Kalibu storyline hapa utaweza kusoma hadithi kutoka kwa waandishi mbalimbali bure bila malipo yoyote. Alika marafiki zako tufurahi kwa pamoja

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Jumapili, 18 Mei 2025

Hadithi: A CROWN OF BADNESS EP 11-15


Mpya


TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 11.

Huku upande wa pili Jacob naye alikuwa anajipanga na anaanda mbinu mbalimbali namna ya kuzirudisha mali zake mikononi mwake tena.

Basi maisha yaliendelea kwa Jacob, na Jacob maisha yake yalikuwa magumu maana alikuwa anaishi kwa kujificha muda wote, na kibaya zaidi hakuwa hata na pesa ya kujikimu maana mara nyingi alisaidiwa na Fatuma, japo Fatuma naye hali yake ya kiuchumi haikuwa nzuri kivile.

Siku moja Jacob akiwa katulia kwenye makazi yake ya kujificha ambapo ilikuwa ni ile nyumba ya Mr Jomo, alisikia mlango unagongwa nje, baada ya kusikia mtu anagonga nje Jacob alishituka maana ilikuwa hiyo nyumba hakuna mtu ambaye amewahi kuja zaidi ya Fatuma, na mara nyingi Fatuma alikuwa kabla hajafika anatoa taarifa kwamba anakuja, sasa Jacob hakuelewa ni nani anagonga mlango kwa muda huo.
Mdogo mdogo Jacob alinyanyuka kwenda mlangoni kusikilizia kwamba nani anagonga mlango, alipo fika mlangoni alikaa kimya kusikiliza, ila bado mtu huyo aliendelea kugonga mlango.
Jacob alijikaza kiume aliamua kufungua mlango, ile anafungua alikutana na mtoto wa kike mwenye sura nzuri ya kiarabu ni hatari, Jacob alipo muona alibaki ameachama maana tangu azaliwe alikuwa hajawahi kukutana na msichana mrembo kama huyo.

"Karibu mrembo" Jacob baada ya kufungua mlango alimkaribisha mrembo huyo huku akiwa anatabasamu na meno yake yote nje.
"Nimefata mzigo wangu" yule mrembo aliongea kwa ukauzu na ilionekana hataki masihara hata kidogo.
"Heeeee!! Mzigo tena!! Mzigo gani??!!" Jacob aliuliza kwa mshangao maana alikuwa haelewi kile kitu huyo mrembo anazungumzia.

Yule mrembo hakutaka maneno mengi, moja kwa moja alizama hadi ndani bila hata kukaribishwa na alipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani.
Jacob alikuwa haelewi kinachoendelea ila kwa akili yake ya kawaida alihisi labda yule ni mtu wake na Mr jomo na amekuja kumcheki Jomo, ila maswali mengi yalikuwa yanakuja kama ni mtu wake Jomo kwa nini anidai mimi hiyo mizigo yake, Jacob hakupata jibu aliamua kuzama huko huko chumbani kumfuata.

Alipo ingia chumbani alishangaa kumuona yule mrembo amefungua kimlango kimoja cha siri ambacho Jacob hakuwahi kugundua kama kipo humo ndani licha ya kuishi miezi zaidi ya saba kwenye nyumba hiyo na hicho kimlango kilikuwa nyuma ya kabati yaani ilikuwa ukigeuza kabati unakutana na mlango wa siri na hiyo Sehemu ilikuwa tofauti na ile aliyo elekezwagwa Fatuma kipindi cha nyuma kuja kuchukua pesa.
Jacob alizidi kushangaa yule mrembo na kujiuliza yule ni nani mpaka anafahamu milango ya siri kwenye nyumba hiyo.
Basi yule mrembo aliingia kwenye kachumba hako ka siri ambako kalikuwa kadogo mno na alipoingia alianza kutafuta kitu, Jacob yeye alikuwa kasimama mlangoni anashuhudia nini kitatokea.
Yule mrembo baada ya kupata kitu chake alirudisha ule mlango na kuliweka kabati kama lilivyo kuwa mwanzo
"Hiki ndo kitu changu nilikuwa nakitafuta! Na nakuonya acha hiyo tabia maana kitu unacho kitafuta kipo njiani kinakuja na ushukuru mimi nina huruma" yule mrembo aliongea maneno ambayo Jacob hakuelewa na alimuonesha kitu ambacho yeye alikuwa anadai apewe kama mzigo wake, hicho kitu kilikuwa ni kitana kidogo cha kuchania nywele.
"Dada nini kinaendelea kwani mi unanijua? Mbona sikuelewa?" Jacob bado alikuwa hamuelewi yule mrembo nini anamanisha

"Sikujui na sina haja ya kukujua na wewe pia huna haja ya kunijua ila ukijikoki tena kwenye mstari wangu hapo utanijua mimi nani" yule mrembo aliongea na awamu hii alikuwa anaongea huku anatabasamu na urembo wake ulikuwa unajizihirisha hadharani.

