha taa za upande wakushoto, kuionyesha kuwa alikuwa anaitaji kuegesha gari pembeni ya maduka ya pale chama, karibu kabisa na saloon kubwa ya Saphia mpemba.******

Naam mida hii, ya saa mbili za asubuhi, ndiyo mida ambayo kijana wetu Masoud, aliekuwa bado amepitiwa na usingizi, kwa kuzowea ratiba yake ya kuamshwa na Salma, kwaajili ya kuajiandaa kwenda kazini, aliamshwa na mlio wa simu yake, akakurupuka na kuitazama, akaona kuwa inatoka kwa baba yake, “mdingi huyooooo, anakumbushia ela yake, akaipokea na kuiweka sikoni, “shikamoo baba” alisalimia Masoud, kwa sauti ya usingizi, “dogo unakula maisha sana, yani sasa hivi ndiyo unaamka?” ilisikika sauti ya mzee Kizinge, iliyoonyesha kuja wa nafuraha kubwa, “siunajuwa mambo ya week enda baba, niambie kunanini tena mapema yote hii?” alisema Masoud, kwa sauti ya mtu mwenye maisha mazuri, mtu ambae awezi kuwa na wasi wasi ya kesho yake, “kwanza umeniuzi sana, unawekutuma ela kwa wapuuzi kama wale, alafu mimi ukanisahau?” aliuliza mzee Kizinge, kwa sauti ya kulaumu.

Ukweli Masoud alishangazwa sana na maneno ya baba yake, na sasa alianza kuona kuna ukweli ndani yake, maana ni mtu wa pili huyu anamweleza kuhusu kutuma fedha kwa kina Anna, japo kiukweli siyo yeye alie tuma, na akuwa na mpango wakutuma, licha ya kwamba akuwa na uwezi wowote wakupata hiyo millioni moja na laki tano, tena kwa haraka kiasi kile, lakini pia atakama angekuwa nazo, asinge mpatia fedha hiyo, sababu tayari alisha mwona kama mwanamke asiefaa, “baba uwe na wasi wasi, jana card iligoma kutoa fedha, ngoja nifike ofisini, nitakutumia” alisema Masoud, kabla ya kukata simu na kutazama muda.

Masoud anashtuka sana, kwakuona kuwa, tayari ilishatimia saa mbili za asubuhi, “inamaana Salma ajanishtua mpaka sasa hivi” aliwaaza Masoud huku anapiga namba ya Salma, simu ambayo ilipokelewa mala moja, “yani kama mawazo yetu yalikuwa sawa, nikasema ngoja nimalize kuongea na Seba, kisha nikupigie, maana nimeshangaa mpaka sasa ujafika kazini, nikajiuliza su hupo na kademu nini” alisikika Salma akiongea kwa sauti ya kudeka.

Hiyo ilimshangaza sana Masoud, “mh! kwani umeshaenda kazini, au ndio unamwogopa huyo bwana wako?” aliuliza Masoud kwa sauti ya kukasirika, “jamani Masoud, usikasirike baby, au ulitaka tuje wote iliaanza kututilia mashaka?” aliuliza Salma kwa sauti ya kubembeleza, na kupumbaza, “kwahiyo minafanyaje, maana ndiyo naamka hapa?” aliuliza Masoud, kama mtu asie juwa la kufanya, “kwani bado hupo nyumbani?” aliuliza Salma, akimalizia kwa kicheko, “ndiyo bado nipo home, yani ndiyo nahamka hapa” alisema Masoud, “basi we tulia, yeye anakuja hapa, akiondoka tu nakufwata, unipe kimoja, alafu tuje kazini, maana mtu mwenyewe amerudi anaumwa” alisema Salma, akionyesha kufurahia sana mpango wake.

Ilimfrahisha sana, maana akuna kitu alikuwa anaogopa au akutaka kitokee, kana kushindwa kuwa huru na Salma, sababu ya ujio wa Sebastian, “poa usisahau ile ela ulimwahidi baba” alikumbusha Masoud, huku akijuwa fika kuwa fedha hiyo, itatoka kwa mwanaume mwenzie, “hooo! nakumbuka, Masoud, wacha kwanza Seba aje, nianipe hiyo laki tano, alafu ashughurikie na swala la kadi” alisema Salma kwa kujiamini, akijuwa wazi kuwa anatarajia kucjukuwa fedha kwa mwanaume huyu na kupeleka kwa mwanaume mwingine. …….endelea…. 

Maoni 1 :

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu