Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Jumamosi, 8 Machi 2025

Ukimaliza Funika 26_27


 


SEHEMU YA ISHILINI NA SITA


ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA TANO: likupatikana fedha ya kumpeleka Masoud masomoni, yani Chuo kikuu kama walivyo aminishwa na kijana huyo akishirikiana na baba yake, ambae pia alikuwa anaamini hivyo, “ukisikia unafiki ndio huo” alisema Mze Kizinge huku nageuka kuwatazama wakina mzee Sanga, ambao walitoa macho kwa mshangao, ambapo waliweza kumwona Kizinge, akiwa ameshika mswaki kwa mkon wa kulia, kikombe mkono wa kushoto, povu la dawa ya mswaki, ikiwa imejaa mdomoni, na kuchefua machoni pa kila mtu. ….…. endelea….


Wakati wakina Mzee Mwaisaka, wakiwa wanashangaa, kauri ya Kizinge, na awajajibu lolote, wakamwona mzee Kisnge anatema povu, na kuwatazama tena, “nani amewaambia bila mimi amuwezi kwenda mafinga, na kwataarifa yenu sasa, bora mtulie hapa kijijini, na izo nauri zenu, mtumieni huyo jamaa yenu, ili zimsaidie, maana huko aliko sijuwi kama anafedha yoyote ya kulipia ata dawa ya kutuliza maumivu” alisema mzee Kizinge, kwa sauti iliyojaa jazbam, huku mdomo wake ulio jaa povu, ukirusha chembe chembe za dawa ya mswaki, na kama kuna mvua inanyesha, hakika ilichefua sana, “tena siyo kitendo cha kiungwana.


Hapo wazee awa wageni wawili walitazamana kwa macho yenye kugubikwa na mshangao, hasira na fadhaha, “bila shaka utakuwa unaania kama ilivyo kawaida yako, ebu jiandae twende mafinga tuka mwone Sinyangwe” alisema mzee Sanga, huku anajaribu kujichekesha kidogo, “shemeji kwani lazima muende na mume wangu, nyie mnaweza kwenda tu mtatuambia gonjwa anaendeleaje” alisisitiza mama Masoud, ambae alikuwa anatoka jikoni na kuelekea nyumba kubwa, akiwaacha wale wazee wawili wanamsindikiza kwa macho yenye kupigwa na butwaha, mpaka alipotokmea nani na kuingia jikoni, ambako kulikuwa na vyombo vichafu vya jana usiku, ambavyo kikawaiada uwa vinamsubiri Arianna kuja kuviosha.


Kiwa jikoni mama Masoud aliweza kusikia vyema maongezi ya wanaume watatu huko nje, “hivi Kisinge kijana wako si anatarajia kumuowa binti wa Sinyangwe?” aliuliza Mwaisaka, kwa sauti tulivu, ambayo aikuwa na dalili yoyote ya kubembeleza au utani, “nani alisema ule ulikuwa ni urafiki wa utotoni tu, aimaanishi kwamba wataowana” alisesema Kizinge, kisha akabugia maji na kusukutua, alafu akayatema kwa nguvu, ptuuu!, “kizinge, kumbuka kuwa Sinyangwe ni baba Anna, mschana ambae tunafahamu mchango wake kwenye Elimu ya Masoud, uwezi kufanyia hivi asa katika kupindi iki kigumu kwake na kwa familia yake” alisema mzee Sanga, safari hii kwa sauti yenye msisitizo,


Hapo kikasikika kicheko kikali toka jikoni, kwa mama Masoud, “umeona baba Masoud, yani wanavyosisitiza uo uchumba, utazani tulisha peleka barua, itakuwa wamesha sikia asoud amesha pata kazi, na sasa akija na gari lake sindio watasema walisha funga ndoa” alisema mama Masoud, huku akimaliza kwa kicheko cha kupayuka, akisaidiwa na mume wake.