Kutokana na urembo wa yule mtoto wa kike na lile tabasamu lake Jacob alijikuta mapigo ya moyo yanaanza kwenda mbio na alikuwa haelewi shida nini na aliacha kufikiria maneno tatanishi ya yule mrembo alianza kufikiria mambo mengine ya kiutu uzima na mawazo yalienda mbali mno alijikuta anakumbuka mpenzi wake Vicky.

Jacob akiwa anamshnga yule mrembo pale chumbani na ule urembo wake wa asili alishangaa kumuona yule dada anaanza kuvua nguo moja baada ya nyingine palepale chumbani, hapo Jacob mapigo ya moyo yalianza kwenda mara mia zaidi.
Yule mrembo akiwa anatabasamu aliendelea kusaula nguo hatimaye alibakiwa na kichupi tu, yaani vitu vyote vilikuwa hadharani peupe, hapo Jacob alijikuta anaanza kupata shida ya kiutu uzima maana suruali yake ilikuwa imetuna ni hatari na ukichukulia na hajawahi kucheza mechi muda mrefu.
Ila Jacob akiwa anawaza kwamba yule mrembo labda anataka kumtunuku na kumpa utamu, alishanga kumuona yule mrembo anachuku kile kitana chake na kuanza kuchana nywele zake za kichwani na alipo maliza kuna maneno aliyaongea kama mtu anayepiga dua.

Baada ya kumaliza yule mrembo alianza kuchukua nguo moja moja kwa ajiri ya kuvaa.

"Dada naomba nisaide japo kidogo naumia mwenzako". Jacob uvumilivu ulimshinda alijikuta anaomba mechi ya kirafiki japo alikuwa hamfahamu huyo mrembo katokea wapi na Jacob muda huo anaomba mechi alikuwa ashaanza kusaula nguo zake maana hisia zake zilikuwa zipo kiwango cha juu sana.

Baada ya kuongea maneno hayo Jacob alishangaa kumuona yule mrembo kabadilika sura na alionekana ni mtu aliyekasirishwa na kile Jacob alichokisema

"Siyo kila chakula ni chakula vingine ni sumu" yule mrembo aliongea na kuchukua nguo zake ili avae aondoke

Kile kitendo cha kuanza kuvaa nguo tu walishituka mlango unafunguliwa kwa nguvu na aliyekuwa ameingia hapo chumbani ni Fatuma.

Je nini kitatokea? Je huyo mrembo ni nani na katoka wapi??
Na je nini kitatokea baada ya Fatuma kuingia mule ndani?

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 12



TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 12.

Kile kitendo cha kuanza kuvaa nguo tu walishituka mlango unafunguliwa kwa nguvu na aliyekuwa ameingia hapo chumbani ni Fatuma.

Baada ya Fatuma kuingia mule chumbani Jacob alishituka kumuona, hata Fatuma naye alishituka kuona kitendo kile maana aliona Jacob kavaa tu bukuta yule mrembo ndo usiseme kavaa tu kichupi na nguo zipo mkononi.

"Jamani samahani kwa kuwaingila starehe zenu". Fatuma baada ya kuona hayo aliongea na kutoka mule chumbani kwa nguvu na hasira, Jacob alijaribu kumkimbilia ili amuelezee ukweli

"Fatuma siyo hivyo! Simama basi nikwambie" Jacob alijaribu kumfuata ila Fatuma hakusimama alitokomea moja kwa moja

Jacob alirudi mule ndani na kuingia kule chumbani hakumkuta yule mrembo na hakuelewa kaenda wapi

