Mpya
Taji la ubaya 41-45
TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"
Sehemu 41.
"Boss angalia kabati hilo lilivyo kaa hapo inaonesha nyuma ya hilo kabati kuna kitu walikuwa wanaficha" Ediga alitoa maelezo ambayo akina Fatuma kule ndani walijua hapo ndo mwisho wao
"Haya ebu ondoeni hilo kabati" hiyo ilikuwa ni amri ya Derick akiwaambia vijana wake, hata akina Jacob kule ndani walisikia maneno hayo.
Kwa mara ya kwanza Jacob alijikojolea kwa kutetemeka, Fatuma naye halikadhalika hivyo hivyo alilimwaga kojo kwa uoga na wote walijua huo ndo mwisho wao kwa sababu roho ya Mr Derick walikuwa wanaijua alivyo mtu wa roho mbaya.
Akina Ediga walianza kupambana na lile kabati kuliondoa pale, lile kabati lilikuwa limetengeneza kinamna yaani, akina Jacob wakiwa wanaingia pale kuna sehemu walikuwa wanaizungusha tu alafu kabati linajigeuza lenyewe.
Sasa akina ediga wenyewe baada ya kuzungusha walianza kutumia nguvu kulihamisha pale, walitumia kama nusu saa walifanikiwa kulitoa, kitendo cha kutoa kabati waliona mlango upo pale ukutani.
"Kabla sijalipua na bomu naomba mtoke wenyewe huko ndani" Mr Derick baada ya kuona mlango ule aligundua lazima ndani kutakuwa na watu tu na alitumia vitisho ili kuwafanya watoke.
Kutokana na akina Jacob walivyo kuwa wanaijua roho ya Mr Derick ilivyo waliamua kutoka wenyewe bila hata kuvutwa maana walijua kweli watalipuliwa kule ndani.
"Hahaaaa Jacob kwa hiyo ulijiona mshindi eee, alafu na huyu demu kumbe Naye mpumbavu hivi eee" Mr Derick baada ya kuwaona wametoka wenyewe alianza kuwazunguka huku akiwa anaongea maneno.
"Sasa Jacob Kabla ya yote naomba twende ukanikabidhi nyaraka zote tena muda huu" Derick alianza kutoa vitisho
"Mzeee naomba tuache basi ikiwezekana hizi mali tugawane pasu kwa pasu" Jacob alijitilisha huruma mbele ya akina Derick.
"Jacob sitaki maneno mengi, we ndo wakunidharirisha mjini hapa kweli?? Ediga wachukueni twende kule kwake akanipatie nyaraka zote" Jacob alikuwa hataki utani kabisa
Basi akina Jacob walifungwa kamba kila sehemu na mdomo, walichukuliwa na kupakizwa kwenye gari.
Gari zilitoka speed ya kufa mtu mpaka kule nyumbani kwa Jacob, baada ya gari kufika akina Jacob na fatuma walishushwa mkuku mkuku na ilikuwa ni usiku wa manane kabisa mwenzi ukiwa unawaka ni balaa.
Baada ya kuwashusha waliogoza mpaka kwenye geti na kufungua kuingia ndani, lakini Mr Derick na watu wote walishangaa baada ya kufungua geti kumuona binti mmoja wa kiarabu akiwa kakaa kwenye varanda ya nyumba hiyo usiku huo na alikuwa hana wasi wasi, Jacob naye alishangaa kwamba ni mtu gani ambaye anaishi nyumbani kwake bila ruhusa yake.
Walisogea mpaka pale alipo yule binti.
"We nani na unafanya nini hapa?" Mr Derick aliuliza kwa ukali
Yule mrembo hakuongea kitu alitabasamu tu, ila Jacob na fatuma walipo angalia vizuri waligundua yule ni shaifa, Jacob alibaki katumbua macho akiwa haamini kama kamuona shaifa tena kwa mara nyingine.
Hapo Jacob aliona kabisa kuna msaada wanaenda kuupata kwa shaifa ila hakujua baada ya msaada huo nini kitafuata! Ndo hapo Jacob alishindwa kuelewa sijui afurahie kuwepo kwa shaifa pale sijui anune alikuwa hata haelewi.