Safari hii, aikuwashangaza wakina mzee Sanga, ila walichukizwa sana, “Kizinge, kwa hili unalolifanya, nahakika malipo yake yapo karibu” alisema mzee Sanga, kisha akamtazama mwenzie, “kaka twende zetu, tunapoteza muda hapa” hapo awakupoteza ata dakika wakaanza kutembea kuzitafuta kilomita zaidi ya kumi kuelekea barabarani ambako wangepata usafari wa kuelekea mafinga, huku vichwani mwao wakimsikitikia bwana Kizinge na familia yake.********


Naam mida hii wapenzi wawili, ambao penzi la lilikuwa limeshamili na kunawili, kama uwa la kondeni, yani Salma na Masoud, walikuwa wamekaa kwenye mhagawa wa jilani na kiwanda wanachofanyia kazi, wakipata soup ya bata mzinga, “baby kesho ni jumamosi, tutafute sehemu ya kwenda kujirusha?” aliuliza Salma, kwa sauti ya kudeka, “nakusikiliza wewe tu mpenzi wangu” alisema Masoud, na wakati huo huo simu yake ikaanza kuita, akaitoa haraka mfukoni, na kuitazama, akaona ni namba ngeni, akaipokea mala moja, “hello” aliita Masoud, kwa sauti flani hivi, ambayo ilificha ata rafudhi yake ya kihehe, hallow ni mimi Emma, nipo na Anna wamemleta baba yake Hospita hapa Mafinga” ilisikika sauti, iliyochangaka, toka upande wapili wasimu, “hooo! Emma ebu subiri kidogo, nipigie baadae kidogo, sasa hii nipo busy” alisema Masoud, akiwa na lengo la kukata simu, “sikia Emma, ongea kwanza na Anna, huyu hapa” alisikika Emmanuel akingea kwa msisitizo, na kabla Masoud ajajibu lolote, akasikia sauti ya Anna, “hallow Masoud mbona ujaniambia kama umepata kazi…” ukweli Masoud akusubiri zaidi, “ok! tutaongea baadae, sasa nipo busy kidogo” alisema Masoud na kukata simu, kisha akaiminya moja kwa moja kutufe cha kuzimia simu, mpaka simu ilipozimika kabisa.


Muda wote salma alikuwa anamtazama tu, “nani huyo Masoud?” aliuliza Salma mala tu baada ya masoud kukata simu, “ni Anna, yule mwanamke niliewai kukusimuliaga” amemfwata rafiki yangu na kuomba anipigie simu” alisema Masoud, huku anaweka simu mfukoni, “kwanini ukutaka kumsikiliza sasa” aliuliza Salma, likiwa swali la mtego, “unazani kuna kitu nimebakiza kwake, sina inshu nae kabisa, yeye si alijifanya mjanja” alisema Masoud, ambae kama ukimsiliza ungejuwa anachosema ni ukweli mtupu. ….…. endelea…. kufwatilia mkasa huu, 



SEHEMU YA ISHILINI NA SABA


ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA SITA: Muda wote salma alikuwa anamtazama tu, “nani huyo Masoud?” aliuliza Salma mala tu baada ya masoud kukata simu, “ni Anna, yule mwanamke niliewai kukusimuliaga” amemfwata rafiki yangu na kuomba anipigie simu” alisema Masoud, huku anaweka simu mfukoni, “kwanini ukutaka kumsikiliza sasa” aliuliza Salma, likiwa swali la mtego, “unazani kuna kitu nimebakiza kwake, sina inshu nae kabisa, yeye si alijifanya mjanja” alisema Masoud, ambae kama ukimsiliza ungejuwa anachosema ni ukweli mtupu. ….…. endelea….


Salma alicheka kwa furaha, huku anamlisha Masou kipane cha chapatti, hakika awakujuwa kuwa kuna mtu yupo mle ndani anawarecord video fupi fupi zisizo zidi dakika moja.******


Taarifa ya tabia za Salma, ambae anatarajia kuwa mkwe wake, zilimshtua sana mama Masoud, hakika alimuamini sana mschana huyo, na kuzania kuwa atakuwa mke bora kwa mwanae wapekee Sebastian, sasa hiki alicho kisikia kwa mume wake, ambae anadai ameshuhudia kwa macho yake, kwamba mschana huyo, mwenye mwonekano wa mwanamke anafaa kuwekwa ndani na kuwa mke wa mtu, kwamba anashiriki mapenzi na mwanaume mwingine, tena akitumia fedha za kijana wao, ambae anaheshimu kila sarafu moja anayo itafuta kwa jasho lake, kumpangia chumba, na kumnunulia vilevi.


