Mpya
Taji la ubaya 51-55
TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"
Sehemu 51.
Huku kwa Jacob pamoja na vijana wake walikuwa wanaliandaa pigo lingine kwa Mr Derick, maana Jacob katika peleleza yake aligundua bwana Derick bado hajakoma kumfuatilia.
"Dulla sikilizeni, kitu cha kufanya kesho usiku inatakiwa twende kwenye ile pub yake ya pale bondeni na tukifika pale hakikisheni tunajaribu kila kitu" Jacob alikuwa anatoa maelekezo kwa vijana wake akiwemo kijana anayeitwa dulla.
Masaa yalisogea hatimaye ikawadia siku nyingine na ilikuwa ni mida ya jioni kabisa, akina dulla walionekana mitaa ya bondeni huko uswahilini ambako ndo ile pub ya Mr Derick ilikuwepo, waliingia mpaka pub na kusoma mazingira yalivyo kaa na kwa muda huo pub ilikuwa imechangamka sana na watu walikuwepo wa kutosha.
Baada ya uchunguzi akina dulla waliondoka, muda ulizidi kusogea mpaka saa sita usiku bado watu walikuwa wanaendelea kuponda raha katika pub hiyo, akina dulla walikuwa karibu na maeneo hayo hayo wanasubiri watu wote watawanyike na siku hiyo Jacob hakuwepo.
Ilipo fika mida ya saa nane za usiku maeneo ya pub palikuwa pametulia yaani watu wote walikuwa wameondoka alibakia tu mlinzi anarinda maeneo hayo na mlinzi mwenye alikuwa bwana Nguna yule aliye kuwa analinda nyumba ya kina Jacob kabla ya kufukuzwa.
Akina dulla walivamia maeneo hayo kwa kasi na kumtihibiti yule mlinzi, walimfunga kamba na kumziba mdomo alafu wakamtia kwenye mfuko.
Kwakuwa walikuwa na funguo za kila aina yaani funguo bandia walikuwa nazo za kila aina, walifungua mlango na kuingia, walichokifanya ni kuvunja kila kitu mule ndani, alafu waliingia mpaka atore ya vinywaji walimwaga petroli kila Sehemu mule ndani na vitu vyote walimwagia petroli, kisha wakatupia njiti ya moto na kuondoka.
Asubuhi na mapema Mr Derick akijiandaa ili aende kwenye gereji yake kuangalia maendeleo ya gari lake, maana tangia gari lake liharibiwe alikuwa hana gari la kutembelea na alilipeleka gereji ili kubadilisha injini ya gari.
Akiwa ndo anatoka alipo fika tu mlangoni simu yake ilianza kuita ,na alipo pokea simu taarifa alizo pewa zilikuwa siyo nzuri kwa upande wake.
Baada ya kupewa zile taarifa ilibidi aende eneo la tukio na alipo fika huko alijikuta moyo wake unaanza kudundia chini ya kitambi maana alikuwa haamini kile anacho kiona.
Yaani pub yake kila kitu mule ndani kilikuwa kimeungua, Derick alivuta picha kwamba ni nani anayeweza kufanya vile ila hakupata jibu alimfikria Vicky kwa kuwa ashakuwa adui yake ila bado aliona hawezi kuwa yeye.
Baada ya kuangalia pembeni Mr Derick aliona watu wakiwa wamemzunguka bwana Nguna na walikuwa wanamhoji kwamba ilikuwaje.
"Heeeeeee!! Nguna kumbe upo hapa ehee nambie ilikuwaje??" Mr Derick naye alisogea pale na kuuliza kwa pupa
Mr nguna alianza kusimulia ilivyo kuwa na alisimulia wale vijana pia aliwaona jioni maeneo hayo, kutokana na maelezo ya bwana Nguna Mr Derick alianza kumfikiria Jacob.
"Huyu mtoto ndo kafikia huku sasa huyu hanijui" Jacob aliongea kwa hasira ni kama ana uhakika kwamba Jacob ndo kafanya vile.
Upande wa vijana wake na bwana Jacob yaani akina dulla walikuwa wanapongezana kwa kanzi nzuri na siku hiyo Jacob aliwapa pesa nzuri nzuri tu ya kwenda kutumbulia bata.
"Jamani sasa subirieni shemeji yenu niliyewaambia nimempata majuzi yaani ni bonge la kifaa, akija hapa lazima wote mpagawe" Dulla alikuwa anamsifia demu wake wakiwa wapo bar wanajirusha.