"We binti inamana we ni bubu?? Nakuuliza we ni nani??" Mr Derick aliuliza kwa mara ya pili kwa kufoka
"Heeee heeee tafadhali baba wee usinifokee kwangu sawa eee? Wew ndo inatakiwa nikuulize wewe ni nani? Kwa sababu hapa ni kwangu mimi na mume wangu"shaifa bila hata ya wasi wasi alijibu, mpaka Jacob mwenyewe alishangaa majibu ya shaifa na hakuelewa huyo mume anaye zungumziwa na shaifa ni yupi
"We binti usitake kuingia kwenye kesi ambayo siyo yako!! Sawa eee we Jacob hii nyumba unataka kuniambia umeuzaa na wakati umesema nyaraka zote zipo huku??" Mr Derick ilibidi awe mkali na alimgeukia Jacob.
Jacob kwa uoga hakujibu kitu, Mr Derick alimuwasha kofi la kufa mtu Jacob
"We mjinga mi nakuuliza we umekaa kimya, nasema hii nyumba umeuza na huyu binti ni nani??" Mr Derick alikuwa hataki masihara hata kidogo
Baada ya lile kofi kwa Jacob ni kama ndo walichokoza moto wa shaifa maana alikasirika mpaka sura ilibadilika
"Hivi nyie mmeyachoka maisha eee?? Aliye kupa ruksa ya kumpiga mume wangu nani? Na kwa nini mumemufunga kamba hivyo? Sasa nasemaje ndani ya dakika tano sitaki kuwaona hapa na mutuache kama tulivyo sawa eee niliko toka nimevurugwa, sitaki hasira zangu ziishie kwenu" Shaifa aliongea kwa hasira tena kibabe mpaka kila mtu alishangaa, na kwa urembo wa shaifa hakuna ambaye angeamini kile shaifa anazungumza.
Jacob alishangaa maneno ya shaifa kwamba yeye ni mume wake, hapo Jacob mapigo ya moyo yalianza kudunda mara mbili, maana alijua hata akisaidiwa hapo na shaifa bado huko mbele yajayo ni taabu kwake.
Nao akina Mr Derick baada ya kusikia vitisho vya mtoto wa kike walianza kucheka, maana maneno yake hayakuendana na yeye alivyo.
"Ediga fungueni na huyo mrembo hiyo itakuwa chakula changu baada ya haya maswala kuisha" Mr Derick kwa zarau aliwaambia akina ediga wamkamate shaifa, maana jamaa tayari alikuwa kashampenda mtoto wa kike jinsi alivyo mzuri.
Kile kitendo cha akina ediga kusogea ili wamkamate, kwanza mtoto wa kike aliruka juu kama anapaa alivyo tua chini tayari kijana mmoja wa Mr Derick alikuwa amekatwa shingo na haikueleweka shaifa kamkataje maana hata kisu hakushika.
Watu wote pale walishanga hayo maajabu, Mr Derick alikuwa hajaelewa mchezo ulivyo fanyika yaan aliona kama mazinga ombwe, Derick baada ya kuona hivyo alitoa bastola yake na kumlenga shaifa, ila alishangaa baada ya kumfyatulia risasi shaifa, ile risasi shaifa aliigonga kwa mkono na ikaenda kumpiga ediga mkono.
Wakiwa hawajaa kaa sawa Shaifa alipita na shingo ya kijana mwingine, hapo Derick alishangaa anabakiwa na vijana wanne wakati walikuwa sita.
Yaani akina Derick walipoteana baada ya kuona shaifa siyo mtu wa kawaida, walikimbia speed za kufa mtu, Mr Derick alikuwa na kitambi ila siku hiyo hakikuonekana kwa speed alizo kimbia, baada ya kufika nje walipanda gari na kupotea.
Itaendelea......
Usikose sehemu ya 42.
TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"
Sehemu 42.
Yaani akina Derick walipoteana baada ya kuona shaifa siyo mtu wa kawaida, walikimbia speed za kufa mtu, Mr Derick alikuwa na kitambi ila siku hiyo hakikuonekana kwa speed alizo kimbia, baada ya kufika nje walipanda gari na kupotea.
Huku nyuma Jacob alikuwa anatetemeka hapo ndo alishuhudia kabisa ukatili wa shaifa maana binti alikuwa anang'oa shingo za watu kama utani vile, yaani Jacob alibaki kaganda mwili wote unatetemeka.
Fatuma yeye baada ya kuona akina Derick wamekimbia uoga ulimuisha kabisa maana shaifa alikuwa anamjua vizuri na alikuwa hamuogopi kwa lolote.
"Jamani karibuni ndani" shaifa aliongea kwa tabasamu kubwa na alikuwa anafungua mlango kuingia ndani yaani kama mwenyeji vile.