"Daaaaa huu ujinga yaani huyu mrembo kaniharibia alafu anaondoka bila mimi kumnyadua sijui kanichukuliaje, alafu naye Fatuma anakasirika kama mimi ndo mpenzi wake!! Aaaaaa! Potelea mbali liwalo na liwe" hayo yalikuwa ni maneno ya Jacob akijiongelesha kwa hasira baada ya kuto mkuta yule mrembo pale chumbani.
"Hii nyumba itakuwa ina milango ya siri mbona sijamuona yule mrembo kule nje kutoka, na humu ndani hayumo" Jacob alianza kuangaza huku na huku kukagua nyumba hiyo vizuri maana alifikiria huyo mrembo kapita mlango gani, maana mlango anao ujua yeye, hakumuona mrembo yule kupita pale.
"Haya ndo madhara ya kuishi nyumba tusizo zijua" Jacob bado alikuwa anajisemesha mwenyewe

Basi maisha yaliendelea na siku zilikata hatimaye ulipita mwezi mzima Jacob alikuwa hajawahi kumuona Fatuma kuja pale anapoishi na hiyo haikuwa kawaida ya Fatuma.

Jacob japo kuwa alikuwa hapendi kuonekana mtaani na watu hovyo hovyo siku hiyo alijikaza kwenda kule alikopanga Fatuma kwenda kujua nini shida japo alikuwa anajua shida ni nini,
Basi kigiza kikiwa kimetanda, Jacob alifika pale anapo kaaa Fatuma aligonga lakini mlango haukufunguliwa, Jacob alizidi kugonga na kugonga baada ya kugonga sana kama lisaa lizima kuna njemba ilitoka mule ndani

"Karibu kijana, naona unagonga kwa nguvu tukusaidie nini??" Ile njemba iliuliza

"Samahani kaka angu mimi namuulizia Fatuma nimemukuta??" Jacob aliuliza kwa uoga maana ile njemba ilikuwa imejazia siyo mchezo.

"We unaulizia wanawake za watu mida hii we nani??" Jamaa aliuliza kwa ukali

"Samahani kaka sikujua kama ni mke wako" Jacob moyo uligonga shoti baada ya kusikia maneno ya ile njemba na Jacob hakutaka tena kuendelea kukaa pale aliamua kurudi home anakokaa.

Jacob akiwa njiani anarudi kwake hakuamini macho yake baada ya kumuona baba yake mkubwa Mr Derick akiwa na Vicky wanaingia kwenye hotel moja ya kifahari, Jacob alijikuta maumivu anayo yapata moyoni mwake ni Zaid ya kuchomwa na kisu alitamani awafuate akawarukie ila ndo hivyo hakuwa na uwezo.
Basi zilipita siku mbili Jacob akiwa anafanya kazi ya kulala na kulia tu mule ndani kwake na njaa ilikuwa inampiga ni hatari maana yule aliye kuwa anampa chakula ndo huyo kimeumana.
Jacob mawazo yalikuwa yanakimbia kichwani kama mwana riadha na alikuwa haelewi dunia inaendaje.
Maneno ya ile njemba kumhusu Fatuma yalikuwa yanajirudia kichwani mwa Jacob na hapo Jacob ndo aligundua kwamba kumbe kaanza kumpenda Fatuma maana ilikuwa ina muuma siyo mchezo.

Basi zilipita siku mbili nyingine Jacob akiwa ametulia zake sebuleni haelewi siku hiyo itaendaje kwake alisikia mlango unagongwa, haraka alienda kufungua mlango lakini kabla hajafungua moyo wake ulisita kufungua mlango huo.
Alitulia akiwa anaendelea kusikilizia jinsi mlango unavyogongwa, alikaa kama dakika tano kimya kilipita, aliamua kuchungulia dirishani alipo chungulia moyo wake ulianza kwenda speed ya fastjet, maana alimuona baba yake mkubwa akiwa na njemba moja wanatoka pale nyumbani.

"Duuuuuu!! Wamejua ninapo kaaa ama?? Au Fatuma kaniuza??" Jacob alianza kujiuliza maswali mengi ambayo hata hivyo hakupata majibu.

Jacob alisubiri giza liingie ili asepe maeneo hayo maana aliona ishakua ni hatari kwa usalama wake, alipanga kuondoka ila hakujua anaenda wapi.

Basi giza lilifika ilikuwa ni saa tatu usiku Jacob alikusanya kila kitu kinacho mhusu na kuondoka ila alipofungua tu mlango uso kwa uso alikutana na Fatuma mlangoni.

