TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Sehemu 26.
Hapo mapigo ya moyo wa Jacob yalianza kuseleleka kwa speed ya juu kabisa na alikuwa haelewi afanye nini, na huku mlango uliendelea kugongwa kwa nguvu.
Jacob mapigo ya moyo yalikuwa juu kiasi kwamba hata mtu angekuwa pembeni yake angesikia jinsi yanavyo dunda, Jacob alizidi kukaa kimya mule ndani huku nje mlango uliendelea kugongwa.
Jacob aliogopa kufungua mlango maana alijua akifungua mlango na ikajulikana kwamba yule Mama amefariki na Jacob ndo yumo mule ndani basi yatatokea kama yaliyo mtokea nyuma kwa Baba yake Mr Deus, Jacob akiwa anatetemeka alikumbuka na mateso ya kule gerezani yalivyo, hapo kimoyomoyo Jacob alijiapia kwamba lazima aukwepe msala ule.
Zilipita kama daki kumi yule mtu aliyekuwa anagonga nje aliacha kugonga baada ya kuona mlango haufunguliwi, Jacob naye mule ndani baada ya kuona mtu aliyekuwa anagonga kaacha na inaonesha kaondoka kabisa Jacob aliamua kufungua mlango ili achungulie mazingira na ikiwezekana achomoke mule ndani na kupotelea kusiko julikana.
Jacob alipo fungua mlango na kuchungulia alimuona Fatuma ndo anaishia kwa mbali anaondoka
"Duuuu!! Kumbe aliye kuwa anagonga ni fatuma!! Nimuite ama??" Jacob baada ya kumuona fatuma aligundua kumbe aliye kuwa anagonga mlango ni fatuma, alitamani amuite ila moyo ulisita na hakujua atajibu nini endapo ataulizwa kuhusu yule Mama aliye fariki mule ndani.
Basi Jacob alicho kifanya aliamua kuanza kumfuata fatuma kwa nyuma kisiri siri ili walau ajue Fatuma anako kaaa, Jacob alifuatilia kama dakika kumi hivi, alikuja kufail baada ya kuona Fatuma anapanda daladala, Jacob alitamani Naye akapande daladala ila ndo hakuwa hata na shilingi mia.
Jacob hapo alibaki dailema alikuwa haelewi ashike lipi, ila alifikiria alikumbuka kwamba kuna nyumba ambayo Mr jomo alikuwaga anakaa uwaga mara nyingi haikaliwi na mtu yeyote hapo alichukua uamuzi wa kwenda kukaa na kujificha kwenye nyumba ile maana hakuwa na sehemu nyingine ya kwenda Zaid ya kule.
Likiwa giza lishaingia Jacob kwa kujificha ficha alitembea mwendo kama wa lisaa lizima, hatimaye alifika kwenye ile nyumba ya Mr jomo, ila alipo fika aliona taa zinawaka kuanzia nje mpaka ndani, hapo Jacob aligundua kwamba kuna mtu anakaa.
Jacob alichoka baada ya kuona sehemu ambayo ndo aliona kama kimbilio lake kuna mtu inaonekana anakaa na hakujua mtu huyo ni nani, basi Jacob alisogea kwenye nyumba ile kwa karibu alianza kuchungulia kupitia matundu ambayo yalikuwa yapo kwenye wigo wa nyumba hiyo, Jacob alishangaa kuona kwa nje ya ile nyumba kwenye kamba zimeanikwa nguo za Fatuma.
"Duuuu!! Inamana yawezekana Fatuma akawa anakaa huku??" Jacob alianza kupata shaka, hapo Jacob aliamua liwalo na liwe aliamua kugonga ili athibitishe anaye kaa pale ni Fatuma au ni mwingine.
Baada ya kama dakika tano alishangaa kumuona Fatuma anafungua mlango.
Fatuma naye baada ya kufungua mlango hakuamini kama anaye muona mbele yake ni Jacob.
Pamoja na kwamba Jacob alimkosea Fatuma, ila kiukweli Fatuma siku ambazo Jacob alikuwa mbali naye mtoto wa kike usingizi ulikuwa hauji kabisa na tayari alikuwa ashaanza kukonda kwa kumuwaza Jacob.
Fatuma baada ya kumuona Jacob alimkimbilia na kumkumbatia kwa nguvu mpaka Jacob mwenyewe alishangaa maana hakuamini kama Fatuma anaweza kumlaki hivyo.
"Jacob naomba usiniache tena, ntakufa kwa pressure mie jamani" Fatuma akiwa kamkumbatia Jacob machozi yalikuwa yanatiririka na maneno ya kimahaba yanamtoka.
Jacob alifurahi sana kusikia maneno ya Fatuma, yaani alijikuta kawa mwepesi kiasi kwamba alisahau kama huko nyuma kaua mtu bila kukusudia na ana kesi ya kujibu.
Basi baada ya fatuma na Jacob kupeana salamu za hapa na pale na kupigana mabusu kadha ya maana waliingia ndani.
"Jacob vipi mbona unaonekana una wasiwasi na unahema kulikoni kwani? Na umejuaje mi nakaa hapa?" Fatuma baada ya muda aligundua Jacob hayupo sawa kiakili kabisa na alionekana ni mtu ambaye kuna kitu anahofia
"Fatuma mi sikuwa najua kama unakaa hapa hicho cha Kwanza, nilikuwa nakuja tu hapa kujificha" Jacob alifunguka
"Jacob kujificha!!? Umeua si ndo maana ake??" Fatuma aliuliza kana kwamba anajua kama Jacob kayakoroga huko aliko toka.
"Fatuma we ndo kila kitu changu kwa Saiz na siwezi kukuficha kitu mi nimeua bila kukusudia naomba Mungu tu anisaidie jamani" Jacob machozi yalianza kumutiririka maana alijua anarudi tena kule kule gerezani kwenda kunyea debe na mateso ya kule alikuwa anayajua vizuri.
"Jacob mi hapo ndo unaniachaga hoi! Sasa huo mchozi wa nini wakati umeyataka mwenyewe??" Fatuma alishangaa alafu aliongea kama mtu ambaye hata hajali chozi la Jacob.
"Fatuma usiongee hivyo jamani mi sikuwa nimekusudia kuua na usiseme nimeyataka hapa inatakiwa unipe tu ushauri nifanyaje?"
"Jacob acha ujinga nakupaje ushauri wakati sijui umemuua Nan na umemuuaje?"
"Fatuma mimi nimemuua yule Mama anaye kaa pale ulipo kuwa unakaa wew, nimemusukuma kidgo tu kaanguka kafa"Jacob aliamua kudanganya hakutaka kuweka wazi kwamba Mama wa watu kafia kwenye kochi wakiwa kwenye shughuli ya kujaza dunia.
"Jacob why hubadilika wew? Kwa hiyo uongo ndo unaona kwa maisha yako ni tiba si ndo maana yake? Ivi we unadanganya hivyo unajua sababu za yule Mama kufa?? Au unaona kudanganya ndo solution? " Fatuma alimshitukia Jacob na inaonekana yeye alikuwa anajua kila kitu.
"Fatuma unamanisha nini!!? Unasema uongo kwani we ulikuwepo?" Jacob alijifanyisha kama kakasirika kwa yeye kubishiwa kile alicho kiamini kwamba ni kweli
"Jacob mi huwezi nidanganya kitu, tena usije rudia kunidanganya kabisa, hata ukunje Sura ulicho ongea ni uongo mtupu eti kumsukuma!! "Fatuma haikumwingia akilini kabisa mpaka Jacob mwenyewe alishangaa na kuanza kuhisi labda wakati yale yanatokea Fatuma alikuwa anachungulia.
"Fatuma sasa we unabisha ulikuwepo basi sema wew ukweli!? Usitake kunivuruga wakati tayari nishavurugika" Jacob alijidai kukunja sura ili kumuonesha Fatuma kwamba alicho kizungumza yeye ni ukweli mtupu.
"Jacob mi najua kila kitu, najua kafaje kafaje mpaka sababu ya kifo chake naijua" Fatuma aliongea maneno ambayo yalimuacha Jacob kapigwa na butwa na kuacha mdomo wazi
Itaendelea......
Usikose sehemu ya 27.
TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Sehemu 27.
"Jacob mi najua kila kitu, najua kafaje kafaje mpaka sababu ya kifo chake naijua" Fatuma aliongea maneno ambayo yalimuacha Jacob kapigwa na butwa na kuacha mdomo wazi
"Heeeeeee!! Unasema?" Jacob alibaki kaachama akiwa haamini yale aliyo sikia, eti Fatuma anajua sababu ya kifo
"Sasa Jacob hapo kipi cha kushangaza? Wewe si nilikuonya ukanibishia ukasema mila zetu hazikuhusu au umesahau?? Yule Mama we umefanya naye mapenzi na ndo sababu ya yeye kufa hakuna cha kumsukuma wala nini? Bisha kama ni uongo??" Fatuma aliongea mambo ambayo yalimuacha Jacob akiwa kaachama.