Jacob alibaki kaganda mlangoni akiwa haelewi afanye nini yaani mawazo yalikuwa yanamjia mengi mno kichwani, alikuwa anawaza akimbie mara akili nyingine inamwambia liwalo na liwe yaani alikuwa kama kapigwa na kitu kizito kichwani.
"Jacob tuingie ndani" Fatuma baada ya kuona Jacob kaganda mlangoni ilibidi arudi kumwambia Jacob aingie ndani
"Fatuma mi nakufa leo, shaifa ataniacha hai kweli mimi" Jacob alikuwa anamuogopa shaifa ni hatari hasa baada ya kuona yale mauaji
"Jacob nimegundua huyu mjinga kakupenda toka moyoni hawezi fanya kitu, na nikwambie kitu ukitaka muendane na shaifa usimbishie vitu vyake sawa ee?" Fatuma alimnong'oneza Jacob na baada ya hapo waliingia ndani, na walikuta shaifa kakaa kwenye sofa hana hata Papara yaani kama kwake vile.
"Fatuma za siku nyingi, naona bado kale kamtindo kako ka kuniingilia mambo yangu bado kunaendelea??" Baada ya akina Fatuma kuingia , shaifa alimudaka Fatuma juu juu kwa maswali
"Shaifa mi sitaki uchokozi kabisa na wewe, nimekuingilia kwa lipi" Fatuma wala alikuwa hamuogopi shaifa Hata kidgo
"Fatuma kwa nini umenichukulia mume wangu? Yaani na wew unajinafasi kama wako vile?"
"Shaifa ivi mi na wewe nani alianza au umesahau kwamba ww ndo umeniingilia kwa mume wangu"
"Fatuma hilo sitaki kujua ninacho jua Jacob ni mume wangu, na nisingelazimishwa kutoa ujauzito wake Saiz ningekuwa nina mtoto na Jacob" shaifa aliongea maneno ambayo yalifanya Jacob na Fatuma wote washangae, kumbe shaifa alikuwa na ujauzito wa Jacob na inaonekana jamii yake ilimlazimisha kutoa ujauzito huo.
Fatuma baada ya hayo maneno aliamua kukaa kimya maana aliona wanako elekea ni kubaya na alikuwa anamjua shaifa vizuri akikasirika.
"Jacob Mimi na Fatuma unamchagua nani??" Shaifa alimugeukia Jacob na kumuuliza swali.
Jacob baada ya hilo swali alianza kutetemeka upya na moyoni mwake alikuwa hamtaki kabisa shaifa, na baada ya hilo swali alitaka kusema anamchgua Fatuma, ila Jacob alipo mwangalia Fatuma kuna ishara aliipata ambayo ilikuwa inaonesha kwamba usinichague mimi, maana Fatuma alikuwa anamjua vizuri shaifa kuliko Jacob.
"Shaifa mi nakuchagua wew" Jacob aliongea japo kwa wasi wasi na kutetemeka
"Jacob hayo maneno yametoka moyoni mwako??" Shaifa aliuliza kwa furaha akiwa anatabasamu.
Jacob alikubali, hapo shaifa alimrukia Jacob na kuanza kumpiga makiss ya kila rangi, Fatuma alikuwa anaumia moyoni tena sana ila ndo hakuwa na namna maana ile ndo ilikuwa njia ya kufanya Jacob awe salama, maana alijua, endapo Jacob angesema anamchagua Yeye hapo ndani palikuwa hapakaliki.
Baada ya yale mabusu shaifa kwa furaha aliingia jikoni kupika yaani kama yeye ndo mama mwenye nyumba.
"Fatuma kwa nini umesema nikubali na kumchagua yeye" Jacob kwa sauti ya chini Aliongea baada ya shaifa kwenda jikoni
"Jacob huyu mi namjua vizuri hatakagi kushindwa na ungesema umenichagua mimi sielewi ambacho kingetokea humu ndani, na ndo maana mi nilikuwa nakusisitizia tufunge ndoa mapema maana nilikuwa najua haya mambo yatakuja kutokea" Fatuma naye aliongea kwa sauti ya chini.
"Duuuuuu! Fatuma ila usijali baada ya hapa tunaenda kufunga ndoa maana mi simtaki shaifa kabisa" Jacob alikuwa hataki kuoa mwanamke kioja
"Jacob kwa saiz hiyo itakuwa ngumu na najua nisipo kaa sawa naenda kukukosa kabisa maana hawa watu wakishapenda mi nawajua vizuri walivyo" Fatuma alikuwa anaongea huku akiwa anatoa machozi na hana matumaini ya Jacob kuja kufunga naye ndoa tena.
Jacob ndo alikuwa anazidi kuchanganyikiwa kabisa akiwa anasikia maneno ya fatuma na alikuwa anamfuta machozi fatuma na kichwa cha Fatuma muda huo kilikuwa kwenye mapaja ya Jacob
"Heheeee heee! Fatuma unanitafuta eee ndo nini kumlalia mume wangu hivyo si kasema hakutaki unalia nini sasa?? Bibi we mi sitaki ugomvi kabisa sawa eee" Shaifa baada ya kutoka jikoni aliona watu wamelaliana alafu wanafutana machozi, hapo wivu na hasira vyote kwa pamoja vilimpanda.
Jacob na Fatuma ilibidi waachiane, baada ya hapo shaifa alileta chakula japo ilikuwa ni usiku wa manane kuelekea asubuhi ila walikula kiani hivyo hivyo.
"Jacob naomba twende chumbani tukalale basi, Fatuma we tafuta chumba cha kulala sawa eee, na buguza na mume wangu mi sipendi kabisa" Shaifa aliongea na kumshika Jacob mkono kuelekea chumbani kulala.
Itaendelea......
Usikose sehemu ya 43
TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"
Sehemu 43.
"Jacob naomba twende chumbani tukalale basi, Fatuma we tafuta chumba cha kulala sawa eee, na buguza na mume wangu mi sipendi kabisa" Shaifa aliongea na kumshika Jacob mkono kuelekea chumbani kulala.
Jacob na shaifa walizama chumbani, Fatuma akiwa anajionea kwa macho, Siku hiyo Fatuma moyo ulikuwa unauma kama unataka kuchomoka yaani kupambana kote kule leo hii anaenda kumkosa Jacob kizembe hivyo.
Jacob akiwa kule chumbani na shaifa kijasho chembamba kilikuwa kinamtoka, yaani alikuwa anaona kama amelala na nyoka, kitu ambacho hata Shaifa aligundua
"Jacob Mbona unaniogopa hivyo? Kwani mi nina kasoro gani au ubaya gani?? Mi mwenyewe nina haki ya kupendwa kama wanawake wengine mbona, au kwa vile unaona sijakamilika??" Shaifa aliongea maneno matamu ya kujitilisha huruma kwa Jacob na alikuwa anaongea huku analia, inaonekana mtoto wakike alikuwa kapenda kweli yaani mpaka Jacob alianza kujiuliza moyoni mwake kwamba jini gani analia hivi.
Shaifa baada ya kulia kama nusu saa alianza kumpapasa Jacob taratibu taratibu (haaa! Jamani mapenzi yaache yaitwe mapenzi) yaani Jacob baada ya kuanza kupapaswa na shaifa mwili ulimsisimuka na alijikuta anatamani ashikwe Zaid ya vile maana mtoto wa kike alikuwa na mkono laini mpaka raha.
Baada ya kama nusu saa tayari Jacob na shaifa walikuwa wapo kwenye ulimwengu mwingine kabisa, yaani walikuwa wanapeana mahaba ya kufa mnyaturu, mpaka Jacob aliisahau kwamba shaifa ni mtu wa namna gani.
Siku hiyo Jacob alipewa mapenzi na shaifa ambayo hajawahi pata kwa mwanamke yeyote tangu azaliwe, yaani alianza kuhisi kama mapenzi yalianzishwa na shaifa, Naye shaifa kutokana na penzi alilopewa na Jacob alianza kuona kama dunia nzima ni yake.
Yaani siku hiyo Jacob alifunga Magori mengi ambayo hayana hata idadi, yaani ilifika mpaka saa nne asubuhi shaifa na Jacob wakiwa hawajaamka kwa uchovu wa mechi waliyo piga.
Fatuma naye kutokana na kukosa kabisa usingizi siku hiyo hakulala kabisa yaani alikuwa macho muda wote, roho ilizidi kumuuma Zaid baada ya kuona Jacob na shaifa wanachelewa kuamka ili walau ajue hali ya Jacob.
Mida ya saa tano shaifa ndo aliamuka na alitoka chumbani akiwa anajinyosha alipo fika sebuleni alimkuta Fatuma ashaamka kitambo na alikuwa amekaa huku akiwa anawaza mengi.