Huku kwa upande wa Mr Derick na wake zake yaani Vicky kama mke mdogo pamoja na Mama Jacob yule wa kurithi walikuwa wamekaa meza moja wanapata chakula.
"Yaani raha kweli siku moja moja nakaa na wake zangu kama hivi safi kweli kweli" hayo yalikuwa ni meneno ya Mr Derick akiwa anawaambia wake zake maana siku hiyo ndo ilikuwa ya kwanza yeye kukaa kwenye meza moja kula chakula na wake zake wote wawili.

"Sawa, ila Derick vipi lakini kwenye ile nyumba ya Mr jomo mligundua nani anakaa huko??" Mama Jacob aliuliza
"Aaaaaaa!! Tuligonga mlango hakuna aliyetokea tukaamua kuondoka" Mr Derick aliongea
"Duuu! Ilitakiwa tujue nani anakaa, isije ikawa ni ndugu zake na Mr jomo wamekuja kupeleleza aliyehusika na kifo cha ndugu yao" Mama Jacob aliongea kwa wasiwasi
"Sidhani kama watajua chochote, ila tutajua tu anayekaa pale maana kuna watu nishawaanda kufanya upelelezi"

Hayo yalikuwa ni mazungumzo yanayo endelea, kwa maneno hayo iligundulika kwamba bado watu hao hawajajua kama anayekaa pale ni Jacob.

Je nini kitatokea?? Je watagundua kama Jacob ndo anakaa pale??

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 13.



TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 13.

Hayo yalikuwa ni mazungumzo yanayo endelea, kwa maneno hayo iligundulika kwamba bado watu hao hawajua kama anayekaa pale ni Jacob.

Huku kwa upande wa Jacob, Jacob alipigwa na butwa baada ya kumuona Fatuma hakuamini macho yake na siku hiyo Jacob alimuona Fatuma ni mrembo kuliko siku zote ambazo amewahi kumuona naye hakujua kwa nini inakuwa vile.

"Jacob Mbona begi tena waenda wapi?" Fatuma aliuliza kwa kutahamaki
"Nahama hapa" Jacob alijibu kifupi na kwa kisirani baada ya kukumbuka maneno ya ile njemba siku ile alipo enda kwa Fatuma
"Heeee mbona unajibu kama vita? Kuhama huko vipi unaenda wapi sasa au ndo umeamua kumfuata huyo mpenzi wako huko huko" Fatuma aliongea akiwa anamanisha
"Fatuma usitake kunichanya sawa eee mi hapa nilipo kichwa changu hakifanyi kazi kwa hiyo ukiendelea kuniuliza maswali ya hovyo mwisho utakuwa mbaya" Jacob bado aliongea kwa hasira maana yeye alijua Fatuma kaja kumkejeri kwa sababu yeye tayari ana mtu wake.
"Jacob ivi wakuwa na hasira ni wewe au ni mimi?? Yaani nilikufaminia na mwanamke na wewe mwenyewe wakati ulijua fika mimi nakupenda wewe, uliona mimi sina hiyo sifa kabisa ukaamua kumchukua mwarabu, we unajua mi nimepitia hali gani mpaka kufikia leo??" Fatuma Aliongea huku mchozi ukimtoka 

"Fatuma walia nini sasa wakati una mume wako umemwacha nyumbani au ndo kutegana?" Jacob alikuwa anamshangaa Fatuma.

"Mumeeee!!" Fatuma alishanga kusikia swala la yeye kuwa na mme.

Jacob hakujibu chochote, wote walibakia kimya huku wakiwa wanatazamana usoni, Jacob alikuwa anamkodorea macho Fatuma kila sehemu ya mwili wake
"Duuuuuu kumbe Fatuma mzuri hivi" Jacob aliwaza baada ya kumwangalia Fatuma kifuani, Jacob sijui tamaa zilimutoka wapi yaani bila kuongea chochote, alimulukia Fatuma pale pale mlangoni na kuanza kumnyonya mate, fatuma alijitahidi kujitoa mikononi mwa Jacob lakini Jacob alikuwa kazamilia maana alikuwa yupo kwenye hali mbaya na ukichukulia ni muda mrefu haja cheza mechi.
Jacob alimvutia fatuma hadi sebuleni, alianza kumvua nguo na haikueleweka Jacob nguvu zimetoka wapi wakati alikuwa hajala siku nzima, 
"Jacob please naomba niachie tuzungumze kwamza" Fatuma aliongea kwa maneno ya upole maana alikuwa kazidiwa nguvu na Jacob.
Jacob hakuelewa lolote aliendelea na kazi yake, hapo ilibidi Fatuma awe mpole amuache Jacob afanye kile alicho dhamiria,
Jacob alifanikiwa kupata kile akitakacho japo kwa shida, ila Jacob alishangaa sana baada ya kukuta Fatuma bado ana usichana wake yaani ni bikira, hapo Jacob alijiona ni mkosaji mkubwa mno maana alivokuwa anamwazia Fatuma ni tofauti kabisa.