"Jacob ni jibu kama ni uongo siyo unaachama, we si umesema ulimsukuma?? " Fatuma alikuwa kamkazia Jacob na aliona jinsi Jacob mdomo unavyo tetemeka
"Aaaaa!! Aaaaa! Inamana aaaaa!! Hiyo ndo sababu!!!??" Jacob hakuamini alibaki kubabaika tu
"Jacob mi nilikuonya hukusikia nilikwambia kwa vile tayari ushalala na mimi huruhusiwi kulala na mwanamke mwingine la sivyo kitatokea kibaya ukawa mbishi,ona sasa umesababisha Mama wa watu kafa kwa ubishi wako, alafu we Jacob umerogwa ama? we ilikuwaje ukalala na Jimama kama lile??" Fatuma alizidi kuongea mambo ambayo yalizidi kumshangaza Jacob.
Jacob alifikiria kwa undani, alianza kuamini maneno ya Fatuma kwamba yawezekana kweli hiyo ndo sababu ya yule Mama kufariki, ila alikumbuka kwamba pia amewahi kufanya mapenzi na shaifa ila shaifa yeye hakufa, hapo tena mashaka yalimjia yaani alikuwa haelewi kipi ni kipi.
"Aaaaaa!! Sasa Fatuma kama hiyo ndo sababu mbona shaifa yeye nililala naye na hakufa kwa nini iwe huyu au hizo mila zenu zinaangalia rangi na kuchagua??" Jacob alipofikilia sana aliona haimjii akilini, aliamua kumuuliza swali Fatuma.
"Jacob hivi we utaacha lini kuwaza ujinga humo kichwani mwako? Na kwanini hutumii akili yako vizuri kufikiria na kunyumbua mambo? Kwanza chuo ulifikaje fikaje? Mbona kama akili yako ni ya mgando?" Fatuma baada ya kujibu swali la Jacob yeye alianza kama kumkashifu vile.
"Fatuma kwa hiyo umeamua kuanza kunitukana? Au umeona kunidanganya mimi na hizo sababu zako za kitoto ndo ntakubaliana na hilo? Eti mila kwa hiyo unaongea hivyo ili iweje sasa?? Mi sitaki dharau" Jacob alipandwa na hasira baada ya kuona Fatuma anampa maneno makali.
"Jacob kama unaona sababu yangu ni ya uongo basi nenda katafute mwanamke mwingine kalale naye uone nini kitatokea na hapo ndo utajua na kunyumbua mwenyewe kwamba kwa nini shaifa hakufa?" Fatuma alimpa Jacob mtihani mzito na baada ya hayo maneno Fatuma aliingia chumbani maana alionekana Naye kapaniki.
Jacob alibaki pale sebuleni akiwa haelewi, yaani huku alikuwa anawaza kwenda kunyea debe, huku anawaza moto wa shaifa, huku anawaza namna ya kurudisha mali za baba yake mikononi mwake na kulipa kisasi, yaani kichwa kilikuwa kinawaka moto, moja ilikuwa haikai mbili haikai.
Jacob akiwa katulia kwenye kochi pale sebuleni, alipitiwa na usingizi alikuja kushituka kushakucha kabisa.
Aliangaza huku na kule hakuona mtu, alipo ingia jikoni alikuta Fatuma anaanda madikodiko.
"Jacob umeamuka" Fatuma aliongea kwa tabasamu mwanana kama siyo yule wa usiku ambaye alikuwa anabishana na Jacob.
"Aaaaaa!! Nimeamka, njaaaa tu ndo inataka kuniua" Jacob akiwa anajinyosha alijibu kichovu.
"Ndo usubiri nimalizie kuandaa chai sasa!"
"Alafu fatuma hivi ulicho ongea jana usiku ni kweli??" Jacob aliuliza kwa utaratibu
"Jacob mi sitaki tuanze kukumbuka ya jana, we ni mwanaume tumia akili yako kunyumbua mambo, kama unaniamini sawa, kama huniamini sawa ila mi sitaki tuanze tena kukwazana asubuhi hii" Fatuma alikwepa swali la Jacob.