"Heeee Fatuma mbona kama unalia?? kulikoni?" Shaifa baada ya kufika sebuleni ilibidi akae na kumuuliza Fatuma
"Shaifa roho inaniuma siyo kitoto yaani moyo wangu ni kama unataka kuchomoka, tafadhali naomba niachie Jacob wangu nakuomba dada shaifa" Fatuma aliamua kuongea ukweli wa moyo wake, yaani machozi yalikuwa yanatoka kama maji kwa mara ya kwanza toka Baba yake na shaifa afariki ndo siku hiyo Fatuma alimuita shaifa dada, mpaka shaifa mwenyewe alishangaa
"Makubwa!! Fatuma leo we wakuniita Dada!? Umesahau kipindi cha nyuma ulisemaje? We si ulisema huwezi niita dada kwa sababu mi na wewe ni tofauti au umesahau na wew hujawahi niita Dada tangia Baba afariki leo kimekupata nini?? Shaifa alishangaa kuitwa dada na Fatuma.
"Pamoja na yote Dada shaifa naomba niachie Jacob wangu mwenzako nimetoka naye mbali kweli" Fatuma alizidi kulia huku akiwa amepiga magoti anambembeleza shaifa.
Ni kweli shaifa alianza kumuonea huruma Fatuma, ila ndo hivyo naye alikuwa anampenda Jacob na alikuwa amepitia mambo mengi magumu juu ya Jacob, leo hii amuache Jacob kizembe hivyo alikuwa anaona ni ngumu.
Muda wote huo wakati hayo yanaendelea Jacob alikuwa ashaamuka anachungulia mlangoni.
"Daaaaa!! Fatuma tunafanyaje sasa najua kweli umetoka Naye mbali lakini mwenzako nahisi kwa saiz siwezi ishi bila Jacob yaani nampenda haswa na kwa raha alizo nipa leo uuuuuuu!! Kumuacha itakuwa ngumu kwa kweli". Shaifa aliongea kwa sauti ya upole huku akiwa anamfuta machozi Fatuma maana tayari roho ya huruma juu ya Fatuma ilikuwa imemuingia.
"Dada shaifa mwenzako nina ujauzito wa Jacob, ww huoni ntakufa kwa pressure endapo ntamkosa Jacob"Fatuma aliamua kuongea maneno ambayo yalimuacha shaifa mdomo wazi mpaka Jacob mwenyewe pale mlangoni alishangaa maana ilikuwa ni habari mpya masikioni mwake.
"Fatuma we mja mzito??" Shaifa alishangaa maana hakuna kitu shaifa alikuwa anakiheshimu kama ujauzito
"Ndiyo Dada shaifa" Fatuma alizidi kutia huruma
(Jamani hapo ndo utaamini kweli mume anauma maana jinsi Fatuma alivyokuwa anatia huruma we acha tu, najua mpenzi msomaji we hukuwepo ila malaika wako alikuwepo)
Baada ya shaifa kusikia hivyo alichoka kabisa aliona kama kweli kamfanyia ukatili wa kutosha Fatuma, tukumbuke japo shaifa alikuwa siyo binadamu wa kawaida ila alikuwa na ubinadamu ndani yake maana Baba yake alikuwa binadamu wa kawaida, kwa hiyo fatuma alikuwa na tabia za binadamu nyingi kuliko hata za ujinini, kwa hiyo maumivu alikuwa anayajua vizuri, pia alikuwa ana hisia za kibinadamu kabisa.
"Fatuma sorry kwa yote najua unaumia na mi sikujua kama we mja mzito, ila naogopa hata nikwmbiaje yaani, mwenzako nahisi nikimuacha Jacob kabisa ntakufa mie, maana muda huu ninao kwambia nimetengwa na koo Yangu na jamii yangu nzima kisa nimekataa kuachana na Jacob na mwenzako nawindwa ni hatari yaani wanatamani muda wote waniue sema ndo hivyo wanashindwa, we fikiria niliamua kutoa ujauzito wangu wa mara ya kwanza kwa sababu ya Jacob, maana nilipewa chaguo nitoe ujauzito wa Jacob au niachane na Jacob ujauzito ubaki, nilichagua kubaki na Jacob, lakini baada ya ujauzito kutoka bado hawakutaka mimi kuwa na Jacob na nilipewa adhabu za kufa mtu na nilifungwa sehemu ambako nilikuwa siruhusiwi kutoka, na ndo maana hata sikuonekana tena kuja kwa Jacob, leo nimepambana nimefanikiwa kukimbia kule nimekuja huku alafu nimuache Jacob kirahisi hivyo kwa kweli nashindwa Fatuma hata ungekuwa wewe usingeweza!! Mi mwenyewe nina hisia na ninatamani siku moja niitwe mama kama wengine na ndo maana sikutaka kuachanishwa na Jacob kama nilivyo achanishwa na wanaume Wangu wa mwanzo" Shaifa alisimulia naye jinsi alivyo mpigania Jacob, ni sawa alikuwa anamuonea huruma Fatuma ila hakuwa tayari kumuacha Jacob kivyovyote vile.