"Fatuma nisamehe, sikujua" Jacob aliongea kwa aibu maana alijua labda Fatuma ni mke wa mtu tayari na ananyaduliwa kila siku.

Fatuma hakuongea neno alichukua nguo zake na kuelekea bafuni ila akiwa ananyenyuka alishindwa kutembea kutokana na maumivu aliyokuwa anayapata.

Basi Jacob alimusaidia kumpeleka bafuni, Fatuma alioga vizuri na kuvaa nguo zake, yaani maumivu aliyokuwa anayasikia yalikuwa ni makubwa, basi Fatuma alitulia kwenye sofa maana alitamani aludi kwake ila hata kutembea alishindwa.
Jacob na fatuma walibaki kutazamana tu usoni na kuoneana aibu, Jacob alitamani akamnunulie Fatuma dawa za kupunguza maumivu muda huo ila ndo hivyo hakuwa hata na shilingi mia.
"Fatuma pole sana na nisamehe kwa yote?" Jacob alivunja ukimya

Fatuma bado alikuwa kimya na alikuwa kanuna ni hatari.

"Fatuma kwani huwezi kuwa na pesa yoyote hapo nikakununulie dawa za kutuliza maumivu hapo barabarani?" Jacob aliuliza kwa aibu maana kufanya kafanya yeye alafu pesa anataka atoe mfanyiwa inahusu, japo kuwa ilikuwa ni aibu kwa Jacob ila haikuwa na namna

"Huoni hata aibu!! Muone" Fatuma naye alivunja ukimya kwa kumpiga dongo Jacob.

Jacob aliona aibu ya mwaka, na alifikiria mbali mno yaani yeye wa kukosa hata elfu mbili ya dawa kweli! Alijikuta anamkumbuka mzee wake Mr deus na machozi yalianza kumbubujika maana hapo alipo alikuwa hajala siku nzima japo ameicheza mechi vilivyo.

"Mwanaume hovyo yaani kubakwa nimebakwa mimi alafu kulia unalia wewe?? Na unabaka alafu huna pesa we mwanaume au mwanamke??" Fatuma hakumuonea hata huruma alizidi kumurushia maneno makali.
Jacob hakuongea neno lolote alitoka pale sebuleni na kuingia chumbani.
Jacob alishika shuka huko chumbani alitamani kujinyonga ili kukwepana na mateso na aibu za dunia hii, ila alipo kumbuka jinsi mzee wake alivyo uawa kikatili alitupa shuka kitandani maana hakutaka kufa kizembe bila kulipa kisasi.

Basi Jacob alikaa kitandani na kupitiwa na usingizi mpaka asubuhi na safari ya kuhama haikuwepo tena.
Jacob alipo amuka asubuhi alienda sebuleni kumwangalia Fatuma, na alipo fika alikuta Fatuma kashapitiwa na usingizi na mapaja yake yalikuwa yamekaa wazi kabisa na ukichukulia weupe wa mapaja ya Fatuma Jacob alisahau kile alichomfanyia mwenzie usiku, alijikuta tena anapandwa na midadi sijui mashetani yalitoka wapi alijikuta anamsogelea Fatuma pale kwenye sofa alipo lala na hakutaka kuchelewa alivua nguo zake na kuanza kumvua Fatuma, ila Fatuma alishituka toka usingizini na alianza kuparangana ili kumtoa Jacob ila alishindwa
"Jacob hivi una nini we mwanaume au umerogwa?" Fatuma aliongea kwa ukali ila Jacob hakutaka kusikia.