"Sasa Fatuma ilikuwaje ukaja kuishi huku na huogopi??" Jacob alibadilisha maada maana aliona wanako elekea wanaweza kosana tena, na yeye akakosa msosi,na hela ya kununua chakula yeye hana.
"Jacob mi nilikuja kuishi huku siyo kwa kupenda, maisha yalinichapa na nilikuwa nimeshindwa kulipa kodi pale, na ndo nikaamua kuondoka, uzuri nilikumbuka kwamba huku kuna nyumba ya bure ambayo haishi mtu yeyote, na kuhusu swala la kuogopa mi siogopi mtu yeyote na sina tatizo na mtu yeyote" fatuma alitoa maelezo yaliyo tosheleza kuhusu sababu za yeye kuhamia kwenye nyumba ya Mr jomo.
Basi chai iliiva, walipiga kifungua kinywa pale na mambo mengine ya hapa na pale yaliendelea, ila Jacob bado alikuwa hana raha kabisa maana alikuwa anawaza kuhusu kifo cha yule Mama na alijua wakigundua ni yeye kahusika lazima watamtafuta.
Wakiwa wametulia walifungua TV na kuanza kuangalia, kitendo tu cha kufungua, taarifa za kifo cha yule Mama zilikuwa zinatangazwa, kumbe yule Mama aliyefia kifuani mwa Jacob alikuwa ni askari mpelelezi kitu ambacho Jacob alikuwa hajawahi kugundua kabisa, na ile taarifa ilikuwa inaonesha kwamba chanzo cha kifo hakijulikani, ila uchunguzi unaendelea kufanyika.
"Jacob ulikuwa kumbe unaishi na askari mpelelezi? we mwanaume unajitafutia matatizo wewe haaa" fatuma naye alishangaa kusikia ile taarifa.
Itaendelea......
Usikose sehemu ya 28.
TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Sehemu 28.
"Jacob ulikuwa kumbe unaishi na askari mpelelezi? we mwanaume unajitafutia matatizo wewe haaa" fatuma naye alishangaa kusikia ile taarifa.
"Daaaaa!! Fatuma unafkri hata nilikuwa najua basi si ndo nasikia hapa" Jacob naye alikuwa anazishangaa zile taarifa.
"Kwani Jacob ilikuwaje ukaanza kuishi na yule Mama??"
"Fatuma mi nilienda pale kukutafuta wew, na nilipofika nilikuta yule Mama ndo yupo pale na alisema hakujui, nilipo mwelezea shida zangu ndo akaahidi kunisaidia" Jacob alitoa maelezo kifupi
"Jacob mi nataka nikupe ushauri tu kidgo, ukiwa kama mwanaume uliye kamilika naomba chagua kitu kimoja cha kufocus nacho ambacho wewe ndo utakipigania na mambo ya kuchanganya vitu utakosa kila kitu, na kitu ninacho kuomba kama una uwezo wa kwenda kanisani kusali anza kwenda maana shaifa hawezi kukuacha kizembe hivyo." Fatuma alitoa ushauri kwa Jacob.
Jacob hakujibu kitu alibaki kakaa kimya anatafakari maneno ya fatuma.
Maisha yaliendelea huku Jacob na fatuma wakiwa wanaishi tena pamoja kwa mara ya pili kama mke na mume na awamu hii ni kama upendo uliongezeka zidi yao maana kila mtu alikuwa kaonja joto la jiwe kukaa mbali na mwenzake.
Jacob aligundua kwamba Mr Derick na Mama yake wanamuogopa wanajua yeye ni mzimu, hapo Jacob alianza kufanya mpango wa kurudisha zile mali zake akiwa anashirikiana na Fatuma, na bahati nzuri kwa Jacob hakugundulika kama yeye ndo kahusika na kifo cha yule Mama kwa sababu hakuna ambaye alikuwa anajua kwamba Jacob anaishi na yule Mama pale nyumbani kutokana na Jacob kujificha muda wote.
Jacob siku moja wakiwa wamekaa kimahaba na Fatuma alianza kukumbuka mambo ya nyuma.
"Ivi fatuma kitu ambacho huwaga unaniambia kuhusu mila zenu ni kweli??"Jacob alikumbushia
"Jacob mi sitaki mada ya ujinga muda huu, na kurudia mambo ni sitakagi kabisa, we kama vipi amini unavyo amini" Fatuma hakupendezwa na swali la Jacob.
Basi hiyo mada iliishia hapo, maisha yalizidi kusonga mbele na maisha yao yalikuwa siyo mazuri hata kidogo kwa sababu mtafutaji alikuwa ni mmoja ambaye ni fatuma, maana Jacob alikuwa hatoki ovyoovyo nje.
"Jacob hivi maisha haya mpaka lini na wakati mali unazo nyingi tu?" Fatuma siku moja aliamua kuvunja ukimya ,na siku hiyo walishinda njaa tokea asubuhi mpaka jioni.
"Sasa Fatuma we unashaulije?"
"Jacob kwa hiyo we hujui? Zile mali si zimeandikwa kwa jina lako ama?"
"Kwa hiyo kama zimeandikwa kwa jina langu we unatakaje??"
"Cha kufanya ni kuiba hati zote za mali, yaani zile kampuni zenu zote na nyumba zenu zote we ni kuziiba, baada ya hapo kitajulikana cha kufanya"
"Fatuma we unafikiria tu upande mmoja, we si unajua mi nilifungwa kwa kesi ya mauaji? Na kitaa kila mtu anajua mi ndo niliua na taarifa za kifo changu nikiwaj jela zilisambaa je unafikiri nikijtokeza hadharani nani ataniamini na sina ushahidi wowote hata hivyo si ntakamatwa kwa kutoroka gerezani"
"Jacob kikubwa tupate hizo hati, baada ya hapo kila kitu kitajulikana na mimi nina imani hati bado hazijabadilishwa jina, ila ukizembea mwisho utakuta siyo mali zako tena"
"Haya nambie sasa tunafanyaje huu mpango?" Jacob alikubalina na wazo la fatuma na alitaka kujua mbinu ya kuiba hati zote za umiliki.
Basi siku hiyo walianda mpango kazi wote na kilicho baki kilikuwa ni kutekeleza mpango huo.
Huku kwa upande wa shaifa, inaonekana mambo yalikuwa siyo mambo
"Dada si uachane na huyo mtu, mbona unapenda matatizo wewe??" Alikuwa ni Sharifa akiwa anampa ushauri dada yake ambaye ilionekana, kuna kikundi kilikuwa kinamlazimisha yeye kuachana na Jacob ila yeye alikuwa hataki kukubali.
"Sharifa, Hadi hapa nimepitia mateso ya kutosha kwa hiyo ushauri wako wa kijinga mi sipendi kabisa, yaani badala ya kunitia moyo na wewe unaongea Ujinga" Shaifa aliwaka inaonekana alikuwa hataki kabisa swala la kuachana na Jacob
"Dada ila mi nakuonea huruma ni wewe" Sharifa alizidi kukazia
"Sharifa naomba tena ukae kimya, ivi unajua jinsi gani nampenda yule mwanaume? Na sitaki ujinga wowote kumhusu mwanaume wangu mbona yule mtoto wa Mama Zurufa yeye mtoto wake kaolewa na mwanaume wa kawaida kwa nini iwe kwangu? Sitakubali" shaifa alikuwa hakubali na inaonekana kuna kitu kilikuwa kinaendelea kwenye hizo koo zao na tamaduni zao ambazo hadi Saiz hatujajua ni koo za namna gani.
Kwa upande wa kina Jacob, siku hiyo ulikuwa ni usiku Jacob na fatuma walikuwa wanazengea zengea kwenye nyumba ya Mr Derick yaani ile nyumba ambayo ilikuwa ya kina Jacob ila Mr Derick ali irithi baada ya Mr Deus kufariki.
Jacob na fatuma baada ya kufika pembezoni mwa fensi ya nyumba hiyo, Jacob alibadili nguo na kuvaa kanzu nyeupe, alafu alichukua marangi ambayo usipo angalia vizuri utajua ni damu, alijimwagia kifuani na usoni alafu mdomoni alimwagia ile rangi na kuweka unga mweupe kabisa, yaani kifupi alikuwa anatisha ukimuona, alafu alichukua na wigi akalivaa.
Basi Jacob aliluka fensi na kuingia ndani, yaani hakupitia mlangoni maana alijua akipita mlangoni lazima bwana Nguna ataanza kupiga makelele na kubumbulua dili.