Jacob akiwa pale mlangoni alikuwa anashangaa jinsi wanawake wanavyo mlilia mpaka naye alikuwa anashindwa kuelewa kwamba yeye ana nini cha ziada haswa, mpaka wamng'ang'anie vile.
Itaendelea......
Usikose sehemu ya 44.
TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"
Sehemu 44.
Jacob akiwa pale mlangoni alikuwa anashangaa jinsi wanawake wanavyo mlilia mpaka naye alikuwa anashindwa kuelewa kwamba yeye ana nini cha ziada haswa, mpaka wamng'ang'anie vile.
Baada ya yale maelezo ya shaifa, Fatuma hakuelewa aongee nini maana ukiangalia ni kweli kila mtu kapitia mitihani yake mpaka leo hii kuwa na Jacob, kwa hiyo kila mtu alikuwa anaona yeye ndo ana haki ya kuwa na Jacob zaidi na bahati mbaya zaidi kwa Fatuma, Jacob alikuwa katamka kwamba anamtaka shaifa mbele ya wote wawili.
Jacob baada ya kuona mazungumzo yameisha na wote wapo kimya alijitokeza na kwenda kukaa kwenye sofa.
"Jacob unajua kama Fatuma ana ujauzito wako??" Shaifa ilibidi amuulize Jacob kwa upole baada ya Jacob kukaa.
Jacob alifikiria jibu la kujibu alimwangalia jinsi Fatuma anavyo tia huruma na akakumbuka mapito waliyo yapitia yeye na Fatuma
"Ndiyo najua" Jacob aliamua kukubali, wakati hajui lolote kuhusu ujauzito
"Sasa kama ni hivyo kwa nini jana ukanichagua mimi wakati unajua Fatuma ana ujauzito wako??" Shaifa alizidi kumtandika Jacob maswali ambayo yalimfanya Jacob asielewe cha kujibu, ila Jacob kuna jibu lilimjia
"Aaaaa nilikuchagua wewe kwa sababu Fatuma alinikonyeza kwamba nikuchague wewe" Jacob aliongea ukweli na sijui alikuwa na maana gani
"Heeee! Unasemaje? Inamana Fatuma ndo alikwambia unichague Mimi? Siyo kwamba ulinichagua kisa unanipenda?" Shaifa alishangaa majibu ya Jacob.
"Shaifa siyo kwamba sikupendi, nakupenda tena sana ila kutokana na ujauzito wa Fatuma niliogopa kwamba nikikuchagua wewe mbele yake atapata madhara, ndo hapo Fatuma alinambia we mchague tu mi sina shida" Jacob alikuwa anajibu kwa kutumia akili mpaka yeye mwenyewe alishangaa kwamba ile akili ya kujibu vile kaitoa wapi.
"Heeeee!! Mbona maajabu Fatuma anavyo kulilia hivyo angeruhusu we ukalale na mimi kweli??" Shaifa bado alikuwa haamini
"Shaifa ni kweli si huyo hapo Fatuma muulize?" Jacob alirushia mpira kwa Fatuma japo hakujua kama Naye Fatuma atajibu kama yeye anavyotaka
"Fatuma anachosema Jacob ni kweli wewe ndo ulimwambia anichague Mimi?" Shaifa alimugeukia Fatuma
"Ndiyo ni kweli" Fatuma Naye aliunga hoja
"Heeee!! Fatuma sasa kama ni hivyo kwa nini unamlilia na kwa nini ulisema anichague mimi kama na wewe bado una mpenda na una ujauzito wake??" Shaifa bado ni kama hiyo kitu ilikuwa haimwingii akilini.
"Shaifa mi nilisema hivyo kwa sababu kwanza nakupenda kama dada yangu kwa hiyo sikutaka uumie maana bila wazazi wako mi nisingekuwa Kama nilivyo leo, pili nilikuwa najua jinsi gani Jacob anavyokupenda maana mara kwa mara tukiwa tumelala naye nilikuwa nasikia anavyo kuota na kutaja jina lako, tatu nilifanya hivyo ili kusiwe na bifu yoyote kati yetu Sisi watatu maana nilijua Jacob akinitaja mimi wewe hautakuwa na furaha na mimi, wakati mimi bado nakukubali wewe kama ndugu yangu wa pekee" Fatuma Aliongea maneno ambayo yalimfanya Jacob atikise kichwa, maana Mama Aliongea uongo ulioenda shule.