Basi Jacob alifanya kile alichotaka na kutulia, na hakuongea neno lolote maana alikuwa ashajizila kwamba liwalo na liwe.
Ila kwa upande wa Fatuma, naye alishangaa awamu hii hakusikia sana maumivu ila kuna karaha alikapata kwa mbali japo kalichanganyikana na maumivu.

"Jacob nin unataka haswa kwangu? Fatuma aliuliza akiwa kakasirika maana alikuwa haelewi kinachoendelea kwa Jacob.

Jacob akiwa hajajibu walisikia mlango unagongwa kwa nguvu, Jacob alimnyamazisha fatuma kwa kidole maana alikuwa na wasiwasi na hao wanaogonga.
Hao watu walizidi kugonga kwa nguvu, na baada ya kuona mlango haufunguliwi walianza kuvunja mlango kwa kukanyaga.

Basi Jacob na fatuma hapo waliondoa tofauti zao ilibidi wafikirie cha kufanya na hapo iliwabidi waende wakajifiche kwenye kile chumba cha siri.

Je nini kitatokea?? Je Fatuma na Jacob watafikia wapi?

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 14.



TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 14

Basi Jacob na fatuma hapo waliondoa tofauti zao ilibidi wafikirie cha kufanya na hapo iliwabidi waende wakajifiche kwenye kile chumba cha siri.

Myoyo yao ilikuwa inaenda speed kali zaidi ya ndege za bombadia kutokana na kachumba hako kuwa kadogo walijikuta wamekumbatiana na wanahemeana ni hatari.

"Hawa wajinga watakuwa wamekimbia na inaonekana kuna siri kwa nini wakimbie sasa??" Walisikia sauti ya Mr Derick ikizungumza sebuleni baada ya akina Derick kutafuta sehemu zote na hawakuona mtu yeyote

"Sasa boss unasema kukimbia watakuwa wamekimbilia wapi wakati mlangoni hawajapita?" Jamaa mmoja aliyekuwa amebatana na Mr Derick aliuliza

"We Magingi tatizo lako akili yako nyingi inatumika kufikiria bangi kuliko vitu vya maana, we kwa akili yako ndogo nyumba ya Jambazi kama Mr jomo inaweza kosa mlango wa siri kweli??" Mr Derick Aliongea kwa kumshangaa jamaa ake ambaye alijulikana kama Magingi

"Boss Kwani lakini we unavyohisi ni akina nani watakuwa wanakaa humu??" Magingi aliuliza

"Unafikiri najua basi, ningekuwa najua si ningelipua nyumba yote wafie ndani tatizo sijui anayekaa humu na ndo nilitaka nijue sasa" Mr Derick naye kumbe alikuwa hajui anayekaa humo ndani ila wasiwasi wake ilikuwa ni kwa nini watu hao wakae kwenye nyumba ya mtu ambaye yeye ndo alihusika na kifo chake.

Basi akina Mr Derick baada ya kutogundua kitu chochote waliondoka.
Baada ya kama Nusu saa kupita akina Jacob walitoka kwenye kile chumba na walikuwa wanatoa jasho kweli kweli maana so kwa presha ile na ukizingatia na udogo wa kale kachumba.

"Jacob imekuwaje kwani hadi wanakuja hapa" Fatuma aliuliza na alikuwa amesahau kabisa kile alicho fanyiwa na Jacob masaa machache yaliyopita na maumivu hakuyasikia tena
"Dear mi mwenyewe sijui na ndo maana umenikuta nataka kuhama kuhofia hilo" Jacob naye alikuwa haelewi

Fatuma baada ya kusikia neno dear kutoka kwa Jacob mwili wake ulisisimuka ni hatari maana alikuwa hajawahi itwa neno hilo na mwanaume yeyote na ukizingatia na alivyokuwa anampenda Jacob hilo jina lilimchanganya

"Fatuma vipi mbona unaduwa kulikoni??" Jacob alishangaa kumuona Fatuma kaduwa

"Jacob hamna kuna kitu nilikuwa nawaza, ila kwa Saiz hapa tuondoke siyo salama tena" Fatuma aliongea huku akiwa ananyanyuka
"Tunaenda wapi sasa??" Jacob aliuliza
"Kwangu tunaenda"
"Kwakoooo!!!??" Jacob alishangaa kusikia eti aende nyumbani kwa Fatuma maana alikumbuka siku ile ameenda kule aliikuta njemba inavimba na kujibweda kwenye chumba cha mrembo
"Heeee!! Jacob Mbona unashituka kwani we kwenda kwangu kuna shida gani??"
"Aaaaaa! Hakuna shida ila naogopa tu"
"Waogopa nini sasa, mwanaume mzima??"
"Aaaaaa!! Naogopa wenye mali si unajua warembo kama ninyi hamksoi watu" Jacob aliongea kwa mtego
"Jacob acha Ujinga ujue, twende huko mengine tutaongea huko"

Basi Jacob alikusanya kila kinacho mhusu na walianza kuondoka, Jacob alikuwa anaogopa na alikuwa anahofia kweli maana yeye alijua Fatuma anaishi na mtu.

"Duuuuuu!! Au atakuwa ashahama mimi nilienda sehemu ambako siko" wakiwa njiani Jacob aliendelea kujiuliza maswali kimoyomoyo

Ila Jacob alishangaa kuona sehemu ni ile ile aliyoukuja siku ile, na walipo fika aliona mlango ni ule ule aliogonga.

"Fatuma kabla hatujaingia una uhakika usalama upo upande wangu?" Jacob bado alikuwa haamini
"Jacob ujue sikuelewi kwani we unatakaje?"
"Fatuma nina wasiwasi ujue, kuna siku nimekuja hapa niligonga mlango kuna njemba ilifungua ilisema wewe ni mke wake kwa hiyo napata wasiwasi"
"Ivi jana wakati unanibaka ulikuta shimo eeee?? Au huyo mwanaume alikuwa anafanya kazi ya kuniramba tu na kuniacha, tumia akili wewe, ivi kwa akili yako ni mwanaume gani anaweza lala na mwanamke na akawa anaangalia tu??" Fatuma Aliongea kama ni mtu anayetoa somo darasani

"Uuuuuuu ila kweli, mbona nilimkuta bikra sasa ile njemba ilikuwa inafanya nini siku ile na ilikuwa ni usiku??" Jacob alijiwazia wakiwa bado hawajaingia ndani

"We Jacob unawaza nini sasa acha ujinga ingia ndani, kama hutaki basi nenda unakojua wewe mwanaume gani unataka kubembelezwa" Fatuma Aliongea kwa hasira, alifungua mlango na kuingia ndani.

Je nini kitatokea?? Ile njemba aliyo ikuta siku ile ni nani ??

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 15.


TAJI LA UBAYA
   (A crown of badness)
     
Mtunzi: "Mwaki Ze Done"

Sehemu 15.

"We Jacob unawaza nini sasa acha ujinga ingia ndani, kama hutaki basi nenda unakojua wewe mwanaume gani unataka kubembelezwa" Fatuma Aliongea kwa hasira, alifungua mlango na kuingia ndani.

Jacob aliingia ndani kinyonge na alivua mzuhura wake ambao alikuwa anautumia kuziba sura yale maana alikuwa katoboa sehemu ya macho tu.

"Jacob nikuulize swali??" Fatuma alimuuliza Jacob
"Inategemeana linahusiana na nini hilo swali kama ni mambo yaliyotokea jana sitaki swali ila kama ni kuhusu mengine uliza" Jacob alijihami maana alikuwa hana jibu la kwamba kwa nini alimbaka Fatuma

"Jacob unanipenda??" Fatuma aliuliza swali hilo kifupi na alikuwa serious kweli yaani

"Ndiyo nakupenda, eheee unataka kusemaje"
"Nilitaka kujua tu kama unanipenda alafu ndo nikwambie siri zangu"
"Ndiyo nakupenda, haya nambie hizo siri"
"Jacob narudia tena kukuuliza unanipenda toka moyoni kabisa na siyo kisa una shida??" Fatuma aliuliza akiwa anamaanisha
"Fatuma we watakaje kwani si nimekwambia nakupenda??"
"Umeanza lini kunipenda?? Baada ya kukumbwa na shida au ebu fafanua??"
"Fatuma maswali sitaki kwani we hujui kwamba upendo wa kweli unazaliwa taratibu taratibu" Jacob alijibu, ila Jacob alishangaa kuona Fatuma anaanza kutetemeka gafra 
"We fatuma una nini kwani??" Jacob aliuliza huku akiwa anashangaa
Fatuma alidondoka chini na kuzima gafra, Jacob alichanganyikiwa na hakuelewa afanye nini alijaribu kumtikisa ila Fatuma hata hakuonesha dalili yoyote.
Jacob hakutaka kuchelewa alivaa Mzuhura wake na kumuweka Fatuma mgongoni ili aanze safari ya kumpeleka hospitali na alikuwa analia ni hatari
"Fatuma please usife, mumy usife!! Utapona dear ntabaki na nani mie!! Dear dear please" hayo yalikuwa maneno kutoka kwa Jacob akiwa analia.