Jacob baada ya kuruka fensi alienda moja kwa moja mpaka mlangoni na Fatuma yeye alikuwa kabakia nje.
Bahati nzuri kwa Jacob siku hiyo Mr Derick hakuwepo alikuwa kalala kwa mke mdogo Vicky, alikuwepo tu mke wake Mama wa Jacob mlezi na muda huo alikuwa anaangalia TV sebuleni.
Jacob baada ya kufika mlangoni alianza kugonga mlango, na kule ndani Mama Jacob aliacha kuangalia TV alisogea mlangoni baada ya kusikia mlango unagongwa.
Itaendelea......
Usikose sehemu ya 29.
TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Sehemu 29.
Jacob baada ya kufika mlangoni alianza kugonga mlango, na kule ndani Mama Jacob aliacha kuangalia TV alisogea mlangoni baada ya kusikia mlango unagongwa.
Baada ya Mama Jacob kufungua mlango, moyo wake ulilipuka baada ya kuona jitu la kutisha, hapo alipiga makelele ya kufa mtu , bahati mbaya naye Nguna hakuwepo pale getini alikuwa kaenda kununua sigara, kwa hiyo hakuna aliyesikia makelele ya Mama Jacob.
Mama Jacob baada ya kuona hivyo alikimbilia chumbani na Jacob hakutaka kubaki nyuma Naye alifukuzia, Mama Jacob alifika chumbani ila kabla hajafunga mlango tayari Jacob alikuwa ashafika na alikuwa anacheka na kuigiza kama ni mzimu.
Kutokana na mapigo ya moyo kwenda mbio Mama Jacob alidondoka na kuzimia kule kule chumbani.
Hapo Jacob aliona ndo muda wenyewe sasa wa kufanya mambo. Kwa kuwa ile nyumba alikuwa anaijua vizuri haikumpa shida alianza kupekua kila sehemu ambapo anajua zile nyaraka zinaweza kufichwa.
Katika kutafuta aligundua chini ya kitanda kuna kibox cha shaba ambacho kilikuwa kimefungwa vizuri na ili kufungua kibox hicho zilikuwa zinahitajika code maalumu.
Jacob baada ya kukiangalia vizuri kile kibox aliamua kukichukua akiwa na imani kwamba zile nyaraka zinaweza zikawa zipo mule ndani.
Basi Jacob hakutaka kuchelewa aliamua kutoka mule ndani Fasta Fasta na kile kibegi mpaka nje kabisa, aliruka tena fensi na kutoka nje kabisa hapo alimkuta Fatuma anamsubiri
"Jacob mara hii tayari?" Fatuma alishangaa maana ni muda mchache Jacob alitumia mule ndani
"Fatuma nahisi itakuwa tayari Maana nimekuta hiki kibox ila sijaangalia ila nahisi zitakuwa humu"Jacob alitoa maelezo
"Jacob acha Mambo ya kuhisi inatakiwa ufanye kitu cha uhakika na je vipi tukikuta humo ndani hakuna kitu? Huoni hapo tutakuwa tumefanya kazi bure, mambo ya kazi moja kurudia mara mbili mbili ujue siyo mazuri kabisa??" Fatuma alimshangaa Jacob kwa kubeba kile kibox akiamini ndo kila kitu.
"Fatuma tuondoke kwanza hapa hayo mengine yanajulikana mbele kwa mbele"
Basi Jacob na fatuma waliondoka na kurudi wanako kaa na walikuwa hawana uhakika kama kwenye box yaliyomo yamo au ndo wamefanya kazi bure.
Huku nyuma kwa mama Jacob kulikuwa hakukaliki, baada ya kuzinduka na kutoona mtu alikurupuka mule ndani mpaka nje, alimkuta bwana Nguna katulia zake anapiga fegi
"Boss kulikoni mbona mbio mbio?" Nguna alishituka baada ya kuona boss wake anakuja kwa speed tena akiwa anahema.