Baada ya muda kama nusu saa alionekana Vicky maeneo hayo akiwa anaingia
"Demu mwenyewe huyo hapo" Dulla aliwaonesha jamaa zake, kumbe demu mwenyewe alikuwa ni Vicky na Vicky aliamini labda dulla anaweza kuwa mtu sahihi kwake.
Baada ya rafiki zake na dulla kumuona Vicky kila mtu alibaki katumbua macho kwa uzuri wa Vicky.
Basi baada ya Vicky kufika pale story za hapa na pale ziliendelea na ilipo fika usiku dulla aliondoka na mpenzi wake.
Huku nyuma jamaa zake walianza kumjadili kwamba labda dulla anatumia mizizi maana waliamini dulla hawezi mpata demu mrembo vile kwa njia ya kawaida ila ndo ukweli dulla alikuwa kampata Vicky.
Ulipita kama mwezi hivi Jacob akiwa anashirikiana na akina dulla katika kazi zake mbalimbali na tayari Mr Derick alikuwa ashajua kwamba mtu aliye husika na yale matukio yote ni Jacob, kwa hiyo Naye alikuwa anaanda pigo kali kwa Jacob.
Balaa lilipo anzia kwa Jacob yaani ni kwamba mambo yote na siri zote ambazo alikuwa anajadili na vijana wake, dulla Naye alikuwa anaenda kumsimulia mpenzi wake Vicky.
Vicky baada ya kujua siri nyingi za Jacob na mipango yake yote dhidi ya Mr Derick, hapo Vicky aliamua kumtafuta Mr Derick ili waungane kumkabli Jacob na alijua wakifanikiwa na yeye atarudi kuishi maisha kama ambayo alikuwa anaishi mwanzo.
Itaendelea......
Usikose sehemu ya 51.
TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"
Sehemu 52.
Vicky baada ya kujua siri nyingi za Jacob na mipango yake yote dhidi ya Mr Derick, hapo Vicky aliamua kumtafuta Mr Derick ili waungane kumkabli Jacob na alijua wakifanikiwa na yeye atarudi kuishi maisha kama ambayo alikuwa anaishi mwanzo.
Vicky alimtafuta Mr Derick wiki nzima hakumpata hapo aliamua kumfuata mpaka nyumbani kwake anako ishi na mke wake Mama Jacob, Vicky bila hata hofu alifika na kugonga mlango.
Siku hiyo Mr Derick alikuwa kakaa na akina ediga na vijana wengine wote ambao huwa anashiriana nao kikazi hata Mama Jacob naye siku hiyo alikuwepo ili kutia mawazo yake.
Siku hiyo walikuwa wanaandaa mipango ya kumkabili Jacob ili wamtie mikononi, wakiwa kwenye mipango hiyo walisikia mlango unagongwa, Mama Jacob alipo enda kufungua alishangaa kumuona Vicky.
"Heeeeee!! We barazuli umefuata Nini huku??"Mama Jacob pale pale mlangoni alianza kuwaka bila haya kumkaribisha mgeni.
"Jamani nina taarifa muhimu sana kuhusu Jacob nimewaletea" Vicky alijitetea, mpaka Mr Derick alisikia kule nje jinsi Vicky na mke wake wanavyo jibishana.
Baada ya kusikia kwamba kawaletea taarifa kuhusu Jacob ilibidi wamuruhusu aingie ili wamsikilize.
"Haya ongea kilicho kuleta na ukiongea upuuzi nakulamba chuma si unanijua?" Mr Derick alimpa ruhusa ya Vicky kuongea tena kwa vitisho.
Vicky alianza kusimulia kile kilichomleta na lengo la kuja pale, baada ya kutoa maelezo yote kila mtu alibaki katabasamu mule ndani.
"Hapo Vicky ndo nakukubaligi kwenye mishe kama hizi japo muda mwingine unaletaga usenge, jamani naamini kile tulichokuwa tunajadili tumeshapata jibu jinsi tutakavyo tekeleza" Jacob aliongea meno yote yakiwa nje.