Baada ya Jacob kumbeba Fatuma ili kumpeleka hospitali alipofika tu nje alisikia mtu anacheka mgongoni.
"We mjinga unanipeleka wapi sasa" Fatuma Aliongea akiwa anacheka kweli kweli

"Ehuuuuuu utaniuwa fatuma ujue" Jacob alimshusha na kupumua kwa nguvu
"Tuingie ndani tuzungumze sasa maana nimegundua una kaupendo ka dhati kwa mbaaaliiii siyo sana lakini" Fatuma aliongea akiwa anacheka
"Acha ujinga yaani huko ndo kupimana upendo au siyo??"
"Bana we twende ndani tuzungumze nina mengi ya kukwambia"
"Fatuma pamoja na hayo mazoea ya hivyo mi sitaki kabisa, na utani mi sijuagi kabisa"Jacob aliongea akiwa kakasirika.
Basi waliingia ndani na kukaa, walitulia kama dakika mbili hivi.

"Sasa si uongee hayo uliyo sema ni mengi??" Jacob alikuwa anasubiri kuambiwa kile alicho ahidiwa kuambiwa.

Fatuma alikaa kimya kama dakika moja na sura yake ilionekana ipo serious na mambo ambayo anataka kuongea.

"Jacob mi nakupenda zaidi ya nijipendavyo, nakupenda mno Jacob ila kwa upande wako sijui ipoje, ila kitu ambacho nakulaumu na kukusikitikia ni kuningilia kimwili bila kujua historia yangu wala kuniju mimi vizuri, na kama umenipenda kwa dhati na utaendelea kunipenda kwa dhati hiyo haitakuwa na madhara makubwa, ila tatizo litakuja pale ambapo wewe umenipenda kwa Saiz kisa wewe una matatizo, na ndo maana nimekuuliza mara mbili mbili kama wanipenda kweli,
Jacob mimi hapa nilipo nilizaliwa kwenye familia ambayo inatokana na uchifu na kwenye huo uko wetu kuliuwa na mila na tamaduni baada ya mtoto wa kike kuzaliwa na mojawapo ya utamaduni mkubwa kwa mtoto wa kike yeyote aliye zaliwa kwenye ukoo huo ni kwamba hataruhusiwa kufanya mapenzi mpaka pale atakapo olewa rasmi, na watu kushuhudia ndoa hiyo, na ikitokea amefanya mapenzi kabla ya ndoa huyo mwanaume ambaye atafanya naye mapenzi inatakiwa asije akashiriki mapenzi na msichana mwingine yeyote zaidi ya huyo, na vivo hivyo kwa msichana hataruhusiwa kufanya mapenzi na mwanaume yeyote zaidi ya huyo" Fatuma alizidi kusimulia

"Eeeee!! Wamanisha nini fatuma kwani tamaduni zenu zinawahusu watu wote?" Jacob alidakia kabla hata Fatuma hajamaliza maana aliona hilo swala kwake litakuwa gumu eti hakuna kufanya mapenzi na mwanamke mwingine zaidi ya Fatuma yaani kitu hicho kwa Jacob kilionekana ni hakiwezekani

"Jacob unashituka nini na umeyataka mwenyewe?? Alafu mbona unanikatisha wakati sijamaliza kukuelezea au unajua kwamba ukifanya nini kitatokea??" Fatuma alimshangaa Jacob kushituka

"Eheee ebu malizia kwanza huo ujinga wa mila Zenu kwamba kwa mfano nisipotekeleza nini kitatokea??" Jacob alikuwa haamini maneno ya Fatuma.

Je nini kitatokea?? Fatuma anayoongea ni ukweli au ndo anamdanganya Jacob ili asimusaliti??

Itaendelea......

Usikose sehemu ya 16.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Write your comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Menu