Shaifa alibaki kakaa kimya, maana katika maisha yake shaifa kitu alichokuwa anapenda ni kusifiwa na kupendwa yaani alikuwa hataki kupingwa kitu chake, baada ya hayo maneno aligundua kumbe Fatuma ni mtu mwema kwake na ni ndugu wa kufa na kuzikana.
Hapo shaifa aliamua kwenda kumkumbatia Fatuma kwa upendo, maana mtu kukuachia mwanaume anayempenda kisa anakuheshimu siyo kazi ndogo
(Wale wazee wa kupenda nadhani tunajua hili swala).
"Fatuma Asante kwa kunijali" Shaifa aliongea kwa tabasamu pana.
"Asante dada shaifa" Fatuma Naye aliitikia kwa heshima, japo Fatuma bado alikuwa haelewi hatima yake yeye na Jacob.
"Sasa jamani sikieni mimi nawaacha hapa naondoka mara moja naweza nikaja baada ya siku tatu nataka nikamwangalie mdogo wangu Sharifa maana mazingira niliyo muacha sina imani nayo kabisa" Shaifa aliwaaga kwamba anaondoka na shaifa alikuwa siyo mjinga hata kidogo japo maneno ya Jacob na Fatuma kayaamini asilimia mia ila alikuwa hana uhakika kama kweli Jacob anampenda, na aliamua kuondoka ili amuache Jacob na Fatuma na atakapo rudi ndo apime upendo wake kwa Jacob, maana aliamini kama kweli Jacob anampenda Fatuma baada ya yeye kurudi atakuwa hana hamu naye kabisa, pia alifanya hivyo kama kumpa Fatuma mtihani wa kumshawishi Jacob Aachane na Shaifa abaki na Fatuma tu, maana shaifa aliamini kama kweli Fatuma ataweza kumshawishi Jacob siku hizo tatu basi atakuwa anapendwa zaidi kuliko yeye na atamuachia Fatuma mwanaume na kama itakuwa tofauti hapo hamuachi ni bora wa share mwanaume.
Hayo yalikuwa ni mawazo ya shaifa na plani yake ya kuwapima hao watu.
Basi shaifa aliaga na kuondoka, hapo kimoyomoyo Fatuma alikuwa ashaanza kupata furaha na kuchekelea maana alijua Jacob anarudi mikononi mwake asilimia 💯.
Itaendelea......
Usikose sehemu ya 45.
TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"
Sehemu 45.
Basi shaifa aliaga na kuondoka, hapo kimoyomoyo Fatuma alikuwa ashaanza kupata furaha na kuchekelea maana alijua Jacob anarudi mikononi mwake asilimia 💯.
Jacob hakufurahishwa sana kuondoka kwa shaifa maana kwa penzi alilo pewa usiku na shaifa alianza kumuona Fatuma ni hamna kitu, yaani moyo wake ulianza kuzama kidgo kidgo kwa shaifa, Yaani Shaifa alikuwa amekamilika kila sekta kwenye uzuri wa sura yupo, kwenye shape ndo usiseme, ufundi kitandani ndo balaa tupu hivyo vitu vilimfanya Jacob asahau kwamba shaifa siyo binadamu wa kawaida.
"Jacob jamani mbona kama unawaza au ndo ushampenda shaifa??" Fatuma baada ya kuona Jacob anawaza ni kama alianza kumgundua vile.
"Hamna Fatuma hata siwazi mbona, ila nataka kujua ni kweli we mjamzito?" Jacob alitaka kujua kama kweli Fatuma yale aliyo ongea mbele za shaifa ni kweli
"Jacob we unafikiri mi ningesemaje? Mi kukukosa ndo sitaki kabisa, ujauzito sina ila ilikuwa plani tu" Fatuma kumbe hakuwa hata na ujauzito
"Heeee!! We mjinga nini yaani nakuteta kumbe huna hata ujauzito, je shaifa akigundua ulikuwa unamdanya huoni kama ni balaa lingine??" Jacob alikasirika
"Jacob kuna kitu kimoja nataka nikuombe leo maana sina uhakika kama tutakuwa wote, maana kwa nilivyo kuona ni tayari kama ushaanza kumpenda shaifa, kwa hiyo mi naomba unisaidie walau nibaki na kumbukumbu" Fatuma alikuwa anaongea huku anatoa machozi yaani ni kama alikuwa anajikatia tamaaa vile.