Upande wa Fatuma tayari safari ya kurudi mjini kuja kuanza kazi ilikuwa imewadia na baada ya kufika alipokelewa vizuri na mkuu wa hospitali na Fatuma alikabidhiwa makazi ya kuishi, Fatuma baada ya wiki moja alikuwa ashaanza kazi na alitafuta binti wa kazi kwa ajili ya kubaki na mwanae yeye akiwa kazini, kiufupi Fatuma alifurahi sana kuanza ile kazi ambayo ndo ilikuwa ndoto yake ya siku zote.
Fatuma alikuwa hajawahi pata muda wa angalau kupumzika kwamba siku hiyo aende walau kumjulia hali Jacob na kwenda kumuonesha mwanae japo alifanyiwa ukatili na Jacob ila kwake bado alikuwa hajaliweka moyoni na alikuwa ashamsamehe kila kitu bila hata Jacob kuomba msamaha
(Wanawake igeni mfano wa Fatuma siyo mnakuwa na visirani na mtu mpaka kufa kwenu).
Jacob akiwa na wale vijana wake walikuwa wanapanga mipango yao namna ya kwenda kuziteketeza zile gereji za Mr Derick na kuharibu gari zote za wateja ambazo zipo kwenye gereji zake ili wamtie hasara na kumkosanisha na wateja wake, akina Jacob walipanga kila kitu na wakakubaliana mipango itakavyoenda.
Na siku zote Jacob akiwa anapanga mipango na wale vijana walikuwa wanatumia ule mjengo mwingine ambao alikuwaga anakaa Vicky mara ya kwanza, na aliogopa kuwapeleka kwake kabisa kwa sababu alikuwa anaishi na Sharifa.
Baada ya hiyo mipango yote kama kawaida dulla naye alienda kumsimulia Vicky kama walivyo panga na akina Jacob, maana jama alikuwa kapenda kweli kiasi kwamba alikuwa anatoboa siri zote yaani mpaka nukta bila yeye kujua kwamba yule anaye mwambia ni mtu hatari kwa upande wao.
"Kwa hiyo dulla, na huyo unayemsema Jacob boss wenu naye atakuwepo??" Vicky alikuwa anazidi kumpeleleza dulla kiaina
"Duuu!! Sijajua kama atakuwepo"
"Dulla bana ebu mpigie simu ujue, maana si unajua boss akiwepo angalau mi nakuwa na Aman kwamba mpenzi wangu utarudi salama, maana mkienda na boss angalau mnakuwa makini na kazi" Vicky alijidekesha akiwa anamwambia dulla.
Dulla jinsi alivyokuwa zoba naye alimpigia simu Jacob na kumuuliza, Jacob alisema kwenye mpango huo hatakuwepo
"Boss mi naomba uwepo maana ukiwepo wewe kazi ndo inaenda vizuri, ujue usipo kuwepo vijana hawajitumi kabisa, alafu ujue siku ile nusura tufelishe mchongo" yaani dulla alikuwa anamshawishi na Jacob awepo ili kumfurahisha mpenzi wake Vicky, baada ya ushawishi huo Jacob alikubali kwamba Naye atakuwepo.
Baada ya mazungumzo ya Vicky na dulla, Vicky alitoka nje mara moja na kumpigia Mr Derick, alimwaga ubuyu wote kwa Mr Derick.
Siku ya tukio lenyewe ilifika, huku Jacob akiwa amejiandaa vizuri bila hata ya kujua tayari mpango wake ushavuja, na ilikuwa jioni ambapo muda waliopanga wa saa saba usiku ndo ulikuwa unaenda kuwadia.
Jacob na wale vijana wake walikusanyika kama kawaida Sehemu moja ambayo huwa wanakutana kila siku na baada ya kukutana walikumbushana majukumu ambayo inatakiwa wakafanye na Jacob aliwasisitizia sana kuendana na muda
"Jamani tukifika pale mi ntakuwa kwenye gari yaan ninyi mtashuka na kwenda kumaliza kazi tuliyo panga na inatakiwa Kazi isiwe Zaid ya dakika kumi, zikishafika hizo dakika mi ntawasha gari na aliye mzembe atabaki huko huko" Jacob alitoa maelezo ya mara ya mwisho kwa vijana hao kabla hawajaingia kazini.
Baada ya yote tayari muda uliwadia na safari ya kuelekea eneo la tukio lilianza bila kujua huko waendako ni balaa zito lipo huko, maana nao akina Mr Derick walikuwa wamejianda vya kutosha.
Itaendelea......
Usikose sehemu ya 53.
TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"
Sehemu 53.