"Nguna inamana hukusikia makelele ninavyo piga? Au unataka nifie ndani? Nakwambia mzimu wa Jacob nusura unimeze na sijui umepotelea wapi" akiwa anahema Mama Jacob alisimulia kile kilicho mtokea
"Heeeee!! Karudi tena!!!?" Nguna nusura naye aanze kukimbia baada ya kuambiwa yale maneno maana miongoni mwa watu waoga na mambo ya mizimu alikuwa ni bwana nguna
"We mjinga unataka kwenda wapi sasa? Ebu mpigie mr Derick umwambie aje maana huko ndani hakuingiliki tena" Mama Jacob alimwambia Nguna baada ya kuona nguna anataka kukimbia
Basi kama nguna alivyo ambiwa alimpigia simu Mr Derick na kusimulia kile kilicho tokea, Mr Derick naye baada ya kusikia habari za mzimu wa Jacob alikataa kuja aliamua kuzima na simu kabisa maana naye bado alikuwa maisha yake anayapenda.
"Boss kasema hawezi kuja, eti tupambane na hali yetu" Nguna alimwambia Mama Jacob kama alivyo jibiwa na Mr Derick
" Huyu mpuuzi kweli, duuu Nguna kule ndani mi sirudi kabisa acha nilale kwenye kibanda chako sawa?" Mama Jacob alianza kuiogopa ile nyumba yake
"Boss sasa ukilala humo mi ntalala wapi??" Nguna naye alikuwa hataki kubaki nje maana tayari alikuwa ashaanza kuogopa
"Nguna we kazi yako si kulinda ama mambo ya kulala ya nini sasa? Kazi yako wewe ni kutulinda sisi pamoja na mali zetu kwa hiyo kaa hapo nje unilinde sawa eee??" Mama Jacob aliongea na kuingia kwenye kibanda cha mlinzi kwenda kulala
"Boss Hapana we kalale ndani bana hiyo siyo Fair kabisa, au unataka mi ndo nife na wakati nyumbani kwetu wananitegemea??" Nguna naye hakukubali aliamua kuzama mule mule ndani kwenye kibanda maana aliona kubaki pale nje pekee yake kwa muda ule ni kujitafutia kifo.
Upande wa akina Jacob baada ya kufika nyumbani, walianza kuhangaika kukivunja kile kibox ili waangalie ndani kuna nini.
Itaendelea......
Usikose sehemu ya 30.
TAJI LA UBAYA
(A crown of badness)
Sehemu 30.
Upande wa akina Jacob baada ya kufika nyumbani, walianza kuhangaika kukivunja kile kibox ili waangalie ndani kuna nini.
Walitumia kama masaa mawili kuvunja kile kibox ila walishindwa, waliamua kukiweka kiporo cha kesho maana tayari ulikuwa ni usiku mnene.
Kulipo kucha tu asubuhi waliamukia Kazi ya kukivunja kile kibox maana code za kufungulia ndo hawakuwa nazo, walipambana kuvunja kile kibox ila bado walishindwa, ilifika mpaka mchana wakiwa bado wanapambana, ilibidi wapumzike kwanza wapate na chakula ili kazi iendelee maana kile kibox kilivyo tengenezwa ilikuwa ni ngumu sana kukivunja kwa kutumia nguvu.
Baada ya kupumzika waliendelea mapambano ya kuvunja kile kibox, walikuja kufanikiwa usiku wa manane kukivunja kile kibox, kama ilivyo imani ya Jacob mule ndani ya kile kibox ndo kulikuwa na nyaraka zote muhimu kuhusu zile mali.
Walipo angalia na kukuta kila kitu kipo vizuri walifurahi na kuruka kwa furaha, japo bado kazi ilikuwa haijaisha maana hawakujua watazitumiaje zile nyaraka kurudisha mali wakati ina sadikika Jacob ashakufa na watu wote wanajua hivyo.
Huku upande wapili kwa Mama Jacob tangia tukio la kutokewa na mzimu limpate alikuwa anaogopa kuingia pekee yake ndani yaani alikuwa anataka kila anapo enda aongozane na bwana Nguna, naye mr Derick hakutaka kurudi kule baada ya kuambiwa Jacob alikuja.
Zilipita kama siku tatu Mr Derick akiwa hajarudi, na ilipo fika siku ya nne hiyo ilimlazimu aende kwa Mama Jacob maana hiyo siku ndo ilikuwa siku ya kwenda kubadili nyaraka zile majina kwani tayari vyeti vya kifo cha Jacob alikuwa ashapata, kwa hiyo ilitakiwa aende kule akachukue zile nyaraka zote.
Mr Derick alifika nyumbani kwake, alipiga honi kwenye geti hakuna aliyefungua aliamua kushuka yeye na kufungua aliingiza gari ndani.