“Yani mwanamke yule anajifanya amemlea binti yake kwa maadiri mema, kumbe ni wauni wakubwa” aliwaza mama Sebastian, ambae siyo kwamba alikuwa anawaza juu ta udanganyifu wa Salma na shangazi yake, pia alikuwa anawaza mwanae Seba, anaipkeaje taarifa ile, je atakubariana na ukweli na kumwacha Salma, au nio kipenda choroho, na ukichukuliwa Seba alisha onyesha upendo wawazi na wa hali ya juu kabisa, kwa mschana huyo mwenye mwonekano wa gome la gogo hozo, kwamba nje zuri nani lina funza.


Alisha mpatia nafasi nzuri kwenye kiwanda chake, huku akimpatia mshara mzuri, alisha patia mpangia nyumba na kumpatia kila kitu, pamoja gari nguo na upendo wa hali ya juu, na akizingaia kuwa kijana wake huyo akuwa na majaribio mengi katika maswala ya mapenzi, nikutokana kuto kushiriki mapenzi mala kwa mala, muda mwingi akiwa anaangaika na kazi kazi zake pamoja biashara zake na za familia, “hapana lazima nifanye kitu, aiwezekani mwanangu amuoe huyo binti mshenzi” aliwaza mama Sebastian, yani mke wa mzee Kiguru, ambae alikuwa anafahamu fika kuwa kijana wake anaingia Dar es salaam usiku ule, akitokea nchini japan, na kwamba siku inayofwata ya ijumaa ingeanyika afla ya kushitukiza, yenye malengo mawili makubwa.


Moja ikiwa ni kutangaza kuanza kwa vikao vya harusi yao, pamoja na kumpa nafasi Salma ya kuanza maandalizi ya send off yake, pili ni kuzindua, na kumwonyesha mchumba wake, nyumba ambayo wangeishi baada ya ndoa, pamoja na kumkabidhi gari aina jingine jipya ambalo angelitumia kama gari lake binafsi, baada ya yalile dogo analo litumia sasa.*******


Naaaam, Emma alijaribu kurudia mala kadhaa kupiga simu ya Masoud, lakini jibu lilikuwa ni moja tu, kwamba aipatikani, hali iyo iliwashtua wote, na kuwashangaza sana, kasoro Anna ambae alimini kuwa inaweza kuwa ni tatizo la kitandao, kama ambavyo inakuwaga kule kijijini, tofauti na wenzake ambao walisha gundua kuwa kuwa simu imezimwa makusudi.


Ukweli baada ya kuona picha ya Masoud kupitia simu ya Emanuel, picha ambayo ilionyesha vyema jinsi kijana huyo alivyo na maisha mazuri, kutokana na kazi aliyo nayo, kila mmoja ilimgusa kwa namna yake, ukiachilia Emma mwenyewe ambae bado alikuwa anajiuliza imekuwaje, Ana na familia yake awajuwi kuhusu maisha mapya na kazi ya Masoud, na nikweli awakuwa wanatania, hii ni kutokana na mwonekano wa Ariana, amae ndie mchumba wa kijana Masoud, maana alikuwa amevaa nguo chakavu, viatu avieleweki ata sura yake ilionyesha kuwa katika maisha yale yale magumu, ambayo alimwacha nayo, usingewaza au kuzani kuwa mschana huyu, alikuwa na umri usiozidi miaka 23, yani alichakaa kiasi cha kuficha uzuri wake wahasiri.


Huku mama Anna akiwa anaumia rohoni kwa kuona kuwa, licha ya yote ambayo binti yake na familia yake, wamemfanyia Masoud, lakini yeye na familia yake, anawezaje kuficha, juu ya maisha yake mapya ya mafanikio, huku wao wakiishi katika hali ngumu ya ufukara, wakishindwa ata kukodisha mashamba yao, ambayo walisha ya kodisha hapo mapema, kwaajili ya kulipia gharama za masomo za kijana huyo, hakika mama Anna aliona wazi jinsi binti yake alivyo achwa kwenye mataa na kijana huyo mhuni asie na huruma wala mapenzi ya kweli kwa binti yake Ariana. ….…. endelea…

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu