SEHEMU YA ISHILINI NA NNE
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA TATU: unaweza kupata ata mbili tatu kwa mashabayako machache” alisema mzee Mdemu, na hapo mama Anna akatazama chini, “baba we, tulisha kodisha muda mrefu, yani huu ndio msimu wamwisho” alijibu mama Anna, akionekana kusikitishwa na jibu alilolitoa, aana alikumbuka kuwa feza za kodi ya shamba, alikuwa ameipeleka kwenye ada na matumizi ya Masoud, mtoto wa mzee Kisinge, ambae alitarajia, angekuwa mkwe wake, ambae angebadirisha maisha yao kwa ujumla, “imekuwaje jamani, mgonjwa amesha tibiwa?” aliuliza Emmanuel mala baada ya kuwafikia. .…. endelea….
Nahapo ndipo mzee Mdemu akaanza kumweleza kijana huyo, wa kijijini kwao, alie wapokea jana usiku, kuwa mgonjwa amefanyiwa vipimo, ambavyo gharama yake imecukuwa kiasikikubwa cha fedha yao, na kufanya wabakiwe na kiasi kidogo sana, na tayari ilisha bainika kuwa, mzee Sinyangwe alikuwa anasumbuliwa na vidonda vya tumbo, vilivyo muhasiri, kwa kiwango kikubwa sana, kiasi cha kuitajika kufanyiwa upasuaji, kwaajili ya kunusuru, kuendelea kuhasirika kwa sehemu nyingine za utumbo wake, iliitajika Tanzania shilingi laki nane, ilikukamilisha upasuaji na matibabu, ambao ulitakiwa ufanyike haraka, kati ya leo na kesho, maana kesho kutwa ingekuwa jumamosi, kwamaana ni siku za week end, siku ambazo ingekuwa vigumu kwa mzee Sinyangwe kupatiwa matibabu.
Walisha juwa kuwa, kule kijijini wasinge pata fedha za kuweza kumtibu mzee Sinyangwe, na pia wasinge wezakumpata ata mtu ambae angejitolea kuwaazima fedha hizo, lakini kwa kijana Emmanuel, ambae akufahamu mausiano ya ulaghai ya familia ya kina Anna, na mzee Kizinge, na kwamba ata siku iliyopita, mzee Kizinge na mke wake, walikataa katakata kuwasaidia wanafamilia awa, kumsafirisha mzee wao kwenda hospital, ambao siyo tu kuwa ni wakwe wenza, pia ata Elimu ya kijana wao Msoud wao ndio waliisimamia.
Emmanuel akawapatia jibu la matatizo yao, “dada Anna kwani ulisha achana na Masoud?” aliuliza Emmanuel,huku anamtazama Anna, “hapana atujaachana, kwanini unauliza hivyo?” alijibu Anna kwa haraka, jibu ambalo liliambatana na swali, “kwanini sasa unaangaika fedha wakati mumeo ni boss mkubwa huko dar?” aliuliza Emanuel kwa sauti yenye kujaa mshangao, “mh! boss wapi wakati bado anasoma, aliuliza Anna, kwa sauiti ambayo aikuwa katika mshtuko wakukubariana na kauri ya Emmanuel, “mh! anasoma wapi, wakati yeye ni manager kwenye kiwanda cha kutengeneza na kuuza vitu vya kwenye majumba” alisema Emmanuel ambae alionekana kuwa na uhakika na kile anacho kisema.
Hapo siyo Anna peke yake, ila ata mama yake na mzee Mdemu, ambao walimtazama Emanuel kwa macho ya kiukaguzi, kwamba yupo sawa au anaweza kuwa katika mwonekano wakuwa na matatizo ya kiakiri, wakamwona kijana Emmanuel akiwa anaipekuwa simu yake kubwa ya kigusa, wao wanaita ya kupyatila.