"Fatuma si useme ni kitu gani? Alafu unalia hivyo kwani mi nimesema nakuacha??" Jacob alikuwa hamuelewi Fatuma ni kitu gani anataka
"Jacob naomba walau nikuzalie mtoto mmoja ambaye hata likitokea la kutokea atabaki kama kumbukumbu" Fatuma alitoa ombi lake.
Jacob alibaki katumbua macho alitamani acheke, lakini kicheko hakikutoka
"Fatuma we mpuuzi kweli sasa hicho ndo cha kuniomba we kama upo tayari sawa mi sina shida kwani huo ujauzito nabeba mimi si unabeba wewe, alafu hiyo itasaidia maana shaifa atajua tulicho mwambia ni kweli" Jacob hakuwa hata na wasi wasi na hilo.
Basi usiku ulifika, Jacob na Fatuma waliendeleza kazi ya kutafuta watoto kitandani, ila Jacob yaani mizuka ilikuwa imepungua sana, yaan alikuwa hana hisia tena na Fatuma na tayari ni masaaa tu alikuwa ashamisi penzi la shaifa.
Yaani siku hiyo aliona Fatuma kama hajui kitu chochote kuhusu mapenzi, wakati kipindi cha nyuma alikuwa anamsifia Fatuma kwamba ndo fundi.
Basi siku hiyo ilipita kihivyo Jacob hakuenjoy kitu chochote kwa Fatuma, japo Fatuma aliigundua hali hiyo kwa Jacob ila ndo hivyo hakuongea kitu chochote maana alihisi akiongea lolote Jacob anaweza Kususa.
Zile siku tatu alizo zisema Shaifa ziliisha na Jacob alikuwa anamsubiri shaifa kwa hamu mno, maana alikuwa kamiss miuno ya shaifa mpaka alikuwa anamuota kwenye ndoto (kweli mapenzi hayazoeleki) yaani kidogokdogo Jacob ndo alikuwa ameanza kumpotezea Fatuma.
"Jacob ina maana Ndo huna hamu na mimi hivyo? Mbona kila nikija kukaa ulipo kaa una ondoka why mume wangu unafanya hivyo??" Fatuma alikuwa ashakuwa mtu wa kubembeleza kila siku kwa Jacob.
"Fatuma ishia hapo hapo! Nani mume wako? Lini tumefunga ndoa? Sitaki mambo ya kitoto mimi ! Alafu nikuchane tu ukweli Fatuma hujui mapenzi bana mwanamke gani kama gogo bwana!! Yaani hata kupetipeti hujui" Jacob alifunguka.
"Jacob si ndo ungekuwa unanielekeza makosa yangu ili nijirekebishe mi ni binadamu kweli yawezekana kuna sehemu sikufurahishi ila nakuahidi ntajirekebisha" yaani Fatuma alibaki mtu wa kumlamba miguu Jacob jinsi alivyokuwa anabembeleza na alikuwa anaona kabisa siyo muda anaenda kumkosa Jacob na alikuwa anaomba shaifa asirudi.
Jacob hakutaka hata kumsikiliza aliondoka na kwenda nje kupunga upepo.
Zilipita Siku tano shaifa akiwa hajarudi, yaani hapo Jacob ndo alikuwa haelewi kitu kabisa.
Siku ya sita Shaifa alirudi na siku hiyo mtoto alikuwa kapendeza mpaka Fatuma aliogopa hapo ndo alijua kabisa Jacob wake kwaheri.
Jacob baada ya kumuona shaifa alimkimbilia na kumkumbatia kwa furaha kweli, yaani Shaifa alikuwa ananukia manukato ambayo hata Jacob hajawahi kuyaona popote.
"Shaifa unanukia vizuri mpaka raha" Jacob uvumilivu ulimshinda ilibidi asifie, yaani huko kwa Fatuma ilikuwa wivu wa kufa mtu moyo ulikuwa unauma kweli.
"Dear nimekuletea zawadi, najua utaipenda" yaani shaifa alikuwa anaongea sauti tamu ambayo hata wewe mpenzi msomaji ungesikia, hata bila kumuona ungempigia kura ya Umiss dunia.
Itaendelea...........
Usikose sehemu ya 46.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Write your comment