Baada ya yote tayari muda uliwadia na safari ya kuelekea eneo la tukio lilianza bila kujua huko waendako ni balaa zito lipo huko, maana nao akina Mr Derick walikuwa wamejianda vya kutosha.
Akina Jacob walifika eneo la tukio, akina dulla walishuka jacob
Yeye alikuwa amebaki kwenye gari, gereji yenyewe ilikuwa imezungushiwa fensi, akina dulla
walianza kunyata ili wamvizie mlinzi na baada ya kumthibiti mlinzi Ndo waingie ndani.
Lakini kabla hawajafika getini walishangaa kundi la watu limewazunguka na kuwaweka kati na matochi yalikuwa yanawamulika usoni walishindwa hata kukimbia, hapo akina dulla waliwekwa chini ya ulinzi wakati kule kwenye gari Jacob alikuwa bado hajaona lile tukio maana gari alikuwa kalipaki kwa mbali kidogo.
Akina Mr Derick baada ya kuwakamata akina dulla walishangaa hawamuoni Jacob, hapo ilibidi akina dulla wabanwe ili wataje Jacob alipo jificha na kutokana na kipigo walitaja kwamba wamemuacha kwenye gari.
Jacob akiwa katulia kwenye gari hana hata wasi wasi anasubiri vijana huko wafanye kazi alishituka baada ya kuona kioo cha gari kimepigwa na gogo zito na kilipasuka chote, akiwa anatahamaki nini kimetokea alishangaa vijana wawili washazama kwenye gari na kumuweka chini ya ulinzi, hapo jamaa ilibidi afungwe na kupelekwa kule waliko wenzake.
Baada ya kuwakusanya wote Mr Derick aliwabeba mpaka kwenye jumba fulani ambalo lilikuwa halitumiki na walifungwa hapo.
Dulla alishangaa na kutahamaki baada ya kuona mpenzi wake Vicky akiwa anaingia na alikuwa hana hata wasi wasi
"Heeeeeee dear umefata nini huku?? Dulla aliuliza kwa mshangao kitu hicho kilifanya Derick na vijana wake wacheke, pia naye Vicky alicheka sana, mpaka hapo dulla alikuwa haelewi mchezo mzima.
Jacob alikuwa naye anashangaa picha linalo endelea na alimshangaa dulla kumuita Vicky dear
"Inamana dulla huyu ndo demu wako ulikuwa unamzungumzia kila siku??" Wakiwa wamefungwa pale chini ilibidi Jacob amulize dulla.
Baada ya dulla kukubali kwamba ndiye hapo Jacob alijua kwamba kumbe sababu ya wao kunaswa ni huyo Vicky
"Jacob hata uniangalie kwa jicho la vipi leo ni mwisho wako" Vicky Aliongea kwa madaha na muda huo anaongea alikuwa anamvuta Jacob masikio, kitu kilicho mfanya Jacob asikie maumivu kupita kiasi (Nadhani ndugu zangu kila mtu anajua maumivu ya sikio)
Jacob alianza kuchezea kichapo ili awaambie nyaraka zilipo, Jacob alipigwa mpaka alizimia ila bado alikuwa hakubaliani na swala la kumuachia mali zake Mr Derick aliona ni bora afe kuliko kumuachia mtu mpuuzi kama yule mali zake.
Baada ya Jacob kuzimia, akina Derick ilibidi wawaache ili wapumzike na waliwaweka kama kiporo, kesho yake asubuhi mateso yaliendelea kwa Jacob na wenzake, ila kipigo kikuu kilikuwa kinaenda kwa Jacob.
Mr Derick alipo ona Jacob ni mgumu kuzungumza aliamua kumfyatulia risasi dulla tena ya kichwani ili amtishe Jacob, Jacob alipo ona dulla kapigwa risasi ya kichwa mwili ulianza kutetemeka hapo aligundua bwana Derick hana mchezo kabisa.
Jacob alianza kufikiria maswali mengi kichwani mwake, je akiwapa hizo nyaraka si bado watamuua, alifikiria mengi mwishowe alipata jibu kwamba ni bora asiwape, akiwa anajiuliza maswali kichwani mwake kijana mwingine alikula chuma ya kichwa, hapo Jacob ndo alichanganyikiwa ilibidi awaambie zile nyaraka ziliko.
"We mjinga kweli na tusipo zikuta huko porini tunaenda kukuulia huko huko unajifanya mafia eee,??" Mr Derick aliunguruma kwa sauti ya ukali mpaka utumbo wa Jacob uliunguruma kwa hofu.
Basi bila hata kucheleweshwa Jacob alifungwa kamba mwili mzima na kuzibwa mdomo ili asiongee chochote, yaani yeye ilikuwa ni kuwaonesha ishara tu ya wapi waelekee, wale vijana watatu walio bakia waliachwa wamefungwa na walikuwa wanalindwa pia.
Safari ya kuelekea kule porini ambako Jacob kaficha zile nyaraka ilianza, na gari ilikuwa inatembea kwa speed ya mwisho kabisa, ilifika Sehemu trafiki wakaisimamisha ili kuona kama kuna usalama, baada ya askari kukagua aligundua kuna usalama maana Jacob alikuwa kainamishwa haonekani, yule askari wa barabarani aliwaangalia wale vijana wa Mr Derick akiwemo na ediga aliona sura zao ni kama zina mashaka hivi, ila aliamua kuwaruhusu waendelee na safari.
Jacob alifikiria mengi mno aliona kwenda kuwakabidhi watu hao nyaraka ni uzembe mkubwa mno, alicho kifanya Jacob baada tu ya kupata upenyo akiwa kafungwa kamba alijirusha dirishani, hakuogopa hata vioo vya gari, yaan alichomoka na vioo vya dirisha la gari na alikuwa ameamua liwalo na liwe.
Baada ya kuchomoka kwenye kioo bahati nzuri ilikuwa hawajafika mbali kutokea kwenye hilo eneo ambapo matrafiki wanasimama, akina Derick baada ya kuona ni kama mambo yanaenda kuharibika, Mr Derick alimfyatulia risasi Jacob pale chini alipo angukia, na kwa nyuma waliona trafiki anakuja kwa speed kali, hapo akina Derick ilibidi kuondoa gari na kukimbia.
Yule trafiki alipo fika pale alipo jirushia Jacob aliona Jacob hata hatamaniki maana vioo vilikuwa vimemkata hovyo na risasi pia ilikuwa imemuingia maeneo ya kwenye bega.
Watu wengi walio kuwa wanasafiri kupitia barabara hiyo walisimama na kushangaa lile tukio na walikuwa wanashangaa limetokeaje tena mbele ya maaskari kabisa na ni asubuhi kweupe kabisa, ila hawakupata majibu.
Basi Jacob alikimbizwa hospitalini na wasamaria wema na alipelekwa ile ile hospitali ya rufaa ambayo ndo Fatuma anafanyia kazi.
Huku nyumbani kwa Jacob, Sharifa akiwa anaangalia TV aliona habari inayomuhusu Jacob, na kutokana na taarifa hiyo ripota wa taarifa hiyo alikosea na kuripoti kwamba Jacob ni kama ameuawa, yaani alikuwa ni kama anathibitisha kwamba Jacob amekufa!!
Sharifa baada ya kuona tarifa hizo mapigo ya moyo yalianza kumuenda mbio na hatimaye alizimia akiwa pekee yake pale nyumbani.
Itaendelea......
Usikose sehemu ya 54.
TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"
Sehemu 54.
Sharifa baada ya kuona tarifa hizo mapigo ya moyo yalianza kumuendea mbio na hatimaye alizimia akiwa pekee yake pale nyumbani.
Sharifa alikuja kuzinduka ishakuwa jioni, na baada ya kukumbuka zile taarifa hapo ndo alikurupuka na kwenda hospitalini kwenda kuona je ni kweli ile taarifa aliyo isikia ndivyo ilivyo, baada ya kuondoka tu huku nyuma Mr Derick aliingia akiwa na vijana wake, walitafuta nyaraka kila Sehemu hawakuona.
"Sasa ediga unajua hapa tunafanyaje , kwa kuwa huyu mpuuzi atakuwa amefariki acha mi nihamie hapa, na kama kuna mtu alikuwa anakaa hapa anahama maana mi ndo mrithi pekee niliye baki" Mr Derick baada ya kushindwa kuzipata nyaraka zote ilibidi aanze kujimilikisha mali yeye mwenyewe akiwa na uhaki kwamba tayari Jacob atakuwa amekufa.
Sharifa baada ya kufika hospitalini alienda mpaka mochwari kuuliza mwili wa Jacob, ila aliambiwa kwamba Jacob bado yupo hai ila hali yake ni mbaya sana, hapo moyo wa Sharifa ulipunguza kwenda kasi japo bado alikuwa na hofu kubwa.
Akiwa anatoka maeneo ya kule mochwari kwenda kwenye wodi za wagonjwa mahututi uso kwa uso alikutana na Doctor Fatuma.
"Heeee!! Sharifa ni wewe ama naota!!??" Fatuma baada ya kumuona Sharifa alishangaa
"Ni mimi dada Fatuma" Sharifa aliongea kwa sauti ya kinyonge na machozi yalikuwa yanamtoka
Fatuma baada ya kuona hivyo ilibidi aanze kumuuliza nini kimetokea??
Baada ya Sharifa kuelezea kila kitu, sasa hapo mapigo ya moyo yalihamia kwa Fatuma, mtoto wa watu alichanganyikiwa nusura azimie
(nyie kupenda kuache kama kulivyo)
Yaani pamoja na Fatuma kwamba alipigwa chini na Jacob ila zile taarifa zilimchanganya ni hatari
Fatuma haraka haraka alienda kwenye wodi aliyoambiwa Jacob ndo kalazwa, baada ya kufika pale hakuamini macho yake baada ya kuona kipenzi cha roho yake kimelala pale kinabembelezwa na Israel mtoa roho.
Fatuma alipo ulizia mbona mgonjwa bado hajaanza kushughulikiwa aliambiwa wanasubiri kibali kutoka polisi, hapo Fatuma aliona wasimtanie yaani Baba wa mtoto wake afe kisa sababu za uzembe kiasi hicho, hapo aliamua liwalo na liwe, ilibidi yeye mwenyewe aingie kazini, japo alikatazwa na mkuu wa hospitali ila yeye alisema hilo haliwezekani.
Fatuma siku hiyo hakurudi hata nyumbani, hakujali huko nyumbani kuna mtoto anahitaji kunyonya ama laa, alichokuwa anataka ni kuhakikisha Jacob anakuwa salama, kibali cha kutibiwa kwa Jacob kutoka polisi ndo kilifika saa sita usiku na muda huo Fatuma alikuwa yeye ashanza kutoa matibabu toka jioni.
Zilipita siku tatu Fatuma hajarudi nyumbani, yaani alikuwa habanduki kwenye kile chumba alicho lazwa Jacob, yaani ilifika kipindi mpaka madaktari wenzake wakawa wanamuonea huruma.
Binti wa kazi naye baada ya kuona boss wake hajaonekana nyumbani siku tatu na mtoto anasumbua ilibdi afwate huko huko hospitalini, baada ya Fatuma kumuona yule binti akiwa na mwanae ndo alishituka na kukumbuka kumbe aliacha mtoto nyumbani
(Jamani mapenzi yaache kama yalivyo)
Zilipita wiki tatu Jacob akiwa bado hajazinduka japo alikuwa ameanza kuonesha dalili nzuri, na kipindi hicho chote Sharifa alikuwa amehamia kwa Fatuma maana kule tayari Mr Derick alikuwa ashajimilikisha mji, na kipindi hicho Mr Derick alikuwa anafikiria namna ya kwenda kuyachukua yale makampuni ili yawe chini yake tena.
Baada ya mwezi mmoja kupita Jacob alirudiwa na fahamu na mtu wa kwanza kumuona akiwa anazinduka alikuwa ni Fatuma, Jacob baada ya kumuona Fatuma jinsi anavyo pambana juu yake machozi yalibaki yanatoka yenyewe maana alikuwa anajutia kile alicho mfanyia Fatuma mwanzo.
Kadri Siku zilivyo zidi kwenda Jacob ndo alikuwa anazidi kuimarika, na Jacob nguvu mpya zilianza kuja baada ya kuoneshwa mwanae na mwanae huyo alikuwa kafanana kila kitu na mzee wake Mr deus, hapo Jacob aliona ni lazima apone ili apambane kwa ajiri ya mwanae.
Naye Sharifa ilibidi amsimulie Jacob kila kitu kilichotokea nyumbani na namna Mr Derick alivyo jimilikisha mjengo.
Baada ya miezi kama miwili Jacob alipona na kuwa fiti, alimshukuru Fatuma kwa ukarimu wake na kumuomba msamaha kwa yale yaliyopita, Fatuma hakuwa na tatizo lolote na Jacob na baada ya Fatuma kuambiwa kwamba shaifa alifariki hapo Fatuma aliona ndo nafasi yake ya kumiliki jimbo mazima maana Jacob alikuwa hana ujanja wa kwenda kokote.
Fatuma pamoja na kufanya vizuri katika swala la kumtibia Jacob mpaka kupona alisimamishwa kazi kutokana na kupingana na sheria za kazi pamoja na mkubwa wake wa kazi.
Hapo Fatuma ilibidi abakie mtu wa kukaa nyumbani na pesa ilianza kukata mdogo mdogo maana alikuwa hana chanzo chochote kinacho muingizia pesa.
Jacob naye alipotea pale nyumbani alipo kuwa amepangaa Fatuma maana kwa muda huo hapo ndo alikuwa naye anakaa, na Jacob hakutaka kuaga mtu yeyote kwa sababu alikuwa na maana yake kufanya vile.
Itaendelea......
Usikose sehemu ya 55.
TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"
Sehemu 55.
Jacob naye alipotea pale nyumbani alipo kuwa amepangaa Fatuma maana kwa muda huo hapo ndo alikuwa naye anakaa, na Jacob hakutaka kuaga mtu yeyote kwa sababu alikuwa na maana yake kufanya vile.
Jacob alikuwa kachafukwa na roho aliona akizidi kucheka na bwana Derick mwishowe atakufa kweli, hapo Jacob alicho kifanya alitafuta vijana kama watatu na kuwashawishi wakafanye kazi ambayo yeye aliwaambia na aliwaahidi pesa nono kabisa, hao vijana nao hawakusita kukubali.
Mida ya usiku Jacob akiwa na wale vijana alio watafuta walionekana wamebeba madumu ya petrol kule ushwahilini mitaa ambako kuna nyumba ya bwana Derick japo kwa muda huo alikuwa haishi huko na alikuwa bado hajampangishia mtu yeyote
Baada ya akina Jacob kufika huko kitu walicho kifanya kwenye nyumba ya bwana Derick kilibaki simulizi mitaani, maana waliichoma moto nyumba yote bila hata huruma.
Mr Derick akiwa kwenye mjengo wa Jacob anajibweda bila hata wasi wasi alipata taarifa kwamba nyumba yake ya kule uswahilini imeungua, hapo jamaa alishangaa na kuchanganyikiwa na alikuwa haelewi nani kafanya vile, akiwa bado hajaa kaa sawa mara walianza kusikia ving'ora vya gari za askari kwa nje.
Mr Derick na mke wake wakiwa bado hawaelewi kile kinachoendelea mara waliona Jacob akiwa na askari anazama mule ndani, hapo Mr Derick alibaki mdomo wazi maana hakuelewa Jacob kaponaje, na alikuwa hana ubishi maana haki ya kuishi pale ilikuwa siyo yake.
Jacob na mke wake walikamatwa kwa kosa la uvamizi, baada ya kufika kituoni, sijui Mr Derick aliwadanganya nini askari walimuachia ndani ya siku moja na taarifa za kuachiwa kwa Mr Derick Jacob naye alizipata.
Jacob hapo ilibidi afikirie kitu cha kufanya maana aliona akichelewa anaweza kuwahiwa yeye, baada ya kufikiria sana alipata jibu, na jibu lenyewe ilikuwa ni kumtumia Vicky.
Jacob aligundua Vicky ni mtu anayependa maisha mazuri na ili kupiga ndege wawili kwa jiwe moja aliona njia pekee ni kumtumia huyo huyo Vicky.
Jacob alipeleleza ni wapi Vicky anakaa, na alipata majibu kwamba Vicky anakaa kwa rafiki yake mmoja ambaye walikuwa wanasoma chuo pamoja kipindi cha nyuma, Jacob hapo ilibidi amfuate Vicky
"Heeee makubwa Jacob we upo serious kweli unataka turudiane au ndo unataka kunitumia kwenye vita yako wewe na Huyo mzee wako??" Vicky Naye alishangaa kuambiwa na Jacob kwamba eti warudiane.
Ila pesa haijawahi shindwa, kutokana na Vicky kupenda pesa na maisha mazuri alikubali vile vishawishi vya Jacob, hapo Jacob aliona lengo lake linaenda kutimia.
Ilipita kama wiki moja hivi, Jacob akiwa anajirusha na Vicky kwenye kumbi mbalimbali za starehe, taarifa hizo zilimfikia mpaka Fatuma pia Naye Mr Derick alizipata.
Fatuma baada ya kusikia taarifa hizo alilia sana, maana alijua kabisa Jacob ni mtu ambaye habadiliki, pia alikuwa anamuonea huruma jinsi Vicky atakavyo fia kifuani mwa Jacob.
Kipindi chote hicho Jacob alikuwa hajawahi kufanya mapenzi na Vicky, na alikuwa anampeleka Vicky sehemu nzuri nzuri ili amuaminishe kwamba yupo serious na hayo mahusiano.
Basi siku moja Jacob alimpeleka Vicky kwenye ile nyumba ya Mr jomo, maana tangia Fatuma ahame pale hiyo nyumba ilikuwa haikaliwi na mtu yeyote.
Baada ya kufika huko Jacob kuna vitu alianza kumshawishi Vicky
"Vicky najua tunapendana, kitu ninacho kuomba naomba umudanganye Mr Derick kivyovyote aje hapa, ili anipe mimi kadi yangu ya benki maana kuna kadi aliichukua wakati anakaa pale nyumbani kwa hiyo we tumia akili yoyote umshawishi aje hapa ili mi nimbane" Jacob alizidi kumdanganya Vicky,
Kwakuwa Vicky naye alikuwa ashaanza kumuamini Jacob, alimpigia simu Mr Derick na alimdanganya Mr Derick kwamba tayari kamuwekea Jacob dawa za kulevya kwenye kinywaji kwa hiyo aje wamalize kazi.
Kwa kuwa naye Mr Derick alikuwa anajua Vicky amerudiana na Jacob aliamini kwamba ni kweli.
Derick aliwakusanya vijana wake ili waende eneo la tukio.
Jacob baada ya kuambiwa Mr Derick anakuja siyo muda, kitu alichokifanya ilikuwa ni huzuni kwa Vicky, Jacob alimnyonga Vicky bila hata ya huruma na baada ya kumnyonga aliwaandikia maaskari ujumbe kupitia simu ya Vicky uliosomeka
"Jamani naombeni msaada Mr Derick na watu wake wanataka kuniua Mimi nipo nyumba namba KB44 mtaa wa xxx" baada ya kuandika ujumbe huo alituma kwa askari na yeye alitoweka maeneo hayo.
Baada ya dakika tano akina Mr Derick walifika eneo la tukio na walizama mpaka ndani maana mlango ulikuwa wazi, wakiwa hawajakaa sawa walishangaa askari zaidi ya ishirini wamefika pale na siraha za kutosha.
Hapo akina Mr Derick waliwekwa chini ya ulinzi na ushahidi ulikuwa ni ile sms waliyotumiwa na marehemu na uzuri walikutwa eneo la tukio
(kweli auwaye kwa upanga naye atakufa kwa upanga, maana Mr Derick naye mbinu kama hiyo ndo alitumia kumkamatisha Jacob kwa askari kipindi cha nyuma)
Baada ya Mr Derick na wenzake kukamatwa walipelekwa kituoni na baada ya siku chache walipandishwa mahakamani, kwa kuwa ushahidi ulikuwepo kabisa walisomewa kifungo cha maisha jera.
Yaani Mr Derick hakuamini kama ndo anaenda kuozea jera, na mke wake Mama Jacob alibaki ni mtu wa kutangatanga hovyo maana nyumba ya uswahilini waliyokuwa wanategemea ndo ilikuwa ishaungua.
Jacob alienda kumchukua Fatuma na mwanaye pamoja na Sharifa na kuwapeleka kwenye mjengo wake na aliwaelezea sababu za yeye kuwakimbia, Fatuma naye alirudishwa kazini kama kawaida, na baada ya wiki moja kupita Jacob na Fatuma walifunga ndoa takatifu.
Maisha ya Jacob yalibaki ni ya raha mstarehe maana yule aliye kuwa anawabuguzi ndo alienda kunyea debe, baada ya mwaka mmoja kupita Jacob alipata taarifa za Mama yake mlezi kufariki kwa BP japokuwa alifanyiwa mabaya na mama huyo ila ilimuuma na alichukua jukumu la kumzika Mama huyo ambaye ndo alimchukulia kama Mama yake mzazi.
MWISHO

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Write your comment