Akuna alie amini usalama wa afya ya akili ya kijana huyu, ambae jana walimkuta akiwa analinda lango la hospital hii, maana nikama alionekana analeta utani, wakati wenzake wapo kwenye shida kubwa, ya kutafuta fedha ya matibabu ya mgonjwa ambae ni mzee Sinyangwe, “Emma, nazani jana uliiona hali ya mgonjwa, kwa hiyo hapa atuna muda wa utani, tunachoitaji ni namna ya kupata fedha, ya matibabu” alisema mzee Mdemu, kwa sauti tulivu yenye tahadhari na kumaanisha anacho kisema, huku bado wanamtazama Emmanuel, wenye simu mkononi, kama vile anatafuja kitu flani, “ewaaaa, hii hapa ebu tazama” alisema Emanuel, huku anawaonyesha kitu kwenye simu, wakanza kumwonyesha, alikuwa ni mzee Mdemu, ambae alitazama juu ya simu, alafu ghafla akamtazama Anna, kama vile anamlahumu kwa kuwaficha kitu.
“vipi mzee mdemu, mbona..?” aliuliza mama Anna, ambae akuweza kumaliza swali lake, na kumtazama Emmanuel kwa lengo la kuitaji kuona kile ambacho mzee Mdemu amekiona kwenye simu ya kijana huyo, lakini Anna ndie alikuwa amesha muwai, maana yeye aliichukuwa simu yenye toka mikononi mwa kijana huyo, ambae wanamfahau toka siku nyingi sana, huko kijijini kwao Malangari.
Mama Ariana, aliweza kumwona binti yake, alie kuwa anaitazama simu ya Emanuel, akiwa ametoa macho kwa mshangao, huku mdomo wake ukiachana kwa butwaha lenye mchanganyiko wa furaha nakuto amini. “kumbe Masoud alisema kweli” mama Anna alimsikia binti yake akisema kwa sauti ya chini, kama ya kunong’ona, iliyoonyesha mshangao wa furaha, wawazi kabisa….…. endelea….
SEHEMU YA ISHILINI NA TANO
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA NNE: Mama Ariana, aliweza kumwona binti yake, alie kuwa anaitazama simu ya Emanuel, akiwa ametoa macho kwa mshangao, huku mdomo wake ukiachana kwa butwaha lenye mchanganyiko wa furaha nakuto amini. “kumbe Masoud alisema kweli” mama Anna alimsikia binti yake akisema kwa sauti ya chini, kama ya kunong’ona, iliyoonyesha mshangao wa furaha, wawazi kabisa….…. endelea….
kuona hivyo mama Ana nae akutaka kubakia nyumba, akasogelea simu ambayo sasa ilikuwa mikononi kwa binti yake Anna, “lakini alichelewa maana Anna ndio kwanza ananyoosha mkono wake kumpatia Emmanuel simu yake, “mmena, Masoud ni boss sikuizi, anakaa Sinza” alisisitiza Emmanuel, na hapo mama Anna akaiona isiwe tabu, “mbona mtazama peke yenu” alisema mama Anna sambamba na kuikwapua simu ya Emanuel toka mkononi mwake, na kutazama kwenye kioo, hapo kwa macho yake aliiona picha ya, kijana mtashati alie kaa kwenye makochi makubwa na mazuri, huku ndani ya chumba hicho ambacho kina mtazamo wa sebule, kilionekana kuwa vitu vya thamani, na vyakupendeza.
Hapo mama Anna,a akamtazama binti yake, kwa mach ya mshangao, “hivi Anna unalifahamu kama Masoud amemaliza chu na kupaa kazi, mbona unasema kuwa alisema ukweli?” aliuliza mama Anna kwa sauti ya chini yenye mshangao na hasira kidogo, “hapana mama, ila alisema akimaliza chuo ataandaa maisha kisha atakuja kutuchukuwa, tukaishi nae Dar” alisema Anna kwa sauti iliyojaa furaha kubwa.
Furaha ambayo iliambukiza kila mtu, pamoja na mzee Mdemu,na mama Anna, “kama ni hivyo basi itakuwa vyema uwasiliane nae, ili kusaidie hiyo fedha ya matibabu” alisema mzee Mdemu, ambae alikuwa amesha tanguliwa na Anna, ambae alikuwa amesha toa simu yake, na kuanza kupekuwa namba za simu za Msoud, na kupiga, lakini ile anapiga tu, akasikia “uwezi kupiga simu hii, ongeza salio kisha jaribu tena” hapo Anna akamtazama Emmanuel, “sina salio, nikupe namba yake umpigie” aikuwa na na kujiuliza mala mbili, Emmanuel akajibu, “nina namba yake, niliongea nae jana usiku, twende hapo nje tuka mpigie” alisema Emmanuel, huku anaongoza kuelekea nje ya jengo lile la vipimo.*******
Naam kijijini Malangari, habari iliyokuwa imesambaa ni juu ya hali mbaya ya mzee Sinyangwe, na jinsi alivyokosa msaada wa usafiri toka kwa mzee Kizinge, ambae ni mkwe mwenza, “lakini wanchofanya ni kitu kibaya sana, yani anawezaje kumnyima usafiri mtu ambae wanaenda kuoa kwake” alisema mtu mmoja, katika maongezi ya juu ya jambo ilo, “isitoshe kaka wao ndio walio msomesha kijana wa Kizinge” alisema mwingine.
Naam upande wa pili mzee Mwaisaka, ambae ni mmoja kati ya watu, walio pata taarifa ya kuugua na kukimbizwa Hospital kwa mzee Sinyangwe, alimpitia rafiki yake bwana Sanga, ambapo walikubariana kuacha shughuri zao zote za siku ile, na kuelekea mafinga mjini, wakawaone mzee mwenzao.
Lakini kabla awajaanza safari, wakaona itakuwa vyema na busara, kama watapitia nyumbani kwa mzee Kizinge, kwakujuwa kuwa ni mkwe mwenza wa mzee Sinyangwe, wakajuwe kama aliambatana na mgonjwa jana usiku, na kama siyo basi lazima angeitaji kuongozana nao.
Kweli mawazo yao yalikuwa sawa kabisa, maana walimkuta bwana Kizinge amesimama uwani anapiga mswaki karibu na mfeleji, uliojaa matembele yaliyo stawi vyema, huku kikombe chake cha maji kikiwa mkononi, hivyo wakaona wasimsemeshe kwanza, kutokana kuwa bado alikuwa povu la mswaki mdomoni, “habari za leo shemeji” alisalimia bwana Sanga, mala baada ya mke wa Kizinge kuibuka pale uwani, akitkea nani ya nyumba kubwa, “salama tu shemeji karibuni” alisema mama Masoud, huku anaelekea kwenye upande wa jiko la nje, “asante shemeji poleni kwa mgonjwa” safari hii alisema mzee Mwaisaka.
Hapo mama Msoud akasimama ghafla na kuwatazama wawili awa, “mgonjwa?” aliuliza mama Masoud, kwa sauti ya mshangao, huku macho yame mtoka kweli kweli, kiasi cha kuwafanya wakina wakina mzee Sanga nao wamshangae mwanamama huyu, “inamaana amjasikia kuwa mzee Sinyangwe amepelekwa Mafinga, hali yake ni mbaya” aliuliza mzee Mwaisaka, kwa sauti ya mshangao.
Hapo mama Masoud akashusha pumzi ndefu, ya afadhari, “mwe menitisha, kumbe mnamzungumzia mzee Sinyangwe, poleni na nyie” alisema mama Masoud huku anaendelea na safari yake, ya kwenda jikoni.
Hakika iliwashangaza sana, wakina mzee Sanga, kwa aina ya ujibuji wa mama Msoud, pale anapo pewa taarifa ya mtu wake wakaribu kama mzee huyo, ambae kijiji kizima kinafahamu juu ya mausiano yao, ya kifamilia, kwamba kijana wao Masoud, ana ausiano yenye malengo makubwa yabaadae, mausiano ambayo yalikuwa mfano pale kijijini Malangari, japo baadae Masou alianza kuonyesha tabia mbaya.
“asante sisi ndio tumepitia bwana Kizinge, twende mafinga tukamwone mgonjwa, alisema mzee Sanga, ambae anfahamu juu ya ukodishaji wa shamba wa mzee Sinyangwe, ilikupatikana fedha ya kumpeleka Masoud masomoni, yani Chuo kikuu kama walivyo aminishwa na kijana huyo akishirikiana na baba yake, ambae pia alikuwa anaamini hivyo, “ukisikia unafiki ndio huo” alisema Mzee Kizinge huku nageuka kuwatazama wakina mzee Sanga, ambao walitoa macho kwa mshangao, ambapo waliweza kumwona Kizinge, akiwa ameshika mswaki kwa mkon wa kulia, kikombe mkono wa kushoto, povu la dawa ya mswaki, ikiwa imejaa mdomoni, na kuchefua machoni pa kila mtu. ….
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Write your comment