SEHEMU YA ALOBAINI NA MOJA
ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI: Muda mfupi baadae safari ilianza, Anna akiwa amekaa seat ya karibu lkabisa na mlango, baada ya gari kuondoka pale stendi, Anna akatoa simu yake na kumpigia, mzee Mdemu, lakini simu aikuita, baada yake akasikia sauti ya mwanamke, “aina salio la kutosha kupiga simu hii, tafahari ongeza salio na ujaribu tena” hapo Anna akakumbuka kuwa alikuwa ameshiwa muda wa maongezi….endelea….
kwamaana ya dakika alizo zipata baada ya kujiunga kifurushi, ila akakumbuka kuwa lazima atakuwa na sms, hivyo akaanza kuandika ujumbe kwenda kwa mzee Mdemu, ikiwa ni taarifa kwenda mama yake.
Lakini uwezi amini, kwamba, licha ya kuandika na kufuta akirudia mala kadhaa, lakini akuweza kupata neno la kumweleza mama yake akaelewa kile kilicho tokea kule dar, na mwisho wake akaghairi kuandika meseji, na kutulia kidogo akitafakari, ukweli alitamani kama Masoud angekuwa mbele yake, akimweleza kitu, lakini tayari alisha kuwa mbali na yeye, ata hivyo Anna akapata wazo la kumtumia ujumbe.
Anna aliafuta namba ya Masoud, na kuanza kuandika ujumbe, “Masoud, najuwa wewe ni wangu, na unajuwa kuwa sina mwanaume mwingine zaidi yako, kuhusu kile kilichotokea, pengine umeteleza kwa bahati mbaya ila nimesha kusamehe, nakumba ukumbuke mipango yetu ya zamani” kisha akaituma kwena Masoud, na kabla ajafika ata maeneo ya kibamba tayari jibu lilikuwa limesha rudi, “kwa hiyo sasa kaa auna mwanaume mwingine, unazani mimi ndio na wezakuwa na mwanamke mchafu, tena onda mawazo hayo kabisa, na usije ukajaribu kuja tena ofisini kwangu, kule kijijini kuna wanaume wengi wanao kufaa, mafute mmoja uwe nae, mimi siyo wa kuwa na mwanamke kama wewe” ujumbe huo ulizidi kumtia uchungu Ariana, ambae alifikia hatua ya kujilahumu kwa kutuma ujumbe kwa Masoud, sasa Anna alishindwa kuzuwia machozi yake na kilio cha kwikwi, ambacho kilionekana wazi wazi kwa abiria wenzake.
Ukweli Anna sasa aliamini kuwa Masoud anachokisema ni kitu cha kweli kabisa, kwamba sasa asinghe mwitaji tena, kama amefikia atua ya kumweleza kuwa anaweza kutafuta mpenzi mwanaume mwingine, kitu ambacho ata watu walioachana awawezi kufanya kwa walio waacha.
Ana kwa kulijuwa ilo, akachukuwa simu yake na kuanza kuandika ujumbe mwingine, kwenda kwa Masoud.********
Kijana Sebastia toka wakati ule ametoka kushuhudia tukio la kuumiza pale kiwandani, kwenye kiwanda ambacho alikifungua yeye mwenyewe, kwa lengo la kuboresha maisha yake, kiwanda ambacho alimweka mwanamke ambae aliamini ndie mke wake mtarajiwa, leo niwazi juhudi zake za uwekezaji katika biashara ya thamani za majumbani, inatumika kulea na kufanyia ngono.
Alienda moja kwa moja kwenye ofisi za benk ya biashara, ambako alipata huduma aliyo hiitaji, na baadae akaenda kwenye benk ya Dar es salaam, ambako alipata huduma, aliyo iitaji, na baada ya kujilizisha, akatoka na kuelekea nyumbani kwake, Mikocheni, ambako licha ya kuwa na kila kitu, lakini bado alikuwa ajaamia, alipofika pale aliwakuta wafanyakazi wake wanaanaa vyakula ambavyo, vilipangwa kutumika kwenye afla iliyopangwa kufanyika jioni ya siku ile, kwaajili ya kuzindia ile nyumba na kutangaza rathmi, kuanza kwa maandalizi ya kufunga ndioa.
Sebastian, aliwaeleza wafanyakazi, wake kwamba akutakuwa na tafrija yoyote, na kwamba viandaliwe vyakula vya wastani, kwaajili yao na yeye pia angekuwepo pale nyumbani, kwa siku tatu na pengine zaidi, akaagiza vinywaji zaidi, zikiwepo wine, maana alisema anaitaji kutumia muda mwingi, wa kutulia akinywa wine.
Lakini wakati anatoa maagizo hayo, mala ghafla nikama alikumbuka jambo, na ghafla akatoka nje na kuchukuwa funguo ya gari lake, kisha akatoka nje, na kuingia kwenye gari, akaliwasha na kuonoka zake.*******
Mida hii Masoud alikuwa getoni kwake, anatazama TV, huku anakunywa bia, simu mkononi anachart na mpenzi wake Salma, ambae mida ile kama kawaida yao alikuwa nyumbani kwao, na ndio wakati ambao alikuwa amepokea sms toka kwa Anna, na kuijibu kwa mtindo wa mwanaukome, maana alimini kuwa Anna asinge msogelea tena, na angeendelea na maisha yake baada ya kukubari matokeo, kuwa yeye Masou sasa ni matawi ya juu, na kwamba awezi kuwa na mwanamke wa hovyo kaa yeye Anna.
Nikweli, dakika chache baadae ukaingia ujumbe toka kwa Anna, ujumbe ambao ulionyesha wazi kukata taaa kwa Anna, na kwamba amekubari kuwa sasa Masoud soyo matawi yake, “nikweli Masoud, wewe ni mwanaume mzuri, mwenye kila kitu, lakini kumbuka kuwa fedha nguo na uzuri wangu nimeutoa sadaka katika Elimu yako, nakutakia maisha mema, ila nakuombea kwa mungu nisikumbuke kila nilicho kufanyia mimi na familia yangu” ulikuwa ni ujumbe mrefu, sijuwi kama unachekesha kwako msomaji, kama ulivyo mchekesha Masoud…….endelea….
Tusaidie ku Share hadithi hii Kwa watu wako
JibuFutaShare hadithi hii Kwa watu wako
JibuFuta