Baada ya Mr Derick kushuka kwenye gari alielekea moja kwa moja mpaka ndani alipo ingia alikuta bwana Nguna kakaa katulia juu ya sofa anatuna na kujibweda kama yeye ndo boss vile, wakati ilikuwa siyo kawaida.
"We nguna umeanza lini hiyo tabia? Yaani unaacha kukaa kule getini ambapo ndo kazi yako unakuja kujikalisha kwenye sofa humu ndani?? Umechoka kazi eeeeee??" Mr Derick aliwaka baada ya kukuta Nguna yumo mule ndani badala ya getini.
"Mr Derick naomba ishia hapo hapo makelele mi sitaki sawa eee? Mi ndo nimemwambia akae humu ndani kwa sababu siwezi kaa pekee yangu humu ndani wakati mzimu unaniwinda! We si uliogopa kuja huku ukaamua kukaa huko huko unagomba nini sasa??" Mama Jacob baada ya kusikia mr Derick anamgombeza bwana Nguna naye alitoka jikoni kafura hasira aliona mwanaume huyo anamuletea utani
"Kwa hiyo we mwanamke unasema huwezi kaa peke yako? Kwa hiyo hata kulala ulikuwa unalala naye"
"Bwana we hayo hayanihusu Kwan nikilala naye kuna maajabu gani? Mi sitaki ujinga eeeeee? Kama mpango wa kuua uliufanya wewe basi pia namna ya kupambana na huo mzimu inatakiwa ujue wewe" Mama Jacob alikuwa kavurugwa yaani alianza kutoboa siri ambazo hata mr Nguna alikuwa hazijui.
Baada ya hayo Mr Derick ilibidi awe mpole maana alikuwa anajua Mama Jacob akikasirika hachelewi kuropoka mambo na aliona anako elekea anaweza weka kila kitu peupe mpaka Mr nguna akajua ambacho alikuwa hakijui.
"Haya Nguna nenda kwenye eneo lako la kazi humu ndani sitaki kukuona"Mr Derick alitoa amri kwa Nguna
Basi Mr nguna aliondoka na Derick aliingia chumbani ili achukue kile kilicho mpeleke, ila alipo angalia pale wanapo wekaga hakuona box
"We mwanamke wew ebu njoo huku chumbani" Mr Derick aliamua kumuita mkewe alijua labda yeye ndo kahamisha
"Eeeeee!! Kulikoni mbona tunaitana kwa hasira hivyo Kama tupo jeshini?" Mama Jacob baada ya kuingia ilibidi aulize
"Vipi wew ndo umehamish box la nyaraka??"
"Derick mi sitaki maswali ya kipuuzi mi nihamishe nipeleke wapi sasa" Mama Jacob naye alikuwa anashangaa
"Wewe acha masihara ujue mi nipo serious, humu ndani tupo wawili atakuwa nani kachukua kama siyo wewe"
"Derick naona umeanza mazoea na mimi eee?? Kumbe ndo maana ulikuwa unakatalia kwa Vicky huko,.unajua upuuzi unao taka kuufunya eee?? Kwa hiyo Derick unataka kunitelekeza na kunizulumu?? Nakwambia hapa patachimbika naomba nyaraka zote zirudi hapa haraka" Mama Jacob alikuwa kapandwa na wazimu alijua kupotea kwa box hilo ni mpango wa Derick.
Siku hiyo palikuwa hapatoshi pale ndani, yaani kila mtu alikuwa anamtuhumu mwenzake kwamba ndo kafanya mpango wa kuiba ili mali amiliki pekee yake, maana mwanzo walikubaliana kwamba watakapo badili jina kwenye zile nyaraka wataweka majina yao wote wawili, yaani mali zitakuwa zao wote, sasa walipo ona hizo nyaraka zimepotea katika mazingira ya kutatanisha hapo ndo kila mtu hakutaka kumwamini mwenzake.
"Derick mi naenda kwa mganga kuagua kama ni wewe itajulikana, kama siyo wewe itajulikana pia" mama Jacob tayari akili yake ilikuwa imemutuma kwenda kwa mganga kuagua aliye iba lile box.
Mr Derick mambo ya waganga ndo alikuwa hataki kabisa, ila aliogopa kumbishia mama Jacob, kwa sababu angebishia angeanza kuonekana yeye ndo kalichukua lile box, kwa hiyo ilibidi awe mpole.
Itaendelea........
Usikose sehemu ya 31

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Write your comment